Ni kwa namna gani Yesu ni Simba wa Yuda?

Ni kwa namna gani Yesu ni Simba wa Yuda?

Bwana Yesu amejulikana kwa majina mengi tofauti tofauti katika biblia, kuna sehemu katajwa kama Mwanakondoo (Yohana 1:29), sehemu nyingine kama nyota ya asubuhi, sehemu nyingine kama Mzao wa Daudi (ufunuo 22:16), sehemu nyingine kama Imanueli, sehemu nyingine kama Simba wa Yuda n.k.

Leo tutaangalia ni kwanini amejulikana kama Simba wa Yuda.

Bwana Yesu kama Simba wa Yuda ametajwa mara moja tu Katika biblia yote!. Na ametajwa hivyo ndani ya kitabu cha ufunuo.

Ufunuo wa Yohana 5:5 “Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba”.

Sasa ili tuelewe kwanini ni Simba?.

Hebu turudi tujikumbushe baraka za ambazo Yakobo aliwabarikia watoto wake wale 12.

Utaona kila mtoto alipewa maneno ya kinabii kwake yeye binafsi, na uzao wake wote utakaofuata baada yake..tunaweza kusoma baraka hizo katika kitabu cha Mwanzo 49.

Mwanzo 49:1 “Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho.

2 Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo,
Msikilizeni Israeli, baba yenu.

Sasa turuke mpaka mstari wa 8, tuone unabii wa Yuda mwana wa nne wa Yakobo..

8 Yuda, ndugu zako watakusifu,
Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia.

9 Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha?

10 Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.

Umeona hapo mstari wa 9 unasema “Yuda ni mwana Simba”..na tena anasema katika mstari wa 10… “Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda”.

Ikiwa na maana kuwa kuna mmoja atakayezaliwa katikati ya kabila la Yuda, ambaye atatawala kama Simba, na tena atakwa ni Mfalme. Na huyo si mwingine zaidi ya Bwana Yesu. Yakobo alimwona Bwana Yesu miaka mingi kabla ya kuja kwake ndani ya uzao wa mwanae Yuda, kama vile Balaamu alivyomwona Yesu ndani ya kusanyiko la Israeli..

Hesabu 24:17 “Namwona, lakini si sasa; Namtazama, lakini si karibu; Nyota itatokea katika Yakobo Na fimbo ya enzi itainuka katika Israeli; Nayo itazipiga-piga pembe za Moabu, Na kuwavunja-vunja wana wote wa ghasia.

18 Na Edomu itakuwa milki Seiri pia itakuwa milki, waliokuwa adui zake; Israeli watakapotenda kwa ushujaa.

19 Mwenye kutawala atakuja toka Yakobo, Atawaangamiza watakaobaki mjini”.

Ndio maana kwenye Ufunuo hapo anakuja kutajwa kama Simba wa kabila la Yuda.

Sasa kwanini awe simba na Dubu au Chui?

Ni kwasababu Simba ni jasiri, haogopi, tena ana nguvu na tena anajulikana kama Mfalme wa pori.

Na Bwana Yesu, maandiko yanasema atakuja kuitawala dunia kwa fimbo ya chuma,  hivyo kama vile simba alivyo mfalme wa pori, kadhalika na Bwana Yesu atakuja kutawala kama Simba baada ya unyakuo wa kanisa kupita.

Je umemwamini Yesu leo?.. Leo kaja kwetu kama Mwana-kondoo, mpole aendae machinjoni, tukikosa kwake tunaomba rehema na anatusamehewa kwasababu neema bado ipo.

Utafika wakati baada ya unyakuo wa kanisa kupita, kutakuwa hakuna tena rehema, huyu Yesu anayetuita sasa kwa sauti ya upole atageuka na kuwa Simba angurumaye..atawararua waovu wote katika ghadhabu ya Mungu mwenyezi, na katika vita vya Harmagedon na kuwatupa waovu wote katika ziwa la moto, mahali ambapo hakuna msamaha. Maandiko yanasema atakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya Mungu mwenyezi..

Ufunuo 19:11 “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.

12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.

13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.

15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.

16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana”.

Na unyakuo wa kanisa ni siku yoyote kuanzia sasa hivi. Mlango wa rehema utakuwa umefungwa.

Swali ni je!, umempokea Yesu? na kuishi maisha ya utakatifu?.

Kama bado hujampokea, basi ni vyema ukafanya hivyo sasahivi, kabla nyakati hizo za hatari hazijafika.. tubu sasa na ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina lake Yesu, upate ondoleo la dhambi (Matendo 2:38). Na Bwana atakurehemu na kukupa uzima wa milele.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Makanwa ni nini katika biblia? (Danieli 6:22)

Kwanini Bwana Yesu alitokea katika ukoo wa Yuda?

Bwana Yesu alikuwa kabila gani?

TOFAUTISHA KATI YA MAFUNDISHO YA YESU, NA YA WAANDISHI.

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments