ALITOKA HUKO, AKAENDA MAHALI KARIBU NA JANGWA.

ALITOKA HUKO, AKAENDA MAHALI KARIBU NA JANGWA.

Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, utukufu na heshima vina yeye milele na milele, amina. Karibu tuyatafakari maneno yake, maadamu siku zenyewe zimekaribia kuisha.

Ukisoma vitabu vya injili utaona jambo la kushangaza sana kuhusu Bwana Yesu. Utaona kuna wakati alikuwa anatembea kwa wazi kabisa katikati ya wayahudi, utalithibitisha hilo katika maneno yake mwenyewe aliyomwambia kuhani mkuu  katika Yohana 18:20, kupindi kifupi kabla ya kusulubiwa, Lakini kuna wakati hakutembea kwa wazi hata kidogo, bali alikwenda mbali na makazi ya watu, karibu na jangwa, akakaa huko yeye peke yake Pamoja na wanafunzi wake tu.

Yohana 11:53 “Basi tangu siku ile walifanya shauri la kumwua.

54 Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi; bali alitoka huko, akaenda mahali karibu na jangwa, mpaka mji uitwao Efraimu; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake”.

Unaweza ukajiuliza kwanini Bwana Yesu aonyeshe tabia kama hii? Ili hali alikuwa na uwezo wa kuishi analivyopenda Bila wasiwasi wowote, kwasababu Baba yake alikuwa Pamoja naye kumpigania na kumshindania asiuliwe kabla ya wakati?

Hiyo ni kutuonyesha kuwa, Kristo, hana utawala wa mabavu, ukimkataa, atakwenda mbali na wewe, na hutamwona haijalishi utamtafuta vipi. Ni jambo ambalo linaendelea sasa hivi katika roho ulimwenguni. Bwana Yesu anaulilia ulimwengu, lakini ulimwengu ndio kwanza unaipinga injili yake, unataka kuiua kabisa isiwaokoe watu.

Tukiona hivi tujue kabisa  Bwana ameshakwenda mbali na watu wa ulimwengu huu, kujificha. Siku hizi kupokea wokovu wa kweli ni ngumu kuliko ilivyokuwa zamani, kwasababu Kristo hapatikani tena kwa uwazi. Na ndio maana, utaona watu wengi wanasema wameokoka, lakini huoni nguvu za wokovu ndani yao..Si jambo la kawaida!!

Bwana huwa anajificha..

Yohana 12:36 “Maadamu mnayo nuru, iaminini nuru hiyo, ili mpate kuwa wana wa nuru. Hayo aliyasema Yesu, akaenda zake, akajificha wasimwone“.

Ukirudi katika maandiko, utaona tena, alipokuwa Galiliya, alipita katikati yao lakini hakutana mtu yeyote ajue kuwa yupo mjini, bali alipita kimya kimya, akawa anawafundisha wanafunzi wake tu.

Marko 9:30 “Wakatoka huko, wakapita katikati ya Galilaya; naye hakutaka mtu kujua.

31 Kwa sababu alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake, akawaambia, …”.

Hata sasa, Yesu anachofanya ni kujidhihirisha kwa watu ambao ni wanafunzi wake tu, usipofanyika mwanafunzi wa Yesu siku hizi za mwisho ni ngumu kuushinda ulimwengu. Mwanafunzi kulingana na (Luka 14:33), ni mtu ambaye amejikana nafsi na kudhamiria kweli kweli kumfuata Yesu.

Ukiwa tutakuwa na wokovu wa midomoni tu, na kusema tumeokoka, Na huku Maisha yetu yapo mbali na Kristo, tusijidanganye, bado hatujakutana na Bwana Yesu. Bali tumemsikia tu kwamba yupo.

Ndugu yangu hizi ni siku za mwisho, Bwana yupo kweli duniani anaokoa watu..Lakini si wote, anawatembelea watu, bali walio wanafunzi kwelikweli. Kuiona miujiza ya Yesu, kusikia injili, kwenda kanisani hakukufanyi uwe umeshamwona Yesu..Hivyo tuitambue tabii hii pia ya Bwana Yesu ili tuepukane na kujificha kwake, kwasababu anafanya hivyo sasa katika roho.

Kama hujaokoka, au ulikuwa unaishi Maisha ya uvuguvugu, yaani Maisha nusu nusu kwa Mungu basi fanya uamuzi wa kumgeukia sasa kwa  moyo wako wote, huku umejikana nafsi yako. Na Bwana Yesu atajidhihirisha kwako. Na atakusaidia kuushinda ulimwengu na kuishi Maisha ya utakatifu.

Ubarikiwe.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

FANYA KAMA UONAVYO VEMA.

KUNA WAKATI YESU ATAPITA NA WATU HAWATAJUA.

UVUVI BORA HAUCHAGUI, CHA KUVUA.

Je! Bwana Yesu alibatiza akiwa hapa duniani?

Kigao ni nini? Na Je kinafunua nini kwa agano jipya?

Tofauti kati ya mbinguni, peponi, Kuzimu, Jehanamu, na Paradiso ni ipi?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Prisca komba
Prisca komba
2 years ago

Amina mtumishi