Nini maana ya Usiwe mwovu kupita kiasi? (Mhubiri 7:17)

Nini maana ya Usiwe mwovu kupita kiasi? (Mhubiri 7:17)

Mhubiri 7:17 “Usiwe mwovu kupita kiasi; Wala usiwe mpumbavu; Kwani ufe kabla ya wakati wako?

Mstari huo haumaanishi kuwa uwe mwovu kiasi, hapana, uovu ni uovu tu, na una hukumu, Uwe unatenda dhambi nyingi au chache, ukifa utahukumiwa na jehanum utaenda..

Lakini kinachomaanishwa, hapo ni kuwa upo uovu unaozidi ambao, unaweza kukusababishia uondoke hapa duniani kabla ya siku zako,..Na aina nyingine ya uovu huu ni ule unaendekezwa kwa muda mrefu, pale unapojua madhara yake lakini hutaki kuacha.

Tengeneza picha unafanya kazi ya ujambazi, wa kuua watu kisa mali, unategemea vipi usipigwe risasi siku moja na polisi?

Wale wahalifu waliosulibiwa na Yesu pale msalabani, walijua kabisa yale yamewapata kwasababu ya makosa yao ya uuaji na wizi, na ndio maana mmojawao akasema.

Luka 23:41 “Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa”.

Au unasafirisha madawa ya kulevya, kimataifa, unategemea vipi usikamatwe na kunyongwa? Au unaiba mali za watu na umeonywa mara nyingi auche lakini husikii unategemea vipi usichomwe moto?

Au unamtukana Mungu unategemea vipi uhai wako usifupishwe? n.k n.k.

Au unauchukua utukufu wa Mungu kupita kiasi unategemea vipi Mungu asikuondoe, kwasababu yeye mwenyewe anasema, mimi ni Mungu mwenye wivu. Mtazame Herode alifanya jambo kama hilo, na Mungu anampiga saa ile ile na chango.

Matendo 12:21 “Basi siku moja iliyoazimiwa, Herode akajivika mavazi ya kifalme, akaketi katika kiti cha enzi, akatoa hotuba mbele yao.

22 Watu wakapiga kelele, wakisema, Ni sauti ya Mungu, si sauti ya mwanadamu.

23 Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho”.

Huo ni mifano michache ya maovu yanavuka mipaka, au yanayoendekezwa kwa muda mrefu. Umekuwa mzinzi au uasherati, na unajua kabisa tabia hiyo haimpendezi Mungu lakini bado unaendelea kufanya hivyo, siku baada ya siku, hapo unajitafutia mwenyewe Mungu kukupiga na janga la Ukimwi, na kufa kabla ya siku zako.

Mhubiri 7:17 “Usiwe mwovu kupita kiasi; Wala usiwe mpumbavu; Kwani ufe kabla ya wakati wako”?

Hivyo lililo la msingi, ni kujiepusha na uovu kabisa, kwasababu ouvu wowote uwe hata kama huna adhabu hapa, lakini kule utakutana nayo. ambayo ni ziwa la moto.

Warumi 2:5 “Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu”,

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

USIWE NA HAKI KUPITA KIASI.

Yuko mwenye haki apoteaye katika haki yake.

Huyu Azazeli ni nani tunayemsoma katika(Walawi 16:8)

Mungu aliposema Yesu ni mwanawe pekee, alimaanisha hakuwa na wengine?

Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu ni wakina nani?

UNYAKUO.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments