Katika (Mathayo 25:8 na Marko 16:8) Wale wanawake walitangaza kufufuka kwa Bwana au walikaa kimya?

Katika (Mathayo 25:8 na Marko 16:8) Wale wanawake walitangaza kufufuka kwa Bwana au walikaa kimya?

Shalom tukisoma Mathayo 25:8 na Marko 16:8, tunaona habari mbili zinachanganya, kuhusu wale wanawake, sehemu moja inasema walikwenda kutangaza na sehemu nyingine inasema walikaa kimya hawakumwambia mtu, je ipi ni sahihi?


Jibu: Tusome.

Mathayo 25:5 “Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa.

6 Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa.

7 Nanyi nendeni upesi, mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu. Tazama, awatangulia kwenda Galilaya; ndiko mtakakomwona. Haya, nimekwisha waambia.

8 WAKAONDOKA UPESI KUTOKA KABURINI, KWA HOFU NA FURAHA NYINGI, WAKAENDA MBIO KUWAPASHA WANAFUNZI WAKE HABARI”.

Tusome tena habari hiyo hiyo katika Marko…

Marko 16:7 “Lakini enendeni zenu, mkawaambie wanafunzi wake, na Petro, ya kwamba awatangulia kwenda Galilaya; huko mtamwona, kama alivyowaambia.

8 Wakatoka nje, wakakimbia kutoka kaburini; KWA MAANA WAMEINGIA TETEMEKO NA USHANGAO; WALA HAWAKUMWAMBIA MTU NENO, MAANA WALIOGOPA”.

Hapo tunasona  habari mbili zinazoelezea tukio moja, lakini ni kama vile habari hizo zinajichanganya, kwamba iweje Mathayo aseme  ”wanawake walikwenda kuwapasha wanafunzi habari” na Marko aseme “hawakumwambia mtu neno”.. Swali ni je! Biblia inajichanganya?.

Jibu ni la! Biblia haijichanganyi hata sehemu moja, isipokuwa ni fahamu zetu ndizo zinazojichangaya…

Awali ya yote ikumbukwe kuwa kifo cha Bwana Yesu, kilihusisha Dini na vile vile kilihusisha Serikali. Kwa maana ya kuwa viongozi wa dini (yaani Makuhani na Waandishi) walimshitaki Bwana kwa Serikali(ambayo ilikuwa ni serikali ya kirumi), na Serikali hiyo ndiyo iliyomsulubisha Bwana Yesu.  Na baada ya Bwana Yesu kufa kaburi lake liliwekewa walinzi kulilinda!. Lengo ni ili wanafunzi wake wasije wakamwiba na kusingizia kafufuka.

Hivyo kulikuwa na hofu kubwa sana, kwa mtu yeyote ambaye angezusha kuwa Kristo kafufuka!.  Kwasababu Serikali ya kirumi ndio iliyokuwa inatawala, na ilikuwa ni serikali ya kikatili, endapo kingezushwa kitu chochote kilicho kinyume na itikadi zao au taratibu zao, sheria ilikuwa ni moja tu! Nayo ni Kifo.

Kwahiyo hata hawa wanawake ambao walitokewa na Malaika na kuwaambia kwamba Bwana kafufuka, wao waliamini, lakini haikuwa vyepesi kwenda kutangaza kwa watu wa nje!. Huko na huko kama Yule mwanamke Msamaria alivyofanya… Isipokuwa kwa watu wachache tu! Wenye imani moja na wao, ambao ndio wakina Petro na mitume wa Yesu.. Hao ndio wanawake waliwapelekea habari za kufufuka kwa Yesu, lakini watu wengine wa nje, kama Mafarisayo au masadukayo, maakida, au ndugu zao ambao hawakumwamini Bwana hawakuwapa taarifa zozote, zilibaki kuwa siri, ndio maana maandiko yanasema hapo hawakusema Neno kwa mtu yeyote.

Kwasababu hata katika hali ya kawaida, Mariamu Magdalena ataogopa vipi kumwambia Petro kwamba Bwana kafufuka?.. Kwani Petro angewafanya nini hao wanawake baada ya kupewa taarifa hizo?, angewapiga? Au angewashitaki kwa Herode?, bila shaka hilo ni jambo ambalo haliwezekani, kwasababu wote hao walikuwa upande mmoja, na tumaini lao ni moja..

Haiwezekani kuogopa kuambiana mambo yaliyojiri kumhusu Bwana wao… isipokuwa kwa watu wa nje, itabaki kuwa siri na fumbo.. ndio maana hata huyo Malaika hakuwaambia wakatangaze habari hizo kwa kila mtu tu!, bali kwa wanafunzi wa Yesu peke yao.

Hivyo hawa wanawake waliificha Siri kwa watu wa nje lakini waliiweka wazi kwa wanafunzi wa Yesu, kama maandiko yanavyosema hapo kwenye Mathayo.

Na hawakuwaambia watu wa nje kwasababu waliogopa!, aidha kuuawa, au kupitia dhiki fulani, kwasababu makuhani na maakida wangewasumbua kuwahoji ni wapi walipomficha..Ndio maana utaona sehemu zote baada ya kufufuka kwa Bwana, mitume pamoja na wanawake hawa, walikuwa wanajificha ndani na kujifungia kutokana na hofu ya kukamatwa, unaweza kuyathibitisha hayo katika mistari hii> Yohana 20:19,  Yohana 20:26 na Matendo 2:1

Ni lipi tunaloweza kujifunza?

Kama kufufuka kwake Bwana Yesu kulivyokuwa kwa siri, kiasi kwamba ni watu wachache sana ndio waliojua na kuthibitisha kwamba Bwana kafufuka, wengine wote hawakujua chochote, Herode na Pilato hawakutokewa na Bwana wala malaika, hivyo hawakujua chochote, vile vile na watu wengine hawakutokewa na Bwana wala Malaika wake kuwajuza kuwa kafufuka, maandiko yanasema watu 500 tu ndio waliotokewa na Bwana baada ya kufufuka kwake kati ya Mamilioni waliokuwa wanaishi duniani,siku hizo..

Ndivyo itakavyokuwa katika siku ya unyakuo.. Itakuwa ni tendo la ghafla na la siri!. Siku parapanda ya mwisho itakapolia, kundi la watu wachache sana duniani litaondoka na kwenda mbinguni, na  wengine wote hawatajua kitu…Hivyo hatuna budi kusimama imara katika Imani, ili siku hiyo ya unyakuo itakapofika tusiukose.

Marana atha

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:

MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.

KIKWAZO CHA EUODIA NA SINTIKE.

NAMNA YA KUMTAMBUA BIBI ARUSI WA KWELI WA KRISTO.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments