MAMA WA MAKAHABA

by Admin | 21 October 2019 08:46 pm10

Ufunuo 17:3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.

4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.

5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.

6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu”

Kuna Maswali machache hapo ya kujiuliza;

1.Kwanini Yohana alichukuliwa katika Roho mpaka jangwani na si mpaka msituni…Ni wazi kuwa roho iliyopo jangwani si roho ya Mungu bali ya yule Adui..Kwasababu Bwana Yesu alisema katika Mathayo 12:43 “Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate”.  Mahali pasipo maji ni jangwani…Hivyo Yohana alichopelekwa kukiona jangwani ni roho ya yule Adui.

2. Swali la pili; Kwanini jambo la kwanza Yohana kuliona ni mwanamke?..Maana alimwona mwanamke na alipomtazama vizuri akamwona ameketi juu ya mnyama mwekundu…Hiyo ikifunua lengo kubwa la yeye kupelekwa huko ni kumwona huyo mwanamke. Na huyo Mwanamke ni nani? na anaonekana amelewa!..Huyo Si mwingine zaidi ya kanisa fulani ambalo tutakuja kuliona mbeleni kidogo. Kwasababu katika maandiko mwanamke anawakilisha kanisa (Waefeso 5:31-32, 2Wakoritho 11:2, Ufunuo 21:9,)

3. Jambo lingine ni kwanini Mnyama aliyempanda huyo mwanamke alikuwa mwekundu sana?..Rangi nyekundu siku zote inaashiria damu!..yaani umwagikaji wa damu! Maana yake huyo mnyama ni mwuuaji…Tengeneza picha Mtu aliyelewa amepanda simba na huku anachupa yake mkononi ya pombe, halafu anazunguka naye mtaani na huyo simba anaonekana ana ghadhabu nyingi, ana meno makali..Utapata picha gani? Ni wazi kuwa utaona huyo mtu kakusudia kudhuru watu kupitia huyo mnyama wake anayemwendesha. Ndivyo huyu mwanamke anavyoonekana hapa.

Hivyo kwa tafsiri yake ni kwamba kanisa hilo linatumia mfumo fulani kuua watu, lilitumia mfumo huo kuua watu katika enzi za zamani, na litatumia  huo mfumo kuua watu wakati wa dhiki kuu, huo mfumo ndio mnyama..

4. Jambo la Nne Mwanamke yule katika kipaji cha uso wake ana jina limendikwa kwa siri..kumbuka sio kwa wazi! kwa siri!  ikimaanisha hataki ajulikane yeye ni nani? na jina hilo linasomeka BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.

Kwanini ni Babeli Mkuu?..Ikimaanisha kuwa kulikuwa na Babeli nyingine zilipita lakini sio KUU, Babeli ile iliyotengeneza mnara ilikuwa ni Babeli lakini sio kuu!..Babeli ya Nebkadneza ilikuwa ni Babeli lakini si kuu!…Hivyo hiyo Yohana aliooneshwa ndio kuu!!

Na kwanini tena ni MAMA WA MAKAHABA?, Ikimaanisha anao watoto ambao nao ni makahaba, na yeye mwenyewe anafanya ukahaba..Na kama yeye ni kanisa ni wazi kuwa waototo wake nao watakuwa ni makanisa na wote wanafanya ukahaba…..Kanisa linalofanya ukahaba kibiblia ni kanisa linaloabudu sanamu, na kuacha sheria za Mungu…Na mwisho inamalizia NA MACHUKIZO YA NCHI…Na sio machukizo ya Mbingu…maaana yake anafanya machukizo akiwa hapa hapa duniani! machukizo ni jambo lolote linalomchukiza Mungu.

Ndugu huyo mwanamke si mwingine zaidi ya KANISA KATOLIKI, Hilo ndio lililohusika kuua zaidi ya wakristo milioni 60 wakati wa kipindi cha giza. Ni kanisa la uongo, lenye kivuli cha ukweli..Na mpinga-Kristo atatokea katika kanisa hilo, na cheo chake kimeshafunuliwa, na hicho si kingine zaidi ya cheo cha PAPA!

Kwa kutumia mfumo wake huo  wa kikatili (yaani huyo mnyama) atawaua watu wengi sana katika kipindi cha dhiki kuu, wakati ambao unyakuo utakuwa umeshapita! Wale watakaoachwa watalazimishwa kupokea chapa ya huyo mnyama, na kupewa kila sababu ya kuingia katika lile ziwa la Moto.

Je! Una uhakika wa kwenda kwenye unyakuo ili uepukane na mambo hayo yote? Kuna mambo mengi sana yatatokea mpinga kristo atakayoyafanya katika siku hizi za mwisho tunazoishi, huu ni ufupisho tu.

Maran atha, Bwana wetu anakuja

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

CHAPA YA MNYAMA NI NINI?

ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO

MPINGA-KRISTO NI NANI?

NITAJUAJE KAMA NDOTO NI YA MUNGU AU YA SHETANI?


Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/10/21/mama-wa-makahaba/