Tusome..
Matendo 3:1 “Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa. 2 Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika MLANGO WA HEKALU UİTWAO MZURİ, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu”.
Matendo 3:1 “Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa.
2 Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika MLANGO WA HEKALU UİTWAO MZURİ, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu”.
Biblia inasema Hekalu lilijengwa vizuri sana, na kwa vitu vya thamani. (1Wafalme 6, imeelezea mwonekano wa hekalu la Mungu). Hivyo Hekalu lilikuwa limejengwa kwa vitu vya thamani, na lilikuwa linamwonekano mzuri..
Tunalithibitisha hilo tena katika kitabu cha Luka..
Luka 21:5 “Na watu kadha wa kadha walipokuwa wakiongea habari za hekalu, JİNSİ LİLİVYOPAMBWA KWA MAWE MAZURİ na sadaka za watu, alisema, 6 Haya mnayoyatazama, siku zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa”.
Luka 21:5 “Na watu kadha wa kadha walipokuwa wakiongea habari za hekalu, JİNSİ LİLİVYOPAMBWA KWA MAWE MAZURİ na sadaka za watu, alisema,
6 Haya mnayoyatazama, siku zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa”.
Umeona?. Kwahiyo Hekalu lilikuwa zuri, na kama tunavyojua..Mlango wa kuingilia mahali popote siku zote unatengenezwa kuwa mzuri kuliko, milango mingine ya ndani midogo midogo, Mlango wa mapokezi unakuwa unapambwa sana. Mageti ya kuingilia mijini yalikuwa yanapambwa sana kuliko mageti madogo madogo ya ndani ya hiyo miji, hali kadhalika hata leo mageti ya kuingilia kwenye maonyesho fulani huwa yanapambwa sana ili kuvutia wanaokuja, na kuyapandisha hadhi maonyesho hayo.
Na ndio hivyo hivyo, Mlango wa kuingilia hekaluni ulikuwa umepambwa sana na wenye mwonekano mzuri, hivyo Wayahudi wakauita Mlango MZURI kwasababu kwanza, ndio ulikuwa mzuri kwa mwonekano kuliko milango yote, na ndio mlango wa kuingilia Nyumbani kwa Mungu wa mbingu na nchi. Hivyo wakauita MLANGO MZURI.
Matendo 3:9 “Watu wote wakamwona akienda, akimsifu Mungu. 10 Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiketi na kuomba sadaka penye MLANGO MZURİ WA HEKALU; wakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata”.
Matendo 3:9 “Watu wote wakamwona akienda, akimsifu Mungu.
10 Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiketi na kuomba sadaka penye MLANGO MZURİ WA HEKALU; wakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata”.
Lakini pamoja na uzuri wake wote, Bwana Yesu alisema hapo kwenye (Luka 21:6)..halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa, na kweli miaka michache tu baadaye hekalu hilo lilipotea, na hakukuwa tena na kitu kinachoitwa MLANGO MZURI, Israeli. Hata waliokimbilia kuingia katika huo mlango walikufa kwa upanga.
Lakini biblia imetaja mlango mwingine MZURI ambao huo unadumu milele..
Tuusome..
Yohana 10: 9 “ MİMİ NDİMİ MLANGO; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. 10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; MİMİ NALİKUJA İLİ WAWE NA UZİMA, KİSHA WAWE NAO TELE. 11 Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo”.
Yohana 10: 9 “ MİMİ NDİMİ MLANGO; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.
10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; MİMİ NALİKUJA İLİ WAWE NA UZİMA, KİSHA WAWE NAO TELE.
11 Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo”.
Yesu ndiye MLANGO MZURI unaodumu milele. Na alikuja ili tuwe na Uzima, kisha tuwe nao tele, je umempokea?. Kama bado basi maisha yako yapo hatarini, hivyo mpokee leo akupe uzima wa milele.
Kama hujampokea na unatamani kufanya hivyo sasa, basi uamuzi unaofanya ni wa thamani, kwa msaada wa namna wa kuongozwa sala ya Toba, basi fungua hapa >> KUONGOZWA SALA YA TOBA.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
YAKINI NA BOAZI.
Kile kinara cha Taa ndani ya Hekalu la Sulemani kilikuwa kinawakilisha nini?
TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?
Kwanini Samweli aliruhusuiwa kuhudumu hekaluni kama vile Walawi wakati yeye ni mu-Efraimu?
MAANDALIZI YA UJENZI WA HEKALU LA TATU YAPO TAYARI.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Nimebarikiwa….
Bwana akubariki zaidi