JE! MTUMISHI KUTOKUWA NA FEDHA NI ISHARA KUWA KUNA TATIZO KATIKA IMANI YAKE?

JE! MTUMISHI KUTOKUWA NA FEDHA NI ISHARA KUWA KUNA TATIZO KATIKA IMANI YAKE?

Jina kuu la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe. Ni siku nyingine tena Bwana ametupa neema ya kuiona, Hivyo ninakukaribisha tujifunze tena maneno ya uzima maadamu siku ile inakaribia.

Watumishi wengi wa Mungu wameshakutana na changamoto kama hii ya watu kuwauliza mbona huyo Mungu wenu mnayemtumikia hawafanyi kuwa matajiri ikiwa yeye ni Tajiri…

Lakini mtu huyu huyu anayeuliza swali kama hili na yeye ukimuuliza Je! Wewe ni mkristo?. Atakuambia ndio, ukimuuliza Je unaiamini biblia unayoisoma atakuambia ndio ninaiamini.

Ukimuuliza tena Je! unamwamini Bwana Yesu? atakuambia ndio, Na vipi kuhusu mitume wake. Je unawaamini nao? atakuambia ndio ninawaamini asilimia mia kuwa walikuwa ni watumishi walioitwa na Mungu kutuletea sisi Imani ya kikiristo..

Lakini ukimwambia Je! Unajua hao unaowaamini sasa kuna wakati hawakuwa na chochote mfukoni mwao lakini Mungu alikuwa anawatumia bila matatizo yoyote. Atakuambia huo ni uongo..

Matendo 3:1 “Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa.

2 Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu.

3 Mtu huyu akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka.

4 Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi.

5 Akawaangalia, akitaraji kupata kitu kwao.

6 Lakini Petro akasema, MIMI SINA FEDHA, WALA DHAHABU, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende”.

Embu jaribu kifikiria kwa ukaribu mistari hiyo. Omba-omba huwa hahitaji pesa nyingi kama vile mtu wa kawaida anavyoweza kuomba. omba-omba huna wanahitaji vichenchi chenchi tu, vilivyobakia mfukoni shilingi 100, mia 200, mia 300 basi ikizidi sana 500. Na ukiwapa wanashukuru sana na kuona kama siku yao imekuwa nzuri sana. Ni hela ambazo mtu wa kawaida haziwezi kumshinda kutoa..

Lakini mitume wa Bwana Yesu Kristo, hawakuwa nazo, walikiri kwa vivywa vyao kuwa hawana fedha wala dhahabu, hawana chochote. Sio kwamba walikuwa nazo wakawa wanazuia kumpa hapana, ni kweli hawakuwa na kitu mfukoni… Lakini hilo halikuwafanya wajione kuwa sio watu walioitwa na Mungu..Badala yake wakamweleza walicho nacho…ambacho ni Jina la YESU KRISTO, na hilo ndilo waliloliona kuwa lina thamani kubwa kuliko fedha zote duniani.

Mtumishi wa kweli wa Mungu anacho kitu ambacho fedha haiwezi kufikia thamani yake, anazo habari za uzima. Injili inayoweza kumfanya mtu apate uzima wa milele jambo ambalo fedha haiwezi kufanya. Hakuna mtu anayeweza kuongeza muda wa Maisha yake kwa fedha. Na ndio maana na sisi tunaoujasiri kusema..Hatuna fedha wala dhahabu lakini tunalo Neno la Mungu linaloweza kuokoa roho za watu.

Hivyo kama mtumishi wa Mungu kwa fedha alizonazo kama uthibitisho wa utume wake, Na si kwa Neno la Mungu. Nataka nikuambie umepotea njia..kwasababu ni kweli wanaweza wasiwe na hicho unachotamani kukiona kwao..Lakini hao ndio watiwa Mafuta wa Mungu wanaokuletea wewe habari njema za wokovu..na uponyaji wa Roho yako, usiwadharau!.

Yule kiwete ambaye tangu kuzaliwa alikuwa hawezi kutembea. Laiti angewadharau wale Mitume na kulazimisha apate fedha kutoka kwao. Angekufa na hali yake, hata angepewa fedha za mchango na watu wote wa dunia nzima. Hakuna matibabu yoyote duniani ambayo yangeweza kumfanya atembee.

Biblia inasema siku za mwisho kutatokea kundi kubwa la watu watakaokuwa wanapenda fedha (2Timotheo 3:2)..Yaani kwao fedha itakuwa ni kipimo cha kila kitu, hadi katika mambo ya rohoni. kama mchungaji huna gari basi hakuna mtu atakayekuja kusikilza Neno la Mungu kanisani kwako hata kama unafundisha kweli kiasi gani..

Kama ukisimama barabarani kuhubiri upo na biskeli na spika yako, hata kama uwepo wa Mungu upo hapo kuwaokoa watu kiasi gani, na ishara na miujiza vinatendeka, watu watageuza vichwa upande wa pili na kuondoka zao. Lakini wakimuona nabii fulani wa uongo anatembea na walinzi, anafundisha mafundisho yake mwenyewe na kuuza chupa za maji ya upako, na Zaidi ya yote hawaambiwi chochote kuhusu Maisha yao ya dhambi. ndio anakuwa wa kwanza kwenda kumsikiliza na kukunua.

Sisemi watumishi wa Mungu wanapaswa wawe maskini, lakini leweke hilo akilini kuwa mambo ya ufalme wa mbinguni hayapimwi kwa mizani ya fedha au utajiri,..Tukilijua hilo tutaweza kujipima sisi na kuchagua ni wapi pa kudumu kujifunza na ni wapi tusidumu, kwa ajili ya usalama wa Roho zetu.. Hizi ni siku zile za hatari ambazo shetani amejikita Zaidi kuwapotosha watu nyuma ya vazi la uzuri na urembo, na utanashati, na mafanikio..lakini ndani yake ni shimo la kuzimu..Hivyo Bwana atusaidie sote.

Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

 

 

Mada Nyinginezo:

ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

CHUKIZO LA UHARIBIFU

NGURUMO SABA

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
M
M
1 year ago

Amina..shukran