Ni lazima tujue namna mbalimbali za kupambana na adui yetu (Ibilisi). Tunajua yeye ni mpinzani wetu, na mpinzani sikuzote huwa si rahisi kukubali kushindwa kirahisi, ni lazima ataleta ukinzani. Na ndio hapo suala la Kukemea linakuja wala hatumbembelezi wala hatumsihi-sihi, bali tunamkemea.
Kukemea maana yake ni kukipinga/ kukifukuza kitu kwa nguvu, kwa mamlaka uliyonayo.
Tunaona sehemu nyingi Yesu akimkemea ibilisi Pamoja na mapepo yake, ambayo yalikuwa yanawatesa watu.
Mathayo 17:18 “Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile”.
Marko 8:33 Akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu
Hivyo na sisi tumepewa mamlaka hiyo, ya kumkemea ibilisi na mapepo yake, na uovu, na magonjwa, na vitu vya asili kwa jina la Yesu na vikatii.
Lakini pia tuna majira si lazima tufanye hivyo, Tutatumia nguvu nyingi sana! Leo tutaona silaha nyingine za Malaika ambayo wanatumia kumshughulikia shetani.. Maandiko yanatuambia wanao uwezo mkuu kuliko sisi lakini hawatumii uwezo wao wakati wote, kufanya hivyo kila wanapokutana na adui yao shetani.
Kwamfano, Wakati Fulani Malaika Mikaeli alipokutana na shetani, wakiushindania mwili wa Musa, maandiko yanasema, hakutumia uwezo wake kumlaumu, bali alisema Bwana na akukemee!.
Yuda 1:9 “Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee”.
Utajiuliza ni kwanini afanye vile? Sio kwasababu alishindwa, lakini alitambua SILAHA kubwa Zaidi itamfutilia mbali adui yake. Kwa namna nyingine Mikaeli alikuwa anamchonganisha shetani kwa Mungu. Na ukikemewa na Mungu unatarajia nini? Kama sio kupotelea mbali kabisa moja kwa moja.
Hivyo shetani anaiogopa vita ya Mungu Zaidi ya ile ya malaika au wanadamu.
Utaona tena jambo kama hili hili alilitenda Malaika mwingine, wakati ule wa Yoshua kuhani mkuu alipokuwa amesimama mbele za Bwana kuomba, na shetani naye amesimama kumpinga. Yule Malaika alimwambia shetani “Bwana na akukemee”.
Zekaria 3:1 “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye. 2 Bwana akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni?”
Umeona? Hivyo si kila wakati unapopishana na adui yako uso kwa uso, ufikirie kurusha makombora, kuvunja, kuharibu na kubomoa ngome, ndio yapo majira utasimama kuomba hivyo lakini pia tulia kwasababu maandiko yanasema VITA NI VYA BWANA. Mkabidhi Bwana yote. Kwamfano shetani amekuletea majaribu ya magonjwa sugu. Mwambie Bwana yaone mateso yangu, UMKEMEE SHETANI. Arudi nyuma yangu.
Sasa Maombi kama haya, usiyaombe juu juu tu,Fahamu kanuni, Ni maombi ya kumwita Mungu aingilie tatizo hilo, amwone mtesi wako, Ili pale anapopatumia kama mlango wa kukusumbua AMKEMEE atoke. Tatizo Lililokutesa kwa muda mrefu Bwana alifutilie mbali, kwa kulikemea.
Ni maombi aliyoyafanya Esta. Alipoona adui yake Hamani, amepanga vita dhidi yake na uzao wake na ndugu zake wauawe. Hakuhangaika, kushindana na Hamani adui yake. Aliona mambo yatakuwa mengi na kuumizana kichwa. Bali alikwenda moja kwa moja kwa mfalme. Akajinyenyekeza mbele zake, akamfanyia karamu kubwa sana, tena akamwomba katika karamu hiyo aje na yule adui yake, washiriki pamoja. ndipo mfalme akamuuliza haja yako ni nini, Lakini tunaona Esta bado hakumwambia tatizo lake kwa haraka,, akamfanyia tena na mara ya pili mfalme na adui yake karamu iliyo kubwa kama ile ya kwanza, akawaalika.. Ndipo Mfalme akamuuliza tena Esta haja yako ni nini?. Ndipo Esta sasa akaeleza akasema, ni HUYU ADUI YANGU HAMANI, amepanga kuniua mimi.
Akamwachia mfalme hukumu yote. Saa ileile Hamani akaenda kutundikwa msalabani, yeye na nyumba yake yote ikauliwa. Na Habari yake ikawa imeisha pale hadi hivi leo. Wala Esta hakuita kikosi, wala hakuchukua upanga, wala hakumwambia mfame muue, mvunje shingo, mchome moto Hamani. Hakusema hayo alichomwomba mfalme ni uhai wake tu (Esta 5).
Na ndivyo Mungu atakavyofanya kwa adui yetu Ibilisi na mapepo yake, pale ambapo tutataka Bwana ashughulike na matatizo yetu, zaidi ya sisi kushughulika nayo kuyakemea. Lakini ni sharti sisi tumkaribie yeye, kwa moyo wa upendo, tumfanyie karamu, ya Kupendeza ndipo tuzikabidhi changamoto zetu kwake.
Hivyo silaha hii ukiitumia vema itakusaidia sana. Jenga ukaribu wako na Mungu, Fanya ibada nyingi, mtolee Bwana sadaka, mwimbie sifa, mtukuze sana, ruka-ruka uweponi mwake, mpendeze moyo wake..( fanya hivi Zaidi ya kurusha makombora, na maombi ya vita) kisha mwishoni ndio mwambie Bwana amkemee adui yako. . Matokeo utayaona makubwa sana, haijalishi tatizo ulilonalo limekusumbua kwa muda mrefu kiasi gani, umepambana nalo kwa muda mrefu kiasi gani, limekuja na kujirudia rudia mara nyingi kiasi gani. Ugonjwa huo hautibiki kwa namna ipi, utakwenda tu.. Safari hii halitarudi kwako tena milele.
Bwana akubariki.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
ESTA: Mlango wa 1 & 2
ESTA: Mlango wa 5, 6 & 7
Je Malaika Mikaeli ndiye Yesu mwenyewe?
VITA DHIDI YA MAADUI
HUDUMA YA MALAIKA WAWILI.
USIRUHUSU INZI WATUE JUU YA ROHO YAKO.
Ni kwa namna gani, upendo husitiri wingi wa dhambi? (1Petro 4:8).
Rudi nyumbani
Print this post
Dinari ilikuwa ni sarafu ya kirumi yenye thamani ya (utumishi wa kibarua wa siku nzima)..Kwamfano leo hii tuseme kibaru atalipwa kwa siku shilingi elfu 20, na ukawa ndio utaratibu wa nchi nzima, kuwalipa vibarua kiasi hiko kwa siku kama mshahara, basi kiasi hiko cha fedha kingekuwa na thamani sawa na Dinari kwa wakati huo.
Tutalithibitisha hilo Zaidi katika ule mfano Bwana alioutoa wakulima walioajiriwa katika shamba la mizabibu..
Mathayo 20:1 “Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu 2 Naye alipokwisha kupatana na wakulima KUWAPA KUTWA DINARI, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu”.
Mathayo 20:1 “Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu
2 Naye alipokwisha kupatana na wakulima KUWAPA KUTWA DINARI, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu”.
Kwahiyo “ malipo ya utumishi wa kutwa nzima wa kibarua” ndiyo yaliyokuwa na uthamani wa “Dinari” na uzito wa sarafu ya Dirani ulikuwa ni “gramu 3.85”,
Kwa urefu kuhusiana na vipimo hivyo fungua hapa >>>VIPIMO VYA KIBIBLIA
Lakini tukirudi katika “Rupia”.. tunaisoma sehemu moja tu katika kitabu cha Ufunuo 6:6
Ufunuo 6:5 “Na alipoifungua muhuri ya tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake.
6 Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa NUSU RUPIA, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu RUPIA, wala usiyadhuru mafuta wala divai”.
“Rupia” ni sarafu nyingine yenye thamani sawa na “Dinari”.. ambayo ilikuwa inatumiwa zaidi namataifa mengine tofauti na Rumi (uthamani wake ulikuwa ni sawa na mshahara wa kibarua wa kutwa)… Na mpaka sasa bado baadhi ya mataifa yanatumia Rupia!.
Lakini ni somo gani tunalolipata kutoka katika thamani hii ya fedha (Dinari na Rupia)?
Somo kubwa tunalolipata si lingine Zaidi ya lile tunalolisoma katika Mathayo 20:1-16, kuwa thawabu za Mungu hazichunguziki.
Kwa urefu unaweza kusoma hapa >>KUMBE MUNGU ANAWEZA KUKULIPA KWA USICHOSTAHILI!
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)
AINA TATU ZA WAKRISTO.
GHARAMA YA UFALME WA MBINGUNI.
SHAMBA HUWA HALIMTAMBUI WALA KUMSUBIRIA MKULIMA.
Je! Ni sawa kuingia katika shamba la mtu mwingine na kula jinsi utakavyo?
Jibu: Tusome,
Ayubu 22:12 “Je! Mungu hayuko mbinguni juu? Tena tazama umbali wa nyota, jinsi zilivyo juu! 13 Nawe wasema, Mungu anajua nini? Je! Aweza kuamua kati ya giza kuu? 14 Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; Naye yuatembea juu ya KUBA YA MBINGU. 15 Je! Utaiandama njia ya zamani Waliyoikanyaga watu waovu?”
Ayubu 22:12 “Je! Mungu hayuko mbinguni juu? Tena tazama umbali wa nyota, jinsi zilivyo juu!
13 Nawe wasema, Mungu anajua nini? Je! Aweza kuamua kati ya giza kuu?
14 Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; Naye yuatembea juu ya KUBA YA MBINGU.
15 Je! Utaiandama njia ya zamani Waliyoikanyaga watu waovu?”
Kuba ni mzunguko wa Anga, Ukitazama juu utaona ncha za mbingu ni kama duara, ndio maana jua wakati wa asuhuhi ni kama “linachomoza kutoka chini upande wa mashariki” na wakati wa mchana linaonekana lipo juu kabisa (utosini) lakini inapofika jioni “linazama tena chini upande wa magharibi”..
Sasa huo mduara wa anga ndio unaoitwa “KUBA” na maandiko yanasema Bwana anatembea juu ya mduara huo, kuonyesha utukufu wake.
Ayubu 22:14 “Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; Naye yuatembea juu ya KUBA YA MBINGU”.
Hivyo andiko hili linaonyesha utukufu na ukuu wa Mungu, kuwa yuko juu sana na mwingi wa uweza.
Je umemrudia yeye aliyezifanya Nyota na Mwezi, na anga na viumbe vyote?..
Mhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.
2 Kabla jua, na nuru, na mwezi, Na nyota, havijatiwa giza; Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua”
Maran atha!
MKUU WA ANGA.
NYOTA ZIPOTEAZO.
Je ile nyota ya asubuhi inamwakilisha shetani au Bwana Yesu?
Huihesabu idadi ya nyota, Huzipa zote majina.
Mbinguni ni sehemu gani?
Je unajua unapofanya mapenzi ya Mungu ni kwa faida yako na si kwa faida ya Mungu?.. Je unajua Mungu hana hasara na wala hajawahi kupata hasara kwa watu kufuata njia zao?…na vile vile hana faida yoyoyote anapata kwa wewe kuwa mkamilifu..
Zaidi sana tunapofanya mema au tunapofanya mabaya, ni kwa faida na hasara zetu wenyewe…ndivyo maandiko yanavyosema.
Ayubu 22:2 “Je! Yumkini mtu awaye yote kumfaa Mungu? Hakika yeye aliye na hekima hujifaa mwenyewe. 3 Je! Mwenyezi hupata furaha katika wewe kuwa mwenye haki? Au je, ni faida kwake, kwamba wafanya njia zako kuwa timilifu?”
Ayubu 22:2 “Je! Yumkini mtu awaye yote kumfaa Mungu? Hakika yeye aliye na hekima hujifaa mwenyewe.
3 Je! Mwenyezi hupata furaha katika wewe kuwa mwenye haki? Au je, ni faida kwake, kwamba wafanya njia zako kuwa timilifu?”
Umeona?..tunapozishika amri za Mungu ni kwa faida ya roho zetu na nafsi zetu ndio Mungu wetu anatukazania tuitafute hiyo…ili tupate uzima wa milele, lakini tunapomkataa yeye (Mungu) yeye hana cha kupoteza, kwasababu vyote vinatoka kwake…badala yake ni kwa hasara zetu na uangamivu wetu wenyewe..
Ayubu 35:6 “Ikiwa umefanya dhambi, umefanya nini juu yake? Yakiwa makosa yako yameongezeka, wamfanyia nini yeye? 7 Ikiwa u mwenye haki, wampa kitu gani? Au yeye hupokea nini mkononi mwako? 8 Uovu wako waweza kumwumiza mtu kama wewe; Na haki yako yaweza kumfaa mwanadamu”.
Ayubu 35:6 “Ikiwa umefanya dhambi, umefanya nini juu yake? Yakiwa makosa yako yameongezeka, wamfanyia nini yeye?
7 Ikiwa u mwenye haki, wampa kitu gani? Au yeye hupokea nini mkononi mwako?
8 Uovu wako waweza kumwumiza mtu kama wewe; Na haki yako yaweza kumfaa mwanadamu”.
Unapozini unajiharibu mwenyewe na si Mungu…
Mithali 6:32 “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake”Unapoiba unajihatarishia maisha yako mwenyewe, unapoua unajimaliza mwenyewe na mambo mengine yote yasiyofaa ni kwa hasara zetu..
Lakini Bwana anapenda kuona tunakuwa na maisha ya milele ndio maana amemtuma mwanae wa pekee kwetu, ili tunapomwamini tuokolewe na tusipotee milele.
Lakini kama tukichagua mauti kwa hiari zetu wenyewe basi hatumpunguzii kitu, zaidi sisi ndio tunaopata hasara.
Ikatae dhambi, mkubali Yesu, mgeukie Muumba wako kabla hujamaliza siku zako za kuishi na utapata faida nyingi.
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Walakini ataokolewa kwa uzazi wake.
USIJISIFIE KARAMA KWA UONGO.
Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu.
BASI NIKAOGOPA, NIKAENDA NIKAIFICHA TALANTA YAKO.
TUNAHESABIWA HAKI BURE KWA NJIA YA IMANI.
Watu wengi wanapofikia hatua ya kuomba, wanashindwa kuomba vizuri au kudumu kwa muda mrefu, sio kwamba hawana nguvu za rohoni, hapana bali wakati mwingine ni kwasababu wanakosa mwongozo wa vitu vya kuombea. Hivyo tumeona tuutoe mwongozo huu mfupi ambao utakusaidia, unapoingia katika maombi yako ya asubuhi. Zingatia: Hii sio kanuni ya daima, Zipo nyakati Roho atakuongoza cha kuombea. Lakini hapa tunakupa mambo muhimu ambayo unapaswa uyajumuishe katika maombi yako ya asubuhi kila siku .
Kiwango cha chini kiwe ni Saa moja (1).
1. SHUKRANI: Ombi la kwanza liwe ni shukrani, Kumbuka umeianza siku mpya, huna budi kutanguliza shukrani kwa Mungu wako, kwa ajili ya uzima, afya,familia,wokovu, chakula,amani n.k.
Wakolosai 3:15 “…..tena iweni watu wa shukrani”
2. MWONGOZO WA SIKU MPYA: Omba Bwana akutangulie katika siku yako mpya. Ukayatende yale yote aliyokusudia uyatende katika siku hiyo. Usitoke nje ya mpango wake. Ili siku Yako isiwe Bure Rohoni.
Mithali 16:3 “Mkabidhi Bwana kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika”.
3. NENO LA MUNGU : Omba uwezo wa kulikumbuka na kuliishi Neno la Mungu katika siku yote mpya. Neno lake Lisidondoke moyoni mwako, Usisahau agizo lake hata moja.Uishi Kwa hilo
Zaburi 119:16 “Nitajifurahisha sana kwa amri zako, Sitalisahau neno lako”.
4. ULIMI WAKO: Katika siku yenye masumbufu na pilikapilika ya mambo mengi, Ni busara umwambie Bwana aweke mlinzi katika kinywa chako usijikwae kwa maneno mahali popote.
Zaburi 141:3 “Ee Bwana, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu”
5. UTUKUFU WA MUNGU: Mwambie Mungu mambo yote uyafanyao ndani ya siku mpya yawe ni kwa utukufu wake. Na sio wa adui au mwanadamu.
1Wakorintho 10:31 “Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu”
6.WAKATI: Omba Mungu akusaidie kuukomboa wakati wako, siku yako isiwe na mapengo, usipite hivi hivi hujafanya jambo la msingi katika wokovu au maisha yako kwa ujumla.
Waefeso 5:15 “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu”
7. INJILI YA KRISTO: Mwambie Bwana akupe ujasiri wa kuwashuhudia wengine injili, popote uwapo. Vilevile ombea injili ya Kristo ienee kwa nguvu siku hiyo ulimwenguni kote. Ombea pia watumishi wa Mungu wanaotenda kazi yake, wapewe nguvu ili waitimize huduma hiyo ya Bwana.
Matendo 4:31 “Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri”
8. NDUGU NA FAMILIA: Ipeleke familia yako/ ndugu zako kwa Kristo akutane nao katika siku hiyo/ waokoke/ wadumu katika wokovu. Umepewa ndugu ili usimame Kwa ajili Yao.
Warumi 10:1 “Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe”.
9. JAMII: Utakutana na watu mbalimbali, mazingira mbalimbali, Hivyo huna budi uyaombee Amani, utulivu n.k. Ili uweze kuishi pia kwa amani, katika utumishi wako Kwa Bwana.
Yeremia 29:7 “Kautakieni amani mji ule, ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, mkauombee kwa Bwana; kwa maana katika amani yake mji huo ninyi mtapata amani”.
10. ADUI: Mwambie Bwana akuepushe na Yule mwovu. Katika siku yako, mwovu asikujaribu katika imani, afya, kazi n.k
Mathayo 6:13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
Ukitumia walau dakika sita (6), kuombea kila kipengele. Utakuwa umekamilisha SAA MOJA (1), La maombi. Na ukijijengea utaratibu wa kufanya hivi kila siku asubuhi, utaona mabadiliko makubwa sana ya maisha yako ya kiroho na kimwili.
WoKovu bila maombi ni sawa na gari zuri lisilo na mafuta. HUFIKI POPOTE.
Bwana akubariki. Nikutakie maombi mema.
LITURJIA NI NINI? NA JE IPO KIMAANDIKO?
Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?(
Sadaka ya Amani ilikuwaje?
KUNA AINA NGAPI ZA MAOMBI?
IJUE FAIDA YA KUFUNGA PAMOJA NA WANYAMA WAKO.
Biblia haijatoa ‘fomula’, ya idadi ya nyakati tunazopaswa kuomba kwa siku. Ila imesema ‘tuombe kila wakati’ na sehemu nyingine imesema ‘tuombe bila kukoma’. Hiyo ni kutupa uelewa kwamba maombi yanapaswa yawe ni endelevu lakini pia yawe ya wakati wote. Na hakuna mahali maandiko yanatoa nafasi ya mwaminio kutokuomba kabisa.
Waefeso 6:18 “kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;”
1Wathesalonike 5:17 “ombeni bila kukoma”
Hivyo ni sisi kutazama, watakatifu walikuwa na desturi gani, na nidhamu gani waliyojijengea katika kuomba. Je! Walitumia vipindi vingapi kwa siku? Vilevile tutaona Bwana Yesu anasemaje kuhusiana na hilo pia. Ili na sisi tuige vielelezo vyao katika utaratibu wetu wa kusali.
DAUDI
Daudi aliomba mara tatu(3) kwa siku . Asubuhi, adhuhuri na jioni.
Zaburi 55:17 Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu.
DANIELI
Danieli pia aliomba mara tatu (3), kwa siku.
Danieli 6:10 Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
Hivyo hii ni kutuonyesha kuwa ilikuwa ni desturi ya watakatifu wa kale, kwenda magotini walau mara 3 kwa siku. Na maombi waliyoyaomba hayakuwa ‘sala’ za dakika tano (kama zile za kuombea chakula). Bali ni maombi ambayo huwenda yalizidi saa moja, kwasababu maombi ya kulalama, na kuugua, (mfano wa hayo ya Daudi) sio ya dakika chache.
YESU KRISTO.
Bwana Yesu aliomba alfajiri na usiku, na majira mengi nyakati za adhuhuri aliahirisha huduma na kwenda mahali pa utulivu kusali.
Marko 1:35 “Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko”
Na usiku
Mathayo 26:40 “Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? 41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu”.
Adhuhuri
Luka 5:16 “Lakini yeye alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba”
Hivyo tunaona pia Bwana aliomba nyakati zote. Alipopata nafasi.
Hivyo kiwango cha chini kabisa cha nyakati za kuomba kwa siku kwa sisi wakristo ni MARA MBILI. Yaani asubuhi na jioni. Unapoanza siku huna budi kuanza na Bwana kwa kumshukuru na kumwomba mwongozo wa siku hiyo, vilevile unapomaliza siku wapaswa ufanye hivyo hivyo.
Na ndio maana Bwana alisema maneno haya, kwa watu wake wanaoomba alisema;
Luka 18:7 Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?
Kumbe usiku na mchana tunapaswa tuombe. Walau mara mbili kwa siku. Alisema, Yeye ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho. Kufunua kuwa yupo katika mwanzo wetu na mwisho wetu. Hakikisha uanzapo siku unatenga muda wa kutosha wa kuingia uweponi, na umalizapo siku unafanya hivyo hivyo. Utakuwa imara sana kiroho.
Lakini zaidi sana Bwana anataka tuwe watu wa kuomba siku zote kufikia hata kukesha. Hivyo ikizidi hapo ni vema sana, kwasababu utajiwekea akiba ya maombi kwa wakati ambao utakuwa na nguvu chache.
JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.
HIZI NI NYAKATI ZA KUFUNGA NA KUOMBA
Fahamu Namna ya Kuomba.
NITAJUAJE KAMA MAOMBI YANGU YAMEFIKA (YAMEJITOSHELEZA)?.
MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.
(Masomo maalumu yahusuyo mifungo na maombi).
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze Biblia Neno la Mungu wetu lililo taa ya miguu yetu na Mwanga wa njia yetu (Zab 119:105).
Biblia inatufundisha sehemu kadhaa FAIDA za kufunga (yaani kujizuia kula na kunywa kwa kitambo) kwamba kwa kufanya hivyo tunafungua milango mingi, ambayo isingeweza kufunguka kwa maombi ya kawaida tu.
Mathayo 17:20 “Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. 21 [LAKINI NAMNA HII HAITOKI ILA KWA KUSALI NA KUFUNGA”.
Mathayo 17:20 “Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
21 [LAKINI NAMNA HII HAITOKI ILA KWA KUSALI NA KUFUNGA”.
Lakini JE UNAJUA FAIDA ZA KUIFUNGISHA NA MIFUGO YAKO PIA? AU KAZI YAKO, AU BIASHARA YAKO?. Si watu tu wanaopaswa kufunga hata wanyama pia.. Utauliza hilo limekaaje?, hebu turejee biblia kidogo nyakati zile za Nabii Yona alipokwenda kuhubiri katika mji wa Ninawi.
Biblia inaonyesha kuwa Mfalme wa Ninawi alipiga mbiu kuwa wanadamu na wanyama wote walioko Ninawi wafunge wasile wala wasinywe (Zingatia hilo: si wanadamu tu bali hata wanyama wa kufugwa).
Yona 3:6 “Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu. 7 Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu ASIONJE KITU, WALA MNYAMA WALA MAKUNDI YA NG’OMBE, WALA MAKUNDI YA KONDOO; WASILE, WALA WASINYWE MAJI; 8 bali na wafunikwe nguo za magunia, MWANADAMU NA MNYAMA PIA, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake. 9 Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe? 10 Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende”.
Yona 3:6 “Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu.
7 Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu ASIONJE KITU, WALA MNYAMA WALA MAKUNDI YA NG’OMBE, WALA MAKUNDI YA KONDOO; WASILE, WALA WASINYWE MAJI;
8 bali na wafunikwe nguo za magunia, MWANADAMU NA MNYAMA PIA, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake.
9 Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe? 10 Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende”.
Unaona alichofanya Mfalme wa Ninawi??…Na matokeo yake tunaona baadaye Mungu anawataja wanyama kuwa wamestahili rehema kwa mfungo huo..Maana yake wanyama nao pia wasingefungishwa huenda wangepona watu tu lakini wanyama wangepigwa (wangekufa!!)..Maana yake uchumi wao watu wa Ninawi ungeharibika, hata baada ya wao kupokea msamaha!!.
Yona 4:10 “Bwana akamwambia, Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuuotesha; uliomea katika usiku mmoja, na kuangamia katika usiku mmoja; 11 na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi YA MIA NA ISHIRINI ELFU, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; TENA WAMO WANYAMA WA KUFUGWA WENGI SANA?”
Yona 4:10 “Bwana akamwambia, Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuuotesha; uliomea katika usiku mmoja, na kuangamia katika usiku mmoja;
11 na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi YA MIA NA ISHIRINI ELFU, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; TENA WAMO WANYAMA WA KUFUGWA WENGI SANA?”
Nataka uangalie hayo maneno ya mwisho ya Bwana… “TENA WAMO WANYAMA WA KUFUGWA WENGI SANA?”
Kumbe hata wanyama pia wanaweza kuingizwa kwenye mkondo wetu wa BARAKA AU LAANA!.. Mfalme wa Ninawi aliliona hili, alijua siku ile ya gharika ya Nuhu hata wanyama waliangamizwa na dunia, na yeye akajua dhambi zimewachafua si tu watu, bali hata na wanyama wao wa kufugwa, hivyo nao pia ni lazima watakaswe kwa toba na kwa kufunga, na utaona aliwavisha mpaka hao wanyama mavazi ya magunia!.
Ni vizuri kulijua hili ndugu, kuwa unapofunga fanya hivyo pia kwa wanyama wako (inaweza isiwe mara kwa mara lakini weka desturi hiyo)!!!
Unapofunga hebu pia funga pia na shamba lako, usinyeshee chochote siku hiyo, usiweke mboleo siku hiyo, wala usilipalilie, kama unafuga kuku, usiwalishe siku hiyo, usilishe ng’ombe wako siku hiyo, usilishe mbuzi wako siku hiyo, vile vile usifungue biashara yako siku hiyo, fanya hivyo kwa Imani na utaona matokeo makubwa sana baada ya hapo!.
Wengi hawaoni matokeo katika kazi zao kwasababu wanasahau kufunga biashara zao, badala yake wanafunga tu wao, pasipo kujua kuwa vifungo pia havipo tu katika mwili, bali pia katika biashara na mifugo, hivyo nayo pia inapaswa ifungishwe.
Maran atha
NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.
HIZI NI NYAKATI ZA KUFUNGA NA KUOMBA.
NINI MAANA YA KUTUBU
Je tunaruhusiwa kutumia vidonge wakati wa kufunga?
Ninawi ni nchi gani kwasasa?
JIBU: Ipo mitazamo mingi, ihusuyo eneo halisi la makaburi ya wazazi wetu wa kwanza, Kwamfano kwa mujibu wa hadithi za kiyahudi, wao wanaamini kuwa Adamu na Hawa walizikwa pale Israeli, mahali palipoitwa Hebroni katika pango lijulikanalo kama pango la Makpela. Ambalo baadaye Ibrahimu na Sara walikuja kulinunua likawa ni eneo la maziko yao ya kifamilia, (Mwanzo 49:29-31) kwa urefu wa habari hiyo fungua hapa usome >>> Pango la Makpela ni lipi,
Wengine, wanaamini kuwa pale Kristo aliposulubiwa Golgota, ndipo palipokuwa kaburi la Adamu, wakiamini kuwa kama Kristo alivyoitwa Adamu wa pili, maana yake ni alikuja kurudisha kile kitu ambacho Adamu wa kwanza alikipoteza, yaani uzima. Hivyo kama Adamu alileta kifo, Kristo alileta uzima kwa msalaba wake, na aliyafanya hayo juu ya kaburi la Adamu.
Lakini je! kuna usahihi kwa mitazamo hiyo.
Kwasababu biblia haijaeleza chochote, kuhusiana na kaburi la Adamu na Hawa, hii yote ni mitazamo, ambayo yaweza kuwa ukweli au uongo, tusiweke imani yetu moja kwa moja katika mitazamo. Kwasababu gharika ilipokuja ilivuruga ramani yote ya ulimwengu, isingekuwa rahisi kupatambua mahali sahihi alipozikwa Adamu, isipokuwa kwa ufunuo.
Na habari hiyo kutoandikwa ni kutuonyesha kuwa hakuna umuhimu sana wa kujua Adamu alizikiwa wapi. Ushindi tulioupata kwa kifo cha Kristo, na kufufuka kwake, ni habari tosha tunayopaswa tuitafakari usiku na mchana, zaidi ya kaburi la Adamu.
Lakini swali ni Je! Yesu amefufuka ndani yako? Fahamu kuwa Ikiwa bado hujazaliwa mara ya pili, kifo kina nguvu juu yako, ukifa hakuna maisha kwako, ni mateso katika moto wa jehanamu. Lakini ukizaliwa mara ya pili uzima wa milele unao na hata ukifa, utakuwa unaendelea kuishi.
Yohana 11:25 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?
Unasubiri nini? Usiokoke leo.
Saa ya wokovu ni sasa, ni pale tu unapotubu kwa kumaanisha kuacha dhambi, na kumwita Yesu ayatawale maisha yako, kisha kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu. Hapo unakuwa tayari umezaliwa mara ya pili. Ikiwa upo tayari kufanya hivyo sasa, basi fungua hapa kwa mwongozo wa Sala hiyo ya toba.>>>KUONGOZWA SALA YA TOBA
KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?
Maziara ni nini? Je! Na Tunaruhusiwa kuyajenga kwenye makaburi yetu?
JINA LAKO NI LA NANI?
Kuhimidi ni nini?(Zaburi 31:21)
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
Kwanini Yesu Kristo ni mwana wa Adamu?
Rudi Nyumbani
Maelezo ya Mithali 28:20
“Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa”.
Mstari huo unatufundisha jinsi pupa (kutaka vya haraka), inavyokinzana na neno “Uaminifu”. Ikiwa na maana mtu ambaye anataka wingi kwa muda mfupi, ni lazima tu atatumia njia isiyo ya haki, ili avipate anavyovitaka. Kwamfano viongozi wa nchi au waajiriwa wenye tamaa ya mafanikio ya haraka, wanaotaka mwezi huo huo wajenge, au wawe na miradi mikubwa, mwisho wa siku huwa wanatumia njia za wizi, ili kufikia mafanikio yao. Hiyo ndio sababu inayowafanya wapoteze uaminifu katika kile walichokabidhiwa.
Na hatma ya hawa watu, ni kukutana tu na matatizo, aidha kufungwa, au kufukuzwa kazi, au kutozwa faini, n.k.. na kuangukia hasara tu sio faida.
Ndio maana ya hili Neno
Mithali 28:20 Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.
Kwasababu mafanikio na pupa, havipatani kabisa. Bali achumaye kidogo-kidogo ndiye atakayefanikiwa(Mithali 13:11)
Yusufu alirekodiwa kuwa ni mwaminifu katika kazi yake. Na hivyo, akabarikiwa na Bwana mpaka akapewa nafasi ya uwaziri-mkuu wa taifa kubwa la Misri (Mwanzo 39:1-6). Danieli alirekodiwa kuwa muaminifu na hivyo akadumu katika falme zote mbili zilizotawala dunia wakati ule, yaani Babeli pamoja na Umedi na Uajemi (Danieli 6:4).
Lakini pia Neno hili linatafsirika rohoni.
Katika kazi ya Bwana, palipo na UAMINIFU, basi mwishowe Mungu huwa anabariki utumishi wa mtu huyo. Alisema maneno haya;
Luka 16:10 “Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. 11 Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli? 12 Na kama hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?
Umeona? Lakini ukikosa uaminifu, ndio utataka utumie njia zisizompendeza Mungu ili uone matokeo unayoyatarajia haraka, ndio hapo utaona mhubiri anatumia njia za undanganyifu kutengeneza shuhuda za uongo, ili watu wajue kuwa anao-upako wajae kwenye kanisa lake. Mambo kama haya hatma yake ni , uangamivu. Wengine, wanahubiri injili ya kisiasa, au vichekesho, wengine wanapachika staili za kidunia madhabahuni na kwenye kwaya, hawahubiri tena kweli, wala hawakemei dhambi, wakihofia watu kukimbia makanisa yao. Wanapoteza uaminifu ili wapate watu wengi kanisani. Hii ni hatari kubwa!
Hawajui kuwa ndani ya uaminifu, zipo Baraka. Na Mungu anaona, Mungu atamnyanyua tu mtu huyo.
Hivyo tupende kusimamia kweli, turidhike na nafasi zetu, tupinge mambo ya giza, TUWE WAAMINIFU katika yote na hakika tutaona Baraka za Bwana.
UAMINIFU NI KIGEZO KIKUBWA CHA KUTUMIWA NA MUNGU.
USIZISHIRIKI DHAMBI ZA WATU WENGINE.
Maana ya Mithali 9:17 “Maji yaliyoibiwa ni matamu, Na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza”
Vifungu vya biblia kuhusu Uongozi.
Nini maana ya Mithali 27:6 “Jeraha utiwazo na rafiki ni amini;
TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO
THAWABU YA UAMINIFU.
Katika biblia mtu ambaye alipokea taarifa iliyofichwa kutoka Kwa Mungu na kuiwasilisha Kwa watu aliitwa mwonaji. Alipokea aidha kupitia, maono, ndoto, au kufunuliwa dhahiri, Mfano wa Hawa alikuwa ni Samweli…
1 Samweli 9:9-12
[9](Hapo zamani katika Israeli, mtu alipokwenda kuuliza neno kwa Mungu, husema hivi, Haya! Twende kwa mwonaji; maana mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani aliitwa Mwonaji.) [10]Basi Sauli akamwambia mtumishi wake, Umesema vema; haya! Twende. Wakaenda mpaka mji ule aliokuwamo mtu wa Mungu. [11]Hata walipokwea kwenda mjini, wakakutana na wasichana, wanatoka kwenda kuteka maji; wakawaambia, Je! Mwonaji yuko? [12]Nao wakawajibu, wakasema, Yuko; tazama, yuko huko mbele yako; fanyeni haraka sasa, maana hivi leo amekuja mjini; kwa sababu watu wana dhabihu leo katika mahali pa juu;
[9](Hapo zamani katika Israeli, mtu alipokwenda kuuliza neno kwa Mungu, husema hivi, Haya! Twende kwa mwonaji; maana mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani aliitwa Mwonaji.)
[10]Basi Sauli akamwambia mtumishi wake, Umesema vema; haya! Twende. Wakaenda mpaka mji ule aliokuwamo mtu wa Mungu.
[11]Hata walipokwea kwenda mjini, wakakutana na wasichana, wanatoka kwenda kuteka maji; wakawaambia, Je! Mwonaji yuko?
[12]Nao wakawajibu, wakasema, Yuko; tazama, yuko huko mbele yako; fanyeni haraka sasa, maana hivi leo amekuja mjini; kwa sababu watu wana dhabihu leo katika mahali pa juu;
Lakini baadaye watu Hawa walikuja pia kuitwa Manabii kama tunavyosoma kwenye vifungu hivyo
Isipokuwa Maana ya Nabii ni Pana zaidi sio tu kupokea taarifa kutoka Kwa Mungu na kuiwasilisha Bali pia alisimama kufundisha na kuwarejesha watu, katika Sheria ya Mungu.ikiwemo kukaripia na kukemea, na kuonya. Mfano wa Hawa ni Isaya, Yeremia, Ezekieli, Yona, Hosea, Mika, Hagai, Malaki na wengine.
Hivyo nabii ni lazima pia awe mwonaji, kwamba apokee pia taaarifa za Moja Kwa Moja kutoka Kwa Mungu, na kufichua Siri zilizositirika lakini mwonaji haikuwa lazima afanye kazi ya kinabii, Bali ni kusema tu kile anachoelezwa, au kufichua Siri zilizojificha, au kuomba mwongozo wa Roho wa Mungu, Kwa ajili ya jambo/tatizo Fulani.
Hivyo kuhitimisha ni kwamba Kuna maandiko mengine yanawataja waonaji, lakini yalimaanisha pia ni manabii, na mengine yanabakia kumaanisha walewale tu waonaji.
Mfano wake ni Samweli, ambaye alikuwa ni mwonaji lakini pia ni Nabii.
1 Mambo ya Nyakati 29:29
[29]Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo na mwisho, angalia, zimeandikwa katika tarehe ya Samweli, mwonaji, na katika tarehe ya Nathani, nabii, na katika tarehe ya Gadi, mwonaji;
Soma pia vifungu hivi, kufahamu zaidi.
(2Samweli 24:11, 2Nyakati 16:7, 29:30,)
IELEWE SAUTI YA MUNGU.
TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.
NA TAA YA MUNGU ILIKUWA BADO HAIJAZIMIKA.
UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?
Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?
NA TAA YA MUNGU ILIKUWA BADO HAIJAZIMIKA
Tofauti kati ya ndoto na Maono ni ipi?