SWALI: Biblia inapowataja ‘waibao watu ‘ sawasawa na 1Timotheo 1:10 humaanisha nini?
JIBU: Tusome;
1 Timotheo 1:8-10
[8]Lakini twajua ya kuwa sheria ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia iliyo halali; [9]akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji, [10]na wazinifu, na wafiraji, na WAIBAO WATU, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;
[8]Lakini twajua ya kuwa sheria ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia iliyo halali;
[9]akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,
[10]na wazinifu, na wafiraji, na WAIBAO WATU, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;
Tangu zamani dhambi ya wizi, haikuwa tu katika vitu na mali, bali ilikuwa hata katika watu. Ndio kilele cha juu kabisa cha wizi.
Wizi huu ulikuwa na malengo mbalimbali mojawapo ilikuwa ni kuwapeleka vitani, lakini pia kuwauza kama watumwa mfano katika biblia utamwona Yusufu (Soma Mwanzo 40:14-15). Na kama tunavyofahamu pia katika historia bara la Afrika lilikumbwa na tatizo hili, katika karne ya 17, waafrika wengi waliibiwa, na kuuza katika mabara ya ulaya.
Lakini kwa nyakati hizi wizi huu, umekuwa mbaya zaidi, kwasababu watu hawaibi tena watu kwa lengo la kuwatumikisha, bali kwa lengo la kuwafanyisha biashara ya kikahaba, wengine kuwaua ili wachukue viungo vyao kwa kazi za kishirikina, wengine wauze viungo vyao vya ndani kama vile figo, ili wapate fedha.
Jambo ambalo ni baya sana, ndio maana kwenye maandiko katika enzi za agano la kale adhabu ya wizi wa watu haikuwa ndogo bali kifo.
Kumbukumbu la Torati 24:7
[7]Mtu akionekana anamwiba nduguze mmojawapo katika wana wa Israeli, akamfanya kama mtumwa, au kumwuza; na afe mwivi huyo; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.
Lakini sisi katika agano jipya, hatuna ruhusa ya kuua watu wa namna hiyo, isipokuwa tuonapo vitendo kama hivyo vikitokea ni ripoti katika vyombo vya dola, hapo utaisaidia jamii, kudhibiti uovu kama huo Lakini pia kumwomba Mungu, aiondoe roho hii chafu isiwepo katikati ya jamii zetu, ili kuiponya kuiponya jamii.
Na Mungu atakubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea. Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
ALIJARIBIWA SAWASAWA NA SISI KATIKA MAMBO YOTE.
Je! Malaika wanazaliana?
USIZISHIRIKI DHAMBI ZA WATU WENGINE.
Mikono iliyotakata ni mikono ya namna gani? (1Timotheo 2:8).
Rudi Nyumbani
Print this post