Title May 2021

KANSA/SARATANI INATIBIKA.

Ni kweli Mungu amewapa wanadamu maarifa, ili yale yanayowezekana katika uwezo wao yatendeke, lakini  ipo wazi kuwa si kila tatizo mwanadamu anaweza kulitatua haijalishi ataonyesha bidii kubwa kiasi gani.

Yapo magonjwa ambayo, sisi kama wanadamu hatuwezi kuyatibu, isipokuwa Mungu tu peke yake.

Yeye mwenyewe alisema..

Yeremia 32:27 “Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza”?

Na sehemu nyingine pia Yesu alisema..

Mathayo 19:26b … Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu YOTE YAWEZEKANA.

Ikiwa na maana hakuna moja linaloshindikana kwake.

Huo ugonjwa wa Satarani, iwe ni ya koo, au ya damu, au ya ngozi, au ya matiti, au ya Shingo ya mfuko wa kizazi, au ya utumbo, au kongosho, au ini, au Mapafu ,au ubongo, au macho, au mifupa, au misuli, au Matezi n.k

Yote hayo, si kitu kwa Mungu. Kumbuka Sababu nyingine kubwa iliyomleta Bwana Yesu duniani, ilikuwa ni kutuponya magonjwa yetu. Na ndio maana ilimgharimu ateseke sana pale msalabani kwa mateso mengi, ili kwa kupigwa kwake kule wewe na mimi tupone.

1Petro 2:24 “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa”.

Mathayo 8:16 “Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya WOTE waliokuwa hawawezi,

17 ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu”.

Hivyo, anachotaka kwanza kwako, ni wewe umwamini kwa moyo wako wote. Utubu dhambi zako zote, ikiwa ulikuwa bado hujamkaribisha katika maisha yako, Kisha baada ya hapo ndipo akuponye magonjwa yako yote kama alivyoahidi katika Zaburi 103:3.

 “Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,”

Hivyo ukiwa upo tayari leo, kutubu dhambi zako, na kumkaribisha Bwana Yesu katika maisha yako. Basi, fuatisha sala hii ndani ya moyo wako kwa imani, ukimaanisha kabisa kumgeukia yeye, na kwamba unamuahidi kuwa akishakuponya utamtumikia yeye daima. Ikiwa upo tayari basi hapo ulipo ikiwa upo katika mahali pa utulivu, unaweza kupiga magoti yako, kisha sema sala hii kwa Imani;

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa kama utakuwa umesema sala hiyo kwa Imani, na kwa kumaanisha kabisa kutoka katika moyo wako. Basi Kristo Yesu ameshakusamehe, hivyo kuwa na amani, na kuanzia sasa uwezo wa kukuponya anao.

Basi nitakwenda kukuombea ugonjwa wako, Kisha Bwana atakufanyia uponyaji.

“Bwana Yesu, nakushukuru wa mwana wako huyu, ambaye ameona kuwa hakuna kimbilio lingine isipokuwa wewe. Naomba Bwana ukamponye magonjwa yake yote yanayomsumbua, iwe ni saratani, au mengine yoyote. Haijalishi madaktari wamesema amebakiwa na wiki mbili aishi au miaka 10. Tunafahamu kuwa wewe ndiye mponyaji. Hivyo nakuombwa Bwana, umponye Mama/dada/baba/kijana/mtoto huyu, anayesoma ujumbe huu. Na kuanzia sasa akawe mzima na huru, akakutumikie na kulitangaza jina lako lako daima kwa watu wote.

Asante Bwana kwa kumponya. Amen”.

Hivyo, kuanzia sasa, uponyaji wako umeshaingia katika mwili wako. Maombi tuliyoyaomba ni mafupi tu, lakini uamini kuwa tayari yameshaumba uponyaji katika mwili wako. Hivyo nachotaka kwako kuanzia sasa, utazame, mahali unapoumwa, na pia anza kufanya mazoezi, au pashughulishe pale ambapo ulikuwa huwezi kufanya chochote, au maajabu ya Yesu Kristo utayaona.

Bwana akubariki sana.

Kwa mawasiliano ili kujifunza zaidi biblia/ Ushauri/ Maombezi/ Shuhuda/Ibada, basi wasiliana nasi kwa namba hizi +255789001312/ +255693036618

Bwana akubariki.

Yerema 30: 17a “Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana,..”

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

YESU MPONYAJI.

JE! UKIMWI UNATIBIKA?

SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.

USIKATE TAMAA UNAPOPITIA MAGONJWA.

NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?

Rudi nyumbani

Print this post

JE! NA SISI NI SHABA ILIAYO NA UPATU UVUMAO?

Jina la Bwana wetu na mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe daima.. Karibu tujifunze maneno ya uzima.

Mtume Paulo aliandika hivi;

1 Wakorintho 13:1 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, KAMA SINA UPENDO, NIMEKUWA SHABA ILIAYO NA UPATU UVUMAO.

2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.

3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu”.

Kifaa chochote cha shaba kikigongwa, au kupulizwa, huwa kinataoa sauti Fulani, kwamfano zile kengele kubwa za kanisani, huwa zinapogongwa basi sauti yake inaweza kusikika mbali kidogo, lakini hasara yake ni kuwa, sauti zile huwezi kuzisikia kwa muda mrefu, zitaenda kwa muda tu na baada ya sikunde tatu au nne zitakwisha kabisa nguvu yake, ni baada ya hapo utaona ukimya mkubwa, hadi zitakapogongwa tena.

Vivyo hivyo na upatu. Upatu ni chombo ambacho kinamuundo wa sahani pana, ambazo kimsingi zinakuwa mbili, sasa hizo sahani zikishagonganishwa pamoja nazo huwa zinatoa sauti Fulani.. Na zenyewe vivyo hivyo, , unaweza kudhani sauti zao zitadumu kwa muda mrefu, lakini baada ya sekunde kadhaa zitaendelea kama mwangwi tu, na mwisho wa siku  zitafifia na baadaye kurudia ukimya wake tena kama mwanzo.

Ndivyo Mtume Paulo alivyoliona kanisa la Korintho na kuwaongezea habari hiyo, aliliona ni kanisa lililokuwa na bidii kubwa sana katika vipawa na karama za Rohoni, Mtume Paulo akilizungumzia hilo katika sura iliyotangulia ya 12. Linanena kwa lugha sana, lina karama zote za Roho, lakini limesahau UPENDO ambao ndio kiini cha Ukristo.

Akawaambia, mtu unaweza ukawa na vyote hivyo, unaweza hata ukautoa mwili wako kuungua moto, lakini kama huna Upendo wa kweli wa Ki-Mungu ndani yako wewe ni sawa na shaba iliayo na upatu uvumao, yaani hayo matendo yako yote hayatakufikisha mbali.. Kama utaotoa mwili wako uungue moto kwa nia ya kujionyesha wewe ni shujaa, au upate sifa, lakini huna Upendo wa kweli na Yule mtu kama jirani yako, wewe sio kitu, akiwa na maana, vitendo vyako vyote hivyo havitakufikisha mbali, mambo hayo yatabatilika tu baada ya muda Fulani kupita.

Na ndo maaana leo hii unaweza kuona kuna watu wakishafanyiwa jambo Fulani na Mungu, basi siku za kwanza kwanza wanajitoa kweli kweli kwake, lakini ukishapita muda fulani utaona wanapoa au wanauacha wokovu kabisa..Sasa hao ndipo ile Shaba iliayo na upatu uvumao, kwasababu kilichowafanya wamfuate Mungu haukuwa UPENDO wao kwake, bali kwasababu walifanyiwa/ watafanyiwa jambo Fulani na Mungu..Hawajui kuwa tabia moja ya  upendo  ni uvumilivu,

Paulo aliendelea kusema..

1Wakorintho 13:4 “Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;

6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;

7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.

8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika”.

Kumbuka Mungu alitupenda BILA SABABU YOYOTE. Sio kwamba tulikuwa wema, au tulistahili, au tulimpa fedha, au chochote, hapana Yeye alitupenda tu, na sisi anataka tuwe na Upendo kama huo kwake, na kwa wanadamu wenzetu. Huo ndio unaoitwa UPENDO wa AGAPE (Upendo wa Ki-Mungu). Tunakuwa tayari kuwasaidia wengine kiroho, hata kama wanatupenda au hawatupendi, wanatusaidia au hawatusaidii. Ndivyo Mungu anavyotaka. Yeye anawanyeshea mvua yake waovu na wema.

Lakini tukikosa hayo yote, na huku tunataka kujaribu kumtumikia Mungu, na huku hatutaki kuwa kuvumilia, hatutaki kumwamini, hatutaki kuacha husuda, na majivuna  hatutaki kufadhili, tujue tu hizo ni mbio za sakafuni, hazitusaidii chochote.

Hata kama tutakuwa tunaona maono mengi makubwa kiasi gani, , bado mbele za Mungu sisi sio kitu.

Kuna mchungaji mmoja huko Jamaika, alikuwa sio tu ni mchungaji mwenye kanisa kubwa, lakini pia alikuwa ni mtu mwenye Karama kali sana ya kinabii, kiasi kwamba, aliposimama madhabahuni, kabla mtu hajaingia kanisani akiwa pale mlangoni tu, aliweza kumtambua na kumwambia, Fulani kwanini jana ulimdanganya mke wako na kuwambia hiki na hiki.. Na saa hiyo hiyo Yule mtu alidondoka kwa machozi mengi akilia na kuomboleza amemkosea Mungu. Mchungaji huyu aliogopeka na kuonekana ni mtakatifu sana.

Lakini siku moja, wakiwa katika ibada ya nguvu sana, na Roho Mtakatifu alishuka katikati yao, alisikia kuhukumiwa moyoni, ndipo akasimama huku akilia na kuliambia kanisa, leo ninatubu dhambi zangu, kwasababu nimekuwa nikilificha kanisa na Roho Mtakatifu, kwa tabia yangu ya Ushoga, ambayo nimekuwa nayo kwa muda mrefu, na nimeshazini na wanaume wengi sana.

Kanisa liliposikia vile liliishiwa nguvu, mpaka wakataka kusitisha karama zote za kinabii katika kanisa, kanisa liwe linaendelea tu hivyo hivyo bila karama yoyote ya Roho.

Unaona! Tatizo sio karama, tatizo ni upendo (Hofu )  wa mtu aliokuwa nao kwa Mungu. Huyu nabii alikuwa ni Upatu uvumao. Hata sasa tunapaswa tujihakiki sana, sisi kama wachungaji, manabii, wainjilisti, na vilevile washirika. Je! Utumishi wetu unaendana na Upendo halisi wa Mungu?. Tusije tukawa ni watu wa kutaabika usiku na mchana, tunatumika kwa nguvu nyingi, tunaona Mungu akiwafungua na kuwaponya wengi, kumbe nyuma ya pazia Mungu anatuona tunafanya kazi bure.

Bwana atusaidie tuupe Upendo kipaumbele cha kwanza. Kwasababu tukimpenda Mungu, hatutaona sababu ya kumvunja moyo kwa matendo yasiyompendeza.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?

NGAZI 7 AMBAZO MKRISTO NI LAZIMA AZIPANDE KUUFIKIA UKAMILIFU.

NJIA YA KUPATA WOKOVU.

JE UPENDO WAKO UMEPOA?

UFUNUO: Mlango wa 3 part 3

Rudi nyumbani

Print this post

USIWE MSIKIAJI TU! BALI MTENDAJI.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia..

Neno la Mungu wetu linafananishwa na vitu vingi katika biblia, kuna mahali linafananishwa na “Taa” (Zab.119:105)”, sehemu nyingine linafananishwa na Upanga wa roho (Waebrania 4:12, Waefeso 6:17)” Na kuna sehemu linafananishwa na “Kioo”. Na leo tutajifunza ni kwa namna gani linafananishwa na kioo, ili tuelewe tabia nyingine ya Neno la Mungu.

Kama tunavyojua kioo kazi yake ni kuakisi taswira ya kitu. Kwa mfano mtu anapotaka kujijua yupoje kimwonekano, hususani uso wake, hakuna namna anaweza kujua uso wake upoje, bila kutumia kioo. Akitaka kujua uso wake upoje na sehemu gani na gani afanye marekebisho ni lazima atatumia kioo kama yupo peke yake.

Kikawaida mtu mwenye busara, anapoamka asubuhi, baada ya kufanya usafi wa mwili wake, kabla hajatoa mguu wake kutoka nje, kwenda kwenye shughuli zake ni lazima ajitazame kwenye kioo.. Ili ajihakiki kama uso wake upo sawa au la!, atajihakiki kama nywele zake zimechanika vizuri, isije kuwa upande mmoja kitana hakijapita vizuri, vile vile atajihakikia hakuna tongotongo lililobaki machoni n.k Hivyo kama kuna kasoro yoyote, atairekebisha pale pale akiwa na kioo chake kabla hajaondoka, kwasababu kioo hakidanganyi!..

Lakini mtu asiyejali, anapoamka asubuhi anaweza kujiangalia mara moja kwenye kioo, akajiona kasoro zake kwamba hajachana nywele, wala hajajipaka mafuta usoni… na kwa kupuuzia atasema nitarekebisha hizo kasoro ndogo muda mfupi  kabla sijaondoka.. watu wa namna hiyo  kama ukichunguza, mara nyingi wanajikuta wanaondoka pasipo kuchana nywele, au kuosha uso vizuri, au kupaka mafuta… Na Utaona baadaye wakishafika mbali  na kupita karibu na kioo chochote huko mjini ndio wanakumbuka aa! kumbe hizi nywele sikuzichana tena!…. Au..aaa nilisahauje tena kupaka mafuta usoni, na tayari nilikuwa nimeshayaandaa pale?.

Sasa hiyo ni kwasababu gani?. Ni kwasababu walijitazama kwenye kioo, na badala ya kurekebisha kasoro zao wakati ule ule walipokuwa wanajitazama kwenye kioo, wakapuuzia wakijitumainisha kuzirekebisha baadaye!. Na mwisho wa siku wanajisahau kuwa bado hawajachana nywele, au kupaka mafuta.na wanajikuta wanaondoka hivyo hivyo.. (majuto ni baadaye wameshafika mbali)

Na ndio Neno la Mungu lipo hivyo hivyo, pindi tunapolisikia Lile ndio KIOO chetu!!.. Linatuonyesha kasoro zetu!… kasoro ambazo hatuwezi kuziona kwa macho! Lenyewe linatuonyesha.. Na lengo la kutufumbulia kasoro zetu, ni ili sisi tuzirekebisha Papo kwa Hapo, na wala si kusubiri kesho au baadaye!.. Hapana bali papo kwa hapo.. Maana yake tunapolisikia Neno la Mungu tunalitendea kazi saa hiyo hiyo, hatuliweki kiporo.. Hiyo ndio tabia ya Neno la Mungu!. Hebu tusome mistari ifuatayo…

Yakobo 1:22  “Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.

23  Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.

24  Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo.

25  Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake”

Umeona hapo?.. “Anajiangalia, kisha anaenda zake na kusahau alivyo”

Neno la Mungu linapokuja mbele yetu, na kuzifunua kasoro zetu, hata kufikia kukubali  kuwa sisi ni wakosaji… hapo ni sawa na kioo kimewekwa mbele yetu kutuonyesha kasoro zetu. Na hivyo Mungu wetu anachokitegemea kwetu ni sisi kujirekebisha wakati ule ule, na si kusubiri baadaye…

kwasababu tukisubiri baadaye, tutajikuta unarudia kujiona tupo sawa! hatuna kasoro yoyote..(Unajikuta unajisahau kuwa wewe ni mtu wa namna gani)..utajiona huna kasoro zozote. Na ndicho kinachowatokea wengi leo. Utaona mtu kasikia injili leo, na kweli imemchoma na kapata kila sababu za kutubu!. Lakini moyoni mwake hayupo tayari kutubu pale pale, anasema atatubu tu!.. pasipo kujua kuwa kioo kipo mbele yake kwa wakati huo, kikishaondoka hapo, kinachofuata ni kujisahau tu yeye ni mtu wa namna gani.

Ndio maana biblia imetuonya hapo juu.. kuwa tusiwe wasikiaji tu!, bali watendaji wa Neno.

Je na wewe ni msikiaji tu? Au ni mtendaji pia!.. Ni maneno mangapi ya Mungu umeyatendea kazi  saa hiyo hiyo baada ya kuyasikia?. Je! Siku ile uliposikia na kushuhudiwa kuwa wazinzi wote watatupwa katika lile ziwa la moto, ulichukua hatua gani?. Je uliacha uzinzi kwa vitendo au kwa mdomo tu!..Je siku ile Neno la Mungu lilipokushuhudia moyoni mwako kuwa fashion, na mavazi yasiyo ya kujisitiri ni dhambi mbele za Mungu, ulichukua hatua gani??. Uliyaacha siku hiyo hiyo au ulisema nitayaacha siku moja!!..

Kumbuka biblia inasema saa ya wokovu ni sasa, na wakati uliokubalika ndio huu. Inawezekana na leo tena umepata nafasi ya kusikia maneno yale yale ya Bwana, kuwa wazinzi, waasherati, wezi, wanaovaa mavazi ya nusu tupu na ya kuonyesha maungo, wanaotazama picha za ngono mitandaoni, wanaojichua, wanaoupenda ulimwengu kuliko kumpenda Mungu..n.k wote hao hawataurithi uzima wa milele. Hichi ni kioo kimewekwa mbele yako!.. kinakuonyesha kasoro zako, ni heri ukazirekebisha sasa, usingoje kesho wala baadaye.

Kama unataka kuzirekebisha sasa, hapo ulipo anguka piga magoti, na kisha kiri mbele za Baba wa mbinguni kuwa umekosa, na tubu kwa kudhamiria kutozifanya tena, kama ulikuwa unafanya uzinzi na uasherati unaachana na mtandao wote uliokuwa unafanya nao uasherati, kama ulikuwa unavaa nguo za kizinzi, unazichoma sasa hivi baada ya toba yako, wala usimpe mtu mwingine na wala usizingojeshe kesho, vivyo hivyo na mambo mengine yote..unayaacha kwa vitendo, angali bado kioo kipo mbele yako sasa.

Na baada ya kutubu hivyo, hatua inayofuata ni ya muhimu sana, nayo si nyingine zaidi ya ubatizo!. Ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kulingana na Matendo 2:38, Na baada ya kubatizwa Roho Mtakatifu atakusaidia kufanya yaliyosalia, kwasababu tayari wewe utakuwa milki yake halali.

Bwana akubariki na Bwana atusaidie.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

MAAGIZO AMBAYO HAYAJAAGIZWA!

NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE

UFUNUO: Mlango wa 1

Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?

WAKATI WA JIONI KUTAKUWAKO NA NURU.

Rudi nyumbani

Print this post

Baghairi ni nini kama tunavyosoma katika 2Wakorintho 11:28?

Baghairi ni neno la kiunganishi lenye maana ya… “Mbali na”. Kwamfano nikitaka kusema.. “Mbali na yote ninayoyapitia bado nitasimama imara katika Imani”..naweza kuisema sentensi hiyo kama ifuatavyo “Baghairi ya yote ninayoyapitia bado nitasimama imara katika Imani”

Sasa katika biblia hilo neno limeonekana mara moja tu!. Katika kile kitabu cha 1Wakorintho 11:28

1Wakorintho 11:27 “katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi.

28 BAGHAIRI ya mambo ya nje, yako yanijiayo kila siku, ndiyo maangalizi ya makanisa yote.”

Jambo dogo tunaloweza kujifunza kupitia mstari huo, ni kwamba.. Mtume Paulo, pamoja na wakristo wa kwanza walipitia dhiki nyingi, kwaajili ya Injili na wala hawakuikana imani, Ndio maana ukianzia juu kidogo, mwa mstari huo, utaona hilo jambo…

Waebrani 13:23 “Wao ni wahudumu wa Kristo? (Nanena kiwazimu), mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana;

katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi.

24 Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja.

25 Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini;

26 katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang’anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo;

27 katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga

mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi.

28 Baghairi ya mambo ya nje, yako yanijiayo kila siku, ndiyo maangalizi ya makanisa yote”.

Bwana atusaidie tuzidi kujikana na kujitoa kwaajili ya injili.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Biblia ina maana gani inaposema akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko?

Neno Bildi linamaanisha nini kwenye biblia(Matendo 27:28) ?

Santuri ni nini? (Danieli 3:5,10)

Je ni kweli imani ya mtu ndiyo itakayomuokoa, na si kitu kingine?

LANGO LIMEBADILIKA.

Rudi nyumbani

Print this post

Je! Mfalme Abiya na Mfalme Asa walikuwa ni ndugu?

Katika 1Wafalme 15:2 na 1Wafalme 15:10 tunaona wote mama yao ni mmoja, ambaye ni Maaka, binti Absalomu. Lakini Mstari wa 8 unasema ni mtu na mwanawe.

Jibu: Tusome,

1Wafalme 15:1 “Mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yeroboamu mwana wa Nebati, ABIYA alianza kutawala juu ya Yuda

2 Miaka mitatu akatawala huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa MAAKA, BINTI ABSALOMU…………..

8 Abiya akalala na baba zake, wakamzika mjini mwa Daudi. Akatawala Asa mwanawe mahali pake.

9 Mwaka wa ishirini wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, ASA ALIANZA KUTAWALA JUU YA YUDA.

 10 Akatawala miaka arobaini na mmoja huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa MAAKA, BINTI ABSALOMU”

Ni muhimu kufahamu kuwa katika biblia, hakuna Neno “BABU” wala “BIBI”. Neno bibi katika biblia lilitumika tu kuwakilisha “Mwanamke mstahiki” kama vile bibi-arusi, au mwanamke mwenye hadhi Fulani (soma Esta1:18, Mwanzo 16:9) lakini sio “mama wa mama” kama leo hii tunavyolitumia, kwamba  wale waliowazaa mama zetu au baba zetu tunawaita “Bibi” au wale mababa waliowazaa baba zetu tunawaita “Babu”. Katika biblia hilo jambo halipo… Yule aliyemzaa baba anaitwa hivyo hivyo “Baba” na Yule aliyemzaa mama anaitwa hivyo hivyo “mama”..haijalishi ni vizazi vingapi vitapita, Yule babu wa babu wa babu, bado ataitwa baba tu!

Kwamfano utaona Mfalme Hezekia katika biblia ambaye alikuwa ni kutukuu cha 13 cha Mfalme Daudi, Lakini Mungu anamtaja kama Daudi ni baba yake na si babu yake. (soma 2Wafalme 20:5) unaweza kusoma pia,  2Nyakati 21:12, kutoka 3:15, Hesabu 32:8, kumbukumbu 1:8, Yoshua 24:2, Waamuzi 2:1, 1Samweli 12:6. N.k. Utaona jambo hilo hilo..

Kwahiyo tukirudi kwenye swali letu, ni kwamba huyu Maaka alikuwa ni mama wa Mfalme Abiya na ni bibi wa mfalme Asa, kwasababu Asa alikuwa ni mtoto wa Mfalme Abiya kama tunavyosoma hapo katika mstari wa 8.

1Wafalme 15:8 “Abiya akalala na baba zake, wakamzika mjini mwa Daudi. Akatawala Asa mwanawe mahali pake”

Kwahiyo biblia ingeweza kumtaja Maaka kama ni bibi wa Asa, badala ya mama lakini haina hilo neno bibi, halipo bali “mama” ndio maana unaona imewataja wote wawili (Abiya na Asa) kwamba mama yao ni mmoja, anayeitwa Maaka.  Na kama ukizidi kuendelea kusoma habari hiyo utaona, huyu Asa alipoingia tu katika ufalme alimtoa bibi yake huyo katika umalkia kwasababu alikuwa ni mwovu mbele za Bwana, kwa namna ya kawaida ni ngumu mtu kumtoa kwenye umalkia mama yake mzazi kwasababu huwa kunakuwa na uhusiano mkubwa sana wa tabia ya mtoto wa kiume na mama yake.

Sasa kwanini Biblia isitumie maneno “Babu” au “Bibi” na badala yake inatumia tu Baba au Mama, haijalishi ni vizazi vingapi vimepita?

Ni kwasababu Mungu anataka kutufundisha jambo Fulani la kiroho, kwamba na yeye mwenyewe si BABU yetu, bali ni BABA YETU haijalishi ni vizazi vingapi kabla yetu.

Kwa ufupi Mungu hana “wajukuu”. Huwezi kusema mimi ni mjukuu wa Mungu, sisi wote ni watoto wa Mungu, na Mungu wetu ni Baba yetu.. ndio maana kaondoa cheo cha “Ubabu” katika maandiko yake.

Mwanao utakayemzaa hatakuita wewe baba, na Mungu amwite Babu, bali atakuita wewe “baba” na Mungu atamwita “BABA” ya herufi kubwa!!. Kwasababu wewe ni kivuli tu! Cha Baba halisi aliye mbinguni.

Waefeso 3:14 “Kwa hiyo nampigia Baba magoti, ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa”.

Maana yake ni kwamba kwa chochote kile unachokifanya anakuchukulia wewe kama mwanae, na baba yako wa kimwili anamchukulia kama mwanae..hivyo katika roho wewe na baba yako wa kimwili ni mtu na kaka yake, hana upendeleo!!. Ukifanya linalostahili makosa atakuadhibu kama mwanae, na si kama mjukuu na baba yako vile vile atamwadhibu kama mwanae.. Kadhalika mkifanya mambo mazuri wote anawapa thawabu kama wanae.

Lakini kumbuka si wote katika hii dunia, Mungu ni Baba yao… wengi bado hawajafanyika watoto wa Mungu, tofauti na inavyoaminika na wengi leo kwamba sisi wote ni watoto wa Mungu! La huo sio ukweli hata kidogo.. wengi ni watu tu walioumbwa na Mungu!, lakini si watoto wa Mungu. Biblia inasema ili tufanyike watoto wa Mungu ni lazima tupasi huu mtihani hapa chini…

Yohana 1:11  “Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.

12  BALI WOTE WALIOMPOKEA ALIWAPA UWEZO WA KUFANYIKA WATOTO WA MUNGU, NDIO WALE WALIAMINIO JINA LAKE;

13  waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu”

Swali ni je!.. Umempokea?..ili upewe huo uwezo wa kufanyika mwana?..

Kama hujampokea fahamu kuwa bado wewe sio mtoto wa Mungu, huwezi kuwa mrithi wa ufalme wa mbinguni. Kwasababu katika hali ya kawaida watu hawawarithishi watu wasio watoto wao mali zao. Vivyo hivyo Mungu hawezi kuwarithisha wale wasio wanawe urithi wake.

Kama unatamani kwenda mbinguni na kuurithi uzima wa milele, leo hii mpokee Yesu maishani mwako, na dhamiria kuacha dhambi na katafute kubatizwa ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu (Matendo 2:38). Na baada ya hapo, Roho Mtakatifu atakayeingia ndani yako atakupa uwezo wa kufanyika mwana, na Mungu kwako atakuwa Baba.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

KWANINI UNAPASWA UWE BIBI ARUSI NYAKATI HIZI ZA MAJERUHI?

Kwa jina lake Ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa.

Mbari ni nini kibiblia?

HAKUNA MTU ANIONDOLEAYE, BALI MIMI NAUTOA MWENYEWE

Rudi nyumbani

Print this post

WALIYATWAA MAVAZI YAKE, WAKAFANYA MAFUNGU MANNE,

Yohana 19:23 “Nao askari walipomsulibisha Yesu, waliyatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu lake; na kanzu nayo. Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu.

24 Basi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile linenalo, Waligawanya nguo zangu, Na vazi langu wakalipigia kura. Basi ndivyo walivyofanya wale askari”.

Ulishawahi kujiuliza ni kwanini biblia haijakaa kimya kuhusiana na mavazi ya Yesu pale Goligotha, na jinsi yalivyopigiwa kura? Mpaka kufikia hatua ya kugawanywa katika mafungu manne (4) kwa wale askari wanne waliokuwa pale msalabani.? Na lile moja la 5 ambalo ni kanzu yake kupigiwa kura?. Haikuandikwa kutengeneza stori tu, kwamba Yesu alikuwa na mavazi matano, bali kulikuwa na maana nzito nyuma yake.

Hiyo ni kuonyesha kuwa hakubakiwa na nguo hata moja muda ule alipotundikwa  pale msalabani. Alisulibiwa akiwa uchi kabisa wa mnyama. Ni jambo ambalo haliwezekani kwamba nguo nyingine zipigiwe kura, na kugawanya, halafu nyingine abakiwe nazo kutundikiwa msalabani, Maandiko hayatuonyeshi hivyo. Kile tunachokiona kwenye misalaba ya kuchonga au kwenye muvi  kwamba Bwana Yesu alisulibiwa akiwa na kipande cha nguo cha kumsitiri, si kweli. Ukweli ni kwamba alisulibiwa akiwa uchi kabisa wa mnyama. Hata hivyo wakati ule wa Rumi wahalifu wote waliouliwa kwa kusulibiwa ilikuwa ni lazima wasulibiwe uchi, ili kwamba sio tu wafe kwa mateso bali pia wafe kwa aibu.

Je! ulishawahi kutafakari kwa utulivu kwanini Kristo aruhusu hayo yote yampitie, wakati alikuwa na uwezo kabisa wa kuyaepuka? Unadhani hakikuwa kitendo cha aibu kile? Kilikuwa ni kitendo kikubwa sana cha aibu, ambacho ninauhakika hata wewe ungekuwepo wakati ule usingedhubutu hata kumwangalia pale msalabani akiwa katika hali ile. Lakini yeye hakuona aibu, kuwekwa uchi, ilimradi tu mimi na wewe tu tuokoke. Huko ni kujitoa kulikopitiliza.

Hakunionea haya mimi, vilevile hakukuonea haya wewe, kinyume chake biblia inatuambia aliidharau aibu,

Waebrania 12:2 “tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba NA KUIDHARAU AIBU, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu”.

Unaona, ukitafakari hilo vizuri, ndugu yangu, hutaona sababu ya wewe kumwonea aibu Bwana wako, katika dunia hii mbovu. Hutaona aibu kuitwa mshamba, kwa ajili yake, hutaona sababu  kuogopa kuitangaza injili yake.

Paulo alisema..

Warumi 1:16 “Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia”.

Alimwambia pia Timotheo maneno hayo hayo;

2Timotheo 1:8a “Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, ..;”

Huu si wakati wa kufikiria Fulani atanionaje, au marafiki watanichukuliaje, au majirani watanizungumziaje ikiwa nitampa Kristo Maisha yangu. Kumbuka Yesu hakukuonea haya wewe, aliposulibiwa uchi mbele ya kadamnasi, mbele ya maelfu wa watu waliokuwa pale Goligota, kwanini wewe umwonee haya yeye wakati hujafikia hata hatua ya kutembezwa uchi barabarani kwa ajili yake?.

Ukimkataa leo wakati utafika atakukataa na wewe.

Marko 8:38 “Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu”.

Tengeneza picha unasimama mbele ya mamilioni kwa mamilioni ya malaika, halafu Kristo anakuonea aibu mbele yao, utajisikiaje? Hali Fulani mbaya,

Hivyo chukua msalaba wako ujitwike umfate Kristo. Hizi ni siku za mwisho, yupo mlangoni kurudi. Kama bado hujatubu basi huu ndio wakati wako, mwamini yeye ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO, upate ondoleo la dhambi zako na yeye mwenyewe atakupa Roho wake Mtakatifu atakayekuongoza katika kweli yote.

Ikiwa utahitaji kuokoka, basi wasiliana nasi kwa namba hizi hapo chini, Nasi tutakusaidia katika hilo.

Bwana akubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

VAZI KUU AMBALO MUNGU AMETUANDALIA KILA MMOJA WETU.

kwanini yule kijana aliitupa ile nguo ya kitani chini na kukimbia uchi?

Kutahayari ni nini katika biblia?(2Timotheo 2:15)

MARINDA KATIKA BIBLIA NI KITU GANI?

Nguo za magunia katika biblia ni zipi?

Rudi nyumbani

Print this post

HAKUNA MTU ANIONDOLEAYE, BALI MIMI NAUTOA MWENYEWE

Yapo mambo mengi Bwana Yesu aliyoyafanya ambayo katika akili za kawaida, ni ngumu kuaminika. Yapo mengi lakini leo tulitazame moja kuu, ambalo hakuna mwanadamu yeyote wala kiumbe chochote kinachoweza kufanya. Na jambo hilo si linguine zaidi ya  UWEZO WA KUUTOA UHAI WAKE NA KUURUDISHA.

Umewahi kujiuliza mtu anawezaje wezaje kuutoa uhai wake yeye mwenyewe na kujirudishia??..Ni kama vile hilo jambo haliwezekani ee?..Lakini liliwezekana kwa Jemedari, Mkuu wa Uzima, Yesu.. Hebu tusome mistari ifuatayo ili tuelewe vizuri….(Zingatia vipengele vilivyoanishwa kwa herufu kubwa)

Yohana 10:15  “kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami NAUTOA UHAI WANGU KWA AJILI YA KONDOO.

16  Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.

17  Ndiposa Baba anipenda, KWA SABABU NAUTOA UHAI WANGU ILI NIUTWAE TENA.

18  HAKUNA MTU ANIONDOLEAYE, BALI MIMI NAUTOA MWENYEWE. NAMI NINAO UWEZA WA KUUTOA, NINAO NA UWEZA WA KUUTWAA TENA. AGIZO HILO NALILIPOKEA KWA BABA YANGU.

19  Kukaingia tena matengano kati ya Wayahudi, kwa ajili ya maneno hayo.

20  Wengi wao wakasema, Ana pepo huyu, tena ana wazimu; mbona mnamsikiliza?.

21  Wengine wakasema, Maneno hayo siyo ya mtu mwenye pepo. Je! Pepo aweza kuwafumbua macho vipofu?”

Hapo Bwana Yesu anasema “Hakuna mtu autoaye uhai wake bali anautoa mwenyewe”.. Utauliza vipi pale msalabani, sio wale watu walimuua??.. Nataka nikuambie kuwa hawakumuua, biblia inasema “yeye mwenyewe aliitoa roho yake (Mathayo 27:50  “Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake”)

Ndio maana baadaye wale askari  walipotaka kwenda kuivunja miguu yake wakamkuta kashakufa..kwasababu kikawaida adhabu ya kutundikwa msalabani inamchukua mtu hata siku 4 ndipo afe..Maana lengo la wao kumsulubisha mtu msalabani sio afe tu!, bali afe kifo cha mateso, kama ingekuwa lengo ni kumuua tu, wangemkata kata na mapanga afe!… Kwahiyo waliposhangaa Bwana Yesu kafa mapema vile pale msalabani, iliwaogopesha na kuwashtusha sana, kuwa Yule ni mtu wa namna gani..Mpaka Pilato naye alishtuka!!.

Marko 15:43  “akaenda Yusufu, mtu wa Arimathaya, mstahiki, mtu wa baraza ya mashauri, naye mwenyewe anautazamia ufalme wa Mungu; akafanya ujasiri, akaingia mbele ya Pilato akauomba mwili wake Yesu.

44  LAKINI PILATO AKASTAAJABU, KWAMBA AMEKWISHA KUFA. akamwita yule akida, akamwuliza KWAMBA AMEKUFA KITAMBO”

Umeona jinsi Bwana Yesu alivyokuwa wa kipekee???. Hakuwa mtu wa kawaida Yule, bali alikuwa ni “Mungu katika Mwili wa kibinadamu”, kwasababu katika hali ya kawaida hakuna mwanadamu anayeweza kuamua kuutoa uhai wake. Unakaa tu na kuamua, kuiondoa roho yako??..hilo jambo haliwezekani kibinadamu.

Na kumbuka ipo tofauti kati ya “kuutoa uhai wake” na “kujiua”. Bwana Yesu hakujiua!, maana yake ingempasa afanye jambo la kujidhuru,  lakini yeye hakufanya hivyo, bali aliutoa uhai wake… Maana yake kama angeamua asiutoe uhai wake angeweza pia kukaa pale msalabani daima, wangempiga na kumtesa lakini asingekufa na wangeshangaa kwanini hafi.. Hiyo ni kwasababu Nguvu za Mauti na Uhai tayari zilikuwa mikononi mwake.

Na hajaishia hapo, anaendelea kusema “Ana uwezo wa kuutoa uhai wake na kuutwa tena”. Maana yake ana uwezo wa KUJIFUFUA PIA!!. Na agizo hilo alipokea kutoka kwa baba. Yaani agizo la kuutoa uhai wake na kuurudisha. Baba alimwambia afanye hivyo.. “sasa sio kosa kusema Bwana Yesu, alifufuliwa na Baba, ni sahihi kabisa kwasababu nguvu zote zinatoka juu, na ili utukufu wote apokee yeye, ni sahihi kusema Baba alimfufua, lakini kiuhalisia ni kwamba Baba alimpa maagizo na uwezo wa kujifufua mwenyewe.”

SASA NINI LENGO LA KUUTOA UHAI WAKE NA KUJIRUDISHIA??

Lengo la Bwana Yesu kuutoa uhai wake na kujirudishia sio kutuonyesha sisi kuwa yeye ni mtaalamu au mtu wa miujiza! Hapana, bali kulikuwa na maana kubwa sana kiroho, kwanini autoe uhai wake na kujirudishia.

Ili tuelewe vizuri hebu tafakari mfano ufuatao.

Umenunua simu na haiwezi kuingia internet, wenye mtandao wakakwambia wanakutumia settings za internet, zikubali na baada ya HAPO ZIMA SIMU YAKO NA KUIWASHA TENA, ili ziweze kufanya kazi. Sasa lengo la wao kukuambia uzime simu yako na kuiwasha baada ya kupokea hizo settings, si kwasababu hawapendi simu yako iwe imewaka muda wote, hapana!.. Lengo la wao kukuambia ufanye vile ni kwasababu zile settings ili ziweze kufanya kazi ni lazima program zote kwenye simu ziache kufanya kazi kwa muda ili hizo mpya zinapoingia zipate nafasi, na unapowasha simu unakuta tayari zile settings za internet zimeanza kufanya kazi kwenye simu yako, na unajikuta unaweza kuingia internet.  Lakini usipofanya hivyo (usipozima simu yako na kuiwasha), utabaki nazo tu ndani ya simu yako na hazitakusaidia chochote.

Na kama umegundua simu yenye uwezo mkubwa kidogo ina uchaguzi wa kujiwasha na kujizima yenyewe yaani “restart button”, kiasi kwamba ukibonyesha hiyo “restart” simu inajizima yenyewe na kujiwasha, pasipo wewe kuizima wala kuiwasha.

Na Bwana Yesu, ni hivyo hivyo baada ya kupokea maagizo ya uzima wa milele, kwamba injili lazima ihubiriwe ulimwenguni kote, Ilikuwa ni lazima “afe na kufufuka”. Kulikuwa hakuna namna..vinginevyo ukombozi usingeenea kila mahali.. Ni kama tu zile settings za internet, zisipofanya kazi katika simu haiwezekani kujiunganisha na ulimwengu wote. Na zinaingia kwa kuizima simu na kuiwasha tena.

Hiyo ndio sababu ya Bwana Yesu kuuondoa  uhai wake yeye mwenyewe na kuurudisha tena. Haleluya!!. Kwa lugha ya kueleweka ni kama ali-restart uhai wake. Alisema maneno yafuatayo..

Yohana 12: 24  “Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi”.

Umeona kwahiyo Bwana Yesu ilimpasa afe, na kufufuka kwa faida yetu sisi, hususani sisi watu wa Mataifa.. Ndio maana hapo alisema “anao kondoo wa zizi linguine” maana yake ni sisi watu wa Mataifa…kondoo wa zizi lake ni wayahudi. Hivyo ili atupate na sisi watu wa mataifa ilimpasa atoe uhai wake na kuutwaa tena..

Yohana 10:15  “kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami NAUTOA UHAI WANGU KWA AJILI YA KONDOO.

16  Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja”

Je umemwamini Yesu?.. Je unamheshimu yeye ambaye aliutoa uhai wake ili kuja kukupata wewe kondoo wa mbali uliyepotea??.  Je umemthamini kwa kutii maagizo yake ya msingi, ya kutubu dhambi zako, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu, pamoja na kupokea kipawa cha Roho wake Mtakatifu juu yako?. Kama bado ni vyema ukafanya hivyo maadamu bado unayo nafasi…

Kumbuka hii ni neema ya kipekee sana tuliyopewa…haitadumu milele..

Waebrania 10:28  “Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.

29  Mwaonaje? HAIKUMPASA ADHABU ILIYO KUBWA ZAIDI MTU YULE ALIYEMKANYAGA MWANA WA MUNGU, NA KUIHESABU DAMU YA AGANO ALIYOTAKASWA KWAYO KUWA NI KITU OVYO, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?”

Na pia…

Waebrania 2:3  “sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;

4  Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe”

Neema ni ipo, lakini haitadumu milele, tukiipuuzia… Bwana anatuita wote tuingie zizini mwake, ni heri tukaingia, lakini tukiipuzia na kuidharau neema, siku moja mlango utafungwa na hautafunguliwa tena..

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.

WAKAMCHA BWANA, NA KUITUMIKIA MIUNGU YAO WENYEWE.

LAKINI NINYI, NDUGU, MSIKATE TAMAA KATIKA KUTENDA MEMA.

SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?

Rudi nyumbani

Print this post

Zile Rangi saba za Upinde wa Mvua zinawakilisha nini?

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia, maneno ya Mungu wetu aliye juu..kwasababu maneno yake ndio Mwanga wa njia yetu ya kuelekea mbinguni, na Taa iongozayo miguu yetu.(Zab.119:105)

Je umewahi kujiuliza kwanini bendera nyingi zinakuwa ni kitambaa chenye rangi mbali mbali, na kila rangi inakuwa na maana fulani?. Utaona mataifa mengi bendera zao zinakuwa  ni mistari tu ya rangi tatu au nne au tano. Na kama ukifuatilia utagundua zile rangi si urembo, bali zimebeba maana fulani kwa hilo Taifa.

Kwamfano bendera ya Taifa la Tanzania ina rangi 4, Nyeusi, Njano, kijani na Bluu. Rangi nyeusi inawakilisha wenyeji wa Taifa hilo (ni watu wenye ngozi nyeusi), rangi ya njano inawakilisha maliasili zote zilizopo ndani ya Taifa hilo, rangi ya kijani inawakilisha mimea na uoto wa asili wote pamoja na mazao ya nchi.. na rangi ya bluu inawakilisha Maji yote ikiwemo bahari, mito na maziwa. Hivyo kama ukiweza kuzisoma rangi hizo tayari utakuwa umeshalielewa Taifa la Tanzania, ni taifa la namna gani hata kabla ya kufika.

Kadhalika na Bwana Mungu wetu anayo bendera yake ambayo inawakilisha tabia zake. Na bendera yake hiyo aliiwasilisha kwetu baada tu ya ile gharika ya wakati wa Nuhu. Na hiyo si nyingine zaidi ya Ule Upinde wa Mvua wenye rangi saba. Kikawaida Bendera zetu zinakuwa ni kitambaa tu kilichochorwa mistari ya rangi, na tunaipandisha inakuwa inapepea angani,  lakini bendera ya Bwana haijachorwa katika kitambaa bali katika anga juu sana, na imechorwa kwa mistari ya rangi saba.

upinde wa mvua

Bendera hiyo Ndiyo inayomwelezea Mungu ni nani kwetu..

Sasa kabla ya kuendelea mbele ni vizuri tukazijua tabia kuu mbili za Mungu, ambazo hizo ndio msingi wa somo letu.. Biblia inasema Mungu ni MWINGI WA HASIRA (Nahumu 1:2) na vile vile biblia inasema Mungu ni MWINGI WA HURUMA.(Kutoka 34:6, Zaburi 145:8, Yoeli 2:13, Yona 4:2). Hizo ndio tabia kuu mbili za Mungu wetu. Ana hasira nyingi sana, vile vile ana huruma nyingi sana. Lakini pamoja na kwamba ni mwingi wa hasira, biblia imesema si mwepesi wa hasira, maana yake si rahisi akasirike kwa haraka.

Hivyo tukirudi katika mifano ya maisha ya kawaida..Mtu anavyozidi kuwa na hasira ndivyo ndani mwake kunavyozidi kuwaka, maana yake ni kwamba ni kama kuna moto unachochowa ndani yake na anazidi kuwa mwekundu, ikiwemo unyama huko huko.. Ndio maana watu weupe wakikasirika ni rahisi kuona hata ngozi za nyuso zao zimebadilika na kuwa nyekundu.. Hivyo rangi nyekundu inawakilisha hasira au ghadhabu..

Lakini vile vile, mtu huyo huyo hasira yake inapoanza kupoa utaona ule wekundu unaondoka na anarudia rangi yake. Ule wekundu unaanza kufifia kidogo kidogo mpaka, unaisha kabisa…

Vile vile Katika mifano mingine ya maisha ya kawaida pia kitu cha moto sana kinawakilishwa na rangi nyekundu, lakini kitu cha baridi kinawakilishwa na rangi ya bluu.. maana yake rangi ya bluu ni rangi ya utulivu uliozidi sana, ni rangi ya upole, ni rangi ya kulipooza jambo la moto!, ni rangi ya kutuliza ghadhabu kwa ufupi ni rangi ya rehema…na ni kinyume kabisa cha rangi ya Nyekundu.

maji ya moto

Kwa mifano hiyo tutakuwa tumeshaanza kuelewa kwanini uwepo upinde angani unaoanza na  Rangi nyekundu, na kisha zifuate rangi nyingine mpaka itokee rangi ya mwisho ya bluu..Utaona kwa jinsi zile rangi zinavyozidi kusogea mbele ile nyekundu inafifia na kuwa rangi ya chungwa (Orange), na kisha njano na kisha kijani… Maana yake hapo, Hasira ya Mungu inapungua kutoka juu kushuka chini, mpaka kufikia kusamehe kabisa..na kutoa neema (Ndio rangi ya kijani iliyopo katikati)..

Na inavyozidi kuendelea utaona Neema ya Mungu inazidi kuwa nyingi na hata kuelekea kwenye rangi ile ya blue ambayo inawakilisha utulivu wa Mungu wa hali ya juu, na Neema isiyo na kikomo..kiasi kwamba Rehema zake ni nyingi mno na hata kuipooza na kuizima ghadhabu yote..Hivyo rangi ya inavyozidi kukolea kuwa bluu ndivyo ndivyo neema zake zinavyozidi kuwa nyingi….Ndio maana hata anga lina rangi ya bluu, kuonyesha wingi wa huruma zake kuliko hasira zake.

Hivyo zile rangi saba zinawakilisha ghadhabu ya Mungu jinsi inavyosogea na kubadilika  kuwa Rehema zake…Ndio maana Baada ya Nuhu kutoka kwenye gharika, Mungu aliirehemu dunia ambayo alikuwa ameighadhibikia kwa ghadhabu kubwa, na kuahidi kutoiangamiza tena kwa maji. Hapo ni hasira zake zimesogea kutoka kwenye nyekundu kwenda kwenye blue.

Ni Mungu tu pekee ndio ana tabia hiyo, hakuna kiumbe kingine duniani, au mbinguni ambacho kina wingi wa hasira na hapo hapo kina wingi wa huruma.

Ndio maana alisema katika..

Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29  Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30  kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”

Haijalishi Umemwudhi Bwana kiasi gani leo, kumbuka huruma ni nyingi, yupo tayari kukusamehe kabisa endapo utamgeukia yeye kwa moyo wako wote na kudhamiria kuacha dhambi. Unachopaswa kufanya ni kutubu mbele zake kwa moyo wa unyenyekevu kabisa na kisha kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu, na kupokea Roho Mtakatifu. Naye atafuta dhambi zako zote, na kukufanya kuwa mtakatifu kana kwamba hujawahi kumkosea kabisa katika maisha yako. Na wala ghadhabu yake haitakuwa juu yako hata kidogo.

Lakini ukipuuzia rehema zake hizo ambazo zinapatikana bure, na kuzidi kuisogelea ghadhabu yake, fahamu kuwa yeye bado hajabadilika, bado ni mwingi wa hasira… alisema…katika Nahumu 1: 2 “Bwana ni Mungu mwenye wivu, naye hujilipiza kisasi; Bwana hujilipiza kisasi, NAYE NI MWINGI WA HASIRA; Bwana hujilipiza kisasi juu ya adui zake, huwawekea adui zake akiba ya hasira”

Ni jambo baya sana kuangukia kwenye hasira ya Mungu, ni heri ukatubu leo na kumwamini..

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

MUNGU HAONI SHIDA KUMUHAKIKISHIA MWOVU ULINZI.

Fadhili ni nini? Nini maana ya “fadhili zake ni za milele” kibiblia?

Je, kama hauna ubatizo sahihi hauwezi kuwa na Roho Mtakatifu?

TAFUTA KUWA NA AMANI NA WATU WOTE.

NIKUPE WEWE URITHI WA BABA ZANGU?

Rudi nyumbani

Print this post

Nondo ni nini kama tunavyosoma katika biblia?

Neno hili utalikuta sehemu nyingi sana katika biblia,  kwa mfano hivi ni baadhi ya vifungu ambavyo utakutana na neno hilo;

Ayubu 13:28 “Nijapokuwa ni kama kitu kilichooza, kinachosinyaa, Mfano wa nguo iliyoliwa na nondo.

Isaya 50: 9 “Tazama, Bwana MUNGU atanisaidia; ni nani atakayenihukumu kuwa mkosa? Tazama hao wote watachakaa kama vazi; nondo atawala”.

Mathayo 6:19 “Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;

20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;

21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako”.

Yakobo 5:1 “Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia.

2 Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo”.

Soma pia Ayubu 4:19, Zaburi 39:11, Isaya 51: 8, Hosea 5:12

Nondo ni wadudu, jamii ya vipepeo, unaweza kuwaona kwenye picha juu. Wadudu hawa, huwa wakishafikia hatua ya kutaga mayai, tabia yao ni kwenda kwenye nyumba za watu, na kutaga maeneo ambayo yana nguo, au sehemu zenye asili ya vitu vya pamba pamba au manyoya kama vile kwenye makapeti, n.k. lengo likuwa ni siku vifaranga watakapototolewa wapate chakula, na chakula chao ndio hizo nguo.

Kwa kawaida wakishafikia hatua ya vipepeo hawana uharibifu wowote, lakini wakiwa bado ni “lava” ndio wanatafuna nguo, na vitu vyote vyenye jamii ya hiyo vilivyopo ndani.

Natumai hata na wewe ulishawahi kuwaona, tazama picha  chini, hao wanaoonekana kama vimbegu vya maboga ndio lava wenyewe.

lava wa nondo

Ndio hapo unashangaa suti yako nzuri uliyoiacha kabatini, umeinunua kwa bei ghali unaikuta na matobo tobo, unadhani ni mende, hujui kuwa ni kazi ya hawa wadudu.

nguo iliyoliwa na nondo

Sasa kibiblia wadudu  hawa walikuwa wanawakilisha uharibifu, wa aina yoyote. Na ndio maana Bwana Yesu alisema;

“Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba”; ..Akiwa na maana kuwa haijalishi ni vitu vilaini au vigumu, kama ni vya chuma, vitaliwa na kutu,  vikiwa ni laini kama nguo bado vitaliwa na nondo. Hiyo ni kuonyesha kuwa hakuna hazina yoyote inayodumu ikiwa haikuwekezwa mbinguni.

Ni ajabu sana, kumwona Mkristo anayo mabilioni ya pesa kwenye account zake za benki, ukimuuliza zote hizo ni za nini atakuambia najiwekea akiba ya baadaye na watoto wangu. Wakati huo huo hajawahi kufikiria hata kumfanyia Mungu kitu. Hajui kuwa mali zina mbawa, kama biblia inavyosema. (Mithali 23:5)

Kunaweza tokea anguko kubwa la uchumi na fedha isiwe na thamani tena, kunaweza tokea wizi, na hazina zako zote zikachukuliwa na wengine, kunaweza tokea matatizo Fulani ya ghafla na hicho ulichojilimbikizia kwa miaka mingi ukakitumia chote kutatua matatizo hayo, au pengine unaweza ukafa na usifaidi chochote katika hicho ulichojikusanyia wakaja kula wengine, na hao wengine biblia inasema hujui kama watakuwa na hekima au wapumbavu, wakazitapanya kizembe, na hazina yako ikawa ni bure..

Lakini mtu anayejiwekea hazina kwa Mungu, Mtu kama huyo hazina yake ni lazima idumu milele. Kwanza itamwongezea ulinzi wa kiroho na kimwili akiwa hapa hapa duniani, pili itaandikwa mbinguni, na siku ile Bwana atakapomlipa kila mtu kulingana na kazi yake ,basi  na yeye pia atapokea thawabu idumuyo milele.

Jiulize ndugu, nguvu zako zote unazipeleka wapi? Au unamwandalia NONDO azile? Kama utashindwa leo hii kuifanya kazi ya madhabahuni, basi hakikisha kuwa nguvu zako unazozitaabikia huko usiku na mchana, unazielekeza kwa Mungu wako, ili Mungu awe na sababu ya kukukumbuka siku ile, aone kuwa hukwenda kutaabika bure, bali kwa ajili yake.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

Kwanini ndugu wanaokaa pamoja wawe kama mafuta ya Haruni?

SWALI: Naomba ufananuzi wa mstari huu, ni kwanini ndugu wanaokaa pamoja wafananishwe kama na mafuta mazuri yashukayo ndevuni mwa Haruni?

Zaburi 133:1 “Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja.

2 Ni kama mafuta mazuri kichwani, Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake”.


JIBU: Tunapaswa tujiulize ni kwanini awe ni Haruni na sio mtu mwingine kama vile Daudi, au Samweli au Eliya?. Haruni alikuwa ni kuhani mkuu. Na ukuhani wake ulikuwa na matokeo pale alipotiwa mafuta na Mungu (Kutoka 30:30, Walawi 8:12).

Hivyo kitendo cha ndugu kukaa pamoja katika Kristo, tena kwa umoja, wakinia mamoja, kwa upendo wote.. Rohoni kitendo hicho kinachukua umbile la kuhani mkuu anayetiwa mafuta mengi sana ambayo hayaishii tu kwenye kichwa au ndevu zake, bali yanatiririka kabisa mpaka kwenye pindo za mavazi yake.

Na kama tunavyojua leo hii, kuhani mkuu tunaye mmoja tu, ambaye ndiye Bwana wetu Yesu Kristo. Hivyo tunapokaa pamoja kwa umoja sisi kama kanisa la Kristo, msingi wetu ukiwa ni Biblia, basi rohoni tunachukua lile umbile la Kristo alipokuwa anatiwa mafuta na Mungu hapa duniani.  Biblia inasema mafuta aliyotiwa yalikuwa ni mengi kuliko  kuhani au mtakatifu yoyote aliyewahi kuishi hapa duniani.

Waebrania 1:8 “Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.

9 Umependa haki, umechukia maasi; KWA HIYO MUNGU, MUNGU WAKO, AMEKUTIA MAFUTA, MAFUTA YA SHANGWE KUPITA WENZIO.

Unaona, Na matokeo ya mafuta yale, ilikuwa si kingine zaidi ya kuwamulikia watu injili ya kweli, kutenda miujiza, kufungua, kukomboa, kuponya n.k.

Luka 4:18 “Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa”.

Ipo siri kubwa sana katika hilo. Leo hii hatuuoni uhai wa Kristo ndani ya kanisa, kwasababu moja tu, hatuna upendo, wala hatunii mamoja, kila mtu anafikiria mambo yake mwenyewe, na sio ya Kristo. Bwana atusaidie tuufikie umoja wa imani, kama lilivyokuwa katika kanisa la kwanza la mitume. Ambalo kwa kupitia kanuni hiyo waliweza kuupindua ulimwengu kwa kipindi kifupi sana. Kwasababu Mafuta ya Kristo yaliyokuwa yanamiminika katikati yao, yalikuwa ni yale yenyewe kabisa. kwa ule umoja tu na mshikamano waliokuwa nao.

Fikiria ni watu ambao walifikia hatua ya kusema, vitu walivyonavyo sio mali zao binafsi bali za shirika. Je na sisi tunaweza kufikia huko?

Bwana atusaidie sana.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

UPAKO NI NINI?

Ukoma wa nyumba ulifunua nini zamani?

Kwanini Kuhani wa Mungu Eli alikufa kwa kuvunjika shingo?

BADO UPO YERUSALEMU TU..GALILAYA HUTAKI KWENDA?

TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.

Rudi nyumbani

Print this post