MNARA WA BABELI

MNARA WA BABELI

Mnara wa Babeli unafunua nini katika roho?

Wanadamu walipofika mahali wakaona kuwa ipo sababu ya kumfikia Mungu., maisha hayawezi kuwa na maana yoyote kama hawataweza kumfikia huyu mwanzilishi wa haya maisha..Hivyo kwa kuwa ile kiu ilikuwa ni kubwa ndani yao, wakabuni njia nyingi nyingi tofauti tofauti za kumfikia yeye,. lakini wakati ulifika wakagundua kuwa tusipokuwa na umoja,. tusipokuwa na usemi mmoja hatuwezi kufanya hivyo.

Ndipo wakaona ni vema wakubaliane kwa nia moja kutatua tatizo hilo. Na ndipo wakaamua kwenda kutafuta nchi tambarare huko Babeli na kuanza kutengeneza mnara mkuu ambao kwa huo walidhamiria kwa njia yoyote ile kumfikia Mungu…

Lakini Mungu aliliona hilo na kuona jinsi njia za wanadamu zitakapoishia ni pabaya pasipo kuwa na tumaini lolote, aliona sayansi zao za nyota na mbingu zitakapoishia, aliona unajimu wao utakapoishia, aliona uandisi wao utakapoishia n.k.

Pia tazama…

1 Jinsi Roho Mtakatifu anavyokuja juu ya mtu
2 Roho Mtakatifu ni nani?
3 Miamba yenye hatari
4 Jinsi unajisi unavyomgharimu mtu
5 Babeli ni nchi gani kwasasa?
6 Ashuru ni nchi gani kwa sasa?
7 Je ni lazima kushiriki Meza ya Bwana?
8 Unyenyekevu ni nini?
9 Nini tunajifunza kwa Theofilo mtukufu
10 Je Mungu huwa anajuta?

Hivyo kwa lugha zile zile na usemi ule mmoja waliokubaliana., katika huo huo Mungu aliwatawanya waende ulimwenguni kote kwasababu ile haikuwa njia sahihi Mungu aliyoikusudia watu wamfikie yeye. Na ndipo Mungu kuanzia wakati huo akaanza kuwatengenezea wanadamu njia iliyo sahihi ya kumfikia yeye, akaanza kuwajengea mazingira yote, tangu wakati wa Ibrahimu mpaka manabii, wote walitabiri juu ya njia hiyo pekee ambayo mwanadamu akiifuata basi moja kwa moja atawasiliana na Mungu, moja kwa moja atamwona Mungu, moja kwa moja atakula na Mungu katika meza moja.

Na ndipo ule wakati ulipofika Akamleta mwanawe wa pekee Bwana wetu Yesu Kristo, yeye ndiye MNARA WETU uliopachikwa pale YERUSALEMU, tofauti na ule wa BABELI..

Lugha moja na Usemi Mmoja

Na kama vile ule wa Babeli ulivyokuwa na lugha moja na usemi mmoja lakini Roho wa Mungu aliusambaratisha kwa kuchafua usemi wao na lugha zao ili wasielewane kwasababu sio NJIA Mungu aliyokuwa ameikusudia, vivyo hivyo mnara huu ulioweka YERUSALEMU, takribani Miaka 2000 iliyopita Roho wa Mungu aliuunganisha kwa lugha moja na usemi mmoja..

Na ndio maana katika ile siku ya Pentekoste, Roho wa Mungu alishuka kwa ishara ya Lugha, watu wakaanza kusema kwa lugha za mataifa mengine, kiashirio kuwa watu waje sasa waujenge huu MNARA MPYA BWANA ALIOUWEKA ILI WAWEZE KUMFIKIA MUNGU.

Kumbuka Babeli ya kwanza iliyoharibiwa, watu walianza kunena kwa lugha mbali mbali lakini hawakuelewana, waliishia kugombana na kutengana. lakini ile siku ya Pentekoste Roho aliposhuka wakristo walianza kunena kwa lugha mbali mbali lakini walielewana, hawakugombana wala kutengana, na ndio maana kuanzia hapo mitume, walianza kukaa pamoja kwa umoja na kwa nia moja. Na watoto wa Mungu kuanza kukusanywa pamoja duniani kote kuanzia Yerusalemu.

Kabla Bwana Yesu kuchukuliwa juu aliwaambia mitume wake maneno haya..

Matendo 1: 8 “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi”.

Ndugu yangu, hutaweza kumfikia Mungu kwa elimu ya dunia hii, sayansi hatakusaidia kuujua mwanzo wa dunia. Wala mwisho wake, haitakusaidia kujua umbali wa kutoka duniani mpaka mbinguni. Haitakusaidia kugundua makao ya roho za watu zilizokufa. Sasa kama ndio hivyo kwanini unaweka tumaini lako huko?. Kwanini unaujenga mnara wa Babeli ambao Mungu alishaulaani?..

Ushirikina haukupi tumaini la maisha baada ya kifo. Ushirikina haukupi amani, ushirikina haukupi kumwona Mungu kwa namna yoyote ile. Maisha ya dhambi hayakupi tumaini la umilele. Hutaweza kumfikia Mungu kwa namna hiyo, uzima wa milele haufikiki kwa njia moja wapo ya hizo bali ni Kristo tu peke yake. Ndiye MNARA WETU.

Madaktari hawawezi kukupa tiba ya kifo, usiudharau msalaba..Unamkataa yeye ambaye sio tu anaowezo wa kukuponya mwili wako bali pia mwenye uwezo wa kuifanya roho na mwili wako usife kabisa hata milele.

Mungu alishatupa ishara siku ile ya Pentekoste, kwa LUGHA zile, akisema NJOONI! MJENGE MPATE KUMFIKIA MUNGU..Huu ndio wakati ndugu,

Bwana alisema katika

Yohana 14: 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”..

Ufunuo 22: 17 “Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure. ”

Kumbuka ndugu Shetani naye anajenga mnara wake mwingine baada ya ule wa kwanza kuanguka. Na mnara huo unafanana sana na huu wa Bwana Yesu. Na anakusanya watu wake kutoka kila mahali duniani kote, kuwaleta katika dini moja, na imani moja, na usemi mmoja. Anakusanya dini zote na madhehebu yote na kuyaleta pamoja. Kuiunda ile chapa ya mnyama, ambapo itafika wakati mtu asipokuwa mshirika wa moja ya madhehebu yake hataweza kununua wala kuuza. Mtu asipokuwa mshirika wa huo mnara hutaweza kufanya lolote.

Kadhalika na mnara wa Yesu Kristo uliopo leo. Bwana anakusanya watu wake kutoka kila mahali, kama huna Roho Mtakatifu, hutaweza kuurithi ule uzima wa milele. Kama hujazaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho huwezi kumwona Mungu, wala kuwa na sehemu katika huo mnara.

Hivyo Usimwache leo ayapite maisha yako ili uweze kumfikia BABA.

Ubarikiwe.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Group la whatsapp

Tafadhali “share” kwa wengine ujumbe huu.


Mada Nyinginezo:

MTETEZI WAKO NI NANI?

BADO KITAMBO KIDOGO HAMNIONI

VIUNO VYENU VIWE VIMEFUNGWA NA TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA

JE! NI SAHIHI KWA MKRISTO KUOA/KUOLEWA NA MTU WA IMANI NYINGINE?

NINI MAANA YA ELOHIMU?


Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
2 years ago

Amen mwalim