Kwanini Samweli aliruhusuiwa kuhudumu hekaluni kama vile Walawi wakati yeye ni mu-Efraimu?

Kwanini Samweli aliruhusuiwa kuhudumu hekaluni kama vile Walawi wakati yeye ni mu-Efraimu?

SWALI: Katika Biblia tunaona, ni Makuhani tu peke yao ndio walioruhusiwa kuhudumu katika Hema ya Mungu, na ndio walioruhusiwa kuingia ndani ya nyumba ya Mungu,ambao walikuwa ni wa kabila la LAWI mwingine yeyote akiingia kule anakufa, lakini katika biblia hiyo hiyo tunamwona mtoto Samweli ambaye hakuwa Mlawi aliwekwa ndani ya ile hema mbele ya lile sanduku la agano, na hakufa na tunasoma Baba yake aliyeitwa ELKANA alikuwa anatokea katika kabila la EFRAIMU, ukisoma 1 Samweli 1 utaona jambo hilo. Hapo nahitaji ufafanuzi kidogo.


JIBU: Tukisoma

1Samweli 1:1 inasema

“ Palikuwa na mtu mmoja wa Rama, Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu, jina lake akiitwa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, MWEFRAIMU”.  

Ni kweli kabisa kwa sentensi hiyo inaonyesha dhahiri kuwa Baba yake Samweli alikuwa ni Mwefraimu, lakini ukijifunza maandiko kwa undani! Utagundua kuwa Elkana Baba yake Samweli hakuwa Mwefraimu bali alikuwa Mlawi. Kumbuka wakati wa agano la kale, Kipindi ambacho Yoshua anaigawanya nchi ya Kaanani kwa makabila yote ya Israeli, Kabila la LAWI halikuwa na urithi wowote, Mungu aliwaweka wawe wakfu kwake kwa ajili ya shughuli ya madhabahuni tu, hivyo walipovuka Yordani walitawanywa na kukaa katikati ya makabila yote kuwahudumia watu katika masuala ya Torati na Ibada,..

Hivyo walawi waliokuwa wanakaa Dani, waliitwa wanadani, walawi waliokuwa Rubeni waliitwa warubeni, vivyo hivyo walawi waliokuwa wanakaa Efraimu waliitwa waefraimu.

Kumbukumbu 18:1 “Makuhani Walawi, kabila yote ya Lawi, wasiwe na fungu wala urithi pamoja na Israeli; watakula sadaka za Bwana zifanywazo kwa moto, na urithi wake.

2 Wala wasiwe na urithi kati ya ndugu zao; Bwana ndiye urithi wao, kama alivyowaambia”  

Sasa kuthibitisha jambo hilo kuwa Samweli alikuwa ni mlawi, turudi katika kitabu cha Mambo ya Nyakati..Tusome.

1 Nyakati 6:33 “Na hawa ndio waliofanya huduma pamoja na wana wao. Katika wana wa Wakohathi; Hemani mwimbaji, mwana wa Yoeli, MWANA WA SAMWELI;

34 MWANA WA ELKANA, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu;

35 mwana wa Sufu, mwana wa Elkana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai;

36 mwana wa Elkana, mwana wa Shauli, mwana wa Uzia, mwana wa Urieli;

37 mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora;

38 mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli.

39 Na nduguye Asafu, aliyesimama upande wake wa kuume, huyo Asafu alikuwa mwana wa Berekia, mwana wa Shimea;

40 mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya;

41 mwana wa Yeatherai, mwana wa Zera, mwana wa Ido;

42 mwana wa Yoa, mwana wa Zima, mwana wa Shimei;

43 mwana wa Yahathi, mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi.

44 Na upande wa kushoto ndugu zao, wana wa Merari; Ethani, mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki;

45 mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia;

46 mwana wa Amzi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri;

47 mwana wa Mali, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, MWANA WA LAWI.

48 Na ndugu zao, Walawi, ndio waliowekwa ili kufanya huduma yote ya maskani ya nyumba ya Mungu”.  

Unaona hapo? Ukiufuatilia huo uzao wa Elkana baba yake Samweli utaona unakuja kuishia kwa LAWI. Kwahiyo ni wazi kuwa Baba yake Samweli, Elkana hakuwa Mwefraimu bali Mlawi..Mungu asingeweza kuruhusu mtu yeyote asiyekuwa mlawi kuhudumu katika nyumba yake au hema yake.   Kwahiyo Samweli alikuwa ni Mlawi, Mlawi mwenye asili ya Efraimu   Ni sawa na leo Mchaga aliyezaliwa Kenya aje kuishi Tanzania, moja kwa moja atajulikana kama ni Mkenya..kwasababu amezaliwa Kenya na si Tanzania, ingawa asili yake na kabila lake ni Tanzania.   Kwahiyo hiyo ndio sababu Elkana baba yake Samweli aliitwa Mwefraimu, ni kutokana na mahali alipotokea na sio kutokana na kabila lake.  

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

MAANDALIZI YA UJENZI WA HEKALU LA TATU YAPO TAYARI.

MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO

YONA: MLANGO 1

JE! ADAMU ALIWASALIANA NA MUNGU KWA LUGHA IPI PALE BUSTANINI?

CHAPA YA MNYAMA

NITAMJUAJE NABII WA UONGO?

PENTEKOSTE NI NINI?


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments