Swali: Kulikuwa na ubaya gani wa Adamu na Hawa kula matunda ya mti wa Uzima, ili wapate tena uzima wa milele baada ya kuupoteza? (Mwanzo 3:22-24).
Jibu: Turejee mistari hiyo..
Mwanzo 3:22 “Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, AKALA, AKAISHI MILELE; 23 kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa”.
Mwanzo 3:22 “Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, AKALA, AKAISHI MILELE;
23 kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa”.
Sababu pekee ya Bwana MUNGU kuwazuia wazazi wetu wa kwanza (Adamu na Hawa) kula yale matunda ya Mti wa Uzima, si kwamba Mungu alikuwa hataki waishi milele!. La!.. kinyume chake ni mpango wake mkamilifu wa Mungu kwamba mwadamu aishi milele.
Tito 1:2 “katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele”
Soma pia 1Yohana 2:25 utaona jambo hilo hilo…
Lakini kwasababu tayari mwanadamu alikuwa ameshaiingiza dhambi ndani yake na katika kizazi chake, hivyo asingeweza kuishi milele katika dhambi, hivyo ni lazima dhambi iondoke kwanza ndani yake ndipo aishi milele, kwasababu kama akiishi milele na dhambi imetawala maisha yao, ni uharibifu mkubwa utaendelea na maisha yatakuwa nje na mpango wa Mungu, kwasababu yeye Mungu ni mkamilifu, hivyo kanuni ya maisha ya milele, ni sharti yasiwe na dhambi.
Kwahiyo BWANA MUNGU akaweka mpango kwanza wa kuiondoa dhambi ndani ya mtu, na mzizi wake, kisha yule mtu apate tena uzima wa milele.
Na mpango wa Mungu wa kuondoa dhambi ndani ya Mtu na kumrejeshea Uzima wa milele, ameushona ndani ya Mwanae YESU KRISTO, kwamba kwa kupitia njia ya kumwamini yeye, na kutubu basi tunaoshwa dhambi zetu na kupata uzima wa milele.
Warumi 5:21 “ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu”. 17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye”.
Warumi 5:21 “ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu”.
17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye”.
Hivyo kamwe hatuwezi kupata uzima wa milele, tukiwa katika dhambi..ni lazima kutubu kwanza na kumwamini Bwana YESU ndipo tupate uzima wa milele.
Na hiyo ndio sababu ya Bwana MUNGU kuifunga ile njia ya MTI WA UZIMA pale Edeni, ilikuwa ni sharti kwanza ADAMU na HAWA watakaswe ndambi zao kwa damu ya Mwanakondoo… Na majira yalipofika Mungu alimtuma mwanae ili afe kwaajili ya wote walio hai, na waliokwisha kutangulia, waliokufa katika haki, ili kwamba wote tutakaswe na kupata uzima wa milele.
Na hili ni la kujua siku zote, kwamba hakuna uzima wa milele kwa mwingine yeyote Zaidi ya YESU KRISTO.
Yohana 3:35 “Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake. 36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia”.
Yohana 3:35 “Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake.
36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia”.
Mistari ifuatayo inazungumzia uzima wa milele ndani ya YESU KRISTO (1Yohana 5:11-13, Yohana 3:16, Yohana 5:24, Yohana 6:54, Yohana 12:50, Yohana 17:2, na Warumi 6:23) .
Je umempokea BWANA YESU?… kama bado unangoja nini?..Fahamu kuwa hizi ni siku za mwisho, majira yameenda sana na ule mwisho umekaribia.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
NAO WALIOKUWA WAMEKUSUDIWA UZIMA WA MILELE WAKAAMINI.
TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.
INJILI YA MILELE NI IPI KATIKA BIBLIA?
MJUE SANA YESU KRISTO.
NGUVU YA UPENDO WA KRISTO.
Rudi Nyumbani
Print this post
SWALI: Nini maana ya Waefeso 6:24, pale inaposema “katika hali ya kutoharibika”?
[24]Neema na iwe pamoja na wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo katika hali ya kutokuharibika.
JIBU: Mtume Paulo alipokuwa anahitimisha ujumbe wa waraka wake kwa waefeso, alimalizia kwa kuwatamkia neno la heri watu watu wale akiwaambia ‘NEEMA ikae pamoja nao.
Lakini tunaona hapo hakukusudia tamko hilo kwa watu wote, bali anasema ikae kwa wale wampendao Bwana, lakini bado sio tu kwa wampendao Bwana.. Bali wampendao katika “hali ya kutokuharibika”.
Yaani kwa ufupi upendo usio poa.. Ndio upendo usio haribika.
Ndio ule unaozungumziwa kwenye 1Wakoritho 13. Kwamba hustahimili yote, huvumilia yote, huamini yote, haupungui Neno wakati wowote.
Ni kuonyesha kuwa Bwana wetu Yesu Kristo anastahili kupendwa daima, zaidi ya vitu vyote, kwasababu ya upendo wake mkuu aliotuonyesha sisi wa kuacha vyote mbinguni kwa ajili yetu, ili tukombolewe. Na kwa rehema zake akatupa na vipawa kabisa, na uwezo wa kuitwa wana wa Mungu, kwa nguvu za Roho wake Mtakatifu aliyetupa . Hakika anastahili kupendwa sana bila ukomo.
Zingatia: Waraka huu sio wa waefeso tu, bali ni wetu pia sote tumeandikiwa. Hivyo tutaongezewa neema ikiwa tutampenda Bwana wetu Yesu Kristo kwa upendo usio haribika. Sio njaa itufanye tumwache, au ufukara, au mke, au kazi, au uzuri, au ubaya, au ndugu, au mali, au afya, au ugonjwa.. au kitu chochote, Bali kila wakati sisi shauku yetu kwa Kristo iwe ni ile ile. Kuomba ni kule-kule, kumtafuta Mungu ni kule-kule. Amen
Neema ya Bwana iwe nasi.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
JE! SISI KAMA WAKRISTO NI DHAMBI KUSHEHEREKEA KRISMASI?.
TUNAHESABIWA HAKI BURE KWA NJIA YA IMANI.
Lalama kwa uhai wa watoto wako wachanga wazimiao kwa njaa(Maombolezo 2:19)
Kwanini Mungu akuumbe hivyo ulivyo? Kwanini asingeweka pembe kichwani kwako, au kwanini asingekuwekea vilemba vya nyama kama vile vya kuku kichwani, au antena mbili kama zile za konokono au mdudu, bali amekuwekea nywele kichwani pako.
Sauti ya Mungu ipo katika maumbile yetu. Sisi kujikuta hivi tulivyo sio kwamba, ndio umbile bora zaidi ya yote Mungu aliloona linamfaa mtu, hapana, tungeweza kuumbwa vizuri zaidi hata ya mwonekano huo tulionao, lakini tumebuniwa hivi, kwa kusudi la kipekee ambalo tunapaswa tulijue, na sio kwa kusudi la urembo.
Kwamfano usipoweza kuelewa utendaji kazi wa mwili wako jinsi viungo vinavyoshirikiana huwezi kuelewa jinsi kanisa la Kristo linavyopaswa kufanya kazi likutanikapo, kwasababu sisi tunaitwa viungo mbalimbali ndani ya mwili wa Kristo.Umeona? Bwana akasema kiungo kimoja kikiumia, vyote vimeumia.
Hivyo tumeumbwa, kimalengo sio kimwonekano bora au kiuzuri,. Ni sawa na mtu aulizwe kati ya jiko, na maua kipi kina umuhimu zaidi kuwepo ndani mwako. Ni wazi kuwa atasema jiko,kwasababu litamsaidia kupika. Hakulichagua kwasababu lina mwonekano bora, lakini kwasababu lina matumizi muhimu zaidi ya vingine.
Vivyo hivyo na wewe ujitazamapo mwili wako, usijitazame kiuzuri kuliko viumbe vingine, au wanadamu wenzako, bali fikiria tu katika picha ya matumizi ya kila kiungo ulichopewa, kinakufundisha nini kuhusu muumba wako au kinatimiza kusudi gani kwa Mungu wako. Hilo ndio lengo hasaa la wewe kubuniwa hivyo ulivyo.
Leo tutaanza na NYWELE, kisha wakati mwingine tutatazama na viungo vingine;
Utazamapo nywele zako Bwana anataka ujue yafuatayo;
Mathayo 10:30 lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. 31 Msiogope basi; bora ninyi kuliko mashomoro wengi
Ni kawaida kudhani kuwa Mungu hathamini, au hajui kila kitu, au anasahau sahau. Lakini sivyo, ukimfuata Mungu, vitu vyako vyote vinavyotoka na kuingia vipo kimahesabu, hakuna kitu kinachotokea kwa ghafla tu, bila yeye kujua au kuruhusu, Hivyo mashaka yakija, kumbuka nywele zako zilivyo nyingi lakini zimehesabiwa, vivyo hivyo mambo yako yote yamehesabiwa.
Zaburi 69:4 Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua
Jinsi nywele zako zilivyo nyingi, maadui nao vivyo hivyo. Na maadui zetu sio wanadamu bali ni mapepo ambayo mara nyingine huweza pia yavaa wanadamu, kutudhuru. Hivyo usiwe mtu wa kunung’unika au kulamimika, ujue kila mwanadamu yupo vitani. Kama Bwana wetu Yesu Kristo hakuwa na dhambi hata mmoja lakini alikuwa na jopo la maadui kwanini wewe usiwe nao. Hivyo kuwashinda ni kuwa mwombaji daima, na kutembea katika njia za Bwana sikuzote. Ukikumbuka kuwa maadui ni jambo la kawaida, kama tu nywele zako zilipo hapo kichwani.
Mathayo 5:36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
Wakati mwingine, tunajiaminisha na kujihakikishia mambo na kuweka na viapo juu yake kana kwamba mambo yote yapo ndani ya uwezo wetu. Kauli kama, “leo nife,kama sitakupa hiyo fedha” au “Mungu anipige hapa hapa kama ninalokuambia ni uongo” Kauli kama hizi, za kuongezea hakikisho lingine juu, hazitokani na Mungu, maneno yetu tumeambiwa yawe ndio ndio, au sio sio, zaidi ya hapo yanatokana na Yule mwovu. Kwahiyo popote unapojiona unakaribia kuzidi mipaka kumbuka hizo nywele zilizo juu yako hujawahi kuzifanya ziwe hivyo ulivyo, Bwana ndiye azibadilishaye, hivyo jiwekee mipaka.
Nywele zako hufunua nguvu zako za rohoni. Wanadhiri wote wa Mungu hawakuruhusiwa kukatwa nywele, Samsoni alipewa nguvu, kwa agano la kutokatwa nywele, kufunua kuwa watakatifu wote nywele zao za rohoni ndio nguvu zao. Lakini unapoacha mpango wa Mungu adui anazikata, kama ilivyokuwa kwa Samsoni. Lakini baadaye alipojua amefanya makosa ziliota tena lakini katika gharama za ‘kutoona’ tena.
Waamuzi 16:22 Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake.
Tunza nguvu zako, usiruhusu kiwembe chochote cha mwovu kikupitie. Kwasababu hata zikirejea tena, hutakuwa kama hapo mwanzo.
Yeremia 7: 29 Zikate nywele zako, Ee Yerusalemu, uzitupe, Ukafanye maombolezo juu ya vilele vya milima; Kwa maana Bwana amekikataa na kukitupa Kizazi cha ghadhabu yake.
Zamani, kukatwa nywele zote kuisha kabisa ilikuwa ni ishara ya kuingia kwenye maombolezo, kwasababu utukufu wako umeuvua.
Maombolezo, kwa agano jipya sio kulia kama msiba, hapana bali kuingia kwenye maombi ya ndani kabisa, ya kuutafuta uso wa Mungu, ambayo huambatana na mifungo. Na leo, ni kila mara tunakwenda saluni kukata nywele zetu. Tujue Bwana anatutaka kama vile tukatavyo nywele zetu mara kwa mara ndivyo tukumbuke maombi ya kujimimina sana mbele zake.
Je! Somo hilo unajifunza mwilini mwako?
Je Bwana Yesu alikuwa na nywele ndefu?
ILI TUONEKANE WAKAMILIFU MBELE ZA MUNGU.
MWOMBENI BWANA WA MAVUNO APELEKE WATENDA KAZI.
Swali: Je kusujudu ni nini, na sisi wakristo tunayo amri ya kusujudu mbele za Mungu?
Kusujudu ni kitendo cha kuinama kwa kuelekeza kichwa chini kama ishara ya kuabudu au kutoa heshima kwa Mungu, mtu au shetani.. Zaidi ya kuinama tu, kusujudu pia kunaweza kuhusisha kupiga magoti na kuinamisha kichwa chini mpaka kufikia kugusa ardhi (soma 2Nyakati 7:3).
Maandiko yanatuonyesha mara kadha wa kadhaa watu wakimsujudia Mungu, na watu wakiwasujudia wanadamu na vile vile wakimsujudia shetani.
1.Watu kumsujudia Mungu
Mfano wa watu waliosujudu mbele za Mungu ni yule Mtumwa, Ibrahimu aliyemtuma kwenda kumtafutia mwanae Isaka, mke.. Maandiko yanasema alipokutana tu na Rebeka na kupata uhakika kuwa ndiye binti aliyechaguliwa na Bwana, basi yule mtumwa alisujudu mbele za Bwana mpaka chini..
Mwanzo 4:24 “Akasema, Mimi ni binti wa Bethueli mwana wa Milka, aliyemzalia Nahori. 25 Tena akamwambia, Kwetu kuna majani na malisho ya kutosha, na mahali pa kukaa wageni. 26 YULE MTU AKAINAMA AKAMSUJUDU BWANA. 27 Akasema, Na atukuzwe Bwana, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, ambaye hakuacha rehema zake na kweli yake kwa bwana wangu. Bwana akaniongoza mimi nami njiani hata nyumba ya nduguze bwana wangu”.
Mwanzo 4:24 “Akasema, Mimi ni binti wa Bethueli mwana wa Milka, aliyemzalia Nahori.
25 Tena akamwambia, Kwetu kuna majani na malisho ya kutosha, na mahali pa kukaa wageni.
26 YULE MTU AKAINAMA AKAMSUJUDU BWANA.
27 Akasema, Na atukuzwe Bwana, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, ambaye hakuacha rehema zake na kweli yake kwa bwana wangu. Bwana akaniongoza mimi nami njiani hata nyumba ya nduguze bwana wangu”.
Wengine waliosujudu mbele za Bwana katika biblia ni Musa (soma Kutoka 34:8-9) na Wana wa Israeli kipindi utukufu umeshuka juu ya Nyumba ya Mungu (2Nyakati 7:3)…pamoja na mwandishi Ezra na wenzake katika Nehemia 8:6.
2. Watu kusujudia Malaika.
Mfano wa watu waliowasujudia Malaika ni Yohana, Mtume wa Bwana YESU.
Ufunuo 22:8 “Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona nalianguka, ili NISUJUDU mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionyesha hayo. 9 Naye akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. MSUJUDIE MUNGU”.
Ufunuo 22:8 “Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona nalianguka, ili NISUJUDU mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionyesha hayo.
9 Naye akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. MSUJUDIE MUNGU”.
Mwingine aliyejaribu kumsujudia Malaika ni Yoshua (soma Yoshua 5:14)
3. Watu kuwasujudia wanadamu.
Mfano wa watu waliomsujudia mwanadamu katika biblia ni wale wana 11 wa Yakobo, ambao walisujudu mbele ya ndugu ya Yusufu, walipofika nchi ya Misri.
Mwanzo 43:27 “Akawaulizia hali yao, akasema, Je! Baba yenu, yule mzee mliyemnena, hajambo? Angali hai? 28 Wakasema, Mtumwa wako baba yetu hajambo, angali hai; WAKAINAMA, WAKASUJUDU”.
Mwanzo 43:27 “Akawaulizia hali yao, akasema, Je! Baba yenu, yule mzee mliyemnena, hajambo? Angali hai?
28 Wakasema, Mtumwa wako baba yetu hajambo, angali hai; WAKAINAMA, WAKASUJUDU”.
Mwingine aliyemsujudia mwanadamu ni Jemedari Yoabu (2Samweli 14:22), mwengine tena ni Arauna (2Samweli 24:20) na yule mwanamke wa Tekoa (2Samweli 14:4).., Hamani aliyesujudiwa na watu (Esta 3:2)
4. Watu kumsujudia shetani na jeshi lake.
Mfano wa watu waliomsujudia shetani na majeshi yake ni Wana wa Israeli, kipindi wanakatiza Moabu, ambapo waliisujudia miungu ya Moabu, na kufanya dhambi kubwa mbele za Mungu..
Hesabu 25: 1 “Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu; 2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, WAKAISUJUDU HIYO MIUNGU YAO. 3 Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli”.
Hesabu 25: 1 “Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu;
2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, WAKAISUJUDU HIYO MIUNGU YAO.
3 Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli”.
Mwingine aliyesujudia mashetani ni Mfalme Yeroboamu (1Wafalme 16:31)
Swali ni je! Watu waliozaliwa mara ya pili (wa agano jipya) ni sahihi KUSUJUDU??
Jibu ni NDIO!.. Lakini anayepaswa na kustahili kusujudiwa ni MUNGU PEKE YAKE!… Wengine waliosalia ambao ni wanadamu au malaika hatupaswi kuwasujudia hata kidogo.. Maandiko kwa kupitia kinywa cha Bwana wetu YESU KRISTO yanatufundisha hilo moja kwa moja..
Mathayo 4:8 “Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, 9 akamwambia, Haya yote nitakupa, UKIANGUKA KUNISUJUDIA. 10 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, MSUJUDIE BWANA MUNGU WAKO, UMWABUDU YEYE PEKE YAKE. 11 Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia”
Mathayo 4:8 “Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
9 akamwambia, Haya yote nitakupa, UKIANGUKA KUNISUJUDIA.
10 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, MSUJUDIE BWANA MUNGU WAKO, UMWABUDU YEYE PEKE YAKE.
11 Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia”
Hivyo anayestahili KUSUJUDIWA ni Mungu peke yake sawasawa na maandiko hayo..
Lakini pia kusujudu na kuabudu ni lazima kufanyike katika roho na kweli ndivyo biblia inavyotufundisha, Kusujudu (kwa kuanguka chini) kunafaa sana kwa maombi ya Rehema na Toba, vile vile kwafaa sana kwa maombi ya maombi ya kupeleka mahitaji, kwani ni ishara ya unyenyekevu na kujishusha mbele za Mungu.
Na kusujudu si kanuni ya maombi, kwamba kila maombi ni lazima yaambatane na kusujudu, na kwamba usiposujudu basi maombi yako hayatasikiwa wala kukubalika,… bali ni tendo linaloambatana na msukumo wa kiungu na mzigo wa Roho Mtakatifu ndani.
Bwana atusaidie.
FAIDA ZA MAOMBI.
UNAMFAHAMU MUNGU WA KWELI?
KWANINI MUNGU HAJIBU MAOMBI?
HUDUMA YA MALAIKA WATAKATIFU.
KUNA AINA NGAPI ZA MAOMBI?