Biblia inamaana gani inaposema ‘tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao’?

Biblia inamaana gani inaposema ‘tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao’?

SWALI: Biblia inamaana gani inaposema ‘tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao’? Mhubiri 3:11


JIBU:

Mhubiri 3:11 “Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho”

Mwanadamu alivyoumbwa ni tofauti na wanyama au viumbe hai vingine.  Kwani vyenyewe tangu vilipoumbwa mpaka sasa havibadiliki, wala haviendelei, kimaarifa, kiuelewa, au kiujuzi.. Lakini sisi wanadamu kila siku ndani yetu kuna kiu  ya kujua zaidi na zaidi, kufahamu zaidi na zaidi, kutafuta zaidi na zaidi, kutokuridhika hata kama tumepata.. Na hiyo ndiyo inayotupelekea kupiga hatua mpya kila leo. Sasa hiyo hali isiyokoma ndani yetu ndio inayoitwa UMILELE.

Na Mungu ameiruhusu iwepo ndani ya mwanadamu, kuvumbua, mambo mapya, tangu zamani hata sasa, na anafanya bidii kutafuta akidhani labda atafikia ukomo anaoutazamia, lakini kila kunapokucha ndipo anapogundua kuwa bado sana kuyaelewa mambo ya Mungu. Wanadhani pengine kwa kugundua ndege, ndio itawafikisha mbinguni, lakini kumbe, ndio wanaona anga halina mwisho.

Maana yake ni kuwa, hata milele yote ya maisha, au ya maarifa, au ya uvumbuzi kamwe hatutakaa tummalize Mungu. Yatosha sisi kukaa katika pendo lake, kuyatenda mapenzi yake katika Kristo Yesu,. Lakini tusipoteze nguvu zetu kumtafiti Mungu, ni heri tutumie hizo kuutafiti utukufu wake ili tumwabudu kuliko kuzitafiti njia zake, au kanuni zake alizojibunia, tutapoteza muda.

Sulemani alisema..

Mhubiri 8:17 basi, niliiona kazi yote ya Mungu, ya kuwa haitafutikani na mwanadamu kazi inayofanyika chini ya jua; kwa sababu mwanadamu na akijisumbua kadiri awezavyo kuitafuta, hata hivyo hataiona; naam, zaidi ya hayo, mwenye hekima ajapodhania ya kuwa ataijua, lakini yeye hataweza kuiona.

Dumu katika mapenzi yake Mungu, tunayojifunza kupitia biblia, kwani hilo ndio FUNGU letu tulilowekewa.

Ndio maana ya hilo Neno; Mhubiri 3:11 “Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho”

Je! Umeokoka? Je! Unatambua kuwa hizi ni nyakati za mwisho, na Kristo yupo mlangoni kurudi? Umejiandaaje? Tubu mgeukie Bwana akuponye.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?

TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.

Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake

KWA MIOYO YAO WAKAREJEA MISRI.

Nini maana ya Usiwe mwovu kupita kiasi? (Mhubiri 7:17)

USINIPE UMASKINI WALA UTAJIRI. (Mithali 30)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Jovitha Runyoro
Jovitha Runyoro
1 year ago

Hello,

Asante nimebarikiwa sana kwa neno.