NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

Nafasi ya mwanamke katika kanisa ni ipi? Je anaruhusiwa kuwa mchungaji, au askofu?

Mtume Paulo alisema,..

 1Wakoritho 14;34 “Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa. Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu? Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana”

Hapa maandiko yanaweka wazi kabisa mwanamke hana nafasi ya uongozi wowote katika kanisa, au kutatua tatizo lolote katika kanisa, Mungu aliuweka huu utaratibu, kulifundisha kanisa, maana mwanamke anawakilisha kanisa la Kristo, na kama vile kanisa limtiivyo Kristo katika kila Neno vivyo hivyo na wanawake wanapaswa kujitiisha chini ya waume zao ikiwemo kuongozwa kwa kila jambo kama maandiko yanavyosema kwenye..

 Waefeso 5:22-23Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. 

23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.

24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.   Kwahiyo mwanamke hajapewa mamlaka yeyote ya kumtawala mwanamume iwe kanisani au nyumbani, Kichwa cha mwanamke ni mwanamume na kichwa cha mwanamume ni Kristo.

Sasa zile huduma tano zilizozungumzwa katika waefeso 4:11( “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe”) hizi zilitolewa kwa wanaume tu ,ofisi hizi tano ni za uongozi katika kanisa hakuna hata moja inayomhusisha mwanamke. ikiwemo maaskofu na mashemasi wote wanapaswa wawe wanaume.

Na Bwana Yesu alitoa sababu katika

 1timotheo 2:11-14 ” Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.”

kwahiyo hapa tunaona kuwa Hawa ndiye aliyedanganywa na sio Adamu. Na Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, kama tu vile sisi tunavyowatii wazazi wetu pasipo shuruti na kuwaheshimu na kuwapa mamlaka yote katika familia ni kwasababu wao ndio waliotutangulia kwanza duniani na ndio waliotuzaa, lakini tunawapa heshima yao je! si zaidi kwa mwanamke kumtii Adamu aliyetoka katika ubavu wake na ndiye aliyeumbwa wa kwanza??..

Kuna baadhi ya wanaojiita watumishi wa Mungu wanaoingiza harambee za kijamii katika kazi ya Mungu na kufundisha kuwa kila kitu mwanaume anachofanya, mwanamke pia anaweza kufanya, hawajui kwamba wanaenda nje ya mpango wa Mungu kwa maana kila jambo Mungu aliweka kwa utaratibu na kwa kulifundisha kanisa.

Tunaona mitume 12 wote wa Bwana Yesu walikuwa ni wanaume, katika agano la kale hakuwahi kuwa na kuhani mwanamke, ilikuwa inafahamika hivyo tangu awali shughuli zote zinazohusu madhabahu ya Bwana zilikuwa zinafanywa na wanaume, lakini mambo haya yalianza kujitokeza ilipofika kuanzina karne ya 20 mpaka leo wanawake walipoanza kutafuta haki sawa ndipo hapo walipoanza kujiingiza katika siasa, na  leo hii shetani amefanikiwa kuingiza hiyo roho katika kanisa na kufanya madhabahu ya Mungu itawaliwe na wanawake. Haya ni machukizo mbele za Mungu, na ni dhambi yenye uzito ule ule sawa na wasiokuwa wa kabila la walawi kuhudumu katika nyumba ya Mungu kwenye agano la kale.

Swali ni je! wanawake wanaofanya hivyo Mungu hayupo nao??

Ni siri kubwa imekaa hapo ambayo watu wengi hawaijui, wanapoona mtu anatenda miujiza, vipofu wanaona, unabii unatolewa n.k. wakidhani ndio uthibitisho kuwa mtu huyo yupo katika njia sahihi biblia inasema

Mathayo 7:22-23 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.”

Kwahiyo tunaona haijalishi unatenda miujiza kiasi gani, uthibitisho pekee wa Mungu kuwa na wewe ni kuyatenda mapenzi ya Mungu ambayo ni kuishi katika Neno lake, na NENO lake ndilo hilo

Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu ” 

Kwahiyo yoyote aendaye kinyume na hayo anaenda nje ya maagizo ya Bwana haijalishi ni miujiza kiasi gani inatendeka kwenye huduma yake, anafanya kazi isiyokuwa na faida.

Je! kazi ya mwanamke ni ipi katika kanisa?
Kuna zile karama Mungu alizitoa kwa wote, kwa mwanaume na mwanamke. (ijulikane kuwa karama ni tofauti na huduma) ukisoma..

1wakoritho 12:4-10 ” Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.

Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.

Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.

Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; ” 

 Hivyo basi Mungu anaweza kumtumia mwanamke kutoa unabii/ujumbe katika kanisa lakini sio kufundisha. Mungu anaweza kumtumia mwanamke kuponya wagonjwa, kunena kwa lugha, kutoa unabii, hizi zote ni karama za Mungu na anaweza kumtumia yeyote, lakini zile huduma ambazo ni ofisi kuu tano yaani, mitume, manabii, wainjilisti,waalimu na wachungaji, ikiwemo na mashemasi, hizi ni huduma za uongozi wa kanisa, na hazimuhusu mwanamke hata kidogo.

Wanawake wanapaswa kujifunza, kwa kuuliza maswali kwa mtu yeyote ikiwemo mchungaji wake yahusuyo masuala yake ya kiroho na pia kuruhusu karama za Mungu kutenda kazi ndani yake, ikiwemo, kunena kwa lugha, kutoa unabii, uponyaji, ishara na miujiza, ndoto,kumsifu na kumwimbia Mungu wao, na kushuhudia wengine katika nafasi uliyopo kwa jinsi Mungu atakavyokujalia.

Isipokuwa kufundisha au kuhubiri kanisani au kumtawala mwanaume kwa namna yoyote na kufungua huduma na kujiita mchungaji, au mwinjilisti au askofu au mwalimu au mtume ni makosa, kama ulishawahi kufanya hivyo pasipo kujua jirekebishe na ukae katika nafasi uliyoitiwa.

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.

NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.

KWANINI MUNGU ANAMPA NABII HOSEA MAAGIZO YA KUMUOA MWANAMKE KAHABA? (HOSEA 3)

KUTOKA 10:1 “BWANA ANASEMA ATAMPA FARAO MOYO MGUMU, ASIMTII, JE! HAPO BWANA ATAMHUKUMU FARAO KAMA MKOSAJI SIKU ILE?”


Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
18 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

Amina

Bright
Bright
2 years ago

Amina. Mbarikiwe Sana kwa neno nzuri na lenye kuzaa matunda. Ila mimi nina swali, naomba msaada tafadhali, Je kama Mchungaji matendo yake ni ya uovu yaani anapotosha kweli ya Mungu kabisa na ni mwanaume, alafu katika kanisa kuna mwanamke ambaye kanisa lote kabisa linaona huyu anafaa katika kweli ya Mungu, je kwake yeye ni dhambi kutumika? Pia kama Debora alikuwa nabii lakini umesema kuwa alikuwa chini ya Kuhani na ni Karama. Je, utumie ni nini? Na kwanini mpaka sasa kuna manabii ambao wanasimamia makanisa na ni wa kiume nao tunawaambia au hatuwaamini, Jez wao ni kama akina nani kama nabii ni Karama na sio huduma? Na mtume kwake inakuwaje? Maana naye unakuta ni wa kiume lakini ana kanisa. Pia naomba aidha uniweke vizuri katika ufafanuzi zaidi ili niweze kujifunza zaidi. Kwamba, wanawake kanisani watumike kama akina nani? Kama huduma ni tano tu, ambazo ni Waalimu, Wachungaji, Wainjilsti, Mitume na Manabii Efeso 4:11.
Na kama hii nafasi kibiblia kabisa ilikuwa ndivyo, tunaona sasa wanaume ndiyo wingu kubwa na watumishi wa uongo kabisa. Lakini utakuta mwanamke unaona kabisa anavyofanya kazi ya Mungu ndivyo sahihi kabisa na inampendeza Mungu, je, huyu tumhukumu???

Emmanuel Kitengule
Emmanuel Kitengule
2 years ago

Nimeelewa vizuri na nimebarikiwa.

MBONIMPA
MBONIMPA
2 years ago

Mungu atusaidie sana kupata ufunuo juu ya jambo hili

Jane
Jane
2 years ago

Vp kuhusu nabii kama Miriam nae unamuweka ktk kundi gani

Kelvin
Kelvin
2 years ago
Reply to  Jane

Dear Admin ninabarikiwa sana na mafundisho yako lakini hili andiko lako linanipa changamoto kidogo. Tunaposoma andiko lolote katika biblia hatua ya KWANZA ni kujiuliza mwandishi alilenga nini Kwa hadhira yake ya wakati huo( EXIGESIS).. tukishaelewa hilo ndipo tunakuja hatua ya PILI ambayo ni Je! Kwetu Leo hadhira ya Sasa, andiko hili tunalitumiaje.. nyaraka nyingi za mtume huyu mwenye neema ya kipekee sana PAULO. Aliandika kulingana na uvuvio wa roho mtakatifu kuendana na mwenendo na tabia ya kanisa husika. Kanisa lililokuwa KORINTHO, THEOLOJIA inaonyesha ni kanisa ambalo neema ya Mungu iliachiliwa kwao Kwa viwango vya juu sana!! KARAMA ZA ROHONI zote(9) na HUDUMA ZA ROHO MTAKATIFU(5) zote zilikuwa zinatenda kazi ndani ya kanisa bila kubagua jinsia!! Sasa ikaibuka watu KUTOKUENENDA KWA UTARATIBU!! wanawake wakawa Sasa ni VURUGU ibadani kila mmoja ANASIMAMA anavyotaka yeye!! Paulo ameeleza yote haya katika nyaraka hizi Kwa KORINTHO..ndipo akachukua hatua ya kuwapiga STOP wanawake anawauliza KWANI KRISTO aliwajia ninyi tu? katika waraka Kwa mwanaye wa kiroho TIMOTHEO, pia aliapply amri hiyo toka katika torati kulingana na HALI NA MWENENDO WA WANAWAKE katika kanisa husika!! ukisema Leo hii TUWAZUIE wanawake ni KUBATILISHA neema ya Mungu.. mbona mtume PAULO huyohuyo katika nyaraka zingine hajazuia na anawaandikia WANAWAKE akina PRISILA ambao ni watumishi!! hebu ni maombi yangu uichunguze hili chapisho vizuri kwamba Je! UJUMBE WA KUDUMU(timeless truth) aliyolenga MTUME PAULO ilikuwa ni kuwazuia wanawake kuwa na HUDUMA??
With humility,
I submit

prisca sanga
prisca sanga
5 months ago
Reply to  Kelvin

Umenena vyema, i was like kuandika hivi, mtoa maada ametafsiri biblia kimwili sanaaa na hajataka kujua intension ya mtume paulo.
Mtume paulo yeye yeyeeee amemtaja prisila for more than 3 times kuwa alitenda kazi pamoja nae and how ikiwa alikuwa anawakataa??
Hapo Utagundua kitu.

Subije
Subije
2 years ago

Nimekuelewa mtumishi wa Mungu, barikiwa sana!

Cathy
Cathy
2 years ago

Somo zuri sana kutukumbusha nafasi ya mwanamke katika kanisa. Ni kweli, mpango wa Mungu lazima uheshimiwe. Ila nina swali, unamwongeleaje mtu kama Debora? Aliyetumika na Mungu kuleta ukombozi Israeli kwa neno la unabii? Je, kufundisha kote kunakofanywa na wanawake ni makosa? Hata kama wanafundisha watoto wao wa kiume na wa kike au wanawake wenzao? Je, ikiwa huyo mchungaji mwanaume anakosea katika utendaji au ufundishaji au uongozi kulingana na biblia, na yuko mwanamke anayelijua neno sawasawa na anataka kumrekebisha mchungaji (privately), je ni kosa pia? Nasubiri majibu yenu.
Asante.

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Somo zuri sana kutukumbusha nafasi ya mwanamke katika kanisa. Ni kweli, mpango wa Mungu lazima uheshimiwe. Ila nina swali, unamwongeleaje mtu kama Debora? Aliyetumika na Mungu kuleta ukombozi Israeli kwa neno la unabii? Je, kufundisha kote kunakofanywa na wanawake ni makosa? Hata kama wanafundisha watoto wao wa kiume na wa kike au wanawake wenzao? Je, ikiwa huyo mchungaji mwanaume anakosea katika utendaji au ufundishaji au uongozi kulingana na biblia, na yuko mwanamke anayelijua neno sawasawa na anataka kumrekebisha mchungaji (privately), je ni kosa pia? Nasubiri majibu yenu.
Asante.

kizilapaul@gmail.com
kizilapaul@gmail.com
3 years ago

Uli ni neno la kweli n’a mina sumbuwa sana kanisa la Mungu Saidi uko kwenu est Africa.ni muinjilisti Paulo kizilapaul@gmail.com Ku toka mashari ya DRcongo.

Friedrich son of JESUS%
Friedrich son of JESUS%
3 years ago

Kweli mtumishi kama huu ni mpango wa shetani basi wanadamu tumeisha,make hadi huwa wanasema BWANA amewaita,watumike.

Joseph Salvatory
Joseph Salvatory
4 years ago

Mh! Hili swala ni swala mtambuka, Mbona ni walimu, na ni Mashemasi. Na zaidi sana wanapangwa katika kutoa hubiri katika Ibada

MILDRED CUSIEL
MILDRED CUSIEL
4 years ago

SIJAKUELEWA NA WALA SINTAKUELEWA