Je! Daudi hakuwa mtoto wa ndoa wa Yese? (Zab 51:5)

Je! Daudi hakuwa mtoto wa ndoa wa Yese? (Zab 51:5)

SWALI: Bwana asifiwe,ukisoma zaburi 51:5,Daudi ana sema mama yake alichukua mimba hatiani, Je kwa mistari hiyo ina maana hakuwa mtoto wa Ndoa wa Yese?


JIBU: Zaburi 51:5 inasema   “ Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani”.

Hatuwezi kutumia kifungu hicho kuhitimisha kuwa Daudi alikuwa ni mtoto wa mke kahaba. Japokuwa kweli kulingana na mazingira yaliyokuwa yanaendelea wakati ule Nabii Samweli anamwendea Yese baba yake Daudi na kumwambia awalete watoto wake wote ili amchague mfalme , na matokeo yake  akawaleta wote na kumwacha Daudi maporini achunge kondoo, inatupa maswali mengi yasiyo na majibu. Kuwa pengine Daudi alikuwa ni mtoto wa nje.

Lakini pamoja na hayo mstari huu bado, haumaanishi kuwa Daudi alizaliwa na mama kahaba.. Kwasababu ukiusoma vizuri mstari huo, hauzungumzii tu siku ile alipotungishwa mimba, bali unakwenda nyuma zaidi hata kabla ya mimba kutungishwa mpaka siku aliyoubwa..anasema Naliumbwa katika hali ya uovu.

Unaona, Daudi alikuwa anajaribu kumweleza Mungu asili yake jinsi ilivyokuwa, kwamba yeye tangu kwenye mzizi huko kabla hata hajaja duniani alikuwa ni mtu ambaye yupo hatiani..

Na ndio maana mistari ya juu inasema..

1 Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.

2 Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu.

3 Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima.

4 Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.

5 Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani

Na ndio maana tena sehemu nyingine, anawasema watu waongo, kwamba watu hao hawajapotea siku ile wanaposema uongo, bali tangu walipokuwa tumboni mwa mama zao. Kuonyesha kuwa asili hiyo ilikuwepo ndani mwao, kabla hata hawajazaliwa.

Zaburi 58:3 “Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao; Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo”.

Unaona? Hata sisi sote, tumekuja katika hali ya hatia, tangu kuzaliwa kwetu, tangu kuumbwa kwetu, asili ya dhambi ipo ndani yetu..Ni mtu mmoja tu ambaye, hakuzaliwa na kosa, wala kutenda kosa lolote, wala chimbuko lake halikuwa na doa lolote na ndio maana alizaliwa na bikira..Na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO mwokozi wetu, yeye ndiye tangu kwenye mzizi, mpaka kwenye shina, mpaka kwenye tawi la matunda hakuwa na doa lolote, wala kosa lolote,wala hatia yoyote, alikuwa ni mkamilifu, hadi kufa kwake.

Hivyo hata kama Daudi alizaliwa na mwanamke kahabu, au mwanamke halali, hilo, sio la muhimu sana kwetu kujua. Tunachopaswa kujua ni kwamba mtu yeyote asipozaliwa mara ya pili haijalishi alizaliwa na kahaba, au mke halali, haijalishi alikuja kuwa yatima au mwenye wazazi, mjane au aliye na mume, tajiri au maskini, kama hujazaliwa mara ya pili na Yesu Kristo hawezi kuurithi ufalme wa mbinguni ..

Yohana 3:3 “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu”.

Kuzaliwa mara pili ndio kunaondoa ile hati ya mashtaka iliyo juu ya kila mmoja wetu, tangu asili.

Hivyo tubu dhambi zako, ukolewe. Ufanyike kiumbe kipya.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

TUNAMHITAJI SANA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUYAELEWA MAANDIKO.

MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU:

Ni kosa gani Daudi alilolifanya katika kuwahesabu watu, mpaka kupelekea vifo vya waisraeli wengi?

UTAWALA WA MIAKA 1000.

Fadhili ni nini? Nini maana ya “fadhili zake ni za milele” kibiblia?

MALIPO YA UPOTEVU.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Samson
Samson
1 year ago

Kila wakat n kuomba kwa iman