Matulizo ya mapenzi ni nini? (Wafilipi 2:1).

Matulizo ya mapenzi ni nini? (Wafilipi 2:1).

Jibu: Tusome,

Wafilipi 2:1 “Basi ikiwako faraja yo yote katika Kristo, yakiwako MATULIZO YO YOTE YA MAPENZI, ukiwako ushirika wo wote wa Roho, ikiwako huruma yo yote na rehema,

2 ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja”.

Mapenzi yanayozungumziwa hapo ni ule Upendo wa Kristo kwetu, Matulizo ya mapenzi yanayonenwa  hapo sio matulizo ya mapenzi ya mwili, bali ni Matulizo ya mapenzi ya KRISTO, (Yaani ile hali ya kupata pumziko ndani ya Pendo la Kristo).

Tunapomfahamu Yesu, na jisni anavyotupenda kwa kiwango anachotaka yeye tumfahamu….basi tunapata pumziko kubwa sana na utulivu mkubwa sana ndani ya roho zetu… (roho zetu zinatulia na kuwa na amani).

Biblia (Neno la Mungu) linasema..

Warumi 8:38 “Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,

39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Ukishajua kuwa hakuna Malaika yoyote anayeweza kumfanya Kristo akaacha kukupenda wewe baada ya kumuamini, ni lazima utapata Pumziko na utulivu ndani yako.

Ukishajua kuwa hakuna mwenye mamlaka yoyote duniani, awe kiongozi wa nchi au dunia, ambaye anaweza kumfanya Kristo akaacha kukupenda wewe, basi unapata utulivu ndani yako.

Ukishajua kuwa hakuna kiumbe chochote kilichopo duniani, au chini ya dunia..kitakachoweza kumfanya Kristo akakuchukia basi unapata Pumziko na utulivu usio wa kawaida. Unakuwa huangaiki tena..

Unapojua kuwa siku ile ulipomwamini Kristo, tayari dhambi zako zilifutwa, katika ulimwengu wa roho ulihamishwa kutoka katika nguvu za giza na kuingizwa katika Pendo hilo la Kristo.. basi unapata amani, utulivu na pumziko ndani yako.

Sasa pumziko hilo, na utulivu huo unaoupata kutokana na upendo wa Kristo kwako, ndio unaoitwa MATULIZO YA MAPENZI.

Nabii Isaya alilion Pendo la Yesu miaka mingi sana kabla ya kuja kwake, aliona Yerusalemu inakwenda kufarijiwa, mapigo yake ambayo Bwana alimwadhibu kutokana na dhambi zake, yanakwenda kuponywa, hofu yake inakwenda kuondolewa na Masihi ambaye atakuja.(na Yerusalemu itapokea Matulizo makubwa)..

Isaya 40:1 “Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu.

2 Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa Bwana adhabu maradufu kwa dhambi zake zote”.

Je Umeyapata Matulizo ya Mapenzi leo?. Umetulizwa na Bwana Yesu, au unataabishwa na shetani?.

Kama hujampokea Yesu, basi huna utulivu ndani yako..wachawi watakusumbua, mapepo yatakusumbua, na vile vile hofu ya mauti itakusumbua. Hivyo mpokee Yesu leo, upate pumziko ndani yako.

Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami NITAWAPUMZISHA.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; NANYI MTAPATA RAHA NAFSINI MWENU;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Group la whatsapp Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp


Mada Nyinginezo:

MAPENZI YA MUNGU NI YAPI?

JINSI YA KUMSIKIA MUNGU, NA KUPOKEA MAFUNUO AU JUMBE KUTOKA KWAKE.

TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:

Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?

Furaha ni nini?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments