Mnara wa Babeli unafunua nini katika roho?
Wanadamu walipofika mahali wakaona kuwa ipo sababu ya kumfikia Mungu., maisha hayawezi kuwa na maana yoyote kama hawataweza kumfikia huyu mwanzilishi wa haya maisha..Hivyo kwa kuwa ile kiu ilikuwa ni kubwa ndani yao, wakabuni njia nyingi nyingi tofauti tofauti za kumfikia yeye,. lakini wakati ulifika wakagundua kuwa tusipokuwa na umoja,. tusipokuwa na usemi mmoja hatuwezi kufanya hivyo.
Ndipo wakaona ni vema wakubaliane kwa nia moja kutatua tatizo hilo. Na ndipo wakaamua kwenda kutafuta nchi tambarare huko Babeli na kuanza kutengeneza mnara mkuu ambao kwa huo walidhamiria kwa njia yoyote ile kumfikia Mungu…
Lakini Mungu aliliona hilo na kuona jinsi njia za wanadamu zitakapoishia ni pabaya pasipo kuwa na tumaini lolote, aliona sayansi zao za nyota na mbingu zitakapoishia, aliona unajimu wao utakapoishia, aliona uandisi wao utakapoishia n.k.
Pia tazama…
Hivyo kwa lugha zile zile na usemi ule mmoja waliokubaliana., katika huo huo Mungu aliwatawanya waende ulimwenguni kote kwasababu ile haikuwa njia sahihi Mungu aliyoikusudia watu wamfikie yeye. Na ndipo Mungu kuanzia wakati huo akaanza kuwatengenezea wanadamu njia iliyo sahihi ya kumfikia yeye, akaanza kuwajengea mazingira yote, tangu wakati wa Ibrahimu mpaka manabii, wote walitabiri juu ya njia hiyo pekee ambayo mwanadamu akiifuata basi moja kwa moja atawasiliana na Mungu, moja kwa moja atamwona Mungu, moja kwa moja atakula na Mungu katika meza moja.
Na ndipo ule wakati ulipofika Akamleta mwanawe wa pekee Bwana wetu Yesu Kristo, yeye ndiye MNARA WETU uliopachikwa pale YERUSALEMU, tofauti na ule wa BABELI..
Na kama vile ule wa Babeli ulivyokuwa na lugha moja na usemi mmoja lakini Roho wa Mungu aliusambaratisha kwa kuchafua usemi wao na lugha zao ili wasielewane kwasababu sio NJIA Mungu aliyokuwa ameikusudia, vivyo hivyo mnara huu ulioweka YERUSALEMU, takribani Miaka 2000 iliyopita Roho wa Mungu aliuunganisha kwa lugha moja na usemi mmoja..
Na ndio maana katika ile siku ya Pentekoste, Roho wa Mungu alishuka kwa ishara ya Lugha, watu wakaanza kusema kwa lugha za mataifa mengine, kiashirio kuwa watu waje sasa waujenge huu MNARA MPYA BWANA ALIOUWEKA ILI WAWEZE KUMFIKIA MUNGU.
Kumbuka Babeli ya kwanza iliyoharibiwa, watu walianza kunena kwa lugha mbali mbali lakini hawakuelewana, waliishia kugombana na kutengana. lakini ile siku ya Pentekoste Roho aliposhuka wakristo walianza kunena kwa lugha mbali mbali lakini walielewana, hawakugombana wala kutengana, na ndio maana kuanzia hapo mitume, walianza kukaa pamoja kwa umoja na kwa nia moja. Na watoto wa Mungu kuanza kukusanywa pamoja duniani kote kuanzia Yerusalemu.
Matendo 1: 8 “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi”.
Ndugu yangu, hutaweza kumfikia Mungu kwa elimu ya dunia hii, sayansi hatakusaidia kuujua mwanzo wa dunia. Wala mwisho wake, haitakusaidia kujua umbali wa kutoka duniani mpaka mbinguni. Haitakusaidia kugundua makao ya roho za watu zilizokufa. Sasa kama ndio hivyo kwanini unaweka tumaini lako huko?. Kwanini unaujenga mnara wa Babeli ambao Mungu alishaulaani?..
Ushirikina haukupi tumaini la maisha baada ya kifo. Ushirikina haukupi amani, ushirikina haukupi kumwona Mungu kwa namna yoyote ile. Maisha ya dhambi hayakupi tumaini la umilele. Hutaweza kumfikia Mungu kwa namna hiyo, uzima wa milele haufikiki kwa njia moja wapo ya hizo bali ni Kristo tu peke yake. Ndiye MNARA WETU.
Madaktari hawawezi kukupa tiba ya kifo, usiudharau msalaba..Unamkataa yeye ambaye sio tu anaowezo wa kukuponya mwili wako bali pia mwenye uwezo wa kuifanya roho na mwili wako usife kabisa hata milele.
Mungu alishatupa ishara siku ile ya Pentekoste, kwa LUGHA zile, akisema NJOONI! MJENGE MPATE KUMFIKIA MUNGU..Huu ndio wakati ndugu,
Yohana 14: 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”..
Ufunuo 22: 17 “Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure. ”
Kumbuka ndugu Shetani naye anajenga mnara wake mwingine baada ya ule wa kwanza kuanguka. Na mnara huo unafanana sana na huu wa Bwana Yesu. Na anakusanya watu wake kutoka kila mahali duniani kote, kuwaleta katika dini moja, na imani moja, na usemi mmoja. Anakusanya dini zote na madhehebu yote na kuyaleta pamoja. Kuiunda ile chapa ya mnyama, ambapo itafika wakati mtu asipokuwa mshirika wa moja ya madhehebu yake hataweza kununua wala kuuza. Mtu asipokuwa mshirika wa huo mnara hutaweza kufanya lolote.
Kadhalika na mnara wa Yesu Kristo uliopo leo. Bwana anakusanya watu wake kutoka kila mahali, kama huna Roho Mtakatifu, hutaweza kuurithi ule uzima wa milele. Kama hujazaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho huwezi kumwona Mungu, wala kuwa na sehemu katika huo mnara.
Hivyo Usimwache leo ayapite maisha yako ili uweze kumfikia BABA.
Ubarikiwe.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali “share” kwa wengine ujumbe huu.
Mada Nyinginezo:
MTETEZI WAKO NI NANI?
BADO KITAMBO KIDOGO HAMNIONI
VIUNO VYENU VIWE VIMEFUNGWA NA TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA
JE! NI SAHIHI KWA MKRISTO KUOA/KUOLEWA NA MTU WA IMANI NYINGINE?
NINI MAANA YA ELOHIMU?
Rudi Nyumbani
Print this post
{Mathayo 16:18 “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”}
Mwanzo 22:17 “katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; “ }
Uzao wa Ibrahimu ni uzao wa YESU KRISTO. Hivyo ili mtu ahesahiwe kuwa ni mmoja wa uzao wa YESU KRISTO ni lazima azaliwe mara ya pili katika uzao wake. Na kuzaliwa mara ya pili si katika mwili bali ni katika roho. Tutakuja kuona baadaye kidogo mtu anapaswa afanye nini ili azaliwe mara ya pili. Lakini sasa tutazungumza faida chache za kuwa mmoja wa uzao huu wa kikuhani wa Yesu Kristo.
1Petro 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu,
Kama tunavyofahamu tabia za watoto nyingi huwa zinarithiwa kutoka kwa wazazi wao, ndio unakuta labda familia moja ni ya watu viongozi ongozi ukichunguza huko utakuta watoto nao wanarithi hizo tabia za kupenda kuwa viongozi na wakishakuwa wakubwa utakuta nao pia ni viongozi.
Tunaona pia jambo hilo hilo linajitokeza katikati ya makabila, utakuta kabila moja watu wake wote wanafanana tabia Fulani, aidha unaweza ukakuta kabila hilo watu wake wanapenda kusoma hivyo wengi wao utakuta ni wasomi, wengine ni wafanyabiashara, jamii nyingine unakuta ni za watu wakatili, nyingine za wa watu watulivu, nyingine ni za watu wakarimu n.k. Sasa hii haiji hivi hivi hapana bali ni tabia zilizorithiwa kutoka kwa mababa zao ambao ni ndio waanzilishi wa koo hizo.
Vivyo hivyo na katika UZAO wa YESU KRISTO. Wote wanaozaliwa humo, kuna roho na tabia zinazofuatana nao katika maisha yao yote. Hivyo wanajikuta zile tabia YESU alizokuwa nazo kama Baba wa ukoo wanazirithi nao pia wanakuwa nazo kwamfano, tabia ya kuchukia dhambi, tabia ya kuwa mtu wa sala, tabia ya upendo, tabia ya kujitoa nafsi yako kwa wengine ikiwemo kusambaza habari njema za ufalme kwa watu wengine.n.k.
Lakini pia ipo SIFA moja kuu leo tutaizungumzia inayotembea katikati ya UZAO huo kikuhani wa Yesu Kristo nayo si nyingine zaidi ya UWEZO WA KUMILIKI MALANGO YA ADUI.
Sasa Malango ya adui ni yapi?
Malango ya adui yamegawanyika katika sehemu kuu mbili.
1) Lango la Shetani kama MBWA-MWITU.
2) Lango la Shetani kama MBWA-MWITU ndani ya vazi la kondoo.
Hayo ndiyo malango makubwa mawili ya shetani anayoyatumia katika siku hizi za mwisho, na katika hayo amefanikiwa kuwapeleka wengi kuzimu na anazidi kuwapeleka wengi sana, hususani kwa njia ya lango hilo la pili
Tunajua siku zote mbwa-mwitu kwa kumwangalia tu utamgundua kiurahisi endapo akiwa katikati ya kondoo, Hivyo shetani jambo pekee leo hii linalomtambulisha kiurahisi kwamba yeye ni shetani si lingine zaidi ya UCHAWI. Hivyo basi huwa anafanya bidii sana kuushambulia uzao wa Mungu kwa njia hiyo. Amefanikiwa kuwadondosha watu wengi ambao sio uzao wa Mungu. Na watumishi wake anaowatumia hapa ni watu waovu, waganga wa kienyeji na washirikina.
Hii ndiyo njia kubwa na ngumu ambayo ndio shetani anaitumia sasahivi kwa bidii zote kuwapeleka wengi kuzimu. Anavamia kundi la Mungu akijifanya kama kondoo, Anafanya hivyo kwa kutumia mitume, waalimu na manabii wake wa uongo kuliangamiza kundi. Silaha yake kubwa ni mafundisho ya uongo, na dini za uongo, Na njia hii anatumia maumbile mengi ya uongo, lengo tu kuwaangusha watu ambao wamesimama katika Imani ya Kristo Yesu.
2Wakorintho 11: 13” Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. 14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. 15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.”
2Wakorintho 11: 13” Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.
14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.”
Sasa kwanini biblia inasema UZAO wako utamiliki malango ya adui. Ni kwasababu Nje ya uzao huo, hutaweza kwa namna yoyote ile kumkwepa shetani na hila zake, kwa njia moja au nyingine utachukuliwa tu.
Wapo watu wadai wao hawadanganyiki katika imani yoyote ile, na huku hawajazaliwa bado mara ya pili hawajui kuwa hata hapo walipo wameshamilikiwa na malango ya kuzimu pasipo wao kujua.
Pia Kuna watu wanasema hawalogeki, na huku wapo nje ya uzao wa YESU kristo. Hawajui kuwa hapo walipo tayari wameshalogwa pasipo wao kujijua… wanadai ukoo wao haulogeki, hawafahamu kuwa ni UZAO mmoja tu ndio unaoweza kumiliki malango ya adui, na huo si mwingine zaidi ya UZAO wa YESU KRISTO.
Haumiliki kwa kukemea mapepo wala kwa maji ya upako au chumvi au mafuta, au udongo hapana bali unamiliki kwa mafuta ya ROHO MTAKATIFU ndani yao. Pale tu mtu anapozaliwa mara ya pili kwa kumaanisha kabisa,moja kwa moja Roho Mtakatifu anaingia ndani yake, kisha yule Roho anamwongoza kumtia katika kweli yote. Sasa hii KWELI YOTE, ndio yale mafuta ya Roho ambalo ni NENO LA MUNGU.
Kwamfano uchawi unapotumwa kwa mtu ambaye ni MZAO WA YESU KRISTO, labda tuseme ni ugonjwa fulani..na unakuta yule mtu wa Mungu hana habari yoyote, sasa kwasababu yeye ni mzao wa Mungu, Mungu hataruhusu ule ugonjwa umpate, atamkingia pasipo hata yeye kujijua kama katumiwa ugonjwa, Au hata kama Mungu akiruhusu ule ugonjwa umfikie, lile Neno la Mungu lipo ndani yake lile Neno linalosema Mathayo 8: “.. Mwenyewe [Yesu Kristo] aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.” ….
Basi atalitumia hilo Neno na kuanzia huo wakati anakuwa na amani akijua kuwa kwanza yeye ni mzao wa Mungu, na hakuna kilichopo juu yake,…Hivyo kule kuzimu wakitazama juu na kuona imani ya yule mtu imesimama, watajaribu kutupa ugonjwa tena na tena na wataona hakuna mafanikio hivyo wataacha kushughulika naye, na baadaye yule mtu anarudia katika hali yake ya kawaida.
Sasa huyo mtu anakuwa kaimiliki kambi ya adui, hakuna uchawi utakaosimama mbele yake, haihitaji maji, wala chumvi, wala mkesha wa maombi kumshinda shetani, ni NENO TU! (Waefeso 6:11-17)
Kwa kuwa shetani kazi yake ni kuakikisha anawaangusha wengi na kuwapeleka wengi kuzimu anajua kuwa akitegemea njia ya uchawi tu peke yake atawakosa wengi, hivyo alibadilisha mbinu na kuhamia kanisani, akijifanya na yeye kuwa mkristo, jambo analohakikisha ni kumtooa mtu katika mstari wa Neno la Mungu, na kumfanya aamini mafundisho mengine ya uongo nje ya Neno la Mungu. Na akishafanikiwa tu hivyo, basi ameshakumaliza…hapa ndipo watu wengi wanapoanguka, na anateleleza jambo hilo kwa kutumia wahubiri wa uongo.
Sasa kama wewe ni mazao wa YESU KRISTO, na yale mafuta yanakaa ndani yako ni rahisi kuwatambua,.Hutawatambua kwa miujiza, hutawatambua kwa karama, hutawatambua kwa chochote kile isipokuwa kwa matunda yao tu. Na matunda yao ni kile wanachokifundisha na kukizalisha, ukisaidiwa na Roho Mtakatifu kuwatambua.
Na ndio maana Bwana Yesu hakusema jihadharini na wachawi, au washirikina au mbwa-mwitu hapana..bali tujihadhari na mbwa-mwitu wanaovaa mavazi ya kondoo.
Mathayo 7: 15 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? 17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. 18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. 20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua”.
Mathayo 7: 15 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.
18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.
20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua”.
Unaona hapo? Msisitizo mkubwa ni kwa hao manabii wa uongo, na hao wapo katika dini na madhehebu, wanaofundisha watu kinyume na Neno la Mungu, wanafundisha mafundisho ya ibada za sanamu na za wafu, wanafundisha watu kwamba hakuna kuzimu, wanaowafundisha watu kuwa Mungu haangalii mavazi bali roho, wasiowafundisha watu kurudi kwa Yesu Kristo mara ya pili, wasiowafundisha watu umuhimu wa ubatizo sahihi na kuzaliwa mara ya pili na kuishi maisha matakatifu na badala yake wanafundisha watu injili tu za mafanikio na faraja katika dhambi, wasiowaonya watu watubie dhambi zao n.k Hawa wote ni watumishi wa Shetani wa hali ya juu zaidi hata zaidi ya wachawi na waganga wa kienyeji na wana kazi moja tu ya KUWAPELEKA WATU KUZIMU katika daraja la kwanza.
Lakini mtu asipotaka kuingia katika ule uzao, hataweza kumtambua shetani kwasababu hana Roho Mtakatifu ndani yake, Warumi 8: 9 “Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. ”
Sasa mtu anaingiaje katika ule uzao wa Yesu Kristo?
Kama tulivyosema mtu anaingia katika uzao huo kwa kuzaliwa mara ya pili tu!, na maana ya kuzaliwa mara ya pili ni KUZALIWA KWA MAJI na KWA ROHO (Yohana 3:3 na Yohana 3:5), ambako huku kunakuja baada ya mtu kudhamiria kutubu kabisa kwa kumaanisha kuacha dhambi zake, na kuanza kuishi maisha mapya katika Kristo na kisha kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kisha kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu atakayemweza na kumsaidia kumwongoza katika kweli yote.
Ubarikiwe!
Tafadhali “Share” ujumbe huu kwa wengine
MUNGU ALIVICHAGUA VITU AMBAVYO HAVIKO.
VITA DHIDI YA MAADUI
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU
“WOKOVU WETU U KARIBU NASI KULIKO TULIPOANZA KUAMINI”
ULE MSALABA UNAOWEKWA KWENYE KABURI, NA ILE IBADA INAYOFANYWA VINA UMUHIMU WOWOTE KWA MKRISTO?
Mwanadamu kaumbwa kwa vitu viwili: MWILI na ROHO, Na kila upande una namna yake ya kutunzwa, na namna yake ya kuangamizwa, kila kimoja kina namna yake ya kupata uzima, na namna yake kupata mauti. Kwamfano mwili unatunzwa kwa vyakula vya kimwilini, na maji ya kimwilini, vivyo hivyo unaharibiwa kwa vitu vya kimwili, mwili ukikosa chakula au maji unakufa, kadhalika ukiunguzwa na moto unakufa.
Na roho pia ipo vivyo hivyo, ili iiishi inahitaji vyakula vya aina yake ya rohoni, na maji yake ya rohoni, hivyo ikikosa hivyo vitu, basi hiyo roho nayo itakufa, na pia roho ikiunguzwa na moto wa rohoni itakufa vile vile, lakini moto wa mwilini hauwezi ukaiunguza roho, kwasababu Mungu alivyoyaumba maumbile ya mwili ni tofauti na yale ya roho.
Tukirudi katika maandiko, Kristo alikuja kuvikomboa vyote viwili (yaani miili yetu na roho zetu), ili vipate uzima wa milele, hivyo kwasababu alikuja kuzikomboa roho zetu, hawezi kutumia zana za mwilini kuzipa roho zetu uzima wa milele, ni sharti azizalishie roho zetu chakula cha rohoni, na maji ya rohoni ili zipate uzima huo. Na ndio maana alisema wazi Katika..
Yohana 6:35 “Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe”.
Unaona chakula na maji yanayozungumziwa hapo sio vya mwilini bali vya rohoni.
Sasa watu ambao watakufa leo hii, ambao hawajaokolewa, moja kwa moja roho zao zinashuka mahali panapoitwa kuzimu au Jehanum. Kule ni mahali ambapo mtu anawekwa kwa muda akisubiria hukumu ya mwisho ya mwanakondoo..
Tunaweza kusema kwa lugha ya sasa ni mahabusu au lockup ambapo mtu anakaa kule akingoja apandishwe kizimbani asomewe mashtaka yake kisha akatumikie kifungo chake aidha cha miaka 10 au 20 au cha maisha. Na ndivyo ilivyo kwa Jehanum hiyo ni tofauti na ziwa la moto. Ziwa la moto lenyewe linakuja mara baada ya hukumu ya mwanakondoo ambapo wakati huo kila mwenye dhambi atatumikia adhabu yake kwa kipimo cha uasi wake alioufanya duniani.
Tazamia pia…
Kumbuka Bwana alipokuwa amesimama katikati ya makutano ya watu wengi akipaza sauti yake kwa nguvu nyingi sana na kwa bidii kuwaambia watu waende kwake wanywe MAJI YA UZIMA yanayotoka kwake hakuwa anatania au anasema mambo ambayo hayana maana sana katika maisha ya mtu, hapana ndugu yangu, Alijua kabisa upo wakati roho za watu zitalia na kuugua kusikoweza kunenwa zikitafuta walau hata tone moja tu ya hayo maji wasilipate…Embu sikiliza Bwana Yesu alivyopaza sauti yake kwa bidii kuwasii watu katikati ya makutano siku ile kwenye sikukuu..
Yohana 7:37 “Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, MTU AKIONA KIU, NA AJE KWANGU ANYWE. 38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, MITO YA MAJI YALIYO HAI ITATOKA NDANI YAKE.”
Yohana 7:37 “Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, MTU AKIONA KIU, NA AJE KWANGU ANYWE.
38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, MITO YA MAJI YALIYO HAI ITATOKA NDANI YAKE.”
Sasa kumbuka haya maji faida yake sio kukupa uzima wa roho yako hapa duniani tu, hapana bali hii inaendelea hata baada ya kufa, lakini watu ambao hawajataka kuyanywa haya Maji sasa hivi, wakati yanapatikana kwa wingi na bure, utafika wakati karibia na kufa au baada ya kufa watatambua umuhimu wa haya maji, na pale watakapoyatafuta watayakosa..wakizitazama roho zao zinaenda kufa kwa kukosa maji, watahangaika kwa namna isiyoelezeka wakiyatafuta hayo maji ya uzima wasiyapate…Ndio tunarudi kwenye ule mfano wa Lazaro Bwana Yesu alioutoa katika..
Luka 16:19 “Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. 20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, 21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. 22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. 23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. 24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro ACHOVYE NCHA YA KIDOLE CHAKE MAJINI, AUBURUDISHE ULIMI WANGU; kwa sababu ninateswa katika moto huu. 25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. 26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. 27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, 28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. 29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. 30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu. 31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu”.
Luka 16:19 “Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.
20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,
21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.
23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro ACHOVYE NCHA YA KIDOLE CHAKE MAJINI, AUBURUDISHE ULIMI WANGU; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,
28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.
29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu”.
Tukisoma habari hiyo, tunaona kabisa wakati unaozungumziwa hapo ni wakati ambao watu wanaishi duniani na wengine wapo katika upande wa pili; aidha kuzimu au mahali pa starehe, Ni wazi kuwa mtu anapokufa bado anaendelea kuishi, mwili wake unabaki hapa hapa duniani lakini roho yake inaendelea kuishi mahali Fulani.
Kumbuka hapo mwili umeshabaki makaburini, kinachoendelea kuishi ni roho, na kama tulivyoona roho haiunguzwi kwa moto wa kawaida kama huu, hapana moto wa roho ni mwingine ambao hata sasa mtu anaweza akauhisi, jaribu kufikiri leo hii umehukumiwa kwenda kunyongwa, ukijua kuwa una dakika chache tu za kuishi, ni dhahiri kuwa ndani yako kutawaka moto ambao huo huwezi kuuelezea kwasababu unajua ni adhabu inayogharimu maisha yako hapa duniani,
Sasa huo unaousikia ndio moto wa roho isipokuwa katika kiwango kidogo sana, unaichoma roho yako, upo moto hasaa usioelezeka ambao utakuja baada ya kifo, pale utakapogundua hakuna mageuzi milele, una kipindi kifupi tu kisha ukatupwe kwenye lile ziwa la moto katika maangamizi ya milele, Utajisikiaje siku hiyo? Hiyo roho yako itakuwa ikihangaika kiasi gani ndugu?.Huo ndio moto yule tajiri uliokuwa unamuunguza kule kuzimu katika vifungo vya giza alivyokuwepo.
Jambo lingine tunaona liliokuwa linamtesa yule tajiri kule kuzimu ni KIU.. Hakuwa na kiu ya maji haya ya kisimani, kwasababu kule kuzimu mwili haupo alishauacha makaburini..Bali alikuwa na KIU YA MAJI YA UZIMA YAUPAO ROHO YAKE UZIMA. Alitamani apate walau tone moja la yale maji, apate uzima kidogo wa roho yake utakaomfanya angalau aishi kidogo, lakini hakupata,.. Alitamani apate nafasi ya pili ya kutubu dhambi zake, ili apate uzima lakini alikuwa ameshachelewa, alitamani abatizwe akitumaini hata siku ile atakayohukumiwa apate neema lakini alishachelewa, alitamani hata afanye ushirika na wakristo lakini muda ulishapita, alitamani akawashuhudie wengine habari njema lakini mlango ulikuwa umefungwa n.k.
Alipokuwa duniani aliikata ile KIU ya kutafuta UZIMA kwa mambo mengine, kwasababu ya utajiri wake akaikata kwa mali akiamini kuwa mali zinaweza kumpa uzima badala ya YESU KRISTO, hatuoni hata watu leo hii wakisema ukipata pesa umepata kila kitu,? Hawajui ya kwamba pesa haimpi mtu uzima, isipokuwa yale maji yanayotoka kwa Bwana YESU mwenyewe. Utajiri wa AFYA ulimdanganya akidhani kuwa afya yake itadumu, kwa lishe bora aliyokuwa akiizingatia na kwa wingi wa matabibu aliokuwa nao hakuna haja ya kumtafuta mwingine wa kumpa uzima, hao wanatosha kukata kiu yake..
Kwa wingi wa ANASA alizozitumainia, akaona zinatosha kumpa amani na furaha na raha, hivyo akapuuzia Amani idumuyo inayotoka kwa Bwana. Utajiri wake wa mambo yote, marafiki, ndugu, jamii, mali, afya, n.k. hakuna hata moja baada ya kufa vilifanikiwa kukatisha KIU iliyokuwa ndani yake..Jambo hilo alikuja kulingundua baada ya kufa.Na ndio maana hapo analia akitaka TONE moja tu la MAJI YA UZIMA.? Ndugu HAYO MAJI yalivyo na thamani kubwa baada ya kufa…Utatamani tone moja tu utakosa.
Leo hii unaweza kuona mtu baada ya kupatwa na mabaya, aidha kaambiwa na madaktari ugonjwa alionao anao mwezi mmoja tu wa kuishi, utaona mtu huyo kama alikuwa sio mkristo anaanza kuhangaika kumtafuta Mungu, lakini hapo kwanza wakati ni mzima alikuwa anaudhihaki wokovu,..Sasa hiyo ndio dalili ya ile KIU HALISI inaanza kuja ndani yake, hapo ndio unaanza kuona mtu anamtafuta mchungaji, anapigia watumishi simu wamuombee, au wamuhubiri n.k.. Sasa akishakufa katika dhambi zake, huko anakokwenda hiyo KIU inajizidisha mara nyingi sana zisizoweza kuelezeka ndipo majuto yasiyokuwa ya kawaida yatamjia.
Huko Jehanum Bwana Yesu alieleza pia kuna FUNZA ambaye hafi kama tunavyosoma katika
Marko 9:43” Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika; 44 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. 45 Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; 46 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. 47 Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum; 48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki”
Marko 9:43” Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika;
44 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.
45 Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum;
46 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.
47 Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum;
48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki”
Ukichunguza hapo utaona huyo FUNZA ni mmoja, ikiashiria kuwa wote watakaokuwa kule wataumizwa na huyo huyo mmoja, dhiki na shida watakazopitia watu wote watakaokuwepo huko zitafanana. Sasa huyu FUNZA ni nani?.
Tunajua siku zote funza huwa hawaji isipokuwa tu pale penye mzoga..Na kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanautafuna ule mzoga mpaka unakwisha.. Sasa huyu FUNZA sio wa mwilini, kwasababu huko hakuna mwili, kazi ya mwili itakuja kuonekana katika ziwa la moto ambalo tutaliona mbeleni kidogo.
Huyu FUNZA ni KUMBUKUMBU ZENYE MAJUTO. Hizi kumbukumbu kila mmoja atakayekuwepo kuzimu, zitamla, kila mmoja atakuwa anajutia maisha yake aliyoishi duniani, atakumbuka kuanzia siku ile alipokuwa mdogo anahubiriwa injili na kuipuuzia, atakumbuka siku aliyokuwa anadhihaki kazi ya Mungu, atakumbuka siku alizokuwa anafanya uasherati huku Roho wa Mungu akimwonya kwamba hicho kitu anachokifanya ni dhambi lakini hakutaka kusikia, atakumbuka siku aliyokuwa anasoma mahubirini na kuyapuuzia,
Atakumbuka muda aliokuwa anakawia kutubu mpaka kifo kilipomkuta kwa ghafla, atasema imekuwaje kuwaje nimefika hapa muda ambao bado?, yale majivuno yangu yananisaidia nini hapa?, ule uzuri wangu uko wapi tena?, zile pesa zangu mbona haziji kunitetea huku,.wale rafiki zangu niliokuwa nafanya nao anasa kumbe walinidanganya,..Ni majuto yasiyoelezeka utakapogundua kuwa wewe ni UZAO wa NYOKA, na ulidanganywa na shetani roho yako inakwenda kuteketezwa. UTALIWA NA HAYO MAWAZO kama vile FUNZA atafunavyo mzoga.
Sasa hayo majuto yatafikia kiwango ambacho hutatamani hata yule adui yako uliyekuwa unamchukia kuliko wote afike mahali ulipo, asifanye makosa uliyoyafanya wewe. Na ndio maana yule tajiri aliomba ndugu zake wakahubiriwe lakini akaambiwa wapo Musa na Manabii wawasikilize wao..Kuna watu leo hii wapo kuzimu wanakuombea wewe usifike kule. Ndugu kule sio mahali pa kufika kabisa.
Sasa baada ya huyo funza kuwala kwa muda mrefu utafika wakati sasa, wafu wote watafufuliwa katika miili yao waliyokuwa nayo hapa duniani, kisha kusimama mbele ya kile kiti cheupe cha Hukumu cha mwanakondoo (YESU KRISTO). (Ufunuo 20:11-15) Bwana Yesu alisema..
Yohana 5:28 “Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu”.
Yohana 5:28 “Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu”.
Sasa hawa wote waliokuwa kuzimu watafufuliwa, na kuvaa miili yao ya duniani waliyokuwepo nayo, ili wahukumiwe na kupewa sababu ya wao kwanini wanastahili adhabu inayofuata. Hivyo kila mmoja atahukumiwa kulingana na matendo yake na wingi wake wa dhambi alizozifanya. Kila mmoja wapo biblia inasema atakuwa na SEHEMU YAKE huko katika ziwa la moto..kwasababu ni ziwa litakuwa na nafasi kubwa, kila mmoja atakuwa na eneo lake peke yake akiungua.
Huko ndiko mwili na roho vyote kwa pamoja vitaangamizwa kwenye moto mkali sana utakaounguza mwili na roho kushinda hata ule uliokuwepo Jehanum. Hivyo ndugu tukiyajua hayo biblia ilishaweka wazi kabisa Katika
Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”
Kumbuka ndugu usifanye makosa kujiona ni TAJIRI na kuyadharau MAJI YA UZIMA kwasababu afya yako ni nzuri, au una mali ya kukutosha, au familia nzuri, au una ulinzi, n.k. hayo yote ipo siku yataondoka lakini KIU itabaki pale pale isipoikata leo hii, hautaweza kuikata kule..Usipumbazike na mambo ya ulimwengu huu yanayopita yakakupa kiburi kwamba Kristo hana faida yoyote katika maisha yako..
Na haya ndiyo Maneno aliyomalizia Bwana YESU katika kitabu cha biblia:
Ufunuo 22:16 “Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi. 17 Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! NAYE MWENYE KIU NA AJE; NA YEYE ATAKAYE, NA AYATWAE MAJI YA UZIMA BURE.”
Ufunuo 22:16 “Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.
17 Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! NAYE MWENYE KIU NA AJE; NA YEYE ATAKAYE, NA AYATWAE MAJI YA UZIMA BURE.”
Tubu ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la Yesu Kristo, na uuishie utakatifu angali muda upo.
Tafadhali “Share” kwa wengine ujumbe huu na Bwana atakubariki.
MAJI YA UZIMA.
EDENI YA SHETANI.
KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA…TUBU UMGEUKIE MUNGU
WALE MANABII 400 WALIOMTABIRIA MFALME AHABU WAKATI WA MIKAYA WALIKUWA NI MANABII WA MUNGU AU?
MUSA ALIUA LAKINI BADO MUNGU ALIMCHANGUA KUWAONGOZA WANA WA ISRAELI, JE! MUNGU ANARUHUSU MAUAJI?
MWENGE WAKO WA UHURU UPO WAPI?
Kitabu kinachoitwa BIBLIA, ambacho tunakifahamu kama Neno la Mungu, kiuhalisia sio Neno la Mungu katika utimilifu wote, hapana bali ni muhtasari au mwongozo wa sisi kulifahamu NENO LA MUNGU katika utimilifu wote. Kwasababu injili inasema katika Yohana 21: 25 “ Kuna na mambo mengi aliyoyafanya YESU; Ambayo yakiandikwa moja moja nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.”….Pia Sulemani aliandika katika Mhubiri 12: 12 “ Tena zaidi ya hayo mwanangu kubali maonyo; hakuna mwisho wowote wa kutunga vitabu vingi…”
Unaona hapo kwahiyo Neno lote la Mungu likiandikwa katika vitabu biblia haisemi uongo ni kweli ulimwengu usingetosha kwa wingi wa vitabu ambavyo vingeandikwa, ni mabilioni kwa mabilioni ya vitabu, kungekuwa na milima ya vitabu ulimwenguni kote kulielezea Neno la Mungu.
Hivyo biblia ni kama ufupisho tu! (summary), wa Neno la Mungu. Kwahiyo ili tuweze kulielewa Neno la Mungu kwa namna ambayo Mungu anataka tulielewe, hatupaswi kuishia hapo kwenye summary peke yake, bali tunapaswa tuzame katika kina na mapana kwa kupitia muhstari ule (Biblia) ili tupate picha yote ya kusudi la Mungu katika maisha yetu kwa ujumla.
Biblia iliposema “UTAFUTENI KWANZA UFALME WAKE NA HAKI YAKE” (Mathayo 6:33)… haikumaanisha kumaliza kusoma vitabu 66 vya biblia, na kukariri mistari yote iliyomo kule, Hapana, wazia hili, mpaka mtu anakuambia utafute kitu Fulani, inamaanisha kuwa hicho kitu anachokuambia ukitafute hakipatikani kiwepesi, ni kitu kilichojificha na ndio maana anakuambia ukitafute, hivyo utahitaji jitihada ya ziada kukipata. Na ndivyo ulivyo ufalme wa mbinguni, upo katika SIRI.
Tuchukulie tu mfano mwepesi katika biblia pale Bwana YESU aliposema “WATAFAKARINI/WAANGALIENI NDEGE, hawapandi wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao je! Ninyi si bora mara nyingi kupita hao?” (Mathayo 6:25, Luka 12:24)..
Bwana Yesu alimtumia kunguru kama mmojawapo wa ndege hao kutupa siri mojawapo ya ufalme wa mbinguni inayohusianishwa na kanuni za kuishi kwa watoto wa Mungu, namna Mungu anavyowahudumia watoto wake. Akatoa mfano wa kunguru ambao tunao kila siku katikati ya jamii yetu, tunawaona maisha yao ni kweli hawapandi wala hawavuni lakini wanakula na kunywa,hawana hazina lakini kesho yake ni lazima wale. Sasa Bwana akasema sisi ni bora mara nyingi zaidi kuliko hao.
Pia tazama..
Lakini tusiishie tu hapo, alisema Neno hili “WATAFAKARINI hao”, ikiwa na maana tusiwatafakari tu jinsi wanavyokula na wanavyokula, bali pia tuende zaidi ya hapo, tuwachunguze na jinsi wanavyoishi, wanavyozaliana wanavyojihudumia n.k ili tupate hekima nyingine ya ziada ndani yake…
Ni wazi kuwa kama Bwana angekuwa na muda wa kutosha angeendelea na kusema “watazameni kunguru jinsi wanavyoishi, hawali vyakula vizuri sana, lakini hawamezi vidonge wala hawana hospitali…” Je! Unahabari kuwa kunguru ni ndege anayeishi muda mrefu sana kuliko wanyama wengi mwituni na ndege wengi?.. Kunguru ni ndege anayekadiriwa kuishi zaidi ya miaka 80, hivyo wapo kunguru wenye umri mkubwa zaidi hata ya wa kwako na wanaishi mijini, lakini katika siku zote za maisha yao, hawajawahi kumeza kidonge wala kulazwa, japokuwa hawali vizuri kama wewe….
Sasa hapo ndio NENO LINAKUAMBIA JE! WEWE SI BORA KULIKO WAO?..kwa namna nyingine kama ukiamini kuwa Mungu anaweza kukufanyia zaidi ya wao, na kukujali zaidi ya wao unaweza kuishi maisha marefu pasipo kumeza vidonge, wala kwenda hospitali, wala pasipo kutazama sana ulaji bora kama ndio tiketi ya wewe kuishi muda mrefu..
Hapo tumetumia tu mfano wa kunguru, Lakini pale mwanzo Bwana alisema WATAZAMENI NDEGE.. Ikiwa na maana tutazame na jamii nyingine zote za ndege kwa jinsi tuwezavyo ili tupate hekima ya NENO LA MUNGU ndani ya maisha ya hivyo viumbe, kisha kwa IMANI tumwesabie Mungu anaweza kututendea sisi mara nyingi zaidi ya hao kwasababu yeye mwenyewe alishasema sisi ni bora mara nyingi zaidi ya hao.
Tukianza kuchambua ndege mmoja mmoja hatutamaliza, lakini unaweza kumtafakari hata kuku ukapata hekima ya NENO LA MUNGU ndani yake, unaweza ukamtazama, mbuni, tai, njiwa, bundi, popo, mashomoro, Yesu aliwatolea mfano katika
Luka 12:6-7 “Je! Mashomoro watano hawauzwi kwa senti mbili? Wala hasahauliwi hata mmojawapo mbele za Mungu. 7 Lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope basi bora ninyi kuliko mashomoro wengi”)
Luka 12:6-7 “Je! Mashomoro watano hawauzwi kwa senti mbili? Wala hasahauliwi hata mmojawapo mbele za Mungu.
7 Lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope basi bora ninyi kuliko mashomoro wengi”)
Kuna ndege wengine ukitafakari hekima Mungu alizoweka ndani yao utashangaa, wapo ndege ambao wao mara baada ya kutaga mayai yao, badala ya kuanza kuyaahatamia kama kuku au bata wafanyavyo, wao badala yake wanakwenda sehemu zenye milima ya volkano mahali palipo na joto Fulani, na kuyaacha mayai yao huko yapate lile joto, na baada ya muda Fulani kupita yale mayai yanajiangua vifaranga yenyewe kisha mama zao wanakuja kuchukua vifaranga vyao na kuondoka.. Neno la Mungu ni lile lile “Je! Ninyi si bora mara nyingi zaidi ya hao..? Inatufundisha nini hapo? kwamba zipo njia zilizozoelewa na watu wengi katika kufanikisha jambo Fulani, lakini ukimwamini tu Mungu kwamba anaouwezo wa kukufanyia na wewe kukutokezea njia Fulani pasipo kutumia nguvu nyingi kuzipata kama wengine…. Sasa hilo ni Neno la Mungu lililofichwa ambalo huwezi kulikuta moja kwa moja kwenye kitabu.
Alisema pia yatafakarini “MAUA YA KONDENI” hayafanyi kazi wala hayasokoti, nami nawaambia hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo ya hayo.Basi ikiwa Mungu huyavika majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?.
Tunayafahamu maua, hayajitaabikii kupata uzuri wake, jaribu kifikira zile harufu nzuri zinazotoka kwenye maua yale, je! Kuna mwanadamu yoyote anaweza kutoa harufu nzuri vile?. Lakini Mungu anatuonyesha nini? Anatuonyesha kwamba tukimwamini yeye, hata yale yaliyo mazuri zaidi ya hayo atatukirimia katika miili yetu ya udhaifu kwasababu sisi ni bora kuliko maua yote na miti yote kondeni.
Kadhalika mahali pengine Bwana Yesu alisema Ufalme wa mbinguni umefanana na “MFANYA BIASHARA” mwenye kutafuta lulu nzuri naye alipoiona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza alivyonavyo vyote akainunua (Mathayo 13:45-46)
Hapo tunamwona Bwana Yesu akitufunulia siri nyingine ya ufalme wa Mungu iliyopo katikati ya wafanya biashara, kwanamna nyingine ili tuweze kulielewa neno la Mungu kwa mapana tunaweza kuwatafakari wafanya biashara wengi tulionao katika maisha yetu ya kawaida, wapo wafanyabiashara wa madini (ambao kwa hapa ndio Bwana Yesu aliowatolea mfano), Kwa namna ya kawaida mfanyabiashara wa madini akiona dini lolote linauzwa mahali kwa bei ya chini, na dini hilo hilo linanunulika kwa bei kubwa sehemu nyingine, ikiwa fedha aliyonayo haimtoshi kulinunua lile jiwe, atafanya sio tu kwenda kuuza mali zake bali pia hata kukopa, ataenda kukopa popote pale ili afikishe kile kiwango cha fedha kwasababu anajua akishalipata atakwenda kuliuza kwa bei ya juu hata mara mbili ya ile aliyonunulia na hivyo kufidia gharama zake zote alizoingia pamoja na faida yake juu.
Vivyo hivyo na katika mambo ya ufalme wa mbinguni.. faida yake na thamani yake mtu akishaiona hapa duniani na katika ulimwengu unaokuja..mtu bila shuruti anajikuta anagharimika kutii maagizo yote ya kuupata, ataacha kila kitu, ataacha mambo ya dunia, fasheni, anasa, wizi, ulevi, usengenyaji,rushwa n.k. ili tu aupate kwasababu anajua faida yake ni kubwa sana mbeleni.
Na sio tu wafanyabiashara wa madini peke yake, huo ni mfano mmojawapo tu Bwana Yesu alitupa ili sisi tupate hekima ya kuwatazama na wengine tujifunze zaidi.. wapo wafanyabiashara wa mazao, mafuta, simu, nguo, n.k.wanaotuzunguka, Ambao kila mmoja ukimchunguza utaona SIRI ZA UFALME WA MBINGUNI zimejificha ndani yao..Hilo ndio Neno la Mungu ambalo huwezi kuliona kwa utimilifu wote kwenye kitabu cha biblia.
Kadhalika Bwana aliwaangalia wakulima, akatoa mfano wa Yule mpanzi aliyekwenda kupanda mbegu zake nyingine zikaangukia kwenye miiba, nyingine kwenye miamba n.k. Ikifundisha jinsi Neno la Mungu linavyopandwa ndani ya mioyo ya watu, na umeaji wake. Hapo ulikuwa ni ukulima wa kale wa kutupa mbegu lakini sasahivi tunao ukulima wa aina nyingi. Kwamfano tunaweza kuitafakari hekima ya ukulima wa sasa..
Kuna wakulima wawili wamenunua mashamba mawili kila mmoja hekari 1000, mmoja akasema nitatumia nguvu zangu kulima shamba langu la hekari 1000 kwa jembe la mkono mpaka liishe, na mwingine akasema hii kazi ni kubwa sana, hivyo nahitaji kutafuta kitu cha ziada kunirahisishia kazi, yeye akaamua ule muda wa asubuhi kuamka na kwenda kulima autumie karakana kubuni nyenzo mbadala itakayomrahisishia yeye kufanya kazi ile kubwa.
Hivyo ilimchukua kweli muda wa mamiezi ya utafiti hatimaye akagundua chombo kinachoitwa TREKTA kulimia..Na wakati mwenzake yupo katika heka ya 600 ambayo kailima kwa miezi kadhaa yeye ndio analeta kifaa chake shambani kianze kazi..Na kilipoanza kazi kwa muda mfupi tu labda wiki moja tu kilikuwa kimeshamaliza kulima hekari zote 1000, lakini yule mwingine alitumia nguvu nyingi mwilini pasipo akili.
Vivyo hivyo inatufundisha nini kwa wakati huu?, utendaji kazi shambani kwa Mungu kwa wakati huu sio sawa na ule wa zamani, ilimchukua Mtume Paulo miaka mingi ya kuzunguka sehemu kubwa ya dunia kupeleka injili kutokana na kwamba nyenzo zilikuwa hafifu.
Lakini kwasasahivi tukitumia njia hiyo tutapata matokeo madogo na kutugharimu muda mrefu, hatuwezi tukategemea sauti zetu tu na wakati kuna vipaza sauti, hatuwezi tukategemea usafiri wa farasi wakati vipo vyombo vya moto, vitakavyokufikisha kwa muda mfupi na haraka, na kufikisha ujumbe ule ule. Hivyo hili ni Neno la Mungu pia ambalo huwezi kulikuta kwenye kitabu cha biblia moja kwa moja japokuwa lipo.
Mahali pengine Bwana alialikwa karamuni, huko huko akauona ufalme wa mbinguni ndani yake. Akatumia hiyo hiyo karamu ya kidunia kufananisha na karamu ya mwanakondoo, alisema Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyeandaa karamu yake, akaalika watu waliostahili waje lakini wakakataa kuja kila mmoja akatoa udhuru, hivyo yule mtu akaaagiza waitwe viwete, vipofu na viziwi kufidia nafasi za wale waliokataa kuja, na mwisho Bwana akasema ufalme wa mbinguni upo hivyo hivyo “walio alikwa ni wengi lakini wateule ni wachache”…Kwa namna ile ile tunaweza kujifunza kwa harusi na karamu za wakati huu wa sasa na kupata hekima nyingi kupitia hizo…
Kwamfano katika harusi za sasahivi ambazo nyingi ni za kipagani, sio kama zamani ambapo mtu yeyote tu alikuwa anaweza kujichomeka kwenye harusi, hapana siku hizi hauingii pasipo kadi, na kadi yenyewe hupewi pasipo mchango.. na mchango wenyewe sio tu ilimradi mchango, hapana ni kiwango Fulani kimewekwa, hata kama umechangia lakini hujafikia hicho kiwango, haupewi kadi..Inafunua siri za ufalme wa mbinguni, mtoto yeyote wa Mungu anapaswa ajue hilo ni NENO LA MUNGU..
Katika karamu ya Mungu hawataingia watu ambao hawajaalikwa, na kualikwa tu haitoshi unapaswa uchangie kitu katika karamu hiyo ili upewe kadi ya mwaliko, na kuchangia huko maana yake ni kuchangia kitu katika injili, mfano kuhubiri habari njema kwa wengine, kuchangia kazi ya Mungu kwa mali zako kwa sadaka na zaka, n.k. Hivyo tusidhani kama kumkabidhi Bwana maisha yetu tu! inatosha, la! Kuna kufanya zaidi, ili tujiweke katika nafasi nzuri ya kuingia katika ile karamu ya mwanakondoo, ambayo itafanyika mbinguni mara baada ya unyakuo.
Kadhalika Bwana alipokwenda kuwachagua wengi wa mitume wake aliwakuta katika kazi ya uvuvi, huko huko akawafunulia SIRI za ufalme wa mbinguni zilizokuwa zimejificha katikati ya shughuli zao za kila siku akawaambia:
Mathayo 13:47 “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na JUYA, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna, 48 hata lilipojaa wakalivuta pwani, wakaketi wakakusanya walio wema vyomboni bali waliowabaya wakawatupa, ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; Malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki.”
Bwana Yesu alizungumza kwa mifano ya namna hiyo mingi na ndio maana akawaambia wanafunzi wake. NINYI MMEJALIWA KUZIFAHAMU SIRI ZA UFALME WA MBINGUNI, lakini wengine sivyo..Kwahiyo sisi wakristo tunapaswa tujifunze Neno la Mungu zaidi ya ule mwongozo tuliopewa. Na ndio hapo wengi wanakwama kwasababu wanategemea mwongozo kupata moja kwa moja majibu yao ya kila kitu…
Ndio hapo utakuta mtu anakuambia ni wapi kwenye biblia pameandikwa mtu asivute sigara, au asitoe mimba, au asitumie madawa ya kulevya, au asipake wanja, au asicheze kamari, asifanye mustarbation n.k….Hawafahamu kuwa biblia ilishazungumza juu ya hayo mambo lakini kwasababu hawajajaliwa kuzifahamu siri za ufalme wa mbinguni wanakuwa vipofu…
Lakini biblia ilishasema katika
Wagalatia 5:19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndio haya, uasherati, uchafu, ufisadi. 20 Ibada za sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitna, faraka, uzushi. 21 Husuda, ulevi, ulafi, NA MAMBO YANAYOFANANA NA HAYO,
Wagalatia 5:19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndio haya, uasherati, uchafu, ufisadi.
20 Ibada za sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitna, faraka, uzushi.
21 Husuda, ulevi, ulafi, NA MAMBO YANAYOFANANA NA HAYO,
katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Unaona hapo? Kitabu cha biblia kisingeweza kutaja mambo yote, na ndio maana ikafupisha kwa kusema NA MAMBO YANAYOFANANA NA HAYO…mambo yenyewe ndio hayo, uvutaji sigara, kamari, utoaji mimba, mustarbation, miziki ya kidunia, pornography, kupaka wanja kama Yezebeli, nk.
Hivyo ndugu, Neno la Mungu unalo hapo ulipo, ukisoma BIBLIA kwa kujifunza utaliona NENO LA MUNGU, lakini ukisoma Biblia kama kitabu tu, utaishia kujiona umefahamu kila habari iliyoandikwa na kuona hakuna jipya la kujifunza.
Bwana anasema UTAFUTENI KWANZA UFALME WAKE…Na yeye anasema ni mkuu kuliko Sulemani (yaani anayo hekima kuliko Sulemani) lakini Sulemani Biblia inamtaja aliitafuta tafuta hekima kwa bidii nyingi mpaka akaiona katikati ya wanyama wote, na miti yote.
1Wafalme 4: 32 Naye [Sulemani] akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano. 33 Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama na za ndege, na vitambaavyo, na samaki.
1Wafalme 4: 32 Naye [Sulemani] akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano.
33 Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama na za ndege, na vitambaavyo, na samaki.
Unaona hapo,? Unaweza kujenga picha sasa Mfalme Mkuu, Mungu wetu YESU KRISTO yeye ambaye ni mkuu zaidi ya Sulemani alitoa mifano mingapi ihusuyo ufalme wa mbinguni kwa kutazama tu mambo yanayotuzunguka?. Hakika Vitabu visingetosha kuandika kila kitu alichokifanya na kusema.
Alituachia tu mwongozo katika kitabu kile kidogo (biblia) vingine sisi kwa msaada wa Roho Mtakatifu tunapaswa tufahamu na kuelewa kwa msaada wa kile..Hivyo ndugu fahamu kuwa hizi ni nyakati za mwisho, Ni wakati wa kuutafuta ufalme wa mbinguni kwa bidii..Leo hii tunajua shule zinazofaulisha huwa zinazingatia vigezo Fulani, utagundua kuwa nyingi zinakuwa ni za Bweni, na zina sheria kali katika masomo na katika ustaarabu, wanafunzi hawaruhusiwi kujihusisha na jambo lolote nje ya masomo, kama vile mapenzi, kazi, n.k.
Utakuta shule inazingatia uvaaji wa sare, kuweka usawa wa wanafunzi wote, kadhalika na waalimu nao wanazingatia kutimiza wajibu wao kufundisha wanafunzi kulingana na muhamala na kuwafauatilia..Hivyo mwisho wa siku shule hiyo unakuta inaleta matokeo mazuri kwa wanafunzi, kuliko shule nyingine ambazo hazizingatii hivyo vigezo…
Vivyo hivyo katika ukristo, Kanisa linafananishwa na shule, mwanafunzi bora ni yule atakayechagua shule itakayomletea matokeo mazuri mwishoni, atakuwa tayari kujizuia na mambo mengine ili kusudi kwamba apate kilicho bora, Mkristo kama mwanafunzi wa Kristo na mshirika wa kanisa hatojali gharama za kuwa mwanafunzi wa Kristo, atakapoambiwa aache kila kitu cha kidunia, ajitenge na uovu hatauliza mara mbili kwasababu anajua faida ya kufanya hivyo huko mbeleni, atakapoambiwa avae mavazi ya kujisitiri hatachukia, atakapoambiwa aache kuabudu sanamu hatachukia, atakapoonywa juu ya dhambi zake hatokwazika, kwasababu anataka kupata cheti bora.
Bwana Yesu akubariki.
Tafadhali “share” kwa wengine ujumbe huu na Mungu atakubariki.
UTIMILIFU WA TORATI.
NJAA IPO?, USIACHE KULA ASALI.
UNAMFAHAMU MUNGU WA KWELI?
BWANA ALIKUWA NA MAANA GANI KUSEMA MATHAYO 5:39 “MTU AKUPIGAYE SHAVU LA KUUME, MGEUZIE NA LA PILI?
ZILE TUNU (DHAHABU, UVUMBA NA MANEMANE) MAMAJUSI WALIZOZITOA KWA BWANA (MATHAYO 2) . ZILIWAKILISHA NINI?
Wengi tunafahamu habari za Yusufu, tunajua alikuwa ni mmoja wa watoto wa Yakobo aliyependwa sana na baba yake, Lakini baada ya kuota zile ndoto tu, ndugu zake walianza kumwonea wivu, na mwisho wa siku wakaamua kumuuza kama mtumwa kwa watu wa mataifa (Wamisri).
Na kama tunavyoisoma habari alipokuwa kule Misri Mungu alikuwa pamoja naye akamfanikisha katika mambo yote, akawa wa pili baada ya Farao mfalme wa Misri, kiasi cha kwamba hakuna mtu yoyote aliyeweza kufika kwa Farao bila kupitia kwanza kwake, Mali na vitu vyote vya Misri Farao alivikabidhisha kwa Yusufu,[Kumbuka Misri ndiyo iliyokuwa ngome yenye nguvu kuliko zote duniani kwa wakati ule], tunaweza kusema mfano leo hii taifa la Marekani lilivyo.
Lakini habari hii ya maisha ya Yusufu na yote aliyoyapitia imebeba siri na ujumbe mzito katika roho kwa kanisa,. Yusufu anafananishwa na Bwana wetu Yesu Kristo, na Farao anafananishwa na Baba yetu wa mbinguni. Wale wana 11 wa Yakobo wanafananishwa na wayahudi [yaani waisraeli], na Taifa la Misri Yusufu alipokimbilia linafananishwa na Kanisa la mataifa [wakristo], na Yule mke wa Yusufu (Asenathi) ambaye alimpata katikati ya wa-Misri kutoka katika jumba la kifalme la Farao, anafananishwa na BIBI-ARUSI safi wa Kristo.
Kama vile Yusufu alivyoonewa wivu na ndugu zake na kukataliwa, kisha kwenda kuuzwa utumwani, vivyo hivyo Bwana Yesu alipokuja duniani kwa ndugu zake wayahudi kama masihi wao waliyekuwa wanamtazamia kwa siku nyingi, walimwonea wivu, alipojishuhudia kuwa yeye ndiye mwana wa Mungu, wakamdharau hivyo wakamfanyia hila, wakamkataa kabisa na kumtia mikononi mwa warumi na kumuua [Huko ndiko kumuuza kwa watu wa Mataifa].
Na ndio maana ukisoma biblia utaona mtume Paulo anawaambia hivi wayahudi;
Matendo 13:46 “ Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza [wayahudi]; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa. 47 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia. 48 Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini. 49 Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote”.
Matendo 13:46 “ Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza [wayahudi]; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa.
47 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.
48 Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.
49 Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote”.
Unaona hapo walimkataa Kristo, ambaye alikuja kwa ajili yao..Bwana hakuwahi kujidhihirisha kwa mataifa hapo kabla, ile neema ilikuwa ni kwa wayahudi tu ndugu zake waliokuwa wakimtazamia kwa muda mrefu, Na ndio maana alisema katika Mathayo 15:24 “…. Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.” lakini kwa kuwa wao walimwonea wivu kama vile wale watoto wengine wa Yakobo walivyomwonea wivu ndugu yao Yusufu, basi ile neema ikaondoka kwao na kuja kwetu sisi watu wa mataifa [ambao katika habari hii tunaweza kusema wamisri],
Lakini jambo lingine pia la kuliangalia ambalo limejificha katika maisha ya Yusufu alipokuwa Misri, ni kwamba utaona watu wengi wa Misri hawakuwa na imani sana na Yusufu, kama alivyokuwa nayo Farao kwa Yusufu. Na ndio maana utaona, wakati wa kile kipindi cha miaka 7 ya neema, ni Yusufu peke yake aliyekuwa akifanya bidii kutimiza yale maono aliyoyaona juu ya njaa itakayokuja kuikumba karibia dunia nzima.
Kama wale watu wa Misri wangekwenda sambamba na Yusufu baadaye utaona baada ya njaa kuanza kuipiga dunia wasingekuwa nao pia wanatangatanga kwenda kuomba na kununua chakula kwa Yusufu, kwa kuwa ni raia wa nchi yao, Yusufu asingewauzia chakula, wala kubadilishana nao chakula kwa mali na mashamba yao..angewapa bure, au kuwauzia kwa gharama ambayo isingelazimu mpaka kutoa mali zao na vitu vyao.
Inaonyesha wazi kabisa wale watu, hawakuyasadiki maono ya Yusufu kwa kiwango kikubwa pindi alipowaambia wakusanye hazina kwa wakati wa ukame unaokuja huko mbeleni. Ni mfano dhahiri wa wingi wa wakristo waliopo leo ambao ni kweli walimpokea Masihi (yaani Kristo) kama Mwokozi wao, lakini wameyapuuzia yale aliyowaambia yatakayokuja kuipata dunia huko mbeleni pindi itakapopitia miaka ya njaa na ukame wa rohoni na wa mwilini ( yaani wakati wa ile dhiki kuu).
Mtu pekee ambaye hakuathirika na ile dhiki ya njaa ilipokuja duniani kote ni MKE WA YUSUFU tu peke yake kwasababu yeye alikuwa katika JUMBA LA KIFALME..Akizipeleleza zile siri za ndani kabisa zilizokuwa katika moyo wa Yusufu..na kama ukichunguza vizuri utaona yule mke Yusufu hakumtwaa ovyo ovyo tu mahali popote hapana, bali alipewa na Farao mwenyewe.. Ni mfano halisi wa BIBI-ARUSI wa KRISTO, wateule wa Mungu, ambao ni Mungu pekee yake ndio anayempa KRISTO.
Kumbuka ndugu, katikati ya wanaojiita wakristo yapo makundi mawili, yupo BIBI-ARUSI wa Kristo yaani MKE wa Bwana Yesu, na wapo Masuria, hawa wanafananishwa na wanawali werevu na wanawali wapumbavu.(Mathayo 25). Katika siku za mwisho makundi yote mawili yatakuwepo, na litakalokwenda kwenye unyakuo ni lile tu la wanawali werevu yaani BIBI-ARUSI wa Kristo.
Sasa kama vile Yusufu alivyokuwa ni mkuu wa Wamisri wote (yaani watu wa mataifa), waliomwendea na kumwomba chakula wakati wa dhiki, ambapo kwa wakati huo mke wa Yusufu alikuwa anakula raha katika jumba la kifalme.
kadhalika na katika siku za taabu za ile dhiki kuu ya mwisho, wapo wakristo vuguvugu ambao wao wasingepaswa kupitia dhiki, lakini wataipitia kwa upumbavu wao, wakati wenzao (wale BIBI-ARUSI wa Kristo) wapo mbinguni kwa Baba kwenye enzi ya kifalme katika karamu ya mwana-kondoo.
Na kama vile dalili ya kipindi cha dhiki kuanza ni kuona ndugu zake Yusufu wanaanza kwenda kutafuta chakula Misri pamoja na wamisri wenyewe kuanza kutangatanga huku na kule kutafuta chakula, Vivyo hivyo Na katika kipindi hichi tunachoishi sasa, Njaa ya kulisikia Neno la kweli inaongezeka.
Wayahudi kwa miaka mingi wamekuwa wakimtazamia masihi wao aje kuwakomboa, lakini hawaoni chochote kwa kipindi chote hicho, lakini nyakati hizi kidogo kidogo, tunaona wanaanza kujua makosa yao, kwamba hakuna Masia mwingine atakayekuja, wanaanza kutambua kuwa kuna chakula Misri yaani kwa Wakristo, wanaanza kuona mbona Yule waliyemkataa ndiye amekuwa TEGEMEO LA DUNIA NZIMA?.
Ndugu yangu siku ile watakapotubu tu!, basi ujue kile kipindi cha DHIKI KUU kimeshaanza, na neema haitakuwepo tena kwa watu wa mataifa, kama ndugu zake Yusufu walivyomlilia ndivyo itakavyokuwa kwa wayahudi kwa wakati huo, waisraeli watafumbuliwa macho kikabisa kabisa na kumtambua Yesu Kristo, biblia inasema watamwombolezea yeye waliyemchoma…
Zekaria 12: 10 “Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza. 11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido”
Zekaria 12: 10 “Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido”
Sasa baada ya hapo itakuwa imebaki miaka michache tu mpaka ile miaka 7 ya mwisho iishe, na baada ya hiyo dunia itakuwa imeisha, wakati huo duniani kutakuwa na dhiki isiyokuwa ya kawaida, huo ndio wakati watu wote watakapojua kuwa YESU KRISTO NDIYE JIWE KUU LA PEMBENI LILE LILILOKATALIWA NA WAASHI, Watu wa ulimwengu wote watajua kuwa ufalme na mamlaka yote ya mbinguni na duniani amekabidhiwa YESU KRISTO, na Hakuna WOKOVU NA UZIMA nje ya yeye. Kama vile watu wa kipindi cha Yusufu walivyofahamu kuwa malmlaka yote na ufalme amekabidhiwa Yusufu.
Unaweza ukaona ni wakati gani tunaishi, Taifa la Israeli linazidi kunyanyuka, hivi karibuni waisraeli watafumbuliwa macho yao na kumtambua Yesu Kristo, je! Wewe ni miongoni mwa Bibi-arusi atakayeenda kwenye unyakuo siku ile kabla ya DHIKI KUU KUANZA? Unamchukulia Bwana Yesu Kristo kwako kama nani?, je! Unamchukulia kama ni mtu wa kawaida tu, au mfalme?, kumbuka Yusufu alivyokuwa gerezani sio sawa na alivyofanywa mfalme, na vivyo hivyo Bwana Yesu Kristo, alivyokuwa pale msalabani kalvari sio sawa na alivyo sasa, Biblia inasema ameketi katika NURU ISIYOWEZA KUKARIBIWA, na maneno yake ni kweli na uzima..
Hivyo kama hujaingizwa katika ile familia ya kifalme, hautaweza kuikwepa dhiki, kama hujazaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho, hautaweza kuuingia katika karamu ya mwana kondoo kule mbinguni, kwanini ukose hayo yote?? Jitahidi kufanya hivyo sasa kabla mlango haujafungwa. Tubu leo mgeukie Bwana azioshe dhambi zako, naye atakupa neema ya kuwa miongoni mwa Bibi-arusi wake. UNYAKUO NI SIKU YOYOTE.
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.
KARAMU YA MWANA-KONDOO.
KAENI NDANI YANGU NAMI NDANI YENU.
KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.
IJUE SIRI YA UTAUWA.
Mambo yote yaliyoandikwa katika agano la kale ni kivuli cha mambo yanayoendelea katika roho katika agano jipya tulilopo sasa. Kwamfano kama vile tunavyoweza kusoma Mungu alivyowaita wana wa Israeli kutoka Misri, kuelekea Kaanani kupitia jangwani, ndio hivyo hivyo Mungu anavyowaita watoto wake leo kutoka katika utumwa wa dhambi [Misri], kisha anawavusha katika bahari ya shamu [ambao ndio ubatizo 1Wakorintho 10], na baada ya hapo safari ya jangwani inaanza ambayo hiyo ni lazima kila mkristo aipitie, mahali ambapo atafundishwa kumcha Mungu, na kumtegemea yeye kwa kila kitu, mahali ambapo Mungu ataruhusu ajaribiwe kwa kila kitu lakini hataachwa. Na hatua ya mwisho ni Kuingia Kaanani, Ambayo nayo inaanzia hapa hapa duniani kisha kumalizikia kwenye nchi mpya na mbingu mpya..
Kadhalika tunajifunza pia jambo lingine katika habari ya Samsoni, ambayo nayo ni kivuli cha mambo yanayoendelea sasa hivi katika roho. Tunasoma Samsoni Mungu alimtia mafuta tangu alipokuwa tumboni mwa mama yake, akifananishwa na kanisa la Kristo jinsi lilivyoanza pale Pentekoste lilikuwa takatifu na safi lisilokuwa na waa lolote, Tunasoma pia Samsoni aliamuriwa na Mungu asikate nywele zake bali azifunge katika vishungi saba, Picha halisi ya kanisa la Kristo ambalo tunaona katika kitabu cha Ufunuo sura ya 2 &3 Bwana Yesu akitoa ujumbe kwa yale makanisa 7, Kumbuka kanisa la Kristo limekuwa likipita katika vipindi 7 tofauti tofauti vinavyojulikana kama NYAKATI 7 ZA KANISA kwa muda wa miaka 2000 sasa, na katika majira tunayoishi ni majira ya kanisa la mwisho la 7 linaloitwa LAODIKIA.
Kama vile Samsoni nguvu zake zilivyokuwa katika zile nywele, hivyo kanisa nalo katika nyakati zote saba limekuwa likitegemea nguvu zake katika NENO LA MUNGU ili likae. Lakini kwa habari mbaya tunasoma Samsoni alionyesha tabia za uasherati za kwenda kuzini na wanawake makahaba na wanawake wasio wa uzao wa Ibrahimu, na ndio hao baadaye waliokuja kujua siri ya nguvu zake, biblia inasema katika Mithali 31: 3 “Usiwape wanawake nguvu zako;”
Lakini Samsoni yeye hakufanya hivyo, badala yake alikubali kulaghaiwa na wale wanawake wasiomjua hata Mungu wa Israeli, wanawake wa kidunia, matokeo yake akaangukia katika mikono ya maadui zake wafilisti kwa muda mrefu, tunasoma;
Waamuzi 16: 15 “Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi. 16 Ikawa, kwa vile alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku, na kumwudhi, roho yake ikadhikika hata kufa. 17 Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu. 18 Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao. 19 Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka. 20 Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa Bwana amemwacha. 21 Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.
Waamuzi 16: 15 “Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi.
16 Ikawa, kwa vile alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku, na kumwudhi, roho yake ikadhikika hata kufa.
17 Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu.
18 Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao.
19 Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka.
20 Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa Bwana amemwacha.
21 Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.
Unaona hapo?. Ndio jambo hilo hilo lililikuta kanisa la Kristo mara baada ya mitume kuondoka, Paulo aliandika hivi…
Matendo 20: 29 “Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; 30 tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.”
Matendo 20: 29 “Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;
30 tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.”
Hivyo katika agano jipya Delila anafananishwa na kanisa kahaba na hili kanisa si lingine zaidi ya kanisa Katoliki, ambalo lilianza kwa kuanza kupenyesha mafundisho potofu ya uongo ndani ya kanisa la Mungu, na hatimaye kufanikiwa kutengeneza dini kabisa, mnamo mwaka 325 WK katika Baraza la Nikea, lilifanikiwa kuyachanganya mafundisho ya kikristo na ibada za kipagani za kirumi, huko ndiko kulikozuka ibada za miungu mingi, ibada za sanamu, kusali rozari, kuomba kwa watakatifu waliokufa kale, mafundisho ya kwenda toharani, kanisa kuongozwa na vyeo vya kibinadamu badala ya karama za Mungu, mambo ambayo hayapo katika maandiko wala hayakuonekana katika kanisa la kwanza.
Na kanisa hili lilipozidi kupata nguvu kwa kuwashawishi watu na kuwadanganya kidogo kidogo nguvu za Roho Mtakatifu zikaanza kupungua katika Kanisa, na hatimaye kupoa kabisa isipokuwa kwa kikundi kidogo sana cha wateule, na kupelekea kanisa kupitia katika kipindi kirefu cha giza kwa zaidi ya miaka 1000, ni kipindi kinachojulikana katika historia kama KIPINDI CHA GIZA.
Katika siku ile kwenye hilo baraza la Nikea ndio siku hiyo huyu mwanamke kahaba [Kanisa Katoliki] anayefananishwa na Delila alifanikiwa kuzinyoa nywele za kanisa la Mungu kabisa, hivyo nguvu za kanisa zilipoa kwa muda mrefu sana, kukawa hakuna tena karama za rohoni, biblia ikazuiliwa kusomwa kwa washirika, zile nguvu za watu kumwamini Kristo zilizoanza pale Pentekoste zikafa, watu waliojaribu kushikilia mafundisho ya mitume waliuliwa, mafundisho ya watu kuhesabiwa haki kwa Imani katika Yesu Kristo yakafa badala yake watu wakawa wanafundishwa kuhesabiwa haki kwa kuwa mshirika wa kanisa Katoliki, utozwaji wa pesa wa vitu vinavyoitwa vya ki-Mungu ukaanza, kwamfano mtu akitaka kuombewa ni lazima atoe kiwango Fulani cha fedha kwa kasisi ili ahudumiwe, mtu akitaka kuwekewa wakfu mtoto wake au mali zake mbele za Mungu, sharti kwanza atoe kitu Fulani, na asipofanya hivyo basi hatapata huduma yoyote, mambo ambayo hayakuwepo katika kanisa la kwanza..n.k.
Lakini kama tunavyosoma baada ya Samsoni kutumika muda mrefu kusaga ngano katika magereza ya Wafilisti tunaona nywele zake zilianza kuota tena pasipo wao kujua. Na zilipomalizika kuota, madhara aliyoyaleta mwisho yalikuwa ni makubwa kuliko yale aliyoyafanya kule mwanzoni kama tunavyosoma..
Waamuzi 16: 22 “Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake. 23 Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu. 24 Na hao watu walipomwona wakamhimidi mungu wao, maana walisema, Mungu wetu amemtia mikononi mwetu huyu adui wetu, aliyeiharibu nchi yetu na kuwaua watu wengi miongoni mwetu. 25 Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili. 26 Samsoni akamwambia yule kijana aliyemshika mkono, Niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia, nipate kuzitegemea. 27 Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu waume kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza. 28 Samsoni akamwita Bwana, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili. 29 Kisha Samsoni akazishika nguzo mbili za katikati ambazo nyumba ile ilikaa juu yake, akazitegemea, moja kwa mkono wake wa kuume na moja kwa mkono wake wa kushoto. 30 Samsoni akasema; Na nife pamoja na hawa Wafilisti. Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote waliokuwa ndani yake. BASI WALE WATU ALIOWAUA WAKATI WA KUFA KWAKE WALIKUWA WENGI KULIKO WALE ALIOWAUA WAKATI WA UHAI WAKE”.
Waamuzi 16: 22 “Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake.
23 Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu.
24 Na hao watu walipomwona wakamhimidi mungu wao, maana walisema, Mungu wetu amemtia mikononi mwetu huyu adui wetu, aliyeiharibu nchi yetu na kuwaua watu wengi miongoni mwetu.
25 Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili.
26 Samsoni akamwambia yule kijana aliyemshika mkono, Niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia, nipate kuzitegemea.
27 Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu waume kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza.
28 Samsoni akamwita Bwana, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.
29 Kisha Samsoni akazishika nguzo mbili za katikati ambazo nyumba ile ilikaa juu yake, akazitegemea, moja kwa mkono wake wa kuume na moja kwa mkono wake wa kushoto.
30 Samsoni akasema; Na nife pamoja na hawa Wafilisti. Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote waliokuwa ndani yake. BASI WALE WATU ALIOWAUA WAKATI WA KUFA KWAKE WALIKUWA WENGI KULIKO WALE ALIOWAUA WAKATI WA UHAI WAKE”.
Kadhalika na katika kanisa jambo ni lile lile ulipofika wakati nywele za Kanisa kuanza kuota tena, [na kuota kwenyewe ni kurudi kwenye NENO kwenye mafundisho ya mitume]..Ndipo hapo Bwana akaanza kuwanyanyua watu wa kulitengeneza kanisa akawanyanyua wakina Martin Luther, mjumbe wa kanisa la tano, katika karne ya 16 akifundisha mafundisho ya kuhesabiwa haki kwa Imani katika Kristo Yesu, na sio katika dini ya kikatoliki, Bwana akawanyanyua wakina John Wesley na wenzake, katika karne ya 18 wakifundisha utakaso wa damu ya Yesu, kwamba Kristo amekuja ili umfanye mtu kuwa mtakatifu kwamba pasipo huo hakuna mtu atakayemwona Mungu, (Waebrania 12:14) na sio kwamba pasipo ushirika wa kanisa watu hawatamwona Mungu…
Vile vile katika kipindi cha kanisa la mwisho la Laodikia ambalo lilianza mwanzoni mwa karne ya 20 mpaka sasa, Bwana aliwanyanyua wakina William Seymor na wengine katika uamsho wa mtaa wa Azusa kule Marekani , na mafundisho ya Ubatizo wa Roho Mtakatifu, ya kwamba Roho Mtakatifu ndio MUHURI WA MUNGU (Waefeso 4:30). Na wote wasiokuwa na Roho wa Mungu hao sio wake (Warumi 8:9), Na ndio maana inajulikana kuwa tunaishi katika nyakati ya KI-Pentekoste kama ilivyokuwa kule mwanzo, na ndio maana katika nyakati hii zile karama zilizokuwa zimeuliwa na Kanisa Katoliki Bwana alianza kuzirejesha tena kuanzia mwanzoni mwa karne ya 20..(Yaani kuanzia mwaka 1900 na kuendelea)
Lakini haya yote ni kwa ajili ya kumwandaa BIBI-ARUSI wa kweli wa KRISTO kwa ajili ya unyakuo uliokuwa karibu kutokea. Zile nywele zimeshafikia ukomo, ni jambo moja tu linasubiriwa, Uamsho wa mwisho wa BIBI-ARUSI kupitia ufunuo wa zile ngurumo 7 kama tunavyosoma katika ufunuo 10:14, Ambazo hizo zitampa Bibi-arusi imani timilifu (Luka 18:8) ya kwenda katika unyakuo, ni uamsho wa kipekee, nao utakuwa ni wa muda mfupi sana utakaokuwa wa nguvu na wa ajabu kuliko hata ule uamsho wa kwanza uliotokea kule Pentekoste kama vile Samsoni baada ya nywele zake kukua tena, maangamizi aliyoyaletea mwishoni yalikuwa ni makubwa kuliko hata yale ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa Bibi-arusi wa Kristo katika hichi kipindi cha kukaribia na unyakuo.
Na wewe je! Ni miongoni mwa watu ambao nywele zao zimekuwa?? Au bado tu unatumikia katika dini na madhehebu? Kumbuka kuota nywele maana yake ni kurudi katika Neno, nguvu za mkristo yoyote Yule hazipo nje ya Neno la Mungu..Biblia inasema usiabudu sanamu, wala usijifanyie sanamu ya kuchonga, lakini kanisa lako linasema ni sawa kufanya hivyo..hapo unapaswa ufuate kile Neno linasema na uweke chini kile kanisa linasema.
Biblia inasema aaminiye na kubatizwa ataokoka, [na maana ya kubatizwa ni kuzamishwa kwenye maji mengi], lakini kanisa linasema haijalishi, linasema ubatizo wa kunyunyiziwa ni sawa..Hapo unapaswa uweke chini mapokeo ya kanisa na kuchukue kile mitume walichokifanya kwenye biblia…
Matendo 2: 37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”
Matendo 2: 37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”
Hivyo ndugu hizi ni siku za mwisho, huu ni wakati wa kuhakikisha nywele zako zinakuwa, tafuta uhusiano wako binafsi na Mungu, Rudi kwenye Neno la Mungu, dini na madhehebu hayatakufikisha popote, kumbuka watakaokwenda kwenye unyakuo ni wachache biblia inasema hivyo..Je! umezaliwa mara ya pili? Kwa kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu.?Mungu akubariki.
UTENDAJI KAZI WA MPINGA-KRISTO.
SIKU YA HASIRA YA BWANA.
SIRI YA MUNGU.
MKUU WA GIZA
NI HALALI KUBATIZA WATOTO WADOGO?
KUNA HUKUMU ZA AINA NGAPI?
1Wafalme 19: 9 Akafika kunako pango, akalala ndani yake. Na tazama Neno la BWANA likamjia, naye akamwambia, UNAFANYA NINI HAPA ELIYA?. 10 Akasema nimeona wivu mwingi kwa ajili ya BWANA Mungu wa majeshi ; Kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu, waiondoe. 11 Akasema, toka, usimame mlimani mbele za BWANA. Na tazama BWANA akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunjavunja miamba mbele za BWANA; Lakini BWANA hakuwamo katika upepo ule; Na baada ya upepo tetemeko la nchi; lakini BWANA hakuwamo katika lile tetemeko la nchi; 12 Na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; Lakini BWANA hakuwamo katika moto ule; Na baada ya moto sauti ndogo ya utulivu. 13 Ikawa Eliya alipoisikia, alijifunika uso wake katika mavazi yake, akatoka, akasimama mlangoni mwa pango. Na tazama sauti ikamjia, Kusema, UNAFANYA NINI HAPA, ELIYA ?.
1Wafalme 19: 9 Akafika kunako pango, akalala ndani yake. Na tazama Neno la BWANA likamjia, naye akamwambia, UNAFANYA NINI HAPA ELIYA?.
10 Akasema nimeona wivu mwingi kwa ajili ya BWANA Mungu wa majeshi ; Kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu, waiondoe.
11 Akasema, toka, usimame mlimani mbele za BWANA. Na tazama BWANA akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunjavunja miamba mbele za BWANA; Lakini BWANA hakuwamo katika upepo ule; Na baada ya upepo tetemeko la nchi; lakini BWANA hakuwamo katika lile tetemeko la nchi;
12 Na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; Lakini BWANA hakuwamo katika moto ule; Na baada ya moto sauti ndogo ya utulivu.
13 Ikawa Eliya alipoisikia, alijifunika uso wake katika mavazi yake, akatoka, akasimama mlangoni mwa pango. Na tazama sauti ikamjia, Kusema, UNAFANYA NINI HAPA, ELIYA ?.
Tukirudi nyuma kidogo katika habari hii, tunasoma kabla ya Eliya kukimbilia mlima Horebu alienda kuwaua wale manabii wa Baali , baada ya kuona Israeli yote imekengeuka kwa kuigeukia miungu migeni, lakini pamoja na kuwaua hao, akapata taarifa nyingine kuwa malkia, [mke wa mfalme Ahabu aliyeitwa Yezebeli] anataka kumwangamiza yeye naye kama alivyowaua manabii wa baali, Kumbuka Yezebeli alikuwa ni mkatili sana alifanikiwa kuwaangamiza manabii wengi wa Mungu waliokuwa Israeli kwa wakati ule, na baadhi yao waliosalia walikuwa wanaishi kwa kujifichaficha mapangoni siku zote za maisha yao.
Hivyo njia pekee Eliya aliyoiona ya kupata suluhisho la mambo yote ni kukimbilia katika mlima wa Mungu uliokuwa mbali sana na Israeli, [Ni ule ule mlima ambao Mungu alisema na wana wa Israeli hapo kwanza] akae huko ajitete mbele za Mungu. Na ndio ule ule Mlima Mungu aliomwitia Nabii Musa ampe yale maagizo na sheria kwa wana wa Israeli kwamba wayashike siku zote za maisha yao, Sasa mlima huo ulikuwa ukijulikana kama mlima mtakatifu wa Mungu kwa wakati ule, ndio unaoitwa mlima Sinai au mlima Horebu.
Hivyo Eliya kwa kufikiria kwake aliona ni vema amwendee Mungu, kama Musa alivyomwendea, kwa kufuata kanuni zile zile,..Na ndio maana tunaona Eliya alifunga siku 40 usiku na mchana bila kula wala kunywa chochote, jambo ambalo Musa alilifanya. Akijua kuwa kule Mungu atazungumza naye kama alivyozungumza na Musa, pengine ataitikisa dunia tena na kuikomboa Israeli kwa Ishara na mapigo makubwa kutoka kwa ile miungu ya kipagani [ma-baali] aliyoacha Israeli kama kipindi kile Bwana alivyofanya kule Misri..Alifika mpaka kilele cha mlima Sinai na kukaa kule, katika pango mojawapo, akingoja Bwana azungumze naye. Na ni kweli tunasoma Bwana alishuka na kuzungumza naye kama alivyozungumza na Musa.
Ndipo sauti ya Mungu isiyoambatana na chochote ikasema naye na kumuuliza, ELIYA UNAFANYA NINI HAPA?. Lakini Eliya hakuielewa kwasababu matarajio yake hayakuwa hayo!!, yeye alitazamia Mungu atazungumza naye kwa moto, na tufani na upepo wa kisulisuli kama alivyofanya kwa Musa mtumishi wake na kwa wana wa Israeli zamani zile kwenye mlima huo huo.. Lakini baada ya kitambo kidogo Bwana akamwambia Eliya toka usimame nje! Utazame uone,…
Ndipo Mungu akapita kwa UPEPO mwingi sana uliopasua miamba, na MATETEMEKO, na MOTO kama Eliya alivyotazamia, kwa mfano ule ule aliojidhihirisha kwa wana wa Israeli na kwa Musa..Lakini pamoja na ishara zote hizo na maajabu yote yale Eliya alipata ufahamu na kugundua kuwa kuna kitu hakipo sawa kwenye hizo ishara zote kadhalika na kwenye ule mlima …
Na ndipo Mungu akazungumza naye tena kwa mara ya pili kwa sauti ya utulivu na kumuuliza.. ELIYA UNAFANYA NINI HAPA?, Hapo ndipo alipogundua ile ilikuwa ni sauti ya Mungu inayosema naye, hivyo kwa aibu na kwa hofu akijifunika uso wake jambo ambalo hapo mwanzo hakufanya iliposema naye kwa maneno hayo hayo!!.. Alipogundua kuwa Mungu hayupo katika mlima Sinai uwakao moto, Mungu hayupo katika matetemeko, Mungu hayupo katika upepo wa kisulisuli na tufani, Mungu hayupo katika nguzo ya moto, Mungu hayupo katika Wingu, Mungu hayupo katikati ya kijiti kinachowaka moto, Mungu hayupo katika mvua ya mawe..Alitambua kuwa Mungu yupo katika SAUTI NDOGO YA UTULIVU, Kwamba hata ishara zile wana wa Israeli Mungu alizokuwa anawaonyesha kule jangwani hazikuwa uthibitisho wa kuwa Mungu alikuwa katikati yao, Mungu alizutumia zile kama ishara tu, ili wamwamini atakapotaka kuzungumza nao wamsikie.. Eliya aliligundua hilo. Zile SHERIA Mungu alizompa Musa ndio iliyokuwa SAUTI NDOGO YA UTULIVU iliyokuwa inasema mioyoni mwao, > usiabudu miungu mingine, waheshimu baba yako na mama yako, usiue, usiibe, n.k..
Hivyo mtu yeyote ambaye angezitii zile sheria hata asingeona ishara yoyote ile, Mungu angekuwa katikati yake, angekuwa ameisikia sauti ndogo ya Mungu ya utulivu..Lakini wengi wao waliona upepo, na matetemeko, na moto, na bahari kugawanyika, na miamba kutoa maji, lakini hawakuitambua sauti ya Mungu iliyokuwa inazungumza nao katikati yao, walidhani kuwa ile zile ishara ndio utimilifu wa wote wa Mungu, mwisho wa siku wengi wakaangamia jangwani.
Kadhalika na katika wakati wetu huu wa agano jipya Kanisa lilipoanza tunasoma katika ile siku ya Pentekoste [Ambao ndio mlima Sinai wetu], Mungu alishusha vipawa na ishara nyingi katikati ya wateule wake, Bwana alishuka na UPEPO wa KISULISULI kama ulivyowashukia wana wa Israeli kule jangwani na Eliya, Soma;
Matendo 2: 1 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. 2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa UPEPO wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama NDIMI ZA MOTO uliowakalia kila mmoja wao. 4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.
Matendo 2: 1 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.
2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa UPEPO wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.
3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama NDIMI ZA MOTO uliowakalia kila mmoja wao.
4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.
Unaona hapo? siku ile ya Pentekoste, Moto ulishuka kama ndimi za moto ukakaa juu ya watu, karama tofauti tofauti zikaanza kujionyesha katikati ya watu, wakaanza kunena kwa Lugha mpya, watu wakaanza kutabiri, miujiza na ishara zisizokuwa za kawaida zikafanyika katikati ya watakatifu, nchi ikatikiswa kwa matetemeko ya nguvu za Roho wa Mungu (Soma Matendo 4:23-31)…Lakini Mungu hakuwepo katikati ya hivyo vitu vyote, Mungu aliviruhusu viwepo kama ishara tu ya watu kuwa tayari kumsikia ni kati gani anataka kusema katikati yao.
Hivyo lile kundi dogo lililokuwa limekusudiwa kumwona Mungu baada ya zile ishara, na maajabu liliisikia ile sauti ndogo ya utulivu na ndio maana tunaona katika ile siku tu ya kwanza ya Pentekoste watu walipokuwa wanazistaajabia zile ishara kuona watu wanashukiwa na ndimi za moto, na kuzungumza katika lugha nyingine mbali mbali ndipo wale watu wakamwambia Petro na mitume wengine, sasa tutendeje ndugu zetu?…Ndipo Petro akawajibu,
Matendo 2: 37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia TUBUNI, MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU.
Matendo 2: 37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia TUBUNI, MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU.
Unaona hapo, wale watu hawakumwambia Petro moto huu ni wa ajabu, upepo huu ni wa kipekee,Hakika Mungu kaonekana, Mungu kajifunua, Mungu ni mwema, leo katutembelea haleluya hapana.! Bali wao moja kwa moja walimuuliza Petro na mitume wenzake, TUTENDEJE NDUGU ZETU?.. Na ndipo ile sauti ndogo ya Mungu ya utulivu ikawaambia “TUBUNI” maana yake ni Geukeni mwache njia zenu mbaya .. Kama tu vile ile sauti ndogo ya utulivu ilivyomwambia Eliya kule mlima, UNAFANYA NINI HAPA ELIYA? “RUDI” KATIKA NJIA YA JANGWA, [maana ya kurudi ni kugeuka urudi ulikotoka].
Lakini katika hichi kipindi cha siku za mwisho, kile ambacho Bwana Yesu alisema katika
Mathayo 7:22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?. 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.” …Kimeshindwa kuisikia sauti ya Mungu inayonena katika utulivu badala yake kimeng’ang’ana na yale madhihirisho ya Roho kwamba ndio uthibitisho kuwa Mungu yupo katikati yao.
Mathayo 7:22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?.
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.” …Kimeshindwa kuisikia sauti ya Mungu inayonena katika utulivu badala yake kimeng’ang’ana na yale madhihirisho ya Roho kwamba ndio uthibitisho kuwa Mungu yupo katikati yao.
Ndugu yangu, ikiwa leo hii utadhani Mungu yupo katika karama yoyote uliyonayo, ukidhani kuwa kunena kwa lugha ndio uthibitisho kwamba umepokea kweli ubatizo wa Roho Mtakatifu, au kufanya miujiza, au kutoa pepo, ndio uthibitisho kwamba Mungu yupo na wewe, huku umeiweka kando ile sauti ya Mungu inayozungumza na wewe kwa utulivu na upole inayokuambia UACHE DHAMBI, NA UTUBU, UKABATIZWE KATIKA UBATIZO SAHIHI, wa jina la YESU KRISTO, Hutaki kuisikia, basi fahamu kuwa utakuwa umepotea bila hata wewe mwenyewe kujijua.
Kama Leo hii hutaka kusikia Neno la Mungu, habari za TOBA na UTAKATIFU kwako hazina maana sana, wewe unachokifuata kanisani ni Upepo wa kisulisuli, na matetemeko na hisia za kiroho pamoja na moto wa Roho Mtakatifu na miujiza na uponyaji, ni kweli hivyo vinapaswa viwepo kanisani, na ni lazima kanisa liambatane navyo, lakini ile sauti ya Mungu iliyosema na Eliya hapo mwanzo bado itaendelea kusema na wewe ndani yako siku zote, UNAFANYA NINI HAPA? UNAFANYA NINI KATIKA DHAMBI??
Ni kitu gani unachokwenda kukitafuta katika nyumba ya Mungu, ni miujiza tu,? ni ishara? Ni uponyaji? Ni kufunguliwa biashara yako?, ni kuombewa upate mtoto?, ni Kufunguliwa upate mume/mke?, ni kuombewa tu ufaulu shuleni?.
Ndugu kama ni mojawapo ya hayo ndio yanayokupeleka huko ukidhani kuwa Mungu kukufanikisha katika hivyo ndio uthibitisho kwamba yupo na wewe, basi hujaisikia bado sauti ya Mungu, yeye alisema wazi kabisa,“mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme wa mbinguni Yohana 3:3” na kuzaliwa mara ya pili ni KUTUBU (KUGEUKA) kwa kumaanisha kuacha maisha uliyokuwa unaishi ya kale, ya ulevi, uasherati, usengenyaji, ushirikina, kutokusamehe, ya chuki, ya wivu, ya ugomvi, ya utukanaji,maisha ya anasa, maisha ya uvaaji vimini, na suruali, maisha ya upakaji wanja na lipstiki na uvaaji mawigi na hereni, maisha ya ibada za sanamu na uvuguvugu.
Na baada ya kugeuka, hatua inayofuata ni kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo, ili hatia ya dhambi zako iondolewe mbele za Mungu na kisha Bwana mwenyewe atakupa uwezo wa kushinda dhambi kwa kupitia Roho wake Mtakatifu katika wakati uliobakia wa maisha yako.
Ndugu sauti ndogo leo ya utulivu inazungumza nawe kupitia maandiko kwamba hakuna mtu atakayemwona Mungu asipokuwa na huo UTAKATIFU, (waebrania 12:14.). Isikie sauti ya Mungu sasa inayosema katika kanisa lake na sio ishara, miujiza, maono, ndoto, uponyaji, n.k…Ukivifuata hivyo kanisani, bado ile sauti itakuuliza FULANI UNAFANYA NINI HAPA?..mimi sipo huko, nipo katika sauti ndogo ya utulivu..
Na kama ni ya utulivu basi ni rahisi kuidharau. Ni maombi yangu ndugu yangu sisi sote tusiiache itupite, Bwana atupe masikio ya kuisikia inaposema nasi katika Neno lake na sio katika miujiza. Hizi ni siku za mwisho tuwe macho.
Mungu akubariki.
HATA ILIPOTIMIA SIKU YA PENTEKOSTE.
NJAA ILIYOPO SASA.
MSTARI HUU UNAMAANA GANI? ″WALAKINI HAUTAPOTEA HATA UNYWELE MMOJA WA VICHWA VYENU? (LUKA21:18).
NITAAMINI VIPI KAMA KUNA MBINGU AU KUZIMU?
Ni rahisi kudhania kuwa mtu akizaliwa mara ya pili, basi anakuwa anampenda sana Mungu kiasi kwamba kukitokea kitu mfano shida, au tabu,au magonjwa, au dhiki na kadhalika anakuwa yupo tayari kupambana nacho ili asimwache Mungu wake au asimkane Kristo,..yaani kwa jinsi anavyompenda Bwana hataweza kuruhusu tabu zimtenge na yeye kama tunavyosoma ilivyoandikwa katika maandiko haya;
Warumi 8: 31 “Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? 32 Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye? 33 Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. 34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea. 35 NI NANI ATAKAYETUTENGA NA UPENDO WA KRISTO? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? 36 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. 37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. 38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote HAKITAWEZA KUTUTENGA NA UPENDO WA MUNGU ULIO KATIKA KRISTO YESU BWANA WETU.”
Warumi 8: 31 “Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?
32 Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?
33 Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.
34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
35 NI NANI ATAKAYETUTENGA NA UPENDO WA KRISTO? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
36 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.
37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,
39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote HAKITAWEZA KUTUTENGA NA UPENDO WA MUNGU ULIO KATIKA KRISTO YESU BWANA WETU.”
Je! Ni kweli hiyo ndiyo maana halisi ya hiyo mistari hapo juu kwamba sisi tunao uwezo wa kupambana na dhiki, tabu, na mateso kwasababu ya upendo wetu mwingi kwa Kristo?. Jibu ni hapana, hakuna mwanadamu yeyote mwenye upendo wa kiwango hicho, ni muhimu kufahamu maana ya huo mstari hapo juu, Biblia inasema JE! NI NANI ATAKAYETUTENGA NA UPENDO WA KRISTO?..Unaona hapo, inasema ni UPENDO WA KRISTO na sio UPENDO WETU SISI KWA KRISTO.
Kuna tofuati kati ya upendo wetu sisi kwa Kristo, na upendo wa Kristo kwetu sisi.
Mtu anapozaliwa mara ya pili kweli kweli [Tutakuja kuona huko mbeleni mtu anazaliwaje mara ya pili], Kuanzia huo wakati na kuendelea ule Upendo wa Kristo unaingia ndani yake, huo sio upendo wake[huyo mtu] kwa Kristo, hapana! bali Upendo wa Kristo kwake. Hivyo Bwana Yesu ndiye anayekuwa anachukua jukumu lote la kuhakikisha ule upendo wake kwako unadumu milele haupotei kwa namna yoyote ile.
Hivyo kuanzia huo wakati linapotokea jambo lolote juu yako mfano iwe ni dhiki, shida, njaa, hatari, adha, upanga n.k. Ni Yesu Kristo ndiye anayehakikisha wewe haujitengi na yeye, na sio wewe utakayehakikisha kwamba hujitengi na yeye. Watu wanaojaribu kufanya hivyo, kwa kujizuia kwa akili zao kutokujitenga na Kristo hawafiki mbali, wanajikuta wanaanguka na watu wa namna hiyo huwa bado hajazaliwa mara ya pili.
Mtume Paulo anasema, …
“38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote HAKITAWEZA KUTUTENGA NA UPENDO WA MUNGU ULIO KATIKA KRISTO YESU BWANA WETU.”
“38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,
Hii ni faida kubwa sana kwa mtu aliyezaliwa kweli kweli mara ya pili, Unakuwa UMETEKWA na UPENDO WA YESU KRISTO mwenyewe, ndio hapo unakuta dhiki inapomjia mtu wa namna hiyo kwamfano, shetani anapomjaribu kwa misiba, badala ya yeye kufarijiwa yeye ndio anawafariji wengine, anapokuwa katika magonjwa ya kufisha, badala amkufuru Mungu yeye ndiye anaonekana mwenye tumaini kushinda hata mtu aliye na mzima, kama vile Ayubu, utashangaa mtu wa namna hiyo anapita katika hali ya kupungukiwa kupita kiasi na njaa lakini bado anafuraha na kumshukuru Mungu, mpaka watu wa nje wanamshangaa ni mtu wa namna gani, yupo katika hali kama hizi lakini bado anashikamana na Mungu wake,
Kadhalika utakuta mtu mwingine [tunawazungumzia waliozaliwa kweli kweli mara ya pili] ni tajiri, lakini hauangalii na kuutumainia utajiri wake kama ni kitu cha thamani sana katika maisha yake, mpaka watu wengine wa nje wanamshangaa wanasema tungekuwa na mali kama za kwako dunia nzima ingetujua, tungetembelea magari ya thamani, tungetia heshima, lakini mtu kama Ayubu pamoja na utajiri wake alisema maneno haya,
Ayubu 31: 25 “Kama nilifurahi kwa kuwa mali yangu yalikuwa mengi, Na kwa sababu mkono wangu umepata vitu vingi; …. 28 Hilo nalo lingekuwa uovu wa kuadhibiwa na waamuzi; Kwani ningemwambia uongo Mungu aliye juu. “
Ayubu 31: 25 “Kama nilifurahi kwa kuwa mali yangu yalikuwa mengi, Na kwa sababu mkono wangu umepata vitu vingi; ….
28 Hilo nalo lingekuwa uovu wa kuadhibiwa na waamuzi; Kwani ningemwambia uongo Mungu aliye juu. “
Unaona sasa uwezo wa namna hiyo, wa kuweza kuendana nayo na kushinda mambo yote hayo pasipo kumwacha Mungu, sio kwa jitihada za mtu binafsi kupambana na hizo hali, hilo haliwezekani kwa mtu yeyote Yule, hiyo ni YESU KRISTO mwenyewe ndio anafanya ndani ya mtu ili kuhakikisha kwamba hakupotezi wewe kipenzi chake, haungamii, hivyo tatizo linapokuja, kabla ya kukufikia wewe, linawasili kwanza kwake, kisha analipatia utatuzi, ndipo litakaposhuka kwako, na litakaposhuka linakuja na dawa madhubuti ya kulishinda, Uwezo wa kipekee unatoka kwa Mungu, na nguvu ya kushinda majaribu na mitikisiko yote..
Ndio hapo watu wa nje watakushangaa unawezaje kushinda hayo yote?, unawezaje kukaa katikati ya jamii ya wazinzi na wewe sio mmojawao?, unawezaje kuwa katika hali ya kutokuwa na pesa lakini bado unamtumikia Mungu, na unayo amani?, Unawezaje kuwa mgonjwa lakini unawaombea wengine, na hauna hofu ya kufa? Unawezaje kuwa na mali na usitamani anasa za ulimwengu huu, wala kiburi, unawezaje kuwa mzuri na bado huvai mavazi yasiyo na heshima n.k…Hawajui kwamba hayo yote hayatokani na upendo wako wewe kwa Mungu..hapana bali yanatokana na UPENDO wa KRISTO kwako .. Yeye ndiye anayefanya juu chini, wewe usipotee katika hizo njia mbovu na majaribu..kama biblia inavyosema:
Zaburi 125: 1 “Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele. 2 Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, NDIVYO BWANA ANAVYOWAZUNGUKA WATU WAKE , TANGU SASA NA HATA MILELE. “
Zaburi 125: 1 “Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.
2 Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, NDIVYO BWANA ANAVYOWAZUNGUKA WATU WAKE , TANGU SASA NA HATA MILELE. “
Sasa karama hii ya UPENDO WA MUNGU KWA MTU, haiji kwa watu wote wa ulimwenguni hapana! Bali inakujua kwa wale tu waliomtumainia yeye {yaani wale tu WALIOZALIWA MARA YA PILI}, wengine ambao hawajazaliwa mara ya pili hawataweza kushinda majaribu na misukosuko, yatakapotokea mawimbi wataanguka tu, zitakapotokea dhiki watakufuru, ikitokea misiba watalaani, hawana raha usiku na mchana, watajitahidi kwa nguvu zao kushinda dhambi na ulimwengu lakini hawataweza, hata wakipata utajiri utawaangamiza, hata wakiwa wagonjwa na maskini watataka kujaribu kuishikilia imani lakini watamkana Kristo, kwasababu hawajazaliwa mara ya pili.
Sasa Kuzaliwa mara ya pili kunakuja kwanza baada ya mtu kutubu dhambi zake, [kumbuka maana ya kutubu ni KUGEUKA], sio kuongozwa sala ya toba, unageuka kwa kudhamiria na kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako, kuyaacha ya kale na kuanza maisha mapya kwa Kristo, na baada ya kutubu, bila kukawia hatua inayofuata ni kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji tele, na kwa JINA LA YESU KRISTO, (kulingana na Matendo 2:38), upate ondoleo la dhambi zako, na hatua ya tatu na ya mwisho ni Roho wa Kristo kuingia ndani yako, sasa hapo ndio lile PENDO LA KRISTO linamiminwa ndani yako. Mtu yeyote akiruka hatua yoyote kati ya hizo, bado hajazaliwa mara ya pili..Kumbuka ndugu hii sio dini wala dhehebu ni maagizo ya Bwana Yesu mwenyewe ambayo yapo kwenye biblia.
Biblia inasema wazi kabisa, katika Yohana 3: 5 “Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.”
Sasa kumbuka kuzaliwa kwa maji kunakozungumziwa hapo ndio UBATIZO WA MAJI, na kuzaliwa kwa Roho ndio UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU. Hapo ndipo unakuwa umeshazaliwa mara ya pili. Lakini Wapo wengine wanataka kubatizwa lakini hawajadhamiria kuacha maisha yao ya kale ya dhambi, hao hata wakienda kubatizwa wanafanya kazi bure, hakuna chochote kitakachotokea katika maisha yao.. Kadhalika wapo wengine, wametubu lakini hawataki kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wanasema ubatizo wa maji hauna maana sana hawa nao pia hawataona mabadiliko yoyote katika maisha yao.. Maagizo yote aliyoyatoa Bwana Yesu hakuna hata moja lisilokuwa na maana, alisema aaminiye na kubatizwa atakoka, na sio aaminiye tu peke yake. Hapana bali vyote viwili vinakwenda pamoja.
Hivyo mtu akizingatia hizo hatua zote za yeye kuzaliwa mara ya pili utapokea UWEZO, wa kutokutenganishwa na chochote kile, iwe shida, dhiki, uzima, mauti, raha, malaika, mamlaka, utajiri, kupungukiwa, upanga, misiba, n.k. kwasababu lile PENDO LA YESU KRISTO tayari litakuwa limeshamiminwa ndani yake. Hivyo ANASHINDA siku zote na ZAIDI YA KUSHINDA.
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine na Mungu atakubariki.
UPENDO
NINI MAANA YA USIPUNGUZE WALA KUONGEZA NENO LA MUNGU?
JE! NI DHAMBI KUSHEREKEA SIKU YA KUZALIWA? BIRTHDAY!
JE! NI HALALI KWA MTU WA MUNGU KUTUMIA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO?
Zekaria 14: 6 “Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba nuru yake haitakuwa na mwangaza na kiwi; 7 lakini itakuwa siku moja, iliyojulikana na Bwana; si mchana, wala si usiku; lakini itakuwa, ya kwamba wakati wa jioni kutakuwako nuru”.
Zekaria 14: 6 “Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba nuru yake haitakuwa na mwangaza na kiwi;
7 lakini itakuwa siku moja, iliyojulikana na Bwana; si mchana, wala si usiku; lakini itakuwa, ya kwamba wakati wa jioni kutakuwako nuru”.
Jaribu kutengeneza picha mfano Inatokea siku moja, wakati wa jioni labda tuseme saa moja hivi muda ambao umezoea kila siku kuona jua likizama ghafla unashangaa kuona mwanga ni ule ule haufifii, tena inafikia saa mbili jioni jambo ni lile lile, kunamulika mwangaza kama wa saa 11 jioni hivi, ni wazi kuwa kwa namna ya kawaida utashangaa sana hiyo siku kimetokea nini?, mbona giza haliingii maana muda wa usiku umeshaanza na sasa ni saa 2 usiku lakini kunaonekana kama saa 11, kwa namna ya kawaida mtu yeyote atakayeliona jambo hilo atashtuka sana.
Kadhalika na katika roho pia Bwana alitabiri itakuja siku moja inayofanana na hiyo, kwamba wakati wa jioni kutakuwa na NURU. Lakini kwa hekima hatuna budi tufahamu huo wakati ni wakati gani, je! Umeshatimia au bado?. Hivyo ili kufahamu ni lazima pia tujue Nuru ni nini na giza ni nini? Na huo wakati wa jioni ni upi?.
Kama tunavyojua nuru ya dunia inaletwa na jua, na hili jua huwa linaangaza katika majira matatu yaani asubuhi, mchana na jioni,..Kadhalika na katika roho Bwana Yesu alisema:
Yohana 8: 12 “…, MIMI NDIMI NURU YA ULIMWENGU, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima”.
Unaona hapo yeye katika roho ndio jua letu lililoanza kuangaza asubuhi, na likaja kuangaza mchana, kadhalika na litaangaza jioni. Kazi yake ni kutia nuru ulimwengu, alianza kutia nuru asubuhi (yaani kanisa la kwanza lilioanza na mitume), akaendelea kutia nuru mchana(yaani katika wakati way ale makanisa 5 yaliyofuata), na akamaliza kuangaza Nuru yake wakati wa jioni (katika kanisa lile mwisho la 7 linaloitwa Laodikia ambalo ndilo hili tunaloishi sasa ). Ufunuo 2 & 3
Na kanisa hili la Laodikia ni wazi kabisa na inajulikana na watu wote kwamba lilianza katika karne ya ishirini, yaani kuanzia mwaka 1906 na kuendelea.. Hivyo sisi wote tuliopo leo tunaishi katika ile NURU ya BWANA ya jioni, kumbuka hakutakuwa na kanisa lingine zaidi ya hili, ni kanisa ambalo litashuhudia kuja kwa pili kwa Kristo. Ilijulikana Katikati ya wakristo wote kuanzia huo wakati wa mwanzoni mwa karne ya karne ya 20 kwamba wao ni WANA WA JIONI, kwasababu walikuwa wanafahamu kabisa ni kweli wanaishi wakati wa jioni kabisa wa nuru ya Kristo kumalizikia.
Sasa katikati mwa karne ya ishirini yaani kipindi cha miaka ya 1940-1980, wakristo wote kutokana na matukio yaliyokuwa yanayaona yakitokea duniani, wakilinganisha na unabii wa kibiblia, walifahamu kuwa karne ile haitaisha bila Kristo kurudi mara ya pili, na ni kweli walikuwa sahihi, ukizingatia kwamba asilimia kubwa wa yale Bwana Yesu aliyoyazungumza katika Mathayo 24 yalitimia katika huo wakati, kwamfano, Bwana alisema.
Kutakuwa na matetemeko ya nchi mahali na mahali, kwa wakati ule yalikuwa ni mengi mno duniani, alisema pia kutakuwa na vita na matetesi ya vita, taifa litaondoka kwenda kupigana na taifa lingine…Jambo ambalo lilionekana wazi katikati ya ile karne ya 20, vita viwili vikubwa vya dunia vilitokea kwa mpigo, jambo ambalo halikuwahi kuonekana hapo kabla katika historia ya dunia, mamilioni ya watu kufa, magonjwa ya ajabu ndio yalianzia kuzuka katika hicho kipindi, kansa, ukimwi, kisukari, Malaria n.k. mambo ambayo Bwana aliyatabiri yatatokea katika siku za mwisho, na kikubwa zaidi kilichowafanya watakatifu wa karne ya ishirini kunyanyua vichwa vyao juu, kama Bwana alivyowaambia katika
Luka 21:28 “Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia”
Ni kutokea kwa kitendo cha kihistoria katika nchi takatifu Israeli, pale waliposhuhudia taifa la Israeli likichipuka tena baada ya ma-karne ya miaka kupita bila kuwa taifa huru, walishuhudia kuona Israeli kupata uhuru wao tena mwaka 1948 na kuwaona wayahudi wakitoka katikati ya mataifa yote ulimwenguni na kurudi katika nchi yao tena.
Ezekieli 36: 24 “Maana nitawatwaa kati ya mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. “
Huko ndiko kuchipuka kwa mtini Bwana Yesu alikokuzungumzia,Maana Taifa la Israeli linafananishwa na MTINI kadhalika pia watakatifu walipokuwa wanaona na miti mingine ikichipuka (yaani mataifa mengine tofauti na Israeli kupata uhuru wao yaani mataifa ya Afrika, Asia na Marekani ya kusini),ambayo hayo yote yalianza kupata uhuru wao mara baada tu ya Israeli kutangazwa kuwa taifa huru, wakilinganisha na maandiko Bwana Yesu aliyoyasema katika..
Luka 21:29 “Akawaambia mfano; Utazameni MTINI na MITI MINGINE YOTE. 30 Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu. 31 Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu. 32 Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie. ”
Luka 21:29 “Akawaambia mfano; Utazameni MTINI na MITI MINGINE YOTE.
30 Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu.
31 Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu.
32 Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie. ”
Hivyo walivyokuwa wanayaona hayo yote yanatimia, walitambua kabisa kwamba karne ya 21 haitafika (yaani miaka ya 2000 haitakuwepo), na walikuwa wapo sahihi kabisa, Sasa kilichotokea na cha kustaajabisha, ni kuona mpaka karne ya 21 inaanza na mwisho bado haujafika…
Na ndio hapo tunarudi kwenye lile andiko letu la msingi..
Zekaria 14: 6 “Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba nuru yake haitakuwa na mwangaza na kiwi; 7 LAKINI ITAKUWA SIKU MOJA, ILIYOJULIKANA NA BWANA; si mchana, wala si usiku; lakini itakuwa, YA KWAMBA WAKATI WA JIONI KUTAKUWA NURU”.
7 LAKINI ITAKUWA SIKU MOJA, ILIYOJULIKANA NA BWANA; si mchana, wala si usiku; lakini itakuwa, YA KWAMBA WAKATI WA JIONI KUTAKUWA NURU”.
Huo wakati ambao Bwana alisema JIONI KUTAKUWA NA NURU, ndio huu tunaoishi sasa (wakati huu wa karne ya 21), Mambo yote yalipaswa yaishe tokea karne ya 20, lakini kwa jinsi Mungu alivyokuwa wa rehema na neema, hataki mtu yeyote apotee bali wote waifikilie toba, akalazimika kuisimamisha NURU ya ulimwengu isizame ( yaani Neema ya Yesu Kristo isiishe) katika hichi kipindi cha wakati wa jioni wa kumalizia..
Ndugu yangu mwisho ungepaswa uwe umeshafika siku nyingi, moja ya hizi siku mambo yote yatabadilika ghafla, kama vile jua linavyokaribia kuzama kidogo kidogo giza linaingia..ndivyo walivyoweza kutambua watu wa karne ya 20, lakini sisi tunaoishi katika Hii NURU ya nyiongeza (watu wa karne ya 21), tupo katika hatari kubwa sana kwasababu Nuru hii haitadumu kwa kipindi kirefu, kadhalika na haitabiriki, siku ya kuondoka kwake haitakuwa taratibu taratibu tena kama mwanzo, hapana, bali itaondoka kwa ghafla, na saa hiyo hiyo giza nene sana litaikumbuka dunia (huo ndio uharibifu wake)…
Ndio lile neno litatimia
1Wathesalonike 5: 1 “Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. 2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku. 3 WAKATI WASEMAPO, KUNA AMANI, NA SALAMA, NDIPO UHARIBIFU UWAJIAPO KWA GHAFULA, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. “
1Wathesalonike 5: 1 “Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.
2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
3 WAKATI WASEMAPO, KUNA AMANI, NA SALAMA, NDIPO UHARIBIFU UWAJIAPO KWA GHAFULA, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. “
Watu wengi wametokea badala ya kumkaribia Mungu awape neema ndio kwanza wanaanza kudhihaki, wakisema hakuna kitu kama hicho kurudi kwa Yesu, Yesu harudi leo wala kesho, miaka na miaka mambo yapo vilevile hawajui kwamba wanaishi katika muda wa nyiongeza wa ILE NURU YA JIONI.. ili watubu..
1Petro 3: 1 “Wapenzi, waraka huu ndio wa pili niwaandikiao ninyi; katika zote mbili naziamsha nia zenu safi kwa kuwakumbusha, 2 mpate kuyakumbuka yale maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana na Mwokozi iliyoletwa na mitume wenu. 3 Mkijua kwanza neno hili ya kwamba KATIKA SIKU ZA MWISHO WATAKUJA NA DHIHAKA ZAO WATU WENYE KUDHIHAKI, WAFUATAO TAMAA ZAO WENYEWE, 4 na kusema, IKO WAPI AHADI ILE YA KUJA KWAKE? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa. 5 Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu; 6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia. 7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu. 8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. 9 BWANA HAKAWII KUITIMIZA AHADI YAKE, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, MAANA HAPENDI MTU YE YOTE APOTEE, BALI WOTE WAFIKILIE TOBA. 10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. 11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, 12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? “
1Petro 3: 1 “Wapenzi, waraka huu ndio wa pili niwaandikiao ninyi; katika zote mbili naziamsha nia zenu safi kwa kuwakumbusha,
2 mpate kuyakumbuka yale maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana na Mwokozi iliyoletwa na mitume wenu.
3 Mkijua kwanza neno hili ya kwamba KATIKA SIKU ZA MWISHO WATAKUJA NA DHIHAKA ZAO WATU WENYE KUDHIHAKI, WAFUATAO TAMAA ZAO WENYEWE,
4 na kusema, IKO WAPI AHADI ILE YA KUJA KWAKE? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.
5 Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu;
6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.
7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.
8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.
9 BWANA HAKAWII KUITIMIZA AHADI YAKE, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, MAANA HAPENDI MTU YE YOTE APOTEE, BALI WOTE WAFIKILIE TOBA.
10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,
12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? “
Unaona ndugu,..tunaishi wakati wa muda wa nyongeza muda wa ile siku iliyojulikana na Bwana, wakati wa jioni, wakati wa NURU YA NEEMA. Je! Bado unaishi katika dhambi? Bado hujazaliwa mara ya pili? Utajitetea vipi siku ile pamoja na huu muda wa nyongeza uliopewa katika hili giza lililopo duniani, utatoa udhuru gani mbele ya hukumu. Kumbuka baada ya hii nuru kuondoka, (ambayo itaisha na UNYAKUO), kutakuwa kumebakia miaka saba tu mpaka dunia kuisha, huko ndiko ile dhiki kuu ya mpinga-kristo pamoja yale mapigo yote yaliyoandikwa katika kitabu cha ufunuo 8 & 16 yatatimia, kisha baada ya hapo itakuja hukumu na kisha ziwa la moto.
Kama hujatubu kwa kumaanisha kuziacha dhambi zako, fanya hivyo leo, ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji tele na kwa jina la YESU KRISTO upate ondoleo la dhambi zako (kulingana na Matendo 2:38), na Bwana atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu..
Bwana akubariki.
ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.
JE! NYWELE ZAKO ZINAOTA AU ZIMESIMAMA?
UNAFANYA NINI HAPO?
UMETEKWA NA UPENDO WA KRISTO?
KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE? NA TENA WANA WA ISRAEL WALIMFUKIZIA UVUMBA MALKIA WA MBINGUNI, NDIO YUPI HUYO?
Mambo ya asili yanafunua mambo ya rohoni, Bwana Yesu alituambia “wana wa ulimwengu huu katika kizazi chao wenyewe huwa na busara kuliko wana wa nuru. (Luka 16:8)”..Neno hili linatuhusu sisi tulio wakristo, Embu tujifunze mojawapo ya busara walionayo wana wa ulimwengu huu, Mtume Paulo alisema katika
“1Wakorintho 9: 24 Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate…”
Kama tunavyosoma katika andiko hilo tunaona jinsi Mtume Paulo alivyoweza kuwatazama wakimbiaji wa kidunia akapata hekima, kadhalika na sisi tujifunze ili tupate hekima mbele za Mungu wetu aliye mbinguni. Kama ulishawatazama wakimbiaji wanaoshiriki katika michezo ya mbio ndefu au fupi, utafahamu kuwa wao huwa hawashiriki tu watu wote ovyo ovyo, yaani tukiwa na maana kuwachanganya watoto, na wazee pamoja na wanawake na wanaume humo humo katika riadha moja, hapana, waligundua wakifanya hivyo basi kutakuwa hakuna usawa wowote na mwisho wa siku katika ugawaji wa tuzo, litapatikana kundi moja la kipekee litakalokomba tuzo hizo zote,(hivyo michezo haitakuwa na maana yoyote) Lakini ili kuweka mambo yote sawa, walifanikiwa kutenganisha mbio hizo kulingana na uwezo wa watu, umri wa watu, pamoja na jinsia za watu.
Kwamfano kama ukitazama wanaoshiriki katika mbio zile fupi tuseme labda zile za mita 100, utakuta zimetengwa mbio za wanaume kivyao na wanaweka kivyao, hawachanganywi kwasababu uwezo unatofautiana kulingana na jinsia, kwamfano kama wanawake watakaoshiriki wapo 10, na wanaume 10, tuseme wakimbie pamoja basi utakuta nafasi zote 10 za kwanza zitachukuliwa na wanaume wote, na kuanzia nafasi ya 11 ndipo mwanamke wa kwanza ataanza kutokea..Hivyo mwisho wa siku inatokea kuwa hatapatikana mwanamke atakaye pokea tuzo yoyote pamoja na taabu zake zote..
Sasa kwa kwa kulitatua hilo, wakatofautisha makundi mawili, wanaume kwa wanaume, na wanawake kwa wanawake,.. Mwanaume atakayemaliza wa mwisho, kwa sekunde tuseme 11, na mwanamke aliyeingia wa kwanza kwa sekunde 12..Yule mwanamke wa kwanza aliyeshinda katikati ya wanawake wenzake, unakuta anapokea tuzo sawa na yule mwanaume aliyeingia wa kwanza kule akiwa na sekunde 8 katika mashindano ya wanaume wenzake. Wote watapokea medali moja (labda tuseme ya dhahabu), kadhalika na wa pili na wa tatu hivyo hivyo kwa pande zote medali zao zitafanana..Ingawa kiuhalisia inaweza kuonekana kuwa wale wanaume wengine waliokosa medali wangestahili kupewa zile tuzo za wale wanawake , kwasababu wao walikimbia ndani ya muda mchache kuliko wao, lakini haiko hivyo katika utoaji wa medali (tuzo). Utoaji unategemea na kundi unaloshiriki. Kadhalika mbio za walemavu, na watoto haziwezi zikawa sana na mbio za watu wazima, lakini medali ya atakayeshinda katikati ya walemavu itakuwa na thamani sawa na medali za wale wazima.
Kadhalika na katika mbio za kikristo, wote tunashiriki mchezo mmoja, wote tunashindana katika mbio, lakini Mungu aliziweka hizo mbio katika makundi tofauti tofauti. Watoto kivyao, wanaume kivyao pamoja na wanawake kivyao. Lakini kwa kila kundi thamani ya tuzo kwa watakaoshinda hazitofautiani.. Lakini Bwana alisema kwetu sisi wana wa Nuru hatuna hekima katika mashindano yetu haya duniani..Wote tunataka tujichanganye tukimbie katika kundi moja wote, wanaume hukohuko, wanawake huko huko, watoto huko huko n.k. Ndugu kwa Mungu hakupo hivyo, Mungu alitoa majukumu katika kanisa, Majukumu ya wanaume na majukumu ya wanawake, na majukumu yanayopaswa yafanywe na wote.
Biblia inaposema katika 1Timotheo 2: 8 “Basi, nataka WANAUME WASALISHE KILA MAHALI, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano”, Haikukosea, Kama inavyotupa mwongozo, mahali popote panapohusiana na kuongoza ibada ikiwemo uongozaji wa maombi, kusalisha, kuelekeza, vyote hivyo vinapaswa katika kanisa vifanywe na wanaume tu. Kwasababu jukumu hili limewekwa katika upande wa mbio za wanaume.
Kadhalika biblia ilisema pia..1Timotheo 2: 11 “MWANAMKE NA AJIFUNZE KATIKA UTULIVU, , akitii kwa kila namna. 12 SIMPI MWANAMKE RUHUSA YA KUFUNDISHA, WALA KUMTAWALA MWANAMUME, bali awe katika utulivu. 13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye”.
Kadhalika biblia ilisema pia..1Timotheo 2: 11 “MWANAMKE NA AJIFUNZE KATIKA UTULIVU, , akitii kwa kila namna.
12 SIMPI MWANAMKE RUHUSA YA KUFUNDISHA, WALA KUMTAWALA MWANAMUME, bali awe katika utulivu.
13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye”.
Unaona? Hili ni agizo la pili la Bwana kwa kanisa, kwamba kazi ya kufundisha, mfano uchungaji, ualimu, uaskofu na ushemasi, haupaswi ufanywe na mwanamke. Na Mungu alishatoa sababu ya kufanya hivyo hapo juu, Hivyo ikiwa mwanamke ataona kama hapewi haki yake na kutaka kwenda kuwa mchungaji au mwalimu ni sawasawa na ameingia katika mbio ambazo sio za jinsia yake, Hivyo matokeo yake mtu kama huyo, ataonyesha kweli nguvu nyingi na jitihada nyingi, lakini hatapokea tuzo yoyote katika siku ile,..Siku ile atasema Bwana mimi nilikuwa mchungaji wa kimataifa kanisani, nilifanya hivi nilifanya vile, lakini Bwana siku ile atamwambia hukupiga mbio mahali panapokupasa. Unaona hapo angepaswa akawe mchungaji, au mwalimu kwa wanawake wenzake, akawe muhubiri kwa wanawake wenzake, lakini sio kanisani penye mchanganyiko wa wanaume na wanawake.
1Wakoritho 14: 34 “Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. 35 Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa. 36 Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu? 37 Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana. 38 Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga”.
1Wakoritho 14: 34 “Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.
35 Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.
36 Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?
37 Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana.
38 Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga”.
LAKINI MBIO ZA WANAWAKE NI ZIPI?
Biblia ilisema tena pale pale kwenye..
1Timotheo 2: 9; “Vivyo hivyo wanawake na WAJIPAMBE KWA MAVAZI YA KUJISITIRI, PAMOJA na ADABU NZURI, na MOYO WA KIASI; SI KWA KUSUKA NYWELE, wala KWA DHAHABU na LULU, wala KWA NGUO ZA THAMANI; 10 bali kwa MATENDO MEMA , kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu. 11 Mwanamke na AJIFUNZE KATIKA UTULIVU, akitii kwa kila namna.”
1Timotheo 2: 9; “Vivyo hivyo wanawake na WAJIPAMBE KWA MAVAZI YA KUJISITIRI, PAMOJA na ADABU NZURI, na MOYO WA KIASI; SI KWA KUSUKA NYWELE, wala KWA DHAHABU na LULU, wala KWA NGUO ZA THAMANI;
10 bali kwa MATENDO MEMA , kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
11 Mwanamke na AJIFUNZE KATIKA UTULIVU, akitii kwa kila namna.”
Mwanamke akidumu katika hali ya utulivu, pamoja na adabu, pamoja na kiasi,(Ikiwa na maana awe mwenye nidhamu pia hasengenyi watu,) pamoja na kujisitiri mwili wake kwa kutokuvaa mavazi yanayoonyesha maungo yake, kwa kutokuvaa suruali kama wanaume, kutokuvaa vimini, haweki wigi, wala lipstick midomoni mwake, wala hereni, anadumu katika utakatifu wote, basi Huyo atakuwa katika mashindano miongoni mwa wanawake wenzake (akina Sara, Rebeka, Hana, n.k.) , na siku ile atapokea tuzo yenye thamani kubwa kuliko hata mwanaume ambaye ni mchungaji au muhubiri au mwalimu ambaye hajatumika katika uaminifu wote katika nafasi yake..Atakwenda kuketi pamoja na Kristo katika kiti chake cha Enzi katika siku ile.
Kuna muhubiri mmoja maarufu wa kimarekani anaitwa Rick Jonyer, anaeleza: siku moja alichukuliwa katika maono na Bwana Yesu juu mbinguni katika ulimwengu wa Roho, alipofika kule alianza kutembezwa katikati ya viti vya enzi, na alipokuwa anapita katikati ya baadhi ya hivyo viti vya enzi aligundua kitu, kwamba mbona viti vingi vinakaliwa na wanawake pamoja na watoto? Ndipo akamwambia Bwana inaelekea huku wanawake na watoto ndio wamechukua nafasi kubwa..Anasema alishangazwa sana kuona wale aliokuwa anadhani wangekuwa wana nafasi kubwa kule, kuona ni wadogo sana.
Unaona hapo Dada katika Kristo?, unaweza ukadhani ukidumu katika nafasi yako kama mwanamke hautapata chochote, hapana! Kinyume chake utapata vyote, Thawabu za Bwana zinapimwa kulingana na umri, jinsia na maumbile…talanta uliyopewa kulingana na jinsia yako itumie hiyo vizuri bila kuingilia mbio za jinsia nyingine, tumia talanta ulizopewa katika uaminifu wote ni mfano tu wa mwalimu aliyetoa jaribio kwa wanafunzi wake wawili, mmoja akampa mtihani wa maswali 10 marefu, mwingine akampa mtihani wa maswali 100 mafupi, Yule aliyepewa maswali kumi akapata 9 kati ya yale kumi na kukosa moja, hivyo akahesabiwa kuwa kapata asilimia 90 kati ya mia (yaani 90%). Lakini Yule aliyepewa maswali mia mafupi akapata hapo maswali 50 na maswali mengine 50 yaliyosalia akakosa hivyo akahesabika kapata asilimia 50 kati ya mia (yaani 50% ).
Hivyo mwalimu wakati wa kugawa tuzo akampa tuzo(zawadi) kubwa Yule wa kwanza aliyefanya maswali kumi na kupata hapo tisa,(asilimia 90% ) kuliko Yule pili aliyefanya maswali 100 mengi na kupata hapo asilimia 50% tu. Na ndivyo Baba wa mbinguni atakavyotoa Tuzo siku ile. Mwanamke Yule ambaye atajitunza katika utulivu wote, na kiasi na kujisitiri, na upole na uvumilivu, na utakatifu, na adabu atafananishwa na Yule mwanafunzi aliyepewa maswali 10 nakupata hapo 9, kuliko mwanaume aliyepewa maswali mia na kupata hapo 50.
Dada kabla ya kujifunza kwa Musa, hebu jifunze kwanza kwa Miriamu dada yake Musa alivyokuwa, kabla hujajifunza kwa Eliya nenda kwanza kajifunze kwa Yezebeli Yule mwanamke aliyempinga Eliya, kabla hujajifunza kwa Petro hebu kajifunze kwanza kwa Miriamu na Martha na Mariam Magdalena, na Susana (luka 8:1-3), wanawake walioshuhudiwa kumuhudimia Kristo kwa kila hali, kabla ya kujifunza kwa Paulo hebu kajifunze kwanza kwa Tabitha na mwanamke Lidia aliyewakaribisha wakina Paulo walipokosa mahali pa kukaa (Matendo 16:13-15).
Hivyo nakupa moyo dada, ambaye umeanza safari yako hii ya kumtii Kristo, na kubaki katika nafasi yako Mungu aliyokuweka, zidi kuwa mtakatifu na kujisitiri na kuwa kielelezo kwa wanawake wengine kwasababu kiti cha enzi mbinguni kinakuongojea.
Hivyo yapo pia majukumu tulikabidhiwa wote, nayo ni kuwa “mashahidi wa Kristo”. Kila mmoja wetu [awe mwanamke au mwanaume] anapaswa popote pale alipo awe kielelezo cha kuwavuta watu wengine katika ufalme wa mbinguni (kwa mienendo na matendo)..Biblia inasema katika
1Petro 3: 15 Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. 16 Nanyi mwe na dhamiri njema,…
1Petro 3: 15 Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.
16 Nanyi mwe na dhamiri njema,…
WITO WA MUNGU
CHAPA YA MNYAMA
TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
KWANINI MTUME PAULO HAKUMSAMEHE MARKO?
BIBLIA INASEMA ASKOFU ANAPASWA AWE MUME WA MKE MMOJA! JE! WALE WASIOOA KWA AJILI YA INJILI HAWAWEZI KUWA MAASKOFU?