TENDA HAKI KWA FAIDA YAKO MWENYEWE.

TENDA HAKI KWA FAIDA YAKO MWENYEWE.

Je unajua unapofanya mapenzi ya Mungu ni kwa faida yako na si kwa faida ya Mungu?.. Je unajua Mungu hana hasara na wala hajawahi kupata hasara kwa watu kufuata njia zao?…na vile vile hana faida yoyoyote anapata kwa wewe kuwa mkamilifu..

Zaidi sana tunapofanya mema au tunapofanya mabaya, ni kwa faida na hasara zetu wenyewe…ndivyo maandiko yanavyosema.

Ayubu 22:2 “Je! Yumkini mtu awaye yote kumfaa Mungu? Hakika yeye aliye na hekima hujifaa mwenyewe.

3 Je! Mwenyezi hupata furaha katika wewe kuwa mwenye haki? Au je, ni faida kwake, kwamba wafanya njia zako kuwa timilifu?”

Umeona?..tunapozishika amri za Mungu ni kwa faida ya roho zetu na nafsi zetu ndio Mungu wetu anatukazania tuitafute hiyo…ili tupate uzima wa milele, lakini tunapomkataa yeye (Mungu) yeye hana cha kupoteza, kwasababu vyote vinatoka kwake…badala yake ni kwa hasara zetu na uangamivu wetu wenyewe..

Ayubu 35:6 “Ikiwa umefanya dhambi, umefanya nini juu yake? Yakiwa makosa yako yameongezeka, wamfanyia nini yeye?

7 Ikiwa u mwenye haki, wampa kitu gani? Au yeye hupokea nini mkononi mwako?

8 Uovu wako waweza kumwumiza mtu kama wewe; Na haki yako yaweza kumfaa mwanadamu”.

Unapozini unajiharibu mwenyewe na si Mungu…

Mithali 6:32 “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake”
Unapoiba unajihatarishia maisha yako mwenyewe, unapoua unajimaliza mwenyewe na mambo mengine yote yasiyofaa ni kwa hasara zetu..

Lakini Bwana anapenda kuona tunakuwa na maisha ya milele ndio maana amemtuma mwanae wa pekee kwetu, ili tunapomwamini tuokolewe na tusipotee milele.

Lakini kama tukichagua mauti kwa hiari zetu wenyewe basi hatumpunguzii kitu, zaidi sisi ndio tunaopata hasara.

Ikatae dhambi, mkubali Yesu, mgeukie Muumba wako kabla hujamaliza siku zako za kuishi na utapata faida nyingi.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

Walakini ataokolewa kwa uzazi wake.

USIJISIFIE KARAMA KWA UONGO.

Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu.

BASI NIKAOGOPA, NIKAENDA NIKAIFICHA TALANTA YAKO.

TUNAHESABIWA HAKI BURE KWA NJIA YA IMANI.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments