Herode aliliwa na chango, Je, chango ni nini kibiblia?

Herode aliliwa na chango, Je, chango ni nini kibiblia?

Matendo 12:21 “Basi siku moja iliyoazimiwa, Herode akajivika mavazi ya kifalme, akaketi katika kiti cha enzi, akatoa hotuba mbele yao.

22 Watu wakapiga kelele, wakisema, Ni sauti ya Mungu, si sauti ya mwanadamu.

23 Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho”.

Hili ni pigo, na sio ugonjwa wa kawaida, na ndio maana hakuna sehemu nyingine yoyote, unaweza kuona ugonjwa huu ukirekodiwa kwenye biblia. Ni sawa na wakati ule wa Mfalme Nebukadreza, alivyojitukuza mbele za Mungu, akajiona kuwa yeye ndiye mfalme wa dunia wala hakuna mwingine kama yeye duniani kote, japokuwa kuwa alionywa hapo kabla,  kwa hizo tabia zake lakini hakusikia, hakujua kuwa ni Mungu ndiye anayewamilikisha wafalme (Danieli 2:21) lakini yeye hakulisikia hilo.. Ndipo siku ya siku malaika wa Mungu akampiga kwa pigo ambalo mpaka sasa, halijulikani lilikuwa ni pigo la namna gani lile, lililomfanya mpaka awe kama mnyama  asiyeeleweka wa kufukuzwa, mbali na makazi ya watu.

Hivyo ndivyo  ilivyomkuta na huyu Herode. Siku moja alikaa katika kiti chake cha enzi akatoa hutuba yake pengine yenye ushawishi mkubwa, hotuba yenye hoja nzuri, iliyojaa sifa na utukufu wake mwenyewe.. Na watu walipoona vile, wakapiga kelele, wakimsifia sana, Lakini ni heri wangeishia hapo, wale watu wakafakia hatua ya kusema ile ni sauti ya Mungu sio ya mwanadamu..yaani kwa namna nyingine ni Mungu ndiye aliyesimama mbele yako na kuzungumza naye. Na yeye Herode akilijua hilo, kuwa yeye ni mwanadamu tu, akazipokea sifa zile. Zilichofuata baada ya pale ni malaika wa Mungu kumpiga kwa pigo hilo la ugonjwa wa ajabu akaliwa na chango.

Chango ni funza, unaweza kutengeneza picha, unatoka muda huo huo, unaanza kuugua na funza  wanatoka katika mwili wako bado ukiwa hai mpaka unakufa. Kama tunavyojua kwa namna ya kawaida  mpaka mtu afikie hatua hiyo ni kwamba alishakufa siku nyingi, mwili ushaoza ndipo funza wanatokeza nje. Lakini yeye yalimkuta bado akiwa fresh duniani.

 Ugonjwa huu kihistoria inasemekana ulimpata mfalme mmoja aliyeitwa Antiokia Epifane,  ambaye huyu alilinajisi hekalu la Mungu zamani, kabla ya Kristo kuzaliwa, enzi ya kipindi cha Wamakabayo, hadi kufikia hatua ya kuingiza nguruwe hekaluni mambo ambayo Mungu aliyakataza, lakini baadaye Mungu alimpiga kwa ugonjwa mfano kama huu, wa majipu mabaya sana ambayo yalimfanya funza watokezee nje ya mwili wake, na kufa.

Ni ugonjwa wa maumivu makali sana,.. Ni ugonjwa ambao si wa kawaida, kwasababu ni wapigo.

Vivyo hivyo na sisi pia tunapaswa, tuwe makini sana. Watu wengi wanadhani, utukufu wa Mungu unachukuliwa pale tu miujiza au uponyaji unapofanyika, katikati ya watumishi wa Mungu.. Jibu ni lala, wote hawa tuliowasoma hawakuwa wakristo. utukufu wa Mungu unachukuliwa hata na watu wa kidunia, na wao pia wanaweza kushiriki mapigo ya Mungu vilevile kama wale wanaoitenda kazi ya Mungu..

Isaya 42:8 “Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu”.

Mungu ni Mungu mwenye wivu, unapokuwa kiongozi, halafu unataka watu wakusifie wewe, kana kwamba unafanya mambo hayo kwa nguvu zako, Humpi Mungu utukufu. uwe makini sana utaliwa na chango,

Unapojaliwa utajiri, au umaarufu kwa watu, halafu wewe kazi ya ni kujisifia tu, kujionyesha wewe ni Mungu-mtu duniani, huwi mnyenyekevu, jiangalie sana utakutwa na matatizo ambayo, hata jamii itashindwa kuelewa chanzo chake ni nini?

Jambo lolote unalolifanya liwe la ki-Mungu, au la Ki-binadamu, ambalo lina sifa yoyote ndani yake.. mrudishie Mungu utukufu, ili Mungu akuhurumie, hii dunia sio yetu, hii dunia ni ya Mola wetu, hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu, kuonyesha kuwa kila alichojaliwa nacho ni kwa uweza wa Mungu.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.

Mlango uitwao “Mzuri” Unaozungumziwa katika Matendo 3:2 ndio upi?

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 10 (Kitabu cha Zaburi).

YEZEBELI ALIKUWA NANI

DANIELI: Mlango wa 12.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments