Title July 2023

Nini maana ya Mithali 5:15-18 anaposema Unywe maji ya birika lako mwenyewe?

Mithali 5:15 “Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako.  16 Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu?  17 Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe.  18 Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako”


JIBU: Mstari huu unawalenga wanandoa, na unafananisha tendo la ndoa kama kisima ambacho kila mwanandoa amekichimba kunywea maji yake hapo ili kukata kiu ile ya mwili. Na kwamba mtu anapoingia katika hali hii, hawezi kunywa maji ya visima vingine na mwingine hawezi kuja kunywa maji ya kisima chake. Kwani vimeundwa mahususi kwa wale tu waliovichimba yaani wanandoa, mwingine yoyote atakayeshiriki ni mauti.

Jambo ambalo ni kweli, madhara ni mengi ambayo mtu anayapata anapotoka nje ya ndoa yake na kukutana na watu wengine kuzini nao, migogoro mingi ya kindoa inayozuka hata kupelekea kuvunjika kwa ndoa zao, wengine hata kuuana ni kwasababu ya tabia hii ya kuingilia ndoa za watu au kutoka nje ya ndoa. Magonjwa yasiyositibika kama ukimwi huingia kwa namna hii.

Na zaidi ya yote mtu afanyaye mambo kama haya ni anakwenda kinyume na agizo la Mungu ambalo litampelekea kuhukumiwa na kutupwa katika ziwa la moto atakapokufa; Maandiko yanasema.

Waebrania 13:4  “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu”.  

Kaa mbali na uzinzi, chimba kisima chako mwenyewe, (Oa au Olewa na mke au mume mmoja). Utulie hapo, epuka tamaa. Siku hizi ni za mwisho Yesu anakaribia kurudi,  mlango ni mwembamba unaoelekea uzimani  imekuwa kawaida, kwa mtu kuwa na wake kando, wakidhani kuwa ndio wamekamilika, hawajui kuwa ibilisi ameshawanasa, ulinzi wa Mungu umeshaondoka ndani yao, wapo hatarini kufa, kuzimu ikiwangojea, Je! Umejiandaaje na jambo hilo?  Ikiwa upo tayari kutubu leo dhambi zako na kuachana na hizo tabia za ibilisi, ili Yesu akusaidie kushinda dhambi basi uamuzi huo ni wa busara, waweza kufungua hapa kwa mwongozo huo wa kuokoka >>>>    KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MAFUNDISHO YA NDOA.

BIRIKA LA SILOAMU.

Birika ni nini?, na yale Matao matano katika birika la Bethzatha ni nini?.

Kisima cha joka na lango la jaa ni nini?(Nehemia 2:13)

Biblia inamaana gani inaposema ‘tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao’?

“Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia;Achukiaye mambo ya dhamana yu salama

Rudi nyumbani

Print this post

Nini maana ya Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza (Yakobo 4:9)

Swali: Biblia inasema katika Yakobo 4:9 kwamba kucheka kwetu kugeuzwe kuwa maombolezo, je Mungu hapendi tuwe tunafurahi? Au maana yake ni nini mstari huu?

Jibu: Turejee

Yakobo 4:9  “Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu”.

 Kicheko kinachozungumziwa hapo ambacho kinapaswa kigeuzwe kuwa maombolezo sio kicheko cha mambo mazuri, kwamba umeona watu wameokoka na ukafurahi na kushangilia na kucheka, kwamba ndio kicheko hicho kibadilike kiwe maombolezo!.

Hapana! Bali kicheko kinachozungumziwa hapo ambacho ni sharti kibadilike na kuwa maombolezo ni kicheko cha mambo mabaya (yaani dhambi). Mtu anapocheka baada ya kupata fedha za dhuluma, kicheko hicho ndicho biblia inachosema kuwa kinapaswa kibadilike kuwa huzuni, Kicheko mtu anachokipata baada ya kumwumiza mwingine au kuiba, au kula rushwa au kudhulumu au kufanya jambo lingine lolote baya hicho kicheko kinapaswa kibadilike na kuwa huzuni.

Maana yake mtu anapogundua makosa yake hapaswi tena kufurahia mabaya anayoyafanya au aliyokuwa anayafanya, badala yake anapaswa aomboleze, mtu aliyekuwa anazifurahia pesa haramu na kuzichekelea pale anapomjua Yesu, anapaswa asiendelee kufurahia maisha anayoishi bali aomboleze kwa kutubu na kujutia alichokuwa anakifanya.

Na kwanini ni muhimu kuomboleza na kutubu kwa mabaya, badala ya kucheka na kufurahia katika mabaya?

Ni kwasababu Bwana Yesu alisema ole wao wachekao sasa maana wataomboleza na kulia..

Luka 6:25 “… Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, kwa kuwa mtaomboleza na kulia”.

Kwahiyo ni heri leo kuomboleza  kwaajili ya dhambi na maovu ili tupate rehema na siku za mwisho tuweze kuokolewa na lile ziwa na moto, kuliko leo kucheka na kufurahia mambo mabaya halafu mwisho wa siku tunatupwa katika ziwa liwakalo moto.

Swali ni je! Mimi na wewe leo tunafurahia nini na kuombolezea nini?

Je ni anasa ndizo unazozifurahia?, ni uzinzi na uasherati ndio unaoufurahia?, je ni mali za dhuluma ndizo zinazokupa kicheko?, je ni wizi ndio unaokuburudisha? Je ni kuanguka kwa wengine ndiko kunakokuchekesha.

Kumbuka neno la Mungu litabaki kuwa lile lile siku zote kuwa “ole wa wanaocheka sasa maana watalia”

Tubu ukaoshwe dhambi zako leo kwa kumwamini Yesu Kristo na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu Kristo.(Matendo 2:38).

Yakobo 4:7  “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

8  Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.

9  Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu.

10  Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza”.

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

KUWA MWOMBOLEZAJI.

Nini maana ya neno ‘mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena’?

MAZUNGUMZO MABAYA HUHARIBU TABIA NJEMA.

Nini maana ya huu mstari; Mithali 10:22 “Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo”

Nini maana ya huu mstari Ayubu 23:10 ‘Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu’?

Rudi nyumbani

Print this post

Nini maana ya huu mstari Ayubu 23:10 ‘Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu’?

Ayubu 23:10 “Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu”

Kila mmoja kaandaliwa mapito yake na Mungu, ijapokuwa hatma yetu ni moja lakini mapito kamwe hayawezi kufanana. Na anafanya hivyo kwasababu ya utofauti wa wito na huduma, aliopewa kila mmoja katika kusudi lake aliloitiwa duniani.

 Hivyo unapookoka anachokifanya Mungu ni kuitazama njia yako, kisha kukupitisha katika mitihani yake ili uweze kufuzu kulitimiza kusudi lake alilokuwekea mbele yako. Hivyo hii mitahani kwa jina lingine ndio yanainaitwa majaribu. Tofauti na baadhi wanavyotafsiri kwamba majaribu ni mitego ya dhambi Mungu anayompitishia mtu. Jibu ni hapana, Kama ni hivyo basi maandiko yangekuwa yanakinzana pale yanaposema, Mungu hamjaribu mtu, bali mtu mwenyewe anajaribiwa na tamaa zake mwenyewe (Yakobo 1:13-15)

Kwahiyo sasa lengo la mitihani hii ni kukuimarisha zaidi. Kwamfano labda wewe umewekewa huduma ya  uponyaji ndani yako. Wakati mwingine Mungu anaweza kuruhusu upite  mapito kama ya kuumwa sana, ili utambue umuhimu wa kuwajali na kuchukuliana na wagonjwa wenye hali mbaya kama hizo, watakaokuja kwako kuhitaji msaada mbeleni.

Ndio maana ya hili andiko ‘yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu’

Kwamfano katika biblia utaona mitume walipitia vipindi vingi mbalimbali vya kuvua samaki, lakini asilimia kubwa ya hivyo hawakuwa wanapata chochote baada ya kutaabika usiku kucha, yamkini wengine walikuwa wanapata lakini wao hawapati chochote, lakini walipokutana na Yesu walipata kirahisi. Ni nini Bwana alikuwa anawafundisha? Ni uvumilivu katika kuwavua watu wake, na kwamba watakapoanza huduma watambue kuwa wokovu unatoka kwa Bwana na sio katika uweza wa nguvu zao.

Vivyo hivyo na wewe utapitishwa katika pito lako la moto, ili kujaribiwa lengo ni kuimarishwa. Wengine wanafanywa watumwa wa kuteswa sana ili watakapofanywa mabwana waweze kuwastahi watoto wa Mungu kwa upole watakaokuja chini yao, wakikumbuka mateso yaliyowakuta wao hayapaswi kwenda kwa wengine.

Mwingine katika utasa, mwingine katika vifungo, mwingine katika ujane, lakini madarasa yao yakishakamilika, basi taabu hizo zinawaacha. Na hivyo wanakuwa tayari kwa ajili ya utumishi wa Bwana.

Halikadhalika na wewe pia ikiwa umeokoka, na unajikuta katika madarasa ya Mungu,  yakupasa useme kama Ayubu ‘yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu’. Na mwisho wako utakuwa ni mkuu sana kuliko mwanzo. Kwasababu siku moja utayafurahia mapito ya Mungu na kumtukuza sana (Yeremia 29:11).

Lakini kama hujaokoka, usiseme unafundishwa na Mungu, hayo ni mafundisho yako au ya ibilisi. Kwasababu Mungu hawezi kumpa mitihani mtu ambaye si mwanafunzi wake. Ni heri ukafanya uamuzi wa busara leo kwa kumkaribisha Yesu Kristo moyoni mwako. Unasubiri nini usifanye hivyo?

Ikiwa upo tayari kufanya hivyo basi bofya hapa kwa mwongozo huo >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO

Ubatizo wa moto ni upi?

MAJARIBU 10 WANA WA ISRAELI WALIYOMJARIBU MUNGU.

Kupwelewa maana yake nini? (Matendo 27:26).

HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?

Kwanini biblia inaitaja mara kwa mara dhahabu ya Ofiri?

KWA KUWA WASEMA MIMI NI TAJIRI.

Rudi nyumbani

Print this post

Fahamu maana ya Mithali 29:4 “Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua.

Mafundisho maalumu kwa watumishi wa Mungu (Wachungaji, Mitume, manabii, wainjilisti n.k.)

Mithali 29:4 “Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua”

Uongozi wa kidunia mara nyingi hutoa picha ya uongozi wa rohoni.

Kama andiko hilo linavyosema, “Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua” maana yake ni kuwa kiongozi anayetawala nchi na huku moyo wake ni wa rushwa, kamwe hilo taifa halitakaa liendelee vile ipasavyo.

Kwamfano, mtu anataka kupitisha bidhaa zisizo na ubora bandarini ili ziuzwe ndani ya nchi. Lakini taarifa zinamfikia kiongozi, badala Yule kiongozi azipige marufuku, anapokea pesa kutoka kwa wale wanaotaka kuingiza, hivyo athari inakwenda kwenye jamii kwa tamaa zake za mali.

Au anaingia mikataba ambayo haina manufaa kwa watu wake, kisa tu kaahidiwa atalipwa pesa nyingi kutoka kwao. Hivyo rushwa zipo nyingi sio tu za kipesa, lakini pia za kiuongozi, kisa Yule ni rafiki, au ndugu, anampa nafasi ya utawala, lakini Yule mwenye ujuzi na ueledi ananyimwa. Sasa taifa lake kiongozi huyu, haliwezi kusimama kwa namna yoyote.

Lakini akiwa ni wa haki (Mtoa hukumu za haki), ni lazima tu nchi hiyo itastawi, Kwasababu maandiko yanasema haki huinua taifa.

Mithali 14:34 ‘Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote’.

Uongozi wa Rohoni.

Vivyo hivyo pia na viongozi wanaongoza kanisa la Kristo ambao kuna watu chini yao wanaowaangalia, katika ngazi yoyote iwe ni Maaskofu, Wachungaji, waalimu, wainjilisti, mitume na manabii. Wakiwa na mioyo ya rushwa ndani yao, kamwe kundi hilo halitathibitika.

Kwamfano, mchungaji anapendelea watu Fulani, anawapa nafasi ya uongozi au anawapa viti vya mbele, kisa tu wanachangia huduma kwa sehemu kubwa, hata kama haiwakidhi wanapewa kisa tu wana fedha nyingi, wanaachwa wale wenye uwezo wa Roho nyuma. Sasa Hiyo rohoni ni rushwa na ni mbaya sana kwa maendeleo ya kanisa.

Yakobo 2:1  Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu.2  Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; 3  nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu, 4  je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu?

Mwingine atauza mafuta, au maji, au chumvi, kisha atasema ni lazima uvinunue ili upokee Baraka zako. Mwingine atasema ili unione mimi nikufanyie maombezi, toa kiwango Fulani, au nikutane na wewe kimwili. Hizo zote ni rushwa za kiroho na zinakuja kwa maumbile mengi sana.

Kunaweza kubuniwa michango ya aina mbalimbali katika kanisa, afadhali lengo lingekuwa ni kwa ajili ya maendeleo ya kazi ya Mungu, lakini unakuta lengo ni ili kiongozi apate fedha ajinufaishe maisha yake.

Mwingine anawachagua viongozi wa kanisani, kindugu, kisa Yule ni mjomba wake, au shemeji yake na kuacha wale walioteuliwa na Mungu.

Yote haya yakiwa ndani ya kiongozi yoyote, ambaye anasimama sio kwa ajili ya kundi bali kwa ajili ya nafsi yake. Kamwe mkusanyiko huo hauwezi kuendelea kiroho. Utazidi kudhoofika, kwasababu umekosa uongozi bora.

Ni vema kujihakiki wewe ambaye umeitwa kulichunga kundi, Maono yako ni nini kwa watu wa Mungu? Je! Ni Uwe tajiri na maarufu kupitia wao? Au ulijenge kanisa la Bwana? Kumbuka utatoa hesabu kwa utumishi wako siku ile ya mwisho, Na kama ukionekana uliwatesa na kuwanyanyasa utakatwa vipande viwili, kisha kutupwa katika ziwa la moto (Mathayo 24:48-51). Na adhabu yako inakuwa kubwa kushinda ya wengine kwasababu ulijua mapenzi ya Bwana wako lakini kwa makusudi hukuyafanya, Hivyo utaadhibiwa sana. Ogopa hukumu ya Mungu. Acha kuiga-iga mifumo ya makristo wa uongo. Tembea katika Neno, kielelezo chako akiwa Kristo ambaye hakuwa na upendeleo wala tamaa ya vitu.

Siku hizi ni siku za mwisho, tubu dhambi zako mgeukie Bwana kwa kumaanisha badili namna ya uongozi wako, simamia haki ya Mungu, uthibitike katika utumishi huo.

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Vifungu vya biblia kuhusu Uongozi.

Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?

Rushwa inapofushaje macho?

Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako (Mithali 27:23)

ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO

Bwana alimaanisha nini kusema “Mwanafunzi hawi mkuu kuliko mwalimu wake”?

Rudi nyumbani

Print this post

Nini maana ya Mhubiri 10:20 inaposema Usimlaani mfalme, la, hata katika wazo lako?

Mhubiri 10:20 Usimlaani mfalme, la, hata katika wazo lako; Wala usiwalaani wakwasi chumbani mwako; Kwa kuwa ndege wa anga ataichukua sauti, Na mwenye mabawa ataitoa habari

JIBU: Ni vema kutambua kuwa aliyeandika habari hii alikuwa ni mfalme, hivyo alitambua vema alichokiandika,  na kwa hekima ya Ki-Mungu akazinakili ili ziwe onyo na angalizo kwetu . Ni wazi kuwa aliwahi kukutana na taarifa nyingi za uasi zilizowahi kupangwa  kinyume chake kwa siri, au  maneno ya unafiki, au ya dhihaka zilizosemwa kwa siri kinyume chake. Na yote hayo yakamfikia kwa haraka sana, kinyume na matarajio ya wale waliyoyapanga. Na huwenda wakawa wanabakiwa na maswali mengi, ni nani anayetoboa siri zao?.Wakakosa majibu

Sasa ni kwanini iwe hivyo?

Ni kwasababu Utawala wowote wa wakuu, unaundwa pia na ulinzi wake maalumu, (unaojulikana na ule wa siri usiojulikana). Kiasi kwamba chochote utakachokipanga kinyume chake kwa siri , tambua tu kitamfikia. Ndio maana hapo anasema usiwalaani katika wazo, au katika chumba chako cha siri.. Akiwa na maana hata wazo lako usiliruhusu kufanya hivyo, kwasababu mtu anayanena yaujazayo moyo wake. Kabla uasi haujatokea nje, unaanzia kwanza rohoni.

Halikadhalika wakwasi wanaozungumziwa hapo, ni watumishi wa wafalme, aidha mawaziri, au maakida, au maliwali ambao kikawaida huwa ni matajiri, vivyo hivyo na wao usijaribu kufanya hivyo ukidhani taarifa hazitawafikia. Zitawafikia, Mhubiri anatumia mfano wa ndege anasema.. ‘Kwa kuwa ndege wa anga ataichukua sauti, Na mwenye mabawa ataitoa habari’. Yaani kwa jinsi ndege wanavyoweza kusafiri kwa haraka, sehemu moja hadi nyingine, kwa wepesi wao na safari yao ya anga isivyo na vikwazo, ndivyo watu usiowajua watakavyoifikisha habari kwa wakuu wao, kinyume na matazamio yako.

Ndivyo ilivyokuwa kipindi cha mfalme Ahasuero, kulitoka watu wawili waliopanga mikakati kwa siri kumuua, lakini taarifa zilimfikia haraka mfalme kwa kinywa cha Mordakai mlinzi wa mlangoni, na wale watu wakagundulikana wakauliwa mara moja. (Esta 2:21-23)

Kufunua nini?

Hakuna jambo lolote la siri ambalo halitajulikana kwa wakuu.

Tunaye Mfalme wa Wafalme, YESU KRISTO ambaye ndiye anayepaswa kuogopwa na watu wote ulimwenguni. Na kwamba hatupaswi kufanya jambo lolote kinafki, au kwa-siri mbele zake, linalokinzana na ufalme wake duniani. Kwasababu yote yatakuja kufichuliwa na kuwekwa wazi siku ile ya mwisho ya hukumu.

Yeye mwenyewe  alisema;

Luka 12:2  “Lakini hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa, wala lililofichwa ambalo halitajulikana. 3  Basi, yo yote mliyosema gizani yatasikiwa mwangani; na mliyonena sikioni mwa mtu katika vyumba vya ndani, yatahubiriwa juu ya dari”

Hivyo uonapo kazi ya Mungu ya kweli inatendeka, kuwa makini sana na kinywa chako, uyapinge hata hayo mawazo yanayotaka kukwambia utukane, au ukufuru, au upinge. Vilevile wewe kama mhudumu wa kazi ya Bwana, tumika kwa uaminifu na kwa hofu ukijua kabisa mambo yako yote yanaonekana wazi mbele za Mungu, hakuna maficho.

Tuwe makini sana na ufalme wa Yesu Kristo duniani.

Je! Upo ndani ya Kristo? Je! Unatambua kuwa hizi ni nyakati za hatari, Yesu yupo mlangoni sana kurudi kulichukua kanisa lake? Unaishi maisha ya namna gani, ukifa leo huko uendako utakuwa mgeni wa nani? Embu tubu dhambi zako mgeukie Bwana akutakase, umtumikie yeye katika kipindi hichi kifupi tulichobakiwa nacho, itakufaidia nini uupate ulimwengu mzima kisha ukapata hasara ya nafsi yako?. Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo, Basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala hiyo ya toba >>>>  KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

YESU NI MFALME WA AINA GANI KWAKO? 

Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?

BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?

Kula uzao wa tumbo lako maana yake nini? (Kumbukumbu 28:53)

JINA LAKO NI LA NANI?

Rudi nyumbani

Print this post

Nini maana ya Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu?

SWALI: Naomba kufahamu maana ya hili andiko;

Mithali 9:13 “Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu”.


JIBU: Kupiga kilele kunakozungumziwa hapo ni zaidi ya ile ya ‘kupaza sauti ya juu’ bali hapo anamaanisha pia ‘Kulazimisha jambo lake lionekane, ambalo limeshindikana kwa namna ya kawaida, hivyo anatumia njia nyingine za usumbufu.(Ndio makelele)

Kwamfano, labda amejiona havutii mbele za watu, anachofanya, ni kusambaza picha za uchi-uchi mitandaoni, au kuvaa nguo za ajabu na kukatiza mitaani, ili wanaume wamwone wamtamani wamfuate. Hizo ni kilele za mwanamke mpumbavu.

Na ndio maana ukiendelea kusoma vifungu vinavyofuata vinamlenga mwanamke wa namna hii, tusome..

Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu.  14 Hukaa mlangoni pa nyumba yake, Juu ya kiti mahali pa mjini palipoinuka,  15 Apate kuwaita wapitao njiani, Waendao moja kwa moja katika njia zao.  16 Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili,  17 Maji yaliyoibiwa ni matamu, Na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza.  18 Lakini huyo hajui ya kuwa wafu wamo humo; Ya kuwa wageni wake wamo chini kuzimuni

Na ndio huyu huyu anayezungumziwa katika Mithali 7:10-11

Ni mwanamke ambaye akiona, hapendezi anakwenda kujichubua na kwenda kujipamba na kujiwekea makucha marefu na kuvaa viatu vilivyoinuka kama kwato, aonekane kama mdoli barabarani, Ili watu wamwangalie wamsifie, au wamfuate wamwoe au walale naye.

Tofauti na mwanamke mwenye busara, biblia inasema huwa ni MTULIVU, na Mpole, na anazingatia sana kuufunika mwili wake. Hana tabia ya kujikweza zaidi ya alivyoumbwa na Mungu, hana makelele, mwenendo wake umenyooka, huwezi mwona anajianika kwenye mitandao ya kijamii, kila tukio yumo na yeye aonekane mrembo, akipost picha zake za uchi-uchi, huwezi mpata hapo.

1Timotheo 2:9  “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; 10  bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu. 11  Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna”

Je! Wewe ni mwanamke mwenye makelele? Au mtulivu. Kumbuka heshima yako na thamani yako ipo katika sitara yako. Ukishindwa kujithamini utaitwa ‘mjinga’, na’ usiyejua kitu’ Kama maandiko yanavyosema hapo.

Jitambue.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang’anywa watoto wake.

Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mikononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?

Nini maana ya huu mstari; Mithali 10:22 “Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo”

Nini maana ya Mithali 27:6 “Jeraha utiwazo na rafiki ni amini;

Kwanini Mungu anajifanya kama hajui mambo?

Rudi nyumbani

Print this post

Nini maana ya huu mstari; Mithali 10:22 “Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo”

Ni kwa namna gani baraka ya Bwana haichanganyi na huzuni, nyuma yake?

Mithali 10:22 “Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo”


JIBU: Kwanza ni vema kufahamu hapo anaposema ‘Baraka ya Bwana hutajirisha’ hamaanishi kuwa kipimo cha kuwa umebarikiwa na Bwana ni utajiri unaofuata baada ya hapo, hapana, Kwasababu wapo watu ambao si wakristo na hawamchi Mungu lakini ni matajiri, na wapo ambao si matajiri na wengine ni maskini kabisa lakini ni matajiri kwa Bwana.

Ufunuo 2:9  “Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani”.

Baraka ya Bwana haipimwi kwa mali, bali kwa mwitikio wa wokovu ndani ya mtu.

Lakini katika mstari huo, anaeleza tofuati iliyopo kati ya utajiri unaopatikana kwa Mungu na ule unaopatikana penginepo. Kwamba ule wa ki-Mungu Hauchanganyi huzuni ndani yake. Lakini ule wa kwingine unafuatana na huzuni nyingi nyuma yake.

Kwamfano mtu amepata mali kwa njia ya biashara ya madawa ya kulevya. Ni wazi mtu kama huyu hawezi kuwa na raha, kwasababu wakati wote atakuwa katika kujilinda, na mashaka ya kukamatwa na vyombo vya dola. Au mwingine kapata utajiri kwa njia ya rushwa, atakuwa na hofu sikumoja  kukamatwa na vyombo vya dola kwa kosa la kuhujumu uchumi. Au mwingine kwa njia ya uganga, atapewa masharti, atoe wengine kafara, au alale chooni sikuzote za maisha yake, ili utajiri wake uendelee.

Hivyo utajiri wowote nje ya ule unaopatikana na Mungu, unavimelea vingi vya mateso. Visasi, vinyongo, wivu, hofu, mashindano n.k. Kwa kifupi ni kuwa hauna raha, Hivyo Bwana anatushauri kama kufanikiwa tufanikiwe kwake ambapo kunaendana na kanuni ya kumcha yeye kwa bidii (Kumbukumbu 28), kufanya kazi halali, na kuwa mtoaji. Na utakapobarikiwa basi Bwana atakupa raha katika vitu hivyo.

Bwana awe nawe.

Je! Upo ndani ya Kristo? Kama ni la! Wakati ndio sasa, geuka  upokee ondoleo la dhambi zako kwasababu muda ni mchache tuliobakiwa nao, tubu pokea wokovu sasa Parapanda inakaribia kulia. Ikiwa upo tayari kutubu leo, basi fungua hapa kwa mwongozo huo. >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

USINIPE UMASKINI WALA UTAJIRI. (Mithali 30)

KANUNI RAHISI YA KUPOKEA BARAKA MARA DUFU.

MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!

USIIKARIBIE DHAMBI, KAA NAYO MBALI.

Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU BARAKA

Ni sahihi kwa mkristo kupokea fedha kutoka kwa mtu anayefanya kazi haramu?

Rudi nyumbani

Print this post

Ni kwa namna gani haki huinua taifa? (Mithali 14:34)

Swali: Maandiko yanasema “Haki huinua Taifa”.. Je hii imekaaje kiundani zaidi?

Jibu: Tusome,

Mithali 14:34 “HAKI HUINUA TAIFA; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote”.

Kwa tafsiri ya kawaida mtu mwenya haki ni yoyote yule anayefanya matendo ya haki bila kujali kile anachokiamini, lakini kibiblia ni tofauti kidogo…Kibiblia  mtu “mwenye haki” ni yule anayemcha Mungu na “asiye haki” ni yule asiyemcha Mungu.

Kwahiyo hata kama mtu atajitahidi kufanya matendo mazuri na yenye kukubalika katika jamii yake yote, lakini kama moyoni mwake hamwamini Mungu, huyo kibiblia ni mtu asiye haki hata kama ana sifa njema.

Kwahiyo wanapoongezeka watu wanaomcha Mungu wengi katika Taifa maana yake “Haki na yenyewe inazidi kuongezeka”. Na matokeo ya kuwepo Wenye haki wengi juu ya nchi kuliko wasio haki ni kunyanyuka kwa Taifa, na kinyume chake wanapokuwepo wasio haki wengi katika nchi kuliko wenye haki basi Taifa linakuwa hatiani kuanguka. Sasa utauliza ni kwa namna gani?.. Hebu tujikumbushe kidogo ile habari ya Ibrahimu na Elohimu wakati ule wa Maangamizi ya Sodoma na Gomora

Mwanzo 18:22 “Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana.

23 Ibrahimu akakaribia, akasema, JE! UTAHARIBU MWENYE HAKI PAMOJA NA MWOVU? 

24 Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, WALA HUTAUACHA MJI KWA AJILI YA HAO HAMSINI WENYE HAKI WALIOMO? 

25 Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki? 

26 BWANA AKASEMA, NIKIONA KATIKA SODOMA WENYE HAKI HAMSINI MJINI, NITAPAACHA MAHALI POTE KWA AJILI YAO. 

27 Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu.

28 Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano. 

29 Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini. 

30 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini. 

31 Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini. 

32 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi.

 33 Basi Bwana alipokwisha kuzungumza na Ibrahimu, akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi mahali pake”.

Umeona? Kumbe Miji ya Sodoma na Gomora yaliteketea kwasababu ya kukosekana wenye haki ndani yake, kumbe wangeonekana tu wenye haki 10, basi miji ile yote ingepona!…lakini walipokosekana ndipo miji ile ikaanguka na kuangamia.

Ikiwa na maana kuwa Amani ya Miji na Mataifa ni kwasababu ya wenye haki ndani yake, ni kwasababu ya watu wa Mungu kuwepo ndani yake, hao wakiondolewa Taifa au mji unaanguka na kuangamia.

Ndio maana maandiko yanazidi kutufundisha kuwa dhiki kuu haitaanza mpaka Kanisa (wenye haki) watakapoondolewa, ikimaanisha kuwa uwepo wa watu wa Mungu katika dunia ndio unaozuia mambo kuharibika.. lakini hao watakapoondolewa ndipo Mataifa yataanguka, na ulimwengu mzima kwa ujumla.

2Wathesalonike 2:6  “Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.

7  Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; LAKINI YUKO AZUIAYE SASA, HATA ATAKAPOONDOLEWA.

8  Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake”

Je na wewe ni miongoni mwa wenye haki?

Kumbuka katika zama hizi tunahesabiwa haki mbele za Mungu kwa njia ya kumwamini Yesu Kristo… Na si kwa matendo yetu yasiyo na Imani yoyote…

Wagalatia 2:16 “hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki”.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu.

SWALI: Nini maana ya huu mstari?

Mithali 14:23 “Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu”


JIBU: Kitabu cha Mithali na Mhubiri ni vitabu vilivyobeba mafunzo mengi sio tu yale ya kiroho bali pia hata ya maisha ya kawaida.Mstari huo unaelezea uzito wa kitu kinachotendewa kazi zaidi ya kile kinachozungumzwa tu. Kwamfano hapo anaanza kwa kusema “katika KILA KAZI mna faida”.. Maana yake ni kuwa katika kazi yoyote (iliyonjema), inafaida nyuma yake,. Iwe ni ya kudharaulika au yenye heshima, iwe ni ngumu iwe ni rahisi, iwe ni ya kipato kikubwa au kidogo, maadamu kazi fulani inatendeka ni lazima faida tu itaonekana nyuma yake.

Lakini mtu akiwa ni wa mipango mikubwa, mikakati mingi, akili nyingi za kubuni namna ya kutenda kitu Fulani, vikao vingi,  halafu hakitendei kazi, Bwana anasema, badala ya faida kinyume chake ni hasara tu atapata..

Vivyo hivyo na katika roho. Bwana anataka tuwe watendaji wa Neno lake, Sio kusikia tu au kuomba tu peke yake. Unaweza ukaomba usiku kucha lakini kama sio mtendaji wa Neno lake uliombalo, ni unapoteza nguvu tu.

Kwamfano unaomba Bwana akusaidie uushinde uasherati, lakini bado unashikamana na vichocheo vyake vyote, una picha chafu kwenye simu yako, kinywa chako kinazungumza mambo ya kizinzi na vijana wenzako, unachati na watu wa jinsia tofauti muda wote, unatazama tamthilia zenye maudhui hayo, unasikiliza miziki ya kidunia, unaishi na boyfriend/girlfriend. Unategemea vipi tamaa zisikutawale? Utaomba usiku kucha na hutaona matokeo yoyote, kwasababu hukitendei kazi kile unachokiomba.

Bwana alisema kama vile mwili bila roho umekufa, vivyo hivyo imani bila matendo imekufa ndani yake.(Yakobo 2:17). Kukitendea kazi kile kimoja ukiombacho, kina nguvu sana kuliko maneno elfu unayoweza kumwomba Mungu mwaka mzima.

Yakobo 1:22  “Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. 23  Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. 24  Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo”.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya “katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni”.

Nini maana ya huu mstari? “Yeye mwenyewe ataokolewa lakini ni kama kwa moto”

Mithali 14:4 ‘Zizi ni safi ambapo hapana ngombe;

Marijani ni nini katika biblia(Ayubu 28:18,Mithali 8:11)?

Nini maana ya mhubiri 9:11? si wenye mbio washindao katika michezo?

BWANA UNIJULISHE MWISHO WANGU.

Rudi nyumbani

Print this post

HATA WAKATI WENU WA MVI NITAWACHUKUENI. (Isaya 46:3)

Isaya 46:3 “Nisikilizeni, enyi wa nyumba ya Yakobo, ninyi mlio mabaki ya nyumba ya Israeli, mliochukuliwa nami tangu tumboni, mlioinuliwa tangu mimbani; 

4 na hata uzee wenu mimi ndiye, na hata wakati wenu wa mvi nitawachukueni; nimefanya, nami nitachukua; naam, nitachukua na kuokoa”.

Mstari huu wa faraja unatuonyesha fadhili za Mungu jinsi zilivyo nyingi kwa watu wake, Anaonyesha jinsi asivyoweza kuwaacha watu wake, tangu wakiwa tumboni mwa mama zao hadi kufikia uzee wao. Kila hatua ya maisha yupo nao, kila pito liwe rahisi rahisi au liwe gumu yupo nao, wakiwa watoto, wakafikia ujana, kisha nguvu zikaisha wakiwa wazee, Mungu yupo nao. Haleluya.

Daudi alilitambua hilo pindi alipoishiwa nguvu zake, akaandika…

Zaburi 37:25 “Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula”.

Hivyo huna haja ya kuhofu kesho yako itakuwaje au uzee wako utaishaje, maadamu upo na Bwana, maadamu unamtumikia, siku hizo zikifika, atakuhifadhi Mungu wako. Mwingine anasema mpaka sasa sina mfuko wa mafao, na nguvu zangu zinakaribia kuisha, ni nani atakayenisaidia, ni nani atakayekuwa karibu na mimi? Jibu ni kuwa  Bwana ndiye atakayekuwa karibu na wewe. Kwasababu tangu zamani ulimtumainia. Lakini hata kama utakuwa na mali, huwezi kuwa raha moyoni wakati huo endapo Kristo hayupo nafsini mwako sasa.

Hivyo wekeza maisha yako kwa Bwana sasa, ili kesho yako pia iwe na matumaini na raha tele. Ikiwa wewe ni kijana wakati huu uliopo, mtafute muumba wako, upokee WOKOVU kwa kumaanisha kabisa kuuacha ulimwengu, mtumikie Mungu, kimbia kweli kweli tamaa za ujanani, kabla zile nyakati mbaya za hatari hazijafika, Kwasababu maandiko yanasema kuna siku-mbaya mbeleni zitawakumba watu ambao hawakumcha Mungu tangu zamani.

Mhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo”.

Ikiwa upo tayari kutubu dhambi zako leo , na kumkaribisha Bwana Yesu maishani mwako, basi bofya hapa kwa mwongozo wa sala hiyo ya toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

TUTAMKARIBIA MUNGU KWA IDADI YA MVI ZETU ROHONI.

Je! Wana wenu huwatoa kwa nani? maana yake ni nini?

NINYI AKINA BABA MSIWACHOKOZE WATOTO WENU

UFANYE WEMA WAKO KATIKA MAARIFA.

ANGALIENI MWITO WENU.

Praitorio ni nini? Na Kwanini ilikuwa ni najisi kwa wayahudi kuingia humo? (Yohana 18:28)

Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang’anywa watoto wake.

Rudi nyumbani

Print this post