Unaweza kuwa umempokea Yesu, na unapitia ugonjwa ambao ni mbaya sana, na pengine usio na tiba, Na unajiuliza inawezekanikaje mimi mtu wa Mungu niwe na ugonjwa kama huu?, au mwanangu? Na mimi namcha Mungu sana na kujitahidi kwenda katika njia zake?.
Ukishafikia hali kama hiyo usianze kunung’unika, badala yake huo ndio uwe wakati wa kutafuta kulijua Neno la Mungu zaidi, kwasababu Neno la Mungu ndio dawa ya kutibu hali unayoipitia.
Sasa kama wewe unadhani ni mtumishi wa Mungu na unapitia hilo tatizo, hebu mtafakari Ayubu, labda yeye alimpendeza Mungu kuliko wewe, lakini aliponywa shida yake wakati wa Bwana ulipofika.
Tukimwacha huyo, yupo mtumishi mwingine wa Mungu, mkubwa sana katika biblia…ambaye Mungu alikuwa anazungumza naye uso kwa uso. Na biblia inasema baada yake hakukuwahi kutokea nabii kama huyo..
Kumbukumbu 34:10 “Wala hajainuka tena katika Israeli NABII KAMA MUSA, ambaye Bwana alimjua uso kwa uso; 11 katika ishara zote na maajabu yote, ambayo Bwana alimtuma kuyatenda katika nchi ya Misri, kwa Farao, na kwa watumishi wake wote, na kwa nchi yake yote”
Kumbukumbu 34:10 “Wala hajainuka tena katika Israeli NABII KAMA MUSA, ambaye Bwana alimjua uso kwa uso;
11 katika ishara zote na maajabu yote, ambayo Bwana alimtuma kuyatenda katika nchi ya Misri, kwa Farao, na kwa watumishi wake wote, na kwa nchi yake yote”
Huyo ni Musa ambaye wengi wetu tunamjua. Lakini Pamoja na Nabii huyu kupata kibali hicho cha kipekee mbele za Mungu, lakini siku moja alishawahi kupata ugonjwa wa laana usio na tiba. Siku moja alishawahi kupata UKOMA tena ule mweupe unaowaka kama theluji.
Kutoka 4: 6 “Bwana akamwambia tena, Sasa tia mkono wako kifuani mwako. Akautia mkono wake kifuani mwake; naye alipoutoa, kumbe! MKONO WAKE ULIKUWA UNA UKOMA, umekuwa mweupe kama theluji”
Huyo ni mtumishi wa Mungu kapata ukoma, ugonjwa ambao ulikuwa ni mbaya kuliko wote nyakati za hizo, na ulikuwa ni ugonjwa wa laana na pigo na usiokuwa na tiba. Hivyo Musa aliupata huu ugonjwa mbele za Mungu. Unaweza kujiuliza kwanini Mungu hakufanya ishara nyingine, mfano wa hizo za nyoka, badala yake akampa hiyo ya Ugonjwa?.
Kwanini asingemwambia tu, tia mkono wako kifuani na ghafla kutokee katika mkono wake dhahabu au almasi, lakini kinyume chake mkono wake uligeuka kuwa mauti,
Na kwanini aitumie hiyo ishara kwenye mwili wa Musa mtumishi wake, na wala si kwa mtu mwingine asiye wake au mnyama?.
Hiyo ni kuonyesha kwamba hata watu wanaompendeza Mungu wakati mwingine watapitia pia magonjwa, tena yale hatari kabisa yasiyo na uwezekano wa kupona, lakini Bwana atayaondoa kama alivyoondoa kwa Ayubu na Musa..
Zaburi 34: 18 “Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa. 19 Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote”.
Zaburi 34: 18 “Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa.
19 Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote”.
Na ndio maana Bwana akamwonyesha Musa ile ishara ya kuugua na kuponywa, kuonyesha kwamba yeye ni Mungu atuponyaye..
“Akasema, Tia mkono wako kifuani mwako tena. Akautia mkono wake kifuani mwake tena, na alipoutoa kifuani mwake, kumbe! Umerudia hali ya mwili wake”.
Hivyo magonjwa, na dhiki za kitambo zisituogopeshe, na kutufanya tunung’unike, au moto wako wa kumtafuta Mungu uzime!.. ni za muda tu! Na zitaisha, Usiache kumwamini Mungu wala usipunguze kumtumikia, kwasababu Mungu atakuponya tu kwa wakati wake..na kila kitu kitarudi kama kilivyokuwa. Wala usiruhusu mawazo yako kila dakika yafikirie ugonjwa wako, mawazo kama hayo yakija yakatae na yapeleke kutafakari vitu vingine, kwasababu vita vikubwa vya shetani vipo katika akili zetu na mawazo yetu.
Mwisho, Neno la Mungu ndio silaha kama tulivyotangulia kusema..usipotaka kusoma Neno binafsi, na mara kwa mara, huwezi kamwe kumshinda shetani, hata uwe mwombaji kiasi gani.. Kwasababu shetani kinachomwogopesha sana, ni jinsi tunavyoyaelewa maandiko. Akijua unayaelewa maandiko vizuri, anakuwa anakuhofu sana..lakini akijua Neno hulielewi vizuri, wewe ndio unakuwa rafiki yake, atakutesa kwa kila aina ya mateso anayoyajua yeye. Na kama hujampokea Kristo neema inakuita leo, mpokee Yesu ufanyike kiumbe kipya.
Bwana akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
USIWE NA HOFU, USHUKAPO CHINI.
NI JAMBO GANI LINALOMTAMANISHA SANA BWANA TUMWOMBE BILA KUKATA TAMAA?
RUDIA, TENA NA TENA KUMWOMBA MUNGU USIKATE TAMAA.
UTAFIKA WAKATI WA WEWE KUACHWA NYIKANI.
RUDI KUMPA MUNGU UTUKUFU.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Amina ubarikiwe mwalimu kwa mafundisho ya maneno ya mungu yenye uzima