Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?

Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?

JIBU: Andiko ambalo linaonyesha kutengwa kwa mwanamke anapotokwa na damu au anapokuwa katika siku zake ni hili;

Mambo ya Walawi 15:19-33

[19]Mwanamke ye yote, kama anatokwa na kitu, na kitu chake alichokuwa nacho mwilini mwake ni damu, ataketi katika kutengwa kwake muda wa siku saba; na mtu ye yote atakayemgusa atakuwa najisi hata jioni.

[20]Na kitu cho chote akilaliacho katika kutengwa kwake kitakuwa najisi; na kila kitu ambacho akiketia kitakuwa najisi.

[21]Mtu ye yote atakayekigusa kitanda chake huyo mwanamke atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.

[22]Mtu ye yote atakayekigusa cho chote ambacho huyo mwanamke amekiketia atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.

[23]Kwamba ni katika kitanda, au cho chote alichokikalia huyo mwanamke, atakapokigusa kitu hicho, atakuwa najisi hata jioni.

[24]Na mtu ye yote atakayelala na mwanamke na unajisi ukawa juu yake, atakuwa najisi muda wa siku saba; na kila kitanda alichokilalia kitakuwa najisi.

[25]Na mwanamke kama akitokwa na damu yake siku nyingi, nayo si katika majira ya kutengwa kwake, au kama anatoka damu kuzidi majira ya kutengwa kwake; siku hizo zote za kutoka damu ya unajisi wake, atakuwa kama alivyokuwa katika siku za kutengwa kwake; yeye yu najisi.

[26]Kila kitanda akilaliacho katika siku zote za kutoka damu kitakuwa kama kitanda cha kutengwa kwake; na kila kitu atakachokilalia kitakuwa najisi, kama unajisi wa kutengwa kwake.

[27]Na mtu ye yote atakayevigusa vitu vile atakuwa najisi, naye atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.

[28]Lakini huyo mwanamke kwamba ametakaswa na kule kutoka damu kwake, ndipo atakapojihesabia siku saba, na baadaye atakuwa safi.

[29]Siku ya nane atajipatia hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, na kumletea kuhani, mlangoni pa hema ya kukutania.

[30]Kuhani atamsongeza mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA, kwa ajili ya kutoka damu ya unajisi kwake.

[31]Ni hivi mtakavyowatenga wana wa Israeli na unajisi wao; ili wasife katika unajisi wao, hapo watakapoitia unajisi maskani yangu iliyo katikati yao.

[32]Hii ndiyo sheria ya mwenye kisonono, na ya mtu ambaye shahawa yake yamtoka, akawa na unajisi kwa hiyo;

[33]na ya mwanamke ambaye yu katika kutengwa kwake, na ya mtu ambaye ana kisonono, kama ni mtu mume, kama ni mtu mke, na ya huyo alalaye na mwanamke mwenye unajisi.

Kumbuka tunapaswa tujue kuwa si kila  jambo ambalo lilitendeka agano la kale, linatendeka vilevile hadi wakati wa agano jipya..mambo mengi yalikuwa ni kama kivuli tu kuwasilisha ujumbe wa rohoni kwa agano letu jipya…kwamfano kwenye suala la chakula utaona Bwana alikuja kurekebisha akasema kimwingiacho mtu hakimtii unajisi bali kumtokacho mtu kwasababu kinamtoka moyoni..hivyo chakula kwa namna yoyote hakiwezi kumfanya mtu amkosee Mungu kikilika kwa shukrani..lakini zamani kwamfano wanyama ambao walikuwa hawacheui(yaani hawawezi kurudisha tena chakula wanapokimeza) walijulikana kuwa ni najisi ikifunulia kuwa kwasasa rohoni wapo watu najisi ambao hawana tabia ya kucheua chakula cha kiroho wanacholishwa..yaani hawana muda wa kuyatafakari ya nyuma waliyofundishwa au waliyofanyiwa na Mungu,  Au kutendea kazi yale waliofundishwa.

Vivyo hivyo na suala la wanawake katika siku zao kwa kawaida damu kama damu haina shida lakini jiulize kwanini hiyo inayotoka katika viungo vya uzazi ilionekana ina unajisi..Hiyo ni kufunua kuwa uchafu unazoalika kutokana na zinaa ni unajisi mkubwa sana kwa mtu.

 Na ndio maana biblia inasema na malazi yawe safi.. (Waebrania 13:4)

Tunapaswa tuitunze miili yetu mbali na uasherati

Lakini haimaanishi kuwa ukitokwa na damu, wewe tayari ni najisi hapana kwasababu lile ni tendo linalokuja lenyewe halipangwi na mwanamke. Hivyo halimtoki rohoni mpaka likamtia mtu unajisi..Mungu alitumia mfano ule tu kuonyesha jinsi mambo yatokayo kule yasivyofaa(katika uzinzi)… Kwahiyo mwanamke akitokwa na damu au asipotokwa na damu hakumzuii yeye kumwomba Mungu wake au kumtumikia madhabahuni pake..

Anachopaswa kufanya ni kujiweka tu katika mazingira ya usafi na uangalifu.

Bwana akubariki.

Mada nyinginezo:

MATARAJIO YA KILA MWANADAMU DUNIANI NI YAPI?

KUNA MAJIRA MUNGU ATAIVURUGA MIPANGO YETU.

UFUNUO: Mlango wa 17

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 9 (Kitabu cha Ayubu).

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

Amina

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Leave your message