KUNA MAJIRA MUNGU ATAIVURUGA MIPANGO YETU.

KUNA MAJIRA MUNGU ATAIVURUGA MIPANGO YETU.

Kuna mhubiri mmoja alisema Mungu havutiwi na ufanisi wetu kwake, bali anavutiwa na Imani yetu kwake, kwasababu biblia inasema.. …lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake (Habakuki 2:4).

Ni kweli kabisa, kwa lugha rahisi, unaweza kudhani unapokuwa fanisi muda wote katika kazi ya Mungu, au mambo yako yanapokwenda sawasawa wakati wote kwenye kazi yake ndicho kinachomvutia sana Mungu.. Lakini ni vizuri tujue tabia za Mungu wakati mwingine zinafanyaje kazi ili yatakapotukutana na hali fulani au jambo fulani  katika ukristo au utumishi tuwe na amani katika hicho.

Haijalishi utakuwa unampendeza Mungu kiasi gani, kuna wakati Mungu ataruhusu mipango yako ivurugike, ataruhusu ratiba zako ziingiliwe, ataruhusu uchelewe au uvutwe nyuma, haijalishi unabidii kiasi gani.. Sasa unapofikia hatua kama hiyo hupaswi kusema kwanini Mungu karuhusu hichi, wakati sioni sababu ya hivi vitu kutokea.. Hatua kama hiyo hupaswi kukata tamaa, au kuhuzunika, bali ujue Mungu anataka uishi kwa kumwamini yeye katika hali zote.

Jiulize ni kwanini wakati mwingine Mungu aliruhusu mtume Paulo, aingiliwe ratiba yake ya kuhubiri injili? Na kupelekwa vifungoni? Unadhani ni kwasababu alikuwa na dhambi, au alikuwa hafanyi kazi ya Mungu kwa bidii? .Pengine alikuwa na mipango mingi sana ya kwenda kuwahubiria watu wengi waliokuwa na shida na vifungo, lakini ghafla mipango yake inaharibiwa.. Lakini hilo halikumfanya mtume Paulo azire, bali alimwamini Mungu, na wakati ulifika alitolewa na akasonga mbele.

Kuna wakati Yeremia anatoka kutoa unabii tu, anajiandaa arudi zake mjini  kwake kupumzika, apokee na mapato yake, ghafla walinzi wa mji wanamkamata na kumsingizia vitu vya uongo, kuwa yeye anakwenda kuwasaliti, matokeo yake wakamkamata na kumrudisha mjini na kumtupa gerezani shimoni kwa siku nyingi, sio kwamba Mungu alishindwa kuzuia yasimpate hayo mtumishi wake mwaminifu, lakini Mungu alikuwa anataka aishi kwa kumwamini yeye.. na sio kwa ufanisi wake.(Soma Yeremia 37). Ipo mifano mingi sana kwenye biblia,

Kuna wakati, Kristo alitaka awe  faragha na wanafunzi wake tu wapumzike na awafundishe, lakini makutano wanamsonga, kiasi kwamba itabidi ahairishe muda wake, awahudumie hao..aliingiliwa mara nyingi,. wakati mwingine wanataka wajitenge wapate nafasi kidogo ya kula lakini wanaingiliwa.(Soma Marko 6:30-42) .Tujiulize na sisi je tunaweza kuruhusu kuingiliwa katika mambo yetu? ..Je! mpendwa anaweza kukufuata wakati ambapo upo buzy kwenye mambo yako ya muhimu, ukayaacha hayo ukamuhudumia?

Tunapokuwa wakristo lazima tuwe tayari kuingiliwa, au kuvurugwa ratiba zetu na Mungu mwenyewe.. Wakati mwingine Bwana alipokuwa safarini kwenda kuhubiri ghafla anatokea mtu anamwambia Bwana twende ukamponye binti yangu, yupo hatarini kufa, anaacha kwenda katika shughuli zake, anakwenda kumponya..

Hivyo kama wewe ni mtumishi wa Mungu, kuna wakati kila kitu kinaweza kwenda kombo, ukaona kama kazi yote uliyoifanya nyuma ni bure, wema wote uliouonyesha ni sawa na bure, jitihada yako yote kwa Mungu inaishia katika hasara, hilo lisikuvunje moyo, hata kwa Yusufu ilikuwa ni hivyo, uaminifu wake wote, kwenye nyumba ya Potifa, alidhania wakati wote kwake utakuwa ni wa kufanikiwa tu, lakini siku mambo yalipomgeukia,pengine alijiuliza maswali mengi sana, ambayo hata wewe leo hii unajiuliza, ni kwanini Mungu aruhusu..

Watu wanaweza kusema kama huyo Mungu wako anakuthamini mbona ameruhusu ukutwe na hayo.. Lakini hawajui kuwa Mungu havutiwi na ufanisi wetu, havutiwi na umahiri wetu kwake, anavutiwa na Imani yetu kwake.. Kwasababu ni kweli kama ingekuwa ni hivyo kamwe asingekaa aruhusu watu wake, wapande na kushuka, wapitie hiki, au kile, wafungwe au wazuiliwe kufanya jambo fulani,  hata asingeruhusu wakati mwingine waugue..

Lakini anayaruhusu ili imani yetu iwepo kwake, siku zote, na yeye jinsi alivyomwanifu, anapotupitisha huko huwa anatuandalia yaliyo bora zaidi, kwahiyo katika hayo unayoyapitia, ni lazima umwamini Mungu kuwa, yeye bado yupo na wewe na kwamba unapaswa usonge mbele.

Hivyo usichukizwe,  usife moyo pale Mungu anapoivuruga mipango yako, kwa ajili ya jina lake. Mwamini yeye, na sikuzote atakuimarisha daima.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

JIFUNZE KUTOA KATIKA HAZINA YAKO VITU VIPYA NA VYA KALE.

BWANA AYAGANGE NA MACHO YETU PIA.

Ayala, Paa na Kulungu ni wanyama gani?

CHUKIZO LA UHARIBIFU

MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
10 months ago

mungu azidi kuwapa uzima na baraka tele nilikuwa kipofu wa neno sasa naanza kuona mwanga mbele yangu mungu awanariki sana nawapenda.

Gerald anthony
Gerald anthony
1 year ago

Hakika nimejifunza mengi sana, na ni mambo ambayo ni ya kweli kabisa wala hakuna mahali palipo fundishwa kinyume na misingi sahihi ya biblia. Mungu akubariki sana na aendelee kukuzidisha zaidi na zaidi.