USIWE NA HOFU, USHUKAPO CHINI.

USIWE NA HOFU, USHUKAPO CHINI.

Shalom, Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.

Mungu anapotaka kumtoa mtoto wake sehemu moja kwenda nyingine anakuwa kama anamrudisha kwanza nyuma ili ampandishe juu katika hatua nyingine…Vitu vya asili pia vinatufundisha, ili Mshale uweze kwenda mbali Zaidi ni lazima uvutwe nyuma kwa nguvu kwa kadiri iwezekanavyo kutoka katika ule uta..ukiuvuta kidogo utakwenda mbali kidogo, ukiuvuta nyuma sana, utakwenda mbali zaidi, vivyo hivyo katika mkuki, au manati. Kila kitu ili kufike mbali ni lazima kirudishwe nyuma kidogo. Kwasababu nguvu ya kwenda mbali Zaidi inaanzia nyuma zaidi.

Baada ya Mungu kuona ukamilifu wa Ayubu, jinsi anavyomcha yeye na anavyojiepusha na uovu…aliona anastahili kubarikiwa baraka mara mbili Zaidi..na ulipofika wakati wa kumbariki alimshusha kwanza chini na kumnyang’anya vile vyote alivyokuwa navyo…na baada ya kumnyang’anya ni sawa na mshale uliovutwa nyuma unaojiandaa kuachiwa uende mbali zaidi , Na,tunaona baadaye Ayubu alipoachiliwa alikuja kupata vitu mara mbili Zaidi.

Mungu alipoona uaminifu wa Danieli katika nafasi yake ya uwakili wa Uajemi aliowekwa kwamba hali-rushwa wala haibi na kwamba ni mwaminifu siku zote katika nafasi yake…ulipofika wakati wa kumpandisha cheo cha ju Zaidi alikuwa hana budi kushushwa kwenye nafasi ile ya chini kabisa mpaka kupelekwa kwenye tundu la simba kuuawa…hapo alikuwa ni sawa na upinde uliovutwa nyuma, na ulipoachiwa alipanda juu Zaidi..akawa mkuu zaidi ya maliwali wote (Danieli 6:28)

Mungu alipoona uaminifu wa Mordekai katika geti la Mfalme kwamba ni mwaminifu, hali rushwa, na katika nafasi yake hajawa mnafiki wala mtu mwenye nia mbaya na mfalme, Zaidi ya yote alimwokoa mfalme na mauti ya watu wabaya, aliokuwa anafanya nayo kazi..Mungu alipoona huo moyo wake mwema na mkamilifu na alipotaka kumpandisha juu…Mordekai alikuwa hana budi kwanza kuvutwa chini, kwani tunaona alitengenezewa visa vya kuuawa mpaka Adui yake mkubwa akaenda kuchonga mti mrefu ili amtundike Mordekai kwa ruhusa ya Mfalme..na Mordekai alikuwa yupo hatarini kufa kama alivyokuwa Danieli…

Lakini Mungu alimwokoa Mordekai na kumpandisha cheo cha juu Zaidi na kuwa mkuu wa majemedari wa Uajemi..Kutoka kuwa mlinzi mpaka kuwa mkuu wa majeshi…Lakini ilikuwa ni lazima kwanza ashushwe chini kiwango cha kukaribia na kufa.

Na ipo mifano mingi katika biblia ya namna hiyo ambapo kabla ya Bwana kumpandisha mtu kutoka ngazi moja kwenda nyingine…anakuwa anamrudisha kwanza ngazi moja chini ili apande juu Zaidi. Hakuna njia ya mkato.

Kwahiyo usiogope unapoona umepoteza kitu fulani unachoona cha muhimu katika Maisha yako, labda kazi au mali kwasababu ya haki unazozifanya…Ukiona umepoteza vyote hivyo na kufikia hatua upo hatarini hata kupoteza Maisha yako, au heshima yako basi fahamu kuwa ni Bwana amekupenda na anataka kukunyanyua juu Zaidi na pale ulipokuwepo…katika hatua kama hiyo usiache uaminifu wako kwasababu ameiona haki yako na hivyo anataka kukupandisha juu Zaidi kama alivyomfanyia Danieli. Lakini njia ya kupandishwa ndio kama hiyo aliyotumia kwa watumishi wake katika biblia..(unatikiswa kwanza kidogo)

Ukiona hata umefungwa kwa kesi ambayo ni ya kusingiziwa au kwa jinsi isivyo haki, ukiona umefilisika kwa sababu hufanyi biashara za magendo na umekataa biashara zisizo halali..hiyo isikusumbue hata kidogo upo katika kipindi cha kuvutwa chini ili upande juu Zaidi..Ni jambo la muda tu!..

Ukiona unamcha Mungu na hapo kwanza mambo yako yalikuwa yanaenda vizuri.. lakini ghafla mambo yameharibika kunatokea visa hivi na vile…kunatokea maadui wengi sana, hatua kama hiyo unapofikia usimchukie mtu bali ujue kuwa upo katika kipindi cha kushushwa ili upandishwe. Hivyo ndivyo Mungu anavyofanya ili kumpandisha mtu kutoka ngazi moja kwenda nyingine.

Lakini kama umepoteza vyote kwasababu ulikuwa mwasherati, au kwasababu umekamatwa unakula rushwa, au fisadi au kwasababu ya wizi au jambo lolote baya ukafungwa au ukafilisika…hapo ni Bwana amekurudi ili utubu…uache wizi wako, uache uasherati wako, uache rushwa zako, uache mambo yote mabaya unayoyafanya na umgeukie yeye kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote. Na baada ya kufanya hivyo ndipo atakufanyia hayo mengine. Lakini usipotubu hakuna lolote litakalotokea la kukunufaisha. Kwasababu hapo Mungu hajakushusha ili akupandishe juu, bali ili utubu kwanza!

Lakini kama unamcha Bwana, umeokoka, umejitenga kweli kweli na ulimwengu..usiogope! tena majaribu yanapokuja ya namna hiyo unapaswa ufurahi kwasababu ndio wakati wa kukumbukwa kwako.

Bwana akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU

DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI:

Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?

JINSI NEEMA YA MUNGU ILIVYOKUWA KUBWA KWA MKE WA LUTU.

BWANA HUWAJUA HAO WAMKIMBILIAO.

RABI, UNAKAA WAPI?

UFUNUO: Mlango wa 1

CHAPA YA MNYAMA

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
11 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Xamwel
Xamwel
1 year ago

Mtumixhi na mi piah muwe mnanitumia mafundisho kwenye email yangu

Aimable Habimana
Aimable Habimana
2 years ago

Mbarikiwe sana watumishi wa Mungu. Niwaombeni muwe mnanitumia mafundisho kwenye e-mail yangu: vonaim131@gmail.com

Rafael
Rafael
4 years ago

Nitumie tafadhazali abari za daudi kwa email yangu

Tenda wema
Tenda wema
4 years ago

Hujambo ndugu.
nimependa mafundisho haya. Tafadhali uwe unani rushia mafundisho haya kwenye email adress yangu. Mungu akubariki na kazi njema.

Anthony
Anthony
4 years ago

For its a holic group

Anthony
Anthony
4 years ago

I would like to join you

Chrisant Sagara
Chrisant Sagara
4 years ago

Asante