Ni kwa namna gani Bwana amekuja kuwafanya wanaoona wawe vipofu?

Ni kwa namna gani Bwana amekuja kuwafanya wanaoona wawe vipofu?

Yohana 9:39 “Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu”

Jibu: Ukisoma habari za Bwana Yesu utaona kuwa alikubaliwa na watu wanyonge na wenye dhambi lakini alikataliwa na watu wa Imani na wa dini (yaani Makuhani, waandishi, mafarisayo pamoja na masadukayo)..ambao wao walikuwa wanajiona wenye haki..

Sasa ili tuelewe vizuri hebu tujifunze katika mfano wa kawaida wa maisha.

Mtu anayetembea gizani na tochi yake mkononi, ule mwanga wa tochi akiutumia kumulika mbele yake katika njia anayoiendea utamfanya aone gizani, lakini akiigeuza ile tochi na kuyamulika macho yake, ule mwanga utamuathiri, utamfanya asione..

Ndivyo Mafarisayo na Masadukayo kilichowapata, walikuwa wanaenda kinyume na Nuru na maandiko yanasema Yesu ndiye Nuru ya ulimwengu (Yohana 8:12).Hivyo ile nuru ikawapofusha macho.

 Laiti mafarisayo na Masadukayo wangeitumia nuru hiyo kumulika njia zao,wasingekuwa vipofu lakini kwasababu walikuwa wanaenda kinyume na ile Nuru, ikawapofusha macho kama ilivyompofusha Sauli alipokuwa anakwenda Dameski kuwaua watakatifu. (Soma Matendo 9:1-19).

Hiyo inatufundisha kuwa wanyenyekevu na kulitii Neno la Mungu..Tukijiona kuwa tunajua kila kitu au tunajua zaidi ya wengine wote, kama Mafarisayo na Makuhani na wala hatuhitaji kujua zaidi, wala kujifunza zaidi basi tujue tunakwenda kinyume na ile Nuru,Basi tufahamu kuwa Neno la Mungu litatupofusha macho, kama lilivyowapofusha mafarisayo, makuhani na Masadukayo.

1 Wakorintho 8:2 “Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua”

Roho Mtakatifu atusaidie na kutubariki.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu?

Maherodi walikuwa ni akina nani, Na kazi yao ilikuwa ni ipi?

NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.

NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.

Hanithi ni nini katika biblia? (kumbukumbu 23:17)

Hanithi ni nini katika biblia? (kumbukumbu 23:17)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments