Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?

Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?

Roho, Nafsi, na Mwili, Je! vina tofauti gani?


JIBU: Mwanadamu ameumbwa katika pande kuu mbili, Upande wa kwanza unajulikana kama utu wa ndani, na upande wa pili unajulikana kama utu wa nje.

Utu wa nje ndio huu mwili wetu, ambao unaona, unahisi, unasikia, unatembea, unalala, unakula, unatamani n.k. Yaani kwa ufupi utu huu wa nje (yaani miili yetu) imeumbwa kwa lengo la kutimiza matakwa yote ya hapa duniani.

Lakini utu wa ndani, kidogo ni mpana kuulewa tofauti na huu wa nje, kwani wenyewe haujaumbwa na kitu kimoja, bali umeumbwa na mambo makuu mawili, la kwanza ni nafsi na la pili ni roho.. Hapa ndipo watu wengi wanapochanganyikiwa namna ya kuvitofautisha vitu hivi viwili.

Je Nafsi na Roho ni kitu kimoja?

Ukweli ni kwamba vitu hivi viwili vimeshikana sana, kiasi kwamba hata katika biblia sehemu nyingi, inataja nafsi na sehemu nyingine roho, unashindwa kuelewa ni kipi kinacholengwa hasaa hapo?.

Tunapaswa tujue kuwa Mungu amevishikamanisha hivi vitu viwili kwa pamoja kwa makusudi kabisa kiasi kwamba vionekane kama ni kitu kimoja, lakini kiuhalisi nafsi na roho ni vitu viwili tofauti..Ni sawa na mtu achukie rangi ya blue, kisha aichanganye na rangi ya njano..Matokeo yake hapo kama wewe ulishawahi kufanya stadi za kazi unaelewa ni nini kinatokea, hapo kinachozaliwa ni rangi ya Kijani..

Sasa mtu akikuambia uchukue rangi ya kijani halafu utoe rangu ya blue ndani yake, au rangi ya njano ndani yake, ni jambo ambalo haliwezekani, au kama linawekezana basi ni gumu sana kulifanya.

Ndivyo ilivyo kwa nafsi na roho, vimeshikamanishwa pamoja, kiasi kwamba hakuna mtu awezaye kuvitenganisha isipokuwa Neno la Mungu peke yake, mwanadamu hawezi, shetani hawezi, wala kiumbe kingine chochote..

Tunalithibitisha hilo katika..

Webrania 4:12 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

13 Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu”.

Unaona hapo? Biblia inasema Neno la Mungu pekee, ndio linaloweza kuchoma hata kuzigawa nafsi na roho..Upo ufunuo mkubwa sana hapo? .Usitamani siku ile nafsi yako nafsi yako itengwe na roho yako,..ni maumivu makali sana ndani utakayoyasikia, ukitambua kuwa ndio mwisho wako umefika, kwamba hutakaa uwepo milele..

Mwanadamu au shetani au kiumbe chochote kinaouwezo wa kuutenganisha “utu” wa mtu wa nje, na ule wa ndani, kwa kufanya jambo jepesi la kumuua tu!, .lakini kuutenganisha ule utu wa ndani yaani nafsi yake na roho yake.. hakuna mtu yeyote anayeweza kufanya hivyo isipokuwa ni Mungu peke yake..

Na ndio maana biblia inasema:

Mathayo 10:28 “Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum”.

Sasa Tofauti ya nafsi na Roho ni ipi?

Tukisoma, Mwanzo pale anasema:

Mwanzo 2:7 “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai”

Jiulize ni kwanini haijasema,.. “mtu akawa mwili hai” badala yake ikasema mtu akawa nafsi hai?. Hiyo ni kuonyesha kuwa pumzi ya uhai iliyotoka kwa Mungu iliingia ndani ya nafsi ambayo ilikuwa tayari imeshaumbwa ukisoma Mwanzo 1:27 utaona hilo …Ilipopokea pumzi hiyo ndipo ikawa nafsi hai.

Sasa pumzi ya uhai inayozungumziwa hapo ndio roho yenyewe..Ambayo inatoka kwa Mungu. Hivyo Roho ya uhai inayotoka kwa Mungu ikikutana na nafsi ambayo Mungu aliumba inamtengeneza mtu wa ndani aliye hai.

Ni sawa na unavyochanganya zile rangi mbili, ya blue na njano, kama tulivyoona hapo juu kutengeneza kijani..Sasa hichi kijani chenyewe ndio mtu wa Ndani.

Hivyo unaposoma biblia sehemu nyingine utaona inazungumzia roho, sehemu nyingine inasema, nafsi, sehemu nyingine inasema moyo, usichanganyikiwe..Fahamu kuwa inazungumzia kitu kile kile kimoja kinachomlenga huyu mtu wa Ndani. Japo ni vitu viwili tofuati.

Kwahiyo hii nafsi ndio mtu mwenyewe na ndio imebeba taarifa zote Mungu alizomuumbia mwanadamu ndani yake, kwa mfano wa Mungu, yaani upendo, furaha, sifa, wivu, ibada, utu wema n.k.. vyote hivyo vinatoka ndani ya nafsi ya mtu.

Kwahiyo ili vyote viweze kufanya kazi vilihitaji uhai ndani yake..na uhai huo ndio roho ya mtu..Ni sawa na balbu..ili iweze kuwaka na kutoa mwanga, inahitaji umeme ndani yake..Hivyo nafsi pia ili iwe hai na kuonyesha tabia zote za ki-Mungu ndani yake ilihitaji roho yenye pumzi ya Mungu ndani yake.

Hiyo ndio tofauti kati ya Roho Nafsi na Mwili..

Hivyo uulinde sana moyo wako kuliko kitu kingine chochote kama biblia inavyosema kwasababu huko ndipo zinapotoka chemchemi za maji ya uzima (Mithali 4:23).

Mhubiri anasema..

Mhubiri 12:1 ‘Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo…’

Anandelea kusema..

6 Kabla haijakatika kamba ya fedha; Au kuvunjwa bakuli la dhahabu; Au mtungi kuvunjika kisimani; Au gurudumu kuvunjika birikani;

7 Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, NAYO ROHO KUMRUDIA MUNGU ALIYEITOA’.

Tubu dhambi zako kama hujatubu umgukie muumba wako aliyekupa roho ya uhai bure angali muda upo..Utafika wakati kwa maumivu makali pumzi ya uhai itaondolewa kwenye nafsi yako katika ziwa la moto na kupata mauti ya pili kama inavyozungumziwa katika kitabu cha Ufunuo 2:11 na Ufunuo 22:6 na 20:14.

Ubarikiwe. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Muhtasari wa maelezo haya kwa njia ya video unaweza kuyapata hapa chini.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=hiXs2a7Im2A[/embedyt]

Roho Nafsi na Mwili, humkamilisha mwanadamu.

Mada Nyinginezo:

KUTOKUIHUBIRI INJILI,KUNA MADHARA GANI?

JE! MTUMISHI KUTOKUWA NA FEDHA NI ISHARA KUWA KUNA TATIZO KATIKA IMANI YAKE?

KILEMBA CHA NEEMA, JE! UMEMVIKA MWANAO?

NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE

 

USIPOLITENDEA KAZI NENO LA MUNGU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
EZEKIEL GOSBERTH
EZEKIEL GOSBERTH
2 years ago

Naona kuuliza juu ya vita vya Ha- magedonia,na juu ya Taifa lililoko mawio ya jua

Anonymous
Anonymous
3 years ago

Amina kwa somo tamu.

Kuna swali limekuja, sasa ikiwa Uhai wa Adamu ulianza pale tu Mungu alipompulizia Roho yake ndipo akawa, inamaana nasi pia uhai huo tunao, kwa nini tuahidiwe kupewa Roho tena ?

Mohamed kassim
Mohamed kassim
4 years ago

Amin stay blessed in grace