Title January 2019

VITA DHIDI YA MAADUI

Shalom karibu tujifunze Neno la Mungu, Maandiko yanatuambia “kumcha Bwana ni chanzo cha Maarifa”… Maneno ya Yesu Kristo yanafaida kubwa katika maisha zaidi hata tunavyofikiri.  Kwa jinsi tunavyozidi kumcha Bwana maarifa yetu ndivyo yanavyozidi kuongezeka siku baada ya siku, mpaka tunapofikia kiwango kile cha Maarifa cha kumfahamu yeye anachotaka tukifikie sisi kama tunavyosoma katika Waefeso 4:13. 

Nilipita sehemu Fulani, nikapisha na dada mmoja aliyekuwa anaongea na mwenzake, walikuwa wanatembea kwa kasi kidogo lakini nilifanikiwa kusikia moja ya kauli zake  akisema “tumepewa mamlaka ya kukanyaga nge na nyoka…akaendelea kumwambia mwenzake “adui yako akija mbele yako usimsubirishe we mkanyage..kwa maana tumepewa mamlaka hayo ”…Akiwa na maana kuwa mtu akija mbele yako ambaye yupo kinyume chako mdhuru kabla yeye hajakudhuru biblia imeturuhusu kufanya hivyo, tena hakikisha unammaliza kweli kweli.

Niliposikia hivyo nilisikitika sana, nikasema Bwana atusaidie kweli kweli,

Ndugu yangu nataka nikwambie..katika Agano jipya hatuna adui yoyote ambaye ni Mwanadamu…Adui yetu ni Shetani na majeshi yake, kwa maana kupigana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, maandiko yanatuambia hivyo… Vita juu ya damu na nyama vilikuwa katika Agano la kale, ndio maana tunawaona watu kama wakina Daudi, Sulemani, Sauli na wengine wote ndio waliokuwa na maadui ambao ni wanadamu kwasababu, bado walikuwa hawalijui agano lililo bora zaidi. Kwa neema Mungu aliyowapa aliwaruhusu wawaone maadui zao kwa njia ya kibinadamu, lakini haikuwa hivyo tangu mwanzo. Tangu Edeni adui wa kwanza wa mwanadamu alikuwa ni shetani.

Kwahiyo baada ya dhambi Mungu aliruhusu tuishi katika vipengele pengele Fulani vya maisha ambavyo vingi havikuwa ni njia kamili au mpango kamili wa Mungu japo aliviruhusu, kwamfano aliruhusu talaka, aliruhusu ndoa za wake wengi. N.k

 Lakini ulipokuja utimilifu wote ulioletwa wa lile Neno lililofanyika mwili ambaye ni Bwana wetu Yesu Kristo, kwa Neema aliweka mambo yote kama yanavyopaswa yawe katika utimilifu wote..ndio maana Bwana aliwaambia “watu haikuwa hivyo tangu mwanzo”,..wao walikazana kumwambia Bwana mbona Musa alifanya hivi, alisema vile…lakini Kristo alizidi kuwaambia haikuwa hivyo tangu mwanzo..

Na leo jambo ni lile lile watu tunaweza kujiuliza mbona Daudi alikuwa na maadui na aliwaua na aliwalaani… na sisi tufanye hivyo hivyo, lakini Kristo anatuambia haikuwa hivyo tangu mwanzo…haikuwa hivyo tangu mwanzo kujilipiza kisasi, haikuwa hivyo tangu mwanzo kumlaani mwanadamu mwenzako (ambaye tunaona roho ya uadui ipo ndani yake)…Utauliza hayo maneno yanatoka wapi kwenye biblia?..soma

Luka 6:28 “wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.”

Mathayo 5:43 “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi”..

38 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho,na jino kwa jino; Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume,mgeuzie na la pili” 

Hayo ni maneno ya Bwana Yesu mwenyewe..anasema “mmesikia imenenwa….”

Sasa swali wamesikia kutoka kwa nani? Jibu ni wamesikia kutoka Kwa mababa waliowatangulia ambao ndio hao wakina Musa, Daudi, Eliya na wengine wote…

Ndugu yangu unaposoma kitabu cha Zaburi, pasipo uongozo wa Roho Mtakatifu wa kujua nyakati Mungu alizokuwa anatembea kwa kila nyakati itakupoteza kwasababu ndani ya Zaburi hiyo hiyo kuna sehemu imehalalisha mvinyo, Ndani ya zaburi hiyo hiyo usipokuwa na msaada wa roho kuielewa unaweza ukajifunza chuki na visasi, ndani ya sheria za Musa na torati pasipo msaada wa roho unaweza kujifunza mauaji na kiburi…Na ndani ya hiyo hiyo biblia unaweza kujifunza uasherati kama wengi sasahivi wanavyoitumia kuhalalisha ndoa za mitara.

Sasa tukirudi kwenye suala la “Maadui zetu”…swali ni je! Maadui wetu ni wakina nani sasa?

Kumbuka Tangu mwanzo adui ni Ibilisi biblia inasema hivyo, yeye ndiye atushitakiaye mbele za Mungu mchana na usiku, na ni mfano wa simba angurumaye atafutaye mtu wa kummeza (1 Petro 5:8). Huyo ndio adui yetu wa kwanza na wa mwisho, hivyo kwa kutumia majeshi yake ya mapepo wabaya..ndio anafanya vita na sisi.

Anayatuma mapepo yake yanawaingia watu, kwahiyo Yule mtu anageuka kuwa ofisi ya shetani kwa kujua au pasipo kujua..ndio hapo unakuta mtu anakuchukia ghafla pasipo sababu, au anakutafutia hila, anaanza kukupiga vita, au kukutafutia madhara, au wivu au anafurahia kuanguka kwako!…au anatafuta namna ya wewe kuiacha imani, sasa chanzo sio Yule mtu, bali ni roho iliyoko ndani yake…roho iliyoko ndani yake ndio roho ya uadui.

Sasa sio jukumu letu sisi kupambana na Yule mtu, kama watu wa agano la kale walivyokuwa wanafanya bali ni jukumu letu kupambana na ile roho inayotenda kazi ndani yake,  Yule mtu yeye ni  kama ofisi tu!! Awe anajua au asiwe anajua.. Watu wa agano la kale kama wakina Daudi walikuwa wanapambana na watu kwasababu bado walikuwa hawajapewa neema ya kujua chanzo cha mambo yote ni wapi lakini sisi tumepewa….

Ndio hapo biblia inatuambia katika

Wafilipi 6:11 “ Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.

12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; BALI NI JUU YA FALME NA MAMLAKA, JUU YA WAKUU WA GIZA HILI, JUU YA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO”

Hapo Neno linatuambia “tuweze kuzipinga hila za shetani na sio mwanadamu”.

Sasa namna ya kuipiga na kuikanyaga hii roho ya adui iliyopo ndani ya ndugu zetu!! Namna ya kuitowesha kabisha, na kuiharibu tumepewa silaha madhubuti za kuiangusha, pasipo kuidhuru ile ofisi shetani anayoitumia, maana nia na madhumuni ni kuipiga ile roho na kuiacha ile ofisi huru iokoke ili itumiwe na Mungu kama ofisi ya Nuru. Haleluya!!, sasa silaha za kuipiga ile roho ndio hizi zifuatazo.

Waefeso 6:13 “Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama..

1)   Basi simameni, hali mmejifunga KWELI VIUNONI– Hakikisha unaifahamu kweli yote ya biblia, unamfahamu Yesu Kristo katika ukweli wote,Maneno ya Mungu kama haya.

2)   Dirii ya Haki kifuani– Hakikisha unauelewa vizuri ufunuo wa kuhesabiwa haki kwa Imani, kwamba sio kwa matendo tunaokolewa bali kwa neema, sio kwa matendo tunaponywa bali kwa neema, si kwa matendo tunapata ulinzi kutoka kwa Mungu bali kwa neema, sio kwa matendo tunampendeza Mungu bali kwa Neema kupitia Yesu Kristo. Hiyo itakusaidia shetani anapoleta mashtaka yake ya kukuhukumu ndani ya moyo wako, au nje unakuwa na mafuta ya kutosha kumshinda hoja zake, na kutokupepeswa na maneno ya mwovu yanapokuja juu yako.

3)    kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani– Hii ni silaha ya tatu madhubuti kabisa ya kuiharibu ile roho ya uadui ndani ya mtu, hatua hii ni ile mtu anapochukua hatua ya kwenda kumhubiria INJILI Yule mtu ambaye roho ya uadui ipo ndani yake, na kumhubiria sio tu kwa maneno bali kwa kielelezo cha matendo, unakwenda kumhubiria habari njema za wokovu, una mwombea, unaonyesha upendo, akikuomba chakula unampa,akikuomba nguo mvike, na hiyo inapelekea  Ile roho iliyoko ndani yake inapungua nguvu kwa kasi sana, na kutengeneza njia ya ushindi wa vita.

4)   Ngao ya Imani –Imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo, kwa lolote lile shetani atakalolileta, una imani kuwa halitafanikiwa, na zaidi ya yote una Imani kuwa wewe ni mwana wa Mungu mrithi wa ahadi zake, na hakuna chochote kitakachokudhuru, hata jeshi la mapepo kiasi gani,hata waganga wote duniani wakiungana kupambana wewe hakuna jambo lolote litakalofanikiwa kwasababu upo chini ya damu. Na unaimani kuwa  lolote umwombalo Baba atakutendea

5)   Tena ipokeeni chapeo ya wokovu– Chepeo ni HELMET kwa kiingereza, kazi yake ni kulinda sehemu ya kichwa..Na sisi tunaposimama mbele ya Adui yetu shetani, silaha yetu nyingine ni tumaini la Wokovu tulionao, kwamba tumemwamini Yesu Kristo aliyetukomboa kwa damu yake, na kutuahidia ukombozi wa miili yetu, kwahiyo hakuna chochote kitakachoweza kututoa kwake kwa kupitia Roho wake Mtakatifu tumetiwa Muhuri mpaka siku ya ukombozi wetu (Waefeso 4:30). Na huko huko ndio unajifunza kusamehe. Kwasababu unajua na wewe ulisamehewa deni kubwa kushinda hilo la ndugu yako.

6)   Upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu– Hii ndio silaha ya mwisho na ya umuhimu kuliko zote.. ukilifahamu Neno la Mungu, hakuna elimu yoyote ya shetani itakayokupiga chenga, kwasababu shetani naye anayo injili yake ambayo inafanana sana na injili ya Kweli, ambayo kwake nayo ni kama UPANGA anayokatakata nayo watu, ndio ile aliyokuwa anataka kumkata nayo Bwana kule jangwani injili ya “imeandikwa”..

lakini Bwana alimshinda kwasababu Neno la Mungu lilikuwa limekaa ndani yake kuliko shetani. Upanga wa Kristo ulikuwa mkali kuliko wa shetani aliweza kumkata shetani kwa kumjua hila zake na njama zake na mawazo yake… Waebrania 4:12 “ Tena Neno la Mungu li hai tena lina nguvu tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake, tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo”.alimshinda kwa Neno.

Hizo ndizo silaha 6 Muhimu na pekee za kushindana na Adui yetu shetani. Sasa kumbuka katika vita adui yako na yeye kavaa kama wewe, na yeye ana kweli yake kiunoni, ana dirii yake kifuani, ana chepeo yake kichwani ana injili yake miguuni, na ana upanga wake mkononi amepewa na shetani. Hivyo Ndivyo alivyo shetani ana injiili yake ya uongo ana imani yake ya uongo, ana wokovu wake wa uongo, ana haki yake ya uongo…yote hayo ni kwaajili naye kujilinda,lakini kwasababu sisi tunavyo vya ukweli na vyenye nguvu kuliko vyake tunamshinda. Lakini kama hatuna hata kimoja cha ukweli atatukatakata na upanga wake na kutuweka chini.

Sasa tutajuaje kwamba tumeshinda vita? Tutajua tumeshinda vita vizuri kama tutakuwa tumefanikiwa kumleta Yule mtu kwa Kristo, au tumempandia mbegu ya Kristo ndani yake, Kwasababu Yule ni mtu wa Mungu, anayestahili wokovu kama wengine tu! Kama sisi,  naye pia Mungu hapendi kumwona anakwenda kwenye ziwa la moto, naye anasikia maumivu kama sisi, na anahisia zote kama sisi tulizonazo.

Lakini endapo tukikosa shabaha! Na kuanza kupambana na Yule mtu badala ya kupambana na roho iliyopo ndani yake, na kuanza kumrudishia ubaya, kuanza kumlaani, kuanza kumwombea afe…na kusema Bwana katupa mamlaka ya kukanyaga nge na nyoka kwahiyo tumkanyage yeye kweli kweli, hapo tutakuwa hatujashinda vita bali tumeshindwa vita!! Na kugeuka kuwa vyombo vya shetani.

Na unajua ni sisi tu wakristo ndio hatuna hekima katika ukristo wetu, lakini watu wa ulimwengu huu kama biblia inavyosema wana hekima katika mambo yao…Kwamfano serikali inapotangaza vita dhidi ya UMASKINI, MARADHI na UJINGA..Huwezi kuona inakwenda kupambana na wagonjwa hospitalini, huwezi kuona inaenda kuua wagonjwa na kusema tunapapambana vita dhidi ya maradhi, au huwezi kuona inakwenda kuwaua maskini wa nchi na kusema tunapambana vita dhidi ya umaskini, au huwezi kuona serikali inakwenda kuwaua au kuwafukuza watu wasio na elimu kwa kisingizio cha kupambana vita dhidi ya Ujinga, badala yake utaona itaenda kutafuta suluhisho na tiba kwa watu wake waondokane na umaskini, maradhi na kukosa elimu..Lakini sisi wakristo ndio namba moja kuuwa watu wenye magonjwa ya kiroho, umaskini wa kiroho na ujinga wa kiroho na kusema ni maadui zetu! Yaani Inaonyesha ni jinsi gani hatujielewi!!!

Wakati Fulani Bwana alipokuwa anakwenda Samaria kuhubiri, wenyeji wa mji ule walimkataa, ndipo wanafunzi wake wakamwambia tushushe moto kama Eliya uwaangamize..lakini Bwana hakufanya vile kwasababu alijua tatizo sio hao watu bali ni roho iliyo ndani yao..akawaambia wanafunzi wake Mwana wa Adamu hakuja kuangamiza roho bali kuokoa.

Luka 9: 52 “akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali.

53 Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu.

54 Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?

55 Akawageukia, akawakanya. [AKASEMA, HAMJUI NI ROHO YA NAMNA GANI MLIYO NAYO.]

56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine”

Sasa kama Bwana hakufanya hivyo kwanini sisi tufanye hivyo?? Tutakuwa na roho gani ndani yetu??..bila shaka itakuwa ni roho ya Ibilisi!! Roho ya kuangamiza badala ya kuokoa…

Nataka nikuambie tu ndugu, nge wetu ni shetani na nyoka wetu ni shetani, hao ndio tuliopewa mamlaka ya kuwakanyaga..na hatuwakanyagi kwa maneno bali kwa hizo silaha 6 hapo juu!!..Maombi ya kuwatakia shari ndugu zako acha kuanzia leo, maombi ya kuwalaani wale wanaokuudhi acha kuanzia leo, muhubiri au mwalimu anayekufundisha hivyo anakufundisha uongo na anakuhubiria uongo!!

Tena wengine wanaaambiwa watu kabisa waandike majina ya maadui zao wayaweke kwenye maboksi wayaombee wafe!! HAYO NI MAFUNDISHO YA MASHETANI!!..Kwanini usiweke jina la adui yako kwenye boksi umwombee ampe Kristo maisha yake? Kuliko kumwombea afe!!.Fikiria ni mama yako anaombewa afe na mtu mwingine wewe utafurahia kitendo hicho?. Mambo yale tunayotaka tutendewe sisi ndio tutendee wengine Bwana alitufundisha hivyo.

Warumi 12:14 “Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.”

Ni maombi yangu kuwa Bwana atakujalia kuyaona hayo na zaidi ya hayo.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

KISASI NI JUU YA BWANA.

KWA KUWA WASEMA MIMI NI TAJIRI.

OKOA BADALA YA KUANGAMIZA!

NA JINA LAKE AITWA, NENO LA MUNGU.

SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.

MAUTI NA KUZIMU ZIKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE.

NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!


Rudi Nyumbani

Print this post

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:

Shalom! Karibu tujifunze Neno la Mungu,leo tutajifunza siri mojawapo ya kipekee iliyolala katika kitabu cha cha Ruthu. Kitabu hichi ni chepesi kukisoma, kwasababu ni kitabu kinachoelezea historia ya maisha ya watu zaidi kuliko unabii, hivyo nakushauri mahali ulipo chukua biblia yake ukipitie kwanza binafsi,kisha tuendelee ni kitabu chenye sura 4 fupi zinazoeleweka, hivyo ni vema ukafanya hivyo ili tuende pamoja.

Kitabu hichi kinaanzana na habari ya mtu anayeitwa Elimeleki, ambaye huyu alikuwa akiishi Israeli zamani kipindi cha Waamuzi, na biblia inatuambia siku njaa ilipokuja katika mji ule, Elimeleki alifunga safari kwenda nchi ya jirani kuishi huko yeye pamoja na mke wake aliyeitwa Naomi pamoja na wana wake wawili wa kiume..Lakini baada ya Muda kidogo mambo yalibadilika Elimeleki alikufa na kumwacha mke wake akiwa mjane na watoto wake wawili katika nchi ya ugenini..

Na Baadaye kidogo watoto wake wote wawili walibahatika kupata wake wazuri tu, lakini kwa bahati mbaya, nao pia walifariki wakiwa bado hawajapata watoto na wale wanawake, Hivyo yule mwanamke mjane Naomi hakufanikiwa kuambulia chochote, si mume, si watoto, wala si wajukuu, na hapa sasa ameshakuwa mzee sana hawezi kubeba mimba tena, hata angesema azae asingeweza tena kwani muda umeshakwenda amekaa ugenini zaidi ya miaka 10, hata hana wa kumsaidia tena, nguvu zake zimeisha kilichobakia ni kurudi tu katika nchi yake Israeli kwenda kumalizia siku zake za kuishi.

Kabla hatujaendelea mbele Embu jiulize, zamani zile za kipindi cha waamuzi kulikuwa na watu wengi mashujaa tu kama tunavyokisoma, kulikuwa na wajane wengi tu, kulikuwa na watu wengi wema tu, Hivyo habari zao zingeweza kuandikwa kama mojawapo ya kumbukumbuku nzuri kama funzo kwa ajili ya vizazi vya mbeleni, lakini ni kwanini habari za watu wengine hazijaandikwa isipokuwa za huyu mtu mmoja tu Elimeleki na familia yake ndizo zimenakiliwa hapa, na kuwekwa kama vitabu vitakatifu?..

Njia za Mungu sio njia zetu, Naomi hakufahamu kuwa japo maisha yake yalionekena kuwa ni ya bahati mbaya mbele za watu, maisha ya kusahauliwa, mtu ambaye sasa hana kumbukumbu tena, ambaye aliyekuwa amefanikiwa sana lakini sasa si kitu, hana mume,wala watoto,wala wajukuu, wala mali, wala chochote kile..hakujua kuwa kumbe Mungu alikuwa anaandika kwa kupitia maisha yake ufunuo mzito ambao ndio huo unakuja kutusaidia hata sisi watu ambao hatukustahili kupata neema za kumjua Kristo. Kwahiyo wakati mwingine maisha ya mtu yanaweza kubeba ufunuo Fulani wa Roho.

Lakini tukiendelea kusoma habari tunaona Naomi sasa anakusudia kurudi katika nchi yake mpweke,mwenye uchungu mwingi, na hapa tunaona anawaambia wale wakwe zake, ambao mwanzoni walikuwa wameolewa na watoto wake wawili kwamba kila mmoja sasa awe na amani kurudi kwa jamaa zake wakaolewe na kufanikiwa na kuishi maisha ya furaha siku zote za maisha yao.

Lakini tunaona wale wanawake wawili mwanzoni wote walikataa kumwacha Naomi peke yake, Lakini hilo halikumfanya Naomi aache kuwasihi wasifuatane naye, kwani hakutaka mtu yeyote abebe wake wowote kwa kulazimishwa, hivyo aliwabariki na kuwaomba warudi kwa jamaa zao wenyewe, lakini kama tunavyosoma habari, moyo wa Ruthu ulikuwa thabiti kuliko wa Orpa, Yeye Orpa baadaye alikubali kurudi kwa jamaa zake lakini Ruthu hakutaka kinyume chake alikuwa tayari kuambatana na Naomi popote aendapo kwa gharama zozote, alikubali kuchukuliana na gharama zote.

Tunasoma:

Ruthu 1: 11 “Naye Naomi akasema, Enyi wanangu, mrejee; kwani kufuatana na mimi? Je! Mimi ninao watoto wa kiume tena tumboni mwangu, hata wawe waume zenu?

12 Enyi wanangu, mrejee; nendeni zenu; kwa kuwa mimi ni mzee, siwezi kupata mume tena. Kama ningesema, Natumaini; kama ningepata mume hata usiku huu, na kuzaa watoto wa kiume;

13 je! Mngesubiri hata watakapokuwa watu wazima? Mngejizuia msiwe na waume? La, sivyo, wanangu; maana ni vigumu kwangu kuliko kwenu, kwa sababu mkono wa Bwana umetoka juu yangu.

14 Nao wakapaza sauti zao, wakalia tena, na Orpa akambusu mkwewe, lakini Ruthuu akaambatana naye.

15 Naye akasema, Tazama, shemeji yako amerejea kwa watu wake, na kwa mungu wake; basi urejee wewe umfuate shemeji yako.

16 Naye Ruthu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe; Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu;

17 Pale utakapokufa nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; Bwana anitende vivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe nami.

18 Basi alipomwona kuwa amekaza nia yake kufuatana naye, aliacha kusema naye”.

Sasa ukiendelea kusoma habari huko mbeleni utaona Ruthu alikubali kuondoka na Naomi katika umaskini wao, Ruthu asijue anapoelekea, asijue wakifika watapokelewa na nini, Ruthu akimtazama mwanamke yule kashakuwa mzee, na yeye bado ni binti kijana, ambaye anao uwezo wa kwenda kuolewa tena, ameacha vijana wazuri wenye mali katika nchi yake mwenyewe, pengine mabinti wenzake wanamkebehi wakimwambia hivi wewe umelogwa na kale kabibi?

Kwani katakupa nini? mwangalie mwenzako Orpa, aliona mbele kuwa huko hakuna tena uelekeo wa maisha, zaidi ni kuzeeshwa tu akili za wazee na kuwahudumia tu, na mwisho wa siku kuwa kama mjakazi wao..Isitoshe anakwenda mahali asipopajua, wala hajawahi kuwafahamu watu wa huko, pengine walimwambia Unakwenda kupotea tu huko na mwisho wa siku utajuta..Wewe bado binti mdogo hata bado hujazaa, unakwenda wapi?

Lakini Ruthu hakujali kuipoteza nafsi yake kuwa ni kitu cha maana sana, kuliko kujitenga na mama wa mume wake marehemu, hivyo aliendelea kufuatana naye tu katika taabu zote kama alivyoapa.

Kumbuka ni sheria iliyokuwa imetolewa na Mungu katika Israeli, kwamba mtu yeyote aliye myahudi asioe mwanamke ambaye si myahudi, kadhalika ni mwiko pia kwa mwanamke wa Kiyahudi kuolewa na mtu wa mataifa, Lakini hapa tunaona Naomi akirudi katika nchi yake mwenyewe akiwa amemwambulia mtu mmoja tu..

Pengine wale ndugu zake waliokuwa wamebaki Israeli walitazamia Elimeleki pamoja na Naomi watarudi na mali nyingi, kondoo, mbuzi, ngamia pamoja wa watoto wao na wajukuu wengi, na wajakazi wengi. Lakini hapa anaonekana Naomi peke yake, na binti mmoja wa kimataifa, na tena kibaya zaidi ni heri angekuwa kijakazi wake, lakini kumbe ni mke wa mtoto wake, jambo ambalo ni machukizo makubwa kwa Israeli.

Lakini kwa jinsi Ruthu tabia yake ilivyokuwa njema, na ya kupendeza watu wote, na kwa ukarimu wake wote aliomfanyia Naomi bibi yake,basi habari zake zikasikika katikati ya jamaa za Naomi. Na siku moja alipokuwa anakwenda kuokota masazo ya nafaka kwenye mashamba ya watu matajiri, aliingia katika shamba la mtu mmoja mkuu sana wa mji huo jina lake Boazi, ndipo Boazi akamwona na kuulizia habari zake, na kuambiwa kuwa huyu ni binti wa Naomi.

Wakati huo huo Boazi na Elimeleki mumewe Naomi walikuwa ni mtu na kaka yake. Hivyo ukiendelea kusoma habari hiyo mpaka mwisho kwa kuwa sasa hatuna nafasi ya kueleza habari yote, utaona kuwa mwisho wa siku Ruthu ambaye ni mwanamke wa kimataifa anakuja kuolewa na Boazi mtu mkuu wa Uzao wa kifalme, na ndiye kwa kupitia huyu Mfalme Daudi alitokea. Daudi ni kitukuu cha RUTHU.

Sasa kama tunavyojua mambo yote yanayotokea katika agano la kale ni kivuli cha mambo yanayoendelea katika agano jipya, habari yote ya Naomi na Ruthu, ni habari ya Kristo na bibi-arusi wake ambayo Mungu alikuwa anaichora kwa kupitia maisha ya hawa watu.

Kumbuka YESU Kristo alishuka kutoka mbinguni na utajiri mkubwa, kama Mfalme, aliyeacha enzi na mamlaka juu mbinguni, alikuja kwa watu wake Wayahudi, na hivyo alikaa nao, alikula nao,mfano tu wa Naomi jinsi alivyotoka Israeli na mumewe na watoto wake, na mali zao nyingi na kukaa katika nchi ya ugenini Moabu.

Lakini haikuwa vile kwa Naomi kama alivyotarajia, Mungu alimpiga na kumwacha pasipo kitu chochote na kubakia yeye tu alivyo. Picha kamili ya Bwana wetu Yesu kristo jinsi alivyopitia, ilimpasa yeye awe mfalme kwa wakati ule aliokuja ulimwenguni kwa mara ya kwanza lakini Mungu hakufanya hivyo kwa wakati ule, kinyume chake, alikataliwa, watu walimwona kuwa si kitu, walimtupa, walimtemea mate, walimpiga mijeledi, walizipiga kura nguo zake, walimsulibisha jaribu kufikiria mtu ambaye angepaswa awe mfalme lakini sasa anakuwa kituko kitu cha kuchekesha hana lolote tena..

Biblia inasema hivi juu yake: 

2 Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.

3 ALIDHARAULIWA NA KUKATALIWA NA WATU; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; NA KAMA MTU AMBAYE WATU HUMFICHA NYUSO ZAO, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.

4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.(Isaya 53)”….

8 Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; NA MAISHA YAKE NI NANI ATAKAYEISIMULIA? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.

9 Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya; Na pamoja na matajiri katika kufa kwake; Ingawa hakutenda jeuri, Wala hapakuwa na hila kinywani mwake.

10 Lakini Bwana aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake;

11 Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao.

12 Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji…

Unaona biblia inasema maisha yake Bwana Yesu ni nani awezaye uyasimulia?..Jinsi yalivyoonekana kuwa ya ajabu mbele za watu waliomwona kama vile maisha ya Naomi. Lakini kumbe Mungu alifanyia vile Naomi kwa makusudi ili ampate RUTHU haleluya..

Angalia ni upendo mkuu namna gani huo, kumgharimu Mungu kwenda kuyaharibu maisha na raha ya mwingine, kwa ajili ya mtu mmoja asiyestahili kupata lolote asiyekuwepo hata katika mzao wa kiyahudi huko mbali katika nchi za wachawi na waabudu masanamu…Kwani hakukuwa na wanawake wazuri Israeli, wenye kumcha Mungu wakati ule, walikuwepo, lakini kwa jinsi Rehema za Mungu zilivyokuwa nyingi, alikwenda kumtafutia Boazi mke mwema katika nchi za mataifa mabovu, tena kwa kuyaharibu kwanza maisha ya Naomi kwa kunyang’anya kila kitu pamoja na watoto wake ili tu Ruthu apate mlango wa kumwendea BOAZI.

Ndugu yangu, mimi na wewe hatukustahili kuitwa bibi-arusi wa Kristo hata kidogo..Wayahudi walistahili heshima hiyo, kwani wao ndio waliochanguliwa na Mungu tangu awali, Lakini Mungu alituhurumia sisi zaidi, na kuja kutuchagua kututoa sisi katikati ya mataifa, Na zaidi ya yote hakuja kututwaa pasipo gharama, hapana bali alimtoa mwanawe wa pekee ambaye ndiye kama Naomi wetu, kuja kuteseka kupoteza kila kitu alichokuwa nacho, kupigwa, kutemewa mate kudharauliwa, kwa ajili yetu, na mwisho wa siku kufa, na kufufuka na alipofufuka alitaka sasa kurudi kwa Baba yake juu mbinguni, katika makao yake aliyotoka huko kama vile Naomi alivyotaka kurudi kwa watu wa jamaa zake.

Lakini sasa tendo la sisi kumfuata Kristo lipo mikononi mwetu, na si mikononi mwake,..Je! tutaamua kuanza naye safari ya kwenda kwa BOAZI wetu mbinguni? Au tutataka kuwa kama Orpa, kuona kuwa Naomi hana faida yoyote kwetu, Yesu Kristo hana chochote cha kutugawia, tukimfuata tutaendelea kuwa maskini, tukimfuata tutakuwa washamba, tukimfuata kampani zetu za Disco na vilabuni zitatuacha, tukimfuata vimini vyetu tutavitupa, tukimfuata, tutaonekana vibibi,. tukimfuata tutakwenda kupotea moja kwa moja na kuwa vichaa..

Ndugu fahamu kuwa huu wakati ambao Bwana ameshakulipia gharama zote, hatakuja tena kukulazimisha, bali kinyume chake atakupa uhuru wa kuchagua, je! utakuwa tayari kujitwika msalaba wako kumfuata kama Ruthu au kuendelea kubaki katika dunia kama Orpa. Ukitaka kubaki kama Orpa ni sawa lakini kumbuka BOAZI yupo Israeli anamsubiria yule aliyetayari kumtii NAOMI, na maagizo yake yote.

Hivyo huu ni wakati wako wa kupiga gharama, mambo ambayo Wayahudi wameyakosa japo walikuwa wanayatazamia tangu zamani yamepewa wewe, mfano tu wa wale wajakazi wa Boazi waliokuwa wanafanya kazi shambani mwake miaka yote, hata mmoja hakuna aliyekuja kuolewa na Boazi isipokuwa mgeni wa mbali wa Ruthu. Ni kwasababu gani?..Ni kwasababu NAOMI ndiye aliyekuwa na SIRI ya jinsi ya kumwingia BOAZI na siri hiyo alipewa Ruthu peke yako.

Na ndio maana Bwana alimaanisha kuwaambia makutana maneno haya..

Luka 9:23 “Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.

24 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.

25 Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?”.

Na alisema “Mimi ndimi njia na kweli na Uzima mtu hafiki kwa Baba ila kwa njia yake yeye

Je! leo hii utachukua uamuzi wa kumfata Kristo? kama vile Ruthu alivyojitoa kikamilifu mpaka kuwa tayari kuacha vyote alivyonavyo kwa ajili ya mkwe wake?.

Hizi ni siku za mwisho Tubu ukabatizwe, moja ya hizi siku bibi-arusi wa Kristo atanyakuliwa kwenda kwenye karamu iliyoandaliwa huko juu ya Mungu mwenyewe, watakaofika huko ndugu si kila mtu anayejiita ni mkristo halafu maisha yake yanaonyesha kabisa hajachukua msalaba wake kumfauta Kristo, mguu mmoja upo nje, mwingine ndani, watakaokwenda kwenye unyakuo ni wachache sana, ni kikundi kidogo sana mfano wa Ruthu pekee yake, wale walioamua kumfuata Kristo kikweli kweli pasipo kuangalia mbele wala nyuma, Nawe usiwe ni mmojawapo wa watakaokosa karamu hiyo. Ni heri upoteze kila kitu sasa kuliko kuikosa karamu ya mwana-kondoo.

Ubarikiwe sana

Print this post

“WOKOVU WETU U KARIBU NASI KULIKO TULIPOANZA KUAMINI”

Kila mmoja wetu anapiga hatua, na hizi hatua tunapiga kuelekea mahali Fulani, ilikuwa juzi ikawa jana, na sasa imekuwa leo, na hiyo ipo bayana kabisa kuwa yapo mambo mazito mbele yetu yanayotusubiri , upo unyakuo mbele yetu, na kama unyakuo hatutaukuta basi kifo hatutakikwepa..Leo unaweza ukasema kesho kutwa nitafanya hivi au nitafanya vile, au mwakani nitakuwa nimeshafika mahali Fulani, lakini kumbuka hata aliyekufa jana naye sio kwamba alijua safari yake imefika, hapana na yeye pia aliiona mbele yake kuwa itakuwa hivi au vile n.k…

Mtume Paulo aliwaambia watakatifu waliokuwa Rumi maneno haya “wokovu wetu sasa upo karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini”..Unaona? Hii ikiwa na maana kuwa leo hii tupo karibu na unyakuo zaidi kuliko ilivyokuwa jana na juzi, kuliko ilivyokuwa enzi za mtume Paulo..Na kama ni hivyo basi inatupaswa sisi watu wa kizazi hiki tuwe makini kiasi gani?..Ni wazi kuwa inatupaswa tumtafute Mungu zaidi, tujishughulishe na mambo ya mbinguni kuliko wao, tuishi maisha ya kujichunga mara nyingi zaidi ya wao.

Je! Unafahamu kuwa kanisa tunaloishi ndilo kanisa la mwisho lijulikanalo kama Laodikia, na kuwa baada ya hili kuisha hakutakuwa na kanisa lingine lolote? kulingana kitabu cha Ufunuo 2&3. Kanisa hili litamalizikia na unyakuo, na ndilo kanisa la 7, Tofauti lile la mitume walilokuwa wanaishi ambao lilikuwa ni kanisa la Kwanza lijulikanalo kama Efeso, Na mjumbe wa kanisa hili la Laodikia ni WILLIAM BRANHAM na alishatoa ujumbe Mungu aliomtumwa kuuleta na kuondoka..Je! unalifahamu hilo?

Unafahamu kuwa unyakuo utakuwa ni kwa siri sana, na si kila mtu atafahamu habari hiyo kama wengi wanavyodhani? Kwamba Kutakuwa na makelele barabarani, na maajali.? Ni kundi dogo sana litakaloondoka, kiasi kwamba ulimwengu hautajua lolote, isipokuwa kikundi kidogo sana.

Unafahamu kuwa Ile Roho ya Mpinga-Kristo tayari imeshaanza kufanya kazi, na hiyo haitendi kazi pengine popote nje ya Kiongozi mkuu wa kidini mwenye wafuasi wengi kuliko wote duniani huko Vatican Roma?

Unafahamu kuwa Injili hii unayohubiriwa moja ya hizi siku itasikika Israeli kwa nguvu na wayahudi wote wataamini, na tukio hilo ukilishuhudia basi ujue kuwa unyakuo ulishakuacha siku nyingi. Kwasababu Mungu alishaahidi kuwa atawarudia watu wake, wayahudi, na siku atakayowarudia unyakuo utakuwa umeshapita.

Kwani ule unabii waliotabiriwa juu yao kwamba watarudi katika nchi yao umeshatimia, jopo kubwa la wayahudi wamesharudi kwao, na wachache waliosalia wanarudi kwa kasi sana, wanachongojea ni kumwagiwa roho ya Neema tu.Wamwamini masihi wao waliomsulibisha. Na kisha wawe tayari kumpokea.

Takwimu zinaonyesha kuwa hakuna taifa ambalo injili ya Kristo Yesu haijahubiriwa mpaka sasa, kila mji na kila kijiji, Yesu Kristo kashatajwa,na kumbuka biblia inasema pindi tu habari njema za ufalme zitakapohubiriwa katika ulimwengu wote hapo ndipo ule mwisho utakapokuja..Unadhani ni kitu gani Mungu anasubiria sasa..

Biblia imesema mambo mengi sana juu ya yatakayotekea siku za mwisho hatuwezi kuyazungumza yote hapa, lakini moja ya dalili ya wazi kabisa ambayo hata wewe unaiona ni juu ya kutokea kwa manabii wengi wa uongo. Wimbi hili lilianza kulipuka mwanzoni mwa miaka ya 2000, lakini limekuja kukolea zaidi kuanzia kipindi cha miaka ya 2010, Hii inayoonyesha wazi ni jinsi ule mwisho unavyokuja kwa haraka sana kushinda sisi tunavyofikiri.

Ishara nyingine ni kuwa Maasi yataongeza..Leo hii tunashuhudia vitendo viovu, na vya kikatili kila mahali, mambo machafu kwenye mitandao, kila aina ya uozo upo wazi siku hizi hadharani, wala sio siri tena hata watoto wadogo hakuna kitu chochote wasichokijua kinachoendelea cha ulimwengu huu.

Biblia inasema wakati huu wa mwisho ukikaribia kufika ndipo wale watu wa kukufuru na kudhihaki watakapoongoza, wakisema iko wapi ile ahadi ya kuja kwake,.. mbona YESU harudi tumwone, miaka 2,000 imepita amekufa nini?, pamoja na hayo mithali kadha wa kadha za kejeli zimetungwa kwa watu wote wote wanaomtazamia Kristo kuja. Hata injili zenyewe zimegeuzwa sasa, hakuhubiriwi tena kuja kwa Kristo kama zamani, bali mafanikio ya kidunia. Injili shetani alizomhubiria Bwana za kumpa Milki zote za dunia endapo akimsujudia.

Na kwa bahati mbaya watu wanaangalia wakidhani kuwa siku hiyo ikikaribia kufika pengine duniani kutakuwa na vita na machafuko ya kila namna.Lakini biblia inatuambia kuwa wakati wasemapo AMANI! AMANI!, ndipo uharibifu unapokuja kwa ghafla..

1Wathesalonike 5:2 “Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.”

Na ndio maana mtume Paulo anasema:

Warumi 13:11 “Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa MAANA SASA WOKOVU WETU U KARIBU NASI KULIKO TULIPOANZA KUAMINI

12 Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.

13 Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.

14 Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake”.

Ndugu kwanini ujiweke katika hali ya hatari kama hii, leo ni siku nyingine, tumeukaribia mwisho kuliko jana, usiseme bado nipo, bado sijawa tayari, utajikuta unaangukia kifo au dhiki kuu gafla. Saa ya wokovu ni sasa,hiyo kesho hata Bwana kasema tusiisumbuke kwasababu hatujui yatakayozaliwa ndani ya siku moja. umekufikia ujumbe huu mahali ulipo, unadhani ni kwa bahati bahati tu. Jua kuwa Mungu anataka kusema na wewe ili ayabadilishe maisha yako.

Bwana anasema, laiti mwenye nyumba angelijua saa ambayo mwizi atakuja usiku basi angelikesha. Hata ingekuwa ni wewe ungefanya hivyo.Lakini kwasababu hutaki kuibiwa usiku na ndio maana kubla hujalala unahakikisha umeufunga vizuri mlango wako kwa makomeo, Sio kwasababu unapenda kujifungia hapana. Ni kwasababu unachukua tahadhari kwasababu hujui ni lini mwizi atakuja.

Halikadhalika mimi na wewe hatujui siku ya kuja kwa BWANA, kwahiyo ni wajibu wetu kukesha, kuamka usingizini, kuvua mambo yetu ya kale, kuanza maisha mapya na Mungu wetu katika kizazi hichi cha hatari tunachoishi. Lakini tunajua tu muda  umekwenda sana.

Ikiwa utataka kutubu kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako, basi Kristo atakupokea na kukuosha dhambi zako.Na ukishabatizwa katika ubatizo sahihi wa kimaandiko (yaani ubatizo wa kuzamishwa na kwa jina la YESU KRISTO), kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako(Matendo 2:38). Basi yeye mwenyewe atakutia muhuri kwa Roho wake Mtakatifu kuwa ni wake,(Waefeso 4:30) na kisha baada ya hapo utaishi katika tumaini ukijua kabisa hata leo hii mambo yakibadilika utakuwa katika upande salama Ikiwa utaendelea kudumu katika njia zake..

Pia na wewe ambaye tayari ni Mkristo kumbuka kuwa “WOKOVU WETU U KARIBU NASI KULIKO TULIPOANZA KUAMINI”. Hivyo huu si wakati wa kulegea au kupoa,au kutazama mambo ya ulimwengu huu, bali huu ni wakati wa kuzidi kujitakasa kila iitwapo leo, maadamu tunaona siku inakaribia na kwamba muda wowote tunaweza kuitwa juu nyumbani kwa Baba. Biblia inasema “tuutimize wokovu wetu kwa kuogopa na kutetemeka Wafilipi 2:12

Ubarikiwe sana.Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


JINSI MWISHO ULIVYOKARIBIA.

AGENDA KUBWA YA SHETANI KWA KANISA HILI LA LAODIKIA.

VIUNO VYENU VIWE VIMEFUNGWA NA TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA

WILLIAM BRANHAM NI NANI?


Rudi Nyumbani

Print this post

NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA!

Shalom karibu tujifunze Neno la Mungu! Katika biblia takatifu leo,tunajifunza kwa sehemu maisha ya Yesu Kristo, ambayo ni muhimu sana kwetu sisi, kwasababu ni tiba ya mambo mengi. Kama biblia inavyotuambi kwamba “inatupasa tumfahamu SANA mwana wa Mungu, hata kufikia cheo cha kimo cha utimilifu wake, ili tusiwe tena watoto wachanga wa kupelekwa na upepo huku na kule (Waefeso 4:14)”.

Tunasoma Bwana wetu Yesu Kristo alikuwa akizunguka mahali na mahali, kuhubiri injili, kwa marika yote na kwa watu wa aina zote, matajiri kwa maskini, wasafi kwa wachafu, wakubwa kwa wadogo hakuchagua kundi fulani tu! bali alienenda kwa wote..Ikifutufundisha na sisi pia kwamba tunapopeleka injili hatupaswi kubagua kundi fulani… kuna watu hawapeleki injili kabisa kwa maskini, na kuna watu pia hawapeleki injili kabisa kwa matajiri, ..hilo Bwana yeye hakulifanya, kwasababu nia yake yeye ilikuwa sio kutafuta faida fulani bali kutafuta roho za watu.

Lakini tunasoma, alipokuwa anaingia kila mahali, kila mtu alikuwa anamdhania tofauti…alipoingia kwa maskini na wenye dhambi alionekana kama mlevi na mtu asiyekuwa na maana…alipoingia kwa matajiri alionekana anatafuta faida fulani labda fedha kutoka kwao…Lakini nia yake haikuwa kutafuta fedha bali kuwafanya watu watubu wamgeukie Mungu..

Mathayo 9:10-13 “Ikawa alipoketi nyumbani ale chakula, tazama, watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja wakaketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake.

11 Mafarisayo walipoona, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?

12 Naye aliposikia, aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi.

13 Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi”.

Unaona hapo Bwana anasema “NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA;”…Nia ya kuingia kwa watoza ushuru ambao walikuwa ndio matajiri kwa wakati huo sio kutaka fedha au zawadi kutoka kwao, hapana bali kutaka rehema…

kwamba wajione kuwa ni wenye dhambi na hivyo watubu!!.

Wengi wetu tunadhani, Bwana ana haja sana na mali zetu tulizonazo…au ana huzuni sana na umaskini tulionao…Nataka nikuambie ndugu yangu, Bwana haji kwako ili kutaka fedha au kukupa fedha, Bwana anakuja kwako kwa ajili ya roho yako, hauzuniki kwasababu ya umaskini wako wa mwilini bali anahuzunika sana kwasababu ya umaskini wako wa rohoni, ahufurahii sana utajiri wako wa mwilini bali anaufurahia sana utajiri wako wa rohoni…

leo hii anazungumza na wewe hapa!! Ni sawa tu na amekutembelea nyumbani mwako, ANATAKA REHEMA NA WALA SI SADAKA…ndio maana alisisitiza na kusema “nendeni mkajifunze nini maana ya maneno haya”…..sentensi hiyo ina maana kuwa hawakumwelewa nia yake ya kuingia kwenye nyumba za maskini na matajiri…hivyo wanapaswa wakakae chini wakajifunze kwa utulivu, wamwombe na Mungu awafunulie, nia ya Kristo ni nini kuwaendea, vinginevyo wataishia kutokumwelewa maisha yao yote…….. Ndugu Kristo anataka utubu uache dhambi, umgeukie yeye ili akupe uzima wa Milele, hataki sadaka yako, Yeye kila kinatoka kwake,

Anataka roho yako kwasababu kuna hukumu mbeleni inakuja kwa watu wote wasiomcha Mungu, na yeye hapendi mtu yeyote apotee kama maandiko yanavyosema. Kaa chini ujifunze ujue anataka nini kwako.

Mfano mwingine tunaweza kujifunza ni wakati Bwana anaingia kwenye nyumba ya mwanamke mmoja anayeitwa Martha, Martha hakuwa Tajiri alikuwa ni mtu wa kawaida tu, na alikuwa na dada yake anayeitwa Miriamu ambaye alikuwa anaishi naye…Siku moja akasikia Bwana anataka kuja kumtembelea nyumbani kwake…Kama tunavyojua wanawake wataanza kuhangaika huku na kule mambo ya jikoni, mara kusafisha sebule, mara kufagia uwani, mara kupika mboga hii na ile, mara kutengeneza kachumbari n.k n.k unakuta shughuli zinakuwa ni nyingi mpaka wakati mgeni anafika zinakuwa bado hazijaisha…Ndivyo ilivyokuwa kwa Martha alikuwa na shughuli nyingi mpaka Bwana anafika bado zilikuwa hajazimaliza…Na mdogo wake Miriamu alipomwona Bwana kaingia akaacha kumsaidia dada yake kazi na kwenda kuketi miguuni pa Bwana akisikiliza maneno ya uzima, wakati huo Martha bado ana vishughuli shughuli vingi huko jikoni..

Pengine akawa anajaribu kumwonyesha Miriamu viishara fulani atoke pale sebuleni , ili aje akashughulike kule jikoni na wenzake..lakini yeye kakazana kumsikiliza Bwana na maneno yake. Martha akashindwa kujizuia akaanza kuzungumza na Bwana..tunasoma habari hiyo katika …

Luka 10: 38 “Ikawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake.

39 Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake.

40 Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie.

41 Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi;

42 lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa”.

Unaona jibu la Bwana hapo??…wengi hata mimi ningeweza kusema Bwana angemkemea Miriamu kwa uvivu..lakini haikuwa hivyo kwa Bwana badala yake alimsifia mbele ya dada yake Martha…Neno ni lile lile.. “Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA”… Bwana hatafuti chakula kizuri, wala maandalizi mazuri, wala sadaka za mtu, wala huduma ya mtu, wala hapendezwi sana na sifa za mtu anazompa zaidi ya Rehema, anataka Toba!! Anataka uzima wa rohoni wa mtu, Hicho ndio cha kwanza anachokihitaji!…kwa ufupi laiti Martha angeanza kwanza kwa kukaa chini na kumsikiliza maneno yake, ndipo baadaye ampikie yeye na wanafunzi wake ingekuwa sawa…lakini yeye alitanguliza huduma kabla mtoa huduma hajatoa huduma yake..na matokeo yake alimwambia “unahangaika na kujisumbua kwa mambo mengi na wakati linalohitajikwa kwa sasa ni limoja tu REHEMA!”..Kaa chini kwanza sikiliza maneno ya uzima na hayo mengine yatafuata baadaye.

Ndugu yangu jifunze ni kitu gani Kristo anataka kwako. Usihangaike, wala usihangaishwe na kutoa sadaka wakati maisha yako ni machafu, ni kupoteza muda tu!! Kristo hajaja kukitafuta hicho kwako, usijisumbue kuhakikisha hukosi kutoa fungu la kumi kila siku na hali ndani ya moyo wako kumejaa kutokusamehe, kumejaa usengenyaji,kumejaa rushwa, kumejaa uasherati, kumejaa ulevi, anasa, pornography, ndani ya moyo wako kumejaa kutokujisitiri, kumejaa masturbation, kumejaa ibada za sanamu na miungu, kumejaa safari za waganga, kumejaa wivu na mambo yote mabaya.. Usijaribu kumfanyie yeye huduma kabla yeye hajakufanyia huduma…utaishia kumhuzunisha badala ya kumfurahisha, anachotaka kwako kwanza ni moyo safi…hiyo ndiyo sadaka ya kwanza anayoikubali mbele zake, Ndio maana Bwana aliwakemea mafarisayo kwa mambo hayo hayo..

Mathayo 23:23 “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache”.

24 Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia.

25 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang’anyi na kutokuwa na kiasi.

26 Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi”.

Usitafute kufunga siku nyingi, au miezi mingi…wakati ndani yako hujataka wala kukusudia kuacha dhambi (kusamehe wale wote waliokukosea na mambo mengine yote)..hiyo siyo saumu Bwana anayoitaka..swaumu Bwana anayoitaka ni hii…

Isaya 58: 3 “Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.

4 Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu.

5 Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana?

6 JE! SAUMU NILIYOICHAGUA, SIYO YA NAMNA HII? KUFUNGUA VIFUNGO VYA UOVU, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?

7 Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?

8 Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.

9 Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;”

Ni maombi yangu Bwana atakujalia kuyafahamu hayo na zaidi ya hayo na kuyatendea kazi. Kama hujampa Bwana maisha yako kikweli kweli, mlango upo wazi lakini sio siku zote, njia ya mlango huo inazidi kuwa nyembamba kwa kadri siku zinavyozidi kwenda, njia hiyo inazidi kusongwa siku baada ya siku, jana ilikuwa rahisi kwako kuokolewa kuliko leo na itafika wakati njia itakuwa nyembamba mpaka hakutakuwa na nafasi tena ya kupita na mlango utafungwa..

Hivyo ni vyema unapoyasikia haya leo uzingatia kumrudia Mungu wako kwa kutubu na kumaanisha kuacha dhambi zako..na maisha ya kale uliyokuwa unaishi yasiyompendeza Mungu, na Bwana atakusamehe na kukukaribisha kwake. Na baada ya kutubu katafute ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako (Matendo 2:38), huo ni muhimu sana, kila aliyeamini alizingatia kubatizwa. Na baada ya hapo Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu, atakayekusaidia kushinda dhambi na kukutia katika kweli yote ya kuyafahamu maandiko. Na kwa kufanya hivyo utakuwa na uhakika wa uzima wa Milele.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine na Bwana atakubariki!


Mada Zinazoendana:

UDHAIFU WA SADAKA!

SADAKA ILIYOKUBALIKA.

TOFAUTI KATIKA YA ZAKA NA SADAKA NI IPI?

IKO NJIA IONEKANAYO KUWA SAWA MACHONI PA MTU.


Rudi Nyumbani

Print this post

NITAIFAHAMU VIPI KARAMA YANGU?.

Zipo karama tofauti tofauti zilizogawanywa na Bwana katika kanisa, hizo tunazisoma katika kitabu cha 1 Wakoritho 12:4-12

4 “Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.

5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.

6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.

7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.

8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;

9 mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;

10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;

11 lakini kazi hizizote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.

12 Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo.”

Vipawa vyote hivi Mungu hugawa kwa jinsi apendavyo yeye..hakuna mtu anayechagua awe hivi au vile, hicho huwa mtu anazaliwa nacho Mungu anakishusha juu yake yeye mwenyewe.

Na vipawa vimegawanyika katika sehemu mbili, mwilini na rohoni, vipawa vya mwilini vinapimwa katika … nguvu,ushupavu, wepesi,akili, uzuri, mbio, uwezo Fulani wa kipekee katika michezo au darasani, uchoraji, au uandishi, ubunifu, au uimbaji, wengine uongozi, wengine ualimu, n.K kuna maelfu ya vipawa hivi na kila mtu anacho cha kwake…na wakati mwingine sio lazima mtu akijue kipawa chake anaweza akawa anakifanya hata pasipo yeye kujijua…Pia wengine wamepewa viwili viwili, wengine kimoja wengine vitano..Mungu ndiye agawaye jinsi apendavyo..

Lakini leo hatuzungumzii vipawa hivyo vya mwilini tutazungumzia vipawa vya rohoni, kama tunavyosoma katika kitabu hicho cha 1 Wakorintho 12..Kumbuka vipawa vya rohoni pia mtu anakuwa anazaliwa navyo, kama tu vipawa vya mwilini, isipokuwa kama mtu hajampa Kristo maisha yake kipawa kile kinaweza kuzimwa na shetani au shetani akakitumia kwa manufaa yake mwenyewe.

Kwamfano mtu anaweza akawa amezaliwa na kipawa cha unabii, lakini kwa kuwa maisha yake ya utotoni hayakuwa ya kikristo au wazazi wake sio wakristo, au wamemweka wakfu katika madhabahu za miungu, sasa kwa kuwa shetani anakuwa na hati miliki naye asilimia 100, basi anakuwa na uwezo wa kuizima ile karama isifanye kazi yoyote…ndio hapo baadaye mtu akishakuja kumpa Kristo maisha yake na kubatizwa anajikuta anaanza kuona maono n.k ambayo hapo kwanza alikuwa hayaoni, sasa, hiyo karama sio kwamba aliipata baada ya kumpa Kristo maisha yake, hapana bali alikuwa nayo tangu alipozaliwa, isipokuwa shetani alikuwa ameizuia. Au pia shetani anaweza asiifukie bali anainyakua na kuitumia kupitisha maono yake ya uongo, mara nyingi watu wa namna hiyo wanaishia kuwa waganga wa kienyeji,wenye roho za utambuzi.

Mwingine unakuta amezaliwa na karama fulani ya uongozi, lakini kwasababu bado hajampa Kristo maisha yake, shetani anaweza akaifukia ile karama, au akaitumia kwa mambo yake, ndio hapo unakuta mtu anakuwa ni kiongozi wa vikundi haramu, au kiongozi wa mambo maovu…Na siku anakuja kumpa Kristo maisha yake kikamilifu anajikuta anachukia zile kazi mbovu na kutafuta uongozi katika kazi za Mungu, ndio hapo unakuta anaenda kuwa Mchungaji, au Shemasi n.k.

Na karama nyingine za rohoni ndio hivyo hivyo kama uimbaji, imani, uinjilisti, ualimu,uponyaji, lugha n.k. Ndio maana kuna umuhimu sana wa Mtu kumpa Yesu Kristo maisha yake na kuzingatia ubatizo sahihi ili Roho Mtakatifu apate nafasi ya kumsafisha maisha yake na kufufua kile kipawa alichokiweka ndani yake.

Sasa wapo wengi wanapenda kujua karama zao, utasikia mtu anakwambia nitaijuaje karama yangu?..mimi sijui karama yangu? Nimejaribu kumwomba Mungu anionyeshe hajanionyesha, nimefunga sana na kusali bado sijaijua n.k

Nitaka nikuambie ndugu, karama yako hutaijua kwa kuichunguza chunguza, wala Mungu hatakwambia una karama hii wala ile, ni mara chache sana Mungu mwenyewe ndio anamwambia mtu karama yako ni hii au ile, wengi wanajipachikia karama kwasababu tu wanaipenda ile karama, lakini karama ya rohoni Mungu anampa kila mtu kwa jinsi anavyotaka yeye sio kwa jinsi anavyotaka mtu. Toa kabisa kwenye akili yako hiyo karama unayodhania ni yako, kwasababu inawezekana ikawa sio yako.

Namna ya kuifahamu karama yako ni rahisi sana…Kwanza kanuni ni ile ile, kumpa Yesu Kristo maisha yako kikamilifu, ikiwa na maana kumwamini Bwana Yesu Kristo kwa ufunuo wa Roho kuwa ni Mwokozi wa Maisha yako,na kwamba alikufa na akafufuka na akapaa mbinguni, na pia anaweza kukuokoa na wewe na kukufanya kiumbe kimpya.

kisha baada ya hayo ni kufuata maagizo yake ya kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, upate ondoleo la dhambi zako na kuzingatia kuishi maisha matakatifu kuanzia huo wakati na kuendelea…Kwa kufanya hivyo utakuwa umeweza kujinasua kutoka kwenye nguvu za giza ambazo zilikuwa zimeshika karama Mungu aliyokuwa amekuwekea ndani yako.…kumbuka shetani hataki ujue karama uliyo nayo kwasababu anajua itamletea madhara makubwa sana katika ufalme wake wa giza..Kwahiyo kitu cha kwanza hatakutumia wachawi wakuloge hapana! Ondoa kabisa hiyo akilini. Bali atakutumia mapepo yatakayohakikisha wewe humpi Kristo maisha yako kikamilifu. Au yatakayo kufanya usisimame imara kwa Mungu. Mapepo YATAKAYOKUFANYA USIMWELEWE YESU KRISTO NI NANI ili yapate uhakika kuwa hutakaa uijue karama yako daima.

Pili baada ya kuzaliwa mara ya pili kwa kumpa Kristo maisha yako, bado usianze kujichunguza chunguza karama yako ni ipi…Subiri!! Usianze kusema aa labda mimi ni mchungaji, au mwalimu au nabii…usifanye hivyo hata kidogo!!! Unachotakiwa kufanya ni kwenda kujiunga na kikundi cha wakristo wenzako kanisani, au mahali unapoishi, au popote pale…kile roho anachokusukuma kukifanya pale kwenye lile kusanyiko pasipo kumwiga mtu mwingine, wala pasipo kusukumwa wala kushuritishwa kifanye hicho…na kama kinakupa amani, na endapo ukijaribu kukiacha kukifanya kinakukosesha raha..hicho hicho kifanye, msukumo huo usiuzimishe endelea nao huo huo…

Baada ya muda Fulani, labda mwezi, au mwaka, au miaka kadhaa Bwana mwenyewe atakufunulia…na atakufunulia kwa namna hii: utaanza kusikia watu wanaanza kukuita mchungaji, au wengine wataanza kukufata na kukuomba uwaongoze katika sala au katika uimbaji…au wengine wataanza kukwambia tunaomba utuombee ukiona watu wengi wanakufuata hata usiowajua wanakuomba uwaombee ni kwasababu hapo nyuma wamekuona kwa muda mrefu kila ukiombea watu wanapona..Hivyo kwa kupitia hao unajua Bwana kakupa karama ya UPONYAJI.

Wengine watakuja wakikuomba uwaongoze katika kuabudu na kusifu, utaona mara kwa mara wanakutaka wewe ufanye hivyo, ni kwasababu wameona kila unapowaongoza kwenye sifa na kuabudu uwepo wa kipekee unashuka juu yao, uponyaji unatokea, faraja zinatokea, na watu wanageuka maisha yao..kwahiyo kwa kupitia hao unajua Bwana kakupa karama ya UIMBAJI.

Wengine watakuja na kukuomba uwaulizie Neno kutoka kwa Bwana, ni kwasababu wamekuona muda mrefu unatoa unabii na unakuja kutimia,unaona maono mara kwa mara nayo ni ya kweli, kwahiyo wakajua lazima utakuwa ni nabii…hivyo kwa kupitia hao ndio utajua kuwa Bwana kakupa karama ya kinabii.

Wengine utaanza kuona wanaanza kukuita mwinjilisti..ni kwasababu wameona mazao mengi uliyoyaleta kwa Kristo katika kuhubiri kwako, tofauti na wengine, hata kama watahubiri kutwa kuchwa, hawawezi kulinganisha na uinjilishaji wako unaoweza kuwavuta watu haraka kwa Kristo. na kama ukiwachunguza utaona hawakuiti hivyo kama kwa kujipendekeza kwako au kwa kutaka kukupa sifa bali utaona ni kama kwa kumaanisha hivi.… kwahiyo hapo utaelewa kwamba Bwana alikuchagua kabla ya kuzaliwa uwe mwinjilisti wake kwa kazi yake maalumu, ya kuvuna roho za watu na kusafisha ghala la shetani.

Wengine watakuja na kukwambia tunaomba utufundishe, ni kwasababu hapo nyuma wamekuchunguza kwa muda mrefu wakajua ukiwafundisha wewe wanaelewa zaidi kuliko mwingine ndio maana wanakufuata uwafundishe, kwahiyo kwa kupitia hao unajua Bwana kakupa karama ya UFUNDISHAJI au UELEKEZAJI.

Wengine watakufuata na kukwambia tunaomba ushauri, utashangaa kila anayekufuata hataki kuombewa, wala kuwekewa mikono hata kama anatatizo kubwa kiasi gani, anataka tu umshauri, anataka tu kukusikiliza umweleze njia impasayo akitoka huyu anakuja mwingine..ujue kwamba wamekuchunguza kwa muda mrefu na kujua kwamba wewe una Hekima..Hivyo wamepata mahali panapostahili..kwahiyo kwa kupitia hao utagundua umepewa karama ya NENO LA HEKIMA. Kwaajili ya kuwajaza hekima watoto wa Mungu.

Wengine watakufuata, wengi tu hawataki kuombewa wanataka faraja tu, na wanakufuata wewe tu, hawaendi hata kwa wachungaji wala manabii, wanakutaka wewe tu, ujue ni kwasababu wameona Maneno ya faraja ndani yako…kwa kupitia hao utajua kuwa kakupa karama ya FARAJA ndani yako. Hivyo ile silaha ya Bwana katika kuwaganga wale waliovunjika mioyo imo ndani yako.

Na karama nyingine zote ndio hivyo hivyo, utazijua kutokana na ushuhuda wa watu, wanakushuhudia wewe ni nani? Mtu hawezi kwenda kwenye duka la madawa kununua unga wa ngano, au hawezi kwenda hardware kununua dawa ya meno kila duka na bidhaa za aina yake..wateja ndio watakaosema pale utapata hichi, na pale kile…Usitafute kujipachikia karama kwa kujitazama au kwa kutafuta sifa Fulani au kwa kuona kwasababu karama ile inapendwa na wengi ngoja na mimi nijipe. Huko ni kujikweza ambapo Bwana Yesu alisema ajikwezaye atashushwa na ajishushaye atakwezwa.

Kila mmoja Mungu kamuumba na upekee wake, sio lazima sauti yako ifanane na ya Yule, kuhubiri kwako kuwe sawa na kwa Yule, hata Mungu japo alituumba kwa mfano wake, lakini lakini alimpa kila mmoja sura yake tofauti japo wote ni wanadamu. Vivyo hivyo na katika karama zake, alimpa kila mmoja wetu karama tofauti na hata ikitokea wawili au watatu au mia wanakarama moja, basi biblia inasema upo utofauti wa utendaji kazi, utendaji kazi wa huyu hauwezi ukawa sawa na wa Yule kwamba kila kitu wafanane hapana ukiona hivyo basi ujue ipo roho ya ufuasi nyuma ya huyo mtu.

Na lengo la hizo karama za rohoni ni tofauti za zile za mwilini, karama za mwilini nyingi zina lengo la kumpatia mtu riziki au kumfanya aishi katika dunia hii, au kumpa Mungu utukufu, mtu anakuwa na kipaji cha kukimbia ili akimbiapo apate tuzo itakayokuwa kama ni sehemu yake ya kupatia kipato, lakini karama za rohoni hazipo kwa lengo hilo…karama zote za rohoni ni kwa kusudi la kulijenga kanisa, kuwafanya watakatifu wawe wakamilifu, na kuwahudumia roho zao, na zote zinakuwa na lengo moja la kuwasafisha watu na kuwatengeneza kwa ajili ya kwenda mbinguni.

Kwahiyo ukiona msukumo wowote ndani yako unakuja kwa lengo la kwenda kujipatika kipato! Hiyo siyo karama ya Roho Mtakatifu, achana nayo ni kutoka kwa Yule mwovu. Karama za Mungu ni kwaajili ya kuujenga mwili wa Kristo na kuwatengeneza watakatifu. Utauliza hilo tunalipata wapi katika maandiko..soma.

Waefeso 4.11 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;

12 KWA KUSUDI LA KUWAKAMILISHA WATAKATIFU, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;

13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;

14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu”

Na Karama ambayo shetani anapenda sana kuwanasa watu wengi ni karama ya kinabii na uimbaji.. Hizi karama mbili ndizo karama ambazo shetani anajua watu wengi wanazipenda, wengi wanapenda kuitwa nabii nabii na wengi wanapendwa kuitwa waimbaji maarufu…. Kwasababu wanapenda umaarufu pamoja na fedha..nataka nikuambie ndugu yangu, asilimia kubwa ya wanaoimba miziki inayoitwa ya injili na manabii…ni waimbaji wa uongo na manabii wa uongo..

Kwanini ni manabii wa uongo na waimbaji wa uongo?? Jibu lipo hapo juu kwenye waefeso 4:12…je! WANAWAKAMILISHA WATAKATIFU??...au wanawaharibu watakatifu kwa mavazi yao na mienendo yao, na mafundisho yao?? JE! WANATUFIKISHA KATIKA CHEO CHA KIMO CHA UKAMILIFU WA KRISTO??...au wanatupeleka katika cheo cha kimo cha kumfahamu shetani? Wanachoimba na wanachokiishi kinawafanya watu watubu, au kuwafundisha watu chuki?

Ni matumaini yangu kuwa Bwana atakujalia kuyafahamu haya na zaidi ya haya. Na hatimaye kuifanya kazi yake kwa uaminifu katika Karama sahihi aliyoiweka ndani yako.

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post

MAOMBI YA YABESI.

Shalom mwana wa Mungu, karibu tujifunze habari njema za Yesu Kristo ziletazo tumaini la maisha yetu ya sasa na ya baadaye. Leo tutajifunza habari za mtu mmoja anayeitwa Yabesi, Pia tutaona jinsi alivyomwomba Mungu kwa bidii na dua yake kusikiwa. Habari hizo tunazisoma katika kitabu cha 1Nyakati 4:9-10, Tusome.

“Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni.

10 Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.”

Yabesi kama tunavyomsoma hapo, mwanzo wa maisha yake haukuwa mzuri kabisa, inawezekana yeye alikuwa mtoto ni wa mwisho kati ya ndugu zake, na wakati alipokuwa anazaliwa kama biblia inavyotuambia mama yake alikuwa katika hali ya huzuni nyingi, pengine alikuwa anapita shida za kiafya hatujui, au pengine kiuchumi, au pengine wakati Yabesi anazaliwa mama yake alikuwa katika misiba mizito ya kufiwa na ndugu zake, yote hayo yanawezekana. Hivyo kutokana na kuwa katika hali ile ya huzuni nyingi jambo hilo lilimfanya aione mimba ya Yabesi kuwa ni tofauti na za watoto wake wengine aliowazaa, pengine wale wangine aliwazaa katika furaha, katika mafanikio, hakuugua sana, aliletewa zawadi nyingi, tofauti na kwa huyu Yabesi, ni wakati wa huzuni na majonzi tu! na ndio hiyo ikampelekea hata kumpa mtoto wake jina la Yabesi. Ikiwa na maana ya HUZUNI.

Na unafahamu zamani zile mfano mtu akipewa jina ni lazima libebe maana kubwa sana juu ya maisha yake ya baadaye. Hivyo Yabesi kuitwa lile jina iliashiria kuwa maisha yake yote yatakuja kuwa ni maisha ya huzuni, uchungu, mtu wa kulemea wengine, mtu wa nuksi na mikosi, tabu, majonzi n.k. Hakuna mtu aliyeweka tumaini lolote jema la Yabesi mbeleni.. Lakini Yabesi aliendelea kukua na hilo jina akiona kuwa hakuna mtu mtaani kwao aliyeitwa kwa jina kama hilo. wakati watoto wengine wanaitwa majina mazuri kama Furaha, Amani, Upendo, Tumaini, Faraja, Godbless, Neema, Rehema n.k. yeye anaitwa, huzuni, msiba, Matatizo, masumbuko, shida, tabu, majuto. Hilo lilimwingia sana moyoni mwake, pengine lilimpa mawazo mengi maishani kufikiri juu ya hatma yake itakavyokuwa, kuwa atakuwa mtu wa huzuni siku zote za maisha yake.

Lakini tunaona biblia inatuambia Yabesi alikuwa na heshima kuliko ndugu zake wote. Aliwazidi wote kwa tabia njema, japo wengine walimwona kuwa ni mtu wa laana tu lakini yeye aliona njia pekee ni ya kutafuta kibali machoni pa Mungu na katika maneno ya watu. Ndipo akaanza kuutafuta uso wa Mungu kwa bidii na kuanza kumuomba dua hizi akisema..

 “Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, NAWE UNGENILINDA NA UOVU, ILI USIWE KWA HUZUNI YANGU!”

Unaona alikuwa anautafuta uso wa Mungu alikuwa anatafuta kufanya mapenzi ya Mungu, na biblia inatuambia “Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.”.. Bwana anasema ni baba yupi mwanawe akimwomba mkate atampa jiwe, au akimwomba samaki atampa nyoka?..Yabesi alimlilia Mungu na Mungu akasikia dua zake, alimjalia kutanuka kwa himaya yake kama alivyoomba, hata zaidi ya ndugu zake Mungu alimjali kutembea naye wakati wote kama alivyomwomba. Lakini kikubwa zaidi tunaona alichomwomba Mungu ambacho kingeweza kuiondoa ile laana yake ya nyuma ni “Mungu amlinde na UOVU”.

“NAWE UNGENILINDA NA UOVU, ILI USIWE KWA HUZUNI YANGU!”. Unaona ? Alifahamu jambo ambalo litakaloweza kuifanya ile laana iwe na nguvu juu yake ni UOVU tu!. Na ndicho alichomwomba Mungu amwepushe nacho, hivyo Mungu akahakikisha anamlinda na Uovu siku zote za maisha yake.Alijua kuwa jambo ambalo litakaloweza kumfanya awe na majuto katika maaisha yake ni OUVU, jambo ambalo litakalomfanya awe na masikitiko, masononeko, bahati mbaya, nuksi, mikosi, tabu, sio mambo aliyotamkiwa huko nyuma, sio majina ya kuzimu aliyoitwa huko nyuma, sio maneno ya laana aliyoambiwa na watu, bali ni Uovu utakaokuwa ndani yake. Na ndio maana Yabesi alijitunza sana tangu zamani, akawa na heshima kuliko ndugu zake zote, heshima inayozungumziwa hapo sio heshima ya kutii watu tu peke yake hapana, bali ni heshima iliyojumuisha vyote, alijiheshimu yeye mwenyewe kwanza kwa kila kitu katika matamshi yake, mwenendo wake, mwili wake aliutunza, na kazi yake,.Na zaidi ya yote akazidi kumwomba Mungu aendelee kumwepusha na Uovu, hivyo Mungu akamsikia na kumwepusha na hayo yote. Hata na yale mengine pia akamjalia.

Kaka/Dada, mwanzo wako inawezekana ulikuwa mbaya ulizaliwa katika vifungo vya giza pale wazazi wako walipokuweka chini ya maagano ya kiganga na kupewa majina ya mizimu, na hivyo hilo jambo limekuwa likikusumbua sana, inawezekana maisha yako ya nyuma yalikuwa ni mabaya sana, mwenendo wako ulikuwa hauvutii, hata mbele za watu wanaokuzunguka, mpaka imefikia hatua ya kupewa majina mabovu, huko mtaani unajulikana kama kibaka, au muhuni, jambazi, au Malaya fulani, au shoga, au teja.. wakati mwingine umelaaniwa na wazazi wako na unajiona wewe hufai tena, au ulipewa majina yasiofaa au ulirithishwa. Nataka nikuambie usiogope! ikiwa utaamua kuanza maisha yako upya sasa kwa Bwana, pamoja na laana hizo zote kuambata na wewe zitageuzwa na kuwa baraka, Yabesi alibebeshwa mzigo mzito kama huo lakini baada ya kuamua kuutafuta uso wa Mungu na kufanya UOVU kuwa ni adui yake aliguezwa na kuwa mtu mwingine zaidi hata ya wale waliokuwa wanajiona ni watakatifu mbele za Mungu.

Na wewe leo hii ikiwa utataka kutubu, kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako, na kuuchukulia kuwa UOVU ni kama ukoma, ni kama chanzo cha laana hizo zote ulizonazo sasa. Ukiamua kabisa kutoka moyoni kumkabidhi Bwana maisha yako leo, kuanzia sasa na kuendelea,kisha ukaenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kimaandiko ambao ni wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO, kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako kama ishara ya kusafishwa makosa yako kwa damu ya Yesu Kristo iliyomwagika pale msalabani. Basi Kuanzia huo wakati ndipo Bwana atakapokupa Roho wake mtakatifu kukusaidia kuishinda dhambi, kwa nguvu zako hautaweza, kwasababu hakuna awezaye kuishinda nguvu ya dhambi isipokuwa Roho Mtakatifu peke yake ndani ya Mtu.

Na dua yako utakayomwomba Mungu akulinde na uovu itakuwa na nguvu sana..Utashangaa unaweza kushinda kunywa pombe, unashinda kuvuta sigara na madawa ya kulevya, unashida uasherati, na ushoga, unashinda pornography, masturbation,unashinda ukahaba,wizi, unashinda usengenyaji, unaishinda hasira, chuki, wivu, majigambo n.k. Na mwisho wa siku unaitwa mbarikiwa mbele za Mungu na ufalme wa mbinguni unakuwa ni wako.Na yale mengine ya maisha yaliyosalia Bwana atakupa.

Hivyo unapoisikia sauti ya Mungu sasa kubali kuitii, na Mungu atakusaidia.

Ubarikiwe sana.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

FAIDA ZA MAOMBI

MAOMBI KWA WENYE MAMLAKA.

NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.


Rudi Nyumbani

Print this post

USHUHUDA WA RICKY:


Ushuhuda huu utakutoa sehemAu moja kiimani hadi nyingine.

Mwinjilisti mmoja wa kimarekani aAjulikanaye kama Rick Jonyer alikuwa akiomba kwa muda wa miaka 26 Mungu amnyakue mpaka mbingu ya tatu kama Bwana alivyofanya kwa mtume Paulo. Na siku moja ilipofika Mungu kusikia maombAi yake alimchukua katika maono mbinguni kama tunavyosoma katika kitabu chake alichokiandika kijulikanacho kama THE FINAL QUEST,Kilichopata umaarufu mkubwa sana  duniani kote. akieleza humo jinsi alivyoonyeshwa mambo mengi yahusuo hali za wakristo wa sasa kwa ujumla, Lakini hasa kwa wakati huu ningependa tujifunze kipengele kifupi cha maono hayo aliyoonyeshwa naamini  lipo jambo kubwa sana la kujifunza .

Rick anasema alipofika wakati wa kupitishwa na Bwana  mbele ya viti vya enzi vilivyopo mbinguni, aliona kiti kimoja kilichokuwa na utofauti kidogo, malaika wamekipamba na kukizunguka pande zote, na juu yake aliketi mfalme mkuu sana, na malaika walisimama pembeni yake wakisubiri maagizo kutoka kwake ya kufanya. Rick anasema alipokitazama kile kiti kwa ukaribu aliona sura ya mtu ambaye alishawahi kumwona mahali, ndipo alipomwomba Bwana amsogelee aongee naye naye alipofika alimwambia: naona kama  sura yako si ngeni machoni pangu, kama nilishawahi kukuona mahali ila sikumbuki ni wapi.

 Lakini yule mtu ambaye jina lake ni Angelo akamwambia ulishawahi kuniona katika maono wakati fulani zamani. Ndipo Rick haraka akajaribu kukumbuka ni wapi ndipo kumbukumbu zake zikamjua kuhusu tukio hilo akasema: siku moja alivyokuwa kijana alitoka ndani na kwenda kukaa nje ya nyuma mbali kidogo na anapoishi sehemu ya utulivu akimsubiria Bwana azungumze naye huku akiwa anasoma biblia yake, anasema maono  yalimjia saa ile ile na katika maono hayo aliona mtu mmoja mkristo mwenye bidii sana katika kumtumikia Mungu, alikuwa anashuhudia watu sehemu nyingi na kufundisha biblia mara kwa mara na kwenda kuwaombea wagonjwa kila mahali. Na muda huo huo akamwona na mtu mwingine tena aliyekuwa wa mtaani asiyekuwa na makazi ya kuishi anazurura tu huku na huko, ni mtu ambaye alikuwa hata akipita njia na kukutana na kitu chochote hata kitoto cha paka alikipiga kwa teke kitoke mbele yake.

Na ndipo Bwana akamuuliza , je kati ya hawa wawili ni yupi anayenipendeza zaidi?

Ni yule wa kwanza!: Rick akajibu kwa ujasiri wote.

Hapana! Ni wa pili. Ndipo Bwana akaanza kumweleza Rick habari zao wote wawili na maisha yao jinsi yalivyokuwa.

Yule wa kwanza alililewa katika familia nzuri, inayomjua sana Mungu na kumcha Mungu daima alililewa katika kanisa nzuri na hata alipata nafasi ya kwenda kujifunza masomo ya biblia katika vyuo. Alipewa asilimia 100 ya neema yangu lakini yeye aliweza kutumia asilimia 75 tu ya neema hiyo.

Lakini yule wa pili alizaliwa kiziwi, alikuwa ni mtu wa kunyanyapaliwa na hivyo alitelekezwa kwenye nyumba za kale sehemu za baridi mpaka siku alipokuja kukutwa na serikali ya nchi yao na kupelekwa katika vituo vya watu wasiojiweza, alihamishwa kituo kimoja hadi kingine, kutokana na kunyanyapaliwa na watu, lakini haikusaidia  mpaka alipojikuta tena yupo mitaani alipokuwepo mwanzo. Hivyo Mungu akamuhurumia na kumpa sehemu tatu za neema yake, lakini alizishinda zote aliacha kuwapiga mapaka barabarani.. 

Pindi Bwana alipokuwa akisema nami niligeuka kumtazama tena huyo mfalme mkuu jinsi alivyoketi kwenye enzi kuu namna ile, mwenye utukufu mwingi kushinda hata wa Sulemani, malaika wamemzunguka kila mahali wakisubiria maagizo kutoka kwake. Ndipo nilipomgeukia tena Bwana na kumsihi BWANA azidi kunielezea juu ya habari ya huyu mtu.

Bwana akasema Angelo alikuwa mwaminifu kwa kila neema niliyompa, Nilimwongezea sehemu nyingine tatu za neema yangu na zote akazitenda kiuaminifu. Akaacha kuiba, hata wakati alipopitia katika mazingira magumu nusu ya kufa kwa njaa lakini hakutaka kuiba mali ambayo haikuwa ya kwake kwa ajili ya kwenda kujishibisha. Alijinunulia chakula chake kwa pesa yake mwenyewe aliyoipata katika kukusanya makopo barabarani  aliyoyauza. Na mara chache  akipata kazi za kusafisha uani katika majimba ya watu.

Angelo alikuwa ni kiziwi lakini alijifunza kusoma. Hivyo nilimpelekea nakala za vipeperushi cha Injili. Na Alipovisoma  Roho wangu alimfungua macho yake na ndipo akayakabidhi maisha  yake kwangu. Nikamwongozea tena sehemu ya neema yangu, na zote hizo alizitumia kuaminifu. Alitamani sana kushuhudia habari zangu kwa watu wengine lakini hakuweza kuongea, lakini japo kuwa alikuwa katika hali ile hakutana habari zangu zisiwafikie wengine.  Alianza kutumia zaidi ya nusu ya alichokipata kusambaza kipeperushi vya injili mabarabarani.

Ndipo nikamuuliza Bwana, Ni watu wangapi aliowavuta kwako?, ni wazi itakuwa maelfu ya watu, mpaka ifikie hatua ya kuketi katika viti vya wafalme ni lazima atakuwa amewavuta wengi.

Lakini Bwana akamwambia: Alifanikiwa kumvuta mtu mmoja tu kwangu. Nilifanya hivyo Ili kumtia moyo alimvuta mlevi mmoja aliyekuwa anakaribia kufa barabarani. Na hiyo ilimtia moyo sana kiasi cha kumfanya aweze kuendelea kukaa  miaka mingi zaidi barabarani kujaribu kumvuta mtu mwingine kwangu. Lakini mbingu nzima ilikuwa inamfurahia kutaka aje huku juu, nami pia nilitamani aje apokee ujira wake. Huyo ni Angelo.

Lakini ni kitu gani kilimfanya Angelo aweze kuwa mfalme hapa? Niliuliza.

Alikuwa mwaminifu kwa vyote alivyopewa aliyashinda yote mpaka alipokuwa kama mimi, yaani KUFA KWA AJILI YA IMANI.

Lakini je! yeye naye alishindaje shindaje, na alikufaje kufaje kwa ajili ya Imani? Niliuliza tena.

Aliushinda ulimwengu kwa UPENDO wangu. Wachache sana wanaweza kushinda wakiwa na vichache. Watu wangu wengi wanaishi katika mazingira mazuri zaidi hata ya wafalme walioishi karne moja iliyopita lakini bado hawana shukrani kwa hayo.Lakini Angelo yeye hakuwa hivyo, yeye aliweza hata kushukuru kwa boksi aliloliokota barabarani na kuligeuza hilo kuwa hata sehemu yake ya kufanyia ibada. Alianza kupenda kila kitu alichokiona na kila mtu,aliweza kupenda hata tunda la tofaa zaidi hata ya watu wanavyoweza kufurahia sherehe kubwa wazifanyapo. Alikuwa mwaminifu kwa kila nilichompa japokuwa nilichompa hakikuwa kikubwa kulinganisha na wengine lakini yeye alikuwa mwaminifu katika hivyo.

Nilikuonyesha maono juu yake wakati ule, kwasababu ulishampita mara nyingi barabarani.

Ndipo nilipotaka kufahamu nilifanya nini nilipomuona.

Bwana akasema ulimnyooshea  kidole chako na kumwambia rafiki yako, kuwa watu kama hao wanaosimama kwenye vituo vya mabasi ni watu waliotumwa na shetani kuuvuruga ukristo, watu waliopoteza mweleko wa imani.

Niliposikia hivyo nilijisikia mnyonge na mwenye aibu nyingi, ndipo nikamwomba Bwana anisamehe akasema umeshasamehewa.

Bwana akaendelea kusema, alikuwa na mengi ya kuwapa watu wangu lakini hawakupenda kumsogelea. Alikuwa mwaminifu kwa alichokipata  alinunua biblia yake, na baadhi ya vitabu kusoma lakini alipojaribu kwenda katika makanisa hakuna mtu aliyempokea. Kama wangempokea basi wangekuwa wamenipokea mimi. 

Ndipo nilipozidi kutaka kufahamu Angelo alikufaje kufaje?

Bwana akasema: Aliganda katika baridi kujaribu kumwokoa mlevi mmoja barabarani.

Ndipo nipomuliza Bwana najua anastahili kuwepo hapa lakini je! si ni wale watu wanaokufa kwa ajili ya injili yako ndio wanaohesabika kuwa ni mashahidi wako waaminifu. Inakuwaje kwa huyu?

Angelo alikuwa anakufa kwa ajili yangu kila siku, aliweza kuwa tayari kuutoa uhai wake kwa ajili ya mtu mwenye uhitaji. Kama Mtume Paulo alivyosema, hata nikiutoa mwili wangu wote uungue na moto kama sina upendo mimi si kitu, lakini kama utautao uhai wako katika upendo hiyo inahesabika sana mbele za Mungu. Angelo alikuwa anakufa kila siku kwasababu alikuwa haishi kwa ajili yake, bali kwa ajili ya wengine. Japokuwa alikuwa anajiona mwenyewe kuwa ni mdogo katikati ya watakatifu lakini kiuhalisia alikuwa ni mkubwa sana. Wale watu wanaojiona kuwa ni wakubwa na kusifiwa na watu wengi wao wanaishia kuwa wadogo huku.

Mwisho wa nukuu.

*******

Ndugu watu wengi wanadhani ili ukubaliwe na Mungu na kupata nafasi ya kumkaribia ni mpaka ufanane na mwinjilisti fulani au nabii fulani, au mwalimu fulani. Lakini hawajui kuwa kila mtu kapewa kipimo chake cha imani. Na kule kinachohesabika ni je umekutumiaje hicho ulichopewa?. Mwanafunzi mmoja anaweza kupewa maswali 10 na kati ya hayo akapata 9 na kukosa 1..Wakati huo huo mwanafunzi mwingine anaweza kupewa maswali 100, akapata 60 na kukosa 40, kwa namna ya kawaida unaweza kusema yule wa maswali 100 ndiye aliyefaulu zaidi ya mwingine, lakini tukirudi kwenye asilimia utagundua kuwa yule aliyepewa maswali 10, ndiye aliyefaulu zaidi ya mwenzake, amefaulu kwa asilimia 90%..Ukilinganisha na yule wa maswali 100 yeye kafaulu kwa asilimia 60%. Ambayo ni ndogo.

Kama aliweza kuwa mwaminifu katika maswali 10 basi atakuwa mwaminifu katika maswali 100, ndivyo ilivyo na kwetu sisi, kila mmoja kapimiwa kipimo chake. Swali je! kipimo chako unakitumiaje?. Umehubiriwa injili mara ngapi ugeuke lakini hutaki?, umehudhuria ibada ngapi lakini bado unaipuuzia neema. Umesikia shuhuda ngapi ubadilike lakini bado upo vile vile,? Unaona ni shida kutenda kazi unachofundishwa kila siku. Siku ile utakuwa wapi?, utawezaje kusimama na yule kipofu aliyekule vijijini yeye aliposikia tu Neno hata bila kuona akaamini na kubatizwa. Lakini wewe unajiona kwasasa hivyo vitu havina umuhimu, Bwana atakapotoa thawabu kwa wale waliomtii utakuwa wapi?. Yeye mwenyewe alisema maneno haya.

Luka 16:10 “Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.”

Nakutia moyo wewe uliyechukua uamuzi wa kumfuata Bwana katika hali zote, kwa moyo wako wote. Wakati wa faraja utakuja na Bwana atakulipa kulingana na uaminifu wako.

Mungu akubariki sana. Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

JINSI YA KUITUMIA VYEMA NEEMA YA MUNGU ILIYO JUU YANGU.

DALILI ZIPI ZITAMTAMBULISHA MTU KUWA AMEFANYIKA KIUMBE KIPYA?

BWANA YESU ALIMAANISHA NINI PALE ALIPOSEMA “MKONO WAKO UKIKUKOSESHA UKATE?


Rudi Nyumbani

Print this post

MTAIFAHAMU KWELI NAYO HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU.


Mtu anayevamiwa na nguvu za giza, kama hajaamua yeye mwenyewe kutaka kuwa huru na hizo roho, hata aombeweje hawezi kuwa huru na hizo roho, hakuna nguvu yoyote iliyokubwa ndani ya mwanadamu kama nguvu ya maamuzi, Hata Roho Mtakatifu mwenyewe hawezi kuyateka maamuzi ya mtu, ingawa anao huo uwezo, lakini hafanyi hivyo…si zaidi shetani? Mwanadamu akiamua kujifunga kwa maamuzi yake, amejifunga, hakuna sala yoyote wala dua yoyote, itakayoweza kumtoa kwa nguvu katika kile alichokiamua. Kwahiyo mtu yoyote ambaye hataki kumpokea Kristo, anakuwa chini ya nguvu za giza kwa maamuzi yake mwenyewe na hivyo hakuna chochote kitakachoweza kuyashinda maamuzi yake.

Sasa Bwana Mungu anachokifanya kwa Yule mtu asiyemwamini ni kumletea nguvu ya ushawishi, itakayomfanya abadilishe maamuzi yake na kumgeukia yeye, lakini sio kumletea nguvu ya kumpindua kwa nguvu kwa kile anachokiamini. Ndio hapo atamletea wahubiri, atazungumza naye moyoni kwa sauti ya faraja na matumaini n.k.Na Yule mtu akishashawishika vya kutosha kumwamini na kumgeukia Mungu, ndipo Roho ya Mungu inaingia ndani yake na kumgeuza kuwa mtu mwingine..Lakini kama Yule mtu hataki ataendelea kubaki vilevile..roho ya shetani iliyo ndani yake itaendelea kuwa na nguvu..Na haiwezi kutolewa kwa kuombewa wala kuwekewa mikono.

Kama maandiko yanavyosema “tena mtaifahamu kweli, NAYO HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU Yohana 8.32”.

Na biblia inatafsiri nini maana ya kweli katika kitabu cha

Yohana 17: 14 

“14 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyowa ulimwengu.

15 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.

16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

17 Uwatakase kwa ile kweli; NENO LAKO NDIYO KWELI”

Kwahiyo tunaona NENO LA MUNGU ndiyo kweli, ikiwa na maana kuwa kwa kupitia Neno la Mungu mtu ndipo anaweza kuwekwa huru, kwa kupitia Neno la Mungu mtu ndio anaweza kufunguliwa na vifungo vya dhambi na shida na mauti, na sio kupitia kumwombea mtu ndio mtu aweze kufunguliwa na kuwekwa huru.

Ndio maana Bwana Yesu alikuja duniani, na Injili ya kumweka mtu huru, alisema “Tubuni kwa maana ufalme wa Mungu umekaribia”, alisema “aniaminiye mimi anao uzima wa milele na nitamfufua siku za mwisho”…alisema “wapendeni adui zetu, waombeeni wale wanaowaudhi,”..alisema “tusamehe wale waliotukosea ili na Baba yetu wa mbinguni atusamehe sisi makosa yetu”. Hayo ndiyo maneno ya kutuweka sisi huru.

Hebu fikiri leo hii mtu kamkosea Mungu labda kaua, au kaiba, au kafanya mabaya mengi,na anakwenda kuomba au kuombewa kanisani kwamba Mungu amsamehe makosa yake, na kupewa matumaini kwamba dhambi zake zimeondolewa na huku analo kundi la watu wengi kichwani mwake ambao hajawasamehe ambao walimwibia naye pia au walimwulia ndugu yake au walimfanyia ubaya fulani? Je! Huyo mtu kasamehewa dhambi zake kweli?, huyo mtu ni kweli kawekwa huru?… Ni wazi kuwa huyo mtu bado kafungwa na yupo chini ya laana na ghadhabu ya Mungu, kwasababu Neno linasema “Msipowasamehe watu makosa yao na Baba yetu wa mbinguni hatatusamehe sisi makosa yetu”..Kwahiyo hakuna maombi yoyote yanayoweza kumfanya huyo mtu asamehewe makosa yake na Mungu, hata afunge miezi na miaka, hata aombewe na kasisi mkuu wa dunia. Hakuna dawa ya makosa yake…Dawa ni moja tu! Kulifahamu NENO LA MUNGU, ambalo ndilo kweli ya Mungu itakayomweka huru…na neno hilo linasema “samehe kwanza watu waliokukosea ndipo na Bwana atakapokusamehe makosa yako”..Hilo Neno ndilo litakalomweka Huru mbali na dhambi, hakuna njia ya mkato au mbadala.                     (MTAIFAHAMU KWELI NAYO HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU).

Hiyo ndiyo sababu Bwana alipopaa duniani aliturithisha NENO LAKE(Biblia Takatifu) badala ya sura yake, sura yake haikuwa na umuhimu sana kwetu kuliko maneno yake. Hakuturithisha  mali, wala chochote kile bali aliturithisha Neno lake, kwasababu kwa kupitia hilo ndio litakalotuweka huru.

Kwahiyo kaka/Dada unayesoma ujumbe huu, tafuta sana kuisoma Biblia, kwa nia ya kujifunza…usipendelee sana kusubiria kufundishwa kanisani au kwenye mikutano, soma mwenyewe biblia, sura baada ya sura, habari baada ya habari na Roho Mtakatifu atakusaidia na kukuongozakatika kweli yote, kwasababu hiyo ndiyo kazi yake…Huko ndiko utakapofunguliwa vifungo vya giza na kuwekwa huru siku baada ya siku. Roho Mtakatifu sio kwa baadhi ya watu tu! Hapana biblia inasema ni kwa watu wote waliomjia yeye…

“Matendo 2:38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”.

Vinginevyo usipoijua Biblia, utapelekwa na kila aina ya upepo, utakuwa na hofu na mashaka, utatanga tanga huku na kule, leo utaambiwa usile chakula hichi ni cha wachawi, kesho utaambiwa kata mti Fulani nyumbani kwako ni wa kichawi, baadaye utaambiwa kuota unasoma, upo darasani basi nyota yako imechukuliwa ipo sehemu fulani, baada ya siku chache tena utaambiwa jina lako liko kwa wachawi, kesho kutwa utaingizwa kwenye maombi ya kutengeneza nyota, na kusambaratisha maadui zako,.utafundishwa kila aina ya elimu, na nyingi ya hizo ni elimu za kuzimu, ambazo biblia inaziita MAFUNDISHO YA MASHETANI!! Ambayo dhumuni kubwa ya mafundisho hayo ni kuwatia watu hofu, na kuwatoa katika mstari wa kujifunza Neno la Mungu na kuanza kujifunza elimu za ufalme wa giza (Ni agenda kamili kutoka kuzimu). Ili watu wakimbilie kuombewa na WASILIJUE NENO LA MUNGU, ambalo ndilo hilo tumeambiwa LITATUWEKA HURU!.

Kwahiyo ndugu, jifunze Biblia kwa bidii zote,tenga kila siku muda wa kusoma maandiko mwenyewe, usisubiri mtu akutolee kipengele Fulani cha maandiko na kukutafsiria na kukutengenezea somo, asipokuwa na mrejeo mwingine wa habari inayofanana na huo mstari.

Epuka sana injili za Mafanikio, unachukuliwa mstari mmoja unatengenezewa somo refu, kusapoti kupata mali/ utajiri, kila mstari unaofundishwa ni kurejeshwa wewe  kwenye mali, na kesho tena utahubiriwa mali, na kesho kutwa tena hivyo hivyo, (zichunguze hizo roho), utakuta zinagusia kidogo sana, au hazigusii kabisa habari za Msalaba,toba,wala utakatifu ambao Biblia imesema hakuna mtu atayemwona Mungu asipokuwa nao (Waebrania 12:14).

Injili ambazo zinakuambia utapokea utajiri/mali ndani ya muda mfupi..Hizo ni injili za Yule Mjaribu; LUSIFA za kumfanya umsujudie yeye. Ambaye alimjaribu Bwana kwa kumwonyesha Milki zote za dunia ndani ya DAKIKA MOJA, na kumwambia Ageuze Jiwe liwe Mkate ndani ya dakika moja. Na kumtumainisha kwamba akijitupa chini ya mnara malaika watatumwa waje kumwokoa, Na shetani anatumia maandiko kuwaonyesha watu milki za dunia ndani ya dakika moja, anatumia maandiko kuwaambia watu wanaweza kugeuza sadaka zao kuwa utajiri dakika hiyohiyo, huku wanapandikiziwa chuki dhidi ya ndugu zao, na kufundishwa kila mtu ni adui yao.

Kama ulishawahi kuingia huko, jiokoe nafsi yako ndugu toka haraka sana, hebu jiulize ni lini kati ya hizo siku ulizoingizwa kwenye hizo injili za mafanikio, baada ya kutoka na kurudi nyumbani ULISIKIA HAMU YA KWENDA KUJITAKASA ZAIDI MBELE ZA MUNGU NA HAMU YA KWENDA KUSOMA NENO?? Kama ulishawahi kusikia hiyo hamu basi baki hapo, maana Mungu yupo, lakini kama hujawahi kusikia hiyo hamu ya kujisogeza zaidi mbele za Mungu badala yake unasikia hamu ya kwenda kumkomoa adui yake, na kutaka ajionee unavyobarikiwa…Hilo ni jaribu ndugu!! Ondoka kabisa! Jiokoe nafsi yako na wala usigeuke nyuma!!. Bwana alizikataa zile mali shetani alizokuwa anataka kumpa ndani ya dakika moja, kwasababu aliona utajiri usioelezeka unaokuja huko mbele.. Na biblia inasema katika Mithali 13: 11 “ Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa”

Bwana akujalie kuyaona hayo mtu wa Mungu, Kama hujampa Bwana Yesu Maisha yako, huu ndio wakati wa kufanya hivyo kwasababu huijui kesho, mgeukie leo, utubu dhambi zako zote kwasababu yeye ni mwaminifu atakusamehe sawasawa na Neno lake, na pia Hakikisha utakwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kulingana na Matendo 2:38 ili upate ondoleo la dhambi zako, na Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi na kukutia katika kweli yote ya Biblia.

(MTAIFAHAMU KWELI NAYO HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU).

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

MANABII WALISEMA “NENO LA MUNGU LIKANIJIA” ..MAANA YA HILI NENO NI NINI?

TABIA YA KIPEKEE USIYOIJUA KUHUSU NENO LA MUNGU.

NENO LA MUNGU KATIKA UTIMILIFU WOTE.

JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?


Rudi Nyumbani

Print this post

KARAMU YA MWANA-KONDOO.

Sherehe za siku hizi zinatupa picha kamili jinsi mambo yatakavyokuja kuwa huko mbeleni baada ya unyakuo kupita. Kama tunavyofahamu leo hii hakuna sherehe yoyote ya arusi utakayokwenda bila mwaliko wowote, vinginevyo ukijaribu kufanya hivyo utajikuta utaishia getini, kadhalika mwaliko peke yake hautoshi ni lazima uambatanishwe na mchango wa kiasi fulani cha fedha vinginevyo hata kama utakuwa na vigezo vyote vya kuingia harusini bado utazuiliwa tu kuingia..

Ukiwa ni msomaji wa biblia utajua kuwa ipo karamu ambayo imekwisha andaliwa huko mbinguni, hii ni karamu iliyo KUU na ya kipekee kuliko zote, iliyoandaliwa na Mungu mwenyewe kwa ajili ya Kristo na bibi-arusi wake (yaani Kanisa). Kama tunavyofahamu utaratibu wa harusi, sharti ndoa ifungishwe kwanza ndipo sherehe ifuate, vivyo hivyo katika utaratibu wa kimbinguni, ni sharti Kristo afunge ndoa kwanza na bibi-arusi wake, ndipo karamu ifuate baadaye. Na ndoa hiyo haifungiwi mahali pengine zaidi ya hapa hapa duniani. Hii inatokea pale mtu mwenyewe binafsi anapochukua uamuzi wa kumfuata Kristo, kwa kuacha maisha yake maovu ya dhambi, na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake, hapo ndipo anakuwa amekidhi vigezo vya kuwa mwalikwa wa karamu ile ya mwanakondoo ambayo itakuja kufanyika baadaye kidogo.

Ndugu, kosa kila kitu, kosa mali, kosa mtoto, kosa uzuri, kosa hata marafiki,potoza hata chochote unachokiona kina thamani, lakini usifikirie hata siku moja kuikosa karamu hiyo, kwasababu mahali popote biblia inapoizunguzia karamu hii inatumia neno HERI..Biblia haina maneno ya kujitosheleza kuelezea maana ya hili Neno heri, yaani tunawezeka kusema, amebahatika sana, au amebarikiwa sana, amependwa bure, yeye atakayepata neema ya kualikwa kwenye karamu hiyo, kwasababu wengi wanaojulikana kama wakristo wataikosa.

Ufunuo 19:6 “Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki.

7 Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni MATENDO YA HAKI YA WATAKATIFU.

9 Naye akaniambia, Andika, HERI WALIOALIKWA KARAMU YA ARUSI YA MWANA-KONDOO. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.”

Unaona hapo? Maandiko yanamalizia na kusema “Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu”, ikiwa na maana kuwa hiyo Karamu ni lazima ije tu kwa wakati uliouamuru Mungu, na tunajua Mungu hasemi uongo. Na wana heri nyingi wale wote watakapata neema ya kualikwa humo.

Tunajua hakuna mtu yeyote asiyefurahia sherehe, au mwaliko wowote wa karamu, hiyo ni asili ambayo Mungu kamuumbia kila mwanadamu kupenda kufurahia mambo mema, lakini aliiweka hiyo kiu kwa makusudi kabisa kwa ajili ya Karamu yake mwenyewe ambayo amewaandalia watoto wake wote. Ili kusudi kwamba watu watazamapo hizi sherehe za duniani wajue kuwa ipo sherehe iliyo kuu ambayo mambo yake biblia inasema jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia inayokuja huko mbeleni, Hivyo mtu aifiripo hayo ni wajibu wake, kujitia moyo kwa kufanya juu chini kuhakikisha na yeye ni mmojawapo wa watakakuwemo kwenye karamu hiyo ambayo itafanyika mbinguni.

Lakini kama tunavyojua bibi-arusi yeyote ni lazima awe na vazi la harusi gauni jeupe zuri safi,refu, hawezi kuvaa kanga na kusema anakwenda kuolewa na ndivyo ilivyo kwa Kristo Yesu, yeyote yule atakayestahili kuwa bibi-arusi wake ni lazima awe na Vazi la harusi jeupe ling’aralo na biblia inasema vazi hilo linawakilisha MATENDO YA HAKI YA WATAKATIFU.

(Ufunuo 19: 7 “Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

8 Naye amepewa kuvikwa KITANI nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo NI MATENDO YA HAKI YA WATAKATIFU”.

Kama vile tunavyoona sasahivi mtu hawezi kupewa kadi ya mwaliko kama hajachangia chochote, vivyo hivyo kusema umeokolewa tu halafu matendo yako hayaakisi wokovu wowote, hauna mchango wowote kwenye wokovu wako, huishi kama mtu anayemngojea Bwana wake aende naye harusini, anasa, ulevi, pornography, matusi, chuki, usengenyaji, uasherati n.k..Basi fahamu kuwa siku ile itakapofika utabaki hapa hapa duniani, hautakwenda na Bwana.

Unyakuo ukishapita, mfano ikiwa ni leo, watakaokwenda kwenye hiyo karamu ambayo itakuwa ni wale biblia inayowaita wanawali werevu tu (Mathayo 25), watajikuta mbinguni, ni karamu ya miaka 7 mbinguni kabla ya kurudi tena kuja kutawala na Kristo kwa muda wa miaka 1000. Mtu asikudanganye kukwambia hiyo itakuwa ni kwa kila mtu, hapana, bali ni kwa wale Kristo aliofunga nao ndoa, wakiwa hapa hapa duniani, na waliokidhi vigezo vyote vya kuhudhuria karamu hiyo yaani wakristo watakatifu, wengine wote waliosalia pamoja na wale wakristo vuguvugu watabaki hapa duniani kwa ajili ya ile dhiki ya mpinga-kristo.

Hata vitu vya asili vinatufundisha, tukiutazama mwezi katika biblia unawakilisha kanisa la Kristo, na ile nyota ya Asubuhi inamwakilisha Yesu. Lakini unaweza ukajiuliza ni kwanini mwezi unabadilika badilika sio kama jua au nyota. Leo utauona upo kama duara, kesho kama mundu, kesho kutwa kama tufe, leo unaonekana nusu kesho robo n.k..Hii inamaanisha kuwa kanisa la Kristo, japo ni kamilifu lakini bado sio wote kwenye kanisa walio wakamilifu. Na kama ukitazama wale wanaotumia Mwezi na nyota kama nembo za taifa lao, wengine wanazitumia kama nembo za dini zao,utaona hawauchori mwezi wote, na nyota pembeni yake. Bali wanachukua kile kipande kidogo sana cha mwezi kama ukucha na kukiweka na ile nyota ya asubuhi.

Hawajui kuwa lile linamfunua Kristo na bibi-arusi wake, kwamba Kristo akija hatalinyakua kanisa zima, hapana bali ni bibi-arusi waliosafi wasio na mawaa katika ya kanisa lote. (Soma mfano wa wanawali werevu na wapumbavu utaliona hilo. Mathayo 25).

Na ndio maana upo umuhimu wa kutengeneza mambo yako sawa sasa kabla siku hizo hazijafika, Bwana anamwalika mtu yeyote aliye tayari, lakini habari mbaya ni kwamba wale wanaoalikwa kwa kuhubiriwa injili kila siku ndio wanaokuwa wakwanza kukawia na kutoa udhuru. Embu soma kisa hiki.

Luka 14: 15 “Basi aliposikia hayo mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye alimwambia, HERI YULE ATAKAYEKULA MKATE KATIKA UFALME WA MUNGU.

16 Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi,

17 akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.

18 Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe.

19 Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe.

20 Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.

21 Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete.

22 Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi.

23 Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa.

24 Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu”.

Unaona hapo ndugu? Kristo anapokuita leo uokoke ni kwasababu anakuwazia mawazo ya amani ili kukupa wewe tumaini katika siku zako za mwisho (Yeremia 29:11). Utajisikiaje leo hii unyakuo usikie umepita huku ukijua wenzio tayari wakati huu wameshabadilishwa miili na kupewa mingine ya utukufu, wakati kama huu wenzako wanauona uzuri wa Kristo aliokwenda kuwaandalia kwa miaka 2000, wanamwona uso kwa uso,wanapata furaha isiyoelezeka wewe upo huku chini unasubiria kukutana na dhiki ya mpinga-kristo isitoshe, ziwa la moto linakusubiria. Utajisikiaje?. Ni kilio cha kusaga meno, ni uchungu uliochanganyikana.

Piga hesabu ikiwa unapenda maisha utaona kuwa ni heri leo utubu uwe mmoja wa bibi-arusi waliotiwa muhuri na Mungu kwa Roho wake. Lakini kama dunia imekuahidia furaha kubwa zaidi ya hiyo basi uamuzi ni wako. Lakini jua kuwa hizi ni siku za mwisho na hatuna garantii ya kizazi kingine mbele yetu. Hili ni kanisa la mwisho linaloitwa Laodikia, na Mjumbe wake ameshapita, ufunuo 3:21 Pia fahamu kuwa wapo wateule wa Mungu duniani (bibi-arusi) usiku na mchana wanamlilia Bwana aje.

Ufunuo 22.17 “Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”.

Bwana akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

NDOA NA HARUSI TAKATIFU.

UMEPATA UHAKIKA WA KUTOKUINGIA HUKUMUNI KATIKA SIKU ILE?

UTAWALA WA MIAKA 1000.


Rudi Nyumbani:

Print this post

KAENI NDANI YANGU NAMI NDANI YENU.

Shalom mwana wa Mungu, karibu tujifunze Neno la Mungu, ambapo leo tutajifunza kwa ufupi juu ya somo lenye kichwa kinachosema “KAENI NDANI YANGU NAMI NDANI YENU”..Maneno hayo aliyazungumza Bwana Yesu, alipokuwa anazungumza na Wayahudi wakati Fulani kabla ya kusulibiwa kwake, Aliwaambia

Yohana 6: 53 “Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.

54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.

56 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu YANGU HUKAA NDANI YANGU, NAMI HUKAA NDANI YAKE”.

Sehemu nyingine pia alisema.. Yohana 15:4 “ KAENI NDANI YANGU, NAMI NDANI YENU. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu”

Sentensi hiyo ni ngumu kidogo kuilewa, lakini hebu tutafakari mfano huu tunaweza tukauelewa zaidi..

Mfano mtu achukue ndoo na aijaze maji hadi juu na kisha achukue glasi aiweke ndani ya ile ndoo, unadhani kitu gani kitatokea hapo?..Ni wazi kuwa ile glasi itajaa maji ikiwa ndani ya ile ndoo…hivyo kwa ufupi tunaweza kufupisha na kusema.. “glasi ipo ndani ya maji na maji yapo ndani ya glasi” Ili kuifikia glasi lazima uyakute maji, na ndani ya glasi pia kuna maji.

Na kwa Mungu ndio hivyo hivyo, “aliposema kaeni ndani yangu nami ndani yenu” alimaanisha kuwa Munguatakuwa nje yetu, kutuzunguka pande zote na pia atakuwa ndani yetu kutulinda na kutuhudumia. Kwahiyo hakuna mashambulizi yoyote yanaweza kutokea nje ya miili wala hakuna mashambulizi yoyote yanayoweza kutokea ndani ya roho. Kwa mtu aliyejiunganisha na Mungu kwa namna hiyo, Kitakachokuwa kinaendelea nje ndicho kitakachokuwa kinaendelea ndani. Hakuna tofauti.

Hakuna kiumbe chochote kilichopo kinachoweza kutoa huduma kama hiyo, hakuna! Kiumbe chochote hata shetani kinachoweza kukupa uhakika wa mwilini na rohoni,..shetani atakupa furaha ya utajiri lakini hatakupa furaha ya rohoni, atakupa utajiri wa nje lakini hatakupa utajiri wa ndani. Mwanadamu atakupa tumaini la ulinzi wa nje lakini hatakupa tumaini la ulinzi wa roho yako, mali zitakupa ulinzi wa nje, lakini hazijuli lolote kuhusu roho yako, ikiwa kuna wachawi au majeshi ya mapepo yanakuvamia mali haziingilii kati.

Daktrari atakutibu mwili lakini hataweza kutibu roho iliyovunjika na kukata tamaa, atatibu majeraha ya nje lakini hatatibu majeraha ya ndani, watatibu mifupa iliyopondeka lakini hawataweza kutibu moyo uliopondeka. Wanadamu watakuondolea hofu ya nje kwa muda, lakini hawatakuondolea hofu ya kifo na magonjwa. Wanadamu watakata kiu na njaa ya miili yetu, lakini hawatakata njaa au kiu ya kutaka kuishi milele.

Yupo mmoja tu! Ambaye ni mtaalamu wa mambo yote ya rohoni..aliyetiwa mafuta na Mungu mwenyewe ambaye anaweza kushughulika na mambo ya rohoni yaliyokosewa ufumbuzi, ambaye anaweza kutegua vitendawili vigumu vya moyo, ambaye anaingia ndani ya mtu, na kumtengeneza na kutatua matatizo yake yote yaliyomo ndani yake, anapenya hata kutenganisha nafsi na roho, na mafuta yaliyoko ndani yake, ni mwepesi wa kutambua fikra za mtu na matamanio ya mtu hata kabla mtu huyo hajayawaza.. Yeye mwenyewe anasema maneno haya..

Isaya 61: 1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.

2 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;

3 kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe”

Huyo ni YESU KRISTO PEKE YAKE na wala hakuna mwingine. Asifiwi kwa ushabiki wa kidini kama inavyofanyika na wengi leo lakini hiyo ndio sifa yake, sio tu Mungu kamuhakiki hata wanadamu sisi wenyewe tumemwakiki na kujua kweli hakuna mwingine kama yeye,na hakuna jambo lolote linalomshinda ndivyo alivyo. 

Dada/Kaka unayesoma ujumbe huu, habari za Yesu Kristo hazitaachwa kutangazwa popote pale, Roho Mtakatifu anatenda kazi kila siku na kila mahali, kama hutasikia hapa utasikia pale habari za Yesu Kristo,

Kwa faida yako na yangu alijitoa kwa ajili yetu, ili sisi tupate msamaha wa dhambi na tupate mema yote ya nchi, hivyo anakuita leo kwa mara nyingine.Una masononeko, suluhisho sio daktari wala sio mimi, una uchungu, una dhambi, una hofu, una shida, una huzuni,una mashaka, umekata tamaa ya kuishi, unahofu ya kukataliwa, Nataka nikuambie Wanadamu wala shetani bado hatujaifikia hiyo sayansi yakutibu hayo mambo magumu ya rohoni, hakuna daktari wala mganga awezaye kutibu hayo mambo na hivyo hata ukienda kwao hawatakusaidia..

Dawa ya hayo mambo Ni YESU KRISTO KUINGIA NDANI YAKO..Basiiii!!!! Huyo ndiye atakayeondoa shida ulizonazo, huzuni, hofu, mashaka, mateso na mambo mengine yote. Mimi nilikuwa na mashaka mengi, mpaka ikafikia wakati nikajua kuwa nini dhambi ya kutokuwamehewa, na hivyo sifai tena.Lakini Kristo aliniponya na ndio maana leo hii nakuandikia ujumbe huu Ni Yesu peke yake ndiye atakayeikata kiu yako.

Unasubiri nini usimpe leo Kristo maisha yako?…anabisha mlangoni leo, mlangoni mwa moyo wako,.Unachopaswa kufanya ni kumfungulia aingie akugange moyo, na yeye akiingia ndani yako haishii kukaa ndani yako anakuzingira pia nje yake..kama glasi iliyoko ndani ya ndoo ya maji.

Ukiwa unatamani kufanya hivyo, hapo hapo ulipo yupo, anza kutafakari maisha yako ya nyuma..maisha uliyoyapitia, dhambi ulizozifanya, shida ulizozipitia, magonjwa, huzuni uliyonayo, hofu uliyonayo, mashaka uliyonayo, na kila kitu ambacho huwezi hata kumweleza mtu. Nyenyekea chini yake na mwelezee, na mwambie akusamehe na kukusafisha, mwambie akutue mizigo ya dhambi na yeye ni mwaminifu atakusaidia.

Hauhitaji kwenda kwa mchungaji, au kwa mtumishi hapo hapo ulipo anakusikia atakusamehe. Na baada ya kufanya hivyo fanya hima ukabatizwe..hayo ni maagizo aliyoyatoa Bwana Yesu kwa ajili ya ondoleo la dhambi, kama tu daktari anapokupa maagizo ya kuweka dawa kwenye maji na kuyaogea ili ugonjwa wako wa ngozi uondoke wote, huwezi kwenda kuweka kwenye glasi na kujipaka, utakuwa umevunja masharti na pengine ugonjwa wako unaweza usipone ..na Yesu alitupa maagizo ya kuondolewa dhambi ambao ndio ugonjwa wa pekee wa roho zetu, na hayo maagizo ni kwenda kubatizwa katika maji mengi kwa jina la Yesu Kristo, ili dhambi zetu ziondolewe kulingana na (matendo 2:38). Na kisha baada ya hapo Bwana atafanya yaliyosalia, atahakikisha anakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi, na kukutia katika kuielewa kweli yote ya maandiko..

Hapo utakuwa umezaliwa mara ya pili, na kuingizwa katika ukuhani wa kifalme, watu wa milki ya Mungu, uzao mteule utakaourithi uzima wa Milele, Na Kristo atakuwa yupo ndani yako na nawewe utakuwa ndani yake, na hivyo lolote utakaloomba utapewa kwasababu wewe tayari ni mmoja wa familia halali ya Mungu, unayejulikana Mbinguni. Atakufariji kwa faraja zote alizokuahidia kwenye Neno lake. Kama Bwan Yesu alivyosema katika.

Yohana 15.7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.

8 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu”

Yohana 14:20 “Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu”.

Bwana akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.

MJUE SANA YESU KRISTO.

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!


Rudi Nyumbani

Print this post