Title July 2019

EPUKA KUTOA UDHURU.

Luka 14:16 “Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi,

17 akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.

18 Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe.

19 Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe.

20 Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.

21 Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete.

22 Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi.

23 Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa.

24 Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu”.

Bwana Yesu alitoa mfano huo wa karamu, kuelezea mambo yanayoendelea sasa katika roho, Kristo kama Bwana Arusi, anaalika watu sasahivi katika ufalme wake, anatuma watumishi wake huku na huko duniani kote…kuwaambia watu habari za uzima…Lakini kinachohuzunisha ni kwamba wengi ambao wangestahili kuwepo kwenye harusi ya mwanakondoo siku ile hawatakuwepo!, wengi ambao wangestahili kuwa wageni rasmi hawataingia kabisa karamuni.

Watu wengi wa dini, au wanaojiita wakristo hawataingia mbinguni, hiyo ni kulingana na maandiko! Hiyo yote ni kwanini?..Ni kutokana na kitu kimoja tu kinachoitwa UDHURU..Kutokuitikia mwaliko kutokana na visababu vidogo vidogo vya kutengenezwa.

Na maandiko yanasema pia, watoza ushuru na makahaba watawatangulia wengi kuingia katika ufalme wa mbinguni.. Ni kwanini?..Ni kwasababu hawana viudhuru katika kuitikia wito wa kumgeukia Mungu, Ni rahisi kumbadilisha kahaba amgeukie Mungu, kuliko kumrekebisha mtu ambaye ni wa kidini, ambaye tayari kashashiba na dhehebu lake, hataki tena kusikia kitu kingine, hata kama ni cha kweli vipi.

Ukiisoma tabia ya hawa watu walioalikwa Harusini na kukataa kuja, utaona kabisa walikuwa ni watu werevu, walikuwa wanatoa hoja za nguvu za kwanini wao kutokuja! Na kweli utaona kwa sehemu Fulani zinamashiko! Au ni za msingi…mwingine kwenda kujaribu ng’ombe, mwingine kaoa ni lazima akae na mke wake kidogo baada ya harusi, mwingine kanunua shamba, ni lazima akalitazame n.k.

Lakini kama ukichunguza sababu pekee za kutokuja sio hizo, lazima kutakuwa na vitu vingine ambavyo havijawapendeza kwenye hiyo karamu, labda pengine mfumo wa sherehe hawakupendezwa nao, au vinywaji wavipendavyo pengine havitakuwepo n.k…hivyo ili kuiepuka hawawezi kusema moja kwa moja hatuji, watatafuta visababu sababu vitakavyowapa kibali maalumu cha kutokufika, ili waeleweke, ndio hivyo vya kununua mashamba, kujaribu ng’ombe na kuoa na kuolewa.

Sasa umewahi kujiuliza kwanini Bwana Yesu alisema… “kama ilivyokuwa siku za Nuhu na za Lutu watu walikuwa wakiuza na kununua, wakipanda na kujenga, wakioa na kuolewa?” mpaka siku ile gharika na moto viliposhuka ghafla na kuwaangamiza wote?..Kuoa sio kubaya, wala kujenga sio kubaya, wala kuuza na kununua sio kubaya…Kibaya ni UDHURU unaoutoa wakati huu wa Neema. Unapofanya vitu vya ulimwengu kama kigezo cha kuepuka mwaliko Mungu anaokupa hicho ndicho kibaya..Na kumbuka Mungu anaujua moyo wako, haiwezekani unapata muda wa kuangalia sinema au kusikiliza umbea masaa 2 au zaidi kila siku lakini muda wa kumtafakari Mungu au kusoma Neno lake au kuhudhuria kwenye nyumba yake angalau mara moja kwa wiki huna…kwa kisingizio una majukumu Fulani? Wiki nzima ulikuwa buzy na kazi umechoka,..Biblia inasema Mungu hadhihakiwi, apandacho mtu ndicho atakachovuna.

Wagalatia 6:7 “ Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele”.

Unapoisikia Injili wakati huu ya kukualika kwenye ufalme wa mbinguni, inayokuambia utubu na uache dhambi na rushwa, na utapeli, na wizi, na ukahaba na wewe unaanza kusema siwezi kuacha kufanya hivyo vitu kwa wakati huu au kubadilika sasa, nina majukumu, Nipo kwenye mipango ya Harusi sina hela, Nipo nasomesha Watoto, Nina viwanja vimewekewa dhamana, nina mkopo ninatakiwa niushughulikie, hata jumapili nakuwa bize sana siwezi kuhudhuria kanisani, bado natafuta fedha za kujenga, mwezi wote huu nitakuwa bize sitapatikana, nitasafiri…

Ndugu, hicho ndio kitu kisichompendeza Mungu, kutoa UDHURU!..Nafasi yako ya wokovu atapewa mwingine! Ambaye asikiapo mara moja tu ataacha!..usidhani Mungu anafurahishwa na udhuru unaoutoa. Kaingia gharama kubwa kukuandalia Karamu yake mbinguni halafu leo, unamwangusha kwa udhuru wako, Vitu unavyovihangaikia vyote vinapita (1 Yohana 2:17)..Na mwaliko huu unaoalikwa leo ni wa muda tu! Hautadumu milele.

Kuna Neema kubwa sana sasa hivi Mungu kaiachilia katika Bara la Afrika, Roho wa Mungu sasahivi anafanya kazi sana Afrika kushawishi watu wamgeukie Mungu kwa nguvu kubwa sana ya ushawishi, ambayo hiyo haipo mabara mengine, ndio maana kwa sehemu kubwa utaona hofu kubwa ya Mungu humu Afrika, mabara mengine ni ngumu sana mtu kushawishika kuigeukia injili, ni kwasababu gani?…Ni kwasababu ile nguvu ya ushawishi (Neema) haipo kwa wingi kama huku, Injili ilianzia Asia na Ulaya na kuzunguka kwenye mabara yote na inamalizikia na Afrika…Na ikitoka huku inarudi Israeli, baada ya hapo ule mwisho unakuwa umefika..Ugumu wa kuiamini injili tunaouona sasa kwenye mataifa yaliyoendelea na utahamia huku pia hivi karibuni wakati kanisa limenyakuliwa, kutakuwa hakuna ile nguvu yakuvutwa tena kwa Mungu, Itahamia Israeli.

Sasa kwanini unaichezea hii Neema iliyopo Afrika sasa?..Neema ambayo inakupa Ushahidi wote ndani ya moyo wako kuwa Mungu yupo, utafika wakati itakuwa ni ngumu hata kuamini kuwa Mungu yupo,..ndicho kinachotokea kwa watu wa mabara mengine, kwasababu anayemfanya mtu amwamini Mungu ni Mungu mwenyewe, sasa akiondoka utamwaminije?, utamfuataje?, utatubuje? (Yohana 6: 44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka).

Wakati utafika Bwana ataingiza kwa nguvu wale ambao hawaujui ukristo kabisa, usishange moja ya hizi siku kuwaona waislamu wengi wanamgeukia Kristo, wahindu wale ambao ni waabudu ng’ombe, wanaokoka ghafla ghafla tu, watu wasioamini Mungu wapagani wanamjia Kristo kwa kasi, ukishaona hivyo ujue kuwa, tayari watu wameshakatwa. Na mambo hayo tumeshaanza kuyaona sasahivi yakiongezeka kwa kasi. Hapo ndipo wengi watatamani kuingia lakini itashindikana,

Mathayo 22:10 “Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi ikajaa wageni.

11 Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi.

12 Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Naye akatekewa.

13 Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

14 Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.”

Kama hujatubu, usiuchezee huu muda, ambao wenzako waliokuzimu wanatamani hata dakika moja tu watengeneze mambo yao na Mungu wanakosa.. unayo nafasi sasa ya kufanya hivyo, pale ulipo tubu kwa kumaanisha kuziacha dhambi ulizokuwa unafanya kisha tafuta ubatizo sahihi wa kuzamishwa mwili wote na kwa jina la Bwana Yesu kwa ajili ya ondoleo la dhambi na Bwana mwenyewe atafanya yaliyosalia kwa kupitia Roho wake Mtakatifu. Nawe utakuwa umeanza mwendo mpya na Bwana, hata kufikia karamu yake kuu aliyowaandalia watu wake tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Pia kwa Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba hizi…

+225693036618 / +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Zinazoendana:

KARAMU YA MWANA-KONDOO.

NDOA NA HARUSI TAKATIFU.

UMEIZALIA MATUNDA MIAKA 4 YA NEEMA ULIYOPEWA?

JINSI YA KUITUMIA VYEMA NEEMA YA MUNGU ILIYO JUU YANGU.


Rudi Nyumbani

Print this post

DAMU YA ZAKARI BIN BARAKIA.

Mathayo 23:29 “Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki,

30 na kusema, Kama sisi tungalikuwako zamani za baba zetu, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii.

31 Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii.

32 Kijazeni basi kipimo cha baba zenu.

33 Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?

34 Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;

35 hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu.

36 Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki.”

Bwana Yesu aligusia vifo vya hawa watu wawili kama mfano alipokuwa anazungumza juu ya hukumu itakayowapata waandishi na mafarisayo na wote walio wanafki, (Ambao kwa sasa inawalenga viongozi wote wa kidini walio wanafiki katika kazi ya Mungu). Kama alivyosema Damu za wenye haki wote zitachanganywa na kuletwa juu yao. Ikianzia kwa Habili, mpaka kwa Zakaria bin Barakia. Wengi wetu tunafahamu habari ya Habili Jinsi ndugu yake alivyomuua kwa jambo moja tu ambalo ni wivu. Kaini baada ya kuona sadaka ya ndugu yake imekubaliwa na ya kwake imekataliwa, moja kwa moja akaamua kumuua ndugu yake, “tukose wote”. Hivyo kwa kuwa Habili alikuwa ni mwenye haki na damu yake imemwagika pasipo kuwa na sababu ya msingi au hatia yoyote, biblia inatuambia…japo alikufa lakini bado anaendelea kunena, kwa namna nyingine ni kuwa damu yake bado inalia katika ardhi…

Waebrania 11:4 “Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, IJAPOKUWA AMEKUFA, ANGALI AKINENA.”

Soma pia Waebrania 12:24,..utathibitisha unenaji wa damu ya Habili. Yeye alikuwa ni mfano mmojawapo aliowakilisha watu wenye haki, waliouawa tangu kuweka misingi ya ulimwengu hadi mwisho wa dunia, na wote hao damu zao zinanena mfano huo huo kama ya Habili mahali Fulani.

Sasa mtu mwingine ambaye tunaona Bwana akimgusia tena katika habari hiyo ya mapatilizo ya damu, ni ZEKARIA, wengi wanamchanganya na Yule Zekaria mwana wa Berekia, aliyeandika kitabu cha Zekaria, lakini tukichunguza kwa undani habari Bwana Yesu aliyokuwa anaizungumzia hapa, haikumuhusu yeye bali ilimuhusu Zekaria aliyekuwa kuhani wa kipindi cha mfalme Yoashi wa Yuda , mwana wa Yehoyada enzi za wafalme. Huyu Yehoyada Mungu alimpa umri mrefu kwa jinsi alivyoijali nyumba ya Mungu na uzao wa Daudi na kuwaongoza watu katika njia za kweli, aliishi miaka 130, Hivyo Zekaria inawezekana alikuwa ni mjukuu wake, ikumbukwe kuwa biblia sehemu nyingi haielezi “Babu na mjukuu”, bali wote wanaitwa “watoto wa”. Hivyo Zekaria bin Barakia Bwana Yesu aliyekuwa anazungumzia hapo ni ndiyo huyu Zekaria mwana wa Yehoyada.

Sasa huyu Yehoyada ambaye alikuwa ni kuhani aliyemcha Mungu sana, kabla ya kufa kwake watu walimcha Mungu, lakini siku alipokufa tu, mfalme na watu wote wakakengeuka waakanza kuabudu masanamu, hata nyumba ya Mungu iliyokuwa inaendelea katika ukarabati ikasitishwa..Wakaanza kufanya maovu, ndipo Zekaria sasa mtoto wake akatumwa na Mungu kwenda kuwaonya, tusome:

2 Nyakati 24:17 “Hata baada ya kufa kwake Yehoyada, wakuu wa Yuda wakamwendea mfalme, wakamsujudia. Naye mfalme akawasikiliza maneno yao.

18 Wakaiacha nyumba ya Bwana, Mungu wa baba zao; wakatumikia maashera na sanamu; ghadhabu ikawajia Yuda na Yerusalemu kwa sababu ya hiyo hatia yao.

19 Hata hivyo akawapelekea manabii, ili kuwarudisha kwa Bwana; nao wakawashuhudia; lakini hawakukubali kuwasikiliza.

20 Na roho ya Mungu ikamjia Zekaria, mwana wa Yehoyada, kuhani; naye akasimama juu ya watu, akawaambia, Mungu asema hivi, Kwani ninyi kuzihalifu amri za Bwana, hata msiweze kufanikiwa? Kwa kuwa mmemwacha Bwana, yeye naye amewaacha ninyi.

21 Basi, wakafanya shauri juu yake, wakampiga kwa mawe kwa amri ya mfalme katika ua wa nyumba ya Bwana.

22 Basi hivyo mfalme Yoashi hakuukumbuka wema, ambao Yehoyada, baba yake, alimfanyia, bali alimwua mwanawe. Naye alipokufa, alisema, BWANA NA AYAANGALIE HAYA, AKAYATAKIE KISASI.”

Kama tunavyosoma hapo wakati Zekaria anakufa kwa kupigwa mawe, alisema maneno hayo “BWANA NA AYAANGALIE HAYA, AKAYATAKIE KISASI.”. Jambo hili hawakufahamu ni jinsi gani lilimuudhi Mungu. Ingekuwa ni heri waishie kuwaua tu wenye haki, lakini wanafika mpaka hatua ya kuwaua makuhani wake na kibaya zaidi wanawaua katika nyumba ya Mungu, mbele ya macho ya Mungu.

Na ndio maana tunaona mamia ya miaka mbeleni Bwana Yesu anawakumbushia wale mafarisayo habari ile ile wasidhani kuwa imesahauliwa, hakuna kilichosahaulika. Aliigusia hii mifano miwili iliyohai kuwakilisha na wengine wote waliotendewa na watakaokuja kutendewa huko mbeleni mambo kama hayo:

Tukisoma katika 

Ufunuo,6:9 “Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.

10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?

11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao”.

Ndugu, Kumbuka kuwa wayahudi wakati wa Dikteta Adolf Hitler waliuliwa kikatili bila hatia yoyote, waliuliwa kwasababu wao ni wayahudi tu, kwasababu Mungu aliwachagua hao basi, hakuna kosa lolote walilolifanya ni WIVU tu kama ilivyokuwa kwa Habili, sasa hawa leo hii roho zao zinalia chini ya madhabahu, zikitaka kisasi kilipizwe..Na sio juu ya waliokufa, hapana bali juu ya hao waliojuu ya nchi, yaani wale waovu waliopo sasa.

Vilevile, tangu kipindi cha mitume hadi kipindi cha matengenezo ya kanisa, historia inarekodi, zaidi ya watakatifu wa Mungu milioni 68 waliuliwa kikatili, na kibaya zaidi asilimia kubwa waliotekeleza shughuli hiyo walikuwa ni viongozi wa kidini ya kikatoliki..Maneno yale yale ya Bwana yanatimia hapo..

Ndugu, tutawezaje kupona kama leo hii hatutauthamini wokovu, kumbuka, mtu yoyote asiye wa Kristo tayari huyo ni adui wake. Anatekeleza ilani ya ufalme wa giza, unashirikiana na matendo ya giza, hata kama hajui…hivyo na wewe pia ikiwa upo nje ya wokovu damu hizi nyingi za watakatifu zitatakwa juu yako. Tubu leo Bwana Yesu akufanye kuwa askari wa ufalme wa mbinguni. Shetani hakupendi, leo hii unayopumzi ni kwasababu Mungu amekuhurumia pengine utubu leo. Lakini wale wasiotaka kutubu tukiachilia ziwa la moto kuna wakati utafika wakiwa hapa hapa duniani watazinywa hizo damu za wenye haki.

Ufunuo 16:4 “Na huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji; zikawa damu.

5 Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi;

6 kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; nao wamestahili.

7 Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, ni za kweli, na za haki, hukumu zako.”

Bwana akubariki. Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.

Pia kwa Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +22589001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Zinazoendana:

JE! DAMU INA UMUHIMU WOWOTE KATIKA MAISHA??

DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?

MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.

ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU:

UFUNUO: Mlango wa 6


Rudi Nyumbani

Print this post

MKATAE SHETANI NA MAWAZO YAKE YA KIBINADAMU.

Marko 8:31 “Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupatikana na mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka.

32 Naye alikuwa akinena neno hilo waziwazi. Petro akamchukua, akaanza kumkemea.

33 Akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”

Katika habari hiyo tunajifunza mambo mengi, jambo la kwanza tunaloweza kujifunza hapo ni jinsi ya kushughulika na roho ya uadui inayotutafuta kila kona, shetani ni adui yetu mkubwa.. na anapenda kutumia Zaidi watu kutushambulia, kutuumiza, hata wakati mwingine kutafuta kutuangamiza na kutuua.. na sisi tukikosa ufahamu na shabaha tunaweza kujikuta tunajibu mashambulizi isivyopasa…tunakipiga chombo cha muhusika badala ya mhusika mwenyewe….badala ya kumdhuru mrusha mkuki, unajikuta unatafuta kuidhuru mikuki.

Katika tukio hilo tunaona Bwana Yesu haraka sana alishajua ni shetani anazungumza ndani ya Petro, pasipo hata Petro kujijua kama anatumika na shetani, yeye alijua tu Bwana Yesu anahuzuni hivyo anahitaji faraja..kwahiyo wazo lilimjia kuwa anahitaji kumfariji Yesu…lakini hakujua kuwa hilo wazo ni kinyume na maandiko…Maandiko yanasema “ni lazima mwana wa Adamu asulubiwe na siku ya tatu afufuke”..

kwahiyo wazo lingine lolote litakaloibuka kinyume na hilo ni kutoka kwa yule Adui……….Kumbuka sio kwamba shetani alimvaa Petro kama nguo na kuanza kuzungumza ndani yake hapana!, aliyekuwa anazungumza pale ni Petro mwenyewe isipokuwa hilo wazo ndio lilitoka kwa shetani, na kumbuka shetani ana uwezo wa kumtupia mtu yeyote mawazo yake, awe mtumishi wa Mungu asiwe mtumishi wa Mungu..na mtu asiyekuwa na Neno vizuri ndani yake ni rahisi kukubali wazo la shetani pasipo kujua kuwa ni wazo la shetani. Ndicho kilichomtokea Petro hakuwa na Neno la kutosha ndani yake kuweza kuchambua wazo la Mungu ni lipi na la shetani ni lipi.

Na Bwana alipojua ni wazo la shetani hilo ndani ya Petro, hakuanza kushughulika na Petro bali na roho iliyopo ndani ya Petro,..na baada ya kuikemea ile roho au lile wazo la ibilisi, aliendelea kutembea na Petro kama kawaida kwani alikuwa bado ni mwanafunzi wake aliyempenda…Na ile ilimsaidia Petro kuwa makini na chochote anachokizungumza, kukilinganisha na maandiko.

Hivyo na sisi tunajifunza hapo namna ya kushughulika na roho ya uadui, hatupaswi kushughulika na yule mtu, bali na lile wazo au roho ndani ya yule mtu, hapo ndipo vita vyetu vilipo…sio kumchukia yule mtu.

Waefeso 6: 12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”.

Lakini jambo la mwisho la kujifunza ambalo ndio kiini cha somo letu leo ni “MAWAZO YA SHETANI”…

Tukirejea hapo juu mstari wa 33 unasema.. “Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu”.

Hapo Bwana Yesu anafunua ni kitu gani shetani anachowaza au kilichopo ndani ya kichwa chake siku zote…yeye siku zote anafikiria mambo ya duniani tu! (mambo ya wanadamu)…mambo ya kimwili, anawaza siku zote ni namna gani mwanadamu atakuwa anafikiri mambo ya hapa duniani tu!..hatataka mtu awe anafikiria mambo ya kimbinguni ya wakati ujao, yeye ni Maisha ya hapa tu!…hataki mtu afikiri ni nini kitamtokea baada ya kufa! Hataki mtu afikirie kwamba kuna kifo cha ghafla! Hataki mtu afikirie habari za Maisha baada ya haya, ndio maana hapa akamrushia Petro wazo haraka sana kumwambia Bwana hatakufa!. Ili amshawishi ajiwekee hazina hapa duniani na asifikiri mambo yajayo.

Ndugu kama ulishawahi kukaa peke yako na kufikiri ni nini kitakukuta baada ya kufa, ni lazima utakuwa umeona Maisha hayana maana kabisa…hiyo ni hatua ya kwanza ya Mungu kukuvuta kwake, kama ulishawahi kuhudhuria msiba, ndio utajua kuwa Maisha haya hayana maana tunapita tu!..Usipende raha raha tu kila wakati! Kila siku kuhudhuria sherehe na party, hudhuria pia misiba, nenda mahospitini hata siku moja, pita tu! Ujifunze….. shetani hapendi! Wewe uende huko atakuambia aah unakwenda kujitoa kwenye mood tu!..atakurushia wazo la kwenda kujifariji na nyimbo Fulani za kidunia.

Hataki uhudhurie huko kwasababu anajua ukitoka pale utakuwa umepata funzo kubwa sana la Maisha, na hivyo atakukosa, na yeye hataki akukose…shetani anawaza yaliyo ya wanadamu tu! Hataki ufikirie mambo yajayo.

Siku moja jioni nilitoka nyumbani nikawa natembea mtaani tu, nikaenda mbali sana mitaa mipya kidogo, njiani nikawa natafakari Maisha yangu binafsi na mambo mengine ya kawaida..nilikuwa nina amani ya kawaida tu! Lakini nilipita sehemu nikakuta geti la nyumba moja limefunguliwa, na watu wanaingia ndani kwa huzuni, nilibahatika kumwona ndugu mmoja nafikiri atakuwa ni ndugu wa marehemu analia mpaka ameshikwa ndipo nikajua kuwa ulikuwa ni msiba, nami pia nilihuzunika kidogo…nikasema hiyo pia ingeweza kunitokea na mimi pia leo hii…

Kwa kitendo kile, kikanifanya nizidi kuingia kutafakari hatima ya Maisha haya zaidi, likanijia andiko kichwani kutoka katika kitabu cha Mhuhiri

Mhubiri 7:1 “Heri sifa njema kuliko marhamu nzuri; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa.

2 Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake.

3 Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, Maana simanzi ya uso ni faida ya moyo.

4 Moyo wake mwenye hekima umo nyumbani mwa matanga, bali moyo wake mpumbavu umo nyumbani mwa furaha”.

Kujifunza juu ya hatima ya haya Maisha sio kukosa tumaini la Maisha hapana! Bali ni hekima..kwasababu hiyo inaonyesha unayapenda Maisha yako, leo utamwuliza mtu una mipango gani ya baadaye, atakupa mipango ya miaka mingi ya mbeleni sana, na ataanza kujiwekea hazina sasahivi…lakini hatakupa mipango ya maisha baada ya kifo, sasa huyu huwezi kusema anaona mbele kwasababu anayeona mbele lazima avuke Maisha haya, azidi kuona mbele Maisha baada ya kufa, huyo ndio anayeona future yake…

Sasa Huyu ni Sulemani ambaye alikuwa na plani kubwa sana za Maisha yake na aliyekuwa ni Tajiri na mwenye hekima ambaye hakuna mfano wake ndiye anayesema haya maneno …”heri kuiendea nyumba ya matanga kuliko nyumba ya karamu”. Ni heri kusikia habari za misiba kuliko kila siku kusikia habari za shangwe tu na sherehe. Kwasababu kwa habari hizo zitakupa chachu ya kutafakari Maisha baada ya hapa.

Usisikilize mawazo ya shetani ambayo hayo ni kukupa wewe tumaini la mambo ya kiulimwengu tu kila siku, anakwambia hutakufa! Utaishi! Na huku upo bado kwenye Maisha ya dhambi, anakuambia utakuwa na heri na kufanikiwa, wakati unaishi na mke/mume wa Mtu. Na wakati maandiko yanasema wazi kabisa roho itendayo dhambi itakufa…shetani atatumia watu kukufariji kwa kila aina ya faraja, atatumia mpaka wanaojiita watumishi wa Mungu kukupa wewe faraja kwamba hutapatikana na mabaya…na wakati maandiko yanasema kinyume na hayo.

Atasema pia, wakristo hawapitiagi dhiki..ndicho alichomwambia Bwana Yesu, kuwa hatakufa..na wakati maandiko yanasema “ulimwenguni mnayo dhiki (Mathayo 16:33)” na “ tena mtakuwa watu wa kuchukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu”..lakini shetani atakwambia mtapendwa na watu wote…tangu lini mafisadi wakawapenda watu wasio mafisadi kama wao?…Danieli alikuwa ni mtu apendwaye mbinguni lakini duniani alikuwa anachukiwa, na watu waliokuwa wanakula rushwa…Na katika Ukristo ni hivyo hivyo zipo dhiki za hapa na pale, ambazo Bwana alituambia mapema kabisa tutakutana nazo ili tuwe na Amani…zitakapotokea tusihuzunike sana.

Hivyo tunajifunza kuyakataa mawazo ya shetani ambayo yanatusukuma kuyatazama mambo ya ulimwengu huu tu, mambo ya kitambo! mambo ya wanadamu Na kutuzuia kutafakari mambo yajayo. Na tunayakataa mawazo hayo kwa formula moja! Iliyorahisishwa katika Neno lake na hiyo ni kwa kutubu kwa kumaanisha kwanza kuacha dhambi na pili ubatizo sahihi wa kuzama mwili wote na kwa jina la Yesu na tatu Roho Mtakatifu..Roho Mtakatifu akishaingia ndani yako ni kama mlinzi wetu, atayaathiri Maisha yako na kuyapeleka anakotaka yeye, kama vile upepo uvumapo usipojua wewe…

atakukumbusha juu ya hatima ya maisha haya na kukupasha habari ya mambo yajayo…

Na baada ya hapo kilichosalia ni kudumu katika kujifunza Neno la Mungu siku zote za wakati wako zilizosalia hapa duniani…ili uwe na uwezo wa kuzipambanua roho, Petro alikuwa hana uwezo wa kuzipambanua roho kwasababu Neno halikuwa ndani yake, laiti angekuwa analifahamu Neno linalosema kuwa “Mwana wa Adamu ni lazima afe kwa ajili ya dhambi ya ulimwengu” yale mawazo yalipokuja kichwani mwake ya kumfariji Bwana angeyakataa…na yeye mwenyewe angesema moyoni mwake, shetani ondoka ndani mwangu na mawazo yako ya kibinadamu, kwasababu Neno linasema hivi na hivi. Na sisi tunapoyajua maandiko ni silaha tosha, biblia inasema Neno la Mungu ni Upanga wa Roho, linamkata kata shetani vipande vipande.

Bwana akubariki sana.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Ibada basi Wasiliana nasi kwa namba hizi..

+225693036618/ +22589001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

JIHADHARI NA ROHO ZIDANGANYAZO.

JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.

JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?

EDENI YA SHETANI:


Rudi Nyumbani

Print this post

MTI UANGUKAPO, PAPO HAPO UTALALA.


Mhubiri 11:3b “…… Na mti ukianguka kuelekea kusini, au kaskazini, Paangukapo ule mti, papo hapo utalala.”

Maisha yetu yanafananishwa na mti, na tunajua siku mti unapoanguka aidha kwa uzee, au kwa kukatwa, kuanguka kwake kunategemea sana jinsi ulivyokuwa. Hata kama ni mnazi unaoonekana umenyooka kama rula, bado unayo sehemu Fulani umelemea upande mwingine, utajua hilo siku ile unapokatwa wakati unadondoka..Kamwe haiwezekani ukawa sawasawa pande zote, na pia ukishalala pale chini, ndivyo utakavyolala hapo hapo milele, kwasababu mti sio kama viumbe hai vingine vinavyoweza kujongea, hata vikianguka vitasimama..Lakini Mti hautembei wala hausogei, hivyo anguko lake ni la milele.

Vivyo hivyo na sisi tunavyoishi, hapa duniani kama unyakuo hautatukuta, basi tufahamu kuwa kifo tutakutana nacho siku moja..Wengi wanasema nikikaribia hicho kipindi nitatubu, nataka nikumbie unapolemea maisha yako yote leo hii ndipo utakapolalia milele siku ile ya kukatwa kwako, huwezi ghafla ghafla tu, ukageukia upande wa pili ingekuwa ni rahisi hivyo Bwana asingekuwa anawahubiria watu injili tangu utoto wao mpaka wanakuwa watu wazima wamgeukie yeye. Si angesubiri tu siku ile wanakufa awahubirie injili waende mbinguni..Haipo hivyo wokovu ni tendo linalogharimu maisha na sio tukio Fulani tu.

Na kama tulivyoona mti unapoanguka unalala hapo daima,iwe ni kaskazini, iwe ni kusini, ndivyo itakavyokuwa baada ya kifo, umeangukia katika uzima utakuwa katika uzima milele, umeangukia katika mauti, utakaa katika mauti daima..Hakuna nafasi ya pili, Wala hakuna nafasi ya katikati.

Hivyo pima maisha yako leo uangalie ni wapi yamelemea kwa sehemu kubwa, na uanze kuyatengeneza upya ili kusudi kwamba hata ikitokea kifo kimekukuta kwa ghafla basi unakuwa na uhakika wa kuangukia mahali salama. Kama bado hujampa Bwana maisha yako, nafasi bado unayo sasa, hapo ulipo tubu na kusema kuanzia leo Bwana ninataka kuegemea kwako, na yeye atakusamehe, kisha kama hujabatizwa nenda kabatizwe, katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji kwa jina la YESU KRISTO, kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako. Na Bwana atakupa Roho wake Mtakatifu kukulinda na kukuongoza sikuzote.

Ubarikiwe sana.

Pia kwa Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

KIFAA BORA CHA MATUMIZI.

JE! UNAWEZA KUBATIZWA NA USIPOKEE ROHO MTAKATIFU?. NA JE! UNAWEZA KUPOKEA ROHO MTAKATIFU KWA KUWEKEWA MIKONO?

TUNAYE MWOMBEZI.


Rudi Nyumbani

Print this post

SI SHETANI BALI NI WEWE. (CHAGUA MEMA)

Moja ya kazi kubwa PIA shetani anayoifanya ni kuhakikisha watu hawaelewi dhambi ni nini?…Na hivyo anatumia nguvu kubwa kuwafanya watu waamini kuwa chanzo cha matatizo yote ni yeye!…hata mtu akifanya uasherati ni shetani! Mtu akiua ni shetani! Mtu akiiba ni shetani!…Lakini wengi hawajui kuwa shetani naye pia hakudanganywa na mtu, hakukuwa na mtu juu yake wa kumdanganya…alijidanganya mwenyewe (moyo wake ulimpoteza mwenyewe Yeremia 17:9).

Sababu ya kutenda dhambi watu wengi ambao hawaelewi huwa wanamtupia shetani…lakini kumbe ni wao..Shetani, anachokifanya yeye ni kupalilia UOVU tu duniani…lakini yeye sio aliyeuumba uovu, Uovu upo katikati yetu uliumbwa na Mungu, kwa makusudi maalumu ya kutambua wema, kwamfano uovu usingekuwepo basi hata wema usingekuwepo, ili kutambua kitu hiki ni kitamu lazima kiwepo kichungu, lakini kama hakuna kichungu, umejuaje kuwa kile ni kitamu?. (Vivyo hivyo na sisi tumeumbiwa tayari mema na mabaya ni sisi kuchagua)…..Na malaika nao waliumbiwa hicho kitu ilikuwa ni kitendo tu cha wao kuchagua…Na shetani na malaika zake wakachagua mabaya (na huko ndiko kuasi), na matokeo yake wakatupwa duniani…

Na huku duniani tayari kulikuwa kuna mti wa mema na mabaya pale Edeni…Kiasi kwamba hata kama shetani asingekuwepo bado Hawa alikuwa anao uwezo wa kuchagua mabaya, kama angetaka……kwahiyo asili ya uovu sio shetani! Uovu ulikuwepo tangu asili, ni kitendo cha watu kuchagua..(pale Edeni shetani alikuwa ni kama dalali tu! Wa kumvutia na kumshawishi mwanadamu achague uovu). Kwahiyo shetani anachofanya sasahivi yeye na malaika zake ni kuipalilia tu ile njia ya ouvu izidi kuwa pana kwa watu….Ukilijua hilo litakufanya kuwa makini kutokufikiria kila kitu chanzo ni shetani.

Kwahiyo mtu anayekwenda kufanya uasherati leo, ni yeye mwenyewe amechagua uovu kwa ushawishi wa nguvu za shetani…zingati hili (Ni huyo mtu kafanya na sio shetani kafanya kwa niaba yake)…Kwahiyo hapo anayestahili kulaumiwa wa kwanza ni huyo mtu, kwasababu kachagua kufanya mabaya…

Ni sawa leo uende sokoni kununua nguo, ukute maduka mawili mbele yako, moja linauza nguo nyeupe lingine nyeusi…na ndani kila mmoja anakushawishi ununue kwenye duka lake…maamuzi ya mwisho yanatoka kwako wewe, na sio kwa mwenye duka…hapo kama utachagua nyeusi au nyeupe na kwenda nyumbani kukuta kasoro, hapo anayestahili kulaumiwa wa kwanza sio muuzaji bali ni wewe ambaye ulikwenda kuchagua…ulipaswa ukague nguo yote kwa makini kabla ya kuinunua, sio kusikiliza tu maneno ya wauzaji na kuamini!

Na ndivyo ilivyo sasa hivi duniani kuna maduka mawili, moja linauza mavazi meupe(ya uzima wa milele), na lingine meusi ni jukumu lako wewe kuchagua lipi linakufaa…kila moja lina watu ndani yake wanaokushawishi na kukuvutia, maamuzi ya mwisho unatoa wewe..sio muuzaji!…Muuzaji anakazi tu ya kukudalalia basi! Mambo mengine unafanya wewe, uchaguzi unafanya wewe na gharama unaingia wewe.

Leo utasikia mtu anakwenda kuzini, halafu anakwambia ni shetani kafanya vile, atakuambia shetani kanipitia tu!… hajakupitia ndugu ni wewe umechagua mwenyewe uovu, kwa kukubali ushawishi wake…Kama ingekuwa ni shetani, basi Mungu asingesema “siku ile kila mtu atasimama mbele ya kiti cha hukumu kutoa hesabu ya mambo yake”…asingesema hivyo, badala yake angesema “shetani atasimama kueleza ni kwanini kawaingia watu na kuwalazimisha wafanye dhambi”…Lakini siku ile kila mtu atahukumiwa kwa aliyoyatenda…kwanini? kwasababu si shetani aliwalazimisha watu kutenda, bali ni watu kwa uchaguzi wao wenyewe walichagua uasi…

Yohana 3: 19 “Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu”.

Kwahiyo mtu yeyote anayetenda dhambi, ni katenda dhambi kwa idhini yake mwenyewe baada ya kuzidiwa na ushawishi wa shetani kufanya hilo jambo. Hivyo hapo shetani ni mtu wa pili kulaumiwa baada yake yeye…wa kwanza kabisa kulaumiwa ni yeye na ndio afuate shetani.

Hebu tafakari juu ya hili ili upate kuelewa kuwa kuna upofu Fulani unaendelea…..Mtu atakapotenda jambo fulani jema, labda amsaidie maskini hatasema ni Mungu kafanya lile jambo…atasema ni yeye kafanya…ukimwuliza imekuaje umefanya hivyo, atakwambia nimeguswa tu kufanya hilo jambo! Na tena ukimwuliza ni wewe au Mungu ndio kafanya hilo jambo atakwambia ni yeye ndiye aliyefanya 100%….. Mungu ni kama kamsaidia tu…na tena ataamini kuwa anastahili baraka kutoka kwa Mungu kwa alichokifanya lakini huyo huyo mtu hebu afanye uasherati utasikia anasema ni shetani huyo!..sio mimi ni shetani, utaona malaumu yote na sababu zote anamtupiwa shetani na kuanza kumlalamikia Mungu kwanini hakumwua shetani…lakini alipotenda mema hakusema ni Mungu kafanya bali alisema ni yeye, tena alipokea utukufu kutoka kwa watu kuwa yeye ndiye aliyefanya ule wema!.

Ndugu kama ni haki yako kupata baraka kutoka kwa Mungu kwa kutenda mema…jua pia ni haki yako kupata laana kutoka kwa Mungu kwa uovu unaoufanya!..Uovu unaoufanya, Mungu wala shetani hawahusiki, ni wewe ndio unaoamua kuufanya..wao ni kama washauri tu!..Ndio maana Mungu pia atawapa thawabu watakatifu wake watakaoshinda mbinguni, siku ile hatajipa yeye thawabu, atawapa watakatifu kwasababu ni wao ndio walioamua kufanya mema, sio Mungu.

Kumbuka pia unapotenda mema ni Mungu ndiye atakubariki, na unapotenda mabaya ni Mungu ndiye atakulaani na sio shetani, kwasababu sio shetani aliyeuumba uovu, ndio maana unaona pale Edeni baada ya Adamu na Hawa kuasi ni Mungu ndiye aliyewalaani na sio shetani!…aliyesema tutakula kwa jasho sio shetani ni Mungu!…aliyesema tutazaa kwa uchungu sio shetani ni Mungu! Aliyeilaani ardhi sio shetani ni Mungu!. Kwahiyo ukitenda uovu leo hii ni umeuchagua kwa hiyari yako mwenyewe na hivyo utakuwa unaishi katika laana kutoka kwa Mungu. Shetani hahusiki hapo!.

Wengi wanawalaumu pia Adamu na Hawa kuwa ndio sababu ya mambo yote..Ni kweli wao walichangia kuifanya njia ya upotevu iwe pana Zaidi lakini ni vyema ukafahamu kitu kimoja…hata kama Adamu na Hawa wasingekula lile tunda, kusingemzia shetani kuwajaribu Watoto wao, na hata kama watoto wao pia wasingekula tunda kwa kukataa ushawishi wa shetani pia isingemzua shetani kuwajaribu wajukuu wao na vitukuu vyao…na ingeendelea hivyo hivyo mpaka mwisho wa vizazi vyote, shetani angekuwa anandelea kuwajaribu tu wanadamu….hata siku wewe unazaliwa ungemkuta shetani naye pia asingeacha kukujaribu kula tunda hata kama vizazi vyako vya nyuma vyote vimeshinda…Kwahiyo hata kama Adamu na Hawa wasingenaswa pengine ungeweza kunaswa wewe!…uthibitisho ni hizo dhambi za makusudi unazozifanya sasa….

Ndio maana huoni mahali popote kwenye Biblia Mungu akiwalaumu Adamu na Hawa, baada ya kutoka pale Edeni..kwasababu wote tumefanya dhambi… Hivyo geuza mtazamo wako wa kuwasingizia baadhi ya watu na shetani kuwa ndio chanzo cha matatizo Fulani, ni kweli wanaweza kuwa wamehusika kwa sehemu Fulani…lakini sehemu kubwa ya maamuzi ipo kwako!!.

Kristo leo anagonga moyoni mwako umegeukie kumbuka shetani anapenda umsingizie yeye ili siku ile ya hukumu ujute! Useme laiti ningepata huu ufahamu angali nipo duniani nisingekuwa mtu wa visingizio…Chagua mema leo usichague mabaya yaletayo laana. Ni rahisi kuchagua mema, yupo mmoja ambaye aliweza kuchagua mema, yeye ndiye anayeweza kutufundisha na sisi namna ya kuchagua mema…na huyo si mwingine Zaidi ya YESU KRISTO, aliyemzungumziwa mahali Fulani hivi…

Isaya 7: 14 “Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.

15 Siagi na asali atakula, WAKATI AJUAPO KUYAKATAA MABAYA NA KUYACHAGUA MEMA”.

Huyu ndio Mkuu wa Uzima, aliyebeba wokovu, hakuna aliyemfuata yeye akajuta, alituambia maneno haya..

Mathayo 11: 27 “Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.

28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.

Hivyo tunamtii na kumfuata kama tulivyo, na mizigo yetu.. kama ni mwasherati unaenda kama ulivyo, kama ni mtazamaji wa pornography unaenda kama ulivyo, kama ni msengenyaji vivyo hivyo, kama ni mlawiti, shoga, mlevi, mtoaji mimba, mwizi,muuaji, mla rushwa, mcheza kamari, mwenye huzuni, mwenye msongo wa mawazo, uliyefungwa na nguvu za giza,..msogelee leo, utue mzigo wako pale… hapo ulipo Tubu kwa kumaanisha kuacha kabisa kufanya hayo mambo, na yeye ni mwaminifu atakusamehe…

Na baada ya kufanya hivyo ili ukamilishe toba yako nenda katafuta ubatizo sahihi wa kuzama mwili wote katika maji na kwa jina la YESU KRISTO, kwaajili ya ondoleo la dhambi zako kulingana na Matendo 2:38, dhambi zinakamilika kuondolewa kwa ubatizo sahihi…na baada ya Hapo Roho mwenyewe ataingia ndani yako na kukuongoza katika kuijua kweli yote ya Biblia na kukusaidia katika kuchagua yaliyo mema na kukataa mabaya..na utakuwa na uhakika wa uzima wa milele.

Kumbuka tunaishi siku za mwisho, siku yoyote Parapanda inalia, na watakatifu watanyakuliwa kwenda juu mbinguni, tujitahidi mimi na wewe tuwe miongoni mwao walioalikwa Karamuni.

Bwana akubariki sana, Tafadhali share kwa wengine ujumbe huu.

Pia kwa Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAP


Mada Zinazoendana:

SHETANI NI NANI?

‘’MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI’’..NA NDIVYO ILIVYO KWA UASHERATI

MKATAE SHETANI NA MAWAZO YAKE YA KIBINADAMU.

DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI:


 

Rudi Nyumbani

Print this post

SIKU YA TAABU YA YAKOBO.


Yeremia 30:7 “Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo.”

Biblia inasema ni siku ambayo haiwezi kufananishwa na siku yoyote katika historia ya siku zote za dunia ambazo zilishawahi kuwepo mambo ambayo yataenda kulikuta Taifa la Israeli, Hicho ndio kipindi cha taabu kuu ambacho Danieli alionyeshwa;

Danieli 12: 1 “ Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile”.

Na Bwana wetu Yesu Kristo alikuzingumzia pia, kuweka msisitizo wa uzito wa dhiki hiyo ..

Mathayo 24:21 “Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.

22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.”

Na cha kuzingatia ziadi ni kuwa dhiki hii haitakuja wakati wowote isipokuwa wakati ambapo Israeli imesharudi na kuwa kitu kimoja kama zamani za kale za mfalme Daudi na Sulemani.

Yeremia 30:1 “Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema,

2 Bwana Mungu wa Israeli, asema hivi, ya kwamba, Uyaandike kitabuni maneno hayo yote niliyokuambia.

3 Kwa maana, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapowarejeza watu wangu wa Israeli na Yuda waliofungwa, asema Bwana; nami nitawarudisha hata nchi niliyowapa baba zao, nao wataimiliki…………

7 “Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo.”

Na jambo hilo lilitimia mwaka 1948, baada ya kukaa zaidi ya miaka 2500 bila kuwa taifa huru, Israeli sasa ni taifa huru, na sisi ni mashahidi kuwa tumeshaanza kuona mwanzo wa utungu wa mambo hayo, kipindi cha vita ya pili vya dunia jinsi wayahudi walivyouliwa kikatili na Dikteta wa kijerumani Adolf Hitler bila sababu yoyote, tafakari jinsi wanawake na watoto walivyokuwa wanachukuliwa uchi, na kudanganywa kuwa wanaenda kuogeshwa kumbe wanafungiwa kwenye mabafu ya gesi za sumu (Gas chambers), na huko ndani kwenye vyumba hivyo, vya giza inatupwa gesi moja kali ijulikanayo kama Zyklon B, inawaua watu kama kuku waliochinjwa, huku damu zikitoka midomoni na puani, ndani ya dakika 4 tu zinakuwa ni maiti zilizolala chini. Na mauaji mengine ya kikatili ukifuatilia katika historia utayaona. Wayahudi zaidi ya milioni 6 waliuliwa kwa namna kama hizo kikatili.

Sasa huo ni mfano mdogo sana,(mwanzo wa utungu) kwa hiyo dhiki itakayokuja huko mbeleni. Mambo yatakuwa mabaya zaidi, kutakuwa kuna mateso ya ajabu ambayo hayajawahi kufanyika popote, kama tu wakati wa Hitler watu walikuwa wanachukuliwa kwa marika tofautitofauti na wanawekwa kwenye barafu wakiwa uchi na wanaangaliwa mpaka wafe, huku wengine wakichukua data, kuchunguza ni rika lipi linawahi kufa katika hali ya ubaridi (na hiyo biblia inaiita tu ni mwanzo wa utungu)…unadhani itakuaje utungu wenyewe ukianza?….pengine watu watalishwa nyama za miili yao wenyewe wangali wakiwa hai….Dhiki hii Mungu atairuhusu kwa watu wake Israeli, na watu wa mataifa wachache ambao walibaki kwenye unyakuo….na hiyo yote Mungu ameruhusu kwa makosa ya Israeli ukiendelea kusoma mistari inayofuata ya hiyo Yeremia 30 utaona, na atakayetekeleza hilo zoezi ni mpinga-Kristo, Wayahudi (Waisraeli) wataadhibiwa hivyo lakini baadaye Mungu atawaokoa..

Lakini mpaka hayo yote yatokee, Kanisa la Kristo litakuwa limeshanyakuliwa, mbinguni, Bibi-Arusi sikuzote haandaliwi kupitia dhiki bali anaandaliwa kwa ajili ya sherehe, na ndivyo itakavyokuwa kwa Bibi-arusi wa Kristo, wakati wote huu ambao yupo duniani sasa anaandaliwa kwa ajali ya karamu ya mwana-kondoo, ambayo Kristo amekuwa akituandalia mbinguni kwa miaka 2000 sasa, Siku watakapoisikia paraparanda ya Mungu ikiwaita, muda huo huo watageuzwa kufumba na kufumbua na kuwa na miili ya utukufu ya kimbinguni, wataungana na wale watakatifu waliolala, kisha kwa pamoja watapaa zao mbinguni, kumfurahia Bwana wao. Hivyo watakaopitia hii dhiki ni wale wanawali wapumbavu, ambao hawakujiweka tayari kwa ajili ya kumlaki Bwana wao akiwa hapa duniani….Hao ndio watakaojumuika na wayahudi,

Mathayo 25:6 “Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.

7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.

8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.

9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.

10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.

11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie.

12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.

13 Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.”

Utajisikiaje, siku ile unaona wenzako wapo juu mbinguni karamuni, halafu wewe umeachwa?, umetengwa na uso wa Mungu milele, Ikiwa neema unaichezea leo, usidhani itakuwepo kipindi kile, wakati huo neema ya Mungu itakuwa kwa wayahudi watu wake, kupigwa kwao upofu leo ni ili wewe na mimi tutubu tumgeukie Mungu, (soma Warumi 11:8-36 )wakati ule ukifika Mungu hatakuwa na habari tena na wewe, au mtu yoyote wa mataifa, bali watu wake, wateule wake wayahudi. Na hao ndio Bwana atakaowakoa.

Hizi ni nyakati za mwisho ndugu, usipumbazwe na huu ulimwengu unaopita, angalia ni faida gani unakuahidia maisha baada ya hapa?, majira yanabadilika haya, matukio yanayotokea duniani, ni kuonyesha kuwa dunia imeshafika OMEGA. Acha kusuasua kwenye njia mbili, huu sio wakati wa kuhubiriwa injili ya kubembelezwa tena, mkabidhi Kristo maisha yako leo, tubu kabisa na umaanishe kumfuata, na yeye ni mwaminifu na mwenye huruma, hata kama dhambi zako ni nyingi kiasi gani ataziweka mbali na wewe. Tubu ukabatizwe, Upokee Roho Mtakatifu.

Bwana akubariki.Tafadhali “Share” Ujumbe huu kwa wengine. 

Pia kwa Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAP


Mada Zinazoendana:

MZEITUNI HALISI UTAKAPOPACHIKWA.

ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU:

MWEZI NI ISHARA GANI KWETU?.

WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA.

ULE MFANO WA WANAWALI 10 (MATHAYO 25), WALE WATANO HAWAKUWA NA MAFUTA YA ZIADA KATIKA CHUPA ZAO JE YALE MAFUTA YA ZIADA YANAWAKILISHA NINI?


Rudi Nyumbani

Print this post

JE! KUBET NI DHAMBI?

Ili kujua kama ku-BET ni dhambi au la! Ni vizuri kwanza kufahamu mapenzi ya Mungu ni yapi?…Huwezi kujua kipi kisichompendeza Mungu kama hujui kipi kinachompendeza…Sasa Mungu alivyotuumba watu wake na viumbe vyake vyote hata Wanyama, alituwekea kitu kinachoitwa dhamira ndani yetu…Hii dhamira kazi yake ni kutulinda sisi tusiende kinyume na mapenzi ya Mungu tunapoishi…Na ipo kwa viumbe vyote (wanadamu na wanyama)..Ndani ya hii dhamira kumefungiwa sheria za Mungu. Kwahiyo pasipo hata Mungu mwenyewe kuzungumza na mtu juu ya jambo Fulani tayari ile dhamira iliyopo ndani yake ina uwezo wa kukamata na kuhisi jambo ambalo sio sawa.

Kwamfano utaona, Simba anauwezo wa kula swala na kumrarua kikatili, lakini simba huyo huyo hamli mtoto wake…ni kwanini? Ni kwasababu dhamira iliyopo ndani yake inamshuhudia kuwa jambo hilo sio sawa…simba hajapewa sheria yoyote na Mungu, lakini ndani ya moyo wake kumefungiwa sheria, kwa kupitia dhamira aliyo nayo. Kadhalika huwezi kuona mbwa au mnyama yoyote analala na mnyama wa jinsia moja naye…

Ni kwanini? ni kwasababu ya dhamira iliyopo ndani yao..inayowashuhudia kuwa jambo Fulani sio sahihi, sio kwamba hawana hisia! Wanazo hisia lakini hawawezi wakavuka hiyo mipaka.

Na wanadamu ni hivyo hivyo, kuna kitu kinaitwa dhamira ambayo hiyo imebeba sheria za Mungu ndani yake, kiasi kwamba mtu anaweza asizijue kabisa amri za Mungu, lakini bado akazitimiza vile vile..

Haihitaji biblia kujua kuwa uuaji ni mbaya, au kuwatesa Watoto wako ni vibaya…Hiyo sheria tayari mtu anazaliwa nayo moyoni mwake…ndo maana hata wanyama pamoja na ukatili wao wote hawayafanyi hayo, hawasomi biblia lakini wanazitimiza sheria za Mungu….Haihitaji biblia kujua kuwa utoaji mimba ni vibaya, au kumdhulumu mtu ni vibaya, hiyo tayari mtu angejua hata kama hajawahi kusikia habari za Mungu. Haihitaji sheria kufahamu kumuoa dada yako/kaka yako wa damu ni makosa, hiyo tayari ipo ndani yako, hata hizo hisia zenyewe hazipo licha tu ya dhamira kukushuhudia.

Sheria ilipokuja, kazi yake ni kuitoa hiyo hiyo sheria kutoka katika roho na kuileta katika maandishi..Na hiyo ni kutokana na ugumu wa mioyo yetu, unajua hata watoto wanapotumwa dukani, na wanaonekana ni wazito kidogo kuelewa au wanasahausahu sahau, basi wazazi wanaamua kuwaandikia kikaratasi kidogo cha maelekezo ili wasisahau. Na sheria ilikuja kwa namna hiyo hiyo. Ililetwa kutufanya tuyakumbuke yale tuliyokuwa tumeyasahau katika roho zetu na dhamira zetu..

Sasa Watu waliokuwa wanaishi wakati wa Nuhu, walikuwa hawana sheria yoyote, Maana sheria ililetwa na Musa miaka mingi sana baada ya gharika?..Sasa unaweza kuuliza kama kulikuwa hakuna sheria, wale watu walihukumiwa kwanini?…Walihukumiwa kwa dhamira iliyokuwepo ndani yao…walikuwa wanafanya mambo ambayo ndani ya dhamira zao walikuwa wanajua kabisa sio sawa…lakini waliendelea kuyafanya! Hivyo ikawa dhambi kwao,(Warumi 1:17-30) Na Mungu akawaangamiza wote kwa gharika. Kwahiyo sheria hii ambayo tayari ipo ndani ya dhamira zetu ndio inayojulikana kama INJILI YA MILELE (Ufunuo 14:6). Kwa maelezo marefu juu ya injili hii ya milele  Bofya hapa >> INJILI YA MILELE

Sasa mpaka sasahivi hii INJILI YA MILELE ipo, Kuna vitu ambavyo havijazungumziwa hata kwenye Biblia takatifu lakini mtu akiona tu! Anajua hiyo sio sawa machoni pa Mungu..Mfano wa vitu hivyo ni Uvutaji wa sigara, utoaji mimba, mtu anayetoa mimba anajua kabisa ndani ya moyo wake anaua na anafanya jambo lisilo sahihi…ingawa ukitafuta mahali popote kwenye biblia palipoandikwa utoaji mimba ni dhambi huwezi kupata…Lakini mtu anayefanya hivyo anajua kabisa na anauhakika ndani ya moyo wake anamkosea Mungu, na ndivyo ilivyo…au mtu anayetumia madawa ya kulevya…anajua kabisa jambo afanyalo sio jema…

Jambo lingine ni mtu anayefanya masturbation, ukienda kumwuliza mtu anayefanya masturbation unajua ni kosa kufanya hivyo, wala hatakubishia Zaidi ataogopa na atakuuliza namna ya kuacha!…lakini ukienda kwenye maandiko ukitafuta mahali popote pamezungumzia suala la masturbation kuwa ni dhambi hutapaona!…lakini kwanini yule mtu ndani ya moyo wake anauhakika kuwa anachokifanya sio sahihi?..

Ni kwasababu ya dhamira iliyopo ndani yake! (Sheria ambayo Mungu alishaiweka ndani ya moyo wake) inayomshuhudia jambo sahihi na lisilo sahihi…Au leo hii ukimfuata mtu anayeangalia pornography, atakwambia kabisa mimi nafanya makosa, wala hatakubishia wala kukuuliza ni wapi pameandikwa hivyo kwenye biblia?…wala hatataka kujua, yeye anachojua kuwa anafanya dhambi, jambo lisilompendeza Mungu, hilo tu!…Au mtu anayecheza kamari, anajua kabisa jambo afanyalo sio sawa, na anajua kabisa huo mchezo ni wa kishetani, anajua kabisa ni mchezo wa dhuluma ambao wakati mwingine unaweza kuhatarisha, uchumi wake, na usalama wake, anajua kabisa Mungu hayupo katikati ya huo mchezo, Na dhambi nyingine nyingi zinazofanywa na wanadamu ndio hivyo hivyo, hazihitaji biblia kuzihakiki, tayari zimeshajihakiki zenyewe ndani yetu.

Sasa tukirudi kwenye suala la KU-BET na lenyewe ni hivyo hivyo, Kubet ni kamari, isipokuwa iliyohalalishwa na nchi.

Hakuna mahali popote katika biblia imezungumzia habari za kubet…Lakini ipo INJILI YA MILELE ndani ya kila mtu…Inayokushuhudia kuwa hichi kitu sio sahihi.

Kama ukichunguza kwa makini mtu anayebet kabla hajaanza kufanya hicho kitu kina kitu ndani yake kinamshtua kwanza, anaanza kukosa amani na anakuwa na mashaka mashaka na huo mchezo, ndio hapo ataanza kujiuliza, hivi kweli huu mchezo ni wa KiMungu? Hayo ndio maswali ya kwanza mtu anayoanza kujiuliza kabla ya kuingia…Na anapoikataa hiyo sauti na kuingia huko, baadaye haisikii tena ndio anaanza kuona ni mchezo wa kawaida tu usio na madhara yoyote, lakini siku za kwanza kwanza atakwenda mpaka kuuliza watu kama ni sawa kuucheza au la?..Ukishaona hali kama hiyo jua kabisa kuna kitu cha hatari unakiendea..

Na ni kwanini unaanza kusikia hivyo viashiria kabla hata hujajiingiza kwenye huo mchezo? Ni kwasababu mchezo huo ni wa kishetani, na unamwingiza mtu kwenye roho moja kwa moja..Mashirika yote ya betting ulimwenguni yanafanya kazi ya shetani kama ulikuwa hulijui hilo ndugu yangu.., yanafanya mambo mengi ya siri ambayo shetani hawezi kuruhusu watu wayajue, ndio mashirika yanayokusanya utajiri mkubwa kwa shetani..Na hayo ndiyo yatakuja kushirikiana na mpinga-Kristo katika kumpa nguvu.

Mashirika hayo mengi yanamilikiwa na vikundi vya kichawi vikubwa duniani kama freemason, brotherhood, yana kivuli cha kulipa kodi, lakini yana agenda nyingine za siri nyuma ya pazia, yanapokea maagizo kutoka kwa lusifa mwenyewe kufadhili mikutano ya hadhara ya ushoga ili kuipalilia roho ya ushoga duniani,..kufadhili haki za mashoga na wasagaji, kufadhili agenda za utoaji mimba n.k kwa nje yanaonekana ni mazuri, lakini wamiliki wa mashirika hayo ni mawakala wa shetani mwenyewe waliowekwa na shetani kwa kazi hiyo.

Na baadhi ya mashirika hayo pia yanafadhili ugaidi kwa siri, ili kuihimiza dunia ilete ustaarabu mpya wa ulimwengu, na pia yanatumia fedha nyingi kuyanyanyua mashirika mengine madogo madogo yanayofanya kazi kama hizo za kuiharibu dunia.…Shetani anafanya kazi kubwa kuachilia mapepo ambayo yatahakikisha watu wengi wanakwenda kubet na kuhakikisha wanakosa, ili aongeze fedha nyingi katika ufalme wake kwaajili ya kumwekea njia mpinga-Kristo. Biblia inasema shetani anampa aliyewake jinsi apendavyo, yeye ndiye anayechagua ni nani apate na ni nani akose, na kumbuka anawapa walio wake, hawezi kumpa ambaye anajua hamsujudii wala haongezi chochote katika ufalme wake..

Mtu anayekwenda kubet kuna pepo Fulani linamvaa, ambalo litamfanya Kesho arudi tena kufanya hivyo hata kama atakosa mara ngapi lakini hatachoka kubet…Mwisho wa siku unakuwa fukara, na bado taabu yako umempa shetani aitumie.

Kwahiyo Biblia inatuambia tutoke huko? (2 Wakoritho 6:15-18)..tutatokaje! Ni kwa kutubu na kudhamiria kuacha hivyo vitu…Biblia inasema shina moja la mabaya yote ni kupenda fedha, unapotamani kupata fedha za ghafla, tambua ni kama mtu aliyewasha WIFI kwenye simu yake, mtu aliyekaribu na yeye anaweza kuupata mtandao wake, na kadhalika mtu anayependa au kutaka kupata fedha za ghafla, anakuwa ni rahisi sana kuonekana kwenye mitandao ya mashetani na kuvaliwa na maroho…

1 Timotheo 6:9 “Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.

10 Maana SHINA MOJA LA MABAYA YA KILA NAMNA NI KUPENDA FEDHA; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.

11 Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole”.

Hivyo tunaonywa tusipende fedha za ghafla! huo ni mtego mkubwa sana shetani anaoutumia…Tembea huko barabarani kwenye nguzo za umeme uone vibao vya waganga,..wote kitu cha kwanza watakwambia…njoo upate utajiri!..Mpango wa Mungu ni kuchuma kidogo kidogo…Sio kwamba hapendi tupate kingi hapana! Ndio mpango wake tuwe na vingi Lakini tukusanye kidogo kidogo…….Tukusanye shilingi mia, mia, kuanzia asubuhi hadi jioni na kupata milioni kumi hiyo ni sawa!….lakini kupata milioni kumi ndani ya dakika moja ogopa sana hizo njia!..Vingi vya hivyo ni mitego ya shetani, Na ndio betting inachofanya.

Mithali 13: 11 “Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa”.

Bwana akubariki sana.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

INJILI YA MILELE.

JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?

KUCHEZA KARATA NI SAHIHI KWA MTU ALIYE MKRITO?

NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.


Rudi Nyumbani

Print this post

MLINZI, NI HABARI GANI ZA USIKU?

Licha ya kulinda, jukumu lingine kuu mlinzi alilonayo ni kuhisi hatari kutoka mbali, Na ndio maana utaona mnyama ambaye Mungu alimuumba kutulinda sisi (Mbwa), licha tu ya kupewa ukali, lakini pia amepewa uwezo wa kunusa mbali, na kusikia, na ndio maana wakati wa usiku utaona mbwa wanabweka sana, hiyo ni kutokana na kuwasikia na kunusa vitu vilivyo mbali sana visivyo vya kawaida, ambavyo hata wewe huwezi kuvihisi au kuvisikia, ule wakati ambao unauona ni wa utulivu na salama lakini kwa Mbwa ni machafuko.

Vivyo hivyo na mlinzi yoyote, hana jukumu la kulinda tu pale adui anapokuja, bali pia anajukumu la kuhisi hatari, na hiyo inakuja kwa kupepeleza, kuchunguza, kutafiti na kutazama, na wakati mwingine kufanya doria, itakayomsaidia kuhisi tatizo kabla halijatokea.. na thamani ya mlinzi sikuzote ipo usiku n.k…

Isaya 21:11 “Ufunuo juu ya Duma. Mtu ananililia toka Seiri, Ee mlinzi, habari gani za usiku? Ee mlinzi, habari gani za usiku?

12 Mlinzi akasema, Mchana unakuja na usiku pia; mkitaka kuuliza, ulizeni; njoni tena.”

Ukisoma hata katika agano la kale utaona walinzi wa miji walikuwa wanakaa katika minara mirefu, ili kuwasaidia kuona kitu kinachokuja kutoka mbali, na wakiona hatari basi bila kuchelewa tarumbeta lilikuwa linapigwa na mji wote kujiweka tayari kwa vita.

Ezekieli 33:1 “Neno la Bwana likanijia, kusema,

2 Mwanadamu, sema na wana wa watu wako, uwaambie, Hapo nitakapoleta upanga juu ya nchi, watu wa nchi hiyo wakimtwaa mtu mmoja miongoni mwao, na kumweka AWE MLINZI WAO;

3 ikiwa, aonapo upanga unakuja juu ya nchi hiyo, apiga tarumbeta na kuwaonya watu;

4 basi mtu awaye yote aisikiaye sauti ya tarumbeta, wala haonywi, upanga ukija na kumwondoa, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.

5 Aliisikia sauti ya tarumbeta, wala hakuonywa; damu yake itakuwa juu yake; lakini kama angalionywa, angalijiokoa roho yake.”

Lakini kama mji utakosa walinzi, au watazamaji, ni dhahiri kuwa utakuwa katika hatari ya kuvamiwa na maadui wakati wowote, na siku maadui watakapokuja watakuja ghafla wenyeji hawatajua chochote kwasababu hawakuwa na waonaji wanaoona mbele yao.

Ndivyo Bwana alivyotabiri jinsi itakavyokuwa katika hizi siku za mwisho, kuja kwake kutakuwa kwa ghafla, kama mwivi usiku wa manane.

(Ufunuo 16:15 “Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake”.)

vile vile mwisho wa dunia utawajia watu kwa ghafla,

(2Petro 3:10 “Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea”.)

na hiyo yote ni kwasababu wamekosa MLINZI katika mioyo yao.

Na ndio maana jambo kuu na la muhimu sana ambalo Bwana Yesu alituachia siku ile aliyokuwa anaondoka, alikuwa ni ROHO MTAKATIFU, akamwita ni msaidizi wetu, kwa namna nyingine ni mlinzi wetu, alijua kabisa, wakati wa giza utapita duniani, na sikuzote giza linaleta usingizi, hivyo kama hatakuwepo mtu wa kuwasaidia kukesha nao, watasinzia na uharibifu utawapata kwa ghafla…

Hivyo akatugawia Roho Mtakatifu, ambaye ndio tupo naye sasa, wote waliompokea kila siku anawashuhudia ndani ya mioyo yao hatari iliyopo duniani sasahivi na jinsi ya kuwa waangalifu. Anawataarifu kila iitwapo leo habari za mwisho wa dunia na kuja kwa Kristo. Na hawa ndio wale hata siku ile ya unyakuo itakapokaribia sana kufika wataifahamu, kwasababu mlinzi wa kuwapasha habari yupo mioyoni mwao.

1 Wathesalonike 5 :1 “Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.

2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.

3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.

4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi”.

Unaona, wale waliojazwa Roho Mtakatifu ndio siku hiyo hatawapa kama mwivi kwasababu, atakuwepo kuwapasha habari juu ya mambo yote yanayokuja. Watajua kabisa wakati wa kuondoka umefika, kama wanavyoshuhudiwa hata sasa, itakapofika kipindi kifupi sana kabla ya unyakuo, mlio wa kengele utazidi kuongezeka ndani ya mioyo yao.

Yohana 16:13 “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, NA MAMBO YAJAYO ATAWAPASHA HABARI YAKE”.

Lakini wale wengine, ambao hawana ROHO MTAKATIFU sasa, ndio wale hata wakisikia kuwa tunaishi siku za mwisho hawashtuki, mioyoni mwao hakuna mabadiliko yoyote, macho yao yamefumbwa, ukiwaambia Yesu Kristo yupo mlangoni kurudi, wanakudhihaki, Na wengine tayari walishampa Bwana maisha yao, zamani walikuwa wanaishi kama wana wa mbinguni lakini baada ya muda na wao wamegueka wakafanana na watu wengine wa kidunia, hao ndio wale ambao wamemzimisha ROHO MTAKATIFU ndani yao, Yule mlinzi anayewalinda amelala, na hivyo hawezi tena kuwapasha habari ya mambo yanayokuja na hatari iliyopo mbele yake.

Mtunzi wa Zaburi aliandika hivi, kwa wachao Mungu..

Zaburi 121:3 “Asiuache mguu wako usogezwe; ASISINZIE AKULINDAYE;

4 Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.

5 BWANA NDIYE MLINZI WAKO; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume.”

Wapo ambao, awalindaye amesinzia, na hao ndio wale wanawali wapumbavu wanaozungumziwa katika Mathayo 25. Ambao kwa pamoja na wenzako (wale wanawali werevu) walikuwa wanamngoja Bwana wao, lakini kwasababu hawa hawakuwa na mafuta ya ziada katika chupa zao, wakarudi baadaye wakakuta mlango umeshafungwa, kule kuishiwa na mafuta ndio kumzimisha Roho..Kwasababu mwanzoni walikuwa nayo lakini baadaye yaliwaishia..Na mafuta siku zote katika biblia yanamwakilisha ROHO MTAKATIFU.

Ndugu yangu nataka nikuambue tunaishi katika siku za mwisho, hakuna mtu asiyejua kuwa Dalili zote zimeshatimia, Jiulize Kristo akirudi leo kulichukua kanisa lake, utaufichia wapi uso wako wewe ambaye bado unasuasua, kwa injili ulizokuwa unahubiriwa kila kukicha lakini bado hutaki kugeuka?. Roho Mtakatifu kila siku anagonga katika mlango wa moyo wako lakini hutaki kufungua. Biblia ipo wazi inasema na mtu yoyote asiyekuwa na Roho wa Kristo huyo sio wake (Warumi 8:9).

Ni maombi yangu utamruhusu huyu mlinzi ayaongoze maisha yako kuanzia sasa katika hichi kipindi kifupi tulichobakiwa nacho kabla ya hii dunia kuisha..Kama ulikuwa umepoa, au umemzimisha Roho Mtakatifu ndani yako, ni wakati wa kutengeneza mambo yako upya sasa. Na kama hujamkabidhi Bwana maisha yako, unachopaswa kufanya ni kutubu kwa kudhamiria kabisa kuacha dhambi, kisha kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi, kwa jina la YESU KRISTO, kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako. Na ukishatii maagizo hayo mepesi Bwana mwenyewe atamshusha Roho wake Mtakatifu ndani yako, kuanzia huo wakati na kuendelea naye atakuongoza na kukupasha habari ya mambo yote yahusiyo saa tunayoishi na siku za mwisho, na hatimaye siku ile haijakujia kama mwivi.

Bwana akubariki sana.

Pia Kwa Maombezi/Ushauri/Ratiba za Ibada Wasiliana nasi Kwa namba

+225683036618/+225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

KAMA MWIZI USIKU WA MANANE:

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA

JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUJA JUU YA MTU.


Rudi Nyumbani

 

Print this post

JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.

Kitabu cha Jeografia, hawajaandikiwa watu ambao sio wanafunzi, kadhalika kitabu cha Fizikia na Baolojia…Vitabu vyote hivi wameandikiwa watu husika…yaani wanafunzi wa masomo hayo..Mtu mwingine yeyote akisoma hataelewa au hakitamsaidia sana…Na maudhui ya vitabu hivyo havijaandikwa kwa lengo la kusomwa tu, bali kujifunza…lengo la mwanafunzi kujifunza mambo yaliyoandikwa ndani ya kitabu kile ni ili kumpa maarifa ambayo yatamsaidia katika maisha yake na pia yatakayomsaidia kufaulu mitihani…asipokielewa kitabu hicho na kukisoma tu kama gazeti, anaweza kweli kukisoma chote ndani ya siku moja lakini utakapokuja mtihani atafeli…Kwasababu waandishi wa vitabu hivyo, lengo lao sio mwanafunzi asome ndani ya siku moja, bali ajifunze kidogo kidogo mambo yaliyopo kule na ayafanyie mazoezi na alinganishe mambo kutoka vitabu vingine, na ndio maana mpaka atakapohitimu inaweza kumchukua hata miaka 4 na zaidi.

Kadhalika na Biblia, NI KITABU CHA MAISHA. Kitabu hichi, hakimuhusu kila mtu, bali kinawahusu wanafunzi tu! Wengine watakisoma kama gazeti na hakitawasaidia chochote, lakini wanafunzi wanakisoma kama ni sehemu ya Maisha yao, future yao ipo hapo, Ndio ufunguo wa Maisha yao…Ndio maana biblia iliposema “Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.(Mithali 4:13)”…Mstari huo haukulenga Elimu ya darasani…hapana! Bali ulilenga Elimu ya Mungu (Elimu ya ufalme wa mbinguni) Mathayo 13:52..maana huo ndio uzima wetu…wengi wanaupeleka mstari huu moja kwa moja kwenye Elimu ya duniani, lakini hiyo si kweli.. “hiyo ni maana ya pili ya mstari huo lakini maana ya kwanza Kabisa Sulemani aliyomaanisha hapo ni ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI”.

Na unapozungumzia Elimu huachi kuzungumzia, Shule, huwezi kuacha kuzungumzia,Waalimu, huwezi kuacha kuzungumzia wanafunzi, wala huwezi kuacha kuzungumzia Mtaala (ambao upo ndani ya vitabu husika).

Na kadhalika Maisha mapya katika Kristo yetu ndio shule yetu, Roho Mtakatifu ndio Mwalimu Mkuu wetu, Biblia ndio Mtaala wetu(Kitabu husika)..na wote waliomwamini Yesu Kristo kwa kuzaliwa mara ya pili, kwa kudhamiria kabisa kumfuata kwa kujikana nafsi zao ndio wanafunzi wake…Utasema hilo linapatikana wapi kwenye maandiko…soma

Luka 14:25 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,

26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

27 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.

Sasa mwanafunzi kabla hajajiunga na shule yoyote ya kidunia, anakubali kuachana na wazazi wake, na ndugu zake, na hata marafiki zake, anakwenda kujiunga na shule ya Bweni…Huko shuleni hataishia tu kukaa mbali na wazazi wake kwa kipindi kirefu, bali atalazimika kuvikataa pia vile vitu vizuri alivyokuwa anavipenda akiwa nyumbani kama Tv, simu, uhuru, nk..anakwenda mahali ambapo hapana uhuru aliokuwa anautaka, mahali ambapo pengine atakutana na changamoto za chakula kibovu, na malazi mabaya.…Na katika Ukristo ndio hivyo hivyo unapoamua kumfuata Kristo ni sawa na umejiunga na shule mpya, Maisha yako ya kale unayakataa, pamoja na mapenzi ya wazazi wako…kwasababu unakwenda kutafuta Uzima wako wa baadaye (future). Na Ukristo sio mteremko kama wengi wanavyofikiri, ukiamua kumfuata Kristo kupungukiwa wakati mwingine kunakuwepo na pia kuna kupitia dhiki nyingi..tofauti na wale watu wanaowahidia watu uongo kuwa watakafanikiwa siku zote.

Vivyo hivyo unapoingia shuleni, unakutana na sheria za shule na moja ya sheria hizo ni mavazi, na mwiko kutoka nje ya uzio wa shule.…shuleni huwezi kujivalia utakavyo, kunakuwa na UNIFORM maalumu…na wote mnafanana…na huwezi kuingia na kujitokea kama unavyotaka, ukitoka bila sababu maalumu ndio umejifukuzisha hivyo…..kadhalika Unapozaliwa mara ya pili, mavazi yako na mwonekano wako ni lazima ubadilike, ulikuwa unavaa vimini ni sharti uache, ulikuwa unavaa suruali wewe mwanamke ni sharti uache, ulikuwa unanyoa kiduku na kuvaa nguzo zinazobana na milegezo wewe mwanamume sharti uache, ulikuwa unapenda kusikiliza miziki ya kidunia, na movie zisizo na maana na fashion za ulimwengu, na kuzurura huku na huko vyote hivyo unaacha!…Na pia Ukristo sio kuingia na kutoka…Ukiingia umeingia! Na ukitoka umetoka…Mwalimu Mkuu huwa hawi mkali kwa Watoto wa mitaani, huwa anakuwa mkali kwa Watoto walioko shuleni kwake, vivyo hivyo Roho Mtakatifu anavyowafundisha watu waliozaliwa mara ya pili ni tofauti na ambao wapo nje.

Baada ya kukubaliana navyo hivyo vigezo, ndipo unapewa MTAALA MAALUMU pamoja na Waalimu wa kukufundisha, na wewe mwenyewe unaongeza bidii zako binafsi kujisomea…Ukisubiri tu kila siku kufundishwa darasani na wewe mwenyewe hutaki kutafuta, utafeli mtihani wa Mwisho, na Katika Ukristo ni hivyo hivyo, umezaliwa mara ya pili, wewe kila siku unapenda tu kufundishwa Biblia, muda wa kujisomea mwenyewe huna, utafeli majaribu na hutaendelea mbele kila siku utakuwa unarudi darasa lile lile, miaka yote wakati wenzako wanaenda mbele..

Na jambo lingine baada ya kujiunga na shule za kidunia ni kwamba utakaa shuleni katika hayo mazingira ya kuteseka kwa muda mrefu kidogo inaweza kuchukua hata miaka kadhaa, lakini siku utakapokuja kufanya mtihani wa mwisho na kufaulu utapokea cheti, ambacho hicho kitaonyesha tofauti yako wewe uliyekwenda shule na yule ambaye hajakwenda…kulivumilia viboko vya shule na kula chakula kibovu na wakati mwingine kulala vitanda vyenye kunguni sio bure!…siku utakapohitimu na kupata cheti heshima yako ndio itakapoonekana kuwa hukuwa mjinga kujikana nafsi yako.

Kadhalika Roho Mtakatifu akishakupitisha katika madarasa yake na kuyahitimu vizuri faida zake utakuja kuziona hapa hapa duniani pamoja na katika ulimwengu ujao…lakini sana utakuja kuziona katika ulimwengu ujao kwasababu vitu vya hapa duniani havidumu, vinapita lakini vya huko mbinguni ni vya milele…Siku zile wateule walioshinda watang’aa kama jua mbele za malaika wa mbinguni…

Mathayo 19:27 “Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?.

28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.

29 Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele”.

Umeona Umuhimu wa kuitafuta Elimu ya ufalme wa mbinguni sasa?..Elimu ya dunia hii inafunua elimu ya ufalme wa mbinguni, Kristo anapokuambia leo utubu na kuacha dhambi, na ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina lake na uache ulimwengu na mambo yake yote, na kisha umfuate sio kwamba anataka atutese, hapana ni kwasababu anataka atusajili kwenye shule yake ambayo baadaye itatupa cheti kilicho bora! Zaidi kuliko vyeti vyote.. Na heshima! Zaidi kuliko heshima zote….na kumbuka hakuna shule yoyote isiyokuwa na sheria ndio maana anakuambia ewe mwanamke jikane nafsi!! acha mavazi yako ya kikahaba, acha mawigi, acha kupaka wanja, acha mavipodozi baki katika hali yako ya asili…kama unapenda kujipamba subiri tukifika mbingu za mbingu utajipamba utakavyo kama kutakuwepo na kujipamba….lakini kwasasa upo shule!..fanya kile Mwalimu Mkuu anachokuagiza ukifanye kwa faida yako…

Ulipokuwa katika shule za kidunia ulipoambiwa uvae sketi za marinda ulitii na usisuke nywele ulitii bila shuruti lakini unapoitafuta elimu ya Roho Mtakatifu hutaki kutiii…nataka nikuambie ukweli bado hujaanza madarasa ya Roho Mtakatifu, bado upo nyumbani wala mtu asikudanganye kuwa upo sawa na Mungu bado haupo sawa, usidanganywe pia Mungu haangalii mavazi anaangalia Roho, ni kweli kabisa anaangalia roho lakini roho inamahusiano makubwa na mwili ndio maana ipo ndani ya mwili, kama vile elimu ya kidunia ilivyo na uvaaji wa wanafunzi wake..Elimu ni ufunguo wa Maisha, yaangalie Maisha yako ya baadaye yatakavyokuwa usijiangalie leo…dhambi za kitambo zisije kukuponza ukaja kujuta milele huko baadaye..Fanyika mwanafunzi wa Kristo leo.

Bwana akubariki sana.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/+225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

NJIA YA MSALABA

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA JIKANE MWENYEWE?

JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?

MJUE SANA YESU KRISTO.


Rudi Nyumbani

Print this post

WEWE SI MALI YAKO MWENYEWE!


1 Wakorintho 6: 19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? WALA NINYI SI MALI YENU WENYEWE;”

Ukilijua Neno hili utauheshimu mwili wako, kuliko hapo kwanza. Kitu kikubwa kisichofahamika na wengi ni kuwa Miili hii tuliyonayo sio mali yetu..hatujapewa dhamana ya kuitawala asilimia 100. Kama ingekuwa ni mali yetu asilimia mia moja, tungekuwa na uwezo wa kuzisimamisha nywele zetu zisiote kwa amri zetu, tungekuwa tunaweza kuiambia mioyo yetu isimame kusukuma damu na ingetutii kama tu vile tunavyoamua kusimama au kukaa…

Kwahiyo unaweza kuona miili hii, tunamamlaka nayo sehemu ndogo sana, tena sana….huwezi kukiongoza chakula tumboni, kinajiongoza chenyewe, huwezi kuuongoza mwili wako utoe jasho unajitoa wenyewe, au kucha kukua…mwanamke hawezi kutengeneza kiumbe ndani ya tumbo lake, kiumbe kinajitengeneza chenyewe ndani kwa ndani, anajikuta tu, uchungu umemfikia na anajifungua mtoto… kadhalika hatuwezi kujifanya tukue..tangu tulipokuwa Watoto tunajikuta tu tunaongezeka kimo na ukubwa bila idhini yetu, vitu kama ini, figo, kongosho, seli zinafanya kazi pasipo hiyari zetu nk…chunguza utagundua kuwa hii miili yetu, tuna mamlaka nayo sehemu ndogo sana, karibia kila kitu kinaongozwa na nguvu nyingine..

Mamlaka tuliyopewa sisi ni uwezo wa kusogeza viungo vyetu vya nje kama miguu, mikono, macho, na uwezo wa kujisogeza kutoka sehemu moja hadi nyingine..basi hakuna kingine cha ziada…Hii yote ni kuonyesha kuwa HII MIILI SI MALI YETU NI MALI YA MWINGINE.

Ni kama tu mtu unapofungua account ya Facebook au ya Bank au anapoisajili laini ya simu…Unapofungua account ya facebook kwa mfano, account hiyo inakuwa ni ya kwako ina jina lako na password yako, kiasi kwamba hakuna mtu anayeweza kujua kinachoendelea ndani ya account hiyo, isipokuwa wewe umwonyeshe… kila kitu unaweza ukakifanya private mtu yeyote asijue unafanya nini, na unaweza kuitumia utakavyo…lakini pamoja na kwamba unao uwezo wa kuitumia utakavyo, bado kuna vitu utakuwa huwezi kufanya…kwamfano ukikiuka sheria za wamiliki wa facebook wanakunyanganya hiyo account, aidha wanakufuta kabisa au wanakublock kwa muda…na huwezi kuirudisha kwa namna yoyote ile,

Hiyo yote ni kuonyesha kwamba hiyo account si yako bali ni yao. Hata kama unauwezo wa kuweka password ngumu kiasi gani, lakini wenyewe wakitaka kujua kinachoendelea ndani ya account hiyo huwezi kuwazuia, wakitaka kukupokonya vile vile huwezi kuwazuia.

Na Zaidi ya yote, jinsi account za facebook na nyinginezo zinavyofanyiwa marekebisho, huwa mwenye account hahusiki, anajikuta tu kuna kitu Fulani kimeongezeka kipya, au kuna kitu Fulani kimeondolewa..Hiyo yote ni kuonyesha kuwa hiyo account ni ya kwako lakini bado sio ya kwako. Ni watu Fulani walikupa tu..

Na hii miili tuliyopewa ni hivyo hivyo, ni Mali ya Mungu…Si mali yetu kabisa, na ilivyowekwa hapa duniani na aliyeiweka (yaani Mungu) kaiwekea sheria na utaratibu wake, namna inavyopaswa iwe…Hakutupa kwa lengo la kuigeuza bango la matangazo, au chombo cha kuharibu wengine, au kituo cha roho nyingine chafu zinazoharibu kukaa…Mwili unaofanya hivyo utafungiwa haki ya kuishi (maana yake utakufa).

Ndio maana kuna umuhimu sana wa kuitunza hii miili tuliyopewa, na kuelewa kwa undani masomo kuhusu NAFSI, MWILI na ROHO.. kwasababu si MALI YETU WENYEWE…Ukiuchora mwili wako tattoo isingekuwa shida endapo ingekuwa ni mali yako…lakini kwasababu si mali yako ni ya mwingine usifanye hivyo, utajitafutia mabaya badala ya mazuri….Ni sawa sasahivi uanze kutumia hiyo account ya facebook vibaya, ukaanza kuitumia kuweka picha chafu na zisizofaa na kuharibu jamii, na kufanya uhalifu, wamiliki wakiligundua hilo unafungiwa mara moja na wala hutapata nafasi ya kuongea nao..kwasababu hata hawajawahi kuzungumza na wewe hapo kabla…password haimaanishi kuwa ndio umepata uhalali wa kuimiliki hiyo account asilimia 100. Kadhalika sio kwasababu unauwezo wa kusitiri siri ndani ya mwili wako kiasi kwamba hakuna mtu awezaye kujua kinachoendelea ndani mwako, na una uwezo wa kutembea kutoka sehemu moja hadi nyingine kama utakavyo, ndio iwe sababu ya kusema huo ni mwili wako…Huo sio wako ni mali ya Mungu, akiutaka anauchukua siku yoyote, na huwezi kumwuliza kwanini.

Hivyo ili tuweze kuishi ndani ya hii miili kwa muda mrefu na kwa kheri hatuna budi kuishi kwa kuzifuata sheria zake, Neno lake linasema…mwanamke avae mavazi ya kujisitiri (1 Timotheo 2:9) basi ni vizuri kutii…usiseme una uhuru juu ya mwili wako, na kuvaa utakavyo, kumbuka huo si wako…

Biblia inasema usichanje chale wala usichore alama (tattoo) katika mwili wako ni machukizo, basi usijifanye wewe ni mgunduzi wa huo mwili, yupo mwenye huo mwili ambaye akiutaka anao uwezo wa kuutahifisha muda wowote.

Walawi 19: 28 “Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi Bwana”.

Biblia inasema uashareti hata usitamkwe kamwe kwenu (Waefeso 5:3)…Usiseme mwili wangu, nina uhuru wa kufanya nitakalo, Hivyo Mungu hawezi kunihukumu kwa kitu ambacho ni mali yangu…Ndugu huo sio mali yako, ingekuwa hii miili ni mali yetu katupa moja kwa moja, wala asingetusumbua kutuwekea sheria sheria,… tungekuwa na uhuru wa kila mtu kufanya atakalo…mtu angeamua kujirefusha kuwa kama mlingoti, ni sawa, mwingine angetaka kujifanya kuwa tembo pia ni sawa…lakini kwasababu ni mali yake, wote anatuweka kwenye kimo Fulani karibia kinachofanana na maumbile yanayofanana, kutimiza kusudi lake yeye na si la kwetu…Kwahiyo Uasherati ni moja ya dhambi mbaya sana ambayo inaweza kusababisha kifo cha ghafla kuliko dhambi nyingine zote..

1 Wakorintho 6: 18 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe”.

Na dhambi nyingine ambazo ni mbaya zinazopelekea kuharibu mwili ni Ulevi, uvutaji sigara, matumizi ya madawa ya kulevya na matumizi ya vipodozi na utoboaji mwili.

Kama uliyafanya hayo pasipo kujua, na ulikuwa hujui kuwa mwili huo ulionao sio mali yako, basi hii ndio nafasi yako ya kutubu, unatubu na kumwambia Bwana hutaki tena hayo mambo na hivyo unataka kutimiza kusudi lake alilolikusudia juu ya mwili wako, baada ya kutubu katafute ubatizo sahihi popote pale, kama hujafanya hivyo, ubatizo sahihi ni wa umuhimu kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako (Matendo 2:38) na ubatizo sahihi ni wa kuzama mwili wote katika maji na kwa jina la Yesu, na baada ya hapo Bwana mwenyewe atakupa Roho Mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi na kukuongoza katika kuijua kweli yote ya Biblia. Hakuna mtu awezaye kushinda dhambi kwa nguvu zake mwenyewe, wote tunamtegemea Roho Mtakatifu kutuwezesha, hivyo Roho Mtakatifu ni wa muhimu sana baada tu ya kumwamini na kubatizwa, maana yeye ndio Muhuri wa Mungu (Waefeso 4:30)

Bwana akubariki.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/+225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

WEWE NI HEKALU LA MUNGU.

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?

‘’MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI’’..NA NDIVYO ILIVYO KWA UASHERATI


Rudi Nyumbani:

Print this post