Je! ni vibaya kutaja Huduma kwa kujipa cheo? Mfano Mighty Prophet, Chief Apostle n.k.?

by Admin | 2 September 2019 08:46 pm09

JIBU: Biblia haikatazi mtumishi yeyote wa Mungu kutambuliwa kwa karama aliyo nayo. Kwamfano kuitwa mchungaji, au mwinjilisti au mtume, au mwalimu au nabii au askofu n,k. Hakuna mahali ilipokataza, Lakini kuongeza Neno hapo juu yake mfano “mkuu” au “kiongozi ” “mighty” “chief” “lead” “great” n.k. hiyo ni roho ya kujiinua na ni roho ya mpinga-kristo yenyewe. Kwani vyeo hivyo vinamuhusu Bwana wetu YESU KRISTO mwenyewe.. Yeye ndiye mchungaji mkuu biblia inasema hivyo..yeye ndiye mtume mkuu, yeye ndiye nabii mkuu, Yeye ndiye Bwana wa mabwana, na yeye ndiye Mfalme wa wafalme.Na ndio maana utaona hakuna Mtume yeyote wa Kristo alijiita kuwa yeye ni mtume mkuu, bali cheo hicho walikitambua kuwa ni cha Kristo mwenyewe.

Waebrania 3:1 “Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana MTUME NA KUHANI MKUU wa maungamo yetu, Yesu, aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu.”

Waebrania 3:20 “Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu MCHUNGAJI MKUU wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu,” 

Unaona? Hivyo hao watu wote wanaojivika hivyo vyeo vya juu zaidi ya walivyopewa, utatambua kuwa dhima yao ni kuvuta watu kwao, wawafuate wao na si Kristo, na ndio maana utaona hawaoni hata haya kujivuka vyeo vya juu kama hivyo. Lakini biblia inasema ajikwazaye atashushwa..Watu wa namna hiyo Bwana mwenyewe atawashusha, kwasababu yeye kasema Utukufu wake hatagawana na mwingine yeyote. 

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?

MPINGA-KRISTO

UNYAKUO.

MANABII WALISEMA “NENO LA MUNGU LIKANIJIA” ..MAANA YA HILI NENO NI NINI?

NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.

FIMBO YA HARUNI!


 

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/02/je-ni-vibaya-kutaja-huduma-kwa-kujipa-cheo-mfano-mighty-prophet-chief-apostle-n-k/