Title April 2019

NJONI, NUNUENI MLE NA MNYWE.

Isaya 55:1-2 “ Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila thamani.

2 Kwani kutoa fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.”

Jina kuu la mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, Nakukaribisha katika kuyachunguze maandiko nilipokuwa ninautafakari huu mstari, picha iliyojitengeneza moja kwa moja katika kichwani kwangu ni sawa mtu mwenye Hoteli maarufu ya 5 STAR Dubai, ambayo kifungua kinywa chake tu asubuhi gharama zake ni sh laki 3, mbali na gharama za chakula cha mchana na jioni, na zile za kulala..halafu leo hii unamwona anajitokeza hadharani anawakaribisha watu wote waje kula na kunywa katika hoteli ile bure, pasipo gharama yoyote…

Na cha kushangaza zaidi anatoa kauli hii “njoo UNUNUE bure”, hakwambii njoo nikupe bure, hapana bali anasema njoo “UNUNUE” bure, hii ikiwa na maana,utakapofika pale utaandikiwa risiti ya ununuzi kama tu vile mtu aliyelipia gharama zote, na hiyo inakupa uhalali wa kuhudumiwa kwa viwango vile vile bila upendeleo sawa tu na mtu Yule ambaye ametoa pesa yote mfukoni.

Lakini utashangaa sana siku ile usipoona watu wengi katika hoteli hiyo maarufu, maswali mengi yanaweza yakaja kichwani mwako sindio?, pengine utasema hawa wameona kama wamedharauliwa au?, au wameshushwa hadhi?, au wanaogopa kwenda kutokana na hadhi ya hoteli ile au? Au wameona kama wanaingizwa mjini au ni nini?..Ni wazi kabisa utajiuliza kwa offer kubwa kama hiyo ni kwanini pakose watu?.

Isaya 55:1-2 “ Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila thamani.

Ndugu ndivyo Mungu anavyotufanyia sisi wanadamu, anatuita tuje tule, tunywe tujishibishe nafsi zetu kwa vinono kwake, bila gharama yoyote, lakini sisi tunapoona tunapewa vyote hivi kwa bei ya bure, tunaona kama havina thamani kubwa kwetu, na hiyo inatupelekea kuudharau wokovu na kwenda kutafuta vitu ambavyo vitatugharimu maisha yetu na mwisho wa siku visituletee faida yoyote katika roho zetu.

Nataka nikuambie, siku zote kitu kikiwa na thamani kubwa sana isiyoweza kufikiwa na wengi mara nyingi huwa kinageuka na kuwa bure, hiyo ni fact kwasababu kitakosa mnunuzi, hivyo thamani yake inarudi tena katika sifuri, na ndio maana ukitazama hata taifa linalodaiwa matrilioni ya pesa na mataifa tajiri, utaona mfano likishindwa kulipa, wale watu wanaandikiwa msamaha, sio kana kwamba hawaithamini au hawaihitaji ile pesa hapana, bali, wanaona huyu mtu hata atoe vitu vyake vyote hawezi kulipa deni hili hivyo ya nini kumdai!..Ni sawa na kupoteza muda tu! Lakini angalia wale wa madeni ya kati na madogo madogo, hao ndio wanaokuwa wa kwanza kusumbua, na usipowalipa kwa wakati watakupeleka mpaka kwenye mahakama za kimataifa, na utapigwa faini juu.

Na ndivyo ilivyo kwa Mungu wetu, siku zote vitu vyake vyote anavitoa bure kwasababu vina thamani kubwa sana, pumzi unayoivuta ingekuwa tunalipia tu hata kwa senti moja kila dakika ungekuwa unadaiwa sh. Ngapi mpaka sasa?,..babu wa babu yako angekurithisha madeni yake, maji ya mvua yanayolinyesha shamba lako pamoja na kuijaza na mito yote ya maji na chemchemi ungekuwa unalipia leo hii ungeotoa sh. Ngapi?,

Nishati inayotoka kwenye jua, ambayo kwa dakika 1 inayo uwezo wa kulihudumia taifa la Marekani tu kwa miaka milioni moja,uchunguzi unasema hivyo,sasa mfano tungekuwa tunapewa kwa gharama kama vile tunalipia luku tungelipa sh.ngapi?

Lakini hayo yote bado si kitu zaidi ya WOKOVU, ambao huo kama tukisema ni kuulipia basi tujue pesa zake ni sawa na hakuna mwisho…Mungu alimtuma mwanawe wa pekee ili kuuandaa wokovu huu na kuunda kwa muda wa miaka 33 na nusu, kila siku usiku na mchana alikuwa anauunda, katika vipindi vigumu na vya majaribu mazito tangu siku ya kwanza, alikuwa anatutengeneza sisi chakula hichi kizuri cha roho kwa kupitia mwanawe mpendwa YESU KRISTO, mpaka alipofikia karibu na kumaliza shughuli hii, Mungu mwenyewe akaingia gharama ya kumngongelea “hati ya dhambi zetu, pale msalabani”. Ili DENI lile kubwa sana lifutwe..ilichukua maisha ya mtu mtakatifu sana asiyetenda dhambi kulifuta Deni hili. Ili tu sasa kila mmoja awe na uwezo wa kuununua wokovu huo kwa bei ya bure.

Na ndio maana Bwana Yesu pale msalabani alimalizia na kauli hii..

IMEKWISHA!!.

Ile hati ya deni la dhambi imekwisha. Na leo anasema tena Haya,

“kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila thamani.

2 Kwani kutoa fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii, MLE KILICHO CHEMA, NA KUJIFURAHISHA NAFSI ZENU KWA UNONO.”

Ununue wokovu huu kwa bei ya bure ndugu, wakati ndio huu, sauti inayokulilia kila siku utubu, haitadumu milele hiyo, mzigo wa dhambi ulionao, siku ile hutaweza kuulipia, unajua kabisa ukifa leo ni moja kwa moja jehanum kwa dhambi zako, siku hiyo utaulizwa kule ni nini shida? Hutakuwa na cha kujitetea, wote watakushangaa wokovu ulipatikana kwa bei ya bure, imekuwaje wewe haukuwa nao??. Isitoshe hizi ni siku za mwisho dalili zote zinaonyesha hatujui kama tunaweza kuwa na vizazi vingine mbele yetu,..Huu ni wakati wa kutafuta mambo ya wokovu wa roho yako sana kuliko mambo mengine yasiyotuahidia uzima wa milele.. Weka Msalaba mbele, dunia nyuma. Imani mbele mali nyuma, Itakufaidia nini upate fedha zote na nafsi yako iangamie?.

Ufunuo 22:17 “Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”.

Tafadhali “Share” Ujumbe huu kwa wengine. Na Bwana atakubariki.

Ikiwa utapenda kumpa Yesu Maisha yako, au kupata ubatizo sahihi, basi tupigie kwa namba zetu hizi +255789001312/ +255693036618. Na pia kama utapenda masomo haya yawe yanakufikia kila siku kwa njia ya Whatsapp. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

NAYE ALIKUWA HANA BUDI KUPITA KATIKATI YA SAMARIA.

LAKINI SISI HATUKUIPOKEA ROHO YA DUNIA.

NI KWASABABU YA YESU KRISTO.

MAJI YA UZIMA.

“WOKOVU WETU U KARIBU NASI KULIKO TULIPOANZA KUAMINI”

TUSIPOUTHAMINI WOKOVU TUTAPATAJE KUPONA?


Rudi Nyumbani

Print this post

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1

Shalom!..Karibu tujifunze Maneno ya Mungu ya uzima, leo tunajifunza kwa uchache juu ya vitabu vya Biblia, jinsi vilivyoandikwa na maudhui yake, kwa neema za Mungu.

Zamani mwanzoni wakati nampa Bwana maisha yangu, nilikuwa siielewi biblia vizuri, vitabu nilivyokuwa navielewa vilikuwa ni vile vya injili tu! Yaani Mathayo,Marko, Luka na Yohana…na katika agano la kale kitabu cha Mwanzo kidogo na Kutoka ndio nilikuwa nikivisoma navielewa, na cha Esta pamoja na Ruthu…kwasababu mtiririko wa hadithi zake umejipangilia vizuri… Lakini vitabu vingine kama Zaburi, Mithali,Ezekieli, Yeremia, Isaya, Danieli, Habakuki, Malaki n.k nilikuwa sivielewi kabisa.. Kwasababu nilikuwa sijui viliandikwa kwa sababu gani..Na mwandishi alikuwa anaviandika katika mazingira gani na kwa malengo gani…kwaufupi vilikuwa vinanichanganya sana.

Kwahiyo niliishia kuhisi tu kuwa kitabu kama cha Isaya, kiliandikwa na Nabii Isaya pengine ndani ya siku moja au mbili, au ndani ya wiki moja, nilikuwa nadhani alikuwa anajifungia ndani na kisha maneno ya Mungu yanamshukia na anayaandika kwenye kitabu aya baada ya aya, hivyo pengine ilimchukua muda kama wa wiki moja hivi kumaliza kuandika sura zote 66…Na vitabu vingine nilijua ndio hivyo hivyo. Lakini kumbe ulikuwa ni uchanga tu wa kiroho.

Hakuna kitabu kizuri na kilichopangiliwa vizuri kama BibliaTakatifu, ni kitabu pekee kilichoandikwa kwa utaratibu mzuri na mpangilio endapo ukikielewa. Leo kwa ufupi tutaanza kujifunza mpangilio huu jinsi ulivyokaa na tutaanza na vitabu vichache..

1) Kitabu cha MWANZO:

Kitabu cha Mwanzo kiliandikwa na Nabii Musa, wakati akiwa jangwani baada ya kuwatoa tu wana wa Israeli Misri, Bwana alimpa ufunuo wa kilichotokea Edeni na hata kabla ya Edeni.

Alimpa ufunuo pia wa jinsi dunia ilivyoumbwa katika siku zile 6, na akaambiwa aandike vile ilivyoandikwa, kumbuka Musa ndiye Nabii pekee aliyekuwa anazungumza na Mungu uso kwa uso.

Lakini pia kitabu cha Mwanzo hakijabeba tu historia ya Adamu na Hawa, Bali pia kimebeba historia ya dunia kuangamizwa kwa gharika, habari za Nuhu na safina, habari hizo pia ziliandikwa na Nabii Musa, ingawa kabla ya Musa pia habari hizo zilikuwa zinafahamika na baadhi ya watu, pia historia ya Wana wa Israeli, kuanzia Ibrahimu mpaka Yusufu na mpaka walipoingia Misri wapo watu wachache walikuwa na rekodi ya chimbuko lako. Kwahiyo Musa wakati yupo jangwani na wana wa Israeli aliagizwa na Mungu aandike mambo hayo, na akayaandika kwenye kitabu na hicho kitabu ndio kinaitwa mwanzo.

 

2) Kitabu kinachofuata ni kitabu cha KUTOKA

Nacho kiliandikwa na huyo huyo Musa, akiwa jangwani pamoja na wana wa Israeli…Kilikuwa ni kitabu kirahisi kwasababu hakikuhitaji ufunuo wowote wa Roho kukiandika, ilikuwa ni kuandika tu mambo waliyokuwa wanayapitia siku baada ya siku,na waliyokuwa wanayaona..tangu Musa alipotumwa na Mungu kwenda kwa Farao, mpaka mapigo Farao aliyopigwa, mpaka kuvushwa bahari ya Shamu, mpaka walivyolishwa mana jangwani, mpaka wakati wa kukabidhiwa amri kumi na kupewa maagizo ya kutengeneza Maskani ya Bwana,…Kwahiyo hakikuwa kitabu kigumu kuandika kwasababu ni maisha waliyokuwa wanayaishi, na mambo waliyokuwa wanayaona..kulikuwa hakuna haja ya mtu kuwaadithia au kungojea ufunuo kutoka kwa Mungu ya jinsi ya maneno ya kuandika kama ilivyo kwenye kitabu cha UFUNUO.

3) Kitabu kinachofuata ni MAMBO YA WALAWI.

 Kitabu hichi kiliandikwa na huyo huyo Musa wakati wana wa Israeli bado wapo jangwani katika safari yao ya kuelekea Kaanani. Baada ya Mungu kuwapa sheria alimwagiza Musa awatenge wana wote wa Lawi, ambalo ndio kabila lake Musa, alifanye kuwa kabila la kikuhani..Na hivyo kama limeteuliwa kuwa kabila la ukuhani, hivyo ni lazima kutakuwepo na majukumu machache machache yanayowahusu hao makuhani walawi (yaani Kabila la Musa).

Kwahiyo Mungu akamwagiza Musa aandike kitabu kitakachowahusu hao walawi na majukumu yao katika utumishi wa kikuhani. Kama ukisoma kitabu cha mambo ya walawi utaona kulikuwa na majukumu mengi sana, ambayo yaliwahusu maana hao ndio waliochaguliwa na Mungu kuwa kama wawakilishi wake duniani, wajukumu yote ya namna ya kuwahudumia wana wa Israeli kuhusu masuala ya kiibada waliyabeba wao,

Kwahiyo ilipasa kiwepo kitabu pekee cha namna ya kuendesha ibada ndani ya hema ya kukutania, ndio maana utaona ndani ya kitabu hicho kimejaa maagizo kwa wana wa Lawi ya namna ya kumtolea Mungu sadaka, utaona wana wa HARUNI (Ambao ndio wana wa Lawi) wanaagizwa nini cha kuvaa wakati wakitumika kwenye hema, namna ya kuiandaa sadaka pindi inapoletwa na wahusika namna ya kuikata kata na kuiweka juu ya madhabahu, na wanafundishwa pia jinsi ya kutumika madhabahuni utaratibu na zamu,wanafundishwa namna ya kuvukiza uvumba, wanafundishwa jinsi ya kufanya upatanisho kwa dhambi za wana wa Israeli, wanafundishwa pia namna ya kumfanyia mtu utakaso pindi anapokuwa najisi, au anapotenda dhambi, wanafundishwa pia sheria za kuwafundisha watu na hukumu zake, ikiwa imetokea mtu amefanya kosa atendewe nini n.k

Kwahiyo kwa ufupi ni kitabu kinachohusu MAJUKUMU YA WANA WA LAWI ndio maana kinaitwa MAMBO YA WALAWI..Musa pamoja na Haruni ndugu yake walikuwa WALAWI. Kwahiyo kabila lao liliteuliwa na Mungu kuwa Kabila la KIKUHANI. Walikuwa hawana jukumu linguine zaidi ya hilo. Kitabu hichi pia kimeelezea maagizo na aina za sadaka wana wa Israeli wanazopaswa kumtolea Mungu..Na jinsi wanavyopaswa wazipeleke kwa makuhani WALAWI.

4) Kitabu  cha Nne ni kitabu cha HESABU:

Kitabu cha Hesabu kiliandikwa na Nabii Musa huyo huyo, wakati bado wakiwa katika safari yao jangwani. Kipindi wana wa Israeli wanatoka Misri walitoka kama jeshi la mtu mmoja..walikuwa ni wadhaifu kwa hiyo Mungu aliwapigania dhidi ya maadui zao kwa asilimia zote, hawakutumia hata upanga wao au visu vyao kushindania wokovu wao…

Ulikuwa ni mkono wa Mungu mwanzo mwisho, hawakunyanyua hata kisu kushindana na maadui zao, utaona Farao adhabu alizokuwa anapata ni Mungu mwenyewe ndio aliyekuwa anahusika mwanzo mwisho, hakuna hata jiwe la mwisraeli mmoja lililohusika, mpaka wanatoka Misri ndio ilikuwa hivyo..Lakini mbeleni utakuja kuona wana wa Israeli wanabadilika tabia, wanaanza kuukataa uongozi wa Mungu na kutaka kujiongoza wenyewe…Na ni kawaida Mungu anapowaonya watu na wanapokataa maonyo huwa anawaacha na kuwapa haja ya mioyo yao kama wanavyotaka..

Utaona walitaka kula nyama, wakati ambao haukuwa wakati wa kula nyama, lakini kwasababu walililia Mungu aliwapa nyama kama wanavyotaka, kadhalika utaona hata walipoingia nchi ya ahadi walijitakia Mfalme, jambo ambalo halikuwa mapenzi ya Mungu wao wawe na mfalme wa kibinadamu, lakini utaona Mungu aliwapa Mfalme kama walivyotaka.

Na kadhalika wakati wakiwa jangwani, baada ya kupewa zile amri 10 na Mungu..mioyoni mwao walikuwa tayari wameshaanza kuukataa uongozi na wokovu wa Mungu, wakaanza kutamani kupambana wao na maadui zao, jambo ambalo halikuwa ni mapenzi ya Mungu wana wa Israeli washike upanga kuuwa maadui zao, lakini kwasababu tayari mioyo yao ilishakuwa migumu, Bwana akawaacha watumie silaha zao kwa wokovu wao…

Lakini hakuwaacha kabisa, akaendelea kuwa nao hata kwa njia hiyo..lakini haikuwa mpango kamili wa Mungu, wokovu upatikane kwa njia ya upanga…Kusudi la Mungu ilikuwa ni kuwapa hiyo nchi ya Ahadi kwa mkono wake mkuu na matendo yake makuu kama alivyofanya kwa wa Misri, kusudi lake lilikuwa ni kuwatoa wakaanani kwa matendo ya kimiujiza pengine kama kwa mapigo yale ya Misri, pasipo hata wana wa Israeli kutumia upanga, Lakini wana wa Israeli waliuharibu mpango kutaka kujipigania..

Kwasababu hiyo basi, Mungu aliruhusu wana wa Israeli, wapange majeshi… WAHESABIWA KULINGANA NA IDADI YAO, wahesabiwe wanaume tu walio na miaka 20 na zaidi, WALIO NA UWEZO WA KWENDA VITANI, waandikwe majina yao na makabila yao, kwasababu ya vita wanavyokwenda kukutana navyo mbeleni. Ndio maana ukisoma pale mwanzo wa kitabu cha HESABU utaona:

Hesabu 1: 1 “Bwana akanena na Musa katika bara ya Sinai, hemani mwa kukutania, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya kutoka kwao nchi ya Misri, akamwambia,

2 Fanyeni HESABU ya mkutano wote wa wana wa Israeli, kwa kuandama jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina ilivyo, kila mtu mume kichwa kwa kichwa;

3 tangu mwenye miaka ishirini umri wake, na zaidi, WOTE WAWEZAO KUTOKA KWENENDA VITANI KATIKA ISRAELI; wewe na Haruni mtawahesabu kwa kuandama majeshi yao”.

Kwahiyo hiyo ndio sababu ya kuandikwa kitabu cha HESABU, Ni Kitabu cha orodha ya mashujaa watakaosimama vitani kulipigania Taifa la Israeli, na kuliingiza katika nchi ya Ahadi, kuanzia huo wakati Mungu akaanza kuwaokoa na kuwapigania wana wa Israeli kwa kutumia majeshi yao wenyewe, huo ndio ulikuwa mwanzo wa wana wa Israeli kupigana vita…wokovu ukawa unapatikana kwa upanga!..Ndio mashujaa kama wakina Yoshua wakatokea huko, kwa kutiwa nguvu za kiMungu ndani yao kama simba, waliyaangusha mataifa saba makubwa ya Kaanani kwa Upanga…

Kwahiyo kama ukikisoma kitabu hichi vizuri utaona mwanzo wa majeshi ya Israeli kwa Idadi yao na makabila yao, utaona jinsi yalivyojipanga kuizunguka hema, wakati wametulia na wakati wanasafiri..Na pamoja na hayo kitabu hichi pia ni ufupisho wa hatua moja moja waliyopitia wana wa Israeli tangu walipotoka Misri mpaka walipoikaribia Kaanani. Na pia Hesabu hiyo hiyo ya majeshi ya Israeli ndio iliyokuja kutumika katika kuigawa hiyo nchi ya Kaanani waliyokuwa wanaiendea, kwamba Kabila lenye watu wengi ndio waliopewa urithi mkubwa zaidi ya kabila lenye watu wachache.

Bwana akubariki sana…

Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312

Kwa mwendelezo >>> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 2

Na pia kama utapenda masomo haya yawe yanakufikia kila siku kwa njia ya Whatsapp basi bofya  link hii kujiunga moja kwa moja >>> JIUNGE- WHATSAPP Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.

SANDUKU LA AGANO LILIKUWA LINAWAKILISHA NINI KATIKA AGANO JIPYA?

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

NUHU WA SASA.

MNARA WA BABELI

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “HERI WALIOTASA, NA MATUMBO YASIYOZAA, NA MAZIWA YASIYONYONYESHA”?


Rudi Nyumbani:

Print this post

NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?

Kama umechunguza utagundua kuwa Wanajeshi vitani sikuzote huwa hawakimbii tu ovyo ovyo kila mahali na kuanza kurusha mabomu na silaha kwa maadui zao kama wanavyojisikia tu hapana, mambo hayawi hivyo vinginevyo wanaweza wakajikuta wao ndio wanakuwa shabaha ya maadui zao, bali huwa wanatulia kwanza na kutafuta mahali pazuri ambapo maadui zao hawatawaona na pia mahali ambapo patakuwa ni rahisi kwao, hapo watapiga maadui zao vizuri na kwa upesi, hata simba porini huwa halikimbilii tu bila malengo kundi la nyumbu analoliona mbele yake na kwenda kumrukia yoyote tu ampendaye hapana, vinginevyo hataambulia chochote lakini kinyume chake utamwona anatulia katika eneo zuri la utulivu na la maficho ambalo litamsaidia kuchora mpango wake kichwani na pia litakalompa wigo wa kuchomoka kwa kasi na haraka kumrukia mnyama kabla hata hajaanza kuongeza kasi ya kukimbia..

Na ndivyo ilivyo hata kwa shetani, si kila eneo atakujaribu tu mwaminio, Mtume Paulo aliwaandikia wakorintho maneno haya 2Wakorintho 2:11 ‘Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake…’

Hii ikiwa na maana kuwa kama tukikosa kuzifahamu fikira zake, basi itakuwa ni ngumu sana sisi kumshinda yeye. Hivyo leo tutazama baadhi ya vipengele vikuu muhimu ambavyo shetani anapenda sana kuvitumia kumshambulia mkristo. Kwa kuyatazama maisha ya Bwana wetu Yesu Kristo tunaweza kuvibainisha vipengele hivyo vikuu.

NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?

1) Wakati unaingia katika maisha mapya ya rohoni:

Hii ipo wazi kabisa wakati tu Bwana Yesu anakuja duniani pale pale shetani alinyanyua vita vikubwa kutaka kumwangamiza mtoto Yesu kwasababu alijua akimwacha baadaye atakuja kuleta madhara makubwa sana katika ufalme wake, kwasababu aliiona nyota yake, na aliufahamu unabii wa kuja kwake, hivyo jambo analohakikisha ni kumwondoa Yule mtu tangu akiwa mchanga..Na mambo kama hayo hayo yatajirudia kwa mtu yeyote atayeingia katika wokovu leo. Hivyo usishtuke kuona mambo yanakubalikia, usishtuke kuona ndugu wanakugeuka au kukuchukia wakati mwingine, usishtuke kupitia majanga kwasababu ya imani yako.. hilo lisikusababishe kuwachukia ndugu zako au jamii, wala kuwalaani fahamu kuwa ni shetani ndiye anayeyasababisha hayo yote kutaka kukuzuia usiupende wokovu. Unachopaswa tu kufanya ni kudumu katika imani kwasababu Bwana atakuwa pamoja na wewe kukulinda na kila aina na madhara atakayojaribu kukuleta kama alivyomlinda mtoto YESU kipindi kile anazaliwa. Kadhalika pia tunaweza kujifunza katika Wanyama wawindao, Watoto wadogo wa Wanyama ndio wanaowindwa sana kuliko Wanyama waliokomaa…utaona mtoto wa tembo au mtoto wa twiga ni rahisi kuwa chaguo la Wanyama kama fisi au chui kuliko twiga mzima au tembo mzima…

2) Wakati ukiwa peke yako:

Sehemu nyingine unayopaswa uwe makini nayo sana ni pale unapokuwa peke yako. Mtu aliye peke yake siku zote nguvu yake inakuwa ni ndogo kuliko anapokuwa na wenzake, hiyo ipo wazi.Hivyo shetani akishagundua kuwa kuna wakati upo peke yako, hapo ndipo anaanza tena kuamsha majaribu yake. Bwana Yesu alipojitenga peka yake kule jangwani siku 40, tunaona shetani ndipo alipomtokea na kumjaribu. Tunaweza kumwona tena Daudi alipokuwa peke yake nyumbani ndipo shetani alipomjaribu na kufanikiwa kumdondosha katika dhambi ya uzinzi. Hivyo chukua tahadhari mara mbili, na ndio maana biblia inatuonya na kutushauri kila wakati katika Muhubiri..

Mhubiri 4: 9 ‘‘Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.

10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!

11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?

12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi

Hata Wanyama wanaowinda kama chui au fisi au simba, huwa wanapenda kumvizia yule mnyama aliye peke yake Zaidi ya kulivamia kundi zima…Na shetani naye ndio yupo hivyo hivyo.

3) Wakati upo katika hali ya udhaifu:

Fursa nyingine shetani anayopenda kuitumia ni pale mkristo anapokuwa katika hali ya udhaifu, shetani anapapenda sana hapo. Wakati Bwana alipofunga siku zile 40 hakumwona adui lakini alipoona tu njaa, ndipo hapo hapo adui akatokea na kuanza kumjaribu, shetani anapenda kutumia madhaifu, njaa, magonjwa, shida, tabu ili kukunaswa kwenye mitego yake.. Ayubu wakati wote hakuwahi kukutana na shetani akizunguza naye kumlaumu kuwa yeye kamkosea Mungu, siku zote hizo hakumwona shetani lakini alipoanza kupitia majanga yale ndipo shetani akamjia kwa vinywa vya wale marafiki zake watatu kumvunja moyo, na kumtaabisha wakimwambia kuwa yeye amemkufuru Mungu ndio maana yamemkuta yale yote..

Vivyo hivyo na wewe unayejijua ni mkristo, kumbuka shetani atakusubiria katika engo hiyo pia, wakati unapitia mazingira magumu, hatakuja wakati upo kwenye raha, au mafanikio, atakutafuta kwenye shida, na misiba, huko ndipo atakapokuletea hata vipengele vya maandiko kichwani mwako, ili tu kukutoa katika mstari wa imani, atakuleta vishawishi vingi, wa watu wengi wa ajabu, atakupa mpaka njia mbadala ya kufanya kama vile alivyomshauri Bwana Yesu ageuze jiwe liwe mkate.

Lakini nataka nikuambie kupitia shida, au udhaifu au taabu ya kitambo fahamu kuwa sio uthibitisho kuwa Mungu amekuacha maadamu unafahamu kuwa uhusiano wako na Mungu bado upo, usiikate imani ndugu..kuwa kama Daudi aliposema Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu nijapopita katika bonde la uvuli wa Mauti, sitaogopa kwa maana wewe upo pamoja nami, gongo lako na fimbo yako vyanifariji.(Zaburi 23).

Tukirudi pia katika mifano ile ile ya Wanyama wawindao kama simba au chui huwa wanapenda kumvamia yule aliye dhaifu, wakishakosa aliye peke yake katika kundi, au aliye mtoto katika kundi, huwa wanatafuta aliyedhaifu, au mgonjwa, kwasababu hawatasumbuka sana katika kumkamata..shetani naye ni kama simba angurumaye akitafuta mtu ammeze..maandiko yanasema hivyo… 1 Petro 5:8

4) Eneo lingine analolipenda kulitumia ni wakati unahama kutoka kiwango kimoja cha utukufu hadi kingine:

Kuna wakati Mungu atayaongeza mafuta yake kwako, kwa ajili ya utumishi wake, hapo napo shetani hatataka atulie kukuangalia tu unakwenda kufanikiwa kuutangaza ufalme wa Mungu, ni lazima alete mawimbi yake. Tunaona Bwana siku ile tu alipokwenda kubatizwa kule Yordani na Roho wa Mungu kushuka juu yake na kumtia mafuta yale ya utumishi mkuu kama ule, tunaona shetani akajidhihirisha kwake alipokwenda kule jangwani..Hii ni kawaida, kwa watumishi wa Mungu kukumbana na mkono wa shetani uso kwa uso safarini katika kuineza kazi ya Mungu. Lakini mwisho wa siku ataishia kushindwa tu, kwasababu vita ni vya Bwana.

Hivyo pia katika eneo hilo zingatia sana, tarajia kukutana naye na hakikisha umwachi atoke salama.

5) Eneo lingine ni Wakati upo katikati ya watu ambao unadhani wanaweza kuwa faraja au msaada mkubwa sana kwako katika imani:

Hii inatokea hususani kwa watu wa imani moja na wewe…Hichi ni chanzo ambacho Mtu hawezi kukitazamia kama shetani anaweza kupitia kukujaribu lakini biblia imekithibitisha chanzo hichi, na kinakuwa na matokeo makubwa sana kwa mtu kama asipokuwa makini. na hivyo tunapaswa tuwe makini katika eneo hilo pia. Hilo tunalithibitisha kwa Bwana wetu Yesu yeye ndiye aliyewachagua mitume wake 12, na yeye ndiye aliyewatenga kwenda kufanya kazi ya kutangaza ufalme wa mbinguni pamoja naye,.na wakati mwingine aliwasifia kwa utumishi wao kwa mfano Petro alipopokea ufunuo wa kuwa yeye ni nani (Mathayo 16) alimsifia lakini mbele kidogo shetani alimtumia kupitisha hila zake..Lakini Bwana alilitambua hilo haraka kwa mafuta yaliyopo ndani yake na kumwambia Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.(Marko 8:33).

Hali kadhalika tunaona baadaye kwa mwingine aliyeitwa Yuda,alikuja kumsaliti, yeye ndio aliyeifanikisha kazi ya shetani kwa ufasaha zaidi mambo ambayo mafarisayo pamoja na wingi wao na utajiri wao walishindwa kumwangamiza Yesu lakini Yuda mmoja tu alifanikiwa kumweka Bwana mikononi mwa maadui zake.

Hivyo ukiwa katika ukristo au katika utumishi hilo usilisahau akilini mwako, usiweke asilimia zako zote kwa mwanadamu mwenzako, kwasababu siku akikusaliti unaweza ukavunjika moyo kiasi cha kufa, jambo hilo lilishawahi kunikuta pia mimi, sipendi likukute na wewe, wewe kaa nao karibu, ombeaneni, pia aminianeni lakini usilitoe hili akilini kuwa inaweza kutokea nafasi shetani kumtumia kukushambulia wewe, Lakini kama ukiwa umelijua hilo mapema halitakusumbua na hivyo mishale hiyo ya shetani kwako ikija itakuwa si kitu. Bwana atakuwa upande wako.

Jambo la mwisho la kufahamu ni kuwa shetani akishaona umezijua njama zake hizi zote, na amezilita kwako na umezishinda, hatakuacha moja kwa moja, fahamu kuwa atatulia tu kwa muda fulani, halafu atarudi tena, Kama tunavyoona kwa Bwana wetu Yesu Kristo tukisoma katika

Luka 4.13 ‘Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda zake kwa muda’’.

Hivyo biblia inatuambia mambo hayo yaliandikwa ili kutuonya sisi…Na sehemu nyingine Bwana anasema “Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele”. (Mathayo 24.25).

Kwahiyo hatupaswi kulala, wala kusinzia, kwasababu adui yetu yeye hakati tamaa, na hiyo inatufundisha tuwe watu wa kukuesha katika roho kila wakati. Kumbuka shetani hawezi kutushinda, pindi tu tunapotaka kutulia katika Neno la Mungu, Hivyo usiogope ikiwa umeyakabidhi maisha yako kwa Bwana kweli kweli na umesimama basi fahamu USHINDI NI LAZIMA.

Bwana akubariki.

Tafadhali “share” ujumbe huu na wengine.

Na pia kama utapenda masomo haya yawe yanakufikia kila siku kwa njia ya Whatsapp  Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Print this post

JIWE LA KUKWAZA

Marko 6:1 ‘Akatoka huko, akafika mpaka nchi ya kwao; wanafunzi wake wakamfuata.

2 Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?

3 Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? WAKAJIKWAA KWAKE’’. 

Tunasoma pia…

1 Petro 2:6 ‘Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.

7 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.

8 Tena, JIWE LA KUJIKWAZA MGUU, na mwamba wa kuangusha, Kwa maana hujikwaza kwa neno lile,wasiliamini,nao waliwekwa kusudi wapate hayo’’.

Shalom! Mtu wa Mungu, karibu tujifunze Neno la Mungu…ambapo leo kwa neema zake tutajifunza juu ya jiwe la kukwaza..

Ulishawahi kutembea barabarani ghafla ukajikwaa, na ulipotazama chini ukagundua ni kipande kidogo cha jiwe ndicho kilichokukwamisha, ambacho hukutarajia kama kikengeweza kukuweka chini, na wakati mwingine unajikuta umepata jeraha Fulani, au kiatu chako kumeharibika, au kama ulikuwa umevaa sandals unakuta imekatika??..Basi kama tukio kama hilo lilishakutokea basi hiyo ni ajali inayoitwa KUJIKWAA.

8 Tena, JIWE LA KUJIKWAZA MGUU, na mwamba wa kuangusha, Kwa maana hujikwaza kwa neno lile,wasiliamini,nao waliwekwa kusudi wapate hayo

 Lakini pia kupo kujikwaa kwingine katika roho, ambapo na kwenyewe kuna hasara zake. Kama tunavyojua hakuna mtu yoyote anajikwaa akiwa amesimama, ni sharti awe katika mwendo Fulani…Na sisi wanadamu wote tupo katika mwendo, tupo safarini ndio maana tuna vipindi vya kuzaliwa, na vya kufa..hiyo ni kuonyesha kuwa duniani tunapita tu!.

Lakini Mungu amesema katika Neno lake, kuwa ameweka JIWE katika njia ya safari yetu. Ikiwa na maana kuwa tunaposafiri ni kama tunavyotembea tunapaswa tuwe makini sio tu kuangalia mbele bali pia kuangalia hatua zetu tunazozipiga, na kuangalia njia tunazozipita…Kwasababu wakati tunapita katika haya Maisha kila mtu lazima akutane na hilo JIWE, na sio kubwa kwa macho, linaonekana dogo na lakudharaulika lakini, linaweza kumweka mtu chini, Mtu akilipita pasipo kuliona atajikwaa na kuanguka, na kuumia lakini aliye makini ambaye anapita huku akitazama mbele na chini, atapunguza mwendo.. Maandiko yanasema..

‘Tazama, naweka katika Sayuni JIWE KUU LA PEMBENI, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika….. Tena, JIWE LA KUJIKWAZA MGUU, na mwamba wa kuangusha’’

Ukisoma maandiko utajua kuwa hilo jiwe si linguine Zaidi ya YESU KRISTO.

Yeye ndio JIWE kuu na Teule..Tunasoma katika maandiko…wakati akiwa hapa duniani, watu hawakumjua kama ndiye Masihi aliyetabiriwa…hawakujua kuwe yeye ni chapa ya nafsi ya Mungu, waliona ni mtu wa kawaida tu! Kwasababu walikuwa wanamjua baba yake, mama yake, walikuwa wanamjua tangu utoto wake walikuwa wanamwona jinsi anavyokua, wanapajua kwao,wanawajua wadogo zake, dada zake, wanalikuwa wanajua mpaka kipato chake alichokuwa anakipata katika ajira yake.

Kwahiyo katika kumjua huko, wakamdharau, wakamwona huyu ni Bwana mdogo tu hawezi kufanya lolote,hawakujua kuwa jiwe dogo tu linaweza kumfanya mtu aanguke chini vibaya sana, dharau zile zikasababisha wasimjue kama Mwana pekee wa Mungu, wasimjue kama Mkombozi, wasimjue kama mpatanishi kati ya wanadamu na Mungu, wasimjue kama Bwana, na Masihi, wasimjue kama Adamu wa Pili, bali wamjue tu kama mwana Kijiji au kama mwananchi wa kawaida tu,Kwahiyo Wakajikwaa kwake..Ni kama mtu apite na ghafla akutane na jiwe na kujikwaa..ndicho kilichowatokea hawa watu.

Lakini sio kwamba hao wana bahati mbaya sana, kuliko watu wa kipindi hichi, hapana! hata Hata leo JIWE hilo lipo…Na kila mtu lazima akutane nalo.. Ni jiwe dogo sana mbele za macho ya watu! Lakini ni Teule mbele za Mungu, ni dogo kiasi kwamba barabarani unaweza usilione, lakini ukijikwaa kwa jiwe ni lazima uanguke..

Ndugu unayesoma ujumbe huu, kama hujampa Bwana maisha yako, ni vizuri ukajitathmini mara mbili mbili. Kwasababu katika safari yako ni lazima utasikia injili tu! Itakufikia popote pale..na Kama ukiikataa na kuidharau na kumdharau Yesu Kristo kwako atakuwa ni JIWE LA KUKWAZA. Utaanguka siku na saa usiyodhani, wakati unakazana mbele kukimbilia malengo yako, yatakatika ghafla utakapojikuta upo kaburini na hatimaye kwenye ziwa la moto.Hapa duniani usisafiri kwa kuangalia mbele tu, bali angalia pia njia unazopita…lipo JIWE limewekwa njiani..ni JIWE la KUKWAZA, kwa wale wasioliona. Hivyo usiwe mmoja wao KUKOSANA NA YESU KRISTO, BWANA WAKO aliyetoa uhai wako kwa ajili yako.

Isafishe njia yako kwa kulitii Neno lake leo, anapokwambia mwanangu NJOO!!! Isikie leo sauti yake ukatubu na kubatizwa kwa jina lake, ili upate msamaha wa dhambi zako na ondoleo la dhambi zako, haijalishi ulimkosea kiasi gani, watu wote tulimkosea lakini ametubadilisha, na wewe pia atakubadilisha, usipoteze muda mwingi kuangalia mambo ya ulimwengu huu, wakati hali yako ya kiroho inadorora kila siku, Isafishe njia yako leo.

Zaburi 119: 9 ‘’Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako’’. Bwana akubariki,

Tafadhali ‘share’ ujumbe hu una wengine.

Na pia kama utapenda masomo haya yawe yanakufikia kila siku kwa njia ya Whatsapp  Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

NITAFANYA YERUSALEMU KUWA JIWE LA KUWALEMEA .

NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.

UAMINIFU NI KIGEZO KIKUBWA CHA KUTUMIWA NA MUNGU.

UMEITIKIA WITO INAVYOPASWA?

JE! UMEFUNDISHWA?

KITABU CHA YASHARI NI KITABU GANI?

Kiyama ni nini?


Rudi Nyumbani

Print this post

TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI.

Shalom! Mtu wa Mungu, Jina la Bwana wetu Yesu Kristo litukuzwe daima, karibu tujifunze Neno la Mungu, na leo tutaenda kuona tabia za wanawake hawa wawili na naamini tutakwenda kujifunza kitu kikubwa hususani kwa upande wa wanawake wakristo. Watu hawa ambao tunakwenda kutazama tabia zao wa kwanza ni MKE WA HERODE, na wa pili ni Yule MKE WA PILATO.

Tunafahamu katika maandiko hawa wote walikuwa ni wake wa viongozi wakubwa waliokuwa wanaongoza Taifa la Israeli kipindi cha Bwana wetu Yesu Kristo, Herode alikuwa ni mtawala wa Galilaya upande wa kaskazini na Pilato alikuwa ni akida wa Yudea upande wa kusini wa taifa la Israeli, hawa wote hawakuwa wayahudi, walikuwa ni WARUMI.

Kumbuka wakati ule Dola ya kiRumi ndio iliyokuwa inatawala karibu dunia nzima, hivyo kama ngome yenye nguvu ilikuwa ni sharti iwe na majimbo mengi au makoloni mengi chini yake ya kuyaamrisha. Kama tu tunavyofahamu kipindi kile cha ukoloni katika nchi yetu hii ambayo mwanzo iliitwa Tanganyika lilikuwa ni koloni la wajerumani, na ndivyo ilikuwa katika kipindi kile cha Bwana Yesu nchi ya Palestina (yaani Israeli), ilikuwa ni moja ya koloni la Warumi, hivyo sheria zote, na maagizo yote yahusuyo utawala pamoja na kodi zote zilikuwa zikisanywa na kupelekwa Rumi makao makuu.

Sasa kipindi kifupi kabla ya kuzaliwa Bwana Yesu KAISARI AUGUSTO ambaye tunamsoma habari zake katika Luka 2:1, ndiye aliyekuwa mtawala mkuu wa Dola hii ya Kirumi huko RUMI. Hivyo yeye pamoja na baraza lake chini yake likamweka Herode kuwa kama mfalme wa taifa lote la Palestina na nchi zilizokuwa kando kando yake. Herode huyu mkuu ndiye anayesifika kwa kulikarabati lile Hekalu lililokuwa limebomoka, (Yohana 2:22) na huyu ndiye aliyetaka baadaye kuja kumwua Yesu pindi anazaliwa mpaka kupelekea Yusufu na familia yake kukimbilia uamishoni Misri.

Sasa baada ya kufa kwake, ilipasa awepo mtu wa kumrithi ufalme wake, hivyo aliacha waraka wa urithi na kusema nchi ile ya Palestina igawanywe kwa watoto wake wote, kwahiyo alipokufa waraka ule ulipelekwa Rumi makao makuu ili kuombwa uthbitishwe na Kaisari, hivyo kaisari akathibitisha migawanyo ile na Palestina ikagawanywa kwa watoto wa Herode mkuu, sasa sehemu zile unazoziona zinatajwa sana katika agano jipya (Ndani ya taifa la Israeli) walipewa watoto wake wawili, ambapo mmoja alipewa atawale Galilaya na mwingine akapewa atawale (Samaria, Yudea na Idumea) karibu nusu ya Taifa zima la Israeli, na watoto wake wengine wawili waliosalia walipewa nchi za kando- upande wa Yordani ng’ambo, Iturea na trakoniki na Dekapoli.(Luka 3:1).

Sasa huyu mtoto mmoja wa Herode ambaye alipewa Galiliya ndio Herode Yule tunayemsoma aliyekuja kumuua Yohana Mbatizaji, na ndio huyu huyu alikuwa anamwinda Bwana Yesu baadaye aje kumuua alipokuwa anahubiri lakini Bwana alimwita Mbweha..Na ndio Yule Yule siku ile ya kusulibiwa kwake Pilato alimpeleka kwake ili ahukumiwe,lakini yeye akamrudisha kwa Pilato tena.

Lakini tukirudi kwa Yule mtoto wa pili wa Herode mkuu, ambaye alipewa kutawala upande wa chini wa taifa la Israeli ambayo ni YUDEA NA SAMARIA yote sehemu kubwa ya Israeli historia inaonyesha naye alikuwa ni mkatili vile vile kama ndugu zake, awali ya yote yeye ndio alikuwa akimtafuta mtoto Yesu, ili amwangamize Yesu aliporudi kutoka Misri na wazazi wake hata baada ya baba yake kufa.

Mathayo 2:19 “Hata alipofariki Herode, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri,

20 akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto.

21 Akaondoka akamchukua mtoto na mamaye, akafika nchi ya Israeli.

22 Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki huko Uyahudi mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akasafiri pande za Galilaya,

23 akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo”.

Huyu alizidi kuwa mbaya sana, Historia inaonyesha alifikia hatua hata ya Kaisari kule Rumi kutopendezwa naye, na kumwondoa kwa nguvu madarakani na kumpeleka uamishoni huko ufarasa na kukaa huko mpaka kufa kwake. Ndipo sasa akahitajika mtu wa kuijaza nafasi yake na ndio tunakuja kuona nafasi yake ikachukuliwa na huyu liwali mpya aliyejulikana kama PONTIO PILATO…atawale miji yote ile ya upande wa kusini.

Sasa mpaka hapo natumai utakuwa umepata picha kidogo, jinsi utawala huo ulivyokuwa umejiganyika, hivyo kipindi kile cha Yohana mbatizaji, na Bwana Yesu, hawa viongozi wawili yaani Herode na Pontio Pilato ndio waliokuwa wanalishikilia taifa la Israeli.

Kwahiyo turudi katika kiini cha Somo letu, tunaona viongozi hawa ambao hata hofu ya Mungu haikuwa ndani yao, watu ambao walikuwa sio wayahudi bali wapagani walikuwa na wake zao kila mmoja na mahali pake. Lakini tunaona tabia za hawa wanawake zilitofautiana sana, hususani pale lilipotokea suala la kuwaangamiza watu wa Mungu.

Kama tunavyofahamu habari mke wa Herode japo alifahamu kabisa kuwa Yohana alikuwa ni nabii wa Mungu kweli, lakini yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kukitaka kichwa cha Yohana, zaidi hata ya wale mafarisayo ambao hao ndio wangestahili kukiomba kichwa cha Yohana lakini sio Yule mwanamke. Yeye alimshawishi mume wake amuue Yohana mbatizaji kwa faida zake mwenyewe..Na Herode naye kwa kutomwogopa Mungu akasikiliza viapo vya mke wake na kwenda kumwangamiza Yohana kule gerezani kwa kumkata kichwa.

Lakini tukirudi kwa mwanamke mwingine pili, ambaye naye pia alikuwa katika kiti cha kifalme, aliketi kama malkia, Tunaona Mume wake alipotaka kwenda kuwapa wayahudi amri ya kumuua Bwana Yesu, yeye alikuja na ushawishi mwingine tofauti na Yule wa kwanza, yeye alimwonya sana mume wake asidhubutu kufanya vile kwani ni mtumishi wa Mungu.

Anaeleza jinsi alivyoteswa sana katika ndoto usiku kabla ya Yesu kusulibiwa, embu jaribu kutengeneza picha analala mara ya kwanza, anaota kama yeye ndio anayemngongelea misumari mtu asiye na hatia, anashtuka anaona ni ndoto tu, halafu analala tena, anaota kitu kile kile, anaamka tena, analala jambo lile lile tena linajirudia, hata mara 10, halafu asubuhi anakutana na mtu Yule Yule aliyekuwa anamwona kwenye ndoto analetwa mbele yake…Sura ile ile ya upole inakuja mbele zake,..

Hakika huyu mwanamke Mungu alimwekea kitu kingine cha ziada ndani yake.

Unaweza ukajiulizwa kwanini mambo kama haya hayakumtokea na Yule mke wa Herode? Pengine Yohana angekuwa mzima mpaka wakati wa Kristo kufa kwake,. Kwasababu kumbuka huyu hana chochote cha kumshinda Yule, wala Yule hakuwa na cha ziada cha kumshinda huyu lakini kwanini haikutokea kwa Yule mwanamke mwingine?.

Kaka/dada Kuna wakati unajiuliza maswali mengi lakini unakosa majibu, kwamfano utakutana na dada mmoja mkristo atakwambia anajisikia aibu kuvaa nguo zinazobana, na zaidi atakwambia ninajisikia kuhukumiwa ndani yangu pale ninapojaribu kudhubutu kuvaa sketi fupi, atakwambia ninajiona kama ninajidhalilisha pale ninapovaa suruali na kutembea nayo barabarani mbele za watu na bado mpendwa huyo huyo atakwambia ninaona kama bado sijawa mkristo pale ninapovaa vimini na kuweka ma-make-up usoni na kwenda kanisani au kutembea mbele za watu…

Lakini wakati huo huo utakutana na dada mwingine naye anasema ameokoka atakwambia mbona mimi ninaona kawaida tu, Mungu haangalii mavazi anaangalia moyo..Utamkuta yupo confortable kutembea na vimini na suruali zinazobana barabarani, na wala hasikii chochote kinachomuhukumu ndani yake na bado anaona hakuna tatizo lolote ni sawa tu..

Embu jiulize ni roho ya aina gani ipo ndani yako?, Jichunguze ujiulize kama ni Roho wa Mungu mbona basi haiugui kwa namna moja na ya Yule mwenzako anayejisitiri?..Au unadhani ile ni roho ya shetani au ni mawazo yake tu yanampelekea kuwa vile? Na ya kwako ndio Roho ya Mungu?..Embu nenda kawaulize kabla ya kukutana na Kristo walikuwa wanavaaje watakueleza…watakuambia tofauti yao kabla ya kukutana na baada ya kukutana na Yesu.

Hujui kuwa unamsulibisha Kristo kwa matendo yako, tufauti yako na Yule mke wa Herode haipo, Roho ya Mungu imeshakufa ndani yako, HAIUGUI tena, unaona kila kitu ni okay!!. Utajitetea nipo katika mazingira magumu ya kuacha, lakini nataka nikuambie hawa wanawake wote wawili walikuwa katika mazingira ya level moja, walikuwa wake wa wakuu, tena wa kidunia, tena sio hata wayahudi, lakini mmoja alikuwa na hofu ya Mungu ndani yake na mwingine hakuwa nayo…Vivyo vivyo na wewe usidhani ni wewe peke yako upo katika mazingira magumu ya kuacha hivyo vitu..Wapo wengi tu, tena zaidi yako wewe lakini kwasababu wao wamekubali kuitii hiyo sauti inayougua ndani yao kila siku. Wamekuwa kama walivyokuwa leo hii..ambaye wewe unawaona washamba wamepitwa na wakati.

Ni maombi yangu utabadilisha mwenendo wako dada yangu, shetani anapenda kuwatumia wanawake, kuunyanyua ufalme wake, ni chombo chepesi cha shetani, alikitumia Edeni anakitumia na sasa..Hivyo wewe dada usifanyike kuwa chombo hicho chepesi chepesi tu cha shetani kukutumia anavyotaka. Sio kila mtindo wa dunia hii unaokuja mbele zako unakufaa.. mingi asili yake ni kuzimu,Biblia inasema unapaswa utufute mwenendo wa wanawake wacha Mungu mfano wa wakina Sara na Rebeka na Hana na sio wasanii wa nyimbo za kuzimu.

1Timotheo 2:9 “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.

11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna”

Halikadhalika na kwa mwanaume unayeweka mlegezo, unanyoa kama jogoo, unachora mwili wako tattoo, na huku unajiita ni mkristo..Jiulize ni kwanini wewe unaonaekana tofauti na wacha Mungu wengine?. Au Roho iliyo ndani yako ni bora zaidi kuliko ya wale wengine..Jiulize ndugu, jitathmini…Tumeambiwa tuzijaribu hizi roho, tunapenda injili za “haijalishi”..Na huku nyuma roho zetu zinaangamiia.

Ni maombi yangu, na matumaini yangu injili itatubadilisha, na kuanza kuenenda katika njia kamilifu za Mungu huku tukitii ile sauti ya Roho Mtakatifu inayougua ndani yetu kila siku kutukumbusha namna kuenenda katika utakatifu wote, mpaka kufikia kuja kwa Kristo Bwana wetu na wote kwenda mbinguni bila hila wa mawaa.

Mungu akubariki sana.

+255693036618/ +255789001312

Na pia kama utapenda masomo haya yawe yanakufikia kila siku kwa njia ya Whatsapp. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

MWANAMKE, BINTI, MAMA.( Sehemu ya 1)

Maherodi walikuwa ni akina nani, Na kazi yao ilikuwa ni ipi?

MWANAMKE YEZEBELI

TUZIJARIBU HIZI ROHO.

MAVAZI YAPASAYO.

MAANA YA RANGI KIBIBLIA.

KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.


Rudi Nyumbani

Print this post

JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI AU KUTOA TALAKA?

Shalom Mwana wa Mungu, karibu tuyatafakari maandiko na kujifunza.Leo kwa Neema za Bwana tutajifunza, ni kwanini Mungu aruhusu katika agano la kale wana wa Israeli waoe mke zaidi ya mmoja (kuoa wake wengi). Huu umekuwa ni mjadala mkubwa sana, usio na mwisho miongoni mwa wakristo wengi wasio na ufunuo kamili wa Roho Mtakatifu kuhusu maandiko hayo.

Kwanza kabisa ni muhimu kufahamu kuwa Mungu hajawahi kumwagiza mtu yoyote mahali popote aoe mke zaidi ya mmoja. Hakuna mahali popote Mungu alishawahi kumpa Mwanadamu hayo maagizo…utaniuliza mbona kwenye kumbu 21:15 na kumbu 25:5 inazungumzia habari ya mtu kuwa na mke zaidi ya mmoja?. Ni kweli habari hizo zinazungumzia kuhusu kuwa na mke zaidi ya mmoja, lakini hiyo bado haimfanyi Mungu kuhalalisha mke zaidi ya mmoja..Nitakuthibitishia hilo leo kwa maandiko.

kulielewa vizuri hili suala, hebu tusome maandiko yafuatayo na kisha tuyatafakari..

Kumbukumbu 17: 14 “Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako ukaimiliki, na kukaa humo; nawe utakaposema, Nitaweka mfalme juu yangu mfano wa mataifa yote yaliyo kando-kando yangu;

15 usiache kumweka yule atakayechaguliwa na Bwana, Mungu wako, awe mfalme juu yako; umweke mmoja katika ndugu zako awe mfalme juu yako; usimtawaze mgeni juu yako, ambaye si ndugu yako.

16 Ila asifanye farasi wake kuwa wengi, wala asiwarudishe watu Misri, ili apate kufanya farasi kuwa wengi; kwa kuwa Bwana amewaambia, Tangu sasa msirudie tena njia ile.

17 Wala asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke; wala asifanye fedha zake na dhahabu kuwa nyingi mno.

18 Tena na iwe, zamani aketipo juu ya kiti cha ufalme wake, ajiandikie nakala ya torati hii katika chuo, kufuata hicho kilicho mbele ya makuhani Walawi;

19 na awe nayo, asome humo siku zote atakazoishi; ili apate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wake, ayashike maneno yote ya torati hii na amri hizi, kwa kuyafanya;

20 moyo wake usije ukainuliwa juu ya ndugu zake, wala asikengeuke katika maagizo, kwa mkono wa kuume wala wa kushoto; ili apate kuzifanya siku zake kuwa nyingi katika ufalme wake, yeye na wanawe, katikati ya Israeli”.

Sasa ukisoma mistari hiyo kwa makini, utaona kuwa Bwana anawapa maagizo wana wa Israeli jinsi mfalme wao anavyopaswa awe siku watakapokuja kumchagua…utaona Mungu anawaambia, mfalme huyo anapaswa asiwe mtu wa kujiongezea mali nyingi wala asiwe wa kujiongezea wake..

Na hiyo ni Kutokana na udanganyifu wa Mali na wa ushawishi wa wanawake wanapokuwa wengi (wake wengi).

Sasa kwa maagizo hayo haimaanishi kuwa Mungu, tayari ndio kawapa amri ya wao kuja kuwa na Mfalme, haikuwa mpango wa Mungu kabisa wana wa Israeli waje kuwa na Mfalme, kwani mfalme wao ni mmoja tu yaani YEHOVA, lakini kwasababu Mungu aliona Mbele kwamba watakuja kukengeuka na kutaka kuwa na mfalme kama mataifa mengine walivyokuwa nao ndio hapo akamwambia Musa awape maagizo ya mfalme atakavyopaswa kuja kuwa..Kwahiyo kile kitendo chao cha kuwa na tamaa ya kutaka mfalme ilikuwa ni dhambi kubwa sana, na Mungu hakupendezwa nacho.

Tunasoma hayo katika…

1 Samweli 8:4 “Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama;

5 wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; BASI, TUFANYIE MFALME ATUAMUE, MFANO WA MATAIFA YOTE.

6 Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba Bwana.

7 Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; KWA MAANA HAWAKUKUKATAA WEWE, BALI WAMENIKATAA MIMI, ILI NISIWE MFALME JUU YAO.

8 Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe”.

Umeona hapo kitu Mungu anachomwambia Nabii Samweli?…

hawakukukataa wewe bali wamenikataa mimi nisiwe mfalme juu yao”.Sasa ingekuwa Mungu amehalalisha wana wa Israeli kuwa na Mfalme kule kwenye nyuma kwenye Kumbukumbu la Torati 17 …asingekasirika hapa kuona wana wa Israeli wanataka mfalme…asingelaumu, lakini badala yake unaona Mungu anachukizwa sana na kitendo hicho cha wana wa Israeli kutaka mfalme.

Umeona? Kwahiyo ni wazi kuwa kule kwenye kumbukumbu 17, Mungu alipotoa maagizo ya namna mfalme atakavyopaswa kuwa sio kwamba ndio alitoa ruhusa wana wa Israeli wawe na mfalme, badala yake ni maagizo yatakayotumika baada ya wao kukengeuka akili na kutaka mfalme..(Kwasababu ya ugumu wa mioyo yao)

Kadhalika na katika suala la ndoa.

Mungu alitoa maagizo katika agano la kale namna watakavyoishi endapo watajiongezea wake…lakini sio kwamba alitoa amri ya watu kuoa mke zaidi ya mmoja! Au kutoa talaka…Mungu hakuwahi kumwagiza mtu kufanya hivyo vitu, wala kumpa hayo maagizo…alizungumzia namna ya kuishi na mke zaidi ya mmoja ndio, na maagizo ya kutoa talaka kwasababu aliona tayari wana wa Israeli walishakengeuka na watazidi kuja kukengeuka na kuweka mioyo yao migumu na kuwa na shingo ngumu, kwa kutaka kila mtu kuwa na mke zaidi ya mmoja, na kila mtu kutaka kumwacha mkewe….na kwasababu walishamkataa Mungu katika fahamu Mungu naye akawaacha wafuate akili zao…Kama vile tu walivyomkataa Mungu asiwatawale na kujichagulia mfalme wao wenyewe, Mungu aliwaacha katika akili zao hizo. Lakini haukuwa mpango kamili wa Mungu tangu awali.

Ndio maana Bwana Yesu alikuja kusema mambo hayo hayakuwa hivyo tangu mwanzo.…

Mathayo 19:3 “Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?

4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,

5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.

7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?

8 Akawaambia, Musa, KWA SABABU YA UGUMU WA MIOYO YENU, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi”.

Kwahiyo kwa maandiko hayo yanatufundisha kuwa mke ni mmoja tu na mume ni mmoja tu! Na hairuhusiwi kumwacha mwanamke, kwasababu yoyote ile isipokuwa ya uasherati tu!..Mtu anayeoa wake wengi na bado anajiita ni mkristo, azini, asitumie kisingizio cha kuwa agano la kale liliruhusu, YESU ni mkuu kuliko nabii yoyote maandiko yanasema kuwa “katika yeye utimilifu wote wa Mungu unakaa kwa jinsi ya kimwili

Hivyo kuoa wake wengi ni kinyume na maandiko, na kutoa talaka kwasababu tu ya kutokuelewana au kuchukiana.(Wakolosai 2:9)”.

2 Timotheo 2:15 “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.”

Bwana akubariki sana.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine..

Mawasiliano: +255693036618 / +255789001312

Na pia kama utapenda masomo haya yawe yanakufikia kila siku kwa njia ya Whatsapp Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

WANA-NDOA: Baba Mkwe, Na mama Mkwe.

Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?

MUNGU KUSEMA NA WEWE PEKEE, HAITOSHI KUKUPA USHINDI.

Wanafunzi wa Yesu, walimaanisha nini kusema kama “Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa”?

Je! Sisi kama wakristo Tunaruhusiwa kuchangia ujenzi wa Imani nyingine?

Je ni kweli ilikuwa desturi ya Bwana kuishika sabato?(Luka 4:16)

Rudi Nyumbani:

Print this post

KWANINI NABII ISAYA ALIAGIZWA KUHUBIRI UCHI?

Habari hiyo tunaipata katika kitabu cha Isaya 20: 1-6

“1 Katika mwaka ule jemadari Yule alipofika Ashdodi,alipotumwa na Sargoni mfalme wa Ashuru;naye alipigana na Ashdodi akautwaa.

2 wakati huo Bwana alinena kwa kinywa cha Isaya,mwana wa Amozi, akisema, Haya, uvue nguo ya magunia viunoni mwako, na viatu vyako miguuni mwako.

3 Naye akafanya hivyo akaenda UCHI, miguu yake haina viatu. Bwana akasema, Kama vile mtumishi wangu Isaya anavyokwenda UCHI, hana viatu, awe ishara na ajabu kwa muda wa miaka mitatu juu ya Misri na juu ya Kushi;

4 vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawachukua uchi, wafungwa wa Misri, na watu wa Kushi waliohamishwa, watoto kwa wazee, hawana viatu, MATAKO YAO WAZI, Misri iaibishwe.

5 Nao watafadhaika, na kuona haya kwa ajili ya Kushi, matumaini yao, na Misri, utukufu wao.

6 Na mwenyeji wa nchi ya pwani atasema katika siku hiyo, Angalia, haya ndiyo yaliyowapata watu wale tuliowatumaini, ambao tuliwakimbilia watuokoe na mfalme wa Ashuru; na sisi je! Twawezaje kupona?”.

Misri wakati huo wa kipindi cha nabii Isaya ilikuwa ni moja ya mataifa matatu makuu yenye nguvu duniani, ikitanguliwa na Ashuru pamoja na Babeli, lakini kutokana na majivuno yake kuzidi na maovu yake kuwa mengi kwa sanamu zake, Mungu alikusudia kuuangamiza, tena sio kwa maangamizi ya kawaida tu bali ya aibu, pamoja na nchi ya kando yake iliyoitwa kushi (ambayo ni nchi ya Ethiopia kwa sasa) lakini kabla ya Mungu kufanya hivyo alimtuma kwanza nabii Isaya awatolee unabii na kuwaonya , ndio hapo tunaona Isaya anaambiwa avue nguo zake na viatu vyake atembee uchi katika hiyo miji awahubirie kuwa wasipotubu, basi mfalme wa Ashuru atakuja kuwafanya hivyo watu wote wa Misri na Kushi, yaani ataipiga miji yao na kisha hataishia hapo tu atawachukua watu mateka wao wakiwa uchi wa mnyama, kutoka Misri mpaka Ashuru.

Tunafahamu kabisa kitendo cha kutembea uchi ni kitendo cha aibu kubwa sana, kwanza utaanzaje anzaje kutembea barabarani uchi,.Nakumbuka wakati Fulani nyuma kabla sijampa Bwana maisha yangu niliota ndoto ambayo siwezi kuisahau nilipoamka nilimshukuru Mungu haikuwa kweli.

Niliota nimejikuta ghafla nipo katikati ya mji, nikiwa uchi wa mnyama,sasa kwa kupaniki nikaanza kutafuta nguo au kitu chochote cha kujifunika lakini nilikosa, nikaanza kutumia mikono kujisitiri, huku nikijibanza kwenye vikona kona vya kuta ili watu wasinione, ikawa nikiona watu wamepungua kidogo ninatokea pale na kwenda kukimbilia kujificha sehemu nyingine, mpaka ikafanikiwa kuwa usiku, ndipo nikakimbia moja kwa moja nyumbani, nikapata unafuu kidogo,.

Nikadhani imeishia hapo hakuna mtu aliyejua, lakini baada ya muda kidogo rafiki yangu mmoja wa kike akaja kunifuata, akaniambia mbona tumeona picha zako za uchi zimezagaa mtandaoni kila mahali? Yule ni wewe kweli au ni mwingine?..Niliposikia vile nilitamani nife palepale ili aibu ile inipotee!, maana picha ikishaingia mitandaoni haitakaa ifutike milele, vizazi na vizazi wataona..na hapo hapo likaja neno la kiingereza mbele yangu ambalo nilikuwa sijawahi kulisikia sehemu yoyote likisema “NUDE”.

Halafu saa hiyo hiyo nikashutuka usingizini..Nikaenda moja kwa moja kutazama kwenye dictionary ya kingereza lile neno lina maana gani..nikakuta linamaanisha UCHI wa mnyama.. Hapo ndipo nikajua nilikuwa uchi katika roho.

Nimetoa mfano huo kuonyesha ni hali mbaya kiasi gani mtu kujikuta upo uchi halafu isitoshe mbele za watu wengi, Kulikuwa kuna sababu kubwa kabisa Mungu kumruhusu Nabii Isaya atembee vile kwa miaka 3 ili watu wa Misri na Kushi waogope kwa mambo yatakayowakuta miaka michache mbeleni.

Kwahiyo ni kawaida ya Mungu, kuzungumza na mtu au watu wake kupitia ishara fulani, tunamsoma pia Nabii Ezekieli, Bwana Mungu alimwambia ale kinyesi, kuwaonyesha wana wa Israeli kuwa wasipotubu, watapelekwa utumwani na watakula chakula kilichotiwa unajisi kwa kinyesi kwa namna hiyo. Na kwasababu wana wa Israeli hawakutaka kusikia jambo hilo lilikuja kutimia kama lilivyo siku walipokuja kuchukuliwa mateka kupelekwa utumwani.

Vivyo hivyo tunamsoma nabii mwingine, ambaye ndiye NABII MKUU , naye Mungu aliruhusu atoe ujumbe wake katika hali kama hiyo hiyo ya kuwa tupu ili watu wake wajiulize ni nini maana ya mambo hayo, watu waogope, watubu, lakini wasipotaka kutubu hali kama hiyo hiyo itakuta huko mbeleni, na huyu si mwingine zaidi ya BWANA wetu YESU KRISTO.

Yeye alitundikwa uchi pale msalabani, mataifa yote yalikuja kuitazama aibu yake, mpaka watu wakasema amelaaniwa huyu..japo kuwa vile hakukuwa kwa ajili yake bali kwa ajili yetu sisi lakini Mungu aliruhusu aenende vile kama ishara ya yatakayowakuta watu wasipotubu huko mbeleni..Wakati ule wanawake walikuwa wanamlilia Bwana, lakini yeye aliwaambia msinililie mimi, hii ni ishara kwa ajili yenu, jililieni ninyi na nafsi zenu, na watoto wenu. (Luka 23:28),

Na kwasababu hawakutubu kama Bwana alivyowaonya na kuwaambia ..“ni mara ngapi amejaribu kuwakusanya pamoja kama kuku akusanyavyo vifaranga vyake lakini mlikataa” hivyo nyumba yao imeachiwa hali ya ukiwa…Mnamo mwaka AD 70, Jeshi la kirumi chini ya Jenerali Titus liliizunguka Yerusalemu, na kuliteketeza hekalu na kuwaua watu kwa kuwachicha kama kuku..

Kulingana na mwanahistoria JOSEPHUS, aliyeandika historia nyingi katika usahihi za kuhusiana na matukio ya nyakati za kale za biblia, anaeleza kuwa, wakati Jeshi la Rumi limeuzunguka mji wa Yerusalemu, walikuwa wanakamata wayahudi kila siku na kuwasulibisha uchi kama walivyomsulibisha Bwana Yesu, anasema ilifika mpaka idadi ya watu 500 kwa siku waliokuwa wanasulibiwa nje ya ukuta wa Yerusalemu, na wote walikuwa wanasulibiwa uchi wa mnyama, anasema ilikuwa ni idadi kubwa mpaka kufikia MTI ya kusulibishia watu maeneo yale ikawa inakosekana …Jeshi la Rumi lilifanya vile kuwahimiza Wayahudi (Waisraeli) wasalimu amri, na wanawake na watoto wauawa kikatili sana.

Kwahiyo Bwana kuangikwa msalabani akiwa tupu (licha ya kuwa msalaba unabeba ufunuo mwingi na tofauti tofauti wa kinabii) lakini pia ile ilikuwa ni ishara kwa Wana wa Israeli kwamba wasipotubu mambo hayo hayo na zaidi ya hayo yatawakuta mbeleni…Bwana alifanyika ishara kama Isaya alivyofanyika Ishara.

Kumbuka Pia Bwana wetu huyo huyo alisema maneno haya katika Ufunuo 16:15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na KUYATUNZA MAVAZI YAKE, ASIENDE UCHI HATA WATU WAKAIONE AIBU YAKE.)

Unaona hapo kwa bahati mbaya siku Bwana atakapokuja atakuta kuna watu ambao wapo UCHI rohoni, (YAANI HAWAJASITIRIWA DHAMBI ZAO)..Hao ndio wale siku ile ya hukumu watasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu na ndipo jambo lao moja baada ya lingine liwe la siri lisiwe la siri, lilifanyika gizani, litachambuliwa mbele ya mataifa yote, na mbele ya malaika wote wa Mbinguni..hatua baada ya hatua, tukio baada ya tukio, ulizini kwa siri, ulitazama pornography kwa siri, ulitoa mimba siri, uliua kwa siri, ulitukana kwa siri, ulikula rushwa kwa siri, yote yatawekwa wazi pale, ndipo hapo mtu atakumbana na aibu isiyoelekeza ambayo hajawahi kuiona katika maisha yake yote, na moja kwa moja atatupwa katika lile ziwa la moto..Lakini kwa mtu Yule ambaye sasa maisha yake yamefichwa na Kristo, siku ile vivyo hivyo dhambi zake zitafichwa na hivyo hatapita hukumuni bali atavuka na kwenda moja kwa moja uzimani.

Warumi 4:6 “Kama vile Daudi aunenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo,

7 Heri waliosamehewa makosa yao, NA WALIOSITIRIWA DHAMBI ZAO.

8 Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi”.

Hilo ndilo vazi ndugu..Hiyo DAMU YA YESU…Lakini kwa bahati mbaya kanisa tunaloishi sisi, ambalo ndio kanisa la mwisho kati ya yale saba, limetabiriwa kuwa kanisa baya kuliko yote, na katikati ya ujumbe wetu tuliopewa, tumeonekana kuwa tu UCHI, tofauti na makanisa mengine ya nyuma yaliyopita..Hiyo ni kuonyesha kuwa tupo katika hali mbaya sana.

Tusome.

Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na UCHI.

18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, NA MAVAZI MEUPE UPATE KUVAA, AIBU YA UCHI WAKO ISIONEKANE, na dawa ya macho ya kujipakamacho yako, upate kuona.

19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”.

2 wakati huo Bwana alinena kwa kinywa cha Isaya,mwana wa Amozi, akisema, Haya, uvue nguo ya magunia viunoni mwako, na viatu vyako miguuni mwako.  3 Naye akafanya hivyo akaenda UCHI, miguu yake haina viatu. Bwana akasema, Kama vile mtumishi wangu Isaya

Unaona hapo?. Huu ni wakati wa kugeuka na kumaanisha kabisa kumfuata Bwana, tuhakikishe uhusiano wetu na Mungu upo sawa kila siku ili siku ile tuwe na ujasiri wa kusimama mbele zake. Ndugu Kudumu katika dhambi hakuna manufaa yoyote, zaidi ni kila siku kuishi katika maisha ya mashaka na hofu, usiikatae neema ya Kristo maishani mwako hiyo ni kwa faida yako mwenyewe. Tubu sasa umaanishe kumfuata Kristo naye atakupokea, naye atakupa VAZI, lililochovywa katika damu yake liwezalo kusitiri aibu yako yote ya rohoni.Na siku ile hutakuwa uchi mbele zake, bali utaweza kuvuka kutoka mautini kwenda uzimani…

Damu ya Bwana wetu YESU KRISTO itukuzwe milele.Amina

Tafadhali “Share” Ujumbe huu kwa wengine. Na Bwana atakubariki.

Mawasiliano: +255693036618/ +255789001312

Na pia kama utapenda masomo haya yawe yanakufikia kila siku kwa njia ya Whatsapp Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

Kwa aibu yako mwenyewe, na kwa aibu ya uchi wa mama yako.

EDENI YA SHETANI

USIACHE KUJIFUNZA NENO LA MUNGU

MAISHA YETU NI MILKI YA YESU KRISTO.

JE! DAMU INA UMUHIMU WOWOTE KATIKA MAISHA??

MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.

USIYAACHE MAVAZI YAKO NA KWENDA UCHI!


Rudi Nyumbani

Print this post

AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!

Luka 24:1 ‘‘Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.

2 Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi,

3 Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu.

4 Ikawa walipokuwa wakifadhaika kwa ajili ya neno hilo, tazama, watu wawili walisimama karibu nao, wamevaa nguo za kumeta-meta;

5 nao walipoingiwa na hofu na kuinama kifudifudi hata nchi, hao waliwaambia, Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu?

6 Hayupo hapa, amefufuka. Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa akaliko Galilaya,

7 akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulibiwa, na kufufuka siku ya tatu’’.

Waebrania 1:4 ' amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao'.Mambo yote yalimalizika siku ile Bwana aliyokata roho, pale aliposema IMEKWISHA!!..Hapo ndio ilikuwa mwisho wa mambo yote, ni sawa na mwanafunzi aliyemaliza mtihani wake wa mwisho wa kuhitimu siku ile anapoweka kalalmu yake chini ..Siku hiyo ndio mwisho wa mambo yake yote yahusuyo shule.

Na Bwana katika siku ile ya Ijumaa, ndio ulikuwa mwisho wa Majaribu yake yote, mwisho wa kazi yake yote, Hivyo mwisho wa majaribu yake ndio ulikuwa mwanzo wa ukombozi wetu! NA Heshima yetu sisi..Haleluya. Siku ile alimaliza yote aliyopaswa kufanya, maumivu, dhiki, taabu, uchungu na kila kitu! Ndio vilikuwa mwisho pale…akaweka rekodi ulimwenguni ya kuwa mwanadamu aliyeishi mpaka kufa bila kutenda dhambi hata moja!..Na kuthibitisha mbele za Mungu kuwa mwanadamu anaweza kuishi pasipo dhambi, Maisha yake yote mpaka kufa, Na ndio maana maandiko yanasema ‘amefanyika bora kupita malaika.

Waebrania 1:4 ‘ amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao’.

Ikiwa na maana kuwa Hakuna malaika yoyote ambaye alishawahi kuwa mkamilifu kama yeye.

Wengi hatujui kuwa malaika nao walijaribiwa kama tunavyojaribiwa sisi, na wapo walioshinda na wapo walioshindwa, walioshinda ndio hao wapo mbinguni sasa, na walioshindwa ndio hao ambao wapo upande wa shetani..Kwahiyo miongoni mwa walioshinda pia wametofautiana ngazi, wapo waliofanya vizuri Zaidi ya wengine..sisi wanadamu hatuwajui ni yupi aliyefanya vizuri Zaidi ya mwingine, pengine tutajua tukishafika huko juu, tutakapopewa miili ya utukufu ya kufanana na wao. Sasa miongoni mwa hao waliofanya vizuri,

 hakuna aliyefanya vizuri Zaidi ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Na kwasababu Mungu hana upendeleo, yeyote aliyefanya vizuri ndiye atakayepewa thawabu kubwa Zaidi. Kwahiyo kwasababu Bwana alifanya vizuri kuliko malaika wote wa mbinguni basi,Mungu akampa Jina ambalo, hakuna mtu aliyewahi kuwa nalo tangu ulimwengu kuumbwa, na Zaidi ya yote akapewa vitu vyote vya mbinguni na vya duniani..Akakabidhiwa mamlaka yote ya mbinguni na duniani juu ya watu wote..kwamba kila goti lipigwe mbele zake. Utasema ni wapi kwenye biblia jambo hilo lipo..soma.

Wafilipi 2: 5 ‘’Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;

6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;

7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;

8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.

9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;

10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;

11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba’’.

Na kwasababu sisi tuliomwamini ni ndugu zake, hivyo hawezi kutuacha chini, ni lazima nasi pia tutamiliki naye, malaika watakuwa chini yetu, kwasababu yeye yupo juu ya malaika wote sharti na sisi tuliokolewa tuwepo naye..Ni sawa na kijana apambane mpaka aipate nafasi ya uraisi, ndugu zake kwa namna moja au nyingine watafika tu ikulu mahali anapokaa..mama yake na baba yake watamtembelea hata ikiwezekana kulala kule,na hiyo ni kwasababu tu wale ni ndugu zake! na si kingine kingine..

Kadhalika na Bwana Yesu kwa Haki yake ambayo imemfanya kupewa mamlaka yote ya mbinguni na duniani, na kupewa enzi yote na kuketi katika kile kiti cha enzi, sasa sisi ndugu zake (ambao ni wanadamu na si malaika) hawezi kututupa, kwa namna moja au nyingine tutafika tu pale alipo haleluya!! Ndio maana kuna umuhimu sana wa kuwa ndugu wa damu wa Bwana wetu Yesu Kristo nikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mara ya pili.

Kwasababu hakuna njia yoyote ya kumkaribia yeye kama hatutazaliwa mara ya pili kwa damu yake!! Kumbuka si kwa damu ya mwanadamu bali kwa damu yake, sio kwa mapenzi ya mwili bali kwa mapenzi yake..wengi wanatenda mema na kufanya mambo mazuri na kusema kwa matendo yangu haya lazima nitamwona Mungu, ndugu yangu usidanganyike…

Unaweza ukatenda matendo mazuri kuliko mkristo yeyote duniani na bado usimkaribie Mungu hata kidogo…kwanini iwe hivyo? Jibu ni rahisi ni kwasababu wewe sio ndugu wa damu wa yule mhusika, kwahiyo matendo yako mazuri ni bure!.

Ndugu yangu kama wewe ni muislamu unasoma ujumbe huu, au mkristo ambaye bado hujayajua vizuri mamlaka Bwana Yesu aliyopewa na vigezo vya kuwa mrithi pamoja naye, na unasema moyoni ninasaidia masikini, ninawaheshimu wazazi, sidhulumu, sifanyi hichi sifanyi kile, ukijidanganya kuwa kwa mambo hayo tu upo karibu na Mungu na huku umemweka Kristo nyuma

Hujazaliwa mara pili katika damu yake, napenda nikuambie ndugu yangu UNAPOTEZA MUDA!!!! Matendo yako ni mazuri lakini hayatakusaidia huko mbeleni. Huko mbeleni ni UNDUGU ndio utakaojalisha kwanza na kisha ndio matendo yafuate!..Ni sawa na kwenda kumfanyia boss wako mema yote unayoyajua duniani na kumpendeza kwa viwango vyote ukitumai kuwa siku moja atakurithisha kampuni lake!!…hilo katika akili yako lifute, kwasababu hawezi kuacha kumrithisha mtoto wake (damu yake) akurithishe wewe?..hata kama mwanawe hana tabia nzuri kama za kwako, hata kama wewe ni mchapa kazi kuliko yeye, siku moja huyo mtoto atakuja kuwa boss wako tu…kwanini?? Kwasababu ya uhusiano wa kidamu uliopo kati ya yule mtoto na baba yake!!.

Na ufalme wa Mbinguni ndio upo hivyo hivyo, ndio maana ufalme wa mbinguni unaitwa URITHI, sio UTAHIFISHWAJI, hapana bali URITHISHWAJI, wanarithishwa WANA WA MUNGU tu. Kumbuka pia ufalme wa mbinguni haukuanza siku ile Bwana Yesu aliposulibiwa, ufalme wa mbinguni ulikuwepo kabla hata ya dunia kuumbwa, ni kitu kinachoendelea, kwahiyo kitakachotokea ni urithishwaji, Na wana wa Mungu ndio watakaourithi, na wana wa Mungu ni wale wote waliomwamini Yesu Kristo na kumpokea kwa kuzaliwa mara ya pili.

Yohana 1:12 ‘Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;

Kwahiyo ndugu yangu, siku ya leo (SIKU YA BWANA KUFUFUKA). Ni siku ya muhimu sana,Bwana anapowatembelea wengi duniani kuwapa wokovu asikupite na wewe. Kama hujazaliwa mara ya pili, huu ni wakati mzuri wa kufanya hivyo…Utauliza unazaliwaje mara ya pili?…Biblia imetupa majibu, kuwa hatuwezi kurudi tena kwenye matumbo ya mama zetu na kuzaliwa tena!!..Kuzaliwa mara ya pili ni lugha ya rohoni, yenye maana ya kufanyika upya kwa Maisha yako ya kiroho, yaani kugeuzwa na kuwa mwingine katika mwelekeo wako wa kiimani.

Hiyo ndio maana ya kuzaliwa mara ya pili. Tunasema Taifa ya Tanganyika lilizaliwa mwaka 1961, haimaanishi liliingia tumboni kwa mama yake na kuzaliwa hapana! Bali ni lugha tu inayomaanisha, kuwa lilifanyika upya kidemokrasia na kuwa taifa huru linalojitegemea mwaka huo. Na katika Imani ya kikristo ndio hivyo hivyo, unapofanyika upya kifikra kwa nguvu za kiMungu, unakuwa umezaliwa mara ya pili. Na zipo hatua chache za kufanyika upya huko…

Yohana 3:1 ”Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi.

2 Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.

3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA MARA YA PILI, HAWEZI KUUONA UFALME WA MUNGU.

4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?

5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO, HAWEZI KUUINGIA UFALME WA MUNGU.

6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.

7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili”.

Kwahiyo hatua za kufuata ili uwe umezaliwa mara ya pili baada ya kumwamini Bwana Yesu Kristo kuwa ni mkombozi wa ulimwengu, na kuwa yeye ndiye aliyeshinda kila kitu, na kukabidhiwa mamlaka yote ya mbinguni na duniani, hatua inayofuata ni kwenda kubatizwa katika maji mengi na kwa jina lake (Yesu Kristo), kuwa kwako kama ishara ya kufa na kufufuka na Kristo, (huko ndio kuzaliwa kwa maji Bwana alikokuzungumzia) na baada ya kubatizwa Bwana Mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu ndani yako atakayekusaidia kushinda dhambi, na kukuongoza katika kuijua kweli yote ya maandiko, na kukulinda, (Huko ndiko kuzaliwa kwa Roho).

Sasas ukikamilisha hatua hizo tatu, yaani kuamini, kubatizwa kwa maji, na kubatizwa kwa Roho Mtakatifu…Utakuwa tayari umezaliwa mara ya pili, umefanyika kiumbe kimpya , nawe unakuwa ni mwana wa Mungu, mrithi wa Mungu.ya kale yote yamepita, Tazama yamekuwa mapya,(2 Wakoritho 5:17) Unakuwa ni NDUGU wa Bwana WETU YESU KRISTO, wa Damu kabisa…Unakuwa mrithi wa ahadi za Mungu, hakuna atakayeweza kukushtaki kuanzia wakati huo, wala hakuna atakayeweza kukutenga na upendo wake…

Ndugu Kwasasa hatuujui vizuri kwa mapana na marefu urithi huo, tunajua kwa sehemu tu! Lakini baada ya maisha haya kuisha, ndipo tutakapomfurahia Mungu, tutamjua kwa mapana na marefu utajiri aliotupa na heshima aliyotuheshimu nayo, kwa kupitia mwanawe mpendwa YESU KRISTO.

Ni maombi yangu kuwa katika msimu huu wa pasaka, Utatambua maana yake katika maisha yako, na pia utafanya maamuzi Mema na ya Busara na Bwana akusaidie.

Mawasiliano: +255693036618

Na pia kama utapenda masomo haya yawe yanakufikia kila siku kwa njia ya Whatsapp  Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

Print this post

CHUJIO HILI NI LA AJABU SANA!

Jaribu kufikiria mtu amepata ajali ya bodaboda, mguu wake umekatika anatokwa na damu nyingi pale chini na kwa bahati nzuri anatokea msamaria mwema ili kutaka kumsaidia, lakini Yule msamaria alipofika kabla kutaka kumsaidia au kufanya jambo lolote alimtazama kwa makini, ndipo alipogundua mahali tatizo lilipo na bila kupoteza muda alikwenda moja kwa moja kwenye uso wake na kutumbua kipele kidogo, kilichokuwa kimejaa usaha pembezoni mwa shavu lake, na kusema afadhali nimekusaidia maana kipele hicho kama usingempata mtu mtulivu kama mimi, usingekiona, sasa nakuona upo sawa ninaweza kuondoka, nitakuja kesho tena kukutazama hali yako unaendeleaje … Na mara Yule mtu kweli akapanda gari lake na kuondoka.

Je! Hapo Ni kweli mtu huyo atakuwa amemsaida Yule alayepatwa ajali pale chini?. Ni kweli kabisa ametoa msaada lakini sio kwa tatizo lililokuwa linatawala kwa wakati ule, msaada kama huo ungemfaa zaidi saa mtu yule akiwa na afya yake na nguvu zake, lakini sio kwa wakati ule ambao amepata ajali mbaya ya kukatika mguu. Hatutakosea kusema mtu huyo ni MNAFKI kwasababu aliliona tatizo kubwa zaidi ya lile lililokuwa nalo lakini badala yake aliliacha hilo na kwenda kushuhulika na mambo madogo yasiyokuwa ya umuhimu kwa wakati huo.

Mambo kama hayo hayo Bwana Yesu aliyaona ndani ya viongozi wa ki-dini waliokuwa wakati ule..

Mathayo 23:23 ‘Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, ADILI, na REHEMA, na IMANI; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.

24 VIONGOZI VIPOFU, WENYE KUCHUJA MBU NA KUMEZA NGAMIA’.

Unaona Watu hawa walifanikiwa kuigeuza sheria ya Mungu nyuma mbele,..yaani yale mambo ya msingi waliyafanya yasiwe na msingi, na yale yasiyo ya msingi yawe ndio ya msingi. Na huku wakitumia kisingizio cha kwamba Mungu ametoa maagizo hayo yafanyike, na hivyo yanapaswa yatekelezwe kwa nguvu zote na kwa bidii…sababu hiyo basi wakaitwa vipofu kwa upambanuzi wao…

mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, ADILI, na REHEMA, na IMANI; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.  24 VIONGOZI VIPOFU, WENYE KUCHUJA MBU NA KUMEZA NGAMIA’.

Walikuwa wanawafundisha watu utoaji wa zaka,(fungu la 10),katika kila mapato mtu ayapatayo..lakini hawakuishia hapo tu walipata ufunuo wa ziada na kwenda mpaka kwenye mboga mboga na viungo,vyote…Lakini mambo yale ya muhimu ambayo Mungu anayahitaji kwanza kuyaona ndani ya mioyo ya watu mambo ya ADILI na IMANI yaliyokosekana ndani ya watu wengi wao walikuwa hawana muda nayo wala hawakutaka kujishughulisha nayo, kwao waliyapa nafasi ya mwisho.

Walikuwa wanasisitiza utoaji mpaka kufikia hatua ya kuwaruhusu watu wafanye biashara katika nyumba ya Mungu ili tu walete zaka za kutosha nyumbani kwa Mungu..Lakini dhuluma na ufisadi vilikuwa vimejaa ndani ya mioyo ya watu. Tabia hiyo iliwapofusha macho sana.

Wanamwona mtu anatenda mambo maovu, hawamsemeshi chochote lakini wakimwona mtu hajaleta fungu la kumi anafuatiliwa kwa umakini na kuwekwa vikao, na kukemewa, na kuambiwa unamwibia Mungu na hivyo Mungu atamlaani. Lakini kuhusu dhambi wazifanyazo kwa siri Mungu hawalaani.

Wanawaona watu hawana maarifa ya mambo ya Mungu katika masuala ya imani, hawafahamu chochote juu ya siri za ufalme wa mbinguni, badala wazingatie hayo kuwafundisha kuwa na kiasi na kuishi kama wapitaji tu katika dunia hii, ya kitambo, hilo kwao halina umuhimu sana walipenda mtu awe tajiri ili alete zaka hekaluni.

Ndio hapo Bwana Yesu anawaambia, “Viongozi vipofu, wenye KUCHUJA MBU NA KUMEZA NGAMIA.”..Jiulize Inawezekanikaje, kumwona ngamia kwenye kikombe cha chai, lakini mbu usimwone, au ngamia anawezaje kupita kwenye chujio halafu mbu akwame..HILI CHUJIO NI LA AJABU SANA!!….. Tunaweza kusema halipo duniani lakini kumbe lipo..

Linawezekana kabisa kutokea kwetu kama na sisi tutakuwa na tabia kama hizo..Ikiwa mafundisho yetu yatelenga kwenye Utoaji, yatalenga kwenye mafanikio ya kidunia miaka yote, yatalenga tu kubarikiwa na kuwa na mali…mwaka mzima tunajifunza na kufundishwa hivyo, lakini siku hata moja hatugusii umuhimu wa Toba, hatugusii umuhimu wa ubatizo sahihi kwa mwaminio, hatugusii juu ya mbingu mpya na nchi mpya zinazokuja, hatugusii juu ya UPENDO kwa Mungu na kwetu sisi sisi kwa sisi, kama ndio amri ya kwanza tuliyopewa na Mungu.

Mathayo 22: 35 ‘Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu;

36 Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?

37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.

38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.

39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako’’.

Unaona Kama hatutakaa kuyagusia mambo hayo ambayo ndio ya msingi Mungu anayotaka kuyaona ndani ya watu, na badala yake tunazungumza tu habari za sadaka au zaka au michango, na u-partinership tuliopo miaka nenda rudi..basi tufahamu kuwa na sisi pia tutaitwa viongozi-vipofu..

Sio kwamba kutoa zaka ni dhambi hapana ndio maana Bwana Yesu alisema “imewapasa kuyafanya hayo” lakini msisahau na yale mengine, ambayo ndio mambo MAKUU YA SHERIA. Hivyo hivyo na wewe unayekwenda kusikiliza, au kuhubiriwa huku unafahamu kabisa uhusiano wangu na Mungu unadorora kila siku, na mahali ulipo unaona kabisa hapakutoshelezi kiroho..Unaendelea kudumu hilo eneo?..Kwa faida ya roho yako ni heri ukatafute mahali patakapo kujenga roho yako sasa..Hakuna dhambi yoyote kufanya hivyo. Kristo ndiye aliyekuita na sio kanisa.

Ni sawa na wewe leo unaumwa na njaa ya siku sita hujala chochote, halafu mtu anakuletea suti nzuri kama kitulizo cha njaa yako, hiyo suti itakufaa nini kwa wakati huo, itakufaa kwa wakati mwingine lakini sio huo,hata kama ukipendeza pasiwe na mtu mfano wako duniani, lakini kumbuka kesho unakwenda kufa… kinyume chake Utamthamini zaidi Yule atakayekuletea sahani ya chakula, hata kama atakuwa amekinunua kwa bei ya chini lakini kinakufaa kwa wakati huo..Kisha baadaye ndio umrudie Yule wa suti kama utakuwa na uhitaji nao.

Hivyo ikiwa mahali ulipo, hapaudumishi uhusiano wako na Mungu, ndugu nakushauri ondoka kwanza hapo katafute mahali chakula kilipo ukishashiba vizuri basi urudi kama kutakuwa na umuhimu..Mafundisho ya mafanikio ya kidunia ni mafundisho madogo sana katika mafundisho ya Ki-Mungu, ambayo hata yakipuuziwa yasifundishwe kabisa hayawezi kuleta madhara makubwa kama yakavyopuuziwa mafundisho ya KI-ROHO Yanayohusu toba, utakatifu na uzima wa roho yako na kumpenda Mungu. Mafanikio ni mazuri na jambo la ki-Mungu kujifunza kufanikiwa, lakini sio jambo la kwanza..Jambo la kwanza ni kuutafuta kwanza UFALME WAKE NA HAKI YAKE, Na hayo mengine ndio yafuate.

Hizi ni siku za mwisho. Je! Umeokolewa?, Je unauhakika umejazwa Roho Mtakatifu?, Kumbuka Neno la Mungu linasema.. “Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.”(Warumi 8:9)…Hivyo kama upo mbali na wokovu tubu sasa ukabatizwe kwa Jina la YESU KRISTO, upate ondoleo la dhambi zako na Kisha Mungu atakupa kipawa cha Roho wake mtakatifu, ambaye atakulinda, kukufundisha, kukuongoza na kukusaidia kushinda dhambi. Na Zaidi ya yote yeye ndiye Muhuri wa Mungu, ukimpata yeye, ni sawa na Barua iliyotiwa muhuri, Utakuwa umehakikiwa kwa viwango vya kimbinguni.

Ubarikiwe sana  na Bwana wa Majeshi Yesu Kristo.

Tafadhali “Share” ujumbe huu kwa wengine. Na Mungu atakubariki.

Mawasiliano: +255789001312

Na pia kama utapenda masomo haya yawe yanakufikia kila siku kwa njia ya Whatsapp  Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

AINA SABA (7) ZA UNAFIKI, AMBAZO UNAPASWA UJIEPUSHE NAZO.

UAMINIFU NI KIGEZO KIKUBWA CHA KUTUMIWA NA MUNGU.

WAKINYAMAZA HAWA, MAWE YATAPIGA KELELE.

KWANINI TUWE WENYE BUSARA KAMA NYOKA?

UPENDO

AGENDA KUBWA YA SHETANI KWA KANISA HILI LA LAODIKIA.

Nini maana ya ugonjwa wa kufisha? (Yeremia 17:9)


Rudi Nyumbani

Print this post

MAOMBI KWA WENYE MAMLAKA.

1 Timotheo 2 : 1-4

“1 Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;

2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.

3 Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;

4 ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli”.

Shalom Mtu wa Mungu, karibu tujifunze maandiko, na leo kwa Neema za Mungu tutajifunza juu “Umuhimu wa kuombea wenye mamlaka”.

Biblia inasema katika Warumi 13:1

“Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.

2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu.

3 Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake;

4 kwa kuwa yeye NI MTUMISHI WA MUNGU KWAKO KWA AJILI YA MEMA. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu.

5 Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri”.

Katika mistari hiyo Mtume Paulo anajaribu kutueleza kwa uweza wa Roho kuwa watu wenye mamlaka ni watumishi wa Mungu,..sasa kuna utumishi wa Mungu wa aina mbili, wa kwanza na wa umuhimu ni ule wa KUHUDUMU KATIKA KAZI YAKE, Yaani kazi ya kuhubiri injili kwa kupitia karama alizoziweka ndani ya kanisa. Huo ndio utumishi wa Mungu wa Kwanza na wenye hadhi ya juu, na wenye thawabu kubwa kuliko zote.

Lakini pia upo utumishi usio wa madhabahuni, huo Mungu kauweka kwa ajili ya kuwapatia mema watu wake na kuwahukumu waasi…Kwa mfano vyombo vya dola, hivyo havihubiri injili ya wokovu lakini ni vyombo vilivyoruhusiwa na Mungu kuwepo ili kukomesha uasi na matendo mabaya katika jamii, n.k. Sasa leo hatutaingia kwa undani kuelezea juu ya utumishi huu, lakini tutajifunza kwa ufupi umuhimu wa kuwaombea wenye mamlaka.

Biblia imetuambia tuwaombee wenye mamlaka, naamini haikumaanisha tuwaombee matatizo yao binafsi, au shida zao binafsi, au mahitaji yao binafsi…ingawa hakuna ubaya wowote kufanya hivyo, sio dhambi ni vizuri pia kufanya hivyo, lakini naamini biblia haikumaanisha hivyo…bali ilimaanisha tuziombee zile nafasi walizopo kwamba zitumike katika njia inayopasa ili sisi tuishi kwa amani…

Kwamfano nafasi ya Uraisi inapaswa iombewe kwamba kila mipango yoyote isiyofaa ya yule adui isipate nafasi katika kiti kile, kwamba kwa yeyote aliyekikalia kile kiti iwe ni mwanamke au mwanamume, Bwana akafunike fikra zake atawale kulingana na mapenzi ya Mungu shetani asipate nafasi.

Kadhalika na katika nafasi zote iwe ni za wizara kwamfano wizara za fedha,afya, maliasili n.k au vinginevyo..zote hizo zinatakiwa ziombewe, kwamba shetani asipenyeze vitu vyake katika hizo nafasi zikatumika vibaya…kwasababu endapo zisipoombewa na shetani akapata nafasi basi matatizo yatatukuta sote, hususani kwetu sisi tunaoamini, kwasababu sisi ndio tageti kubwa ya shetani..

Hebu jaribu kufikiria, leo vita vitokee, mabomu yakapigwa huku na kule, barabara zikaharibika, miundo mbinu ya maji na umeme ikaharibika…unadhani na wewe mtu wa Mungu utaacha kuathirika kwa namna moja au nyingine?..utaathirika tu!

Kwasababu na wewe unahitaji barabara kwenda kazini kwako au kwenda kuhubiri, unahitaji umeme kuendesha biashara yako kama unayo, unahitaji maji kwa ajili ya kuishi, n.k sasa hivyo vyote vimeharibika unadhani na wewe utaacha kupata shida hata kama unamtumainia Mungu?..Ni kweli Bwana anaweza akakuhifadhi wewe kupona lakini kwa shida sana! Katika wengi watakaokufa kwa matatizo hayo unaweza usiwe mmoja wao kwasababu unamcha Mungu, lakini utakuwa katika dhiki nyingi…Nuhu alisalimika kwenye gharika lakini maisha ndani ya gharika hayakuwa ya raha kabisa..kukaa miezi mitano kwenye boti, ndani giza, hakuna kutembe tembea..wewe ni kitandani, kwenye kiti na kusikia sauti za wanyama tu, na watu wale wale uliowazoea! Yalikuwa ni maisha ya shida ingawa kasalimika.

Unakumbuka wakati wa Wana wa Israeli kuchukuliwa utumwani Babiloni? Kitu gani kilitokea?.. kabla ya kuchukuliwa mji ulizungukwa na majeshi ya Babeli kwa muda wa miaka 2, hakuna kutoka wala kuingia,chakula chote ndani ya mji kikaisha, njaa ikawa kali mno, na hiyo njaa iliwaathiri hata watu wa Mungu waliokuwemo ndani ya huo mji.

Mfano Nabii Yeremia alikuwepo ndani ya huo mji! Kuna wakati walimshika wakawa wanampa mkate mmoja tu kwa siku!…tengeneza picha Nabii wa Mungu, ambaye Mungu alimwambia “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.Yeremia 1:5”..Nabii wa mataifa!! Lakini leo hii anashindia mkate mmoja tu kwa siku, kwa kipindi kirefu.

Na tunaona baada ya miaka miwili kuisha, watu wakazidiwa njaa ndani ya mji ikabidi mfalme atafute njia ya kutoroka, siku hiyo hiyo ndio majeshi ya Babiloni yalipoingia ndani ya mji na kuwaua watu kama kuku..walikufa wayahudi wengi sana..na kibaya zaidi wachache waliosalia walichukuliwa mateka mpaka Babeli..Na Nabii Ezekieli alikuwa ni miongoni mwa waliochukuliwa mateka pamoja na Nabii Danieli…

Hebu fikiria Nabii wa Mungu Ezekieli aliyeonyeshwa na Mungu maono makubwa kama yale, na yeye anakuwa ni miongoni mwa mateka wale! Waliofungwa minyororo na kupelekwa utumwani! Na Danieli naye vivyo hivyo..sasa kama manabii wa Mungu yaliwakuta hayo pale nchi yao ilipovurugika unadhani yataachaje kutukuta mimi na wewe endapo nchi tunazoishi zitachafuka?!!…Ni wazi kuwa tutateseka tu! Hakuna namna! Inaweza isiwe kwa kiwango kikubwa kama watu wasiomjua Mungu, lakini tutateseka tu!

Ndio maana Paulo anasema…

“1 Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;

2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu”.

Unaona hapo! Nia na madhumuni ni ili tuishi maisha ya Amani na Utulivu…Tusipoishi kwa amani hata Injili tutaihubiri kwa tabu, kama hakuna utulivu hata raha ya kuishi hakuna.

Biblia inatabiri, amani ya dunia kuvurugika, hiyo ni lazima itokee, lakini sio kabla ya unyakuo kutokea! Baada ya unyakuo kupita ndio mambo yote ya ulimwengu yataharibika, itakuja dhiki kuu juu ya nchi ambayo haijawahi kutokea mfano wake,lakini kabla ya unyakuo mambo hayo hayatatokea..utatokea utungu tu! Lakini sio uhalisia wa mambo yenyewe, kutatokea matetesi ya vita lakini sio vita vyenyewe..kama tunavyoona sasa, kuna matetesi ya vita mahali na mahali, hiyo ni kuonyesha kuwa tunaishi katika siku za kumalizia.

Kwahiyo ni wajibu wetu kuombea nafasi zote za uongozi, ili shetani asipate nafasi, na ili tuishi kwa amani katika hichi kipindi cha kumalizia, Na kumbuka shetani anapojaribu kushambulia hizi nafasi lengo lake kubwa si kuiletea dunia dhiki!! Hapana bali lengo lake kubwa ni kuwaletea Wakristo dhiki!..ndio maana Paulo anasema “ili tuishi kwa amani na utulivu”..sio “ili dunia iishi kwa amani” bali ili sisi (tulioamini-wakristo) tuishi kwa amani na utulivu. shetani siku zote hatafuti kuwatesa walio wake, bali wasio wake, anawawinda wakristo kuliko kitu chochote kile! Anawachukia kuliko!..

kwahiyo atatafuta kila njia ya kuwaangamiza, na njia mojawapo ndio hiyo kuvuruga ngazi za juu za mamlaka…utasikia leo, sheria imetoka hakuna kuhubiri mabarabarani, wala kwenye mabasi, unadhani hilo ni jambo la kawaida kwa kiongozi kusema hivyo kama sio roho ya ibilisi nyuma yake inamwendesha?. kesho utasikia hakuna ruhusa ya kujenga kanisa,..baada ya siku kadhaa utasikia mswada bungeni hakuna ruhusa ya kuhubiri kama hujapitia chuo Fulani cha biblia n.k hiyo yote ni mipango ya ibilisi kutumia ngazi za juu za utawala kupunguza nguvu za wakristo, na Injili ya Mungu kusonga mbele. Ndio maana dua na sala ni muhimu sana juu ya nafasi hizo ili shetani asipate nafasi.

Kwahiyo kila unaposali mtu wa Mungu, usisahau kuziombea hizi ngazi za utawala, kuanzia ngazi ya Uraisi mpaka ngazi ya mtendaji wa kata, mpaka ya balozi wa nyumba kumi. Zote hizo Bwana azifunike, na azilinde dhidi ya mipango yote ya Yule adui.

1 Timotheo 2 : 1-4  “1 Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;

Bwana akubariki sana.

Tafadhali “share na wengine” Maran atha!

Mawasiliano: +255693036618 / +255789001312

Na pia kama utapenda masomo haya yawe yanakufikia kila siku kwa njia ya Whatsapp. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

Sadaka ya Amani ilikuwaje?

Sadaka ya kutikiswa ilikuwaje?

Birika ni nini?, na yale Matao matano katika birika la Bethzatha ni nini?.

FAIDA ZA MAOMBI.

MAOMBI YA YABESI.

RABONI!

KUNA AINA NGAPI  ZA MAOMBI?


Rudi Nyumbani

Print this post