Title March 2023

ATAANGAMIZWA NA KUTENGWA NA WATU WAKE.

Karibu tujifunze biblia.

Matendo 3:22 “ Kwa maana Musa kweli alisema ya kwamba, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye katika mambo yote atakayonena nanyi.

23 Na itakuwa ya kwamba kila mtu asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake”

Unabii huo unamhusu Bwana Yesu Kristo, lakini swali la Msingi hapa, je! Ni wakati gani ambao “watu wataangamizwa na kutengwa” kwa kutomsikiliza huyu Masihi…Kwasababu ni wengi leo hawamsikilizi wala kumtii lakini hawaangamizwi wala kutengwa na watu wao.

Hapo kuna mambo mawili ambayo yatatimia kwa pamoja.. 1) KUANGAMIZWA, na 2) KUTENGWA.

Haya ni mambo mawili ambayo yatatimia kwa wakati mmoja kwa wote ambao hawatamsikiliza Masihi.
Sasa swali, ni hili unabii huo utatimia lini wa watu kuangamizwa na kutengwa?

Tusome,

2Wathesalonike 1:7 “na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; WAKATI WA KUFUNULIWA KWAKE BWANA YESU kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake

8 katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu;

9 watakaoadhibiwa kwa MAANGAMIZI ya milele, KUTENGWA na uso wa Bwana na UTUKUFU WA NGUVU ZAKE;”

Umeona hapo?. Kumbe wote wasioitii injili, leo siku ya mwisho (ya kufunuliwa Bwana Yesu) wataangamizwa!, na sio tu kuangamizwa, bali pia “watatengwa na uso wa Mungu” na “kutengwa na utukufu wa nguvu zake”…Maana yake wataanza kwa kutengwa kutoka kwa ndugu zao (wakati wa kutenganishwa kondoo na mbuzi Mathayo 25:31-35) na pia watatengwa na vitu vyote Mungu alivyoviumba ikiwemo dunia na kila kitu…sawasawa na Mithali 2:21-22.

Mithali 2:21 “Maana wanyofu watakaa katika nchi, Na wakamilifu watadumu ndani yake.

22 Bali waovu watatengwa na nchi, Nao wafanyao hila watang’olewa”

Ni jambo baya sana kutengwa na uso wa Mungu na kuangamizwa!..
Wengi leo wanamkataa Yesu na kuikataa Injili wakidhani ipo njia nyingine ya kufika mbinguni.. Bwana Yesu yeye mwenyewe alisema kwa kinywa chake kuwa..

Yohana 14:6 “..Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”.
Hakuna njia nyingine ya kumfikisha mtu mbinguni isipokuwa njia ya Msalaba!.. Usidanganyike kwa vyovyote vile.

Mwisho wa dunia unakuja, Mpokee Yesu leo, Itii injili yake inayosema… usizini, usiibe, usivae mavazi ya nusu tupu, usivae mavazi yapasayo jinsia nyingine, usijichore mwili, usitukane n.k

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?

Ni kwa namna gani Kristo analitakasa kanisa kwa Maji katika Neno? (Waefeso 5:26)

Je Mungu ana njia ngapi za kuzungumza?

Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?

REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.

Rudi nyumbani

Print this post

Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza Naam, wanne walio na mwendo mzuri.

SWALI: Naomba kufahamu ni hekima gani tunaipata nyuma ya vifungu hivi, vinavyosema “Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri”. 


JIBU: Mithali 30:29 “Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri.  30 Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hajiepushi na aliye yote;  31 Jimbi aendaye tambo; na beberu; Na mfalme ambaye haasiki”. 

Swali la kujiuliza ni kwanini wameonekana wana mwendo mzuri na wa kupendeza, jibu ni kwasababu ya tabia yao ya ujasiri na kuamini kuwa wao ni wamiliki.

kwamfano Simba ni mfalme wa pori, kila kitu kilicho mbele yake anakiona ni chakula, hivyo hana uoga na lolote. Anamiliki wanyama wote , hata wale wanaoonekana ni wakubwa na wenye nguvu kuliko yeye. Wote wanamkimbia.

Anamtaja pia jimbi/jogoo, ambaye na yeye ni mfalme wa shamba, usemi wa “kutanua mbawa” umeanzia kwake. Yeye anaamini anaweza kumiliki mitetea yote na kundi lote la kuku. Watafiti wanasema kule kuwika kwa jogoo, sio bila sababu tu. Hapana, bali ni anatuma ujumbe kwa majogoo wengine wasimsogelee kwenye miliki yake na kutafiti kama yupo ambaye anamkaribia, ajiandae kwa mapambano. Tofauti na ndege wengine walio madume, hawana tabia za kujimilikisha kama Jogoo, au kupigana ili kumiliki shamba.

Anamtaja pia Beberu,(Mfalme wa zizi) katika kundi, beberu utamtambua  tu kwa tabia zake, hujiaminisha sana, muda wote hatulii, analimiliki kundi lote kana kwamba yeye ndio mchungaji-msaidizi (Zekaria 10:3). Katika Historia unabii wa  Aleksanda mkuu aliyetawala Ugiriki ya kale, ambaye aliteka ngome nyingi sana, kila alipopatamani alikwenda na akashinda alifananishwa na beberu katika maandiko Kutokana na Tabia zake hizo (Danieli  8:5). Hata sasa mataifa yanayotaka kumiliki mataifa mengine kwasababu ya nguvu zao za kijeshi, au kiuchumi au kisiasi, hujulikana kama mataifa ya kibeberu.

hiyo ni kufuatana na Tabia ya beberu ya kupenda kumiliki zizi.

Lakini wa mwisho anamtaja pia, Mfalme asiyeasika. Ambaye ni mtawala wa Nchi. Kama tunavyojua wafalme ndio viongozi wa taifa, humiliki vyote, na yoyote atakayekatiza mbele yake kujaribu kuuangusha ufalme wake, humuua. Mfalme ni zaidi ya raisi, Wafalme wengi waliteka ngome kwa vita, sio kwa kuchaguliwa, Ujasiri na misimamo yao huwamilikisha.

Ni hekima gani tunaipata?

Hivyo mwandishi wa mithali anajaribu kuonyesha , ujasiri na ushujaa ambao na sisi tunaweza kuupata endapo tutakuwa ndani ya Kristo. Bwana atatufanya tuwe na roho kama za wanyama hawa, mienendo yetu itakuwa bila WOGA sikuzote. Tutaishi kama watu wasio na mashaka kwa lolote. Hatutaogopa wanadamu, wala matatizo, wala wachawi, wala magonjwa, wala shida yoyote. Kwasababu tunajua uwezo wa kuyashinda hayo na kuyamiliki tunao mfano wa Simba na mfalme.

Bwana Yesu aliye mfalme wetu, anayemiliki sasa mbinguni na duniani, Simba wa Yuda, aliyashinda na sisi pia tutayashinda endapo tutakuwa ndani yake alisema hivyo.

Yohana 16:33  “…jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu”.

Je! Utapenda kumpa leo Yesu maisha yako? Ili aanze upya na wewe, akupe tumaini jipya la uzima wa milele? Na ujasiri wa kuishi hapa duniani bila woga?

Kama jibu ni ndio basi fuatiliza mwongozo huu, na Leo Leo utaupokea wokovu >> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!

NI NINI KITAKACHOTUFANYA TUPIGE MBIO BILA KUPUNGUZA MWENDO?

Biblia inamaana gani kusema “vipo sita, naam saba”?

Ni kwa namna gani Yesu ni Simba wa Yuda?

Je ni kweli Isaka alifarijika kwa kifo cha mamaye? (Mwanzo 24:67)

Kupwelewa maana yake nini? (Matendo 27:26).

YATAMBUE MAJIRA YA KUJILIWA KWAKO.

INAYOENDELEA SASA NI HUDUMA YA RUTHU.

Rudi nyumbani

Print this post

Kwanini jiwe la kusagia Mungu alikataza lisiwekwe rehani? (Kumbukumbu 24:6).

Jibu: Turejee,

Kumbukumbu 24:6 “Mtu awaye yote asitwae jiwe la kusagia, la juu wala la chini, kuwa rehani; kwani hivi ni kutwaa maisha ya mtu kuwa rehani”.

Jiwe la kusagia lilikuwa ni jiwe lililotumika katika kusagia nafaka enzi za zamani, na hata sasa katika baadhi ya jamii.. Lilikuwa ni jiwe kubwa ambapo nafaka kama ngano inawekwa juu yake, na kisha jiwe lingine dogo linawezwa juu yake na kusaga nafaka hiyo.

Lilikuwa pia ni jiwe ambalo linapatikana karibia katika kila nyumba.. ni kama vile leo, jiko ilivyo zana ya msingi karibia katika kila nyumba, hata yule maskini kabisa hawezi kukosa jiko, vile vile na hili jiwe lilikuwa ni zana ya msingi sana.

Sasa Mungu alikatakaza Jiwe hilo (liwe la juu au la chini) lisiwekwe rehani kwa vyovyote vile, Maana yake kama mtu kamkopesha maskini, hapaswi kukubali rehani iwe jiwe la kusagia, kwasababu endapo Yule maskini kashindwa kulipa mkopo ule, basi jiwe lile jiwe la kusagia litachukuliwa na kwenda kuuzwa ili deni lile lilipwe, na hivyo Yule maskini atabaki hana hilo jiwe, na hivyo atashindwa kusaga nafaka zake kwaajili ya chakula chake cha kila siku, hata nafaka zile chache ambazo atazipata katika shamba lake, atashindwa kuzisaga kama riziki, na hivyo anaweza kufa kwa njaa.

Lakini rehani ya vitu vingine kama vyombo, au mashaba iliruhusiwa, kwasababu mtu angeweza kuishi bila hivyo vitu,  lakini si bila jiwe hilo la kusagia.

Jambo hilo linatufunza nini?

Tunajifunza kuwa na huruma kwa watu wa hali ya chini, Ni vizuri kutoa mkopo lakini si kila mkopo ni lazima tupate rehani, mikopo mingine tunaweza kuitoa tu bila kumweka mtu rehani, (hususani kwa wale watu ambao ni hali ya chini sana kiuchumi), hiyo itaonyesha upendo wetu na wema kwa watu na hata kuwafanya wavutiwe na imani yetu na kumfuata Mungu wetu.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

JIWE LILILO HAI.

JIWE LA KUSAGIA

Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika..

Biblia inapotumia neno “Bila kazi ya mikono”, ina maana gani?

LIONDOE JIWE.

Rudi nyumbani

Print this post

Je ni kweli wanafunzi wa Yesu walikuwa hawanawi mikono?

Swali: Je ni kweli Bwana Yesu mwenyewe na wanafunzi wake walikuwa hanawi mikono kabla ya kula?..kulingana na Mathayo 15:2, na Luka 11:37

Jibu: Turejee,

Mathayo 15:1 “Ndipo Mafarisayo na waandishi toka Yerusalemu walipomwendea Yesu wakisema

2 Mbona wanafunzi wako huyahalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula”

Tusome tena, Luka 11:37..

Luka 11:37  “Alipokuwa akinena, Farisayo mmoja alimwita aje kwake ale chakula; akaingia, akaketi chakulani.

38  Farisayo huyo alipomwona, alistaajabu kwa sababu hakunawa kabla ya chakula”.

Je ni kweli Bwana Yesu na wanafunzi wake walikuwa hawanawi mikono kabla ya kula kulingana na mistari hiyo?

Jibu ni la! Bwana Yesu na wanafunzi wake walikuwa wananawa mikono kabla ya kula, huo ni usafi wa kawaida tu ambao kila mtu anao.

Hauwezi kutoka kushika mavumbi halafu uanze kula hivyo hivyo, labda uwe hauna akili timamu. Na Bwana pamoja na wanafunzi wake walikuwa ni watu wenye akili timamu, kama Bwana aliweza kuwaosha wanafunzi wake miguu kunawa mikono ni nini kwake? (Yohana 13:9-10).

Sasa swali kama Bwana na wanafunzi walikuwa wananawa mikono, kwanini Mafarisayo na Masadukayo waseme alikuwa hanawi?

Jibu ni kwamba Mafarisayo walikuwa wanafuata desturi za wazee, ambao kulingana na sheria ilikuwa kabla ya kula ni lazima mtu aoshe mikono mpaka kwenye kiwiko!.. Jambo ambao halikufanywa na wanafunzi wa Yesu wala Bwana Yesu mwenyewe… kwani Bwana na wanafunzi wake walikuwa wananawa tu kawaida, bila kufikisha maji kwenye viwiko.

Marko 7:2  “wakaona wengine katika wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najisi, yaani, isiyonawiwa.

3  Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao”

 Kama tu leo sisi tunavyonawa kabla ya kula, tukitaka kula huwa tunaosha tu viganja, lakini hatuoshi mkono mzima mpaka kwenye kiwiko, hivyo kulingana na desturi za wayahudi, mtu aliyeosha kiganja tu, bila kufika mpaka kwenye kiwiko, mtu huyo anahesabika kama bado hajanawa kabisa.

Hivyo kulingana na desturi hizo za kiyahudi, hata sisi tunaonawa sasa katika viganja tu, mbele zao tunahesabika kuwa  watu wanaokula bila kunawa!. Kwahiyo na Bwana pamoja na wanafunzi wake hawakuwa wananawa hadi kwenye viwiko, ndio maana wakashutumiwa vile, lakini walikuwa wananawa kama tu sisi tunavyonawa sasa.

Na ni kwasababu gani wanafunzi, hawakufuata desturi hizo za wazee za kunawa mpaka kwenye kiwiko?

Bwana Yesu alishatoa sababu kuwa kinachomwingia mtu hakiwezi kumtia unajisi bali kinachomtoka.

Mathayo 15:17  “Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?

18  Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.

19  Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano”

Hivyo na sisi tujihadhari sana na vitu tunavyovitoa katika vinywa vyetu kwasababu vinakuwa vinatoka mwilini, lakini zaidi sana tujitahidi kuwa wasafi kimwili, kwasababu hata Bwana Yesu alikuwa ananawa.

Bwana atubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

Biblia inapotumia neno “Bila kazi ya mikono”, ina maana gani?

Mikono iliyotakata ni mikono ya namna gani? (1Timotheo 2:8).

MPENDEZE MUNGU ZAIDI.

Biblia inasemaje kuhusu Kazi?

Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?

Rudi nyumbani

Print this post

Wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza

SWALI: Naomba kufahamu kwanini mafuta yaliendelea kutumika wakati Yesu tayari alikuwa ameshakuja duniani?

Marko 6:12 “ Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu. 13  Wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza”


JIBU: Ndio, Bwana Yesu alikuwa na kanuni nyingi za kuwaponya watu, kuna wakati alitamka tu na mtu akapokea uponyaje wake, utakumbuka habari ya Yule mtu aliyepooza alimwambia jitwike kitanda chako uende nyumbani(Marko 2:1-9),  vilevile kuna wakati alimgusa kwanza mgonjwa, kisha akaponywa, utamkumbuka Yule mkoma,aliyemfuata na kumpigia magoti kumwomba amponye, maandiko yanasema akamgusa na kusema nataka takasika,(Marko 1:40-42). Vilevile Kuna wakati alitoa tu agizo la kutekelezwa na katikati ya agizo hilo, mtu anapokea uponyaji wake, ile habari ya wale wakoma 10, inatuthibitishia hilo,(Luka 11:17-19) na kuna wakati alitumia visaidizi, kama udongo, mate, kama ishara ya nje, ya mtu Yule kupokea uponyaji wake. Ukisoma habari ya Yule mtu ambaye alikuwa kipofu tangu kuzaliwa utali hakiki hilo nalo (Yohana 9:6).

Na hapa ndivyo ilivyokuwa aliwapa maagizo wanafunzi wake, Pale alipowaita na kuwatuma kwenda kuhubiri injili Ukisoma kuanzia mstari wa 7, Utaona aliwapa maagizo hayo ya kutoa pepo, na bila shaka na ya kuwapaka mafuta wote waliokuwa wagonjwa kwa jina lake.

Lakini hiyo haikuwa staili, kwamba kila mahali watakapokwenda wawe na chupa za mafuta, au maji, au udongo au chochote.

Hata sasa, hatupaswi kudhani Bwana hawezi kutuagiza tutumie kitu chochote cha asili kama ishara ya nje ya kuachilia uponyaji wake. La! Tusifikiri hivyo, Lakini hilo halipaswi lifanyike mara zote, au kama staili, kama inavyofanywa sasa, watu hawahubiri tena Neno la Mungu, kinachopigiwa kampeni ni mafuta na maji ya upako. Lakini mitume hawakufanya hivyo, ukisoma mstari wa 12, hapo anasema “Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu”. Umeona, Walijua jukumu lako kubwa ni kuwahubiria kwanza watu habari za dhambi zao. Na katika huduma hayo mengine yanafuata tena kwa uongozo wa Roho Mtakatifu.

Ni jambo linalosikitisha sasa, Jina la Yesu halitumiwi tena, shetani ameingilia eneo hili na kulivuruga, watu wakidhani hiyo ndio kanuni ya Mungu iliyobora ya watu kupokea uponyaji,  wamemgeuza kama mganga wa kienyeji ambaye yeye kazi yake ni kutoa tu miti-shamba lakini hajali hali ya mtu ya kiroho.

Wengine wanakimbilia lile andiko la Yakobo ambalo linasema,

Yakobo 5:14  “Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.

15  Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa”

Wanasahau kuwa kilichotangulia ni kuombewa kwanza..kuungamanishwa dhambi zake, kupatanishwa na Mungu, kisha ndio mafuta yafuate, kwa jina(agizo) la Bwana.

Tukikariri kwamba wakati wote tunapaswa tutumie chumvi kisa Elisha aliagizwa atupe chumvi kwenye chemchemi ya maji ili aondoe mapooza(2Wafalme 2:19-22), basi tukariri pia kitendo cha kulala juu ya maiti, kila tunapowaombea wafu ili wafufuke, kwasababu Elisha naye alifanya kitendo kama hicho(2Wafalme 4:32-34). Unaona, tutaonekana ni wachawi.

Ndugu, kuwa makini na staili za kisasa za uponyaji, ni makundi machache sana yanayoongozwa na Bwana kutumia vitu hivi vya asili katika kufanya huduma, na utaona havitumiki mara kwa mara au kila siku bali kwa mwongozo Fulani. Lakini ukiona mahali hapo ndio imekuwa staili, kimbia hapo Mungu hayupo hiyo ni ibada ya sanamu. Wana wa Israeli walimkosea Mungu hivyo hivyo, baada ya kuona Mungu amewaponya kwa kuitazama  ile nyoka ya shaba, Musa aliyoagizwa aiunde kule jangwani,  wao wakadhani Mungu sikuzote yupo katika sanamu ile, matokeo yake ikawa walipofika katika nchi ya ahadi wengine waliendelea kuiunda, wakiitazama ili kutatuliwa matatizo yao, ikawa ni chukizo kubwa sana kwao. Mpaka baadaye sana mfalme Yosia alipokuja kuivunja vunja, ndipo hasira ya Mungu ikaisha.(2Wafalme 18:1-5)

Hivyo usigeuze kitu chochote kuwa sanamu yako, kukitegemea hicho angali maisha yako yapo mbali na dhambi utakumbana na laana badala ya  baraka. Tumepewa jina la YESU hilo ndio mwanzo na mwisho. Vinginevyo vyote tusubiri kwanza uongozo wa Roho Mtakatifu, kama haupo, tuache.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

NEHUSHTANI (NYOKA WA SHABA).

Ni kwa namna gani Kristo analitakasa kanisa kwa Maji katika Neno? (Waefeso 5:26)

NITAJUAJE KAMA MAOMBI YANGU YAMEFIKA (YAMEJITOSHELEZA)?

MAOMBI YA KUFUNGULIWA KIUCHUMI.

Je Kauli ya Mungu katika Warumi 11:4 na 1Wafalme 19:18 inajichanganya?

VITA BADO VINAENDELEA.

Rudi nyumbani

Print this post

Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme.

SWALI: Katika Mithali 30:24, tunaona wanatajwa wanyama wanne, wenye akili sana, lakini naomba kufahamu juu ya Yule wanne ambaye ni mjusi, Anaposema “Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme” Maana yake ni nini?


JIBU: Tusome,

Mithali 30:24 “Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana.  25 Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari.  26 Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.  27 Nzige hawana mfalme; Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi.  28 Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme”

Mjusi ni kiumbe ambaye ameumbiwa wepesi wa kupanda na kupita karibia sehemu zote yenye upenyo hata ule mdogo sana, uwezo wa mikono yake unamfanya aweze kusimama katika pembe yoyote ile ya ukuta, iwe ni ukuta wa juu, au wa pembeni, au wa chini, kwake vyote ni sawasawa, tofauti na wanyama wengine, ambapo pengine hutegemea kucha zao, ambazo hizo zinawasidia kupanda baadhi ya maeneo tu kama miti.

Na ndio maana utawakuta katika kila nyumba, hawazuiliki, hadi katika majumba ya wafalme biblia inasema hivyo utawakuta, mahali ambapo pana ulinzi, pana uangalizi, lakini wao wanaingia huko bila shida yoyote na kufanya makazi.

Ni kutufundisha nini katika hekima yake?

Ni kwamba, na sisi tunapokuwa ndani ya Kristo tunapewa mikono kama ya mjusi katika roho. Uwezo wa hali ya juu kupanda kila kuta ngumu, Hatuzuiliki kwa kitu chochote, popote tutakapotaka kupafikia tutapafikia, hata katika malango mazito ya ibilisi tutayamiliki.

Mwanzo 22:17 “katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; NA UZAO WAKO UTAMILIKI MLANGO WA ADUI ZAO;  18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu”

Je! Unataka uupokee uwezo huo? Kanuni ni moja tu, nayo  ni kumpa Kristo maisha yako, jikane nafsi yako, simama kikamilifu na Bwana, kisha utaona jinsi Mungu anavyokupigania kuangusha kuta na kumshinda ibilisi kiwepesi, ziwe za kimaisha au za kiroho. Kwako hakuna kikwazo kitakachokuwa kigumu kukishinda.

Bwana akubariki.

Je! Utapenda kufahamu hekima iliyo nyuma ya wale watatu waliosalia?

Fungua link hizi>>>

Wibara > Wibari ni nani?(Mithali 30:26)

Nzige >TUWATAFAKARI NZIGE WA JANGWANI.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

Nzige, Parare, madumadu na tunutu ni wadudu gani? (Yoeli 2:25)?

Biblia inapotumia neno “Bila kazi ya mikono”, ina maana gani?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 5

Mikono iliyotakata ni mikono ya namna gani? (1Timotheo 2:8)

Ayala, Paa na Kulungu ni wanyama gani?

Je! Lewiathani ni nani?

Lumbwi ni nini katika biblia?

tofauti iliyopo kati ya Imani na ujasiri, ni ipi?

Biblia inasemaje kuhusu Kazi?

Rudi nyumbani

Print this post

Ni kwa namna gani Kristo analitakasa kanisa kwa Maji katika Neno? (Waefeso 5:26)

Jibu: Turejee..

Waefeso 5:25  “……kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;

26  ili makusudi alitakase na KULISAFISHA KWA MAJI KATIKA NENO;

27  apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa”..

Siri ya kanisa kutakaswa kwa “Maji” inaanzia pale Msalabani, wakati Yule Askari anamchoma Bwana mkuki ubavuni, biblia inaonyesha kuwa palitoka “Maji na Damu”. Ikifunua kuwa Maji ni lazima yahusike katika hatua za utakaso wetu, ndipo damu ya Yesu iweze kututakasa kabisa. Utauliza tunazidi kulithibitisha vipi hilo? Tusome Matendo 2:37-38

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38  Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”

Umeona hapo?.. Anasema tubuni mkabatizwe, mpate ondoleo la dhambi.. kwahiyo kumbe ubatizo unahusika sana katika kusafika utu wa ndani.. maana yake utakaso wa  Damu, unategemea ubatizo wa Maji, ili  Roho Mtakatifu aweze kukaa ndani ya mtu.  

Vitu hivi vitatu vinaenda pamoja (DAMU, MAJI na ROHO Mtakatifu). Huwezi kukichukua kimoja na kukiacha kingine!… Wala kusema kimoja kina umuhimu kuliko kingine… Vyote hivi vitatu vina umuhimu na maandiko yanasema vinapatana katika UMOJA!

1Yohana 5:9  “Kisha wako watatu washuhudiao duniani], ROHO, NA MAJI, NA DAMU; na watatu hawa hupatana kwa habari moja”.

Hiyo ndio sababu pia kwanini tunapaswa tubatizwe!.. Wengi leo wanaupuuzia ubatizo wa maji wanasema hauna umuhimu sana, ubatizo wa Roho Mtakatifu ndio wa muhimu.. Pasipo kujua kuwa Roho, na Maji na Damu vinapatana katika Umoja, ndio maana Bwana Yesu alimwambia Nikodemo kuwa kama hatazaliwa kwa MAJI (maana yake kwa ubatizo wa maji) na kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu, hatauona ufalme wa mbinguni, na huko ndiko kuzaliwa mara ya pili.

Maana ya kuzaliwa mara ya pili ni kubatizwa katika maji na katika Roho Mtakatifu.

Yohana 3:4  “Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?

5  Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa MAJI NA KWA ROHO, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

6  Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.

7  Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili”.

Na ubatizo ulio sahihi ni ule wa maji Tele (Yohana 3:23) na kwa jina la Bwana Yesu (Matendo 2:38, Matendo 8:16, Matendo 10:48 na Matendo 19:5)

Bwana akubariki.

Ikiwa bado hujapata ubatizo sahihi, basi unaweza kuwasiliana nasi, tutakusaidia juu ya hilo, kwa Neema ya Bwana.

Shalom

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.

TOFAUTI YA UBATIZO WA YOHANA NA UBATIZO WA BWANA YESU

NUNUA MAJI YA UZIMA.

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

MAAGIZO YA BWANA YESU NI BORA KULIKO MAAGIZO YA DAKTARI

Rudi nyumbani

Print this post

BWANA ni mtu wa vita,  BWANA ndilo jina lake.(Kutoka 15:3)

SWALI: Naomba kufahamu maana ya huu mstari..Kwanini biblia imtaje Mungu kama mtu, angali maandiko yanasema yeye sio mtu.

Kutoka 15:3

[3]BWANA ni mtu wa vita,  BWANA ndilo jina lake.


JIBU: Neno hilo halimaanishi kuwa Mungu ni mtu, Bali biblia hutumia mifano halisi ya kibinadamu kuwasilisha picha Fulani Rohoni..

Kwamfano ukisoma andiko lingine linalopatikana katika Mithali 30:26, utaona mnyama anayeitwa Wibari anatajwa kama mtu..

Mithali 30:26

[26]Wibari ni watu dhaifu;  Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.

Tunafahamu kabisa wanyama hawa wibari(Pimbi) sio watu, isipokuwa kwa wingi wa akili zao, mwandishi anawafananisha na watu, Ni kwasababu gani? Ni Kwasababu ijapokuwa ni waoga, wadhaifu, wanawindwa na kila mnyama mkali..lakini hawajengi nyumba zao katika sehemu dhaifu kama kwenye viota, au kwenye mashimo, au vichaka, ambapo ni rahisi kuvamiwa au kuharibiwa na majanga, Bali wanaweka makazi Yao katika miamba mikubwa iliyojificha sana  Mahali ambapo ni ngumu adui kuwashambilia.. wanafananishwa na watu waliojenga maisha yao juu ya MWAMBA, pekee yaani Yesu Kristo

Mathayo 7:24  “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 25  mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba”

Hivyo tukirudi katika andiko hilo, anaposema “BWANA ni mtu wa vita”. Anajaribu kumfananisha Bwana na shujaa wa kivita, jemedari mwenye uzoefu mkubwa sana katika vita vikali, mfano wa Sauli, au Daudi, ambao walikuwa wanasimama mstari wa mbele katika vita, ili sisi tupate picha jinsi gani Mungu wetu alivyo mkuu sana, pale anapoitwa Bwana wa Majeshi, tumwelewe uweza wake wa kutupigania na kutusaidia kuangusha ngome za ibilisi jinsi ulivyomkubwa haijalishi zimekita mizizi kiasi gani.

Zaburi 24:8 “Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita”

Hivyo mstari huo hakumaanisha kuwa yeye ni mtu.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

Ufunuo 12 inaelezea vita vya wakati upi?

Kati ya Unyakuo,dhiki kuu, utawala wa miaka 1000 kipi kinaanza

NIMEAZIMIA KUWAKUSANYA MATAIFA. NIPATE KUWAMWAGIA GHADHABU YANGU

Nini maana ya ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi wala siku ya sabato?

VITA DHIDI YA MAADUI

Nini maana ya mhubiri 9:11? si wenye mbio washindao katika michezo?

NA WATU WOTE WALIKUWA WAKIAMKA MAPEMA, WAENDE HEKALUNI.

Shetani anaishi wapi, Je! Amefungwa au yupo kuzimu?

Rudi nyumbani

Print this post

Je ni kweli Isaka alifarijika kwa kifo cha mamaye? (Mwanzo 24:67).

Jibu: Tusome,

Mwanzo 24:67 “Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mamake”.

Andiko hilo halimaanishi kuwa Isaya alipendezwa na kifo cha mamaye Sara, na hivyo akapata faraja kwa kufa kwake, bali linamaanisha kinyume chake.

Ikumbukwe kuwa Isaka alikuwa ni mwana pekee wa Sara, na Isaka alimpenda sana mama yake, na siku mama yake alipokufa ni wazi kuwa alihuzunika kwa kipindi kirefu,  lakini sasa kipindi anampata Rebeka kama mke wake, ile huzuni ikapungua kwa kiasi kikubwa na akajihisi faraja kama tu ile aliyokuwa anaipata kutoka kwa mama yake.

Ni nini tunajifunza kutoka katika habari hiyo?.

Hapa tunajifunza jinsi mwanamke wa kiMungu anavyopaswa awe!..

Rebeka alikuwa ni mwanamke wa mfano wa kuigwa, kwani aliweza kuwa faraja kwa mume wake kiasi kwamba mume wake akasahau uchungu wote wa kufiwa na mamaye (Maana yake Rebeka alikuwa ni mke kwa Isaka na hapo hapo mama kwa Isaka, kumlea na kumtia moyo). Lakini leo hii wanawake wengi wanafanyika mishale kwa waume zao, na si faraja.

 Mama, dada, binti, msichana kabla ya kwenda kujifunza kwa akina Musa, Eliya, na Danieli, hebu kwanza tenga muda wa kujifunza juu ya wanawake hawa.. Kwasababu tabia ya Musa haitakusaidia sana katika uanawake wako zaidi ya akina Rebeka, au Sara au Mariamu au Ruthu..

Ukitaka kuwa mke bora na mama bora kajifunze kwa akina Hana, Debora, na Tabitha..ukitaka kuwa binti bora nenda kajifunze kwa mashujaa wote wa kike katika biblia kabla ya kuwakimbilia wanaume.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

MISTARI YA BIBLIA YA FARAJA.

Tofuati kati ya kifo na mauti ni ipi?

CHUKI ULIZO NAZO KWA MAADUI ZAKO, SIZO ALIZONAZO MUNGU JUU YAO.

KWANINI KRISTO AFE?

Nilikuwa naomba kujua utofauti kati ya DHAMBI, UOVU na KOSA kibiblia.asante!!

Rudi nyumbani

Print this post

USIRUHUSU INZI WATUE JUU YA ROHO YAKO.

Kibiblia mapepo yanafananishwa na inzi.

Inzi siku zote huvutiwa na mazingira ya aina mbili. Ya kwanza ni uchafu. Mahali palipo na uchafu hapakosi inzi, Na ndio maana Bwana baada ya kuhakikisha taifa la Misri linanuka uvundo, kwa harufu na uchafu wa wale vyura waliokufa, akawaanda na inzi waje juu yao ili wayafurahie mazingira yao. Ndio hapo utaona akawaleta wengi sana juu ya wamisri wakawa kero kubwa sana kwao.

Kutoka 8:24 “Bwana akafanya; wakaja wingi wa mainzi kwa uzito sana, wakaingia nyumbani mwa Farao, na katika nyumba za watumishi wake, tena katika nchi yote ya Misri; nayo nchi iliharibiwa kwa ajili ya wale mainzi”

Lakini sio hilo tu, watu wengi wanapuuzia wakidhani kuweka mazingira tu safi ndio kutawafukuza. Lakini pia inzi wanavutiwa na mazingira ya vidonda. Palipo na vidonda, utaona inzi wengi wanakusanyika kwenye eneo hilo.

Maana yake nini? Rohoni ukiwa na majeraha ambayo hayajafunikwa au kutibiwa, kunaweza kukusababishia kuvuta uwepo wa mapepo juu ya maisha yako, Unaweza kweli ukawa umejitahidi kuwa mbali na uchafu wa rohoni na mwilini, huibi,huzini,  unaishi maisha ya utakatifu, unatumika kanisani n.k.

Lakini kama una majeraha rohoni mwako,ambayo hayajatibiwa, bado mapepo yanaweza kupata nafasi ya kukusumbua. Una kinyongo cha muda mrefu na mwenzako, hujaachilia, hujasemehe, una uchungu, una wivu, una hasira zisizoachilika,. Fahamu kuwa hayo ni mazingira mazuri ya mapepo.

Ndio hapo utaona mkristo, ameokoka halafu analipuka mapepo, au anasumbuliwa na nguvu za uovu. Unajiuliza mbona huyu hana maisha machafu lakini yanamkuta haya? Sababu kubwa ni eneo hili. Ndio maana biblia inatuambia tulinde sana mioyo yetu kuliko vyote tuvilindavyo. Moyo hukaribisha roho za nje kiwepesi.

Tibu moyo wako, jiachie kwa Yesu, kubali kujikana nafsi, kubali kujishusha, kubali kusamehe, kubali hata kupoteza hicho ulichonacho, ili uiponye nafsi yako. Wivu, hasira, chuki, visitawale kabisa maisha yako. Viwe na adui wako.

Unaweza kusema hizi hali nitazishindaje? Jibu ni kuwa yote hayo yanawezekana endapo tu, utaishi maisha ya kumtazama Kristo, zaidi ya nafsi yako. Macho yako yakielekea kwa Yesu tu daima ukajifunza kwake, kidogo kidogo utaona  tabia za mwilini zinaanza kukuachia, unajifunza tabia za Yesu. Na yeye mwenyewe atakusaidia kukuponya kabisa kabisa kwasababu aliahidi hivyo katika Neno lake.

Hosea 6:1 “Njoni, tumrudie Bwana; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu.  2 Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake”.

Alisema pia..

Yeremia 30:17 Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye.

Jeraha zetu za rohoni ameahidi kuziponya. Na  Neno lake ni kweli halitanguki, limethibitishwa. Hivyo anza sasa kumkaribia Kristo na kujifunza kwake.(Mathayo 11:28-29)

Bwana akubariki.

Maombi yangu:

Ee, Baba tumejifunza jinsi adui yetu ibilisi anavyopata nafasi katika mioyo yetu pale tunaposhindwa kuzitibu jeraha zetu. Lakini leo tumetambua makosa yetu, nasi tunatubu mbele zako. Tunaomba utusamehe Baba yetu, Tumedhamiria kutoka katika mioyo yetu kukufuata wewe, na kujifunza kwako, Tunaomba ututibu majeraha yetu yote, yaliyodumu kwa muda mrefu na mfupi, ondoa hasira, ondoa vinyongo, kutokusamehe, wivu, ndani yetu. Nasi tunaamini tangu siku ya leo unatukamilisha.  Asante        Baba kwa kutusikia. Tunaomba tukishukuru katika jina la Yesu Kristo. Amen.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

Kwanini wakristo walipomuona Petro akigonga walisema “Ni malaika wake”?

SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.(Opens in a new browser tab)

SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.(Opens in a new browser tab)

KUOTA UNA MIMBA.(Opens in a new browser tab)

KATAA KUWA EUTIKO, WA KUSINZIA IBADANI.

Dina akatoka kuwaona binti za nchi. (Mwanzo 34:1)

Kama Kristo alizichukua dhambi zetu na kutusamehe kwanini kila siku tunatubu?

Rudi nyumbani

Print this post