Ni kwa namna gani, haki yetu inapaswa izidi ya mafarisayo?

by Admin | 6 February 2024 08:46 pm02

Bwana alimaanisha nini katika Mathayo 5:20 aliposema..

[20]Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. 

Ni haki ipi hiyo.

JIBU: Katika andiko hilo tunaona Bwana akiainisha kigezo cha mtu kuingia kwenye ufalme wa Mungu..kwamba kigezo chenyewe ni “HAKI” …

Haki ni kitu kinachomstahilisha mtu kupokea kitu fulani. Kwamfano tunasema mtoto ana haki ya kulindwa…ikiwa na maana kilichomsababishia apate haki ya kulindwa ni ile hali ya utoto wake.

Mfano mwingine, tunasema ni mtu mzima ana haki ya kuoa au kuolewa na mtu amtakaye, katika wakati auchaguaye yeye. Tafsiri yake ni kwamba kinachompa haki ya kuwa hivyo ni kwasababu yeye ni “mtu-mzima”. Angekuwa mtoto asingekuwa na haki hiyo.

Sasa tukirudi katika habari hiyo tunaona kilichowafanya waandishi na mafarisayo wajihesabie haki kwamba wao ni warithi wa ufalme wa mbinguni. Ilikuwa ni kuitimiza sheria kwa matendo yao. Ambayo kimsingi wao wenyewe hawakuweza kuishika..kwa nje walionekana sawa lakini ndani walikuwa mbali na sheria yao. Kwasababu hakuwahi kutokea mtu hata mmoja aliyeweza kumpendeza Mungu kwa matendo yake, yeye mwenyewe.

Hivyo njia yao ya kupata haki, ambayo ni kwa matendo ya sheria haikuwa sawa. Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake na wale waliomsikia kwamba haki “ yao” isipozidi ya mafarisayo na waandishi kamwe hawataweza kuuingia ufalme wa mbinguni.

Swali je ya kwao inapaswa iweje. Je ya matendo ya sheria zaidi ya yale au vinginevyo?

Haki Yesu aliyoileta ambayo itampelekea mtu kurithi uzima wa milele ni kwa njia yake yeye mwenyewe .Ambayo sisi tunahesabiwa haki kwa kumwamini, kama mwokozi wa maisha yetu. Bila kutegemea matendo yetu ya haki. Yaani ni haki tuipatayo kwa neema.

Hivyo, wote wanaoipokea haki hiyo basi uzima wa milele ni wao. Na kwasababu ndio njia ambayo sisi tutamfikia Mungu. Basi neema yenyewe inatufundisha pia kuyazaa matunda ya Roho. Na hivyo tunaitimiza sheria ya Mungu mioyoni mwetu bila unafiki. Mbali na mafarisayo ambao walitegemea akili zako na nguvu zao.

Hata sasa ikiwa unategemea jitihada zako, zikupe haki mbele za Mungu, ndugu umepotea. Hutaweza Itegemee neema ya Mungu. Na hiyo itakusaidia kuyatimiza hayo mengine kwa Roho Mtakatifu.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

TUNAHESABIWA HAKI BURE KWA NJIA YA IMANI.

FUNDISHO KUU LA NEEMA YA MUNGU KWETU.

Nini maana ya kumsulibisha mwana wa Mungu mara ya pili?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/02/06/ni-kwa-namna-gani-haki-yetu-inapaswa-izidi-ya-mafasayo/