TUNAHESABIWA HAKI BURE KWA NJIA YA IMANI.

TUNAHESABIWA HAKI BURE KWA NJIA YA IMANI.

Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia neno la Mungu wetu lililo taa ya miguu yetu na mwanga wa njia yetu (Zab.119:105).

Neno la Mungu linasema..

Warumi 5:1 “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo”.

Je! ni haki gani hiyo tunayohesabiwa, ambayo tukiisha ipata basi tutapata amani?

Jibu ni kwamba si haki moja!, bali ni haki ZOTE Njema!… Mfano wa hizo ni kama zifuatazo…

1.HAKI YA KUISHI MILELE.

Tunapomwamini Bwana Yesu tunapata haki ya kupata UZIMA WA MILELE.. ambayo tuliupoteza pale Wazazi wetu wa kwanza walipoasi.

Yohana 11:25 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;

26  naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?”

Pia Yohana 3:36, Bwana Yesu anasema maneno kama hayo hayo…

2. HAKI YA KUWA NA UZIMA, NA AFYA.

Isaya 53:5 “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”

Hivyo magonjwa hayatatutawala, bali uzima na afya, kama tukiwa ndani ya Yesu, maana yake  AFYA ni haki yetu!.. tunapopitia maradhi ya muda mrefu maana yake hapo ni shetani katudhulumu haki yetu, hivyo hatuna budi kuishindania haki yetu mpaka tuipate katika mahakama ya kimbinguni, huku tukitumia katiba yetu biblia. Na tunapong’ang’ania kwa bidii bila kuchoka, wala kukata tamaa basi tunaipata haki yetu ya kuwa wazima siku zote.

3. HAKI YA KUMWONA MUNGU.

Unapomwamini Yesu ni haki yako kumwona Mungu katika maisha haya na katika yale yajayo.. Kumwona Mungu si lazima tumwone kwa macho, bali utamwona  katika maisha.. Maana yake utapitia vipindi vingi vya maisha ambavyo vitakujulisha kuwa Mungu yupo nawe, pia utaona miujiza mingi ya kiMungu ambayo itakujulisha kuwa Mungu yupo nawe, na zaidi sana kila utakapomwita Mungu utamwona..

Mathayo 28:20 “……….na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari”.

4. HAKI YA KUPOKEA ROHO MTAKATIFU.

Zamani Roho Mtakatifu alikuwa anashuka juu ya baadhi ya watu tu (ambao ni manabii) tena kwa kitambo kidogo, lengo ni kuwapa ujumbe kutoka kwa Mungu, na baada ya hapo anaondoka.. Kwasababu ROHO TAKATIFU ya Mungu haiwezi kukaa ndani ya Mwanadamu aliye mchafu.

Lakini baada ya Bwana YESU kuja, kaja kutuletea Haki ya sisi kuwa na Roho Mtakatifu ndani yetu, jambo ambalo si la kawaida..

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38  Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39  Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”

Hivyo yale matunda ya Roho tunayoyasoma katika Wagalatia 5:22, ambayo ni upendo, amani, furaha n.k Hayo yote ni haki yetu sisi kuyapata.. Kuwa amani ni haki yako wewe uliye ndani ya Kristo, kuwa na furaha ni haki yako.

5. HAKI YA KUFANIKIWA KIMWILI NA KIROHO.

Tunapomwamini Bwana Yesu na kukaa ndani yake, hatupati tu haki ya vitu vya kiroho, bali pia tunapata haki ya vitu vingine vya kimwili ikiwemo mafanikio.

3 Yohana 1:2  “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo”

Pia Neno la Mungu linasema..

2Wakorintho 8:9  “Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake”.

Na haki nyingine zote zilizosalia, ni Ahadi yetu. Ndio maana kuna umuhimu mkubwa sana kuingia ndani ya Kristo.. Ukiwa nje ya Kristo, shetani atakudhulumu haki zako zote hizo na hakuna popote utakapokwenda kushitaki.

Bwana akubariki.

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?

Sadaka ya Amani ilikuwaje?

UMEITIMIZA HAKI YOTE?

Je! Shetani anao uwezo wa kuumba, kama Mungu?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
JEM
JEM
1 year ago

tukisoma matendo ya mitume, tunaona watu wote waliokuwa wakibatiza walikuwa wakishukiwa naroho tafauti nasasa
swali: ule ulikuwa mpango wa mungu katika ule mwanzo wa kanisa? au tufanye je ili nasisi tuwe kama wao?
na zaidi tangu niokoke sijawayi hona watu wakijazwa roho pindi wanapobatizwa hata kwa jina la yesu!!!