Title 2018

MAMBO YATAKAYOTOKEA ISRAELI SIKU ZA HIVI KARIBUNI.

Ishara kubwa Bwana Yesu aliyowapa wanafunzi wake ambayo kwa hiyo waliambiwa watakapoiona basi wajue kuwa “muda wa mavuno umekaribia” ni ishara ya MTINI. tukisoma Mathayo 24:32 inasema “Basi KWA MTINI JIFUNZENI mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu;

24.33 nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.

Na tunajua kuwa “mtini” alioumaanisha hapo si mwingine zaidi, zaidi ya TAIFA LA ISRAELI (Yeremia 24), Ikiwa na maana kuwa tutakapoona taifa la Israeli linaanza kuchipua na kuchanua tena, basi majira ya mwisho wa dunia yamekaribia sana. Kumbuka Mungu katika mpango wake wa wokovu alianza na Israeli na katika kutimiliza atatimiliza na taifa hilo hilo, kwasababu makao ya MFALME YESU atakapokuja kwa mara ya pili kuutawala huu ulimwengu mzima katika nchi ya wenye haki, hayatakuwa katika mojawapo ya nchi hizi za mataifa tulizopo sisi na zitakazokuwepo huko hapana, bali makao yake yake makuu yatakuwa pale Israeli nchi takatifu. Alishuka hapo mara ya kwanza, atashuka hapo hapo mara ya pili. Hivyo ni lazima kwanza pale patakaswe kisha mataifa mengine yafuate kabla ya yeye kuteremka ulimwenguni.

Hivyo Mungu akishamaliza kupatakasa Israeli, ndipo atakapoitumia Israeli kuitakasa dunia nzima kwa fimbo yake. Na ndio maana Mungu alisema hivi juu ya Israeli. 

Yeremia 51:20 “ WEWE U RUNGU LANGU NA SILAHA ZANGU ZA VITA; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;

21 na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake;

22 na kwa wewe nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na kwa wewe nitawavunja-vunja kijana mwanamume na kijana mwanamke;

23 na kwa wewe nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng’ombe; na kwa wewe nitawavunja-vunja maliwali na maakida.”

Unaona?. Sasa kulingana na unabii wa kibiblia katika hatua tuliyopo sasa tunatazamia kushuhudia VITA KUU MBILI KUBWA zitakazopiganwa pale Israeli kabla ya mambo yote kuisha. Vita ya kwanza ni ile inayozungumziwa katika Ezekieli 38-39, ambayo ndio itakayofuata muda mfupi ujao Na vita ya pili ni ile ya HAR-MAGEDONI (Ufunuo 16:16), hiyo itakayokuja kuhitimisha utawala mbovu wa huu ulimwengu, unajulikana kama vita ya Mungu mwenyezi.

VITA YA ULIYOZUNGUMZIWA KATIKA EZEKIELI 38-39.

Siku zote Mungu kabla hajafanya jambo kubwa litakaloleta madhara huwa anatanguliza kwanza madogo madogo ili kuwakumbusha watu wachukue tahadhara kwani makubwa zaidi ya hayo yanakuja mbeleni. Na ndio maana Bwana Yesu alisema, kutakuwa na vita, na tetesi za vita, kutakuwa na njaa na matetemeko ya ardhi, hayo yote ni MWANZO WA UTUNGU, Unaona Hapo utungu wenyewe bado haujafika. Ukifika inamaanisha maafa yatakuwa makubwa zaidi kuliko haya tuyaonayo. Na ukitazama kwa ukaribu haya matetemeko ya ardhi tunayoyaona ulimwenguni na kusema ni makubwa, yanayoangamiza maelfu haya yote si kitu, Yapo matetemeko hasa yatakayokuja siku ile ya mwisho hii dunia itakapotikiswa pale visiwa na milima vitakapohama kwa nguvu ya tetemeko la ardhi ambalo Mungu atalileta mwenyewe duniani kote, na mvua ya mawe makubwa sana ambayo haijawahi kunyesha tangu ulimwengu kuumbwa, hapo ndipo wanadamu wote waliosalia wakati huo watalia na kuomba milima iwaangukie wajisitiri mbali na hasira ya Mungu. Ni mambo ya kutisha sana.

Ufunuo 6.12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,

13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.

14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.

15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,

16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.

17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”

Vivyo hivyo na kwenye suala la magonjwa na vita. Magonjwa yaliyopo leo yanatabika na homa zake ni za wastani, kadhalika na yanapatikana maeneo Fulani Fulani tu sio kila mahali haya yote ni mwanzo wa utungu,lakini yale yatakayoletwa na Mungu katika siku ile ya ghadhabu ya hasira yake, biblia inasema kutakuwa na jipu baya na bovu juu ya watu wote ulimwenguni walioipokea ile chapa ya mnyama. Jaribu kufikiri ukimwi na kansa, au ebola ni magonjwa yanayoogopeka, Lakini biblia haijayaona hayo, mpaka kulizungumzia hili jipu bovu tu lenyewe…ni baya kiasi gani mpaka wanadamu watamtukana Mungu kwa maumivu ya ugonjwa huo. Sio kutamani kuwepo huko ndugu.

Sasa tukirudi kwenye suala la vita. Leo Tunaweza kushuhudia vita ya kwanza na vya pili vya dunia vilivyoua watu zaidi ya watu milioni 80, huo ni mwanzo tu wa utungu, na lakini ipo vita itakayopiganwa siku za mwisho ambayo ndio ile ya mwisho inayojulikana kama HAR-MAGEDONI. Watu watakaouawa ni idadi kubwa mito ya damu itabubujika Israeli kwa wingi wa watu watakaouawa.

Sasa tuitazame Israeli kama jinsi ilivyofananishwa na mtini kuchipuka kwake, ambako kulikuwa ni mwaka 1948.

Tunaona kuwa tangu huo wakati Israeli ilipokuwa Taifa huru tena, mvutano mkubwa ulianza kujitokeza mashariki ya kati na duniani kote kwa ujumla. Nchi za kiharabu zikiigombania Israeli na mataifa mengine yakizisapoti.Mpaka kupeleka Israeli kuwa na maadui wengi pande zake zote. Watu wasifahamu kuwa jambo hilo linatoka kwa Bwana mwenyewe ili kuonyesha kuwa moja ya hizi siku mataifa yote yatahukumiwa na rungu la Bwana Israeli.

Hiyo Iliendelea hivyo hivyo mpaka kupelekea mwaka 1967 mataifa yote ya urabuni yakiongozwa na Syria kujikusanya kwa ajili ya kuipoteza Israeli katika ramani ya dunia. Lakini jambo hilo kama tunavyosoma katika historia, Israeli ilizipiga silaha zao za vita na vita kuisha ndani ya siku 6 tu. Kupeleka mpaka Israeli kuteka sehemu ya kubwa ya taifa lake ambalo hapo kabla lilikuwa haliyamiliki pamoja na nchi za kando kando.

Sasa hayo nayo ni mwanzo wa utungu ili kutupa sisi picha ya mambo yatakayokuja kutoka siku za hivi karibuni. Hii ilikuwa ni mataifa ya uarabuni lakini siku zinakuja mataifa yote ulimwenguni yataungana kwenda kupigana na Israeli hiyo ndiyo vita ya Har-magedoni.

Hivyo tukisoma kitabu cha Ezekieli 28-39, tunaona vita nyingine hapa ukiwa na muda wako mwenyewe unaweza kusoma sura zote mbili upate kuiona habari nzima ni vita ambayo itapiganwa tena kipindi hichi karibu na unyakuo kutokea. Embu Tusome mistari michache tu ya mwanzo.

EZEKIELI: MLANGO 38

1 Neno la Bwana likanijia, kusema,

2 Mwanadamu, kaza uso wako, umwelekee Gogu, wa nchi ya Magogu, mkuu wa Roshi, Mesheki, na Tubali, ukatabiri juu yake,

3 useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ewe Gogu, mkuu wa Roshi, na Mesheki, na Tubali;

4 nami nitakugeuza na kutia kulabu katika mataya yako, nami nitakutoa, pamoja na jeshi lako lote, farasi na hao wapandao farasi, wote wamevaa silaha za namna zote, jeshi kubwa sana, wenye ngao na kigao, wote wakishika upanga;

5 Uajemi, na Kushi, na Putu, pamoja nao; wote wana ngao na chapeo;

6 Gomeri, na vikosi vyake vyote; nyumba ya Togarma, pande za mwisho za kaskazini, na vikosi vyake vyote; naam, watu wengi pamoja nawe.

7 Ujiweke tayari, naam, jiweke tayari, wewe na majeshi yako yote waliokukusanyikia, nawe uwe jemadari wao.

8 NA BAADA YA SIKU NYINGI UTAJILIWA; KATIKA MIAKA YA MWISHO, UTAINGIA NCHI ILIYORUDISHIWA HALI YAKE YA KWANZA, BAADA YA KUPIGWA KWA UPANGA, ILIYOKUSANYWA TOKA KABILA NYINGI ZA WATU, juu ya milima ya Israeli, iliyokuwa ukiwa wa daima; lakini imetolewa katika kabila za watu, nao watakaa salama salimini wote pia.

9 Nawe utapaa juu, utakuja kama tufani, utakuwa kama wingu kuifunika nchi, wewe, na vikosi vyako vyote, na kabila nyingi za watu pamoja nawe.

10 BWANA MUNGU ASEMA HIVI; ITAKUWA KATIKA SIKU HIYO, MAWAZO YATAINGIA MOYONI MWAKO, NAWE UTAKUSUDIA KUSUDI BAYA;

11 nawe utasema, Nitapanda juu niiendee nchi yenye vijiji visivyo na maboma; nitawaendea watu wanaostarehe, wanaokaa salama, wote wakikaa pasipo kuta, ambao hawana makomeo wala malango;

12 ili kuteka mateka, na kuwinda mawindo; uugeuze mkono wako juu ya mahali palipoharibika, ambapo sasa panakaliwa na watu, na juu ya watu waliokusanyika toka mataifa, waliopata ng’ombe na mali, wakaao katikati ya dunia.

13 Sheba, na Dedani, na wafanya biashara wa Tarshishi, pamoja na wana-simba wake wote, watakuambia, Je! Umekuja kuteka mateka? Umekusanya jeshi lako, ili kuwinda mawindo? Kuchukua fedha na dhahabu, kuchukua ng’ombe na mali, kuteka mateka mengi sana?

14 Basi, mwanadamu, tabiri, umwambie Gogu, Bwana MUNGU asema hivi; Katika siku ile watu wangu, Israeli, watakapokaa salama, hutapata habari?

15 Nawe utakuja kutoka mahali pako, kutoka pande za mwisho za kaskazini, wewe, na watu wa kabila nyingi pamoja nawe, wote wamepanda farasi, kusanyiko kubwa, na jeshi kuu;

16 NAWE UTAPANDA JUU UWAJILIE WATU WANGU, ISRAELI, KAMA WINGU KUIFUNIKA NCHI; ITAKUWA KATIKA SIKU ZA MWISHO, NITAKULETA UPIGANE NA NCHI YANGU, ILI MATAIFA WANIJUE, nitakapotakaswa kwako, Ewe Gogu, mbele ya macho yao.

17 Bwana MUNGU asema hivi; Je! Wewe ndiwe niliyemnena zamani za kale, kwa vinywa vya watumishi wangu, manabii wa Israeli, waliotabiri siku zile kwa muda wa miaka mingi, ya kwamba nitakuleta upigane nao?

18 Itakuwa katika siku hiyo, Gogu atakapokuja kupigana na nchi ya Israeli, asema Bwana MUNGU, ghadhabu yangu itapanda katika mianzi ya pua yangu.

19 Kwa maana katika wivu wangu, na katika moto wa ghadhabu yangu, nimenena, Hakika katika siku ile kutakuwako tetemeko kubwa katika nchi ya Israeli;

20 hata samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama wa kondeni, na vitu vyote vitambaavyo juu ya nchi, na wanadamu wote walio juu ya uso wa nchi, watatetemeka mbele ya uso wangu; nayo milima itatupwa chini, na magenge yataanguka, na kila ukuta utaanguka chini.

21 Nami nitaita upanga, uje juu yake katika milima yangu yote, asema Bwana MUNGU; nao upanga wa kila mtu utakuwa juu ya ndugu yake.

22 Nami nitamhukumu kwa tauni, na kwa damu; nami nitanyesha mvua ifurikayo, na mvua ya mawe makubwa sana, na moto na kiberiti juu yake, na vikosi vyake, na watu wa kabila nyingi walio pamoja naye.

23 Nami nitajitukuza, na kujitakasa, na kujidhihirisha, mbele ya macho ya mataifa mengi; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana”.

Sasa Nchi ya Magogu, biblia inayoitaja hapo ni eneo linalojulikana kama URUSI kwasasa. Hivyo nchi hii leo tunaoina ni nchi yenye nguvu sana kiasi kwamba inalitishia hata taifa la Marekani kwa nguvu zake na ukuu wake. Lakini biblia inasema siku moja mawazo yataliingia hili taifa ili kwenda kuishambulia Israeli. Na kibaya zaidi halitashuka peke yake, hapana bali litashuka na majeshi ya mataifa mengine mengi kama tunavyoyasoma hapo juu. Na mengi ya hayo yatakuwa na haya mataifa ya kiharabu, ambayo hayo kimsingi ni maadui wa Israeli tangu zamani, pamoja na nchi nyingi zilizokando kando ya Urusi.

Wote watapanga vita kuiendea ile nchi ndogo sana Israeli. Kama tunavyoona hata sasa Taifa linaloongoza kuwa na maadui wengi duniani ni taifa la Israeli, hivyo Urusi kwa kujipendekeza na kujionyesha kuwa yeye anayo nguvu na kwamba anaweza kuwasaidia watu waliowashindwa ISRAELI. Yeye naye siku hiyo atapanga vita na mabomu yake ya Atomiki ili kwenda kulisambaratisha taifa lile. Hawajui kuwa hapo ndipo Mungu alipokusudia uwe mwisho wa mataifa hayo yote chini ya jua. Siku hiyo Urusi itapotezwa kwenye ramani ya dunia, kwasababu Bwana atakuwa upande wa Israeli. Na wa-Rusi siku hiyo watasoma maandiko haya ya Ezekieli na kutambua kuwa unabii huo ulikuwa unawahusu wao.

Kumbuka vita hiyo japo itauwa watu wengi sana kiasi kwamba biblia inasema mizoga yao itakuwa inazikwa kwa muda wa miezi 7 ikikusanywa tu, na silaha zao zitakuwa zikitumika kama kuni kwa muda wa miaka 7, lakini huo utakuwa ni mwanzo tu wa utungu. Vita yenyewe kuu bado. Vita ya Har-magedoni ambayo itahusisha mataifa yote ulimwenguni.

Tutakuja kuizungumzia vizuri vita hii [Har-Magedoni] katika makala nyingine. Lakini tufahamu kuwa vita inayozungumziwa katika Ezekieli 38-39 ipo mbioni kutokea, kama tunavyoona sasahivi mvutano ulivyo mkubwa mashariki ya kati na ishara kuwa vita vinajiandaa kupiganwa muda wowote. Hivyo ndivyo Mungu anavyozidi kuitasa Israeli kidogo kidogo, Na ndivyo pia wanavyojiandaa kumpokea Masiya wao.

Swali tujiulize wakati sasahivi neema inarudi Israeli, mimi na wewe mpaka mambo hayo yatakapotokea tutakuwa wapi? Kumbuka ndugu tuliambiwa tukiyaona hayo yanaanza kutokea basi tunyanyue vichwa vyetu, kwa kuwa ukombozi wetu umekaribia. Ikiwa na maana UNYAKUO wetu upo karibu.

Kristo yupo mlangoni ndugu. Unasubiri nini usiufanye leo wito wako na uteule wako imara?. Walioishi kipindi chote cha nyuma kuanzia miaka ya 1900 kurudi nyuma mpaka kipindi cha kanisa la kwanza hawakukishuhudia kitu hichi sisi tunachokishuhudia leo yaani taifa huru la Israeli. Na biblia ilishasema kizazi hiki hakitapita, sasa unasubiri nini usiushindanie wokovu katika muda huu mfupi uliobaki?.

Ungependa mambo hayo yakukute kwa ghafla, Bwana amesema dunia hii itaangamizwa kwasababu ya maovu yake. Na wenye haki watapata kwa Mungu waepushwe nayo.. je! Na wewe ungependa uwe miongoni mwa watakaoharibiwa katika ile siku ya Bwana? Kama sivyo mgeukie Kristo, ambaye yeye ndio safina pekee iliyothibitishwa na Mbingu kwa wokovu wa mwanadamu.

Bwana akubariki.

Tafadhali “share” kwa wengine ujumbe huu.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

 HOME

Print this post

MAFUNUO YA ROHO.

Neno Ufunuo maana yake “NI KITU KILICHOFUNULIWA”..Ikiwa na maana kuwa, hapo kwanza kilikuwa kimefungwa na sasa kimefunuliwa. Hapo kwanza kilikuwa hakionekani sasa kinaonekana, hapo kwanza kilikuwa hakieleweki sasa kinaeleweka.

Zipo funuo za aina nyingi. Mwana sayansi alipochunguza vitu vya asili ndipo akapata ufunuo wa kutengeneza ndege, alipochunguza kwanini Tai anapaa ndipo alipogundua kitu kinachoitwa ndege, Baada ya uchunguzi wa tabia za mawimbi ya sauti na mwangwi akapata ufunuo wa kutengeneza kifaa kinachoitwa simu..ambapo hapo kwanza mambo hayo yalikuwa hayajulikani. Hivyo hivyo mpaka Akapata ufunuo wa kutengeneza magari na mambo mengine mengi.

Hivyo Roho ya mwanadamu Mungu aliyoiweka ndani yake ndiyo inayovumbua mambo ambayo kwa akili za kawaida yanaonekana kama hayawezekani. Lakini roho ya mwanadamu haiwezi kuvumbua chochote endapo mtu hatakaa katika hali ya utulivu na katika hali ya uchunguzi wa hali ya juu. Ndio maana wanasayansi na wagunduzi wengi, wanapoteza masaa mengi ya utafiti kwa kutulia na kutafakari na kujifunza pasipo kujichanganya na mambo mengi..lengo lao sio wajiumize hapana! Lengo ni ili waweze kuipa akili nafasi ya kutafakari mambo kwa undani kwa utulivu na utaratibu pasipo kuingiliwa na mambo mengine. Na hivyo wanapata matokeo makubwa wanapata Ufunuo/ uvumbuzi wa jambo Fulani..Yale mafumbo magumu waliyokuwa hawawezi kuyapatia ufumbuzi Roho zao zinawapatia ufumbuzi.

Kadhalika na Roho Mtakatifu naye..yeye ndiye ayachunguzaye mafumbo ya Mungu, na kuyapatia ufumbuzi..Na ndio maana ukisoma kitabu cha Ayubu 28, Utaona Bwana akiitafuta tafuta hekima kwa kuichunguza, hata kuipata na kumwambia mwanadamu..Hivyo utaona Roho ya Mungu, inapeleleza na kutafuta tafuta duniani kote mambo yamuhusuyo Mungu na Mwanadamu.

Zekaria 4: 7 “..naam, hizi saba ndizo macho ya Bwana; yapiga mbio huko na huko duniani mwote”.

Kwahiyo ili mtu awe na ufahamu juu ya mambo ya Mungu, ni lazima awe na Roho Mtakatifu kwasababu yeye pekee ndiye ayajuaye na kuyachunguza na kuyavumbua mambo ya Mungu..Kama vile  mwanadamu yeyote ili avumbue jambo Fulani ni lazima awe mwanadamu vivyo hivyo na kwa Mungu, ili kuyafahamu mambo yake ni lazima tuwe na Roho yake ndani yetu.

1Wakorintho 2: 10 “LAKINI MUNGU AMETUFUNULIA SISI KWA ROHO. MAANA ROHO HUCHUNGUZA YOTE, HATA MAFUMBO YA MUNGU.

11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.

12 Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu”

SASA NI KWA NAMNA GANI TUNAWEZA KUPOKEA MAFUNUO KUTOKA KWA ROHO MTAKATIFU ALIYE NDANI YETU?

Ni kwa njia moja tu tunayoweza kupokea Mafunuo ya Roho Mtakatifu..Na hiyo si nyingine zaidi ya kama ile ile wana-sayansi wanayoitumia…Wao wanajifungia ndani na kutafakari, na kusoma vitabu vingi, na kujizuia na mambo mengi…ILI Roho zao ziinuke zipate umakini wa hali ya juu ili kupata ufunuo.

Kadhalika na Ufunuo wa Roho, hauji tu kwa kuusubiria, hapana, bali unakuja KWA KUJIZUIA NA MAMBO MENGI YA ULIMWENGU HUU, NA KUFUNGA, na KUSOMA VITABU VINGI, VYA HISTORIA NA VYA WAHUBIRI MBALI MBALI AMBAO BWANA KAWATIA MAFUTA KWELI, na KWA KUCHUNGUZA VITU VYA ASILI KWA UNDANI sana. Kwa kujiweka katika hayo mazingira unampa ROHO MTAKATIFU NAFASI KUBWA SANA YA YEYE KUKUFUNULIA JAMBO AMBALO HAPO KWANZA ULIKUWA HULIJUI. Kwa kukufunulia Siri iliyopo ndani ya Yesu Kristo kwa undani.

Tunaweza tukaona mifano kadha wa kadha kwenye Biblia..Danieli baada ya kuchunguza chunguza kwa wahubiri waliomtangulia kabla yake mambo waliyokuwa wanayahubiri…alikutana na nyaraka za nabii Yeremia ambazo zilikuwa zimeandikwa miaka kamili ya wana wa Israeli kukaa utumwani..Na baada ya kupata ufunuo huo, akaendelea kumwomba Mungu aelewe vizuri maana ya hayo mambo..Na ndipo akaamua kufunga na Bwana akamfunulia zaidi ya pale, Malaika Gabrieli alikuja na akamfunulia MAJUMA SABINI YATAKAYOANZA BAADA YA WAO KUTOKA UTUMWANI.

Danieli 9: 1 “Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya Wakaldayo;

2 katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danielii, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini.

3 Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu”.

Mfano mwingine tonamwona Yule Mkushi aliyekuwa ametoka Yerusalemu kuhiji enzi za Mitume wa Kristo aliyekuwa anatafuta kuchunguza kwa bidii maandiko, Na katika kusoma kwake alikutana na maandiko magumu sana hakuyaelewa yaliyoandikwa na nabii Isaya…lakini kwasababu alikuwa na kiu ya kutaka kujua Bwana alimtimizia haja ya moyo wake na kumtumia ufunuo kupitia Mtumishi wake Filipo..Jambo hilo tunaweza kulisoma katika kitabu cha…

Matendo 8: 26 “Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa.

27 Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu,

28 akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya.

29 Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo.

30 Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma?

31 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye.

32 Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.

33 Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi.

34 Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine?

35 Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu.

36 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe?

37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.]

38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza.

39 Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi.

40 Lakini Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akahubiri Injili katika miji yote, hata akafika Kaisaria”.

Unaona! Ukichunguza wote hawa, Roho Mtakatifu aliwafunulia kwasababu walikuwa na kiu, na walikuwa wanajitahidi kusoma maandiko na kuchunguza. Roho Mtakatifu hawezi kukufunulia jambo lolote kama hutaki kujizuia na mambo Fulani, na kuchukua gharama Fulani, Kama hutaki kutaka kujua mambo yanayokuja ya kwenda mbinguni basi hutajua chochote mpaka kanisa litakaponyakuliwa na hivyo kubaki katika dhiki kuu ya Mpinga-Kristo, na kutupwa katika lile ziwa la moto baadaye. Utaendelea kufikiri tu bado mamilioni ya Miaka mpaka Kristo arudi.

Mfalme Nebukadneza wa Babeli ambaye hakuwa hata mkristo, wakati Fulani usiku alipokuwa amejiegeza kitandani mwake akitafakari ni mambo gani yatakayotokea siku za Mwisho…pasipo kujua chochote usingizi ukampitia akiwa bado katika hayo mawazo na alipokuwa katika usingizi ule akaota ndoto sanamu kubwa ipo mbele yake ina kichwa cha dhahabu, na kifua cha shaba na mikono ya fedha na miguu ya chuma..Aliposhtuka aliisahau ile ndoto, lakini alijua kabisa ni ndoto yenye mahusiano na siku za mwisho, kwasababu ndio mawazo aliyokuwa anayawaza kabla hajalala..(Danieli 2:27-29)..na kwa kupitia Nabii Danieli Roho aliweza kumfunulia Nebukadneza mambo yatakayokuja kutokea siku za Mwisho.

Unaona hapo? Roho anawafunulia hata watu wasiokuwa wake, mambo yatakayokuja kutokea siku za mwisho, Na wewe je! Alishawahi kukufunulia kwamba tunaishi katika nyakati gani?, na ni mambo gani yatakayokuja kutokea siku za mwisho? Ulishawahi kukaa chini na kutafakari mambo yatakayokuja kutokea nyakati za Mwisho? Ulishawahi kukaa chini ukatafakari yale maneno Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake katika Mathayo 24??…aliposema mmoja atatwaliwa mmoja ataachwa ulishawahi kuketi chini na kutafakari mambo hayo?.

Muhubiri mmoja, Mjumbe wa Mungu anayeitwa WILLIAM BRANHAM, siku moja asubuhi wakati ametoka kulala tu! Akiwa amejiegemeza kichwa chake juu ya mto, akitafakari itakuwaje siku ile atakayoenda kumwona Bwana mawinguni, akiwa anatafakari akidhani kuwa mwendo ndio amekaribia kuumaliza, ghafla alisikia sauti ndogo ikimwambia “akaze mwendo ndio kwanza safari inaanza” wakati anaitafakari hiyo sauti alijikuta ametokea mahali palipo pazuri sana pa utulivu, penye nyasi nzuri ambazo anasema hajawahi kuziona hapo kabla, akawaona wadada na wakaka wengi wa makamu ya miaka kama 20-30 hapo, wamevaa vizuri sana, wanamjia wakiwa na nyuso za furaha, wote wakawa wanamkumbatia kila mmoja akimwambia “oo ndugu yetu wa thamani…oo ndugu yetu wa thamani” wote walionyesha nyuso za furaha na raha isiyokuwa ya kawaida..William akasikia ile sauti ikimwambia “hawa wote unaowaona ni wale watu uliowaleta kwa Kristo kupitia injili yako, waliotangulia kulala, sasa wako hapa wanakushukuru” Akashangaa sana kuona jinsi walivyo wengi..

Wakamwuliza akisema..lakini mbona wengine niliwaleta kwa Kristo wakiwa wazee, inakuwaje hapa nawaona wote ni vijana, akaambiwa huku hakuna wazee wote ni vijana..Akasikia ile sauti ikimwambia “siku ile ya mwisho” akaze mwendo ndio kwanza tu anaanza safari. Lile ono likampotea na alivyorudi katika hali yake ya kawaida, hiyo ilimtia nguvu kukaza mwendo zaidi ili siku ile afike sehemu ile ya Raha.

Unaona! Huyu ndugu BRANHAM ni moja ya watu, waliokuwa wakitafakari tu vitandani mwao, kama Mfalme Nebukadneza alivyofanya na ROHO MTAKATIFU akawafunulia baadhi ya mambo yajayo.

Ni maombi yangu kuwa BWANA ATAKUKIRIMIA NA WEWE KUYAFAHAMU MAFUMBO YAKE. Ni maombi yangu kuwa Bwana atakupa ukurasa mpya kuanzia leo, kutaka Kupata ufunuo kutoka kwake, Ni maombi yangu kuanzia leo Bwana atakujalia kutafuta kujifunza kwa bidii kama Danieli, mpaka Kupata kufunuliwa mambo yajayo. Ni maombi yangu kuwa Bwana atakupa kutafakari na kudadisi mambo yajayo mpaka atakapokupa ufunuo kama aliompa Nebukadneza, au aliompa mhubiri William Branham, Ni maombi yangu kuwa Bwana atakupa kuyadadisi maandiko sana, mpaka Roho atakapomtuma Mtumishi wake atakayekuelewesha vema mafumbo yake..kama alivyofanya kwa Yule Mkushi alipotumiwa Filipo.

Bwana Yesu akubariki.

Usiache “kus-share” ujumbe huu kwa wengine.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

TUSIPOUTHAMINI WOKOVU TUTAPATAJE KUPONA?

DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI:

JINSI MWISHO ULIVYOKARIBIA.

MANA ILIYOSHUSHWA KUTOKA MBINGUNI


Rudi Nyumbani

Print this post

ITAFAKARI VEMA KAZI YA MUNGU

Tukijua kuwa Mungu ni zaidi ya sisi tunavyofikiri, Na kwamba hukumu zake hazichunguzi (kama inavyosema Warumi 11:33), Siku hiyo tukifahamu mambo hayo kwa undani tutaishi maisha ya kumwogopa na ya kujichunga kila siku, Siku tukijua kuwa mambo yote mtu atendayo aidha yawe maovu au mema hayaji kwa nguvu zake mwenyewe bali ni kutoka kwa Mungu, ndipo tutakapomwopoga sana Mungu na kujua kuwa yeye si mwanadamu na kwamba mawazo yake si mawazo yetu.

Biblia inasema:

Mhubiri 7:13 “Tafakari vema kazi yake Mungu; kwa sababu ni nani awezaye kukinyosha kitu kile alichokipotosha yeye?”.

Watu wengi hawapendi kusikia maneno hayo kwamba Mungu anao uwezo wa kumletea mtu nguvu ya upotevu ili apotee,. Ni kweli Mungu hawezi kumletea mtu nguvu ya upotevu kwa yeye ambaye hajaijua neema bado lakini kwake yeye aliyeisikia na kuipuuzia na kuikataa, nguvu hiyo ya upotevu inaachiliwa juu yake, na nguvu hiyo haitoki kwa shetani bali inatoka kwa Mungu mwenyewe.

Soma >>

1Wathesalonike 2:10 “na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.

11 KWA HIYO MUNGU AWALETEA NGUVU YA UPOTEVU, WAUAMINI UONGO;

12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.”

Kama tu vile mtu anayempokea Kristo kwa mara ya kwanza Mungu huwa anamshushia uwezo /nguvu ya kushinda dhambi na kufanyika kuwa mtoto wa Mungu (Yohana 1:12), kadhalika na wale ambao wanaikataa neema ya msalaba au wanaoipuuzia sasa, utafika wakati hii nguvu ya upotevu itokayo kwa Mungu inaachiliwa wao nao juu yao. Hivyo watu wa namna hiyo inafika wakati hata wahubiriweje injili, hata wauone ukweli kiasi gani, hawawezi tena kuamini. Hali yao ya rohoni inazidi kuwa mbaya kuliko hata waliyokuwa nayo mwanzoni, kule kuchomwa rohoni pale mtu anapotenda jambo baya kunakufa, dhamira yake inakuwa imekufa, mtu kama huyo dhambi inakuwa ni kitu cha kawaida sana kwake, hata akibaka mnyama, hata akiua, hata akifanya ushoga, hata akikufuru mbele za Mungu kwake ni kama jambo la kawaida tu,.

Ni kwasababu gani?, Ni kwasababu ile nguvu ya upotevu itokayo kwa Mungu imeachiliwa juu yake ili auamini uongo siku ile akahukumiwe ili ashuke moja kwa moja katika ziwa la moto, kwasababu hakuipenda kweli apate kuokolewa bali alijifurahisha katika udhalimu.. Na Watu wa namna hiyo kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda ndio mwisho wa siku wanaishia kuipinga biblia, wanaishia kusema hakuna Mungu, biblia ni kitabu kilichotungwa na watu, wanakuwa wanaishi tu kama wanyama duniani wasioweza kujizuia. Watu wa namna hiyo wanawaona hata wale wengine wanaotafuta wokovu kama ni watu wasioelimika, watu waliokata tamaa ya maisha, watu wajinga wasio na mwelekeo.

Biblia imetumia lugha hii kuwazungumzia jinsi walivyo watu wa namna hiyo..

Yuda 1:11-16 “ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung’olewa kabisa;

13 ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele.

14 Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,

15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.

16 Watu hawa ni wenye kunung’unika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno makuu mno ya kiburi, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida.”

Sasa watu wa dizaini hii hata uwahubirieje injili hawawezi kubadilika wala hawatakaa wabadilike kwasababu ni Mungu wenyewe ndiye aliyewakusudia mabaya, na ndio maana biblia inasema:

Mhubiri 7:13 “Tafakari vema kazi yake Mungu; kwa sababu ni nani awezaye kukinyosha kitu kile alichokipotosha yeye?”.

Ndugu, Njia za Mungu huwa ZINATISHA, na ndio maana tumeambiwa TUZITAFAKARI VEMA KAZI ZAKE, sio tu kuzichukulia juu juu, Tukidhani kuwa hukumu za Mungu zinachunguzika kwamba nitaokoka tu siku moja! Au Tunasema Mungu ataokoa tu!, Mungu tu ataokoa tu! Na huku tunadumu katika dhambi tukidhani kuwa neema ni kitu cha kukifanyia mzaha. Kumbuka hilo neno lenyewe NEEMA ni kitu kinachoonyesha kuwa ni jambo AMBALO HUKUSTAHILI KULIPATA NI KWA HURUMA TU UMEPEWA, lakini unaendelea kulifanyia mzaha kana kwamba ulistahili kuipata ni haki yako?.

Unadhani NGUVU HIYO YA UPOTEVU itakapokujia juu yako ikiwa hautubu leo, na kusimama imara katika Kristo siku ile ya hukumu utasema Mungu ni MDHALIMU alikuletea mabaya kwa makusudi?. Ndugu Itafakari vema kazi ya Mungu ili ujue leo hii unasimamia wapi?.

Mungu alishamaliza mambo yote kabla hata ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, majina ya watakaookolewa Mungu alishayaandika katika kitabu cha uzima kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa biblia inasema hivyo

Ufunuo 17.8 “Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. NA HAO WAKAAO JUU YA NCHI, WASIOANDIKWA MAJINA YAO KATIKA KITABU CHA UZIMA TANGU KUWEKWA MISINGI YA ULIMWENGU, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako”.

Embu tafakari kwa makini habari hii utajifunza jambo.

Warumi 9:11 “(kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye),

12 aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo.

13 Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.

14 Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha!

15 Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye.

16 Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu.

17 Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote.

18 Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu.

19 Basi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana ni nani ashindanaye na kusudi lake?

20 La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi?

21 Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?

22 Ni nini basi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kuudhihirisha uweza wake, kwa uvumilivu mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu;

23 tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu;”

Je! Wewe ni chombo cha ghadhabu kilichowekwa tayari kwa uharibifu, au ni kile chombo cha rehema?. Jua tu ikiwa unaukwepa msalaba, ikiwa unaukwepa wokovu, ikiwa unaikwepa toba, ile nguvu ya upotevu mfano wa ile iliyokuwa juu farao ambayo HATA AONE MIUJIZA MIKUBWA KIASI GANI HAWEZI KUTUBU, NDIYO ITAKAYOKUJA JUU YAKO KAMA UTAENDELEA KUUPINGA WOKOVU NDANI YA MOYO WAKO.

TAFAKARI VEMA KAZI YAKE MUNGU. Ili ujiokoe nafsi yako, Epuka Injili ya maneno ya faraja kila siku unaambiwa kwamba Mungu ni Mungu wa rehema. Lakini upande wa pili wa Mungu hagusiwi ambao unasema BWANA NI MWINGI WA HASIRA, ni nani awezaye kusimama mbele ya hasira yake, ni nani awezaye kukaa katika ukali wa hasira yake? (Nahumu 1 )

Kwa kulijua hilo, utafahamu kuwa Mungu hadhihakiwi na hapo ulipo hupaswi kuendelea kudumu katika dhambi. Na ndio maana biblia inasema “(Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)”

Kwa nini usiwe mmojawapo wa kondoo wa Kristo?. Ikiwa upo tayari sasa kuwa mmojawapo unachopaswa kufanya ni kukusudia wewe mwenyewe kutoka moyoni mwako Kutubu na kuacha dhambi kabisa..Kumbuka kutubu ni KUGEUKA( au KUACHA) na sio sala ya toba tu.

Hivyo ukiwa umedhamiria kufanya hivyo wewe moyoni mwako kwa dhati kabisa na kutaka kumwishia Kristo kuanzia sasa na kuendelea. Unachopaswa kufanya ni kwenda kutafuta mahali ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kimaandiko, yaani ubatizo wa kuzamishwa, katika maji mengi na jina linalotumika liwe ni JINA LA YESU KRISTO na si linginelo. Ili upate ondoleo la dhambi zako, Kulingana na matendo 2:38,na Bwana mwenyewe atakupa Roho wake Mtakatifu kuanzia huo wakati na kuendelea kukusaidia kuukulia wokovu na kuishinda dhambi.

Mungu akubariki sana.

“Share” Ujumbe huu kwa ndugu zako, Na Mungu atakubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

UNAFANYA NINI HAPO?

UMETEKWA NA UPENDO WA KRISTO?

WAKATI WA JIONI KUTAKUWAKO NA NURU.

TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.

NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.


Rudi Nyumbani

Print this post

SADAKA ILIYOKUBALIKA.

 

SADAKA ni moja ya maagizo muhimu sana, na yanayobeba Baraka nyingi sana kwa Mtu, kama ikitolewa kulingana na Neno na kwa Hiari ya mtu pasipo kulazimishwa au kusukumwa na mazingira Fulani. Lakini sadaka hiyo hiyo isipotolewa jinsi inavyopaswa inaweza ikaleta LAANA kubwa sana, badala ya Baraka. Kwasababu biblia inasema katika..Mithali 15:8 “Sadaka ya mtu mbaya ni CHUKIZO KWA BWANA; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake”.

Biblia inaposema mtu mbaya ina maana gani?

Mtu yeyote Yule ambaye haishi kulingana na Neno la Mungu, mtu huyo ni mbaya mbele za Mungu. Mtu yeyote anayejua kuwa kufanya jambo Fulani ni dhambi na bado analifanya mtu huyo ni mbaya mbele za Mungu. Mtu yoyote anayejua uasherati ni dhambi na bado anaufanya, mtu yeyote anayejua rushwa ni dhambi na bado anatoa au anapokea, mtu yeyote anayejua usengenyaji ni dhambi na bado anasengenya, mtu yoyote anayejua kuwa matusi ni dhambi na bado anatukana mtu huyo mbele za Mungu ni mtu Mbaya,

Mtu yoyote anayejua ulevi, anasa, wizi ni mbaya na bado anafanya mambo hayo mtu huyo ni mbaya mbele za Mungu, Na hivyo sadaka zake ni MACHUKIZO MAKUBWA MBELE ZA MUNGU. Apatapo chochote kwa njia hizo na kuzipeleka Madhabahuni kwa Bwana sadaka yake mtu huyo ni MACHUKIZO, na hivyo atakuwa ameenda kujitafutia laana badala ya Baraka. Kwahiyo kwake linakuwa ni chukizo litakalomletea Uharibifu wake mwenyewe. Biblia inasema katika..

Kumbukumbu 23: 17 “PASIWE NA KAHABA KATIKA BINTI ZA ISRAELI, wala pasiwe na HANITHI katika wana wa Israeli wanaume.

18 USILETE UJIRA WA KAHABA, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; KWANI HAYA NI MACHUKIZO KWA BWANA, MUNGU WAKO, YOTE MAWILI”.

Unaona hapo! Bwana alikataza sadaka zozote, zitokanazo na njia zilizo nje ya Neno lake, zisifike kabisa nyumbani mwake.

Watu wanapokosa shabaha ni kufikiri kuwa Ukristo ni kwenda kanisani na kutoa sadaka, basi au kusaidia wajane na mayatima…Hawajui kuwa Ukristo ni zaidi ya hapo. Kumpendeza Mungu sio kumpa yeye sehemu ya mali yako na kuishi maisha unayotaka..Hapana Mungu sio mfanya biashara kwamba anakutafuta wewe ili apate kitu kwako, wala sio mwana-Hisa kwamba anawekeza kwetu ili baadaye apate kitu kutoka kwetu. Yeye mwenyewe anasema Dunia yote ni yake, sasa ana haja na kitu gani? Bwana Yesu alisema maneno haya..

Mathayo 9: 13 “Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA;”

Na pia anasema katika Waebrania 10:6

“Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo;

7 Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) NIYAFANYE MAPENZI YAKO, MUNGU.”

Unaona hapo? Bwana anachotaka kutoka kwetu ni REHEMA, yaani anataka mtu atubu, asafishike na kuwa msafi kweli kweli anayekubaliwa na Mungu, atende mapenzi ya Mungu…Hiyo ndio sadaka inayompenda Mungu.

Wakati Fulani Mfalme Sauli alipewa maagizo kutoka kwa Bwana akawaangamize jamii ya watu Fulani, aangamize na mifugo yao yote na kila kitu, ili kutimiza kisasi cha Bwana juu ya hao watu, lakini Sauli hakufanya vile, hakuitii sauti ya Mungu kwa kuangamiza kila kitu, na badala yake akamuacha mfalme wao hai, na akachukua wale ng’ombe walionona ili akamtolee Mungu wa Israeli sadaka zile mambo ambayo Mungu alimkataza asiyafanye.. Kwa mawazo yake alijua Mungu atamheshimu na kumpenda kwasababu amemletea sehemu zilizonona za nyara za Maadui zao. Lakini mambo yalimbadilikia mbeleni alipokutana na Samweli nabii wa BWANA…

1 Samweli 15: 20 “Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya Bwana, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa.

21 Ila watu waliteka nyara, kondoo na ng’ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, KUSUDI WAVITOE DHABIHU KWA BWANA, MUNGU WAKO, huko Gilgali.

22 Naye Samweli akasema, JE! BWANA HUZIPENDA SADAKA ZA KUTEKETEZWA NA DHABIHU SAWASAWA NA KUITII SAUTI YA BWANA? Angalia, KUTII NI BORA KULIKO DHABIHU, NA KUSIKIA KULIKO MAFUTA YA BEBERU.

23 Kwani KUASI NI KAMA DHAMBI YA UCHAWI, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme”.

Kwa kosa hilo moja tu! Sauli alipoteza ufalme wake, na Mungu alimwacha tangu siku ile. Kwasababu hakuwa mtii mbele za Mungu na badala yake akadhani kuwa uhusiano wake yeye na Mungu haujalishi sana, bali kinachojalisha ni kiasi gani cha sadaka anachomtolea.

Mahali pengine Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake..

Mathayo 5: 23 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, NA HUKU UKIKUMBUKA YA KUWA NDUGU YAKO ANA NENO JUU YAKO,

24 Iache Sadaka Yako Mbele Ya Madhabahu, Uende Zako, Upatane Kwanza Na Ndugu Yako, Kisha Urudi Uitoe Sadaka Yako”.

Unaona! Unaweza ukawa tayari umeshajiandaa kutoa sadaka yako kwenye madhabahu ya Mungu, lakini ndani ya moyo wako kuna mtu mmegombana, au kuna mtu umemkosea, au kuna mtu umemsengenya au kitu kilicho kibaya umekifanya, Bwana Yesu anatuonya Nenda kwanza kapatane na ndugu yako kisha ndipo uje utoe ile sadaka,.. Lakini tusipofanya hivyo na kuitoa ile sadaka.. yatakukuta kama yaliyomkuta Mfalme Sauli. Badala ya kupokea Baraka unapokea Laana. Badala ya kuinuliwa unashushwa.

Hivyo maisha yetu matakatifu ndio sadaka ya kwanza Mungu anayoitaka katika maisha yetu, ukiwa mwasherati tubia kwanza uasherati wako kwa kumaanisha kuuacha kwasababu maana ya kutubu sio kuomba msamaha tu! Bali ni KUGEUKA ndipo ukamtolee Mungu sadaka yako, ukiwa mlevi tubia kwanza ulevi wako kwa kumaanisha kuuacha kabisa ndipo ukamtolee Bwana sadaka zako, na vivyo hivyo mambo mengine yote yaliyo nje na Neno lake unayoyafanya. Yaache kwanza ndipo ufikirie suala la Sadaka..

Isaya 1: 11 “Huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea UNA FAIDA GANI? Asema Bwana. Nimejaa mafuta ya kafara za kondoo waume, na mafuta ya wanyama walionona; nami siifurahii damu ya ng’ombe wala ya wana-kondoo wala ya mbuzi waume.

12 Mjapo ili kuonekana mbele zangu, ni nani aliyetaka neno hili mikononi mwenu, kuzikanyaga nyua zangu?

13 MSILETE TENA MATOLEO YA UBATILI; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya na sabato, kuita makutano; SIYAWEZI MAOVU HAYO NA MAKUTANO YA IBADA.

14 Sikukuu zenu za mwezi mpya na karamu zenu zilizoamriwa, NAFSI YANGU YAZICHUKIA; MAMBO HAYO YANILEMEA; NIMECHOKA KUYACHUKUA.

15 Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu.

16 JIOSHENI, JITAKASENI; ONDOENI UOVU WA MATENDO YENU USIWE MBELE ZA MACHO YANGU; ACHENI KUTENDA MABAYA;

17 JIFUNZENI KUTENDA MEMA; TAKENI HUKUMU NA HAKI; WASAIDIENI WALIOONEWA; MPATIENI YATIMA HAKI YAKE; MTETEENI MJANE.”

Neema ya Bwana Yesu Kristo izidi kuwa nawe.

Ubarikiwe sana.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Rudi Nyumbani

Print this post

NI WAKATI UPI UTAUONA USO WA KRISTO?

Habari ya huyu kipofu unaweza ukawa umeshaisoma mara nyingi sana, lakini lipo jambo limejificha ambalo kila mtu anapaswa alijue, tafadhali soma tena kwa utaratibu na kwa utulivu kisha tutatazama ni wapi tunapaswa tuzingatie sana sana pale tunapodhani kuwa Mungu kutufanikisha au kutuwezesha katika mambo yetu ni uthibitisho kuwa tumemwona yeye.

Embu tusome tena pamoja kwa utulivu:

Yohana 9:1-41 
“1 Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. 

2 Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? 

3 Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake. 

4 Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi. 

5 Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu. 

6 Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho, 

7 akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona. 

8 Basi jirani zake, na wale waliomwona zamani kuwa ni mwombaji, wakasema, Je! Huyu siye yule aliyekuwa akiketi na kuomba? 

9 Wengine wakasema, Ndiye. Wengine wakasema, La, lakini amefanana naye. Yeye mwenyewe alisema, Mimi ndiye. 

10 Basi wakamwambia, Macho yako yalifumbuliwaje? 

11 Yeye akajibu, Mtu yule aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka macho akaniambia, Nenda Siloamu ukanawe; basi nikaenda na kunawa, nikapata kuona. 

12 Wakamwambia, Yuko wapi huyo? Akasema, Mimi sijui. 

13 Basi wakampeleka kwa Mafarisayo yule aliyekuwa kipofu zamani. 

14 Nayo ilikuwa sabato, hapo Yesu alipofanya zile tope na kumfumbua macho. 

15 Basi Mafarisayo nao wakamwuliza tena jinsi gani alivyopata kuona. Akawaambia, Alinitia tope juu ya macho, nami nikanawa, na sasa naona. 

16 Basi baadhi ya Mafarisayo wakasema, Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato. Wengine wakasema, Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo? Kukawa matengano kati yao. 

17 Basi wakamwambia yule kipofu mara ya pili, Wewe wasemaje katika habari zake kwa vile alivyokufumbua macho? Akasema, Ni nabii. 

18 Basi Wayahudi hawakusadiki habari zake, ya kuwa alikuwa kipofu, kisha akapata kuona; hata walipowaita wazazi wake yule aliyepata kuona. 

19 Wakawauliza wakisema, Huyu ndiye mwana wenu, ambaye mnasema kwamba alizaliwa kipofu? Amepataje, basi, kuona sasa? 

20 Wazazi wake wakawajibu, wakasema, Tunajua ya kuwa huyu ndiye mwana wetu, tena ya kuwa alizaliwa kipofu; 

21 lakini jinsi aonavyo sasa hatujui; wala hatujui ni nani aliyemfumbua macho. Mwulizeni yeye mwenyewe; yeye ni mtu mzima; atajisemea mwenyewe. 

22 Wazazi wake waliyasema hayo kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayahudi walikuwa wamekwisha kuafikiana kwamba mtu akimkiri kuwa ni Kristo, atatengwa na sinagogi. 

23 Ndiyo sababu wale wazazi wake walisema, Ni mtu mzima, mwulizeni yeye. 

24 Basi mara ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu, wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyo ni mwenye dhambi. 

25 Basi yule mtu akajibu, Kwamba yeye ni mwenye dhambi sijui. Najua neno moja, kuwa mimi nalikuwa kipofu na sasa naona. 

26 Basi wakamwambia, Alikutendea nini? Alikufumbua macho jinsi gani? 

27 Akawajibu, Nimekwisha kuwaambia, wala hamkusikia; mbona mnataka kusikia tena? Ninyi nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake? 

28 Basi wakamshutumu, wakasema, Wewe u mwanafunzi wake yule; sisi tu wanafunzi wa Musa. 

29 Sisi tunajua ya kuwa Mungu alisema na Musa; bali yule hatujui atokako. 

30 Yule mtu akajibu, akawaambia, Hii ni ajabu! Kwamba ninyi hamjui atokako, naye alinifumbua macho! 

31 Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo. 

32 Tokea hapo haijasikiwa ya kuwa mtu ameyafumbua macho ya kipofu, ambaye alizaliwa hali hiyo. 
33 Kama huyo asingalitoka kwa Mungu, asingeweza kutenda neno lo lote. 

34 Wakajibu, wakamwambia, Ama! Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufundisha sisi? Wakamtoa nje. 

35 Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu? 

36 Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini? 

37 Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye. 

38 Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia. 

39 Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu. 

40 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo, wakamwambia, Je! Sisi nasi tu vipofu? 

41 Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa.”

Amen!

Katika habari hiyo kuna maswali kadhaa ya kujiuliza,

La kwanza ni kwa nini Bwana hakumponya huyu kipofu wakati ule ule alipokutana naye hadi kumwambia kwanza aende kunawa katika birika la ALIYETUMWA ( yaani SILOAMU?) ndipo atakapofunguliwa macho yake.?Unadhani alishindwa kumfungua macho muda ule ule?.

Pili Kulingana na habari baada ya kufunguliwa macho yake ni kweli alipata kuona kwa namna ile Kristo aliyokuwa anaitarajia?.

Ukichunguza kwa makini utaona kuwa Yule mtu hakumjua YESU ni nani, wala alipotokea wala alipoenda wala hakumwona uso wake hata baada ya kufunguliwa macho yake. Haikujalisha alifunguliwa macho kiasi gani yeye alichoweza kufanya ni kwenda tu kuendelea kufanya shughuli zake za nyumbani kwao za kila siku mpaka ilipofikia wakati majirani zake walipoanza kumuuliza habari za kufunguliwa macho yake..Ndipo akaanza tena kunena habari za YESU.

Kama tunavyosoma alianza kupitia mitikisiko pindi tu alipoanza kumkiri Kristo maishani mwake. Hapo ndipo vita kutoka kwa watu mbali mbali, kutoka kwa wakuu wa dini vikaanza, kukanwa na wazazi, kupuuziwa na majirani kulipoanza. Kwasababu kumbuka kwa wakati ule wayahudi wote walikuwa wameshakwisha kupatana kuwa akitokea mtu yeyote atakayemkiri Kristo kuwa ni mwokozi adhabu yake itakuwa ni kutengwa na sinagogi daima, kwa leo tunaweza kusema kutengwa na kanisa. Na kumbuka kutengwa na sinagogi kwa wakati ule ni zaidi ya hapo, kulikuwa ni sawa na kutengwa na jamii nzima ya wayahudi kwasababu Taifa zima lilikuwa na DINI moja na Utamaduni mmoja..Tofauti na sasahivi ambapo mtu akitengwa na jamii yake anaweza akakubaliwa na jamii nyingine kwasababu tamaduni zipo nyingi na kuna haki nyingi za kibinadamu mtu kuishi anavyotaka…Hivyo mtu aliyekuwa anadhubutu kufanya vile alikuwa hachukui uamuzi mwepesi, bali ni uamuzi wa kujikana kweli kweli, ulikuwa ni uamuzi mzito mno.. Na ndio maana ukisoma wapo wengi waliomwamini YESU lakini pale ilipofikia hatua ya kumkiri walishindwa

Yohana 11: 42 “WALAKINI HATA KATIKA WAKUU WALIKUWAMO WENGI WALIOMWAMINI; LAKINI KWA SABABU YA MAFARISAYO HAWAKUMKIRI, WASIJE WAKATENGWA NA SINAGOGI.

43 Kwa maana walipenda utukufu wa wanadamu kuliko utukufu wa Mungu.

44 Naye Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi”

Na kama tunavyosoma baada ya Yule kipofu kujadiliana na wale mafarisayo kwa muda mrefu ndipo waakamua kumchukua kwa nguvu na kumtupa nje ya Sinagogi…Maskini mtu Yule akitazama wazazi wake hawakutaka kusimama upande wake japo walijua ukweli kuwa ni Yesu ndiye aliyemponya, wale majirani zake hakuweza kumtetea kwa wakati ule wakiogopa kutengwa na jamii nzima, wala mtu yeyote aliyefahamu ukweli hakudhubutu kusimama upande wake, wote walikaa kando wakiogopa kumkiri BWANA, Hivyo Yule mtu akafukuzwa asionekane tena katikati ya mikusanyiko ya waaminio iliyokuwa katika miji ile, ilikuwa bado nusu tu apigwe kwa mawe kama angeendelea kudumu eneo lile na kushindana na wale viongozi wa dini,..

Lakini tunasoma alipokuwa mwenyewe pale nje ndipo Kristo AKAMJIA. Haleluya, na kwa kuwa yeye hakuwahi kumwona uso wake hata siku moja japo alifunguliwa macho na yeye, alipokuja Bwana hakuweza hakumtambua, mpaka Bwana alipomuuliza “WEWE WAMWAMINI MWANA WA MUNGU? Ndipo Yule mtu akajibu: Ni nani, Bwana, nipate kumwamini?..Bwana akamwambia “UMEMWONA, NAYE ANAYESEMA NAWE NDIYE.” Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia.

Na mwishoni Bwana akamalizia na kumwambia maneno haya..

“39 MIMI NIMEKUJA ULIMWENGUNI HUMU KWA HUKUMU, ILI WAO WASIOONA WAONE, NAO WANAOONA WAWE VIPOFU.

40 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo, wakamwambia, Je! Sisi nasi tu vipofu?

41 Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa.” 

Kaka/dada inawezekana Bwana alishakufungua katika vifungo vyako kule “KWA ALIYETUMWA (SILOAMU)”..Siloamu wako anaweza akawa mchungaji Fulani, mtumishi Fulani, huduma Fulani vyovyote vile. Inawezekana ulipokwenda ulipokea majibu ya maombi yako uliyokuwa umemwomba Mungu siku nyingi, ulipokwenda uliponywa, ulipokwenda ulifunguliwa, ulipokwenda upata kile ulichokuwa unakihitaji kwa muda mrefu..Lakini je! Ni KWELI ULIKUTANA NA KRISTO?. ULIUONA USO WAKE?

Yule kipofu japo alifanyiwa muujiza mkubwa kama ule lakini hakuwahi kumjua Kristo, wala kumwona sura yake..Lakini baada ya kuanza kumkiri tu na kuichagua ile njia ILIYOOGOPWA NA WENGI, iliyokuwa ya hatari ya kujikana maisha kwa ajili ya jina lake. Ndipo alipokwenda kukutana na YESU uso kwa uso kule nje! Na kumfahamu vizuri yeye ni nani. Unadhani alishindwa kumkana kusema tu vile ili kuwaridhisha mafarisayo. Hakushindwa lakini alitaka kutafuta kitu kilicho bora zaidi ya aliyotendewa, Alipotengwa kando ndipo Yesu akamjia.

Ni wengi leo hii, wanadai wamemwona Mungu katika maisha yao kisa tu wamefanikishwa katika mambo yao na shughuli zao. Lakini ukiyatazama maisha yao je ni kweli wameiendea njia ya msalaba, ya kujikana nafsi na kujitwika msalaba wako kwa ajili ya Kristo, na kuamua kuishi maisha matakatifu, utagundua hawajafanya hivyo na bado wanadai wamemwona Mungu.

Wanaogopa wakijaribu kufanya hivyo watatengwa na wazazi wao, wanaogopa kudharauliwa na marafiki zao, wanaogopa kuonekana ni watu wa ajabu washamba, wakiogopwa kuchukiwa na watu wa ulimwengu huu… Hawajui kuwa kule kufanikiwa kwao ilikuwa ni kwa ajili ya kulikiri jina la Kristo kwa maisha yao na si kwa midomo tu. Na pia ni kwa ajili ya wao kujitengenezea njia nzuri ya kwenda kukutana na Kristo lakini wao wanaikwepa. Dada/Kaka Kristo anapatikana katika njia iliyokataliwa, hapatikani kwa  wakuu wa dini,wala wa madhehebu anapatikana nje kule mahali palipokataliwa..Yule kipofu hakukutana na Kristo alipokuwa na wale mafarisayo, na wakuu wa dini, hapana badala yake alikutana na Yesu mahali ambapo hata yeye mwenyewe hakutarajia, mahali walipokuwa wamemtenga.

Kumbuka Kristo leo hii ametupwa nje na ulimwengu, Na ndio maana anasema Ufunuo 20: 20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

Ili uwe na mahusiano binafsi na YESU katika maisha yako ni lazima uchukue uamuzi wa kujitwika msalaba wako na kumfuata.

Ni wale tu watakaokubali kutupwa na wao nje ndio watakaokutana na Kristo huko vinginevyo utabakia kumsikia tu, haijalishi ni kwa namna gani utakuponya magonjwa yako, haijalishi ni kwa namna gani atakufanikisha katika biashara zako, haijalishi ni kwa namna gani atakukirimia mahitaji yako. Kama hutakubali kutupwa nje na ulimwengu kwa ajili ya jina lake, hutakaa UMWONE YESU KAMWE!

Ndio maana sehemu nyingine Bwana Yesu anajulikana kama JIWE KUU LA PEMBENI ambalo limekataliwa na waashi wengi. Kristo hapatikani kwa Padre, kwa Mchungaji, kwa Papa, kwa Watumishi, au kwa mtu yoyote anayejiita Mtu wa Mungu.. Kristo anapatikana mahali palipokataliwa na Ulimwengu..Mahali penye njia nyembamba.. 

Luka 13: 22 “Naye alikuwa akipita katika miji na vijiji, akifundisha, katika safari yake kwenda Yerusalemu. 

23 Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia, 

24 JITAHIDINI KUINGIA KATIKA MLANGO ULIO MWEMBAMBA, KWA MAANA NAWAAMBIA YA KWAMBA WENGI WATATAKA KUINGIA, WASIWEZE”.

Njia ni nyembamba ndugu iendayo uzimani..Tujitahidi uipite hiyo sasa, kabla Mlango wa Neema haujafungwa, kwa kumwamini Yesu Kristo, Mkuu wa Uzima, na MSHIKAJI WA MAMLAKA YOTE, Kwa kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na Kwa Jina lake, na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

Bwana akubariki sana.Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

UKIAMINI NA UKIMKIRI YESU KWA KINYWA CHAKO, UTAOKOKA.

NJIA YA MSALABA

IKO NJIA IONEKANAYO KUWA SAWA MACHONI PA MTU.


Rudi Nyumbani

Print this post

JE! UNAMPENDA BWANA?

Bwana Yesu alisema “MTU AKINIPENDA  ATAZISHIKA AMRI ZANGU (Yohana 14:15)” lakini tunaona hiyo pekee haitoshi kwasababu kama  ingekuwa inatosha Bwana asingemwambia tena Mtume Petro mahali pengine  maneno haya…

Yohana 21:15 “ Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia , Naam ,Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu.
16 Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu.
17 Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu.

Kwahiyo tunaona licha ya kuzishika amri zake, kuna mambo mengine matatu ya yatakayokamilisha upendo wetu kwa Kristo.  Nayo ni (1) KULISHA WANA-KONDOO WAKE, (2) KUCHUNGA KONDOO ZAKE (3) KULISHA KONDOO ZAKE.

KUZISHIKA AMRI:

Kuzishika Amri za Mungu ni kuzielewa, kuzipenda na kuziishi, na sio kuzikariri  na yeyote aziishie amri za Mungu  amri hizo zinapaswa zisiwe nzito kwake, Maagizo ya Mungu yanapaswa yawe ni mepesi kwake kuyashika kwasababu Roho wa Mungu anakaa ndani yake, hivyo Nira ya Kristo kwake inakuwa ni laini, na mzigo unakuwa mwepesi,hajisikii uzito wala hajilazimishi kuzitimiza sheria za Kristo ndani yake..

Hatatumia nguvu nyingi kujizuia kutenda dhambi, hivyo anakuwa anazitimiza pasipo kujiweka katika utumwa, hawi chini ya utumwa wa sheria, kwasababu Nia ya Mungu sio sheria zake ziwe mzigo mzito kwetu, nia yake sio tuzishike amri zake kwa uchungu na mateso na utumwa ..hapana na ndio maana alisema katika..

Kumbukumbu 30: 10 “ukiwa utaifuata sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa kuyashika maagizo yake, na AMRI ZAKE zilizoandikwa katika chuo hiki cha torati; ukimwelekea Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote.

11 Kwa maana maagizo haya nikuagizayo leo, SI MAZITO MNO KWAKO, WALA SI MBALI.

12 Si mbinguni, hata useme, Ni nani atakayetupandia mbinguni akatuletee, aje atuambie tusikie, tupate kuyafanya?

13 Wala si ng’ambo ya pili ya bahari, hata useme, Ni nani atakayetuvukia bahari, akatuletee, aje atuambie, tusikie, tupate kuyafanya?

Unaona ili kuzishika Amri za Mungu,  ni lazima Kuwepo na wepesi ndani yako ambao Mungu ameuweka, ili Sheria zake zisiwe nzito mno kwako. Hivyo kwa kuishi maisha kama hayo ya kutimiza sheria za Mungu pasipo utumwa. Huko ndiko kuzishika Amri za Mungu. Na huko ndiko kumpenda Bwana. Lakini kufanya hivyo pekee hakutoshi kuonyesha upendo wetu kwa Bwana. Lipo jambo lingine la ziada la kufanya ili kutimiza upendo wetu kwake.

Na jambo hilo si lingine zaidi ya kulitazama kundi la Mungu kwa kulilisha na kulichunga.Ndio maana Bwana alimwuliza Petro mara tatu swali lile lile? Je! wanipenda?

 NINI MAANA YA KULISHA KONDOO WAKE:

Kama neno lenyewe lilivyo “kondoo wake”  ikiwa na maana kuwa sio kondoo wa mtu Fulani, bali ni kondoo wa Kristo. Hivyo mtu hawezi kujiamulia tu, njia au namna ya kuwalisha,  kwa lugha nyingine Petro aliambiwa yeye ni  mchungaji aliyeajiriwa kuwachunga na kuwalisha kondoo, hivyo kondoo hata mmoja asipolishwa inavyopaswa ataulizwa na aliyemwajiri, kwasababu kondoo sio wake, bali ni wa mtu mwingine.

Kondoo wanawakilisha watu wa Kristo waliomwamini yeye, na wachache wanaohitaji kumwamini.. hao ndio kondoo wa Kristo, biblia inasema tuwalishe hao, na chakula chao sio nyasi bali ni NENO LA MUNGU lisilochanganywa na chochote..  Kazi kubwa ya mchungaji ni kwenda huku na huko kutafuta mahali penye nyasi zinazowafaa kondoo.. Kadhalika Sisi kama wakristo tuliookolewa tunalo jukumu la kuwaongoza wenzetu, au kuongozana sisi kwa sisi mahali panapopatikana Neno la Uzima.

Ukimwona ndugu yako anahangaika huku na kule, ni wajibu wako kama mkristo kumwelekeza kwa upendo mahali ambapo anaweza kuishibisha nafsi penye Neno la Uzima. Huko ndiko kumpenda Kristo. Maadamu ndani yetu kuna nuru kidogo ambayo haimo ndani yao.

KUCHUNGA KONDOO WAKE.

Kama neno lilivyo “kondoo wake” ikiwa na maana kuwa “sio kondoo wa  mtu fulani” bali ni kondoo wa Yesu Kristo, hivyo hatuwezi kujichagulia njia ya kuwachunga..Tunapokea maagizo kutoka kwake namna ya kuwachunga.

Sasa Bwana Yesu alisema “Tujihadhari na mbwa mwitu wakali” na pia alisema “tujihadhari na mbwa mwitu wanaokuja na mavazi ya kondoo”…Sasa dhumuni la mbwa mwitu kuvaa mavazi ya kondoo ni ili na yeye aonekane kama kondoo ili asitumie nguvu nyingi kuwakamata kondoo. Sasa hao Bwana ndio aliosema tujichunge nao sana, na tukiisha kujihadhari nao, tuwachunge na ndugu zetu dhidi yao.. HUKO NDIKO KUCHUNGA KONDOO WAKE.

Sasa hawa mbwa-mwitu ndani ya mavazi ya kondoo ni wakina nani?

Mathayo 7: 15 “Jihadharini na manabii wa uongo, WATU WANAOWAJIA WAMEVAA MAVAZI YA KONDOO, WALAKINI KWA NDANI NI MBWA-MWITU WAKALI. Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?”

Unaona, Manabii wa uongo ndio mbwa-mwitu ndani ya mavazi ya kondoo.  Na manabii wa uongo sio tu manabii, hapana bali hata waalimu wa uongo, wachungaji wa uongo, watumishi wa uongo, wainjilisti wa uongo, maaskofu wa uongo, mashemasi wa uongo, wapendwa wa uongo, waimbaji wa uongo n.k hawa wote kwa pamoja wanaunda kundi linalojulikana kama manabii wa uongo.

Yaani watu wote ambao kwa nje wanajulikana kama ni wakristo lakini ndani katika maisha yao ya siri sio wakristo hata kidogo, ni watu wa ulimwengu huu, walevi, watukanaji, vuguvugu, waasherati, walaji rushwa n.k…Na bado wanahubiri na kushuhudia na kuimba. Wengine wanajiita PAPA wakiwapoteza watu waabudu sanamu Mungu alizozikataa.Hiyo ndio roho  ya mpinga-kristo.

Hao ndio Bwana, aliotuonya tulichunge kundi lake dhidi yao, ikiwa tumeona mtu ajiitaye mkristo halafu ni mwasherati au mlevi au mwabudu sanamu,tunapaswa tujihadhari naye Hatupaswi kuwashauri watoto wa kiroho(kondoo wa Kristo) kuambatana nao, ni lazima tutawachunga kondoo wa Mungu dhidi yao..Na zaidi ya yote tutawafundisha hila za hao manabii wa uongo, na Roho ya Mpinga Kristo inavyotenda kazi, Biblia inasema

1Wakoritho 5: 9 “Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi.

10 Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang’anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.

11 Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba MSICHANGAMANE NA MTU AITWAYE NDUGU, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.

12 Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu hao walio ndani?

13 Lakini hao walio nje Mungu atawahukumu. NINYI MWONDOENI YULE MBAYA MIONGONI MWENU.”

Hivyo tunapoona ndugu yetu, anapotea na uongo wa adui ni jukumu letu sisi,  kumwokoa, hatuwezi tukasema tunampenda Kristo na tukaacha kulipenda na kundi lake, Popote pale tulipo katika hatua yoyote ile ya kiroho, ni wajibu wetu kuwasaidia walio chini yetu..

Hata katika familia jukumu la kulea watoto sio la wazazi peke yake, lakini utakuja kukuta kwamba hata watoto wana jukumu la kuleana wao kwa wao..kaka au dada anawalea wadogo zake na hao wadogo wanawalea walio wadogo zaidi. Na katika familia ya Mungu ni hivyo hivyo, ndio jukumu tulilopewa kulishana na kuchungana.

Kuchunga kondoo wa Kristo sio jukumu la mchungaji kanisani tu au muhubiri bali ni jukumu la Kila Mkristo.

Bwana atusaidie sote tuweze kumpenda yeye kweli kweli, KWA KUZISHIKA AMRI ZAKE na KULICHUNGA KUNDI dhidi ya mbwa mwitu wakali lake na KULILISHA chakula cha Neno la Uzima.

Mungu akubariki.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine…

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

MAFUNUO YA ROHO.

ITAFAKARI VEMA KAZI YA MUNGU

SADAKA ILIYOKUBALIKA.

JE! MUNGU ATAIANGAMIZA DUNIA TENA BAADA YA GHARIKA YA NUHU?

MANENO HAYA YANA MAANA GANI? “..KWA SABABU HAMTOI ROHO KWA KIPIMO. (YOHANA3:34)”

NI KWA JINSI GANI MUNGU ANAPATILIZA MAOVU YA BABA ZETU SAWASAWA NA KUTOKA 20:5-6?

Je Kauli ya Mungu katika Warumi 11:4 na 1Wafalme 19:18 inajichanganya?.


Rudi Nyumbani

Print this post

KITENDAWILI CHA SAMSONI

Waamuzi 14: 13”……… Basi wakamwambia, Haya, tega kitendawili chako, ili tupate kukisikia. 14 Naye akawaambia, KATIKA HUYO MWENYE KULA KIKATOKA CHAKULA, KATIKA HUYO MWENYE NGUVU UKATOKA UTAMU

Kitendawili hichi Samsoni alisukumwa kukisema baada ya kukutana na tukio la ajabu katika safari yake alipokuwa akishuka kwenda Ufilisti yeye pamoja na wazazi wake kwa ajili ya kumchumbia binti aliyekuwa amemwona huko katika kijiji kimoja kilichoitwa Timna.

Sasa wakati akiwa njiani alikutana na Simba mwenye nguvu ambaye alitaka kumrarua, lakini Samsoni alipomwona alinyanyuka na kumshambulia kama biblia inavyosema jinsi alivyo mpasua haraka sana ni kama vile mtu anavyompasua mbuzi, Samsoni hakutumia silaha yoyote mkononi, ni kitendo kilichochukua sekunde chache tu, na shughuli yote ilikuwa imekwisha, akaendelea na safari yake.,

Hilo lilikuwa jambo la kawaida kwake halikumwingia sana moyoni mwake, lakini jambo lililomshangaza ni baada ya kurudi kutoka huko Timna yeye pamoja na wazazi wake na kukuta ule mzoga wa simba umezungukwa na nyuki wengi sana na ndani yake kuna Asali.

Ni jambo la kushangaza! Hata sisi sote tunajua Moja ya wadudu walio wasafi na hawatui katika vitu vilivyo na uozo au uchafu wowote ni NYUKI. Nyuki huwa utawakuta sana sana kwenye maua, mazuri, na kwenye miti yenye matunda na yenye harufu wakitafuta vimelea vizuri vingi tofauti tofauti kwa ajili ya kutengeneza asali yenye ubora ule tunaouna..

Na kamwe haijajawahi kutokea nyuki kutua kwenye mizoga na miozo, tena cha kushangaza zaidi ndani ya muda ule mfupi kwenye mzoga wa Yule Simba walikuwa tayari wameshatengeneza asali nyingi, na wakati nyuki kutengeneza asali iliyotayari kulika tunajua inachukua sio chini ya miezi 6 na kuendelea.

Hivyo Samsoni kuona jambo lile ilimshtusha sana, mpaka kugundua kuwa lipo somo kubwa ndani yake anapaswa ajifunze, na baada ya kutafakari kwa utulivu sana ndipo akatunga kitendawili kile na kuwapelekea wafilisti.

Akawaambia: “Katika huyo mwenye kula kikatoka chakula, Katika huyo mwenye nguvu ukatoka utamu.(Waamuzi 14:14)”

Samsoni akijua kabisa hakuna hekima yoyote ya kibinadamu inayoweza kukitegua kitendawili kile isipokuwa Mungu au yeye peke yake awafunulie. Na ndio maana ukisoma hiyo habari utaona wale wafilisti walipoona muda wao waliopewa wa kurudisha majibu unakaribia kuisha na bado majibu hawana, wakatumia hila ya kumshawishi Yule binti wa kifilisti aliyekuja kumchumbia amulize Samsoni tafsiri ya kitendawili kile..Na baada ya Yule binti kumbembeleza sana ndipo Samsoni akawafunulia tafsiri yake. Lakini alikasirika sana kwasababu walitumia hila kupata majibu na tafsiri yake ilikuwa ni hii:

Wakamwambia:,NI KITU GANI KILICHO TAMU KULIKO ASALI? NI KITU GANI KILICHO NA NGUVU KULIKO SIMBA?

Kwa lugha rahisi tunayoweza kuielezea kitendawili hicho kwa sasa ni hii “CHAKULA KITAMU KULIKO VYOTE MFANO WA ASALI, HUWA KINATOKA KWA WANYAMA WAKALI NA WENYE VITISHO KAMA SIMBA”…Pia haijabadili maana tukisema “HAZINA KUBWA ZA MAFANIKIO YOTE, HAZIPATIKANI PENGINEPO ISIPOKUWA KATIKA MAZINGIRA YA MAJARIBU MAZITO, AU VITISHO AU MAADUI WAKALI”.

Samsoni hakutazamia kuwa katika yule Simba aliyekuwa anataka kumrarua ndani yake kuna ASALI. Hakutazamia kuwa kutoka kwa Yule adui yake ambaye alikuwa anataka kummeza huyo huyo ndiye atakayeweza kumtolea chakula chake cha kila siku.. Na ndio maana ukisoma habari za Samsoni maisha yake kuanzia huo wakati na kuendelea hakuwahi kuwaogopa maadui zake walipokuja kushindana naye..Ilifika wakati alikuwa anajiona salama zaidi kwenda kulala katikati ya hema za wafilisti [maadui zake] zaidi hata ya alipokuwa nyumbani kwao Israeli ni kwasababu gani? Ni kwasababu alijua kuwa “ katika huyo mwenye kula, ni lazima kitoke chakula tu, na katika huyo mwenye nguvu utatoka utamu nao”.

Ujasiri huo huo aliokuwa ndani ya Samsoni tunaweza kuuona pia ukijidhihirisha ndani ya Manabii wa Mungu miaka mingi baadaye baada ya kufa Samsoni. Ule ujasiri tunauona tena juu ya huyu nabii aliyeitwa ELISHA. Tunasoma habari zake katika 2Wafalme 6. Siku moja mfalme wa Shamu alikasirika sana baada ya kuona siri zake zinafichuliwa na Elisha huko Israeli, Kila alipopanga njama dhidi ya waisraeli Elisha alifunua siri zao na mikakati yao.

Hivyo huyu mfalme wa Shamu akaamua siku moja kupanga majeshi yake yote kuenda kuuhusuru huo mji aliokuwa anaishi Elisha, Na walipoamka asubuhi kumbe jeshi lote la Shamu limewazunguka kama tunavyosoma habari Yule mtumishi wake Elisha aliogopa sana kwasababu alijua siku hiyo ndio mwisho wake umefika, Lakini Elisha alimwambia usiogope simba hawa..Ndipo Yule kijakazi akafunguliwa macho yake na kuona jeshi kubwa la malaika limewazunguka kuwapigania na kuwashindania.

Vivyo hivyo ilitokea wakati huo huo hilo jeshi la shamu liliuzunguka tena mji wa Samaria ili kutaka kuungamiza mji wote na vitu vyao vyote, Elisha naye akiwa humo humo ndani, Hao washami waliuzingira mji wote kwa muda wa siku nyingi, kiasi kwamba hakukuwa hata na mtu wa kuingiza na kutoa chakula mle mjini, matokeo yake kupelekea chakula kupungua sana na uchumi wa mji kuporomoka kwa kiwango kikubwa, njaa ilikuwa kali kiasi kwamba hata mavi ya njiwa yalikuwa ni chakula kinachouzwa kwa kugombaniwa na kwa bei ya juu sana.. Kichwa cha punda nacho kiliuzwa kwa bei ya juu sana, watu walikuwa wanakufa kwa njaa na Elisha naye yupo ndani yake.

Mfalme wa Israeli alipoona Elisha ndiye wakati wa nyuma aliwaombea rehema hao hao maadui zao waliokuja kuwahusu wasiangamizwe, akakasirika sana na kutuma mtu aende kumuua lakini Elisha, hakuwa na wasiwasi wowote wala hofu yoyote, kwasababu alilitambua lile neno kama la Samsoni:

KATIKA HUYO MWENYE KULA, KITATOKA TU CHAKULA, NA KATIKA HUYO MWENYE NGUVU NI LAZIMA UTOKE UTAMU”.

Hivyo Elisha akasubiri mpaka dakika ya mwisho, hakudhubutu kufungua kinywa chake na kumkufuru Mungu kwamba kwanini Mungu amewaacha mpaka wamefikia hatua hiyo? kama walivyokuwa wananung’unika wana wa Israeli kule jangwani. Bali yeye alitulia kimya mpaka Yule mjumbe aliyetaka kuja kumuua alipofika.Na ndipo Neno la BWANA likamjia Elisha na kumwambia Yule mtu.

2Wafalme 7: 1 “Elisha akasema, Lisikieni neno la Bwana; Bwana asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria.

2 Basi yule akida, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia [Elisha], Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula.”.

Unaona? Watu hawakusadiki maneno yale, ni sawa leo hii mtu aseme bei ya gari lililokuwa linauzwa milioni 20 sokoni, kuanzia kesho na kuendelea litakuwa linauzwa kwa shilingi elfu 50…Kwa namna ya kawaida hilo haliwezi kuwezekana, na ndio maana hata Yule mjumbe kutoka kwa mfalme akamdhihaki Elisha na kumwambia hata kama MUNGU angefungulia madirisha ya ngano kutoka mbinguni hilo jambo lisingewezekana..hata kama magari yote ulaya yangetupwa Tanzania kama nguo za mitumba, hilo jambo lisingewezekana unaona?.

Lakini hawakujua kuwa Mungu si wanadamu..Hawakujua kuwa Yule SIMBA aliyekuwa anataka kupambana nao kumbe ndiye aliyewaletea ASALI NYINGI..Wale waliowahusuru pande zote ndio waliowaletea wao chakula.

Angalia jambo Mungu alilofanya. Kumbuka wale nao wasingeweza kuwazunguka wayahudi siku hizo zote bila kuwa na chakula, na nyara, na wanyama wengi na maghala ya nafaka pamoja nao. HIVYO KITU ALICHOFANYA BWANA NI KUWASIKILIZISHA SAUTI YA VITA USIKU WA MANANE, NA VISHINDO VIZITO VYA FARASI NA TETEMEKO la nchi kiasi kwamba wale Washami wakayeyuka mioyo wakidhani kuwa Israeli imekwenda kukodi mataifa jirani ili waje kuwasaidia..Hivyo jambo la haraka haraka ambalo wangeweza kufanya ni kuondoa maeneo yale kwa kasi sana wao kama wao pasipo kuchukua kitu chao chochote.

WALIACHA MAGHALA YAO YA CHAKULA, NYARA ZAO, HAZINA ZAO, FEDHA ZAO, WANYAMA WAO WENGI SANA.

Na asubuhi ilipofika wayahudi walishangaa wasione mtu, hivyo wakaenda kuchukua zile nyara zao zote, chakula siku ile kikawepo kingi kiasi kwamba bei ya chakula ilishuka ghafla na kuuzwa kwa bei ile ile Elisha mtu wa Mungu aliisema. Hivyo njaa iliyoikumba mji ilikoma ndani ya siku moja. Na uchumi wa Israeli wote kunyanyuka ndani ya siku moja.

Ni kwasababu gani? Ni kwasababu Elisha alijua katika huyo mwenye kula, kitatoka tu chakula, na katika huyo mwenye nguvu ni lazima utoke utamu”.

Nataka nikutie moyo wewe uliyeamua kuchukua uamuzi wa kumfuata Kristo kwa gharama zozote zile, usitishwe na majaribu yatakapokujia, usitishwe na hila za maadui, usitishwe na vikwazo, fahamu tu huko ndiko utajiri wako ulipo, huko ndiko chakula chako kilipo.. Wana wa Israeli walipokuwa wanapita katika hali ngumu kwa kitambo tu badala ya kuusubiria wokovu wa Mungu wao moja kwa moja walianza kumnung’unikia kana kwamba Mungu anawatesa..

Na ndio maana Mungu hakupendezwa nao kwasababu walikosa ufahamu kuwa mara nyingine kwa kupitia njia zile ndio Mungu alikuwa anawaletea hazina zao. Wakristo tunaomsubiria Bwana tukijifunza kanuni hizi hatutakuwa watu wa manung’uniko tunapokutana na vikwazo, na maadui badala yake ndio tutafahamu kuwa wakati wa mbaraka wetu ndio umekaribia.

Yusufu alipopelekwa katika gereza la wafalme mahali ambapo alikuwa anasubiria wakati wowote kukatwa kichwa, kama tu vile alivyomtabiria Yule muokaji wa mfalme kuwa atakatwa kichwa si zaidi yeye aliyekuwa anashutumiwa kwa kulala na mke wa mfalme..alifahamu kabisa yupo pale kusubiria siku ya kukatwa kichwa, lakini hakunung’unika na kulalamika akisema ni kwa nini Mungu mimi ninateseka huku muda wote huu angali ninalicha jina lako? Hakudhubutu kusema vile, yeye aliungojea tu kwasababu alitambua kuwa

katika huyo mwenye kula, kitatoka tu chakula, na katika huyo mwenye nguvu ni lazima utoke utamu”. Na tunasoma Kutoka kwa Farao ulitoka utamu.

Na kweli ulipofika wakati, Yule Yule aliyekuwa anamtazamia amuue, alikuja kumfanya kuwa waziri wake mkuu.

Hivyo kaka/dada uliyekombolewa kwa damu ya Bwana Yesu, usihangaike huku na kule jaribu linapotokea mbele yako, wala usilione ni kubwa, tulia na utauona wokovu wa Bwana katikati ya hatari, utiwe nguvu katika jaribu lolote unalopitia siku moja Mungu atakuthibitisha kwasababu huko ndiko kutokako utamu wa maisha yako ya sasa na ya baadaye.
Amen!

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

UKOMA NA UJANE ULIO NDANI YAKO, UMEUPATIA TIBA?

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

USIACHE KUJIFUNZA NENO LA MUNGU

NINI MAANA YA HUU MSTARI “NIMEVIPIGA VITA VILIVYO VIZURI, MWENDO NIMEUMALIZA, IMANI NIMEILINDA”?

NI LAANA IPI HIYO MUNGU ALIMAANISHA ATAIPIGA DUNIA NAYO KATIKA MALAKI 4:5-6?

JE! MWANADAMU WA KWANZA KUUMBWA NI YUPI MZUNGU MWAFRIKA AU MCHINA?


Rudi Nyumbani

Print this post

SIRI YA KUFANIKIWA KWA MTUME PAULO.

Ukisoma biblia kuna maneno  mtume Paulo aliyasema ambayo kwamfano yangetamkwa leo mbele za watu wengi, kimsingi yangeonekana kama ni kufuru. Jaribu kuwazia heshima Mungu aliwayowapa  mitume wake  12, hata kabla hawajaanza  kutumika  Mungu aliwaandaa kwa muda wa miaka 3,ukizingatia maandalizi yao hayakuwa kama haya ya kwetu, wao walipewa nafasi ya juu sana ya kipekee ya kuishi, kula, kulala na mkuu wa uzima mwenyewe kwa muda wa miaka mitatu na nusu.

Watu ambao Kristo mwenyewe alisema wamesha kuwa safi kwa lile Neno alilokuwa anawafundisha (Yohana 15:3), watu ambao Yesu aliyewatawaza mwenyewe na kuwatia mafuta wawe misingi ya Kanisa lake takatifu lililohai, Watu waliokuwa wamejaa Roho wa Mungu wenye sifa, na vyeo, walioheshimiwa na kuogopwa na kila mtu katika kanisa la Kristo mitume 12 wa Bwana.


Lakini ilifika wakati  siku moja mkristo mmoja aliyechipukia chini asiyejulikana sana ambaye hata hakuwepo siku ya Pentekoste anasimama kwa ujasiri na kuyaeleza makanisa  hakuna kitu cha ziada alichokiona wanacho zaidi yake yeye, licha ya kuwa na sifa nyingi katikati ya watakatifu lakini bado anasema wote wao ni mamoja kwake,. Habari Hiyo Tunaisoma katika..

 Wagalatia 2:6 “Lakini wale wenye sifa ya kuwa wana cheo; (walivyokuwa vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwanadamu); nasema, hao wenye sifa hawakuniongezea kitu; 

7 bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili ya wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa;

 8 (maana yeye aliyemwezesha Petro kuwa mtume wa waliotahiriwa ndiye aliyeniwezesha mimi kwenda kwa Mataifa); 

9 tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;”

Unaweza ukajiuliza  ni kwanini mtume Paulo alisema vile?, unadhani ni kwa kuonyesha kiburi chake kwa kufanikiwa kwake au vinginevyo?, jibu ni hapana lakini aliuzungumza ukweli wote katika Kristo, kwamba Mungu hapokei uso wa mwanadamu yoyote na ndivyo ilivyo. Kama biblia inavyosema katika

Matendo 10:34 “… Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; 

35 bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.”

Mtume Paulo alionyesha kuwa sio cheo, wala maono,wala karama wala sifa yoyote ile itokayo kwa Mungu au kwa mwanadamu ndiyo kiashiria cha mtu huyo kuwa analo daraja kubwa mbele za Mungu, na kwamba hakuna yeyote atakayeweza kuwa juu yake kisa tu kaitwa  na Mungu.. Ilifikia wakati Mtume Paulo kwa neema za Mungu alizopewa alijishuhudia katika Roho kuwa kati ya waliomtangulia hakuna aliyetenda kazi zaidi yake yeye. ( 1Wakorintho 15:10), Leo  tunaweza kujifunza machache juu ya matukio ya mitume yaliyorekodiwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume.

MATENDO YA MITUME:

Ndugu kitabu cha Matendo ya mitume, unajua ni kwanini kiliitwa vile?. Kilitwa vile kwasababu Ule ulikuwa ni uwanja wa mapambano katika roho kati ya mitume wa Kristo wote waliokuwepo kwa wakati ule, Kila mmoja akionyesha matendo ya Imani yake katika mashindano yaliyokuwa yamewekwa mbele yake.Lakini kama ukichunguza kwa makini utaona mwanzoni kabisa mwa sura za mwanzo za kitabu kile,

Ulikuwa unaweza kusoma habari za watu wengi na watakatifu wengi, na ushujaa wao wote waliokuwa wanaufanya, pamoja na habari za mitume mbalimbali wa Kristo, utaona kulikuwa na watu 500 waliotokewa na Kristo baada ya kufufuka kwake  kama alivyotokewa mtume Paulo,Ambao Bwana alifanya makusudi kujidhihirisha kwao ili wakawe mashuhuda wa kutangaza habari ya kufufuka kwake, utawaona pia wale watu 120 waliokuwako siku ile ya Pentekoste, utamwona Filipo,akitenda kazi ya Mungu kwa bidii, kadhalika utaona  habari ikirudi tena kwa Yohana, Utamwona Barnaba, utamwona Stephano, utamwona Petro, utawaona wakina Prisila na Akila, utamwona Anania, Apolo, utamwona nabii Agabo, Marko, Sila, luka, na wengineo.

Na kila mmoja ambaye habari zake zilisikika,  Mwandishi aliyevuviwa na Roho aliyekiandika  kitabu kile cha matendo ya mitume aliziweka habari zake, hakukuwa na upendeleo wowote. Na ndio maana ukichunguza mwanzoni walianza wengi kwa moto, habari za kila mmoja zikawa zinagusiwa, mara huyu, mara  Yule, lakini ukizidi kuendelea mbele kuanzia sura ya 13…mpaka ya mwisho kabisa wa sura ya 21 utaona ni Paulo tu peke yake ndiye anayezungumziwa kana kwamba hakukuwa na wengine wanaofanya ziara au wanaotenda kazi ya Mungu.

Sio kana kwamba hawakuwepo, walikuwepo, lakini aliyeonekena anapiga mbio zaidi ndio habari yake iliyopewa uzito mkubwa zaidi kuandikwa. Ni kama leo tu kwamfano  ukiangalia kwenye TV labla wanariadha wanaoshiriki katika michezo ya kukimbia umbali wa km 40, utaona kwa pale mwanzo  kamera haimlengi mtu Fulani mmoja maalumu, bali watu wote, kwasababu bado haijajulikana mshindi atakuwa ni nani, hivyo Yule anayeonekana inaongoza wenzake kamera itamchukua,

Kadhalika akipitwa tu kidogo kamera itahahamia kwa mwingine hivyo hivyo. Lakini ukiangalia wakishafika labda km ya 30 kuelekea 40 hapo wameshaachana nafasi kubwa sana, utaona kamera inamchukua tu Yule wa kwanza peke yake mpaka anapokwenda maliza. Kana kwamba ni yeye tu ndiye anayeshiriki michezoni lakini ukweli ni kwamba huko nyuma kuna umati wa mamia ya watu nao pia wanapiga mbio isipokuwa wameachwa nyuma sana.

Na ndivyo ilivyokuwa katika kitabu cha matendo ya mitume, Walianza wengi, lakini aliyemaliza ni mmoja. Naye si mwingine zaidi ya Mtume Paulo. Sio kana kwamba yeye alikuwa na kitu cha ziada sana zaidi ya wale wengine hapana, walikuwepo watu 500 waliotokewa na YESU kama yeye, na wengi wao walikuwepo siku ya Pentekoste na pengine hata kabla ya hapo, Bwana alitazamia na wao pia wapige mbio lakini kilichomtofautisha Mtume Paulo na wengine ni kwamba yeye alikuwa akimwomba Mungu neema na akionyesha bidii katika Bwana.

Lakini mambo hayo yanatufundisha nini?. Hayo yalitendeka katika kanisa la kwanza, lakini pia  lilikuwepo kanisa la pili na la tatu na la nne mpaka la mwisho la saba ambalo ndilo hili tunaloishi mimi na wewe, na kila kanisa linao mitume wake [watumishi wa Mungu],  nao pia kitabu cha matendo yao kinaandikwa mbinguni wanarekodiwa wanaopiga mbio,

Lakini swali je! Ni nani atakayemaliza na ushindi kwa Laodikia?.. Ni William seyomor, mwanzilishi wa kanisa la Pentekoste, ni Billy Granham? ni Oral Robert, ni WILLIAM BRANHAM mjumbe wa Kanisa la LAODIKIA? Ni TL Osborn Ni Hellen white? Ni Kulola, ni Kakobe, ni mchungaji wako, mwalimu wako wa madarasa ya jumapili? au ni WEWE?..

Hakika unaweza ukawa ni wewe.

Wote wanaodai walitokewa  na YESU na kupewa huduma kubwa wawe ni mamoja kwako, kwasababu wapo sio tu kutokewa , bali pia kuishi naye na kulala naye lakini bado walipitwa katika mbio, wanaodai wameonyeshwa maono makubwa sana watakuwa ni wainjilisti wa kimataifa wawe ni mamoja kwako, walio na sifa kubwa katika taifa na kanisa kuwa ni watumishi wa Mungu wawe ni mamoja kwako, wanaojulikana kuwa ni wajumbe wa makanisa na manabii wa vizazi wawe ni mamoja kwako Mungu hapokei uso wa mwanadamu.

Tujifunze kwa Mtume Paulo mtu ambaye hapo mwanzo aliuharibu uzima wake kuliko watu wote, lakini baada ya kutubu kwake alisimama na kuanza upya na kushinda kuliko wote  waliomtangulia yeye alisema maneno haya:

1Wakorintho 9: 23 “Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine. 

24 Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate. 

25 NA KILA ASHINDANAYE KATIKA MICHEZO HUJIZUIA KATIKA YOTE; BASI HAO HUFANYA HIVYO KUSUDI WAPOKEE TAJI IHARIBIKAYO; BALI SISI TUPOKEE TAJI ISIYOHARIBIKA. 

26 Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; 

27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa”.

Alisema pia..

2 Timotheo 2: 4 “Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari. 

5 HATA MTU AKISHINDANA KATIKA MACHEZO HAPEWI TAJI, ASIPOSHINDANA KWA HALALI. 

6 Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza wa kupata fungu la matunda. 

7 Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote.”

Je! Mambo ya dunia bado yanakusonga na huku bado unataka ufanikiwe zaidi ya hao mashujaa wa imani Hilo wingu kubwa la mashahidi lililotutangulia lililonenwa katika Waebrania 12 wanapaswa wawe mamoja kwetu?. Weka kando mizigo yote ya dhambi chini, tubu dhambi zako anza kumwangalia Bwana kwasababu ushindi hakika utaupata kama ukishindana kihalali.

Waebrania 12:1 “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu, 

2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.”

Ubarikiwe sana.

Tafadhali “share” kwa wengine ujumbe huu.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

SIKU ZA MAPATILIZO.

WEWE NI HEKALU LA MUNGU.

ALITOKA HUKO, AKAENDA MAHALI KARIBU NA JANGWA.

MARIAMU

Podo ni nini na umuhimu wake ni upi rohoni?

JE! KUSHIRIKI AU KUJIHUSISHA KWENYE MICHEZO NI DHAMBI?

Tofauti kati ya mbinguni, peponi, Kuzimu, Jehanamu, na Paradiso ni ipi?

JE! NI DHAMBI KWA KIJANA ALIYEOKOKA KUVAA SURUALI ZA KUBANA (MODEL), KUNYOA MITINDO?


Rudi Nyumbani

Print this post

JINA LAKO NI LA NANI?

Bwana Mungu alipowaumba Adamu na Hawa, tunafahamu hakuwaumba wote kwa wakati mmoja, bali alianza kumuumba Adamu kwanza kisha Hawa baadaye, Ndoa ya Adamu na Hawa  ndio ndoa ya kwanza  kabisa kufungishwa, na ilifungishwa na Mungu mwenyewe.

Lakini jambo la kujifunza mara tu baada ya mtu wa kwanza kuumbwa Bwana Mungu, alimpatia jina “Adamu” na baadaye alipomfanya Hawa kutoka katika ubavu wa Adamu hakumpatia jina lolote lile badala yake Adamu ndiye aliyekuja kumpatia jina mkewe na kumwita Hawa..kwasababu alisema yeye ndiye mama wa wote walio hai (Mwanzo 3:20), Lakini jina hilo Hawa halikutoka kwa Mungu bali kwa Adamu. Kwanini Mungu hakumpa Hawa jina hilo tutakuja kuona sababu tutakavyozidi kusoma.

Lakini hebu tutazame kwa ufupi nguvu iliyopo katika jina, katika maisha ya kawaida ukilitaja jina la Raisi wa nchi ni tofauti na jina la Waziri wa nchi, na ni tofauti na jina  la mbunge au balozi, kila jina lina nguvu yake na heshima yake. Jina lenye cheo kikubwa ndilo lenye  nguvu zaidi na heshima kubwa zaidi.

Barua ikiandikwa kwa jina la Raisi itaheshimika zaidi kuliko  ikiandikwa kwa jina la Balozi.  Kadhalika biashara yenye jina kubwa ni raisi kupata mapato mengi kuliko, yenye jina lisilojulikana, Kwahiyo unaweza ukaona kuwa jina la mtu au kitu au bidhaa linaweza likabeba nguvu kubwa sana ndani yake.

Sasa Bwana Mungu alimpatia jina mtu wa kwanza, akamwita ADAMU, jina hilo lilikuwa na nguvu ya kutosha na heshima ya kutosha ya kuweza kutiisha na kumiliki fahari  na milki zote za mwilini na za rohoni Bwana Mungu alizompa Mwanadamu. Na ndio maana tunaona mwanamke hakupewa jina lingine lolote na MUNGU,  lilikuwa ni jina moja tu walilopewa na Mungu Adamu na Mkewe, liwapasalo wao kufanyia mambo yote. Tunaweza tukasoma jambo hilo katika kitabu cha Mwanzo..

Mwanzo 5:1-2 “Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; 

2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki AKAWAITA JINA LAO ADAMU, siku ile walipoumbwa.”

Unaona hapo? Akawaita jina lao ADAMU!!, hakumuita mwanamume peke yake ADAMU bali pia alimwita mwanamke ADAMU. Ikiwa na maana kuwa ni Jina moja tu walilopewa liwapasalo wao kutawala na kumiliki milki zote za ulimwengu huu. Heshima yao na nguvu yao ilikuwa ndani ya hilo jina.  Jina Hawa lilitoka kwa Adamu tu kama utambulisho kwa mkewe, lakini mbele za Mungu jina lao lilikuwa ni moja tu nalo ni ADAMU!

Lakini tunaona baada ya Adamu na mkewe kuasi kwa kutokutii maagizo ya Mungu, na kula matunda  waliyoagizwa wasiyale, heshima yao ilishuka, wakafukuzwa  kutoka katika ile bustani ya Edeni. Na hapo ndipo jina lao likashuka thamani. Nguvu ya lile jina ikashuka. Hata simba akawa hamwogopi tena mwanadamu, baadhi ya wanyama badala ya kumwogopa na kumkimbia mwanadamu, wakaanza kutafuta  kumla, ardhi badala imzalie Adamu na mkewe vyakula vizuri ikaanza kumzalia michongoma na miiba n.k

Hivyo Heshima ya mwanadamu ikapotea, na Bwana Mungu kwa kulijua hilo na kwa kumuhurumia mwanadamu, akamleta Adamu wa pili, ambaye angempa jina lisiloweza kuharibika, ili kwa jina hilo aweze kurudisha heshima na milki zote ambazo mwanadamu wa kwanza kazipoteza,

 Adamu huyu wa pili naye pia anaye mke wake aliyetwaliwa kutoka ubavuni mwake lakini mke wake sio wa mwilini bali wa rohoni.  Na Adamu huyu wa pili ni YESU KRISTO ambaye mkewe wake NI KANISA LAKE TEULE ALILOLITOA KUTOKA UBAVUNI MWAKE PALE KALVARI, walipomchoma mkuki ubavuni kulitoka MAJI na DAMU, ikifunua kuwa kanisa lake linazaliwa kwa DAMU YAKE iliyomwagika pale Kalvari na Linazaliwa kwa MAJI..Haleluya..

2Wakorintho 11: 1 “Laiti mngechukuliana nami katika upumbavu wangu kidogo! Naam, mchukuliane nami. 

2 Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; KWA KUWA NALIWAPOSEA MUME MMOJA, ILI NIMLETEE KRISTO BIKIRA SAFI. 

3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo”.

Unaona hapo? Na kama vile Mungu hakumpa mkewe Adamu jina lingine vivyo hivyo na Mke wa Bwana Yesu Kristo hakupewa jina lingine lolote isipokuwa jina la Yesu.

Matendo 4: 12 “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, KWA MAANA HAPANA JINA JINGINE CHINI YA MBINGU WALILOPEWA WANADAMU LITUPASALO SISI KUOKOLEWA KWALO”.

Hivyo jina la bibi-arusi(mke) wa Yesu Kristo linalojulikana mbinguni ni moja tu nalo si lingine zaidi ya YESU. Ndilo alilopewa na Baba,  Yohana 17: 6 “Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika”.

Ukisoma Yohana 1:25-26 utaona tena jambo hilo:

 “Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma. Nami naliwajulisha JINA LAKO, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.”

Hivyo malaika au mapepo wakimwona bibi-arusi wa Kristo popote  pale ni sawa na wamemwona Yesu Kristo mwenyewe, Sasa Katika hilo Jina bibi-arusi wa Kristo anaokolewa,  hilo hilo anabatiziwa, anaponywa magonjwa yake, anafanya miujiza yote na zaidi ya yote amepewa mamlaka ya kufanya chochote  atakacho kwa jina hilo.

Wakolosai 3.17 “na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote KATIKA JINA LA BWANA YESU, MKIMSHUKURU MUNGU BABA KWA YEYE”.

SASA BIBI-ARUSI WA KRISTO NI NANI?

Bibiarusi wa Kristo ni mtu yeyote aliyemwamini na kumkubali Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yake, aliyetubu dhambi zake zote kwa kumaanisha kuziacha, na kusafishwa kwa DAMU yake na kusafishwa kwa MAJI ambalo ni Neno lake, ambao ni UBATIZO wa Maji MENGI katika Jina LAKE, yule anayeishi maisha matakatifu na ya kujichunga wakati wote huyo ndiye bibi-arusi wa Bwana Yesu au mke wa mwanamkondoo.

Je! wewe ni bibi-arusi wa Kristo? Kumbuka huwezi ukamiliki chochote kama jina lako halijabadilishwa, je! mbinguni unajulikana kama nani? Adamu na Mkewe walijulikana kama ADAMU, Kadhalika Kristo na wateule wake wanajulikana kwa jina moja nalo ni Jina la Yesu, je! na wewe ni miongoni mwa kundi  lililobadilishwa jina na kupewa jina la Yesu?? kama hujazaliwa mara ya pili na kuwa bibi-arusi wa Kristo huwezi kuwa na jina hilo. Heshima yako katika ulimwengu wa roho bado haipo,hofu itakusumbua,  magonjwa yatakutesa, nguvu za giza zitakutesa, mauti itakuandama, na mambo yote mabaya yatakuwa sehemu yako. Kwasababu haupo chini ya Jina moja lililoadhimishwa na Mungu kwa ukombozi.

Wafilipi 2: 9 “Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, AKAMKIRIMIA JINA LILE LIPITALO KILA JINA;  ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;”

11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.”

Ni maombi yangu kuwa huyu Bwana Yesu, asikupite leo hii, kama hujampokea Yeye umpokee leo, ayageuze maisha yako, na akuingize katika milki ya watu wa Mungu, na kwa jina lake akulinde, upate ushindi angali muda bado upo. Kwasababu jina hilo ni ngome IMARA. Kumbuka Jina la YESU linakaa ndani yako na sio ulimini mwako. Likiwepo humo basi lolote utakalolitamka kwa ulimi wako litafanikiwa sawa na mapenzi yake. Lakini ikiwa hautaokolewa au upo vuguvugu jina la YESU halina nguvu yoyote ndani yako.

Ubarikiwe sana.

Group la whatsapp Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine na Mungu atakubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

JE! MWANADAMU WA KWANZA KUUMBWA NI YUPI MZUNGU MWAFRIKA AU MCHINA?

NI RAHISI KWA NGAMIA KUPENYA KATIKA TUNDU LA SINDANO, JE! NI SINDANO IPI HIYO INAYOZUNGUMZIWA?

JE! MABALASI BWANA ALIYOYATUMIA KUGEUZIA MAJI KUWA DIVAI, YALITUMIKA TU KWA KAZI HIYO?

LENGO LA SHETANI KWA WATOTO WA KIZAZI HIKI.

UKOMA NA UJANE ULIO NDANI YAKO, UMEUPATIA TIBA?

MKUMBUKE MKE WA LUTU


Rudi Nyumbani

Print this post

TUNAYE MWOMBEZI.

Maombolezo 3:22 Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.
23 NI MPYA KILA SIKU ASUBUHI; Uaminifu wako ni mkuu.
24 Bwana ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, Kwa hiyo nitamtumaini.

Jina la Bwana na mwokozi wetu YESU KRISTO lihimidiwe milele. Leo ni siku mpya ambayo Bwana aliibuni tangu zamani kwa ajili yangu mimi na wewe ili tuiishi, tulipoamka asubuhi leo tumebahatika kupewa neema ya kusikia sauti nzuri ya milio ya ndege ikimsifu Mungu kwa furaha mitini, Tukikumbuka kuwa Leo tu ya tarehe hii yenyewe zaidi ya watu 151,600 watakufa ulimwenguni kote hiyo ni kulingana na takwimu za sensa ya dunia, lakini mimi na wewe Bwana ametukirimia neema zake za kipekee, sio tu kuamka salama bali pia kupata nafasi ya kufungua simu zetu na kuingia mitandaoni na kutazama yaliyojiri huko, mpaka unapokutana na ujumbe huu..

Unadhani utakuwa umefanya jambo gani jema mbele za Mungu mpaka uifikie siku ya leo?. Jaribu kufikiri juu ya hilo, je! Ni utakatifu wako?, je! Ni kwasababu unayo afya? Je! Ni kwasababu wewe ni kijana?.

Utagundua ni huruma tu za Bwana kwamba hatuangamii..Mungu anatuhurumia ndugu yangu, rehema zake ikishaitwa tu LEO asubuhi zinakuwa mpya tena kana kwamba hazikuwepo jana na juzi, zinakuwa mpya kama vile leo ndio mara ya kwanza kuachiliwa juu yetu..Mara nyingi tunamkosea Mungu wetu kwa namna zote lakini REHEMA zake ni nyingi kwa watu wote. Yaani Kwa waliookolewa na kwa wale ambao hawajaokolewa, wote rehema za Mungu zinakaa juu yako kwasababu yeye mwenyewe alisema anawaangazia jua na kuwanyeshea mvua yake wote waovu na wema.

Hivyo kwa sisi TULIOOKOLEWA pale tunapokaribia kuzama katika maji ya mauti kutokana na mapungufu yetu au madhaifu yetu na majaribu mazito hakika tunaye mwombezi wetu naye ni YESU KRISTO Bwana wetu, yeye pekee ndiyo hiyo hizo REHEMA YA MUNGU KWETU, na HURUMA yake Mungu kwetu. Biblia inasema katika

1Yohana 2:1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki…

Unaona yeye Bwana kila ikiitwa Leo anatupelekea dua zetu kwa Baba, hakika sifa na heshima na utukufu tunamrudishia yeye kwa upendeleo huu wa ajabu..Na kama sio yeye leo hii sisi tunaoitwa watakatifu tungeshaangamia siku nyingi. Siku ile tungewezaji kusimama kwa hoja yetu?. Hakika Wana AMANI tele wote walio katika Kristo YESU siku zote. Haleluya.

Lakini kwa ambaye hajaokolewa naye pia rehema za Mungu zipo juu yake: Lakini ni kwasababu gani haangamii?. Sio kwamba Bwana YESU yupo anamwombea juu mbinguni hapana?, yeye hilo halimuhusu kwasababu wakati Bwana angali akiwa hapa duniani hakudhubutu kufanya jambo kama hilo kwa yeyote Yule asiyeupande wake bali yeye mwenyewe alisema katika Yohana 17: 9 “Mimi nawaombea hao; SIUOMBEI ULIMWENGU; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako;”.

Unaona hapo mtu mwenye dhambi haombewi lolote na Bwana YESU, ni mtu aliye katika hukumu siku zote akisubiria siku ile kusimama mbele ya kiti cheupe cha enzi cha Mungu ahukumiwe kisha atupwe katika lile ziwa la moto, lakini kama ni hivyo basi ni kwanini haangamii?.Ni kwanini mpaka leo anaishi, anapumua, ana afya, anafanikiwa, angali YESU hamwombei juu mbinguni?. Ni kwanini mpaka leo shetani hatamwangamiza?

Ni kwasababu moja tu ambayo hiyo tunayoisoma katika,

Ezekieli 33: 11 Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli?

Ezekieli 18: 23 Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi?

Unaona ni kwasababu gani huangamii ewe mtu mwovu?..Ni kwasababu Rehema za Bwana zimekushikilia mpaka sasa ili UTUBU. Unafahamu kabisa maisha unayoishi nje ya Kristo huna raha nayo,unastahili kwenda kuzimu, lakini bado unazidi kuishi hivyo!, unafahamu kabisa uzinzi na ukahaba unaoufanya utakupeleka jehanum lakini bado unazidi kudumu katika mambo kama hayo, unafahamu kabisa ukiwa nje ya YESU KRISTO hutaweza kusalimika, hutaweza kuikwepa hukumu ya Mungu, lakini ni kwanini unaendelea kufanya hivyo?. Idadi kubwa ya watu wanaokufa leo haumo katikati yao, unadhani hao waliokuwa na dhambi nyingi sana kuliko wewe?.

Siku ya leo ni mpya, rehema za Bwana zipo juu yako, zikikuvuta utubu, lakini usipofanya hivyo leo, ipo siku mauti itakukuta kwa ghafla na kule uendapo utaufichia wapi uso wako? utakuwa ukijutia siku zile zote neema ya Mungu ilipokuwa inakupigia kelele masikioni kila siku asubuhi utubu lakini hukutaka. Yatakuwa ni majuto makubwa kiasi gani?

Ndugu kwa haya maneno machache, ikiwa Kristo hayupo ndani yako leo, fanya uamuzi wako binafsi sasa. Unachopaswa kufanya ni wewe mwenyewe utubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kabisa kuziacha, uamue kabisa kuanzia sasa unaanza maisha mapya ndani ya Kristo YESU. Kumbuka toba ni kugeuka na sio kuongozwa sala Fulani tu. Wewe peke yako chukua uamuzi wa kugeuka hiyo ni bora zaidi ya sala yoyote unayoweza kuongozwa, na ikiwa toba yako imetoka moyoni kweli kweli na sio kidesturi za kidini au kimazoea. Basi uwe na uhakika Bwana amekusamehe.

Lakini hiyo peke yake haitoshi, Biblia inasema “aaminiye na KUBATIZWA ataokoka (Marko 16:16)”. Hivyo unaukamilisha wokovu wako kwa kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na uwe katika jina la YESU KRISTO..hapo utakuwa na uhakika wa kupata ondoleo la dhambi zako, na kisha kuanzia huo wakati Bwana atakupa Roho wake MTAKATIFU akulinde mpaka siku ya ukombozi wa mwili wako, yaani unyakuo (Matendo 2:38).

Kumbuka ubatizo sahihi ni muhimu, ikiwa ulibatizwa ulipokuwa mchanga, au ulibatizwa kwa kunyunyiziwa maji, au ulibatizwa kidini tu, au kimazoea na haukutubia dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha siku ulipobatizwa, basi ni sharti ukabatizwe tena kwa ubatizo wa maji tele na kwa jina la YESU KRISTO, na sio kwa jina la Baba na mwana na Roho Mtakatifu kama inavyofanyika kimakosa kwa watu wengi, bali kwa jina lake Yesu Kristo ili upate ondoleo la dhambi zako, Hiyo ni kulingana na vifungu hivi vya maandiko (Mdo 2:38, mdo 8:16, ,mdo 10:48, na mdo 19:1-5).

Hivyo ukiwa utazingatia hayo yote, na kuyaishia maisha matakatifu Bwana akubariki kwa kuwa hapo utakuwa umezaliwa mara ya pili. Na ndio kuanzia huo wakati wewe nawe unakuwa na MWOMBEZI mbinguni, ambaye hapo kwanza haukuwa naye..Naye si mwingine zaidi ya BWANA YESU KRISTO kuhani wetu mkuu aliyetupatanisha sisi na Mungu kwa damu yake. Utukufu na heshima na enzi vina yeye milele na milele AMINA.

Ikiwa utatenda dhambi pasipo kujijua, au dhambi ya kutokukusudia au dhambi ya madhaifu yeye yupo siku zote kukuombea mbele za BABA, akulinde na Yule mwovu kwa Kuwa Kristo ameshakuwa mtetezi wako basi mbele za Mungu ukiwa chini hiyo neema hauhesabiwa kuwa na hatia makosa yako yanasitiriwa kwasababu rehema zake hazitakoma juu yako milele na milele. Na hatuhesabiwi haki kwa matendo ya sheria bali kwa Neema;

Ndio lile neno lililosemwa na manabii hapo linatimia..

Warumi 4:6 “uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo,

7 Heri waliosamehewa makosa yao, Na waliositiriwa dhambi zao.

8 Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi.”

Hivyo ubarikiwe wewe uliyechagua uamuzi huu bora wa kumwamini YESU KRISTO.

Tafadhali “share” habari hizi kwa wengine.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU.

UZAO WA NYOKA.

MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.

JE! KUSHIRIKI AU KUJIHUSISHA KWENYE MICHEZO NI DHAMBI?

JE! NI DHAMBI KWA KIJANA ALIYEOKOKA KUVAA SURUALI ZA KUBANA (MODEL), KUNYOA MITINDO?

JE! MBINGUNI KUTAKUWA NA KULA NA KUNYWA?. KWANINI, TUIMBE, JE! KUNA ULAZIMA WOWOTE WA KUFANYA HIVYO?


Rudi Nyumbani

Print this post