Category Archive Wanawake

JE WEWE NI ALAMOTHI?..BASI TIMIZA YAFUATAYO!

Masomo maalumu yahusuyo (Wanawake na mabinti).


Alamothi ni nini? Na nini ufunuo wake? (1Nyakati 15:20)

Jibu: Tusome,

1Nyakati 15:19 “Hivyo hao waimbaji, Hemani, Asafu, na Ethani, wakaagizwa kupiga matoazi yao ya shaba kwa sauti kuu;

20 na Zekaria, na Yaasieli na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na Eliabu, na Maaseya, na Benaya, wenye vinanda vya SAUTI YA ALAMOTHI”

“Alamothi” maana yake ni “wanawake vijana”… Hivyo hapo anaposema vinanda vya sauti ya Alamothi, maana yake ni vinanda vya sauti za “wanawake vijana”.

Hiki ni kipindi ambacho Mfalme Daudi alikuwa analitoa sanduku la Agano la Bwana kutoka nyumbani kwa Ben-edomu na kulipandisha Yerusalemu.

Na wakati wanalipandisha Daudi aliwaandaa wana wa Asafu (watu walio hodari wa kuimba) wenye matoazi pamoja na kundi lingine la watu nane (8) viongozi wa sifa, wenye vinanda vitakavyotoa sauti kuwafuatiliza wanawake vijana waimbaji (Alamothi).

Ni nini tunajifunza?

Kikubwa tunachoweza kujifunza ni jinsi “wanawake walivyo na nafasi kubwa katika kumwimbia Mungu”. Daudi aliona, wana wa Asafu pekee haitoshi (ambao ni wanaume) …..zinahitajika pia sauti za wanawake vijana, katika kumwimbia Mungu. Na utaona jambo hilo Mungu alilikubali sana na likawa Baraka sana kwa Mfalme Daudi.

Na Mungu ni yule yule hajabadilika, kama alizikubali sifa za Daudi na kundi lake, atafanya hivyo hata leo, ikiwa tutasimama vyema katika nafasi zetu.

Ikiwa wewe ni mwanamke au binti.. fahamu kuwa sauti yako ni ya thamani sana katika kumwimbia Mungu, (ndio maana si nzito kama ya mwanaume). Hivyo chukua nafasi hiyo katika kulitimiza kusudi la Mungu ndani yako. Tafuta namna yoyote umwimbie Mungu na Bwana atakubariki.

Zaburi ya 46 ambayo iliandikwa na wana wa Kora, ni Zaburi maalumu kwa ALAMOTHI. Ni nyimbo iliyokusudiwa iimbwe na Maalamothi, yenye kumtukuza Mungu kuhubiri uweza wake.

Zaburi 46:1 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

2 Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.

3 Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.

4 Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye juu.

5 Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa; Mungu atausaidia asubuhi na mapema.

6 Mataifa yalighadhibika, falme zikataharuki; Alitoa sauti yake, nchi ikayeyuka.

7 Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.

8 Njoni myatazame matendo ya Bwana, Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.

9 Avikomesha vita hata mwisho wa dunia; Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari.

10 Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.

11 Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu”

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE

Kwanini wajane vijana hawakupaswa kuandikwa?

Ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi pamoja na sauti ya vinanda.

TATIZO LA NDANI LINALOWASUMBUA VIJANA, WALIOOKOKA.

Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza Naam, wanne walio na mwendo mzuri.

Rudi nyumbani

Print this post

MAOMBI MAALUMU YA WA-WAMAMA / WANAWAKE WA KANISANI.

Kama mwanamke uliyeokoka. Fahamu kuwa una wajibu wa kujiombea wewe, kuombea jinsia yako, na kuliombea Kanisa la Kristo kwa ujumla. Huu ni mwongozo wa kipengele muhimu vitakavyokusaidia katika maombi yako. ambavyo kama utakuwa ni mwombaji wa mara kwa mara katika maeneo hayo, basi unajijengea mazingira ya kuwa  mwanamke bora, mama bora, na zaidi sana mtumishi bora wa Bwana katika mwili wa Kristo.

Mwongozo huu unaweza kuutumia pia muwapo wanawake wawili au watatu katika kikundi chenu cha maombi, au kanisani. Na hivyo kila kipengele tenga muda wa kutosha kuomba.

  • Omba Bwana akufanye kuwa shujaa wa injili, pia omba Bwana anyanyue jeshi la wanawake watetea injili, watumike vema katika nafasi zao kanisani,na nje ya Kanisa, kuwaokoa wenye dhambi. Katika maandiko Mfano wa Hawa ni Prisila Matendo 18:18, 26. 

NANGA: Zaburi 68:11 “Bwana analitoa neno lake; Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa;”

  • Omba Bwana akupe uwezo wa kuirithisha imani kwa vizazi vijavyo, Pia awanyanyue wanamwake  vijana/wazee wengi wa namna hiyo, wenye uwezo wa kuirithisha imani ya Kristo kwa vizazi vingi mbeleni. Imani isiishie kwao tu, bali hata kwa vijukuu na vitukuu vyao.

Mfano wa wanawake  hawa alikuwa ni Loisi.

NANGA: 2Timotheo 1:5  nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo

  • Omba Bwana aamshe kwako na kwa wanawake wote Roho ya uombolezaji(kuugua ndani) mtakaosimama katika mahali palipo bomoka kwa ajili ya kulinyanyua kanisa na wenye dhambi.

NANGA: Yeremia 9:17 Bwana wa majeshi asema hivi, Fikirini ninyi, mkawaite wanawake waombolezao, ili waje; mkatume na kuwaita wanawake wenye ustadi, ili waje;  18 na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji.  19 Maana sauti ya maombolezo imesikiwa toka Sayuni, Jinsi tulivyotekwa! tulivyofadhaika sana! Kwa sababu tumeiacha nchi, kwa kuwa wameangusha makao yetu.

  • Omba Bwana aamshe Kiu ya kupenda kujifunza Neno, ndani yako na kwa wanawake wengine wote wamchao Mungu. Mfano wa Hawa alikuwa ni Mariamu Dada yake Martha.

NANGA:  Luka 10:39  Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake.

  • Omba Bwana akupe Roho ya upole na utulivu; Sio ya vurugu au  kutanga-tanga huku na huko kiroho, au kimwili. Sawasawa na Agizo Mtume Petro aliloliandika kwa kanisa (1Petro 3:1-6).

NANGA: 1Petro 3:4  bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.

  • Bwana aweke Roho ya utii, wewe na kwa Wanawake wote wamchao Bwana ndani ya Kanisa. Mfano wa ile iliyokuwa ndani ya Sara, ambayo aliweza kumtii Mungu, lakini pia mume wake.

NANGA:  1Petro 3:6 Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote

  • Bwana akupe Roho ya kupenda kujisitiri, na kuvaa mavazi ya jinsia yako, vilevile awape na wanawake wote watakatifu moyo huo.  (Kumbu 22:5)

NANGA:  1Timotheo 2:9  Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani

  • Bwana akuumbie Roho ya kujitoa kwake Bwana, kwa mali zako, na kwa nguvu zako. ( Mfano wa hawa alikuwa ni Mariamu magdalena, Mshunami (Yohana 12:3, 2Wafalme 4:8-18))

NANGA: Luka 8:3  na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao

  • Bwana aiamshe Roho ya ‘usaidizi’ katika huduma, pia iumbike katikati ya wanawake. Kumbuka wewe kama mwanamke umepewa karamu kubwa sana ya usaidizi tangu kuumbwa kwako. Ombea itende kazi vema ili iifaidie kanisa na familia.

NANGA:  Mwanzo 2:18  Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye

  • Bwana akuumbie Roho ya uaminifu hata pale ambapo hujapata kitu chochote. Usimwache Bwana.

NANGA: Luka 1:6  Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama. 7  Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana

  • Akupe Roho ya kumwimbia Mungu kwa moyo wote wa furaha na kuchangamka Mfano wa wanawake mashujaa waliomcha Mungu zamani, ambao hawakuona aibu kumwimbia Bwana kwa mioyo yao yote.

 NANGA: Kutoka 15:20 Na Miriamu, nabii mke, ndugu yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza.  21 Miriamu akawaitikia,Mwimbieni Bwana ,kwa maana ametukuka sana;Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini

  • Omba Bwana akuumbie Nguvu ya “maombi ya kung’ang’ania” mpaka ipatikane ichipushwe pia miongoni mwa kundi Mfano wa Hawa alikuwa ni Rispa binti aya ambaye aliweza kukesha milimani kufunga na kuombeleza kwa miezi mingi mpaka mfalme akasikia habari zake, akatoa agizo juu yake

NANGA: Soma – 2Samweli 21, yote

  • Bwana akupe Roho ya Uwazi na kusaidiana kwa umoja na wanawake wenzako wacha Mungu ndani ya kanisa na pia iwepo  kwa wanawake wote.

NANGA: Luka 24:22  tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema, 23  wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai

PIA OMBA…

  • Bwana akuumbie Roho ya uangalizi na ulezi kwa watoto, na vijana katika maadili ya kumcha Bwana

NANGA: 2Yohana 1:1  Mzee, kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuao ile kweli;

  • Upewe Roho ya huruma na ya kutunza uhai. Mfano wa hawa ni  (yehosheba). Aliuhifadhi uzao wa kifalme katika  Israeli kwa kumficha mtoto asiuawe.  (2Wafalme 11:2). Ilikuwa pia kwa mama yake Musa, lakini pia kwa Shifra na Pua wazalisha wa kiebrania

NANGA:  (Soma Kutoka 1:15-19)

  • Roho ya unyenyekevu na ya kujiachilia kwa Bwana moja kwa moja, bila kigugumizi chochote cha rohoni. Mfano wa Ruthu kwa Naomi, ambaye alijitoa kwa mkwewe katika hali zote bila kujali ujana wake, au umaskini wa mkwewe.

NANGA: Ruthu 1:16 Naye Ruthuu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe; Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu;  17 Pale utakapokufa nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; Bwana anitende vivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe name

  • Akupe Moyo wa ujakazi mwema wenye manufaa, utakaowaleta wengine kwa Kristo ikiwa wewe ni mwajiriwa mahali fulani (Mfano wa hawa alikuwa ni Roda, &  Yule kijakazi wa Naamani) – 2 Wafalme 5:1-19, Matendo 12:13
  • Bwana akupe moyo wa kupenda kudumu hekaluni mwa Bwana. Vivyo hivyo na wanawake wote kanisani. Mfano ni Ana binti Fanueli.

NANGA: Luka 2:36  Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. 2.37  Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba

  • Bwana akupe ufahamu wa kuyatunza Maneno ya Mungu moyoni wako. Usiwe wa kutokuzingatia kile Mungu anachosema na wewe. Mfano bora ni  (Mariamu mamaye Yesu)

NANGA: Luka 2:51  Nao hawakuelewa na neno hilo alilowaambia. 51  Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake

  • Roho ya kupenda kujitaabisha kwa Bwana katika hekima yote ya ki-Mungu itokee ndani yako na kwa wanawake wengine. (Martha)-

NANGA: Luka 10:40  “Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi;..”

  • Bwana akujalie wewe na wanawake wote Roho ya nguvu na ya ujasiri ya kuweza hata kuliamua taifa. Mfano wa Debora, katika nafasi yako kama mama.

NANGA: Waamuzi 4:4 Basi Debora, nabii mke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule.  5 Naye alikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue

  • Roho ya kuthamini, Bwana alivyoviweka mkononi mwako, kuvilinda na kuvitafuta pindi vipoteapo.

NANGA: Luka 15:8  Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione? 15.9  Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea.

  • Bwana akupe Roho ya kuridhika na hali, na mwonekano wako, kutoongeza mapambo mwilini. Usiwe kama Yezebeli-2Wafalme 9:30
  • Bwana awajalie wanawake wote wakue kiroho, ili wasichukuliwe mateka na watu wadanganyifu (2Timotheo 3:6)
  • Bwana awafariji wajane wote, lakini pia awape moyo wa kupenda kutoa na kutumika (Mfano wa Yule aliyetoa senti mbili, Yule aliyetembelewa na Eliya)-

NANGA: Soma (Marko 12:42, 1Wafalme 17:12, Luka 7:11)

OMBA PIA…

  • Roho ya kuwajibika kwa wanawake, Bwana aiamshe kwako na  katika kanisa (kupenda kushughulika Mithali 31:10-31
  • Bwana awajalie wanawake wote Wajawazito kujifungua salama.(Kutoka 1:15-17, Isaya 66:9)
  • Mabinti/ wanawake katika kanisa wanaotaka kuolewa, Bwana awape wenzi sahihi (Abigaili aliolewa na Nabali mume asiyestahili. -1Samweli  25)  Jambo hilo lisitokee ndani ya kanisa.
  • Magonjwa yanayoishambulia jinsia ya kike. Bwana ayafute mbali na wewe na ndani ya kanisa la Mungu (Marko 5:25-34)

PIA OMBA HIZI TABIA ZIONDOKE NDANI YAKO NA WANAWAKE WOTE…

  • Roho ya kujichanganya na makundi yasiyofaa/ kutokuwa na mipaka, itoweshwe (Dina hakuwa na mipaka,  akahadaiwa na watu wa kidunia – Mwanzo 34:1).
  • Roho ya utoaji mimba, ipotelee mbali kwa wanawake wacha Mungu na kwa jamii yetu (Kutoka 20:13, Ayubu 3:3-12).
  • Bwana aifutilie mbali tabia ya kupuuzia maono: Mke wa Herode alisemeshwa kwa ajili ya haki ya Yesu lakini hakuchukua hatua stahiki, kama Bwana alivyotaka (Mathayo 27:19)
  • Wanawake wa kikristo wanaonyanyaswa kijinsi agh. Kulazimishwa kuolewa, kukeketwa, kubakwa, kupigwa, kunyimwa haki za elimu, na kumcha Mungu n.k. Bwana afutilie mbali hiyo roho; > Mfano ni Kisa cha Tamari na amnoni (2Samweli 13)
  • Nguvu za giza zinazowavaa wanawake kiwepesi, zisipate nafasi ndani ya kanisa la Kristo.( Marko 16:9)
  • Roho ya udanganyifu wa nyoka, (kushawishwa) Bwana aifukuzie mbali na kanisa lake takatifu (Mwanzo 3:1)
  • Roho ya uuaji ya Yezebeli na Athalia, na herodia  isipate nafasi ndani ya Kanisa la Bwana –, (2Wafalme 11:1, Mathayo 14:8)
  • Roho ya kiburi isitokee miongoni mwa kundi (Vashti –Esta 1:12)
  • Roho ya masengenyo, na udadisi ifutwe katikati ya kundi la Kristo (1Timotheo 5:13)
  • Roho za ndoa kuvunjika, na magomvi zisitoe mzizi ndani ya kanisani.  (Waefeso 5:33)
  • Roho ya kukufuru kama ya Mke wa Ayubu Bwana aifutilie mbali. (Ayubu 2:9)
  • Roho ya kupenda ulimwengu na mambo ya kidunia, iondoshwe (Mke wa Lutu) –Mawnzo 19:26
  • Roho ya tamaa ya kuiba vya Mungu, isichipuke ndani ya kundi la wanawake ( mkewe Safira) Matendo 5:1
  • Roho ya uzinzi ife iyeyushwe kabisa (mke wa potifa)- Mwanzo 39:7
  • Roho ya ushirikina na uchawi isipate nafasi miongoni mwa wanawake (mganga wa Sauli)-Samweli 28:11
  • Roho ya mashindano itoweke miongoni mwa wanawake (Lea na Raheli, wanawake hao)-Mwanzo 29:30
  • Roho ya kuzira/ kukwazika mapema hata kutaka kuacha kutumika ifitwe miongoni mwa wanawake (Hajira- Mwanzo 16:9)
  • Roho ya kutumiwa na adui (u-agent), ili kuliangusha kundi ifutwe (Delila –Waamuzi 16)
  • Roho ya kusema uongo/  kutumia hila,  isionekane ndani ya kundi (Mama yake Yakobo – Rebeka- Mwanzo 27:6)
  • Roho ya uchungu usiokoma moyoni, vinyongo, visasa, kutokuachilia, kutokusamehe, iyeyuke ndani ya wanawake.(Yakobo 3:14)
  • Roho ya matabaka, ndani ya Kanisa ipotelee mbali(Wafilipi 4:2). Sintike na Euodia
  • Roho ya udhuru isisimame ndani ya kundi la wanawake kanisani. – (Matendo 1:14)
  • Roho ya kudharau, watu wa Mungu, au kazi ya Mungu, isiwe na sehemu miongoni mwa wanawake( Mfano wa Mikali, binti Sauli. 2Samweli 6:16

Kwa ushauri/ Msaada/ Maombezi /Ratiba za ibada, wasiliana nasi kwa mawasiliano haya;

Na, Mwl Denis & Devis Julius

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

KANUNI YA KUOMBA NA KUPOKEA.

MWONGOZO WA MAOMBI YA WAHUDUMU/ WASIMAMAO MADHABAHUNI.

Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?

NIFANYE NINI ILI MUNGU AYAJIBU MAOMBI YANGU?

MWANAMKE, BINTI, MAMA.( Sehemu ya 1)

Rudi nyumbani

Print this post

Mabibi wastahiki walikuwa ni watu gani? (Esta 1:18).

(Mada maalumu kwa wanawake)

Jibu: Mabibi Wastahiki ni “wanawake wa heshima”.. kundi hili la wanawake lilihusisha wake za Wafalme, Maliwali au Maakida au Majumbe..

Wakati mfalme Ahasuero alipowafanyia maakida wake na maliwali wake karamu, biblia inatuambia kuwa Malkia Vashti (mke wa mfalme), yeye naye aliwafanyia wanawake (ambao ni wake wa hao maakida na maliwali) karamu.

Esta 1:2 “siku zile mfalme Ahasuero alipoketi katika kiti cha enzi cha ufalme wake, huko Shushani ngomeni;

3 mwaka wa tatu wa kumiliki kwake, ikawa aliwafanyia karamu maakida wake wote na majumbe wake; wakuu wa Uajemi na Umedi, watu wenye cheo na maakida wa majimbo, wakihudhuria mbele zake. 

4 Akawaonyesha utajiri wa ufalme wake mtukufu, na heshima ya enzi yake bora siku nyingi, maana siku mia na themanini……………………..

9 Tena Vashti, malkia, naye akawafanyia karamu WANAWAKE NDANI YA NYUMBA YA KIFALME YA MFALME Ahasuero”.

Sasa hao wanawake waliokuwa wake za “maliwali na maakida” ndio waliojulikana kama “mabibi wastahiki”.. wakiongozwa na Malkia Vashti.

Lakini tunachoweza kujifunza ni kuwa ile karamu ya hawa wanawake haikuwa na utukufu wowote, kwani iliishia kuleta aibu kubwa katika ufalme wote wa Uajemi. Kwani Malkia Vashti alikosa utii kwa Mfalme alipoitwa, na Zaidi sana alionyesha dharau hizo mbele ya Mfalme na waliwali wake wote.

Na huenda pia kiburi hicho kilichochewa na jopo la wale wanawake wengine wastahiki waliohudhuria karamu hiyo ya Malkia Vashti. Hiyo ikifunua kuwa hakuna cha maana walichokuwa wanakizungumza au kukipanga katika hiyo karamu Vashti aliyowaandalia, huenda yaliyokuwa yanazungumziwa kule ni UMBEA TU na kusema mapungufu ya waume zao!

Hiyo ikamfanya Vashti apoteze umalkia wake, na hata hao wanawake wengine ambao wastahiki kuzidi kutawaliwa na waume zao.

Esta 1:16 “Basi Memukani akajibu mbele ya mfalme na maakida, Huyu Vashti, malkia, hakumkosa mfalme tu peke yake, ila na maakida wote, na watu wote pia walioko katika majimbo yote ya mfalme Ahasuero. 

17 Kwa maana tendo hilo la malkia litajulikana na wanawake wote, hata waume zao watadharauliwa machoni pao, itakaponenwa ya kuwa mfalme Ahasuero aliamuru Vashti, malkia, aletwe mbele yake, bali hakuja. 

18 Hata na leo hivi mabibi wastahiki wa Uajemi na Umedi waliokwisha kuzisikia habari za tendo lake malkia watawaambia vivi hivi maakida wote wa mfalme. Hivyo kutatokea dharau nyingi na ghadhabu tele.

 19 Basi mfalme akiona vema, na itoke kwake amri ya kifalme, nayo iandikwe katika sheria za Waajemi na Wamedi isitanguke, ya kwamba Vashti asifike tena mbele ya mfalme Ahasuero; na umalkia wake mfalme ampe mwingine aliye mwema kuliko yeye.

 20 Basi mbiu ya mfalme atakayoipiga itakapotangazwa katika ufalme wake wote, nao ni mkubwa, wake wote watawaheshimu waume zao, wakubwa kwa wadogo.

 21 Basi neno hili likawapendeza mfalme na maakida; naye mfalme akafanya sawasawa na neno lake Memukani.

 22 Kwa maana alipeleka nyaraka katika majimbo yote ya mfalme, kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake, ya kwamba kila mwanamume atawale nyumbani mwake, na kuitangaza habari hii kwa lugha ya watu wake”.

Tabia kama hii inaendelea mpaka leo kwa baadhi ya wanawake walioolewa!, ambao baada ya kuolewa wanawaona waume zao kama si kitu tena, na hata kupoteza UTII kwao!. Pasipo kujua kuwa kwa kufanya hivyo wanazidi kujipotezea nafasi zao ndani ya familia zao, kwani badala ya kuwa kichwa Mungu anawaweka kuwa wa mwisho.

Neno la Mungu linasema wanawake na wawatii waume zao.

1Petro 3:1 “Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;

2  wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.

3  Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;

4  bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.

5  Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, NA KUWATII WAUME ZAO”

Soma tena Waefeso 5:24 na Tito 2:5 utaona jambo hilo hilo, sasa mwana-mama unatolea wapi kiburi!!!. Badilika, na anza kuwa mtii, ikiwa haupo ndani yako, na hiyo ni kwa faida yako na familia yako. Kitabu cha Esta, huenda kingepaswa kiitwe kitabu cha Vashti, lakini kwa kiburi chake, umalkia wake akapewa Esta.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

ESTA: Mlango wa 5, 6 & 7

LITANIA YA BIKIRA MARIA JE! NI SALA YA KIMAANDIKO?

YESU ANAKWENDA KUIBADILISHA OFISI YAKE.

NI KIJIJI CHA AINA GANI UPO?

MAJESHI YA PEPO WABAYA.

Rudi nyumbani

Print this post

Mwanamke aliyepotelewa na sarafu yake.

Huu ni mwendelezo wa Mafundisho maalumu yawahusuyo wanawake.

Mwanamke aliyepoteza shilingi moja.

Luka 15:8  Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione? 9  Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea.

Bwana Yesu alipenda kutumia mifano halisi ya kimaisha kutufundisha habari za rohoni. Kwamfano katika habari hiyo tunafahamu mfano huo ulikuwa analenga mambo ya ufalme wa mbinguni, jinsi Mungu anavyomthamini mtu wake mmoja aliyepotea katika dhambi, pindi atubupo na kurejea. Kwamba tendo  hilo linamfanya yeye pamoja na malaika zake mbinguni kufurahi sana.

Lakini leo nataka tujifunze kuhusu mfano huo katika uhalisia wake wa kimaisha kama ulivyoandikwa. Kuna maswali lazima ujiulize kwanini amtaje mwanamke na sio mwanaume. Kisha aipoteze shilingi yake pale NYUMBANI kwake, na sio sehemu nyingine, labda barabarani au sokoni? Tofauti na mfano uliotangulia ambao unamzungumzia Yule mtu aliyepotelewa na kondoo mmoja akawaacha wale 99 akaenda kumtafuta Yule mmoja huko maporini.

Na hatua ambazo alitumia kuitafuta shilingi ile hadi kuipata, kuna funzo gani pia?.

Kumbuka kimaandiko aliyekabidhiwa nyumba aisimamie ni mwanamke, ndio maana biblia inasema,

Mithali 14:1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

Na hazina yake inapatikana humo, lakini pia ikipotea, basi hupotelea humo humo.

Tukisema nyumba hatumaanishi, gorofa, na sebule na jiko. Hapana, bali tunamaanisha wale waliomo mule. Hao ndio hazina yake hasaa.

Sasa katika mfano huo mwanamke huyu alikuwa na shilingi 10, labda tuseme hao ni watoto 10, au ndugu 10, lakini mmoja akapotea, huwenda akawa mtundu, au mwizi, au kibaka, au shoga, au jambazi n.k.  Lakini Mwanamke huyu hakukata tamaa na kukaa chini na kusema, Ahh! Ninao hawa 9, wenye kujitambua na wenye nidhani. Embu ngoja niachane na Yule pasua kichwa mtukutu, mwenye kiburi, asinipe presha, nifarijiwe na hawa wanangu 9 wazuri. Hapana, bali alilazimika kufanya jambo ili kuhakikisha amempata na Yule.

Hivyo kama tunavyosoma, hakukaa tu hivi hivi, na kuzungumza. Bali alichukua hatua fulani, na hatua zenyewe ndio hizi tatu.

  1. Kuwasha taa
  2. Kufagia nyumba
  3. Kuitafuta kwa bidii

Hii ikiwa na maana gani? mpaka anafikia hatua ya kuwasha tamaa, maana yake ni kuwa chumba hicho kilikuwa na giza, hivyo asingeweza kuipata shilingi yake katika mazingira yale. Tafsiri yake ni nini? Alimkaribisha Kristo. Ambaye ndio Nuru ya ulimwengu katika nyumba yake.

Hivyo hatua ya kwanza katika kutatua tatizo lake, alimtambua Kristo kwenye nyumba yake. Na sasa Nuru ilipomulika ndipo akatambua kuwa nyumba ilikuwa chafu. Kama asingewasha taa, kamwe asingeweza kugundua kuwa Vitu havipo katika mpangalio wake. Hivyo ikampasa aanze kwanza kuifagia nyumba ile, aipangilie vizuri. Makombo yaliyodondoka sakafuni ayafagie, vikombe na vijiko vilivyokaa hoe hae, aviweke mahali pake, nguo ambazo hazijakunjwa aziweke kabatini, uwazi uwepo. Hakukimbilia kuitafuta shilingi yake katika hatua hiyo. alijua hawezi kuipata katika mazingira yale, machafu, imejificha sana.

Hivyo ikamchukua muda Fulani mrefu kuisafisha nyumba yake, mpaka hatimaye, pengine baada ya saa 6, ikawa safi. Kila kitu kikawa katika mpangilio wake.

Ndipo sasa akaenda katika hatua ya mwisho ya “kuitafuta kwa bidii ile shilingi”.  Akaanza kupita eneo moja baada ya lingine, hakutoka nje ya nyumba kwenda kuitafuta barabarani, hapana bali pale pale ndani kwasababu alijua fedha zake hazijawahi kutoka nje ya nyumba.

Na hatimaye akaipata. Na mwisho wa siku akawaalika na marafiki zake, wakafurahi pamoja. Kwasababu ilimgharimu kuipata tena.

Hii ni kufunua nini?

Wanawake wengi wanapoona aidha ndugu zao nyumbani, au watoto wao, au ndoa zao zimeharibika,. Wengine wanakimbilia kwa waganga ili wasaidike, hapo umepotea, wengine wanakimbilia kwa washauri wa kijamii, bado hujapata suluhisho. Suluhisho pekee ni Nuru ya ulimwengu. Yesu Kristo, aimulikie kwanza nyumba yako.

Na Yesu anachokifanya ni kukuonyesha madhaifu uliyokuwa nayo, uchafu uliomo nyumbani mwako, ili urekebishe (ndio ufagie). Sasa wengine wanapofikia hatua hii, wanapoona wanahubiriwa waishi maisha ya utakatifu, wawe watu wa ibada majumbani mwao, wawe waombaji, wafungaji, wafukuze tabia zisiojenga majumbani  mwao, waweke mipaka Fulani kwenye familia zao. Wanaona kama wanatwikwa mzigo juu ya mzigo. Wanamkimbia Kristo, wanabakia kulia tu, na kuhuzunika..

Wanachofikiria tu, ni utatuzi wa tatizo, mume aache pombe (aokoke), watoto wawe wasikivu, nyuma iwe na amani, n.k.  lakini hawataki wao wenyewe kurekebisha baadhi ya mambo makwao. Hapo ndugu ukikwepa hatua hii, sahau kukipata unachokitafuta. Hata upewe bahari nzima ya mafuta ya upako, na pipa la chumvi. Unapoteza muda, hutatui jambo lolote.

Kristo anataka usafi kwanza, ndipo akupe jicho la kuiona shilingi yako iliyopotea. Sasa ikiwa utatimiza mambo hayo mawili yaani KRISTO ndani yako, na usafi wako. Kinachofuata ni kutafuta ulichokipoteza.

Hii ndio hatua sasa ya kumuhubiria, kumshauri, kumwonya, kumvuta kwa Bwana. Sasa ukiendelea hivyo hivyo, muda si mwingi utampata kiwepesi sana haijalishi alikuwa amepotea kiasi gani, au alikuwa sugu namna gani. Hakuna linaloweza kujificha mbele ya Nuru. Tatizo lolote sugu unalolijua wewe la kifamilia, kwa kufuata kanuni hizo litatatulika tu.

Hivyo wewe kama mwanamke, itambue huduma hii iliyopewa na Bwana, laiti kama wanawake wote, wangekuwa ni wa kujiwajibisha kwa namna hii, jamii zetu na familia zetu zisingekuwa na migogoro mingi,wala injili isingekuwa ngumu sana kuihubiri kwasababu tayari walishatangulia walioweka misingi bora nyuma. Hii ni huduma kubwa sana kwa mwanamke na Bwana anaithamini sana.

Simama katika nafasi yako wewe kama mama, wewe kama Dada, nyumba au familia itasimama, endapo wewe utasimama.

Bwana akubariki

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mafundisho mengine:

MAFUNDISHO KWA WANAWAKE

MWANAMKE ABIGAILI ANAFUNZO GANI KWA WANAWAKE?

Je mwanamke Fibi, alikuwa ni askofu wa makanisa, kama mitume?

BADO TUTAHITAJI TU KUSAIDIANA.

Je Mungu anaketi katika giza? (1Wafalme 8:12)

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)

Rudi nyumbani

Print this post

JE UNAMTUMIKIAJE BWANA?

Mafunzo maalumu kwa Wanawake.

Karibu tujifunze Biblia,

Je Bwana alishakufanyia muujiza wowote katika maisha yako?..Na ukaufurahia?.. Je baada ya hapo ulimfanyia nini Bwana?.. Je uliishia kushukuru tu na kuendelea na mambo yako? Au kuna lingine la ziada ulilifanya?, kama hukufanya chochote au hukujua nini cha kufanya basi leo fahamu yakupasayo kufanya!

Hebu tujifunze kwa baadhi ya wanawake katika biblia ambao hawakuwa Mitume, wala Waalimu, wala Maaskofu wala wachungaji lakini walikuwa wakimtumikia Bwana Yesu.. na kisha tutazame walikuwa wakimtumikia kwa namna gani?

Mathayo 27:55  “Palikuwa na wanawake wengi pale wakitazama kwa mbali, HAO NDIO WALIOMFUATA YESU TOKA GALILAYA, NA KUMTUMIKIA.

56  Miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yusufu, na mama yao wana wa Zebedayo”.

Hawa wanawake walikuwa wakifuatana na Bwana Yesu kila mahali.. Lakini je! Walikuwa wanafuata naye kumtazama uso?, au kumsikiliza tu anayoyahubiri?..Jibu ni La! Biblia inatuambia walikuwa pia WAKIMTUMIKIA!!.. Sasa swali wakimtumikia kwa nini?..tusome mistari ifuatayo..

Luka 8:1  “Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye,

NA WANAWAKE KADHA WA KADHA ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,

3  na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, WALIOKUWA WAKIMHUDUMIA KWA MALI ZAO”.

Umeona hapo?.. Walikuwa wakimhudumia kwa MALI ZAO!. Ikiwa na maana kuwa gharama kubwa za kuipeleka Injili zilikuwa zinabebwa na hawa WANAWAKE!..  hata ule mkoba ambao Yuda alikuwa anaushika, huenda sehemu kubwa ilijazwa na hawa wanawake!.

Na kwanini wanawake hawa walipata msukumo huo mkuu wa kumhudumia Bwana kwa mali zao?.. Jibu ni kwasababu walitendewa miujiza na Bwana, walitolewa pepo waliokuwa wanawatesa, waliponywa magonjwa  yao yaliyokuwa yanawatesa, walipewa wokovu ndani yao ambao uliwapa Amani na tumaini la maisha..Hivyo wakaona si sawa kumtazama Yesu kwa uso tu na kumshukuru kwa maneno tu!, bali pia kwa vitendo.

Ndipo wakaona wavunje vibweta vyao ili Bwana akaende miji mingi Zaidi kuhubiri, wakaona watoe hazina zao ili wanafunzi wa Bwana wasipungukiwe wanapokwenda kuhubiri miji na miji. Na hivyo wakawa mashujaa wa Imani ambao mpaka leo tunawasoma.

Na sio hao tu, bali pia tunamwona na Mkwe wake Petro, (Mama yake mkewe) ambaye alikuwa anaumwa homa, biblia inasema baada ya Bwana kumponya, alinyanyuka na kuanza KUMTUMIKIA BWANA!.

Mathayo 8:14 “Hata Yesu alipofika nyumbani kwa Petro, akamwona mkwe wa Petro, mamaye mkewe, amelala kitandani hawezi homa.

15  Akamgusa mkono, homa ikamwacha; NAYE AKAONDOKA, AKAWATUMIKIA”

Je na wewe Mama unamtumikia nani?, Na wewe binti unamtumikia nani?…Je umemtumikia Bwana kwa kipi tangu alipokuponya?, tangu alipokufungua?, tangu alipokuinua?, tangu alipokupa wokovu bure?.. Je unamtumikia kwa maneno tu, au pia na vitendo?.

Ni kweli wewe sio Mchungaji, wala Mwalimu, wala Mhubiri, wewe ni kama tu Mariamu Magdalena, au Susana..basi fanya kama hao!.. Na kumbukumbu lako litadumu kama la hao wanawake lilivyodumu, Bwana atakuheshimu na kukuona wewe ni mtumishi wake kama tu walivyo Mitume kwasababu na wewe pia unamtumikia kwa mali zako.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

Katika (Mathayo 25:8 na Marko 16:8) Wale wanawake walitangaza kufufuka kwa Bwana au walikaa kimya?

WANNE WALIO WAONGO.

JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?

Rudi nyumbani

Print this post

MWANAMKE ABIGAILI ANAFUNZO GANI KWA WANAWAKE?

Abigaili.

Huu ni mwendelezo wa mafundisho maalumu yahusuyo wanawake.

Na Leo tutaisikia sauti ya Mungu iliyokuwa nyuma maisha ya huyu mama aliyeitwa Abigaili.

Abigaili ni mwanamke aliyeolewa na mwanaume ambaye halikuwa chaguo la Mungu kwake, ijapokuwa mwanaume huyo alikuwa tajiri, hatujui ni nini kilimsukuma Abigaili katika ujana wake kukubali kuolewa na mwanaume yule, labda pengine Nabali hakuanza vile, alikuja kubadilika baadaye, au pengine wazazi wake walimshurutisha aolewe naye kwasababu ya utajiri aliokuwa nao.

Lakini mwanaume huyo halikuwa chaguo sahihi la Abigaili Kutoka Kwa Mungu, kwani Nabali hakuwajali watu wa chini kabisa, Wala hakuwa mtu wa kurudisha fadhila. Utakumbuka wakati ambapo Daudi anakimbizwa na Sauli, akiwa kule  maporini, alikutana na kundi kubwa la mifugo wa huyu Nabali, hivyo Daudi alichofanya ni kuwapa hifadhi watumwa wake, kuwahakikishia ulinzi, dhidi ya wavamizi wa mifugo ya wachungaji,kwasababu Nabali alikuwa na mifugo mingi sana na kipindi ambacho wanakwenda kuwakata manyoya kondoo wao, waporaji wenye silaha Huwa wanawavamia sana wafugaji..hivyo walidumu na Daudi Kwa muda wote huo mpaka walipomaliza shughuli zao.

Lakini siku moja Daudi alipungukiwa chakula yeye na jeshi lake hivyo wakaona mtu wa karibu atakayeweza kuwasaidia ni huyu Nabali. Ndipo Daudi akatuma wajumbe kwake kumuomba chochote alichonacho awasaidie.Lakini badala ya kupokea fadhili akapokea matusi. Ndipo Daudi akakasirika sana akataka kwenda kumuua Lakini mke wake alipopata habari akafanya kinyume chake akaaanda vyakula na kumpelekea Daudi, ndipo hasira yake ikageuka.

Embu tukisome kisa hichi Kwa ufupi;

1 Samweli 25:9-38

[9]Basi walipofika vijana wake Daudi, wakamwambia Nabali sawasawa na maneno hayo yote kwa jina la Daudi, kisha wakanyamaza.

[10]Naye Nabali akawajibu wale watumishi wa Daudi, akasema, Huyu Daudi ni nani? Na mwana wa Yese ni nani? Siku hizi kuna watumwa wengi wanaomtoroka kila mtu bwana wake!

[11]Basi mimi je! Nitwae mkate wangu, na maji yangu, na machinjo yangu niliyowachinjia hao watu wangu wakatao manyoya kondoo zangu, na kuwapa watu ambao siwajui wametoka wapi?

[12]Basi vijana wake Daudi wakageuka, wakaenda zao, wakarudi, nao wakaja wakamwambia sawasawa na maneno hayo yote.

[13]Kisha Daudi akawaambia watu wake, Haya! Jifungeni kila mtu upanga wake. Nao wakajifunga kila mtu upanga wake; Daudi naye akajifunga upanga wake; nao wakapanda nyuma yake Daudi, wapata kama watu mia nne; na watu mia mbili wakakaa na vyombo vyao.

[14]Lakini kijana mmojawapo alimpasha habari Abigaili, mkewe Nabali, kasema, Tazama, Daudi alituma wajumbe kutoka nyikani waje ili kumsalimu bwana wetu, naye akawatukana.

[15]Walakini watu hawa walitutendea mema sana, wala hatukupata dhara, wala sisi hatukupotewa na kitu cho chote, wakati wote tulipofuatana nao, tulipokuwako mavueni;

[16]watu hao walikuwa boma kwetu usiku na mchana, wakati wote tulipokuwa nao tukiwachunga kondoo.

[17]Basi sasa ujue na kufikiri utakayotenda; kwa sababu yamekusudiwa mabaya juu ya bwana wetu, na juu ya nyumba yake yote; kwa kuwa yeye ni mtu asiyefaa kabisa, hata mtu hawezi kusema naye.

[18]Ndipo Abigaili akafanya haraka, akatwaa mikate mia mbili, na viriba viwili vya divai, na kondoo watano waliofanyizwa tayari, na vipimo vitano vya bisi, na vishada mia vya zabibu, na mikate ya tini mia mbili; akavipakia vitu hivi juu ya punda.

[19]Akawaambia vijana wake, Haya! Tangulieni mbele yangu; angalieni, mimi nawafuata. Ila hakumwambia mumewe, Nabali.

[20]Ikawa, alipokuwa amepanda punda wake, na kutelemka penye sitara ya mlima, tazama, Daudi na watu wake walikuwa wakishuka kumkabili; naye akawakuta.

[21]Basi Daudi alikuwa amesema, Hakika ni bure nilivyokuwa nikilinda nyikani yote aliyo nayo mtu huyu, asipotewe na kitu cho chote cha mali yake yote; naye amenilipa mabaya badala ya mema.

[22]Mungu naye awafanyie hivyo adui za Daudi, na kuzidi, nikimwachia katika wote walio wake hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka asubuhi.

[23]Ndipo hapo Abigaili alipomwona Daudi, alifanya haraka kushuka juu ya punda wake, akamwangukia Daudi kifulifuli, akainama mpaka nchi.

[24]Akamwangukia miguuni pake, akasema, Juu yangu, bwana wangu, juu yangu mimi na uwe uovu; tafadhali mjakazi wako na anene masikioni mwako, nawe uyasikilize maneno ya mjakazi wako.

[25]Nakusihi, bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa, yaani, Nabali; kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma.

[26]Basi sasa, bwana wangu, aishivyo BWANA, na iishivyo nafsi yako, kwa kuwa BWANA amekuzuia usimwage damu, tena usijilipize kisasi mkono wako mwenyewe, basi sasa adui zako, na hao wamtakiao bwana wangu mabaya, wawe kama Nabali.

[27]Na sasa zawadi hii, mjakazi wako aliyomletea bwana wangu, na wapewe vijana wamfuatao bwana wangu.

[28]Nakuomba ulisamehe kosa lake mjakazi wako, kwa kuwa hakika BWANA atamfanyia bwana wangu nyumba iliyo imara, kwa sababu bwana wangu anavipiga vita vya BWANA; tena uovu hautaonekana ndani yako siku zako zote.

[29]Na hata ijapokuwa binadamu angeinuka akuwinde, na kuitafuta nafsi yako, hiyo nafsi ya bwana wangu itafungwa katika furushi ya uhai pamoja na BWANA, Mungu wako; na nafsi za adui zako ndizo atakazozitupa nje, kama kutoka kati ya teo.

[30]Tena itakuwa, hapo BWANA atakapokuwa amemtendea bwana wangu sawasawa na mema yote aliyoyanena juu yako, na kukutawaza juu ya Israeli;

[31]hili halitakuwa kwazo, wala chukizo la moyoni kwa bwana wangu, ama ya kuwa umemwaga damu bure, ama ya kuwa bwana wangu amejilipiza kisasi mwenyewe; tena hapo BWANA atakapokuwa amemtendea bwana wangu mema, ndipo umkumbuke mjakazi wako.

[32]Naye Daudi akamwambia Abigaili, Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye amekuleta hivi leo kunilaki;

[33]na ibarikiwe busara yako, na ubarikiwe wewe, uliyenizuia hivi leo nisimwage damu, wala kujilipiza kisasi kwa mkono wangu mwenyewe.

[34]Kwa kuwa ni kweli, aishivyo BWANA, Mungu wa Israeli, aliyenizuia nisikudhuru, kwamba hungefanya haraka kuja kunilaki, hakika huyu Nabali asingaliachiwa hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka asubuhi.

[35]Basi Daudi akapokea mkononi mwake vitu vile alivyomletea; akamwambia, Haya! Kwea kwa amani kwenda nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako, nami nimeukubali uso wako.

[36]Kisha Abigaili alimjia Nabali; na tazama, alikuwa amefanya karamu nyumbani mwake, kama karamu ya kifalme; na moyo wake huyo Nabali ukafurahiwa ndani yake, kwa maana amelewa kabisa. Kwa sababu hiyo hakumwambia neno, dogo wala kubwa, hata kulipopambazuka.

[37]Ikawa asubuhi, divai ilipokuwa imemtoka Nabali, mkewe alimwambia mambo hayo, na moyo wake ukafa ndani yake, akawa kama jiwe.

[38]Tena ikawa, yapata siku kumi baadaye, BWANA alimpiga huyo Nabali, hata akafa.

Ni nini mwanawake wanapaswa wajifunze kuhusiana na maisha ya Abigaili.

  1. Mwanaume Bora si yule mwenye Mali:

Kundi kubwa la wanawake wengi wa sasa wanaotaka kuolewa kigezo wanachokitazama Kwa wanaume ni Mali, wanasahau kuwa hata shetani hutoa Mali. Nabali alimsumbua sana Abigaili katika maisha yake ya ukamilifu, na kama asingekuwa na bidii katika busara yake angeshauliwa mbali na Daudi pamoja na Mali zao. Kufunua kuwa Kristo kama mfalme wetu, Huwa anaziadhibu familia Kwa makosa ya wanandoa wasiowajibika kiroho. Haijalishi wingi wa Mali walizonazo. Wewe kama mwanamke unayekaribia kuolewa kumbuka mwanaume anayemcha Mungu ndio chaguo sahihi kwako, na si vinginevyo.

  1. Pili Abigaili analiwakilisha kundi la wanawake ambao, wameshaingia katika ndoa za watu wasiosahihi.

Wanawake wengi wapo kwenye ndoa, lakini baadaye sana ndio wanakuja kugundua kuwa waume walionao hawakuwa Kutoka Kwa Bwana. Wengine ni wazinzi, wengine ni walevi kama Nabali, wengine hawajali kazi za Mungu Wala Roho zao wenyewe, wengine majambazi, wengine wanawatesa n.k.

Lakini utaona busara ya Abigaili haikuwa kwenda kutafuta mwanaume mwingine aolewe naye, kisa mume wake ni mpumbavu, ila aliendelea kudumu katika haki na ukamilifu, aliendelea kumwombea rehema mume wake hata Kwa maadui zake. Ijapokuwa alikuwa mjinga, lakini hakujaribu kujitenga na mumewe, alimwachia Mungu amfanyie wepesi. Na tunaona Mungu mwenyewe ndio alikuja kushughulika na Nabali akamuua, Kisha Abigaili akawa mke wa Mfalme Daudi. Pumziko la ndoa yake likaja.

Hata sasa wewe kama mwanamke ambaye upo katika ndoa chungu. Huitaji kuizira ndoa hiyo, badala yake omba rehema, na wokovu Kwa mume wako kwa Yesu. Naye ataugeuza moyo wake. Bwana hatatumia njia ya kumuua, lakini ataua uovu na ubaya ulio ndani yake. Na atakuwa tu mume Bora, lakini  usichoke kuomba ukasema nimeomba sana sijaona mabadiliko.yoyote… wewe endelea kuomba hata kama itapita miaka 20, ujue Mungu anaona na kusikia maombi Yako tu, atatenda jambo. Huyo atakuwa mume Bora zaidi ya unavyodhani, usipozimia moyo.Hivyo iga busara ya Abigaili.

Anza sasa kuijenga ndoa Yako. Bwana akubariki.

Shalom.

Je! Umeokoka? Je unafahamu kuwa hizi ni nyakati za mwisho na Mlango wa neema unakaribia kufungwa? Unasubiri nini usiokoke? Itakufaidia nini uupate ulimwengu wote halafu upate hasara ya nafsi Yako? Ikiwa upo tayari kumkabidhi Leo Bwana Yesu maisha Yako. Basi wasiliana nasi Kwa namba zetu hizi Kwa ajili ya mwongozo huo Bure.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MASOMO MAALUMU KWA WANAWAKE.

NI KITU GANI TUNAJIFUNZA KWA RISPA, BINTI AYA?

Je! kuna mwanamke mwingine aliyempaka Bwana marhamu (manukato) zaidi ya Mariamu ndugu yake Lazaro?

Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo; Nayo hushukia pande za ndani za tumbo

Na ulimi laini huvunja mfupa.(Mithali 25:15)

Kwanini Yesu Kristo ni mwana wa Adamu?

MISTARI YA BIBLIA YA FARAJA.

Rudi nyumbani

Print this post

Biblia inasemaje kuhusu Nywele?

Biblia imetoa maelekezo kuhusu Nywele kwa jinsia zote mbili (Ya kike na Kiume).

JINSIA YA KIUME:

Biblia inasema Mwanaume hapaswi kuwa na Nywele ndefu.. kwasababu kichwa chake yeye ni Utukufu wa Mungu..

1Wakorintho 11:3 “Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu

Hivyo kwa Mwanaume kuziweka Nywele zake kuwa ndefu ni aibu kwake na ni kukiaibisha Kichwa chake hicho ambacho ni  Kristo.

Tusome..

1Wakorintho 11:14  “Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake?”

Na sio tu hatakiwi kuwa na Nywele ndefu, bali hata “Kufunika kichwa” awapo ibadani, maana yake ni kwamba  mwanaume anapokuwa ibadani hapaswi kuvaa kofia, au kuweka kitu chochote kichwani kinachoashiria kufunikwa kwa kichwa chake (maana yake kichwa chake siku zote kinapaswa kiwe wazi).

Na vile vile Mwanaume hapaswi kusuka Nywele, wala kuweka mitindo mitindo kichwani kwasababu kichwa chake ni utukufu wa Mungu.

JINSIA YA KIKE:

Katika jinsia ya Kiume tumesoma kuwa ni aibu kwa mwanaume kufunika kichwa, lakini tukirudi katika jinsia ya kike ni kinyume chake. Kwamba ni Aibu mwanamke kuwa na Nywele fupi na ni FAHARI MWANAMKE KUWA NA NYWELE NDEFU.

1Wakorintho 11:15 “Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi”.

Wanawake wote ni sharti waache nywele zao ziwe ndefu kulingana na biblia, kuzikata Nywele au kuzifanya fupi, pasipo sababu yoyote ya msingi kama vile magonjwa, au udhaifu wa mwili, ni kwenda kinyume na maagizo ya Mungu.

Ndio maana Upara (Ulaza) huwa hauwapati wanawake, bali wanaume tu!!..Hiyo ni kuonyesha kuwa wanawake wamekusudiwa kuwa na Nywele vichwani mwao wakati wote wa maisha yao, na wanaume ni kinyume chake.

Na zaidi sana biblia inazidi kuelekeza kuwa hata kama Mwanamke atakata nywele zake kutokana na matatizo Fulani Fulani, labda magonjwa au kutokana udhaifu wa nywele kukatika zenyewe basi hapaswi kutembea nje akiwa na nywele zake hizo fupi, bali anapaswa afunike kichwa chake kwa kitambaa au kwa kitu chochote kile.

1Wakorintho 11:6  “Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.

7  Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume”.

Na mwanamke anapokuwa ibadani awe na nywele ndefu au fupi, ni Agizo la Bwana kwamba afunike kichwa chake, kwasababu kuu 2

Sababu ya Kwanza ni ili asikiabishe kichwa chake ambacho ni MWANAUME. Na sababu ya pili ni kwaajili ya MALAIKA. Tunapokuwa ibadani Malaika wa Bwana wanahudumu pamoja na watakatifu. Malaika hawa Bwana aliowaweka kwaajili yetu wana uhusiano mkubwa sana sisi katika kutuhudumia Soma Mathayo 18:10.

Kwahiyo tunapokuwepo katika ibada na ndani yake kukawa kunafanyika mambo ambayo ni kinyume na Neno la Mungu, malaika hawa wanaondoka, na hivyo kufanya ibada kupoa na utukufu wa Mungu kupungua.

Na pia Wanawake hawapaswi kusuka nywele zao, au kuvaa wigi, au kuzibadilisha maumbile nywele zao aidha kwa kuziweka kemikali, au dawa za kuzifanya zilale, Biblia haijawapa maagizo ya kuzifanya nywele zilale au zing’ae au ziwe kama za jamii ya watu Fulani, Hapana!.. imesema “ZIWE NDEFU!!” Basii!!..

1Timotheo 2:9  “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

10  bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.

11  Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna”

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 2: Upande wa wanawake)

Je kuchonga Nywele na Ndevu ni dhambi?

MSHAHARA WA DHAMBI:

FUVU LA KICHWA.

NGUVU YA MNADHIRI WA BWANA.

Rudi nyumbani

Print this post

Walakini ataokolewa kwa uzazi wake.

SWALI: Biblia inaposema mwanamke ataokolewa kwa uzazi wake, inamaanisha nini?

1Timotheo 2:14 “Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.

15 Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi”.


JIBU: Tofauti na inavyotafsiriwa na watu wengi, kwamba andiko hilo linamaanisha kuwa mwanamke yeyote ambaye atakuwa na watoto wa kulea, basi mwisho wa siku ataokolewa kwa kutimiza tu kusudi hilo.  Mtazamo ambao sio sahihi na unakinzana na maandiko, Kwasababu kama kila mwanamke angekuwa anaokolewa kwa namna hiyo, hata wanawake wachawi nao wangeokolewa kwasababu na wao pia wanao watoto wa kulea.

Lakini biblia ilimaanisha nini kuandika hivyo? 

Mtume Paulo aliandika maneno hayo, kuonyesha jinsi gani huduma ya mwanamke ambaye ana watoto jinsi ilivyo na nguvu hata kusababishia wokovu kwake mwenyewe IKIWA atawalea watoto wake katika misingi ya imani, upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi kama ilivyoainishwa hapo..Na sio kwa kuzaa tu basi.

Kwasababu atakuwa ameifanya huduma ya kuokoa kizazi kingine.. Tengeneza picha kama wanawake wote ulimwenguni wangekuwa wanatimiza wajibu wao huu wa kuwalea watoto wao katika misingi ya imani, leo hii, kusingekuwa na haja ya kuhubiri injili kwasababu watoto wote wangekuwa tayari wanamjua Mungu. Lakini injili imekuwa ngumu kwa kizazi cha sasa kwasababu jambo la kwanza mzazi analolithamini kwa mtoto wake ni elimu tu, Mungu ni ziada, mtoto akifaulu darasani ndio furaha yake kubwa, wakati hajui hata mstari mmoja wa biblia. Hajui hata pambio moja la kumsifu Mungu. Mzazi haoni aibu hata mtoto wake anakuwa hadi mtu mzima hajui biblia ina vitabu vingapi.

Kwahiyo hapo mtume Paulo alikuwa anaonyesha nguvu iliyopo katika mwanamke kulea watoto wake vema, ambayo mwisho wa siku itampelekea hata na wokovu wake mwenyewe. Kwamfano Mungu akiona mtoto Yule ambaye alilelewa katika misingi kama Samweli, amekuwa sababu ya wokovu kwa Israeli, unategemea vipi Mungu amwache mama aliyemlea?. Ni sawa tu na yule anayewavuta watu kwa Kristo, ambao biblia inasema kitendo hicho kina nguvu ya kuokoa roho ya mhubiri na kufunika wingi wa dhambi zake.

1Petro 5:20 “jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi”.

Kwahiyo ikiwa wewe ni mwanamke na Mungu kakujalia watoto ujue jukumu lako la kwanza, la injili ni kwa watoto wako, hakikisha hao wanakuwa katika misingi ya kumcha Mungu, wafundishe, na pale wanapokosea Mungu kakupa ruhusu ya kuwaadhibu, lengo ni kuwaweka katika mstari wa kumcha Bwana, na sio kuwatesa. Ukifanya hivyo matokeo yake utakuja kuyaona baada ya haya maisha hapa duniani.

Tito 2:4 “ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao;

5 na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe”.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

MWANAMKE ULIYEKOMAA KI-UMRI, ITAMBUE HUDUMA YAKO.

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.

Raheli aliwalilia vipi watoto wake?

MWANAMKE, BINTI, MAMA.( Sehemu ya 1)

TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:

Rudi nyumbani

Print this post

MWANAMKE, BINTI, MAMA. (Sehemu ya 3)

Hii ni sehemu ya tatu ya mfululizo wa masomo kwa wanawake, katika sehemu ya kwanza  na ya pili tumeona, ni kwanini Bwana aliwatambua baadhi ya wanawake, kwa jinsia zao, na sio kwa majina yao, kwa kuwaita “wanawake”, na sehemu nyingine kuwatambua kwa mionekano yao kwa kuwaita “Binti” na sio labda kwa majina yao..ipo sababu, ikiwa hujapata bado, chambuzi zake, basi tutumie msg inbox tukutumie..

Lakini leo tutasonga mbele tena, kuona ni kwanini baadhi ya wanawake, aliwatambua kwa majina ya “MAMA”.

Mama ni cheo cha ukomavu, kwasababu mpaka uitwe mama ni wazi kuwa lazima utakuwa na watoto uliowazaa au unaowalea chini yako. Sasa tukirudi kwa Bwana Yesu, kuna wanawake aliwaona ni “Wamama rohoni”, sio mwilini, kwasababu kulikuwa na wanawake wengi, lakini si wote aliwaita “Mama” kama tu vile si wote aliwaita “Binti yangu”, bali baadhi tu.

Sasa embu twende tukasome baadhi ya Habari katika biblia kisha tuone, ni nini Bwana anatufundisha katika Habari husika. Mwanamke wa kwanza tutakayemtazama ni yule mkananayo. Tusome;

Mathayo 15:21 “Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni.

22 Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.

23 Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.

24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.

26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.

27 Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.

28 Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, MAMA, IMANI YAKO NI KUBWA; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile”.

Angalia asili ya huyu mwanamke, hakumtafuta Bwana kwa shida zake mwenyewe, au kwa matatizo yake mwenyewe, bali alimtafuta Bwana Yesu kwa shida za mwanawe.. Japokuwa mwanzoni hakujibiwa chochote, hata baada ya pale alipewa na maneno ya kukatishwa tamaa ya kuitwa mbwa, lakini bado hakuacha kuomba kwa shida ya mtu mwingine, kwasababu uzito wa mwanae ulikuwa kama wakwake.

Hiyo ni kuonyesha ni jinsi gani asivyojali vya kwake tu, bali hata vya wengine…

Mwanamke mwingine ni Mama yake Yesu mwenyewe, ambaye tunamsoma katika Yohana 2:1-4 siku ile alipoalikwa katika Harusi..

Yohana 2:1 “Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.

2 Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.

3 Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai. 4 Yesu akamwambia, MAMA, TUNA NINI MIMI NAWE? Saa yangu haijawadia”.

Angalia tabia yake alijali shida za wengine, aibu za wengine, akazifanya kama ni za kwake. Na kumpelekea Kristo, na muda huo huo akamwita “mama”

Mwingine ni Mariamu Magdalena, asubuhi ile ya kufufuka kwa Bwana, alikuwa akilia pale makaburini ndipo Yesu akamtokea na kumwambia “Mama unalilia nini?” Saa hiyo hiyo Yesu akamtuma kwa ndugu zake kwenda kuwatangazia injili. Akawa mtu wa kwanza kupewa neema ya kuwahubiria watu wengine Habari za kufufuka kwa Bwana Yesu. (Yohana 20:11-18)..

Neema hiyo si kila mwanamke atapewa, bali ni wale “wamama rohoni tu” Wanawake waliokomaa kiroho,ambao wanajua wajibu wao kwa Bwana, wanajua kuwaongoza wengine katika njia za Mungu, haijalishi umri wao Rohoni watu kama hawa, wanawekwa kundi moja na akina Sara, na Rebeka, na Mariamu, na Elizabeti na wengineo. Kwasababu wamevuka viwango cha utoto, hadi kufikia hatua ya utu uzima ya kuzaa na kulea.

Swali ni je! Wewe, dada upo katika kundi gani? Bwana anapokuona anakutambuaje? msichana? Au Mtu? Mtoto? Au Mama?. Kabla hujafikiria kuyatazama Maisha ya mitume wa Yesu mfano wakina Petro waliishije, embu tafakari kwanza, Maisha ya wanawake wacha Mungu katika biblia waliishije. Hiyo itakusaidia sana mwanamke.

Tamani sana, Kristo akutambue kama “Mama” Ni heshima ya juu sana, Kristo anaweza kumpa mwanamke, iliyosawa na ya “Kitume”. Kua kiroho timiza wajibu wako wa kuitangaza injili na pia kuwasaidia wengine kumjua Mungu rohoni.

Bwana akubariki.

Maran atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

MWANAMKE, BINTI, MAMA. (Sehemu ya 2)

Hii ni sehemu ya pili ya mfululizo wa masomo kwa wanawake, katika sehemu ya kwanza tumeona, ni kwanini Bwana alipokutana na yule mwanamke mwenye dhambi, alimtambua kwa jinsia yake (Yaani “mwanamke”) na sio kwa mwonekano wake wa kike pengine wa kiumri au  wa kimaumbile. Hiyo ni kufunua kuwa ujumbe alioubeba yule mwanamke ulikuwa ni wa kijinsia.. yaani maalumu kwa wanawake. Hivyo kama hukupata maelezo yake, unaweza kunitumia ujumbe inbox nikakutumia.

Leo tutaenda katika sehemu ya pili: ya BINTI.

Mahali pengine, Bwana Yesu, aliwatambua wanawake wengine kama, binti zake.. Na cha ajabu ni kuwa, wengine walikuwa pengine wana umri mkubwa kuliko yeye, lakini bado aliwaita BINTI zake, akifunua kuwa kutazama kwake hakukuwa katika jicho la kimwili bali la rohoni. Embu tusome, kisa hiki kimoja..kisha tuone ni ujumbe gani Bwana alitaka kuupitisha kwa ulimwengu kupitia mwanamke huyu.

Mathayo 9:20 “Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake.

21 Kwa maana alisema moyoni mwake, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona.

22 Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, BINTI YANGU; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.”.

Swali la kujiuliza ni kwanini alimtambua mwanamke huyu kama binti na sio pengine kama Mama, au bibi?

Ni kwasababu ya Imani yake ya kipekee aliyokuwa nayo kwake..Ambayo hakuiona kwa watu wengine wote waliomfuata, ijapokuwa alihangaika kwa miaka 12 kutafuta suluhu la matatizo yake asipate, lakini alipofika kwa Yesu kwa mara ya kwanza tu hakumuhesabia kama mmojawapo wa wale matapeli aliokutana nao, huko nyuma, waliomchukulia fedha zake.

Bali alimwamini moja kwa moja kwa asilimia 100, akasema, nitakapoligusa tu pindo la vazi lake, muda huo huo nitakuwa mzima, kumbuka hakusema sio “naamini nitapona, au pengine nitapona” hapana, bali alisema “NITAPONA” kuonyesha kuwa alikuwa na uhakika wa yule aliyekutana naye sio mbabaishaji au tapeli…. Na ndio maana akaona hata hakuna sababu ya kwenda kumsumbua kuzungumza naye, au kumwomba aje kumtembelea, Bali aliona pindo la vazi lake, tu linatosha yeye kuwa mzima..

Na Yesu alipoiona Imani yake saa ile ile akamgeukia na kumwita “Binti yangu”.. Akampa nafasi ya kipekee sana Kama Mtoto wa kike aliyemzaa yeye mwenyewe, ambaye ana haki zote za kupokea mema yote ya Baba yake.

Tujiulize ni wanawake wangapi leo Bwana anaweza kuwaita binti zangu? Usidhani Kristo kukuita binti yake, kwasababu ya umri wako mdogo, au mrembo wako, au utanashati wako, hilo halipo, yeye hana jicho la mwilini, kama sisi tulilonalo, haangalii umri wala umbile.

Kama wewe ni mwanamke lakini unafika kwa Kristo ili kujaribu jaribu tu, uone kama Bwana atakujibu au la!,atakusaidia au la! unamlinganisha na wale waganga wa kienyeji uliowahi kuwatembelea huko nyuma.. uone kama atajibu au la!. Ujue kuwa wewe sio binti wa Yesu.

Mabinti wa Yesu, tangu walipokutana na Yesu utawakuta wametulia kwa Bwana hadi sasa, wanaouhakika na waliyemwendea, hawahitaji kusaidiwa na mtu, kuelewa kuwa Yesu ni muweza, wanafanya mambo yao wakiwa wame-relax, huwezi kuwakuta leo kanisani Kesho, disco,  leo wamevaa magauni, Kesho wanakatiza barabarani na visuruali na vikaptura, leo kwa nabii huyu Kesho kwa yule..huwezi kuwakuta wapo namna hiyo.

Hao ndio binti za Mungu. Na faida yao ni kuwa kwasababu wameshaitwa binti za Mungu, tayari wanaourithi kutoka mbinguni. Jambo ambalo wengi hawajui wakidhani kila mtu atakuwa mrithi wa kila baraka ya Mungu mbinguni.

Dada/mama/bibi tambua ni nini Kristo anatamani kuona kwako, acha kutangatanga na huu ulimwengu, Acha kujaribu jaribu, maanisha kumfuata Kristo.. Yeye mwenyewe anasema.

2Wakorintho 6:17 “Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.

18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu WANANGU WA KIUME NA WA KIKE”,

Kumbuka hizi ni siku za mwisho, Kristo anarudi siku yoyote. Bado tu hujatulia kwa Bwana? Injili tuliyobakiwa nayo sasa hivi sio ya kubembelezewa tena wokovu, ni wewe mwenyewe aumke usingizini, umtafute Mungu wako. Kwasababu muda umeshaisha.

Maran atha..

Usikose sehemu ya tatu na ya mwisho ya Makala hii, ambayo, tutaona pia ni kwanini Bwana Yesu aliwatambua wanawake wengine kama MAMA.

Bwana akubariki..

Maran atha

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post