Title February 2021

Biblia ina maana gani inaposema akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko?

JIBU: Tusome,

Mithali 10:10 “Akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka”.

Kukonyeza ni ishara inayojulikana  kama ya undanganyifu au ya kupoteza uaminifu. Ni jambo la kawaida tumekuwa tukiliona hata katika maisha ya kawaida, kwa mfano, labda mteja, mmoja amekwenda kununua bidhaa Fulani kwa muuzaji sokoni, Sasa ikatokea, ghafla muuzaji mwingine akakatiza anauza bidhaa kama ile ile, Ni kawaida ya mnunuzi  kutaka kuulizia bei halisi ya hiyo bidhaa kwa muuzaji mwingine, Sasa kama kweli yule muuzaji wa kwanza aliambiwa bei halali ,hatoonyesha chochote, lakini kama alitaka kumuuzia kwa bei ya juu Zaidi kuliko ilivyo kawaida, yule muuzaji wa kwanza atatumia ishara Fulani, aidha kumkonyeza muuzaji mwenzake, ili akae kimya..Asimwambie bei halali.

Sasa hiyo ni dalili ya kukosa uaminifu.

Mfano mwingine, utakuta labda mtu na familia yake wamealikwa kwenye sherehe fulani, na kule kwenye sherehe pengine baba wa familia hiyo akakutana na wanawake wengine wazuri, akawatamani, sasa njia ambayo anaweza kutumia kuwasiliana nao, kirahisi ili pengine baadaye wakutane, ni kwa kumkonyeza,..Huo ni mfano tu.

Umeona  kitendo hicho  kimetumika kama  ishara ya udanganyifu.

Biblia inasema..

Mithali 6:12 “Mtu asiyefaa kitu, mtu wa uovu; Huenda njiani mwenye kinywa cha upotofu.

13 HUKONYEZA KWA MACHO, hunena kwa miguu, Huwaashiria watu kwa vidole vyake”

Na kukonyeza kwa siku hizi kumezidi hata kule kunakojulikana kwa kutumia jicho, zipo ishara nyingi za kukonyeza inategemea na mahali husika. Wakati mwingine hata lugha Fulani inaweza kutumika kukonyeza.

Sasa biblia inasema watu wa namna hiyo huleta masikitizo. Na masikitizo hayo huja kote kote, kwake, pamoja na kwa yule aliyemkonyeza. Ikiwa na maana mwisho wake hauwi mzuri sikuzote. Ni uchungu na majuto.

Biblia inatuonya tusiwe watu wa hila, za kutumia ishara za udanganyifu kuleta madhara, au uharibifu kwa wengine.

Hilo ni kosa.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

Mfalme Ahazia alianza kutawala akiwa na umri gani?

SWALI: tukisoma  2Mambo ya Nyakati 22:2.Inasema Hivi..

“Ahazia alikuwa na umri wa miaka AROBAINI NA MIWILI ALIPOANZA KUTAWALA; akatawala mwaka mmoja huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Athalia binti Omri”.

NA tena Tukisoma  2Wafalme 8:26 inasema Hivi..

“;Ahazia alikuwa na umri wa miaka ISHIRINI NA MIWILI ALIPOANZA KUTAWALA; akatawala mwaka mmoja huko Yerusalemu. Na jina la mamaye aliitwa Athalia binti Omri mfalme wa Israeli”.

>>Hapa sijaelewa Kwenye Hizi Habari Kwa maana Kwenye 2Nyakati unasema Ahazia alianza kutawala akiwa na miaka 42 ila Kwenye 2Wafalme Inasema Ahazia alianza kutawala Akiwa na miaka 22..Naona Hii mistari Kama Inajipinga Yenyewe.

Umri hasaa wa Ahazia alipoanza kutawala ni upi?


JIBU: Vifungu hivyo vinaonekana kama vinajipinga, aidha kimojawapo kimekosewa au vyote, wengine wanasema ni hitilafu katika uchapishaji wa maandiko ya kale. Lakini kama ingekuwa ni hitilafu kwenye  uchapishaji, ni wazi kuwa tangu zamani Wayahudi wangeshaliona hilo na kulirekebisha, kwasababu wale wapo makini sana katika uandishi wao, hususani katika mambo matukufu ya Mungu,  lakini maandiko hayo yalikuwepo hivyo hivyo kwa maelfu ya miaka mbeleni. Na hawakuona hitilafu yoyote.

Lakini swali ni je, Ahazia alianza kutawala akiwa na umri wa miaka mingapi?

Ukweli ni kwamba alianza kutawala akiwa na miaka 22, kwasababu kama angekuwa ameanza kutawala akiwa na miaka 42, maandiko yangekuwa yamekosewa kwasababu utawala wa baba yake uliisha akiwa na umri wa miaka 40  (Soma 2Wafalme 8:17, 2Nyakati 21:20) . Hivyo, kama  Ahazi angekuwa ameanza kutawala akiwa na umri wa miaka 42 basi angekuwa amemzidi baba yake kwa umri wa miaka 2 zaidi jambo ambalo haliwezekani kabisa.

Lakini ni kwanini, sehemu nyingine ionyeshe alianza kutawala akiwa na miaka 22, na sehemu nyingine miaka 42?

Zipo thathimini nyingi, lakini tukitazama historia fupi  ya baba yake huyu Ahazia itatupa mwanga kidogo wa kuelekewa kwenye jibu letu. Baba yake huyu Ahazia aliitwa, Yehoramu. Yehoramu alikuwa ni mtawala mbaya sana mwenye uchu wa madaraka na ubinafsi, kwani hata Baba yake (Yehoshafati) alipokufa, licha ya kwamba aliwaachia mali nyingi yeye pamoja na ndugu zake, lakini pamoja na hayo alikwenda kuwaua wote, ili yeye avimiliki vyote.

Tendo hilo la kumwaga damu zisizokuwa na hatia za kuwaua ndugu zako, lilimuhuzunisha sana Mungu, ndipo Mungu akamlaani kwa kumpiga  na ugonjwa huo usiokuwa na tiba wa kutokwa na utumbo.

Hivyo, hilo lilimfanya asiweze, kutawala vema katika hali ile ya kuugua..akawa kama mtu wa kukaa ndani tu aliyetengwa.

Sasa kumbuka na biblia haieleze kama alikufa kwanza ndipo mtoto wake, akachukua ufalme, hapana, inasema, alianza kutawala akiwa na miaka32, kisha akatawala miaka 8 tu. Lakini haisemi kwamba alikufa, hapana, kwahiyo pengine aliendelea kuishi, kwa kipindi kingine mbele akiwa kama mfalme asiyekuwa na kazi yoyote.

Hiyo ikapelekea wenyewe wa Yerusalemu kumfanya mwanawe kuwa mfalme, hivyo Ahazia akawa mfalme akiwa na umri wa miaka 22, lakini hakuwa mfalme kamili kabisa,kwasababu baba yake alikuwa bado hajafa. Ndipo alipokuja kufa huko mbeleni, Ahazia tayari alikuwa ameshafikisha umri wa miaka 42, ndipo wakamfanya kuwa mfalme kamili wa Yerusalemu. Akatawala miaka mmoja tu. Ambao ulianza kuhesabiwa katika umri wake wa 42

Hivyo biblia  inaposema alianza kutawala akiwa na miaka 22 katika kitabu cha Wafalme, na miaka 42 katika kitabu cha Mambo ya Nyakati, biblia haijipingi, ni pengine tumekosa historia ya kutosha ya matukio yote ndani ya biblia ndio maana tunaona kama baadhi ya vifungu vimekosewa, lakini ukweli ni kwamba maandiko matakatifu hakuna mahali yalipokosewa..

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Je! Ni ipi tarehe sahihi Evil-merodaki alimtoa Yekonia gerezani?

MAPEPO YANATAFUTA HIFADHI NDANI YAKO KWA BIDII SANA.

Biblia ilimaanisha nini iliposema “Mwanamke atamlinda mwanamume” Yeremia 31:22?

KURUDI ISRAELI KWASASA NI KUGUMU, SIO KAMA KULE MWANZONI.

Maseyidi 12 wa Ishmaeli, ni wakina nani?.2)Taa ya Mungu ambayo ilikuwa haijazima wakati wa Eli ni ipi?

Rudi nyumbani

Print this post

Biblia ilimaanisha nini iliposema “Mwanamke atamlinda mwanamume” Yeremia 31:22?

JIBU: Tusome,

Yeremia 31:22 “Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume”.

Katika biblia hususani agano la kale utaona sehemu nyingi, Mungu akilifananisha Taifa la Israeli na mwanamke aliyeolewa, na Bwana Mungu mwenyewe akijifananisha kama Mume wa Taifa hilo, Ndio maana mwanzo kabisa katika zile amri kumi alizozitoa Mungu, alianza na kusema yeye ni Mungu mwenye “Wivu”, wivu unaozungumziwa hapo ni wivu wa mwanaume kwa mke wake.

Kwahiyo popote pale Israeli ilipoasi na kumwacha Mungu na kwenda kuabudu miungu mingine, katika roho ilitafsirika kama ni mwanamke aliyemwacha mumewe na kwenda kufanya uzinzi nje ya ndoa. Kwahiyo Taifa la Israeli lilifananishwa na mwanamke aliyeolewa, au binti aliyeposwa.. unaweza kusoma hayo binafsi katika mistari ifuatayo. (Isaya 54:5, Yeremia 3:1-14, Yeremia 13:27, 1Nyakati 5:25, Hosea 3:1-5, Zaburi 106: 33-41, Ezekieli 23:21-29).

Kwa msingi huo, tunaweza kurudi kusoma Yeremia 31:22 “Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume”.

Hapo mwanamke anayezungumziwa ni Israeli (Yaani Taifa la Mungu), Huyo ndiye binti mwenye kuasi, kwanini ametajwa kama binti mwenye kuasi, ni kwasababu alikuwa amemwacha Mungu ambaye ndiye mume wake na kwenda kutanga-tanga kuabudu miungu mingine.

Sasa hapo anasema Bwana ameumba jambo jipya.. “mwanamke atamlinda mwanamume”..maana yake hapo kale ni “mwanamume ndiye aliyekuwa anamlinda mwanamke”. Sasa kulinda kunapozungumziwa hapo sio ulinzi dhidi ya maadui, La!. Bali ulinzi wa kimapenzi. Maana yake katika jambo hilo jipya, Mwanamke atakuwa na wivu mwingi juu ya mume wake, Maana yake atakapoona mumewe kamwacha, atajisikia vibaya na wala hataruhusu hilo jambo, wakati wote atatamani awe karibu na mume wake kuliko kawaida, hatoruhusu mahusiano yake yaharibike kwa vyovyote vile. Tofauti na hapo kwanza ambapo Mwanamume ndiye aliyekuwa anatia bidii kumlinda  mkewe.

Sasa tafsiri yake katika roho ni kwamba wakati utafika ambapo Taifa la Mungu ambalo linafananishwa na mwanamke, litakuwa linampenda Mungu sana, na kumtafuta, na kumwonea Mungu wivu lenyewe..Maana yake Mungu ataweka kitu ndani ya watu wake ambacho kitawafanya wao wenyewe watafute kumpenda Mungu sana na kwa bidii. Ndio maana mbele kidogo katika hiyo hiyo sura ya 31, ya kitabu hicho hicho, utaona Bwana Mungu analiweka hilo sawa, kwamba itakuwaje.

Tusome..

Yeremia 31:31 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.

 32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa MUME KWAO, asema Bwana.

  33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

 34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena”.

Umeona hapo?..Mstari wa 32 anasema “ingawa nalikuwa mume kwao”. Lakini agano lake walilivunja…Lakini katika agano hilo jipya, wao wenyewe watamtafuta Mungu, hawatahitaji tena kusukumwa sukumwa. Kuna kitu kitaingia ndani yao ambacho kitawafanya waulinde upendo kwa Mungu wao.

Na agano hili jipya, au “jambo jipya” lilianza siku ile ya Pentekoste ambapo Roho Mtakatifu alishuka katikati ya watu wake, siku hii, ndipo wakati ambapo Mungu alianza kutia sheria ndani ya mioyo ya watu, kiasi kwamba kwa yeyote ambaye atapokea Roho Mtakatifu, hatahitaji tena kusukumwa sukumwa katika kumtafuta Mungu, kuna kiu Fulani ya kipekee itaingia ndani yake, hiyo itampeleka mwenyewe kumtafuta Mungu, atajikuta tu anatafuta kuulinda uhusiano wake na Mungu usipotee (Hapo anamlinda mwanamume wake yaani Yesu), hatahitaji kuambiwa na Mungu hapaswi kujichubua, hapaswi kuiba, hapaswi kubeti, hapaswi kuvaa nguo nusu utupu, kwani ndani yake tayari ipo sheria, iliyoingia, ambayo inamshuhudia kabisa kwamba anapovaa mavazi yasiyompasa anafukuza uwepo wa Mungu ndani yake.

Kwahiyo kwa mtu aliyepokea Roho Mtakatifu, tayari jambo jipya limeumbika ndani yake. Na biblia inasema wote wasio na Roho Mtakatifu hao sio wake (Warumi 8:9). Na habari nzuri ni kwamba Roho Mtakatifu sio wa watu baadhi tu Fulani. La!.. Bali ni zawadi kwa wote ambao wanamkimbilia Bwana.

Matendo 2:39 “Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”.

Kwahiyo tunaishi katika siku ambazo ili kumpendeza Mungu ni lazima tuwe na Roho Mtakatifu. Swali ni je! Jambo jipya limeumbika moyoni mwako?..Je kuna nguvu inayokusukuma kwa Mungu? Je kuna hofu ya Mungu ndani yako ambayo inakufanya uhakikishe unaulinda wokovu wako?..Kama ndiyo basi usimzimishe huyo Roho aliyeko ndani yako, kwasababu huyo ndio Muhuri wa Mungu kwetu (Waefeso 4:30). Lakini kama hiyo nguvu haipo ndani yako, basi unaihitaji leo kwasababu pasipo Roho kamwe hatuwezi kumkaribia Mungu.

Hivyo kama unataka kumpokea Roho Mtakatifu maishani mwako, ni sharti kwanza umwamini Yesu maishani mwako, kwamba alikuja kufa kwaajili ya dhambi zako, na pia akafufuka, na sasa anaishi. Na baada ya hapo, tubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, hakikisha unaziacha kwa vitendo, maana yake kama ulikuwa unaiba unaacha kuiba,kama ulikuwa mzinzi unaacha uzinzi, kama ulikuwa unaufuata ulimwengu huu, unaacha. Na baada ya hapo Roho Mtakatifu ataanza kukupa amani, ambayo itakamilika baada ya wewe kwenda kubatizwa ubatizo sahihi, kama bado hujabatizwa. Ubatizo sahihi ni ule wa kuzama kwenye maji tele na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38, 8:16, 10:48, 19:10).

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Nini maana ya “wanawake saba watamshika mtu mume mmoja”

KWANINI UNAPASWA UWE BIBI ARUSI NYAKATI HIZI ZA MAJERUHI?

NA ROHO NA BIBI-ARUSI WASEMA, NJOO!

KARAMU YA MWANA-KONDOO.

Rudi nyumbani

Print this post

Shubaka ni nini kibiblia? (Mithali 7:6)

Shubaka ni dirisha, lililojengwa kwa kupishanisha vipande vya mbao au chuma au kitu kingine chochote, kama pazia, katikati ya dirisha hilo. Tazama picha.

Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili,

Ujenzi wa madirisha mengi ya kisasa, Haupo kwa muundo huo. Madirisha ya kisasa, yapo wazi sana, nikiwa na maana huwezi kuona kitu chochote kimekatiza katikati,pengine utakuta ni kioo tupu eneo lote, lakini kwa zamani madirisha ya shubaka yalikuwa ni kawaida kuyakuta karibu katika nyumba zote.

Neno hilo kwenye biblia utalipata katika habari hii;

Mithali 7:4 “Mwambie hekima, Wewe ndiwe umbu langu; Mwite ufahamu jamaa yako mwanamke.

5 Wapate kukulinda na malaya, Na mgeni akubembelezaye kwa maneno yake.

6 Maana katika dirisha la nyumba yangu Nalichungulia katika SHUBAKA YAKE;

7 Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili,

8 Akipita njiani karibu na pembe yake, Akiishika njia iendayo nyumbani kwake, 9 Wakati wa magharibi, wakati wa jioni, Usiku wa manane, gizani.

10 Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;

11 Ana kelele, na ukaidi; Miguu yake haikai nyumbani mwake.

12 Mara yu katika njia kuu, mara viwanjani, Naye huotea kwenye pembe za kila njia.

13 Basi akamshika, akambusu, Akamwambia kwa uso usio na haya,

14 Kwangu ziko sadaka za amani; Leo hivi nimeziondoa nadhiri zangu;

15 Ndiyo maana nikatoka nikulaki, Nikutafute uso wako kwa bidii, nami nimekuona.

16 Nimetandika kitanda changu, magodoro mazuri, Kwa matandiko ya Kimisri yenye mistari.

17 Nimetia kitanda changu manukato, Manemane na udi na mdalasini.

18 Haya, na tushibe upendo hata asubuhi, Tujifurahishe nafsi zetu kwa mahaba. 19 Maana mume wangu hayumo nyumbani, Amekwenda safari ya mbali;

20 Amechukua mfuko wa fedha mkononi; Atarudi wakati wa mwezi mpevu.

21 Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda.

22 Huyo akafuatana naye mara hiyo, Kama vile ng’ombe aendavyo machinjoni; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu;

23 Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.

24 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu.

25 Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake.

26 Maana amewaangusha wengi waliojeruhi, Naam, jumla ya waliouawa naye ni jeshi kubwa.

 27 Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti”.

22 Huyo akafuatana naye mara hiyo, Kama vile ng'ombe aendavyo machinjoni; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu;

Hiyo ni kutukumbusha kuwa, Mungu pia, anatutazama kutoka juu mbinguni akiyaangalia matendo yetu, na mienendo yetu katika madirisha na shubaka zake mbinguni, yeye ndiye anayechunguza na kujua siri zote za mioyo ya watu, na mwisho wake utakuwaje. Hivyo ni wajibu wetu tusiwe wajinga kama yule kijana, bali tuikwepe mitego ya ibilisi kwa kuzishika amri za Mungu na kuziishi.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

Maseyidi 12 wa Ishmaeli, ni wakina nani?.2)Taa ya Mungu ambayo ilikuwa haijazima wakati wa Eli ni ipi?

SWALI: Naomba kuuliza watumishi wa Mungu katika Mwanzo 17:20 anaposema kwa habari ya Ishmaeli atazaa maseyidi 12, hao ndio akina nani kwa Sasa?

2) Pia katika 1samweli 3:3 anasema kipindi Samweli anaitwa na Mungu taa ilikua haijazimika bado Nia taa gani hiyo? Asante Sana Ni hayo.


JIBU: 

  1. Tusome..

Mwanzo 17:18 “Ibrahimu akamwambia Mungu, Lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako.

19 Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake.

20 Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu”.

Neno Seyidi linamaanisha  mtawala, hivyo hapo biblia ilimaanisha kuwa Ishmaeli atazaa watawala 12.. ambao  utaona wakitajwa kwa majina  katika Mwanzo 25:13

Mwanzo 25:13 “Na haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, kwa majina yao, na kwa vizazi vyao. Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, ni Nebayothi, na Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu,

14 na Mishma, na Duma, na Masa,

15 na Hadadi, na Tema, na Yeturi, na Nafishi, na Kedema.

16 Hao ndio wana wa Ishmaeli, na hayo ni majina yao, katika miji yao, na katika vituo vyao, maseyidi kumi na wawili kwa kufuata jamaa zao.

Katika historia  wana hawa wa Ishmaeli walikuwa watu wakuu sana, na ndio chimbuko la mataifa ya kiharabu tunayoyaona sasahivi  kule mashariki ya kati.

2) Je ni Taa ipi hiyo inayozungumizwa katika 1Samweli 3:1?,

Tusome.

1 Samweli 3:1 “Basi, mtoto Samweli akamtumikia Bwana mbele ya Eli. Na neno la Bwana lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri.

2 Ikawa wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona),

3 na taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la Bwana, palipokuwa na sanduku la Mungu;

Inadhaniwa kuwa hiyo ni ile taa ya hekaluni, lakini ukitafakari kwa ukaribu, utaona kuwa biblia haikumaanisha ile taa ya hekaluni au ile ya kwenye hema ya kukutania, bali ilimaanisha pumzi au uhai wa Eli, ukikumbuka kuwa habari iliyokuwa inazungumziwa hapo juu ni kuhusu uzee wa Eli, ambapo inasema umri wake ulikuwa umeshaenda sana mpaka macho yake yalikuwa yameshaanza kupofuka.

Biblia inasema..

Mithali 20:27 “Pumzi ya mwanadamu ni taa ya Bwana; Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake”.

Unaona? Hivyo hapo ilimaanisha kuwa Pumzi ya uhai wa Eli ilikuwa bado haijamuacha.

Hiyo ni kutukumbusha pia, kuwa upo wakati na sisi Taa ya Mungu itazima ndani yetu. Na kama tunavyojua taa ikizimika huwa kunakuwa na giza na sikuzote gizani hakuna shughuli yoyote inayoendelea. Vivyo hivyo na siku ambayo kila mmoja wetu atakufa, huko atakapoenda hakuna jambo lolote la kimaendeleo atakalolifanya, Hatakuwa na nafasi ya pili ya kutubu ikiwa alikufa katika dhambi, hatakuwa na nafasi ya pili ya kufanya marekebisho ikiwa alizembea zembea katika masuala ya wokovu wake akiwa hapa duniani. Atakachokuwa anasubiria huko ni hukumu tu.

Mhubiri 9:5 “kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa”.

Hivyo tunapaswa tujithamini maisha yetu tunamalizaje mwendo tukiwa hapa duniani? . Kwasababu huko ng’ambo hakuna nafasi ya pili.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

Wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa.

SWALI: Biblia inamaanisha nini iliposema “wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa;?

JIBU: Tusome vifungu vyenyewe..

2Petro 2:12 “Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao;

13 Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, WAKIDHANIA KUWA ULEVI WAKATI WA MCHANA NI ANASA; wamekuwa ni mawaa na aibu wakifuata anasa zisizo kiasi katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi”;

Hapa Mtume Petro, alikuwa anaeleza jinsi watu waovu wanavyoenenda katika tamaa za mwili, ukisoma tokea juu utaona akiwafananisha na watu wa Sodoma na Gomora..Na moja ya tabia zao ndio hiyo aliyosema “Wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa” akiwa na maana kuwa, wamefikia hatua ambayo kwao anasa zao kama ulevi hawazifanyi tena usiku, bali hata mchana.

Ikumbukwe kuwa anasa zote huwa zinajulikana kuwa zinafanyika usiku.. Na ndio maana wakati ule wa Pentekoste, Roho aliposhuka, wale watu waliwashutumu mitume kuwa wamelewa kwa mvinyo, Lakini Petro aliwaaambia, hakuna aliyelewa, kwasababu sasa hivi ni saa tatu ya mchana (akiwa na maana ni saa 9 alasiri), hakuna mtu anayelewa muda huo.

Matendo 2:13 “Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya.

14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.

15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana”;

Soma pia..

1Wathesalonike 5:7 “Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku”.

Umeona, hivyo mpaka mtu imetokea anafanya anasa kama ulevi wakati wa mchana,. Ni mtu aliyevuka mipaka, haoni tena shida kufanya mambo yake maovu hadharani amewazidi hata  wenye dhambi wengine wafanyao mambo kama hayo.Ndivyo walivyofanya watu wa Sodoma na Gomora, walivuka mipaka waliuanika ushoga wao hadharani, bila aibu yoyote.

Ni kama vile tu leo hii, hakuna staha tena duniani, mambo ya giza yanafanyika wazi kwenye matamasha, kwenye TV, yanatumwa Whatsapp, yanaonekana Youtube na kwenye mitaa yetu.

Hii ni kuonyesha kuwa tunaishi katika majira ya kurudi kwa pili kwake Yesu Kristo. Wakati huu ni wa kuilinda mioyo yetu isilemewe na mambo ya kidunia, kama alivyofanya Lutu alivyokuwa Sodoma. Kwasababu ulimwengu huu utakwenda kuangamizwa kwa moto muda si mrefu, kama mtume Petro alivyomalizia kusoma katika waraka huo.

2Petro 3:10 “Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,

12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?”

Je umeokoka? Je parapanda ikilia leo unaouhakika wa kwenda mbinguni?. Majibu sote tunayo.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

KURUDI ISRAELI KWASASA NI KUGUMU, SIO KAMA KULE MWANZONI.

Isaya 10:22 “Maana watu wako, Ee Israeli, wajapokuwa wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki tu watakaorudi; kuangamiza kumekusudiwa, kunakofurika kwa haki”.

Wana wa Israeli walidhani, kuchukuliwa tena utumwani na kurudishwa (Babeli na Misri)  kungekuwa ni kurahisi kama ilivyokuwa wakati ule walipotolewa Misri. Walidhani Mungu atakuja kuwatoa tena kama taifa kwa mkono hodari wa nabii kama Musa, na wote watarudi nchi yao.

Lakini mambo hayakuwa hivyo, Mungu aliwaonya mapema akiwaambia hilo jambo halitakuwepo, na ndio maana alitumia muda mrefu sana kuwasihi, watubu waache njia zao mbaya, lakini hawakusikia badala yake wakawa wanawapiga manabii wake na wengine kuwaua,

Lakini siku ya siku ilipofika, yale mataifa 10 yalichukuliwa utumwani Ashuru,  na biblia inatuonyesha hakuna hata mmoja aliyerudi hadi wakati huu wa sasa.. watu wote waliendelea kubaki kule kule,  hata na lile taifa moja la Yuda, ambalo lilikuja kuchukuliwa nalo baadaye Babeli na Nebukadreza, japokuwa nalo lilikuwa na watu wengi sana, lakini ni kikundi kidogo sana, yaani watu wachache sana ndio Mungu aliwarudisha, na hiyo ilikuwa tu ni kuwatunzia uzao vinginevyo wangefananishwa na Sodoma na Gomora, kwa jinsi ambavyo wangepotea wote.

Warumi 9:27 “Isaya naye atoa sauti yake juu ya Israeli, kusema, Hesabu ya wana wa Israeli,ijapokuwa ni kama mchanga wa bahari,ni mabaki yao tu watakaookolewa.

28 Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya nchi, akilimaliza na kulikata.

29 Tena kama Isaya alivyotangulia kunena, Kama Bwana wa majeshi asingalituachia uzao, Tungalikuwa kama Sodoma, tungalifananishwa na Gomora”.

Sasa biblia inasema mambo hayo yaliandikwa kwa mifano ili kututahadharisha na sisi tulio katika nyakati hizi za hatari (1Wakorintho 10:11). Kwasababu kanisa la Israeli la mwilini lilikuwa linawakilisha kanisa la Kristo la rohoni sasa hivi. Kumbuka mara baada ya Israeli kuingiliwa na ukengeufu,  pale walipoanza kuabudu miungu mingine, hapo ndipo Mungu alipokusudia kuwaangamiza wote, mikononi mwa maadui zao.

Vivyo hivyo na katika Kanisa la Kristo leo hii, Bwana alishatabiri kuwa kuwa kuna majira litaingiliwa na ukengeufu..ndio yale magugu yaliyopandwa na ibilisi ndani ya kanisa (Mathayo 13:24-30).. Sasa ukengeufu huu, ndio unaowafanya wakristo wengi wawe vuguvugu kupita kiasi, Hatushangai kuona idadi ya watu wanaojiita wakristo duniani ikizidi kuongezeka, sasa hivi ni Zaidi ya bilioni tatu.. Ni kama mchanga wa bahari tu, hata zaidi ya walivyokuwa Israeli.

Lakini hiyo sio tija kwamba wote tutaokolewa siku ile.  Ni mabaki tu ndio yatakayookoka, ambayo Yesu aliyafananisha na ‘kundi dogo’

Luka 12:32 “Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme”.

Na ndio maana Bwana Yesu alisema. Walioitwa ni wengi lakini wateule ni wachache. Hichi ni kipindi cha kurekebisha mienendo yetu kama wakristo, kwasababu kurudi Yerusalemu kwa sasa ni kugumu sio kama kule kwa kwanza. Nguvu ya kukuvuta umgeukie Mungu sasa sio kama ile ya kwanza ulipoanza kuamini.

Ni wachache tu ndio watakaorejea, na sisi tuwe miongoni mwa hao. Mungu anatuita kuache dhambi, tumgeukie yeye, tusiungalie ulimwengu, kwani unapoteza sana.. Kwasababu hizi ni nyakati za mwisho na Kristo yupo mlangoni, wakati huu ni ule wa kumalizia, siku yoyote, wakati wowote, tunaweza kushuhudia tendo hilo kuu la unyakuo. Ambapo kwa upande mmoja utakuwa ni furaha na shangwe, lakini kwa upande mwingine kilio na kusaga meno na majuto makubwa.

Bwana atusaidie.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Ni nani aliyesema “Nitume mimi”? katika (Isaya 6:8)

PINDO LA VAZI LAKE SASA LIMEREFUSHWA.

JE UPENDO WAKO UMEPOA?

Fuawe ni nini? Kama tunavyosoma katika Isaya 41:7

EPUKA KUUNDA MATARAJIO YAKO, KWENYE AHADI ZA MUNGU.

Rudi nyumbani

Print this post

Amri zilizo ndogo alizozizungumzia Yesu ni zipi?

SWALI: Tukisoma  Mathayo 5:19 Inasema..

“Basi mtu ye yote atakayevunja AMRI MOJA katika hizi ZILIZO NDOGO, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu ATAKAYEZITENDA na KUZIFUNDISHA, huyo ataitwa MKUBWA katika ufalme wa mbinguni”.

Swali langu 👆Amri ndogo zinazozungumziwa hapo ni zipi? Ningependa kuzijua!

Kama kuna Amri ndogo ,bila shaka na Amri kubwa au kuu zitakuwepo pia ningependa kufahamu hilo.

Asante na Mungu awabariki kwa majibu yenu.


JIBU: Ukisoma maneno ya juu yake yaliyotangulia utaona anasema.. sikuja kuitangua torati bali kuitimiliza, Hii ikiwa na maana kuwa vipo vipengele vya torati ambavyo havikukamilika, au havikueleweka kwa wengi ndio sasa yeye akaja kuviweka sawa, na kuvimalizia..

Sasa kwa wayahudi (Yaani mafarisayo  na waandishi) waliona kama ni sheria mpya Yesu anawaletea watu, sheria ambazo Musa hakuziandika, visheria vidogo vidogo ambavyo si lazima mtu kuvishika, japo vinaelezea uhalisia.

Kwa mfano Musa aliwaagiza wasizini, lakini jambo lingine lolote linalohusiana na uzinzi, kama vile kutazama pornography, au kufanya masturbation ni sawa, lakini Yesu alipokuja na sheria mpya kwamba kila amtazamaye mwanamke kwa kumtamani ameshakwisha kuzini naye.. Waliona kama ni jambo la ziada  (kama sheria ndogo tu), lakini hawajui kuwa mtu ambaye atazishika hizo ndizo zitakazomfanya awe mkubwa sana katika ufalme wa mbinguni.

Vilevile Musa alisema usiue, lakini Bwana Yesu akasema mtu atakayemwonea ndugu yake hasira tayari ni muuaji. Hivyo hatupaswi kuwekeana  vinyongo sisi kama ndugu, haijalishi tumeudhiana sana kiasi gani. Sasa ikitokea unapuuzia maneno haya, ujue kuwa katika ufalme wa mbinguni unaonekana ni mdogo sana, haijalishi kuwa hujawahi kufikiria hata kuua.

Musa alisema Jicho kwa jicho, na jino kwa jino, lakini Yesu alisema, tusishindane na watu waovu, mtu akupigaye shavu la kuume mgeuzie na la kushoto.

Musa alisema, usiape uongo, lakini Yesu alisema usiape kabisa kwa kiapo chochote.

Alisema tena mpende jirani yako, mchukie adui yako, lakini Yesu alisema wapendeni adui zenu waombeeni wanaowaudhi..n.k n.k.

Sasa amri kama hizo za Yesu  zilionekana ni ndogo hivyo zikadharauliwa, wengi wakawa hawazishiki, ni sawa na leo hii tu, mtu akuambie umuombee adui yako, ni jambo ambalo unaweza ukalidharau, na ndio maana huwezi kulisikia kwenye vinywa vya watumishi, vilevile ni ngumu kuviona watu wakiviishi, zinapuuziwa lakini ndizo zinazotupa ukubwa mbinguni.

Ndio maana Yesu alisema pale juu.. “Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni”(Mathayo 5:20).

Akiwa na maana tukiyatenda tu yale ambayo watu wa dini wanayatenda kwa desturi na mazoea, hatuna cha ziada ndani yetu, tujue kuwa mbinguni hatutaingia.

Nasi tunafundishwa, tuyashike kwa kuyaishi na kuyafundisha, sana hayo maagizo ya Yesu, ambayo ndio yanayokamilisha torati nzima. Soma  kitabu Mathayo sura ya 5 mpaka ya 7 utapata maagizo hayo yote kwa urefu.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

TUTAMKARIBIA MUNGU KWA IDADI YA MVI ZETU ROHONI.

Shalom, nakukaribisha katika kuyatafakari maneno ya uzima, biblia inatuambia..

Mithali 16:31 “KICHWA CHENYE MVI NI TAJI YA UTUKUFU, Kama kikionekana katika njia ya haki”.

Wengi wetu tunatafuta wokovu ili tu tuende mbinguni,  tunadhani wokovu ni kumkiri tu Yesu na kubatizwa, basi imeishia hapo, tunachosubiria tu ni  kufa na kwenda mbinguni.. Ndugu Mawazo kama hayo ndiyo yanatufanya kila siku tuwe watu wa kulegea legea watu wa kusubiri subiri,tukisema siku moja wataokoka, siku tunayokaribia kufa, siku ambayo tukishatimiza malengo yetu ndio tutakayomtumikia Mungu, hatujui kuwa kuchelewa kwetu kunatupotezea nafasi nyingi na kubwa sana mbinguni.

Ndugu yangu, maisha ya mwilini ni kivuli tosha cha maisha ya rohoni. Kama vile katika mwili kuna hatua, ya utoto, utu uzima na uzee, na kwamba ili mtu afikie ile ya mwisho ni lazima azipitie hizi za kwanza zote, vivyo hivyo na rohoni..

Kumbuka Uzee siku zote una kibali, una heshima,  na una utukufu,

Biblia inasema..

Walawi 19:32 “Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee; nawe mche Mungu wako, Mimi ndimi Bwana”.

 Unaona na utukufu wake unadhihirishwa kwa zile mvi zinazotokea juu ya kichwa chake. Hali kadhalika rohoni, kwa jinsi mtu anavyokua kiroho, anavyodumu katika wokovu, anavyomtumikia sana Bwana, ndivyo mvi zake zinavyoongezeka kidogo kidogo, na kwa jinsi atakavyoendelea kung’ang’ana na Bwana atafikia  hatua kichwa chake chote kinajaa mvi, kinakuwa cheupe pe chote.

Ukishafikia hatua hiyo rohoni, ujue wewe ni mtu ambaye utakuwa karibu sana na Mungu utakapofika mbinguni.

Ukisoma kitabu cha Ufunuo, utawaona kuna wazee 24 mbinguni, Wale ni malaika wa Mungu, ambao wanafanana na wanadamu wazee, utajiuliza ni kwanini Mungu kawaweka pale kama wazee  na si vijana au watoto ili wakizunguke kiti chake cha enzi, tena wakiwa katika idadi yao hiyo ndogo ya 24?. Hiyo ni kuonyesha kuwa watu wa namna hiyo, ndio watakaokuwa karibu sana na Mungu hata wakati ule ukifika.

Ufunuo 4:3 “na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi.

4 Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu”.

Na kama tunavyojua ili kumtambua mzee  utaona mvi nyeupe katika kichwa chake. Katika biblia tunamwona Bwana wetu Yesu Kristo akiwa kama mzee wetu wa kwanza rohoni mwenye nywele hizo nyeupe..

Ufunuo 1:14 “Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto”;

Sasa kama tulivyosema, mpaka mtu afikie hatua ya uzee, ni sharti kwanza apitie utoto na ujana,..Vivyo hivyo rohoni ili tufikie ukomavu Mungu anaoutarajia kwetu hatuna budi kuukulia wokovu vya kutosha angali tukiwa hapa hapa duniani.

Inashangaza kuona mtu anayachukulia maisha yake ya rohoni, kirahisi rahisi tu, leo inapita bado yupo katika dhambi, kesho nayo hivyo hivyo, mwezi unapita, miaka inapita, anasikia tu injili anapuuzia, bado hajali maisha yake ya milele yatakuja kuwaje huko atakapokwenda, yeye anajitaabisha tu na haya maisha ya kitambo ya miaka 80, lakini yale ya mabilioni ya miaka hayaangalii. Anadhani kule ni kufa na kuingia tu, hajua kuwa zipo nafasi na vyeo, ambavyo si watu wote watapewa na Mungu.

Mwingine atasema ameokoka, lakini miaka nenda rudi, bado ni mchanga kiroho, hakui yupo pale pale, maisha yake hayana ushuhuda, ukimuuliza ni nini umefanya kwa Mungu wako, hana, yeye ni kusikiliza tu, basi, akidhani ndicho Mungu alichotuitia hapa duniani.

Tunapaswa tukifika kule tutambuliwe kwa mvi zetu rohoni, tumemtumikia Mungu wetu kweli kweli, sio tunatambuliwa kama vitoto vichanga tena.

Unapoyasikia maneno haya, usiyapuuzie, kumbuka unapaswa uwe ndani ya Kristo ukimtumikia kwa muda wa kutosha ukiwa hapa duniani, ili ujijengee daraja zuri kule unapokwenda, usidhani wokovu ni kuamini tu basi..wokovu ni maisha, kila siku unajenga maisha yako ya baadaye, kama vile unavyojijengea maisha yako ya mwilini.

Hivyo mimi na wewe kuanzia sasa, tutamani kuwa karibu na Mungu, kwasababu tukifa kule tutatambuliwa kwa idadi ya mvi zetu rohoni.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

Bwana Yesu alimaanisha nini kusema “yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari?”

SWALI : Shalom .. Tukisoma Mathayo 5:43-45 Inazungumzia juu ya mtu ili awe mkamilifu hana budi kumjali mwingine hata kama Anatukosea,kwamba sisi tumeambiwa tuwaombee tuwapende N.K..Sasa tukisoma tena Mathayo 18:6..Inasema Hivi..

“Bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.”..Sasa Hapa mtumishi Sjaelewa kwenye Haya maneno aliyoyazungumzia Bwana katika huu mstari, Kwasababu Mathayo 5:43-45 inasema tuwaombee ila hapa Mathayo 18:6 inasema afadhali Afungiwe jiwe ikiwa na maana Aangamizwe..Naona pananitatiza kidogo


JIBU: Bwana Yesu alisema hivi katika Mathayo 5:43-44

“43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;

44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,”

Bwana alimaanisha kweli kusema hivyo, kwa namna ya kawaida ukishakuwa  mwanadamu tu, mwenye kitu Fulani kipekee ndani yako, ni lazima utakuwa tu na maadui, wengine watakuwa maadui zao kutokana na wivu, aidha  wa utumishi wako, au ndoa yako, au mafanikio yako, au cheo chako, au kipawa chako, au mwonekano wako, n.k.  Na wivu huo unaweza kufikia hatua hata ya hao watu kutaka kukuua.

Lakini ukijikuta katika hali kama hiyo  wewe kama mkristo unapaswa ufanyaje? Je na wewe uwalipizie kisasi, jibu ni la hapo unapaswa tuwe kama Bwana Yesu alivyokuwa, pale ambapo walimtundika msalabani aliwaombea msamaha, pale ambapo Stefano anauliwa kwa kupigwa mawe mbele ya Paulo aliwaombea na kusema Bwana asiwahesabie kosa lile.

Umeona ni jukumu letu kuwaombea rehema.

Lakini pamoja na hayo kuna wakati mtu anafanya makosa kinyume na Mungu mwenyewe, na hiyo ni hatari zaidi, kwasababu japo Mungu  kasema yeye ni mwingi wa rehema lakini pia ni mwingi wa hasira,  Na ndio maana utasoma hapo, Bwana Yesu akisema..

Mathayo 18:6 “bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari”

Unapaswa uwe makini sana na Watu waliomwamini Bwana Yesu, hususani wale ambao ni wachanga kiroho, watu waliotubu dhambi zao na kumwelekea Bwana, kwa mioyo yao yote, halafu wewe unakwenda kuwaondoa katika mstari wa wokovu kwa namna moja au nyingine, ukifanya hivyo ujue hukumu yako ni kubwa sana.

Katika biblia utamwona mtu mmoja anaitwa Balaamu, huyu alijua kabisa wana wa Israeli wanaenda sawa na Mungu wao, sasa akatafuta njia ya kuwakosesha kwa makusudi ili wafarakane na Mungu ili waadhibiwe.. Hivyo akabuni njia ya kuwakosesha, kwa kuwaletea wanawake wa kimataifa ili wazini nao, (jambo ambalo Mungu aliwakataza wana wa Israeli)  kisha baada ya hapo Mungu awaadhibu na kuwaacha..Na kweli adhma yake ilifanikiwa, na matatizo yakawakumba kweli wana wa Israeli (Ufunuo 2:14).

Leo hii wapo watumishi wanaozini na washirika wao, mpaka imepelekea, wale wengine ambao walikuwa wameanza kuamini wameuacha wokovu, kutokana na matendo mabaya ya viongozi wao. Sasa watu kama hawa wanamudhi sana Mungu, hawajui tu. Mpaka kufikia hatua kama hiyo ya Mungu kusema..ingemfaa zaidi mtu kama huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake akatupwe baharini… Ni Kuonyesha kuwa hukumu yake ni kubwa sana…Hata akifungiwa jiwe kubwa na kwenda kutupwa kwenye vilindi vya bahari kwa tendo hilo bado Mungu anaona ni sawa tu, amestahili.

Lakini swali ni je! Kwa ruhusu hiyo, tukawafungue watu mawe shingoni? Jiulize Wewe unaweza kufanya hivyo? Unaweza kudhubutu kumtupa mwanadamu mwenzako baharini? Au ulishawahi kufanya hivyo?. Kuna wakati Mungu alikuwa anamwambia Musa kwa hasira kwamba ajitenge na wana wa  Israeli ili awaangamize kwasababu wamemwacha upesi na kugeukia kuabudu masanamu. Na yeye atamfanya kuwa taifa kubwa.

Lakini Musa alizituliza hasira za Bwana, akawaombea rehema, Sio kwamba angekubali Mungu asingetimiziwa aliyoahidiwa, angetimiza kweli, Mungu angeenda kumfanya kuwa taifa kubwa, na yeye angekuwa mfalme juu yao, lakini bado asingekuwa mkamilifu mbele za Mungu. Na ndio maana mtu kama Musa alipata kibali cha kipekee sana mbele za Mungu.

Kumbukumbu 9:12 “Bwana akaniambia, Ondoka huko, shuka upesi; kwa kuwa watu wako uliowatoa Misri wamejiharibu; wamekengeuka mara katika njia niliyowaamuru; wamejifanyia sanamu ya kusubu.

13 Tena Bwana akasema nami zaidi, akaniambia, Nimeliona taifa hili; na tazama, ni taifa lenye shingo ngumu;

14 niache, nipate kuwaangamiza, na kulifuta jina lao chini ya mbingu; nami nitakufanya wewe uwe taifa kubwa lenye nguvu kuwapita wao”.

Nasi pia, Tunapaswa tuitulize hasira ya Mungu, kwa kuwaombea rehema, na Sio kwa kuitekeleza.

Maombi ya kuwaangamiza maadui zetu, tunapaswa tujue kwa mkristo, hayana nafasi.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

NITAFANYA YERUSALEMU KUWA JIWE LA KUWALEMEA .

Kongwa ni nini kwenye biblia?(Wagalatia 5:1)

Kwanini wale dubu waliowauwa vijana wa Elisha walikuwa wa kike?

Kwanini Yesu aliwakataza mitume wake kumdhihirisha?

KWASABABU MUDA TULIOBAKIWA NAO SI MWINGI.

NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.

Rudi nyumbani

Print this post