Nini maana ya ELOHIMU?

Nini maana ya ELOHIMU?

JIBU: Kwanza kumbuka katika lugha ya kiswahili hilo neno ELOHIM, halionekani likitajwa katika biblia yetu kwasababu halipo katika lugha ya kiswahili. Hili ni neno la Kiebrania linalomaanisha Mungu, Kama tukisoma katika sura ya kwanza kabisa ya kitabu cha mwanzo biblia inasema “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi”..Hii ni katika lugha yetu ya kiswahili lakini kwa kiebrania inatafsiriwa hivi; Hapo mwanzo ELOHIM aliziumba mbingu na nchi.

Unaona tofauti hapo? na neno hili limetokea kwenye agano la kale mara 2500 katika biblia yao ya kiyahudi, lakini kwetu limetafsiriwa kama Mungu. Wakati mwingine hili neno ELOHIM limefupishwa kama “EL” ..Na ndio maana sehemu nyingine anajulikana kama EL’Shadai ikiwa na maana kuwa yeye ni “Mungu mwenyezi” kwa lugha yetu ya kiswahili (Mwanzo 17:1, kutoka 6:3 )..Sehemu nyingine anatajwa kama EL ROI, ikimaanisha “Mungu anayeona”(Mwanzo 16:13)..

Kadhalika sehemu nyingine anatajwa kama El Elyoni ikimaanisha “Mungu aliye juu”…Haya majina yote utayakuta katika nakala za biblia ya kiebrania. mahali pengine tuliomwona Bwana Yesu akilitamka hili jina kama lilivyo, pale alipokuwa msalabani tunaona alisema..EL’OI ELOI lama Sabakthani…tafsiri yake ni Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?.. 

Kwahiyo jina Elohimu ni Mungu ikimaanisha kwamba ni Mungu asiyekuwa na mwanzo, wala mwisho, Mungu mwenyezi, muweza yote, muhukumu, muumba, n.k. kwa ufupi hilo jina Elohimu linabeba tabia zote za Mungu. 

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

JINA LA MUNGU NI LIPI?

USILITAJE BURE JINA LA BWANA!

ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.

MUNGU MWENYE HAKI.

DAMU YA ZAKARI BIN BARAKIA.


 

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Yohana Thomas Said
Yohana Thomas Said
1 year ago

Barikiwa sana muandishi

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Barikia sana

Isaac jakait omuse
Isaac jakait omuse
1 year ago

Luka 17:20 -26 tasiri