Lakini tukirudi kwa mwanamke mwingine pili, ambaye naye pia alikuwa katika kiti cha kifalme, aliketi kama malkia, Tunaona Mume wake alipotaka kwenda kuwapa wayahudi amri ya kumuua Bwana Yesu, yeye alikuja na ushawishi mwingine tofauti na Yule wa kwanza, yeye alimwonya sana mume wake asidhubutu kufanya vile kwani ni mtumishi wa Mungu.
Anaeleza jinsi alivyoteswa sana katika ndoto usiku kabla ya Yesu kusulibiwa, embu jaribu kutengeneza picha analala mara ya kwanza, anaota kama yeye ndio anayemngongelea misumari mtu asiye na hatia, anashtuka anaona ni ndoto tu, halafu analala tena, anaota kitu kile kile, anaamka tena, analala jambo lile lile tena linajirudia, hata mara 10, halafu asubuhi anakutana na mtu Yule Yule aliyekuwa anamwona kwenye ndoto analetwa mbele yake…Sura ile ile ya upole inakuja mbele zake,..