Je mwanamke Fibi, alikuwa ni askofu wa makanisa, kama mitume?

Je mwanamke Fibi, alikuwa ni askofu wa makanisa, kama mitume?

SWALI: Je mwanamke Fibi, alikuwa ni askofu wa makanisa, kama mitume? Kulingana na (Warumi 16:1)

Warumi 16:1

16:1 “Namkabidhi kwenu Fibi, ndugu yetu, aliye mhudumu wa kanisa lililoko Kenkrea;

2 kwamba mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu; mkamsaidie katika neno lo lote atakalohitaji kwenu; kwa sababu yeye naye amekuwa msaidizi wa watu wengi, akanisaidia mimi pia”.


JIBU: Fibi hakuwa askofu wa makanisa, wala maandiko hayasemi hivyo, bali alikuwa ni “Mhudumu”..Yaani alikuwa akilihudumia kanisa la Kristo lililokuwa Kenkrea. Ni mwanamke aliyekuwa akilijali sana kanisa kwa kuwasaidia watu wengi, ikiwemo na mtume Paulo pia. Pengine kwa mali zake, kama walivyofanya wakina Yoana na Susana, waliomuhudumia Bwana kwa mali zako (Luka 8:3), au alivyokuwa Martha na Miriamu jinsi walivyompenda Bwana na kujitaabisha kwa ajili yake..

Au kama alivyokuwa Dorkasi, ambaye, kanisa zima lililokuwa Yafa lilimshuhudia, jinsi alivyotoa sadaka nyingi na kuwashonea watakatifu mavazi. Ndivyo ilivyokuwa pia kwa huyu mwanamke ambaye aliitwa Fibi. Pengine alikuwa anawakaribisha watakatifu na kuwapa makao nyumbani kwake, au alikuwa anachapisha injili za mitume na kuyasambazia makanisa yaliyokuwa Kenkrea.

Kwa ufupi ni kwamba Fibi likuwa ni muhudumu kweli kweli kwa Bwana, kiasi cha kuwafanya mitume wampe heshima ya kipekee katika kanisa.

Lakini hiyo haimaanishi kuwa yeye naye alikuwa ni Askofu (Mwangalizi), wa makanisa kama mitume. Hapana andiko limeweka wazi kabisa kuwa mwanamke hana uongozi wowote katika kanisa. Ni kinyume na utaratibu wa Mungu.

1Timotheo 2:11 “Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.

12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.

13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.

14 Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa”.

Lakini tunajifunza nini kwa Fibi?

Hii ni kuonesha jinsi gani mwanamke anaweza kumtumikia Bwana katika nafasi yake, na akawa na heshima kubwa katika kanisa la Kristo, mfano wa Fibi. Ni vizuri wewe kama mwanamke uifahamu nafasi yako, katika mwili wa Kristo, kisha simama katika hiyo, watazame kwanza wanawake wenzako katika biblia jinsi walivyoenenda, na jinsi walivyokuwa wanamtumikia Mungu na wewe waige, kabla hujakwenda kuwatazama kwanza mitume wanaume.

Hiyo ni muhimu sana kufahamu hilo, usije ukawa unapiga mbio bure, halafu baadaye unapokea thawabu isiyolingana na juhudi yako.

Ikiwa wewe ni mwanamke na utapenda kupata mafundisho ya namna hiyo yanayohusiana na huduma za wanawake katika kanisa, basi nitafute inbox kwa namba hizi +255693036618, nikutumie mafundisho hayo, au fungua link hii utakutana nayo, moja kwa moja >>>  https://wingulamashahidi.org/2021/07/21/masomo-maalumu-kwa-wanawake/

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

NI KITU GANI TUNAJIFUNZA KWA RISPA, BINTI AYA?

Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?

MAMA UNALILIA NINI?

Unyenyekevu ni nini?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
2 years ago

Swali: tukisoma Luka 2:36, inasema kulikuwa na nabii mke,aitwae Hana, na vile vile na tukisoma kutoka 15:20 na Nabii mke aitwaye Miriamu,…Sasa swali Je kulingana na Waefeso 4:11, inasema..

Waefeso 4:11
11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na *wengine kuwa manabii;* na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;

Sasa swali langu, hawa manabii wanawake kazi yao ni mini.? Maana tunaona Yoeli 2:28, inasema wore walimwagiwa vipawa wanaume kwa wanawake.

Prisca komba
Prisca komba
2 years ago

Kwahy mwanamke kuw mwalim ni kosa ?

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Amen ubarikiwe.