Title November 2023

Ielewe kwa kina Waebrania 13:5 maana yake.

Kwanini Mungu  anasema tusiwe na ‘tabia’ ya kupenda fedha? Tuwe radhi na vitu tulivyo navyo?. Ujasiri gani unaotaka kutuaminisha kwa kauli hiyo katika zama hizi ambazo tunajua bila fedha huwezi kutatua changamoto nyingi za kimaisha?

Waebrania 13:5  Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. 6  Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?

JIBU: Ametuagiza hivyo kwasababu ya hakikisho alilotuahidia katika kauli yake aliyosema “sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa”. Ukiitafakari kauli hiyo haimaani kuwa hatutakaa kamwe kupitia  vipindi vya kupungukiwa, hapana, lakini anasema sitakupungukia ‘kabisa’, yaani ikafikia hatua ya kukosa kabisa hitaji Fulani, mpaka kufa na kuwa omba-omba barabarani, hapo hatutapafikia.

Daudi anasema..

Zaburi 37:25 Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula

Umeona ameahidi kuwa nasi nyakati zote,

 Ni kweli upo wakati ambapo ukiitazama baadaye yako au kesho yako unaona giza, lakini bado Bwana anasema usiwe na hofu, kwasababu hiyo kesho yenyewe itajisumbukia, yeye mwenyewe atatengeneza njia ya namna ya kukusaidia katika siku hiyo uliyopo.

Lakini ubaya ni pale ambapo tutataka Mungu atupe sawasawa na wingi tunaoutarajia. Kibiblia hilo sio hakikisho la Bwana, anaweza kukupa cha wakati huo tu, au akakupa zaidi ya hivyo ulivyomwomba. Ni jinsi yeye apendavyo, na anafanya hivyo kwa sababu zake mwenyewe ambazo ni njema kwako, lakini mwisho wa siku yote yatakuwa sawa tu, usiwe na hofu.

Pia ni vema kufahamu kuwa kauli hiyo haitufanyi sisi kuwa wavivu tusubirie tu kitu kutoka kwake. Hapana, anataka tujishughulishe katika sehemu mbili.

Sehemu ya kwanza ni kuutafuta ufalme wake, na haki yake.

Mathayo 6:33  Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 34  Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.

Yaani uwe katika utumishi wa Bwana, unamtafuta na unaifanya kazi yake, kama vile mwajiriwa, alivyo katika utumishi wake. Ukifanya hivyo kwa uaminifu Bwana hawezi kukupungukia kabisa atakupa tu rizki yako, kwa njia zake mwenyewe.

Na sehemu ya pili ni aidha tuwe katika kufanya kazi za mikono. Tunapojishughulisha, na kitu Fulani cha kutupatia kipato, Bwana atatusaidia huko huko, kutujazwa mema yake.

Na kwasababu Bwana hataki mioyo yetu izame kule moja kwa moja, anataka  tupate na nafasi ya kumfanyia ibada, na ndio maana  ameahidi hatatuacha kabisa, Hivyo usione shida kufunga biashara yako, na kwenda kwenye maombi muda wa maombi ufikapo, jumapili kuahirisha kazi zako zote na kwenda nyumbani kwa Bwana, ondoa hofu kuwa utapoteza wateja. Kumbuka tu ile kauli ya sitakuacha kabisa, wala kukupungukia kabisa.

Hata kama utapoteza hiyo, Bwana atakufungulia rehema zake na kukupatia ili bora zaidi ya ile.

Hivyo kwa hitimisho ni kuwa wewe kama mwana wa Mungu, hupaswi kuweka moyo wako kwenye mali au fedha, yaani kufikiria kwamba bila kuwekeza sana maisha yako huko utapata shida mbeleni. Hapana, bali upatapo kingi au kidogo, basi ridhika maadamu Kristo yupo ndani yako, ameahidi kukusaidia nyakati zote.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho,

Kupiga ramli ni nini katika biblia?

Je kauli ya Bwana Yesu inajichanganya? Katika Yohana 8:14 na Yohana 5:31?

Kwanini Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wasikisaze chakula?

Jiepushe na tamaa ya Mali/kupenda fedha.

JUA HALITAKUPIGA MCHANA, WALA MWEZI WAKATI WA USIKU.

Rudi nyumbani

Print this post

Ielewe Wafilipi 4:8, Ina maana gani kwa mwaminio

Wafilipi 4:8  Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.

Katika vifungu hivyo utaona neno “yoyote” limetumika sana. Ikiwa na maana yapo mengi, ya aina mbalimbali, ambayo hayajaandikwa hapo.  Na hapo biblia inaegemea katika “yale yaliyo mema”.

Tukumbuke kuwa biblia haijaandika matendo yote mema mwanadamu anayopaswa kuyafanya. Kama ingekuwa hivyo basi kingekuwa ni kitabu kikubwa sana, ambacho hakuna mwanadamu yoyote angeweza kukimaliza kwa kukisoma. Lakini imetoa kama muhtasari tu, au mwongozo wa kufuata.

Kwamfano huwezi, kuona katika maandiko tunaagizwa ‘tuimbe kwaya kanisani’, lakini hayo ni moja ya yenye kupendeza, au kuona tunaambiwa tuhubiri injili kwa njia ya maigizo. Lakini, tumebuni wenyewe na mwenye dhambi anapotizama filamu hizo, huwa inachangia katika kuwasogeza karibu kwa Kristo. Maadamu haivitoki nje ya maudhui mema.

Au tunapotumia vipaza sauti, au tunaposambaza vipeperushi vya injili barabarani, huwezi ona agizo hilo, popote kwenye maandiko. Lakini ni moja ya yale yaliyo ya kweli.

Hivyo kwa hitimisho ni kuwa yapo mambo mengi ambayo tunaweza kuyafanya, na Bwana hatuzuii kuyatafakari, ndio maana akamalizia kwa kusema ‘yatafakari hayo’. Maana yake tutafiti na tutumie njia zote, ambazo tunaona hatma yake itakuwa ni kuujenga ufalme wa Mungu, au kuufanya uependeza zaidi.

Angalia katika ujuzi wako, angalia katika elimu yako, ni kwa namna gani utafanya jambo la ki-Mungu lenye kukuletea sifa njema kwake. Utumishi wa Mungu sio pale madhabahuni tu kuhubiri, utumishi wa Mungu ni mpana. Hivyo Hapo hapo ulipo tafakari  ni kwa namna gani utaujenga ufalme wa Mungu wako, na Bwana atakupa akili njema.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mafundisho mengine:

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA TITO.

Nini maana ya kikombe cha maji ya baridi(Mathayo 10:42)?

Mambo yale yaliyo mbali, na yale yaendayo chini sana,

NAFASI YAKO NI IPI KATIKA MWILI WA KRISTO?

Matulizo ya mapenzi ni nini? (Wafilipi 2:1).

Birika ni nini?, na yale Matao matano katika birika la Bethzatha ni nini?

REKEBISHA YAFUATAYO ILI MAMBO YAENDE SAWA.

Rudi nyumbani

Print this post

NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE.

Karibu tujifunze biblia.

(Masomo maalumu  kw wanandoa).

Waebrania 13:4 “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu”.

Hapa biblia inataja vitu viwili; 1) NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE, na 2) MALAZI YAWE SAFI.

Tutazame moja baada ya lingine.

1.NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE.

Hapa anasema “Na iheshimiwe na watu wote”..maana yake si mtu mmoja tu au wawili au watatu, bali wote. Sasa swali ni makundi gani ya watu wanaopaswa kuiheshimu ndoa, na ndoa inaheshimiwaje.

Kundi la kwanza la watu wanaopaswa kuiheshimu ndoa, ni wanandoa wenyewe!..(Na kumbuka ndoa ni ile ya mume mmoja na mke mmoja). Na kundi la pili ni watu wa nje, wasiohusiana na hiyo ndoa.

Kwa wanandoa wanapaswa kuiheshimu ndoa yao kwa kuzuia kitu chochote ambacho kinaweza kuifanya ndoa hiyo iwe ndaifu au ivunjike. Na vitu vinavyoweza kufanya ndoa iwe ndaifu au kuvunjika kabisa ni pamoja na kukosa maelewano, Ugomvi, mafarakano, kukosa utii na upendo,uvumilivu, na uaminifu..haya ni baadhi ya mambo yanayodhoofisha ndoa na hata kuivunja kabisa.

Hivyo wanandoa ni lazima wafanya wawezavyo kutunza upendo wao wa kwanza walipokutana, Amani yao kwanza, furaha yao kwanza, maelewano yao kwanza, na mengineyo mazuri waliyokuwa nayo kipindi wanakutana. Kwa kufanya hivyo watakuwa wameiheshimu ndoa yao na itadumu daima.

Na kwa namna gani wanandoa wanaweza kurudisha upendo wao wa kwanza?…si kwanjia nyingine bali ile ya kutubu na kunyenyekea, na kujazwa Roho Mtakatifu, kwamaana yeye pekee (Roho wa Mungu) ndiye mwenye kutoa matunda yanayohitajika katika ndoa..

Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”.

Kundi la pili la watu linalopasa kuheshimu Ndoa, ni watu wa nje wasio wanandoa. Ikiwa na maana kuwa mtu yeyote wa nje iwe ndugu, au rafiki, au jamaa, au jirani, au mpita njia, hapaswi kuwa sababu ya ndoa ya mwingine kudhoofika au kuvunjika.

Maana yake kama huhusiki na ndio hiyo, basi hupaswi kupanda mbegu za fitina katika hiyo ndoa, hupaswi kufanya wanandoa wachukiane, watengane, waumizane, au wafanye lolote litakalowatolea heshima wanandoa hao. Unachopaswa kufanya ni kuwaombea na kuwashauri ikiwa wamefungua mlango huo!, na ushauri unaopaswa kuwapa ni ule wa kibiblia na si wa kidunia.

Vile vile wewe kama mtu usiyehusika na ile ndoa, hupaswi kumtamani mke/mume wa jirani yako, wala kujaribu kumshawishi uwe naye!..ni lazima uiheshimu ndoa yake, vile vile hupaswi kuanzisha mahusiano yoyote yenye viashiria vya kukushuku, au kuleta tashwishi kuhusu uhusiano wako na yeyote katika ndoa, ni lazima ukae mbali kwa kadiri uwezavyo, isipokuwa kwa sababu maalumu ambazo zitaweza kueleweka katika pande zote mbili. (Kwa kufanya hivyo utakuwa umeiheshimu ndoa ya mwingine).

2.MALAZI YAWE SAFI.

Hili ni jambo la Pili: Malazi yawe masafi.

Malazi yanayozungumziwa hapa ni mahali wanandoa wanapokutana kimwili, maana yake mahali hapo panapaswa pawe pasafi daima, pasiwe pachafu!. Na uchafu unaozungumziwa hapo si usafi ule wa vumbi katika kitanda, au jasho la mwili, (huo unafaa lakini sio unaozungumziwa hapo).

Uchafu unaozungumziwa hapo ambao ni najisi ni uchafu wa Zinaa, pamoja na kukutana kimwili kinyume na maumbile kwa wanandoa.

Unapokuwa mwanandoa ni amri kutokutana  kimwili na mwanamke/mwingine  tofauti na uliyefunga naye ndoa!, unapolala na mtu mwingine hapo umefanya malazi kuwa machafu, na ni dhambi kubwa!. Vile vile katika kukutana ni lazima iwe kwa namna ya asili. Na si kinyume na maumbile!. Biblia inasema wafiraji hawataurithi uzima wa milele.

1Wakorintho 6:9 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, WALA WAFIRAJI, WALA WALAWITI”

Soma pia 1Timotheo 1:10.

Iheshimu ndoa yako, vile vile heshimu ndoa za wengine.

Je umeokoka?..Fahamu kuwa Kristo anarudi!, na tupo nyakati za hatari.

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mafundisho mengine:

MAFUNDISHO YA NDOA.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.

Pale mwanandoa mmoja anaposhindwa kutimiza wajibu wake ufanyaje?

FAMILIA TAKATIFU: Marimu na Yusufu.

KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 2: Upande wa wanawake)

Rudi nyumbani

Print this post

Nini maana ya kikombe cha maji ya baridi(Mathayo 10:42)?

SWALI: Kikombe cha maji ya baridi ni  kipi Bwana alichokitaja katika;

Mathayo 10:42  Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake


JIBU: Ni kawaida mtu anayetoka kufanya kazi ngumu, labda ya shamba, au wanaoshiriki katika michezo labda riadha au mipira, utaona huduma ya kwanza wanayoihitaji, sio chakula, bali ni maji, kwasababu mwili huwa unapoteza maji mengi sana pale jasho linapotoka. Na gharama ya maji sikuzote ni ndogo kuliko chakula. Hivyo mtu yeyote huwa ni rahisi kupata huduma hiyo, kwani mtu anaweza kumtolea ndani mwake kwenye pipa lake la kutunzia maji masafi, au kuchota kisimani, na kumpa n.k. Na pale anapompa ya baridi kabisa basi humfanya mtu yule ayanywe yale maji sio tu kwa kukata kiu lakini pia kwa burudiko.

Vivyo hivyo na Bwana naye anawafananisha watu wake, na watenda kazi waliotoka kufanya kazi ya kuchosha, hivyo na wenyewe huwa wanakuwa na kiu chao, wanahitaji maji yao. Lakini zaidi sana maji baridi. Na mtu anayefanya hivyo Mungu amemuahidia kumpa thawabu yake.

Maji ya mwaminio ni yapi?

Yanaweza kuwa ni vyakula: Kwamfano umuonapo, mtumishi wa Mungu labda anahudumu au anahubiri pengine kwenye masoko, au mahali fulani kwa muda mrefu, na wewe ukathamini kumpatia chakula au hata chupa ya maji. Akanywa au akala ashiba akamshukuru Mungu. Hiyo ni thawabu kwako kwa Mungu.

Yaweza pia kuwa sadaka yako: Kile kidogo, kinachoweza kumtunza hata kwa siku hiyo, kwa ajili ya usafiri, au sabuni, au vocha kwa ajili ya mahitaji yake madogo madogo. Bwana amekuahidia pia thawabu yako hata kama utakiona ni kidogo, si zaidi  ukampa vya ziada? Kinabadilika kuwa kikombe cha maji ya baridi.

Yaweza kuwa pia ni “vitu”: Mfano mwingine hana fedha au chakula, lakini ana kitu Fulani cha kumpa, labda nguo, au kiatu, au simu, au huduma n.k. Hicho nacho Bwana anakihesabu kama kikombe cha maji ya baridi.

Hivyo kwa hitimisho ni kuwa zipo thawabu mbalimbali ambazo Bwana anatoa, kwa kutenda mema, zipo thawabu za kuwasaidia maskini, zipo thawabu za kuwasaidia ndugu, lakini zaidi pia Bwana ameahidi thawabu kwa wale wote wanaowajali watumishi wake.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mafundisho mengine:

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA.

JE NI KIKOMBE KIPI UTAKINYWEA SIKU ILE?

YESU ANA KIU NA WEWE.

UWE KIKOMBE SAFI 

AGENDA KUBWA YA SHETANI KWA KANISA HILI LA LAODIKIA.

MAJI YA UZIMA.

Rudi nyumbani

Print this post

Je agano la kale litatoweka kabisa kulingana na Wabrania 8:13?

Jibu: Tusome,

Waebrania 8:13 “Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka”.

Neno “kuukuu” maana yake ni “kitu kilichochakaa/ kilichoisha muda wake”.. Hivyo hapo biblia inaposema kuwa Agano la kwanza amelifanya kuwa kuukuu tafsiri yake rahisi ni kwamba “Agano la kwanza yaani lile la kale amelifanya kuwa chakavu (lililoisha muda wake)/ lisilofaa tena”.

Lakini swali ni je!.. kupitia mstari huo inamaanisha kuwa Agano la kale litapotea kabisa na halitatumika?…kiasi kwamba halifai tena wala halitatumika?

Jibu ni la! Bwana Yesu alisema mwenyewe kuwa “hakuna yodi moja wala nukta moja ya torati itakayoondoka (soma Mathayo 5:18)”… Na Zaidi sana alisema hakuja kuitangua torati bali kuitimiliza.

Mathayo 5:17 “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.

18  Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie”.

Sasa swali linarudi pale pale kama hivyo ndivyo kwamba Bwana YESU hakuja kuitangua torati bali kuitimiliza, na kwamba agano la kale bado litaendelea kuwepo, ni kwanini hapo katika Waebrania 8:13 biblia iseme kuwa litatoweka kabisa?. Je! Biblia inajichanganya??

Jibu ni La! biblia haijichanganyi bali tafakari zetu ndizo zinazojichanganya!.

Ili tuelewe vizuri tutafakari mfano ufuatao.

Kampuni moja limetoa aina Fulani la gari, na aina hiyo ya gari ikatumika kwa miaka kadhaa, lakini baada ya miaka 10 ikatoa toleo lingine jipya la aina ile ile ya gari, na hivyo kampuni hilo likaacha kuzalisha lile toleo la kwanza lililo dhaifu na kujikita katika uzalishaji wa toleo jipya.

Sasa ni wazi kuwa kwa jinsi miaka inavyozidi kwenda lile toleo la kwanza litaenda kupotea kabisa na kubaki hili la pili… kwa lugha nyepesi tunaweza kusema kuwa… “Kampuni lile limelifanya toleo la kwanza kuwa kuu, na hivyo lipo karibuni kutoweka kabisa”.

Lakini kwa kutoa toleo jipya haimaanishi kuwa limelipinga lile la kwanza, kwamba badala ya kuzalisha magari sasa linazalisha treni. Hapana! Bali kinyume chake limeliimarisha lile la kwanza, ikiwa na maana kuwa kama tairi za toleo la kwanza zilikuwa dhaifu, basi toleo la pili limeziongezea uimara, lakini gari ni lile lile, vile vile  kama mwonekano wa toleo la kwanza ulikuwa si mzuri basi toleo la pili limeongeza uzuri wa kimwonekano lakini gari ni lile lile.

Na ndivyo katika habari ya agano jipya na lile la kale, Hakuna kilichoondolewa, na kuletwa kingine kipya, bali ni kile kile kilichokuwepo kimeimarishwa Zaidi, kuwa bora Zaidi, kuwa imara Zaidi, kuwa chenye uwezo Zaidi n.k

Kwamfano biblia inasema katika mojawapo wa amri katika agano la kale kuwa “usizini” ikaishia hapo… Sasa hii amri ilikuwa ni dhaifu, kwasababu inasema usizini tu!, mtu anaweza asizini kweli lakini moyoni mwake akalipuka tamaa..

Lakini sasa Bwana YESU aliye mjumbe wa agano jipya anakuja kuitimiliza amri hiyo kuwa “mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye nafsini mwake”. Hata kabla ya kwenda kufanya kile kitendo.

Mathayo 5:27  “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;

28  lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake”

Na vile vile katika amri ya “kuua” ni hivyo hivyo…(soma Mathayo 5:21-22).

Kwahiyo kwa lugha nyepesi ni kwamba Agano la pili ni toleo jipya la Agano la kwanza. Lakini mambo ni yale yale.

Sasa ni swali lingine.. Ni wakati gani ambapo agano la kale lilianza kuwa kuu kuu?

Jibu: Ni wakati wa kuja kwa Bwana Yesu kwa mara ya kwanza.

Kipindi Bwana Yesu alipokuja, yeye ndiye wa mwanzilishi wa agano jipya, na kuanzia huo wakati ndio agano la kale katika maarifa yake machanga lilipoanza kuisha muda wake, na mpaka leo hatulitumii tena, limetoweka! Na nguvu katika damu ya Yesu ndani ya agano jipya inatawala.

Ndio maana maarifa machanga ya agano la kale, mfano matumizi ya damu za wanyama kama sadaka za kafara zimebaki kutumiwa na watumishi wa shetani, na katika ukristo Damu ya Yesu ndio utimilifu wa Torati za kafara. Na yeyote anayetumia kafara za wanyama leo hii, awe anajiita mtumishi wa Mungu au mtu yeyote yule anafanya ibada za miungu.

Kwahiyo leo hii katika ukristo hatuna matambiko, wala kafara za wanyama, wala utakaso kupitia damu za wanyama, wala hatuishi kwa kujizuia kuua lakini mioyoni tuna hasira, au tamaa.. bali tunaishi kwa Roho mtakatifu na tunamuabudu Mungu katika roho na kweli.

Bwana atubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MJUMBE WA AGANO.

Je! waliokufa kabla ya Bwana Yesu wataokolewaje?

LISHIKILIE SANA LILE AGIZO LA KWANZA.

Tofauti kati ya ufalme wa mbinguni na ufalme wa Mungu ni ipi?

Kiti cha Rehema kilikuwaje? (Kutoka 40:20)

Rudi nyumbani

Print this post

Fahamu maana ya Mhubiri 10:9 Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo;

SWALI: Nini maana ya Mhubiri 10:9 Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo; Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo.


JIBU: Mstari huu unatuonyesha hatari ya kazi yoyote inayotendwa na mtu. Hapo ametumia mfano wa wanaochonga mawe. Wajenzi wa zamani walikwenda kuchonga mawe miambani kwa ajili ya ujenzi wa majengo yao, lakini wakiwa kule walikutana na hatari nyingi, aidha kuangukiwa na mawe hayo, na kuwaponda viungo vyao, vifaa vyao  vya uchongaji kuwajeruhi.

Vilevile anatumia tena mfano wa wanaopasua miti, kwa ajili ya mbao za ujenzi, bado na wao pia wanakutana na hatari, aidha kuangukiwa na miti yenyewe, au shoka kuteleza na kumjeruhi mtu au yeye.

Kumbukumbu 19:5 kama aingiapo mtu na mwenziwe mwituni kwenda kukata kuni, akapeleka mkono wake na shoka ili kukata mti, likatoka shoka katika mpini, likampiga yule mwenziwe hata akafa; basi na akimbilie katika miji hii mmojawapo awe hai.

Ni sawa na mjenzi ambaye amezoea kupiga sana nyundo au kuwepo maeneo ya ujenzi muda wake mwingi, utaona upo wakati nyundo itateleza na kumponda kidole chake, au atakanyaga msumari n.k. Tofauti na kama angekuwa hajishughulishi na kazi hiyo yupo nyumbani tu.

Hii ni kufunua nini rohoni?

Kama wana wa Mungu tufahamu kuwa kazi yake ya kwenda kung’oa mapando ya mwovu, katika shamba la Bwana  tutarajie kukutana na madhara yake, si wakati wote utakuwa ni mwepesi tu (yaani kuvuna), zipo nyakati tutakutana na kupigwa, au kudhalilishwa, au kufungwa na wakati mwingine hata kuuawa. (Mathayo 10:17-19)

Mtume Paulo alipokuwa katika ziara zake za kupanda ukristo Asia na Ulaya, alikutana na hatari nyingi, ikiwemo kupigwa mawe na watu wabaya, kufungwa, na kurushiwa vitisho mbalimbali. Wamishionari kama dr David Livingstone walioleta injili Afrika zamani walikutana na hatari za magonjwa kama malaria, na wanyama wakali.

Lakini katika yote, Bwana ameahidi, mafanikio makubwa,  kuliko hatari zake. Hivyo hatupaswi kuogopa na kudhani kuwa kazi ya Mungu ni kazi ya kwenda kujichinja wakati wote. Hapana, zipo nyakati nyingi za raha, na mafanikio makubwa ya rohoni yasiyokuwa na ghasia yoyote, lakini Bwana hajatuficha pia hatari zake wakati mwingine. Ili tutakapokutana nazo tusihuzunike moyo na kukata tamaa, bali tuendelee na kazi.

Bwana akubariki.

Je! Umeokoka? Je! Umesamehewa dhambi zako? Kama ni la, ni nini kinachokusubirisha? Ukifa leo utakwenda wapi, kumbuka lipo ziwa la moto, kumbuka ipo hukumu kwa waovu. Tubu leo mgeukie Kristo akusafishe dhambi zako,  Ukabatizwe katika jina la Yersu Kristo upokee ondoleo la dhambi. Hizi ni siku za mwisho, Kristo anakaribia kurudi.

Ikiwa upo tayari leo kufanya hivyo basi fungua hapa kwa mwongozo huo>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618. Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mafundisho mengine:

Yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.

Je! fedha ni jawabu la mambo yote? (Mhubiri 10:19).

TUUTAFUTE UMOJA WA ROHO.

Fahamu maana ya Mithali 28:20 Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele;

NI KWA NAMNA GANI SHETANI ANAIZUIA INJILI?

FANYA MAAMUZI KABLA HAZIJAKARIBIA SIKU ZA HATARI.

Rudi nyumbani

Print this post

Je! fedha ni jawabu la mambo yote? (Mhubiri 10:19).

Jibu: Tusome,

Mhubiri 10:19 “Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; NA FEDHA HULETA JAWABU LA MAMBO YOTE”.

Kulingana na huu mstari je ni kweli fedha ni jawabu la kila kitu?.

Jibu ni La! Fedha haitoi jawabu la mambo yote, kama ndio basi fedha ingeweza kununua uzima wa milele, hivyo kusingekuwa na haja ya Bwana Yesu kutoa uhai wake kwaajili ya uzima wa roho zetu.

Lakini biblia inatufundisha kuwa tumekombolewa kwa damu ya Yesu na si kwa fedha.

1 Petro 1:18 “Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu

19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo”.

Vile vile fedha haiwezi kutibu kifo, wala kununua amani, kwasababu wapo watu wenye pesa nyingi lakini hawana amani n.k.

Lakini kama hivyo ndivyo kwamba fedha si jawabu la mambo yote, kwanini bi lia iseme no jawabu la mambo yote?.

Ili kupata jibu la swali hili ni vizuri tukausoma mstari huo kwa kutafakari kwa kina sehemu za kwanza za mstari huo na zile za mwisho.

Mstari huo unaanza kwa kusema.. “Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko” na unandelea kwa kusema… “Na divai huyafurahisha maisha”…na unamalizika kwa kusema “NA FEDHA HULETA JAWABU LA MAMBO YOTE”.

Sasa swali ni mambo gani hayo ambayo fedha inaleta majibu yake?.

Jibu: Ni mambo hayo yanayotajwa hapo juu, maana yake yahusuyo karamu hizo ziletazo kicheko zenye ulevi…. na si mambo mengine tofauti na hayo.

Na kweli mambo ya kidunia karibia yote jawabu lake ni fedha, maana yake ukiwa na fedha utaweza kuyafanya au kuyapata, na ukizikosa fedha pia unaweza kuyakosa.

Anasa zote za kidunia zinahitaji pesa, na wanaotaka anasa wanazitafuta pesa kwasababu hilo ndio jibu lake.

Lakini wana wa Mungu, hawaishi kwa fedha wala fedha si jawabu la mambo yao yote…bali Damu ya Yesu ndio jawabu la mambo yao yote.

Wana wa Mungu hata pasipo pesa wanaweza kuishi vizuri kabisa, na pia hawana tabia ya kupenda fedha, bali fedha yao ni Damu ya Yesu katika Roho Mtakatifu.

Je upo ndani ya agano la damu ya Yesu au Mungu wako ni fedha?.

Waebrania 13:5 “Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa”

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Aibusu midomo atoaye jawabu la haki (Mithali 24:26)

KUOTA UNAPEWA PESA, KUNA MAANISHA NINI?

Pesa za bindoni ni nini?(Marko 6:8)

MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO.

KANUNI YA KUOMBA NA KUPOKEA.

Rudi nyumbani

Print this post

SHUGHULIKA NA TABIA ZA KURITHI.

Zipo tabia au mienendo ambayo inaweza kurithishwa kutoka kwa wazazi au mababu/mabibi kwenda kwa watoto au wajukuu. Kama vile jinsi sura, maumbile, rangi, kimo, na mwonekano vinavyoweza kurithishwa kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto, kiasi cha kwamba mtoto anazaliwa na anakuwa amefanana na baba yake vile vile au bibia yake au mama yake….halikadhalika mambo ya ndani kama vile tabia au mienendo, mtu anaweza kurithi kutoka kwa wazazi wake au mababu zake/mabibi zake.

Ikiwa na maana kuwa kama Mzazi alikuwa na tabia ya ulevi kuna uwezekano na mwana wake naye akaja kuichukua hiyo tabia kama hatashughulika nayo, vile vile kama Mama alikuwa ni kahaba kuna uwezekano na binti naye akaja kuwa kahaba vile vile.

Ezekieli 16:44 “….KAMA MAMA YA MTU ALIVYO, NDIVYO ALIVYO BINTI YAKE”.

Kama mzazi alikuwa ni mtu wa hasira, au mwuaji ni rahisi na mwanae kuja kuwa mtu wa namna hiyo hiyo, kama mzazi au babu alikuwa mwizi, au mkorofi ni rahisi na mtoto wake au mjukuu wake kuja kuchukua hiyo tabia.

Hivyo ni muhimu sana kushughulika na Mienendo ya kurithi!… Ukiona una tabia fulani ambayo pia ipo au ilikuwepo kwa wazazi wako basi shughulika na hiyo tabia mapema.

Zifuatazo ni njia za kushughulika na tabia za Kurithi.

1. ZAMA KATIKA AGANO LA DAMU YA YESU.

Damu ya Yesu pekee ndio inayovunja na kufuta maagano yote ya ukoo na tabia zote za kurithi. Utauliza kivipi?..tusome maandiko yafuatayo..

1Petro 1:18  “Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; MPATE KUTOKA KATIKA MWENENDO WENU USIOFAA MLIOUPOKEA KWA BABA ZENU;

19  bali kwa DAMU YA THAMANI, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo”.

Hapo anasema “MPATE KUTOKA KATIKA MWENENDO USIOFAA MLIOPOKEA KWA BABA ZENU”..Kumbe kuna mienendo inatoka kwa mababa na si yetu!, bali tumepokea!.. na sasa ni kitu gani kinaweza kuifuta hiyo mienendo?..si kingine bali ni Damu ya Yesu pekee sawasawa na huo mstari wa 19.

Na tunaoshwaje kwa Damu ya Yesu?..

Si kwa njia nyingine bali ile ya KUTUBU, kwa kumaanisha kuacha hiyo mienendo tuliyoirithi na hatua ya pili ni KUBATIZWA katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu na hatua ya tatu nay a mwisho ni  KUPOKEA ROHO MTAKATIFU. (sawasawa na Matendo 2:38).

Baada ya hapo ile damu ya Yesu ambayo mpaka leo inatiririka pale Kalvari katika ulimwengu wa Roho, itakutakasa kwa namna isiyoweza kuonekana kwa macho na utakuwa safi, na mizizi ya tabia zote za kurithi itakuwa imekufa hapo..tabia za hasira, vinyongo, chuki, ukahaba, uhuni, vita, wizi, ulevi, uchoyo, ubinafsi n.k zitakuwa zimeondoka.

2.DUMU KATIKA UTAKASO

Baada ya kupokea utakaso wa Damu ya Yesu kwa njia ya kutubu na  kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu sawasawa na Matendo 2:38, hatua inayofuata si kulala tu!, na kusubiria matokeo!!…bali ni kudumu katika agano hilo la Damu ya Yesu, kwanjia ya kuomba mara kwa mara na kuondokana na vichocheo vyote vya dhambi, pamoja na kumtumikia Mungu.

Usitubu na kubatizwa halafu ukaendelea kwenda kwa waganga, au kufanya matambiko ya ukoo, au kutenda dhambi..(hapo zile tabia hazitakuondoka bali ndio zitakita mizizi zaidi)

Lakini ukizingatia hayo maandiko yanayotufundisha kwa moyo wote, basi fahamu kuwa hakuna tabia yoyote ya kurithi itakayosalia ndani yako, bali utakuwa safi daima na hivyo hata kufanyika baraka kwa vizazi vyako vilivyopo na vitakavyokuja. Na Zaidi sana badala ya watoto wako kurithi tabia za kishetani kutoka kwako watarithi tabia za kiungu, kwasababu  tabia za kurithi zinakuwa pia zinabeba laana na baraka nyuma yake..

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?

UMUHIMU WA KUZALIWA MARA YA PILI.

TABIA KUU TATU ZA WAHUBIRI WALIORUDI NYUMA NA KUMWACHA MUNGU.

NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.

MAZUNGUMZO MABAYA HUHARIBU TABIA NJEMA.

Rudi nyumbani

Print this post

Je ni sawa kuomba novena ya Mtakatifu Rita wa Kashia?

Mtakatifu Rita, ambaye kwa kanisa katoliki anajulikana pia kama ‘mwombezi wa mambo yasiyowezekana’, na ‘mfanya miujiza’.

Ni mama aliyezaliwa mwaka 1381, katika mji unaitwa Kashia, taifa la Italy. Aliolewa akiwa na umri mdogo lakini baada ya mume wake na watoto wake wawili  kufa aliamua kujiunga na utawa, ijapokuwa alipitia changamoto, kujiunga na jamii hiyo kwasababu tayari alikuwa ameshaolewa(sio bikira), lakini mwishoni alifanikiwa.

kulingana na kanisa katoliki maombi ya Rita yaliwaletea wengi majibu, lakini pia alitambulika kwa jeraha dogo kwenye kipaji cha uso wake, wakiamini kuwa ni alama ya ukristo, kufuatana na mateso ya Yesu msalabani, mahali alipowekewa taji ya miiba. Alikufa kati ya umri wa miaka  75-76.

Na ilipofika tarehe 24 May 1900, papa Leo XIII, Alimtangaza kuwa mtakatifu. Yaani ukitangazwa kuwa mtakatifu, unakidhi vigezo vya kuwa mwombezi wa walio hai.

Tangu huo wakati wakatoliki wengi dunia wamekuwa wakimfanyia novena, na litania. Na wengi wakishuhudia kuwa matatizo yao sugu, yakitatuliwa, hivyo imemfanya kuwa maarufu sana.

Lakini Je! Jambo hili ni kweli? Ni vema kufahamu kuwa katika maandiko matakatifu (BIBLIA), Hakuna mahali popote, tunafundishwa kuwa watakatifu waliokufa zamani au sasa wanaweza kutuombea. Zaidi sana wanakuwa hawaelewi neno lolote linaloendelea duniani, biblia inasema hivyo katika;

Mhubiri 9:5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

Umeona? Kwahiyo desturi hii, ya kupeleka maombi yetu kwa watakatifu watuombee, ni ya kipagani, Ni ibada za sanamu,  ambayo asili yake ilianzia kwenye dini zinazoamini mizimu inaweza kuwasiliana nasi. Kusema hivi haimaanishi tunawapinga wakatoliki, au tunatangaza chuki hapana, bali tunasemezana ukweli ili tupone, kwasababu safari yetu ni moja sote tuurithi uzima wa milele, sisi tunasema ni wakristo.

https://www.high-endrolex.com/11

Haijalishi utakuwa ulifanya novena ya Rita ikakuletea majibu kiasi gani, bado ni ibada ya sanamu, kumbuka pia shetani analeta majibu, si ajabu mambo hayo kutendeka, ili watu wapumbazike katika hayo.

2Wakorintho 11:14  Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.

Mwombezi wetu ni mmoja tu naye ndiye YESU KRISTO (1Yohana 2:1). Lakini sio pamoja na Petro, au Paulo, au Eliya, au Mariamu, au Yusufu. Hao wote ni watakatifu ambao walihitaji ukombozi tu kama sisi, na wenyewe walituelekeza kumtazama Yesu Kristo, na sio wao.

Mtume Paulo alisema maneno haya;

1Wakorintho 1:13  Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?

Hivyo hakuna haja ya kupeleka maombi yako kwa mtakatifu yoyote, na vilevile wale walio kule hawawezi kutuombea sisi pia. Halikadhalika wewe huwezi kumwombea mwenye dhambi aliyekufa, kwamba Bwana amtoe matesoni. Imani hiyo haipo pia katika biblia. Soma (Waebrania 9:27). Mafundisho ya watu kupitia toharani hayapo katika biblia.

Tujifunze kusoma biblia tutafunguka kwa mengi, mapokeo ya kidini sio Neno la Mungu. Hao wanaoabudu miti na mawe twaweza kuwacheka, lakini tukawa kama wale tu isipokuwa katika mfumo mwingine, tusipopenda kusoma biblia. Tukikataa kuwa wafuasi tu wa kidini tukapenda Neno la Mungu, Roho Mtakatifu atatusaidia kufunguka kwa mengi.

Hivyo ikiwa wewe ulikuwa ni mmojawapo wa wanaopeleka maombi kwa Rita wa kashia, au  kwa mtakatifu mwingine yoyote acha sasa kufanya hivyo. Tubu dhambi ukabatizwe, upokee Roho Mtatakatifu ambaye atakuongoza na kukutia katika kweli yake yote(Yohana 16:13).

Ikiwa upo tayari leo kuokoka, basi waweza fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

Novena ni nini? Na je ipo kibiblia?

Roho Mtakatifu ni nani?.

LITANIA YA BIKIRA MARIA JE! NI SALA YA KIMAANDIKO?

KUNA AINA NGAPI  ZA MAOMBI?

Kuomba katika roho ni kupi? na je nifanye nini ili niweze kuomba hivyo?

SISI TU MANUKATO YA KRISTO.

MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.

Rudi nyumbani

Print this post

USIKWEPE CHUO CHA UTAKATIFU.

Zawadi kubwa Mungu aliyompa mwaminio ni UTAKATIFU. 

Utakatifu ni ile hali kuwa mkamilifu kama Mungu, kutokuwa na dosari au kasoro yoyote, msafi asilimia mia moja, bila kosa lolote ndani yako. 

Sasa heshima hii tumetunukiwa na Mungu, jambo ambalo hapo zamani halikwepo, ilihitaji matendo ya haki ya Mtu kuufikia, lakini hapakuwahi kutokea mwanadamu yoyote aliyeweza kufikia cheo hicho cha juu sana cha Mungu, yaani kutokuwa na dhambi kabisa.

Lakini pale tunapomwamini Bwana Yesu, siku hiyo hiyo, Mungu anatufanya Watakatifu kama yeye, haijalishi bado tutakuwa na asili ya dhambi nyingi kiasi gani. Hiyo ndio maana ya neema. Tunaitwa watakatifu bila ya kujisumbua kwa lolote.

Lakini sasa lengo la Mungu sio tuwe “watakatifu katika dhambi” Bali “tuwe watakatifu katika utakatifu”. Hivyo kuanzia huo wakati anaanza kumfundisha mtu kuusomea hadi kuuhitimu Utakatifu wake,aliopewa ili aendane na cheo alichotunukiwa tangu mwanzo.

Na hapo mtu akishindwa kupiga hatua, basi anaondolewa heshima hiyo kwake, na hivyo hawezi tena kuwa kama Mungu, na matokeo yake wokovu unampotea.

Mwaka Fulani hapa nchini kwetu kulikuwa na askari mmoja aliyeonyesha kitendo cha kishujaa kukataa rushwa ya milioni 10, ambapo alishawishiwa aipokee ili aifute kesi ya watuhumiwa wawili waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka,. Lakini yeye hakukubali, na ilipokuja kubainika, mkuu wa jeshi la polisi (IGP) akafurahishwa naye, Akampandisha cheo (kwani alikuwa ni askari wa chini). Lakini cha kushangaza baada ya kama miaka mwilini tukaja kusikia Yule askari aliyepandishwa cheo ameshushwa cheo kile. Kufuatilia ni kwanini imekuwa hivyo? Jeshi la polisi likatoa taarifa kuwa alionyesha utovu wa nidhani, wa kukataa kwenda kwenye mafunzo ya cheo chake kipya.  Akidhani kwasababu IGP amempandisha basi inatosha hakuna haja ya mafunzo tena. Akasahau kuwa ufahamu wake wa kielimu ni lazima uendane na cheo chake, kwamba akiwa bado na cheo kikubwa, wakati huo huo anapaswa aendelee kusoma,na kujifunza kimatendo, ili aweze kutumika ipasavyo. Lakini akashushwa cheo na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kukataa kutii amri ya jeshi.

Ndivyo ilivyo katika UTAKATIFU tunaopewa na Mungu bure, ni lazima tuutendee kazi kwa kila siku kupiga hatua mpya ya mabadiliko. Huwezi kusema umeokoka (wewe ni mtakatifu), halafu maisha yako ya mwaka jana na mwaka huu ni yaleyale wewe sio mtakatifu.  Kila siku lazima uwe na mabadiliko, ulikuwa unabeti, unaacha kubeti, ulikuwa unavaa mavazi ya uchi uchi, unayachoma moto, ulikuwa unajichubua, unaacha, ulikuwa unasengenya unakaa mbali na wasengenyaji, ulikuwa unakesha kwenye muvi usiku kucha unaacha hayo, unatumia muda wako mwingi kwenye kujisomea biblia, ulikuwa ni mtu wa rushwa unaanza kuondoa vitendo hivyo kwenye biashara yako. Ulikuwa huwezi kufunga na kuomba unaanza kujizoeza kuwa mtu wa rohoni, unafunga, unaomba, na kukesha, Huko ndiko Mungu anakokutaka. Anaona umekiheshimu cheo alichokupa.

Ukiwa ni mtu wa kupiga hatua kila siku, basi Mungu atazidi kukuona wewe ni MTAKATIFU na hivyo utakuwa karibu na yeye. Lakini ukiishi hoe hae, hutambuliki kama umeokoka, au vipi, tabia zilezile za zamani unaendelea nazo, wala hujihangaishi kuziondoa. Usijindanganye wewe umeokoka.

Bwana atusaidie..

Je! Upo ndani ya Kristo? Je unataarifa kuwa hizi ni siku za mwisho? Yesu amekaribia kurudi? Ni nini utamweleza Mungu siku ile endapo leo utaukataa wokovu unaoletwa kwako bure..  Tubu dhambi zako, mgeukie Bwana, akupe Roho Mtakatifu, akupe heshimu hiyo ya utakatifu. Hivyo Ikiwa upo tayari kufanya hivyo basi fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa sala ya toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

FUNDISHO KUU LA NEEMA YA MUNGU KWETU.

MATUNDA 9 YA ROHO MTAKATIFU

UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.

USITAZAME NYUMA!

Kwanini hatuirithi neema kama tunavyoirithi dhambi?

HATARI YA KUHUBIRI INJILI TOFAUTI NA ILIYOANDIKWA KWENYE BIBLIA.

Wakili ni nani kibiblia? Uwakili ni nini?

Rudi nyumbani

Print this post