Title October 2018

UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?

Mathayo 7:15 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.

16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?

17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.

18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.

19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.

20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.

21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. “

Kuna watu wanasema usizihubiri hizi habari, we fundisha TU watu watubu wawe wakristo inatosha ndiyo kazi yako!. Swali ni je! ukishakuwa mkristo ndio mwisho wa safari?, unahitaji kukua na ndio safari inapoanzia  na sio inaishia. Hivyo basi unahitaji chakula ili ukue, na ujue ni chakula gani unapaswa ukile, maana vyakula ni vingi vijengavyo na vibomoavyo, Hivyo ni kuwa makini kujua ni chakula kipi ule na kipi usile kwa usalama wa roho yako na hatma yako ya milele.

Tunaishi katika kipindi cha hatari ambacho hakijawahi hata kutokea katika vizazi vyote vya nyuma, ambacho kina mchanganyiko mkubwa wa MANABII WA UONGO NA MANABII WA KWELI, Na wote wanafanya kazi moja ya KUVUNA ROHO ZA WATU, aidha kuzipeleka kuzimu au mbinguni, ni kipindi cha hatari sana tunachoishi. Ni muhimu kufahamu unavunwa upande gani, ili usije ukajikuta unadondokea sehemu ambayo haujatarajia.

UPOTOFU ULIOPO SASA:

Jambo kubwa linalowachanganya watu wengi ni kuona pale mtu anayejiita mtumishi wa Mungu halafu bado ni mwasherati, mtukanaji, mlevi, anapenda anasa, na bado miujiza inatendeka na yeye, anafufua wafu, anaombea watu wanaponywa, anatabiri na unabii unakuja kutimia, ananena kwa lugha n.k. kiasi ambacho kinamfanya mtu mchanga ashindwe kuelewa inawezekanikaje huyu mtumishi anafanya mambo ya kidunia lakini bado ishara na miujiza zinatendeka na yeye, Na wala hatumii uchawi ila  anatumia jina la YESU na nguvu za Mungu zinashuka. “HII NI SIRI” na ni jukumu kwa kila mkristo anayethamini maisha yake ya kiroho kufahamu..kumbuka (kuna wanaotumia nguvu za giza kutenda miujiza, siwazungumzii hao, hao ni rahisi kuwagundua lakini nawazungumzia wale wanaotumia nguvu za Mungu ambao ni ngumu kuwatambua.)

Tusome, mstari ufuatao unawazungumzia hao wanaotumia nguvu za Mungu ; kumb.13:1-5″

1 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu,

2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo;

3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.

4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.

5 Na yule nabii, au yule mwotaji wa ndoto, na auawe, kwa kuwa amesema yaliyopotoka juu ya Bwana, Mungu wenu, aliyewatoa katika nchi ya Misri, akakukomboa katika nyumba ya utumwa, apate yule mtu kukupotoa katika njia aliyokuamuru Bwana, Mungu wako, uiendee. Ndivyo utakavyouondoa uovu utoke katikati yako. “

Unaona hapo? Huyo nabii hapo katoa unabii kwa uweza wa nguvu za Mungu na ikatokea, lakini anawafundisha watu waende kinyume na maagizo ya Mungu. Vivyo hivyo na hata sasa katika kipindi hichi cha mwisho Mungu ameamua kuachia mvua yake (UPAKO) kwa watu wote waovu na wema kutujaribu sisi kama TUNAMPENDA BWANA NA KUYASHIKA MANENO YAKE AU LA!. 

 Mtu anaweza akaja kwako na kutoa unabii na ukatimia na kufufua wafu, na kuponya wagonjwa lakini akafundisha injili nyingine akakwambia  ulevi ni sawawanawake kwenda na mitindo ya kisasa ni sawa (anasema Mungu haangalii mavazi anaangalia roho )akakufundisha kuupenda ulimwengu ni sawa, kuoa wake wengi ni sawa, Dunia haiishi leo wala kesho kula maisha, kuwa na pesa nyingi ndio kigezo cha kubarikiwa na Mungu, Mungu siku zote ni Mungu mzuri na hawezi kuwahukumu watu aliowaumba. n.k. na bado mtu huyo akatoa mapepo na kufufua wafu. Na wewe kwasababu NENO na kumpenda Mungu hakupo ndani yako, ukadhani anazungumza ukweli au katumwa na Mungu kwasababu tu! ametoa unabii ukatokea, NDUGU USIDANGANYIKE UMEPOTEA!! .  Biblia inasema jiepushe na huyo mtu, CHUKUA TAHADHARI KWA USALAMA WA MAISHA YAKO..KIMBIA! HARAKA SANA NI BWANA NDIYE ANAYEKUJARIBU KUONA KAMA UNAMPENDA KWELI NA KULIFUATA NENO LAKE AU LA!

Leo hii wewe unayejiita mkristo unapenda injili za kufarijiwa tu! siku zote unapendwa kuambiwa “ALL IS WELL” ulimwengu hautakuja kuteketezwa,tunaishi chini ya neema, mafundisho unayoyapenda wewe ni KUTABIRIWA MAFANIKIO TU!. Lakini fahamu jambo moja BWANA YESU hakuacha enzi na mamlaka mbinguni ili aje kutufia sisi mlabani tuwe MABILIONEA, bali kwa ajili ya dhambi zetu.(hicho ndicho kiini cha injili) yeye mwenyewe alizungumza ..mathayo 16:24-27

” Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.

25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.

26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? 

Leo mkristo anadai anamfuata YESU, lakini kigezo cha kumfuata YESU ni kuwa na MSALABA wako, sasa wewe MSALABA WAKO UKO WAPI?, Jihadhari na haya mafundisho ya uongo yanawapeleka maelfu wa waaminio kuzimu kila siku pasipo wao kujua.

Hawa manabii wa uongo, Bwana Yesu alisema tutawatambua kwa  MATUNDA YAO na sio kwa upako wao, kwasababu Mungu anaweza akamtumia mtu kama chombo tu cha kuazima akishamaliza shughuli nacho anakiacha, mfano tunaona Mungu alimtumia Punda kuongea na Nabii Balaamu kumpa ujumbe, lakini baada ya punda kutoa ujumbe alirudia katika hali yake ya kawaida ya upunda, vivyo hivyo na Balaamu mwenyewe alikuwa ni MCHAWI lakini Mungu alimtumia yeye kuwabariki Israeli, (hesabu 22:21-29), Na pia Mungu aliwatumia wale manabii 400 kumdanganya mfalme Ahabu kwasababu Mungu alikuwa amekusudia mabaya juu yake. (1 wafalme 22:6). Kwahiyo kuwa na upako mtu kuona maono, au kuwa nabii, au kunena kwa lugha au kuponya au kufanya miujiza yoyote ile, sio kigezo cha huyo mtu kuwa NABII WA MUNGU. Tutatawatambua kwa matunda yao (AMBAYO NI NENO LA MUNGU). Nabii wa kweli ni yule anayekuja na ishara pamoja na NENO lakini lililokuu ni NENO.

Kipime mtu anachokuambia je! kinaendana na NENO la Mungu? kama hakiendani na NENO la Mungu weka kando haijalishi anawashirika wengi kiasi gani, au anakubalika kiasi gani, au kanisa ni kubwa kiasi gani, au anaupako kiasi gani. KIMBIA! HILO NI SINAGOGI LA SHETANI!.. 

  • Ukiona unadumu kwenye mafundisho yanayokupeleka wewe kuutazama ulimwengu kuliko kumtazama KRISTO! KIMBIA!  KWA USALAMA WA MAISHA YAKO!!.
  • Ukiona unahubiriwa injili za mafanikio tu! Haufundishwi kufikia toba, au utakatifu maana biblia inasema pasipo huo utakatifu hakuna mtu atakayemwona Mungu (waebrania 12:14). KIMBIA!
  • Ukiona unahubiriwa injili ya kutoa tu! kutoa tu! toa zaka, panda mbegu, n.k. Lakini NENO halihubiriwi, ONDOKA HAPO! Bwana Yesu alisema hivi..mathayo 23:23-24″Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. VIONGOZI VIPOFU, WENYE KUCHUJA MBU NA KUMEZA NGAMIA. ” …KIMBIA! JIOKOE NAFSI YAKO.
  • Ukiona unaenda katika nyumba ya Mungu, hauhubiriwi NENO bali SIASA, usitazame nyuma hata kama kuna miujiza inatendeka kiasi gani....KIMBIA KAMA UNAIPENDA NAFSI YAKO!
  • Ukiona kiongozi wako wa dini, Anaelekeza watu kwake, na sio kwa KRISTO, anajisifu na kujitukuza yeye, utukufu wa Mungu anauchukua yeye.Hapo  hapana tofauti na ibada za sanamu, fahamu kuwa unamwabudu mtu na sio Mungu, isaya 42:8″ Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. “.usimsikilize nabii huyo biblia inasema hivyo… KIMBIA!

Jiulize Wewe unayejiita mkristo  tangu ulipoamini, maisha yako ya kiroho yamesonga mbele kiasi gani. utakuwaje mkristo halafu biblia husomi!??  sasa utawatambuaje manabii wa uongo au manabii wa ukweli kwa namna hiyo watakapokujia na mafundisho yao??. Utakuwa unapelekwa na kila upepo unaokuja wa elimu yoyote. Maana njia pekee ya kumpima nabii wa uongo au Nabii wa ukweli ni kwa NENO TU!. Na sio kitu kingine. Jijengee kila siku tabia ya kusoma NENO na kuomba. Hizi ni nyakati za hatari tunaishi zile zilizotabiriwa kuwa watatokea manabii na makristo wengi wa uongo nao watawadanganya wengi yamkini hata walio wateule. Kumbuka ni wateule ndio wanaozungumziwa hapo kuwa wanaweza wakadanganywa sasa jiulize wewe ambaye sio mteule utaonekania wapi? wewe ndio hautaelewa chochote kinachoendelea utaishia kuwashangilia na kuwasifia kama Bwana Yesu alivyotabiri juu ya manabii wa uongo.

2 Petro 1:10″ Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.”

KWAHIYO NDUGU HUU NI WAKATI WA MUNGU KUTUJARIBU SISI KAMA TUNAMPENDA YEYE NA KULISHIKA NENO LAKE AU LA!. Biblia inasema, MPENDE BWANA MUNGU WAKO, KWA MOYO WAKO WOTE, KWA ROHO YAKO YOTE, KWA NGUVU ZAKO ZOTE, NA KWA AKILI ZAKO ZOTE.

Mungu hadhihakiwi usipoweza kufanya hivyo jua tu utaangukia kwenye huu mstari ufuatao;

2 Thesalonike 2:10-12″… na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
11 KWAHIYO MUNGU AWALETEA NGUVU YA UPOTEVU, WAUAMINI UONGO;12  ILI WAHUKUMIWE WOTE ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu. “

MARAN ATHA!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.

ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!

MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.

NITAAMINI VIPI KAMA KUNA MBINGU AU KUZIMU?

KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE? NA TENA WANA WA ISRAEL WALIMFUKIZIA UVUMBA MALKIA WA MBINGUNI, NDIO YUPI HUYO?


Rudi Nyumbani

Print this post

TAFUTA KUJUA MAMBO YAJAYO

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, aliye Mfalme wa wafalme, na mkuu wa uzima, libarikiwe!

Karibu tujifunze Neno la Mungu, leo tutajifunza umuhimu wa kutaka kutafuta kujua mambo yajayo, Kwasababu biblia inasema katika..

Mathayo 7: 7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
8 KWA MAANA KILA AOMBAYE HUPOKEA; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa’.

Umeona! Bwana amesema kila aombaye hupokea, na kila atafutaye ataona ikiwa na maana kwamba, chochote mtu atakachokihitaji kama akikitafuta kwa bidii atakipata, kama atakitamani na kukihangaikia kwa bidii atakipata, na sheria hiyo haipo tu kwa wakristo bali hata kwa watu wasio wa Kristo, na viumbe vyote mtu yeyote hata asiye mcha Mungu akiamua kutafuta kitu chochoe katika ulimwengu huu kwa bidii atakipata tu! kwasababu ndivyo ilivyo “kila atafutaye atapata”…

Lakini leo hatuzungumzii namna ya kutafuta vitu vya ulimwengu huu, kwasababu Bwana Yesu mwenyewe alisema…”itatufaidia nini kuupata ulimwengu mzima na kupata hasara ya nafsi zetu ?”

Akimaanisha kuwa tusiwekeze nguvu zetu kubwa kutafuta mambo ya ulimwengu huu yanayopita badala yake tuwekeze nguvu kubwa kutafuta kujua mambo ya ulimwengu ujao yasiyoweza kuharibika. Na sheria ni ile ile kwamba “tukitafuta kwa bidii tutapata”

Lakini kama tunavyojua zipo gharama za kutafuta kitu, katika maisha ya kawaida hakuna mtu yeyote anayetafuta elimu ya kidunia katika hatua za awali akajihusisha na mambo ya ulimwengu huu, kwanza kabisa wengi wa wazazi huwa wanawapeleka watoto wao shule za bweni, na shuleni kule wanazuiliwa kuwa na vitu vyovyote vitakavyoweza kuathiri taaluma ya watoto wao, ndio hapo mwanafunzi atazuiliwa kuwa na simu, redio, atazuiliwa pia kuwa mzururaji, zaidi ya yote atazuiliwa hata kuingia jikoni,au kujishughulisha na kazi yoyote ya kujipatia kipato, yeye kazi yake iliyompeleka pale ni moja tu!! yaani kutafuta elimu. Kwahiyo waalimu wanafahamu endapo mwanafunzi akijihusisha na mojawapo ya mambo hayo, wanajua kabisa mwanafunzi yule hatapata kile alichoenda kukitafuta pale.

Hivyo analazimika kufungiwa shuleni, ananyimwa uhuru kwa asilimia kubwa, anakuwa ni sawa na kama yupo gerezani hivi, ananyimwa kujihusisha na mahusiano yoyote yale,tena wakati mwingine analazimika kupelekwa shule ya jinsia moja tu! isiyo ya mchanganyiko, Na zaidi ya yote kama mwanafunzi yule anajielewa atazidi kujiweka kwenye utumwa mwingine ulio mkali zaidi ya ule, ndio hapo masaa yake mengi atatumia kusoma hata ya usiku wa manane, muda anaolala utakuta ni masaa machache sana…ataendelea kwenye hicho kifungo kwa muda wa miaka kadhaa akitafuta tu! kilicho bora na hatimaye atakipata! Lakini je! asingeingia gharama za kuingia kwenye hicho kifungo kikali na cha kijitaabisha hivyo je! angekipata kilicho bora??

Ndio maana Bwana Yesu alisema katika Mathayo 17: 21 “[Lakini namna hii haitoki ila kwa KUSALI NA KUFUNGA.]”

Unaona hapo aliposema kufunga hakumaanisha kuacha kula tu! bali alimaanisha kuacha kujishungulisha na mambo mengine ya kando ambayo yanaweza kuathiri kile kitu unachokitafuta. Hiyo ndio maana ya “kufunga” Kama vile mwanafunzi anavyofunga kwa kujizuia na mambo mengi ili apate anachokitafuta, anafunga kuwa mzururaji, kumiliki simu, kuangalia tv n.k

Mfano mzuri tunaweza kujifunza kwa kiumbe kama kuku, yeye atakapofika wakati wa kuyahatamia mayai yake, analazimika kufunga siku 21, lengo la yeye kufunga sio kwasababu anataka kuutesa mwili wake bila sababu, au kwasababu kapewa masharti ya kufanya hivyo, au kwasababu anatimiza wajibu Fulani, hapana bali ni kwasababu anajua endapo akienda kutembea huko na huko yale mayai aliyokuwa akiyahatamia yatapoteza lile joto na hivyo kuwa viza, na aambulie kutopata kile alichokuwa anakitafuta.

Kadhalika na tunapoutafuta ufalme wa mbinguni, tunapaswa tufunge! Na kufunga sio kuacha kula tu, hiyo ni moja, maana kuu pale ya kufunga ni tunatakiwa tufunge mambo ya ulimwengu huu yanayotuzuia tusifikie malengo yetu, kama vile kuku anavyolihifadhi joto lake kwa siku 21 kwa uvumilivu wote, na sisi vivyo hivyo tunapaswa tulihifadhi joto letu, kwa Roho Mtakatifu tuliyepewa kwa kipindi chote tunachoishi hapa duniani, Biblia inasema katika Luka 12: 35 “taa zenu ziwe zinawaka;…nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao,” hivyo tunapaswa tufunge uasherati, tufunge anasa, tufunge kiburi, tufunge kuzurura huku na kule kutafuta mambo ya ulimwengu huu yanayoharibika na utafutaji wa mali uliopitiliza…zaidi tuelekeze macho yetu mbinguni..kwasababu muda uliobaki ni mchache sana.

Kadhalika na maana ya kusali pia sio tu kujifungia ndani tu, na kupeleka mahitaji mbele za Mungu, hapana ni zaidi ya hapo, maana ya kusali pamoja na kupeleka mahitaji yetu na haja zetu mbele za Mungu ni kukaa katika uwepo wa Mungu muda mrefu ukitafuta kujua na kujifunza huku na kule kuhusu mahali ulipotoka, ulipo sasa na unapoeleka. Hiyo ndio maana ya sala.

Kaka/Dada tafuta mambo yajayo kwa “KUFUNGA NA KUSALI” wafunge marafiki wasio na maana wanaokuvuta katika mambo ya ulimwengu huu, ni afadhali uwe peke yako lakini unaenda mbinguni kuliko kuwa miongoni mwa kundi kubwa linalokwenda Jehanamu ya moto. Rafiki anayekudharau wewe unapomtafuta Mungu au anayekushauri namna ya kumtafuta Mungu wakati yeye mwenyewe hamtafuti ni Mlevi, msengenyaji, mla rushwa huyo atakupeleka jehanamu, tangu lini kipofu akamwongoza kipofu mwenzake? Bwana Yesu alisema wote watatumbukia shimoni..

Dada unayesoma hapa usipotaka kufunga mambo ya ulimwengu huu na kutazama macho yako..usipotaka kufunga uvaaji mbaya, usipotaka kufunga uvaaji wa mawigi, na kupaka wanja na lipstick, usipotaka kufunga usengenyaji wako, usipotaka kufunga tamaa za kuwa maarufu kama wanawake wa ulimwengu huu Kristo atakapokuja hutajua chochote…Hebu jifunze kwa mwanamke Ana wa kwenye biblia aliyefunga mambo yake yote na kuamua kutazama na kutafuta mambo yanayokuja ya mbinguni..

Mwanamke Ana, alifiwa na mume wake akiwa na umri mdogo, na akaamua kutokuolewa tena akafunga mambo yote na kuanza kujishughulisha katika kutafuta mambo yanayokuja tu…Wakati huo Masihi (Yesu Kristo) bado alikuwa hajazaliwa, lakini kwa jinsi alivyokuwa anatia bidii kutafuta sana…Bwana akamfunulia MAJIRA YA KUJA KWAKE, akashuhudiwa kumwona Bwana uso kwa uso. Hivyo wakati wakuu wa dini, hawajui majira ya kuzaliwa Bwana, Mwanamke Ana tayari alikuwa anajua kalenda ya Mungu. Wakati wanawake wengine wanafurahia fashioni za ulimwengu mwanamke Ana, alikuwa anajua Kristo yupo mlangoni kuja ulimwenguni. Tunasoma habari hiyo katika..

Luka 2:36 “Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.

37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana KWA KUFUNGA NA KUOMBA.

38 Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake”

Na mambo haya haya yatatokea katika siku hizi za mwisho, wakati wewe dada unaendelea kujifurahisha na mambo mabovu ya ulimwengu huu, wapo wanawake wenzako mahali fulani Bwana ameshawapa kalenda yake ya kurudi kwake mara ya pili, wakati wewe unasema Kristo haji leo wala kesho wapo wanawake wenzako mahali Fulani ambao dunia inawaona washamba leo, wanazungumza na Bwana uso kwa uso, na wameshuhudiwa mambo mengi.

Kadhalika ndugu unayesema Kristo, haji leo wala kesho, hivyo ni wakati wa kuishi unavyotaka, ni vizuri ukafahamu kuwa ni maelfu wanaowaza kama wewe, lakini wapo wachache wanaofahamu nyakati za kujiliwa kwao, wapo wachache ambao wameamua kweli kufunga mambo ya ulimwengu huu na kuamua kumtafuta muumba wao, ambao tayari wameshapewa kalenda yote ya kurudi kwa Bwana..wakati ulevi wako unastawi, rushwa yako inastawi, kiburi chako kinastawi, anasa zako na uasherati wako unastawi..wenyewe wanainua vichwa vyao juu wakiitazama jinsi ile siku inavyokaribia…

Jifunze kwa Simeoni ndugu yangu, mtu aliyeishi wakati mmoja na mwanamke ANA, yeye naye Roho alimshuhudia kwamba hatakufa hata atakapomwona Kristo akifika ulimwenguni.. Wakati dunia nzima haielewi chochote..Tunayasoma hayo katika..

Luka 2:25 “Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu MWENYE HAKI, MCHA MUNGU, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.

26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.
27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,

28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,

29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;

30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako,

31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;”

Ni maombi yangu kuwa Bwana ataigeuza nia yako na mtazamo wako kuanzia leo na kuendelea, uanze kutamani kujua mambo yajayo, Roho yule yule aliyemfunulia ANA na SIMEONI kuja kwake, mara ya kwanza, Roho huyo huyo anaweza kuyafunua macho yako leo ukaona jinsi kuja kwake mara ya pili kulivyo karibu, endapo tu utakusudia KUFUNGA mambo yote ya ulimwengu na kujitenga kumtafuta Mungu kama Ana na Simeoni.

Kama hujampa BWANA YESU maisha yako, ni vizuri ukafahamu kuwa Hakuna Uzima nje ya yeye, wasanii maarufu wamepita, maraisi washupavu wamepita,.Raisi tu wa Marekani aliyemaliza muda wake, leo hii umeshaanza kumsikia anafifia lakini huyu YESU mpaka leo hii anatangazwa, habari zake hazichakai na ndivyo ilivyo kwa wale wote wanaomcha yeye, hivyo nakushauri kama hujampa maisha yako, tubu leo na ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo upate ondoleo la dhambi zako nawe utakuwa na uhakika wa uzima wa milele.

Mungu akubariki.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine na Bwana akuongezee Neema yake.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

MIISHO YA ZAMANI.

MATUMIZI YA DIVAI.

ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU

KAINI ALIPATIA WAPI MKE?

JE! SHETANI ANAWEZA KUYAJUA MAWAZO YA MTU?

SANDUKU LA AGANO LINAWAKILISHA NINI?


Rudi Nyumbani

Print this post

MSHIKE SANA ELIMU.

ELIMU ni UFUNGUO wa maisha, hiyo ni kweli, lakini ELIMU ILIYO SAHIHI sio tu ufunguo wa maisha, bali pia ni ufunguo wa kila kitu. Na kwa jinsi elimu ya mtu huyo itakavyozidi kuwa kubwa zaidi ndivyo uwezekano wa mtu huyo kufanya mambo yote unavyozidi kuwa mkubwa zaidi.

Kumbuka zipo Elimu kuu tatu zilizopo ulimwengu sasa. 

1)Elimu ya ufalme wa mbinguni.

2)Elimu ya kidunia

3)Elimu ya ufalme wa giza

Leo hii tunaweza kufurahia mafanikio tuliyoyafikia ya kiteknolojia kwa mfano kuchat na watu mitandaoni, kupaa angani kwa ndege, kuzungumza na ndugu zetu walio mbali kwa simu, kutunza vyakula katika majokofu, katazama tv n.k..sio kwasababu dunia imebalika maumbile yake tofauti na ya zamani hapana!, Ni kwasababu wapo watu waliokaa chini kwa muda mrefu mahabara, na katika makarakana usiku na mchana, wengine hata kutokuoa au kuhatarisha maisha yao, wakisoma na kujifunza kanuni za huu ulimwengu jinsi ya kuendana nazo na kwa namna gani watazitumia kubuni njia mbadala ya kuunda vitu. Na kwa bidii yao ya kujifunza na kusoma sana kwa muda mrefu ikawapelekea kugundua vitu ambavyo hata kwa namna ya kawaida unaweza ukasema haviwezakani kutokea. Lakini tunaviona katika jamii zetu kila siku vipo..

Kadhalika shetani naye hakuna jambo ameweza kufanikiwa kulipata kwa mwanadamu kirahisi rahisi kama sio kwa Elimu. Alisoma kanuni za Mungu za uumbaji kwa muda mrefu sana, hivyo kwa kuwatazama viumbe wake na vitu vya asili na nguvu na mamlaka Mungu aliyoweka ndani yao, akagundua kuwa akiwafanya waende kinyume na zile kanuni basi yeye atakuwa na uwezo wa kuzitumia kwa manufaa yake. Na ndio maana jambo la kwanza pale Edeni Shetani hakuja kwa utisho wowote wa silaha kwa Adamu na Hawa hapana bali alikuja na UDANGANYIFU. Ambao alijua kwa huo ataweza kuwadhoofisha UWEZO wao hivyo kirahisi atawapokonya mamlaka yao waliyopewa na Mungu katika hii dunia..

Na ndivyo alivyofanya na kufanikiwa kuuweka ulimwengu chini yake mpaka tunaona alipokuja Bwana wetu Yesu Kristo kuyachukua yale mamlaka tena Adamu aliyoyapoteza. Na haishii hapo tu! kwasababu shetani lengo lake ni kutaka kuwa kama Mungu, na kwasasa ameshafahamu kuwa hawezi tena kufikia malengo yake kwasababu ya YESU basi anachokifanya ni kuwa piga upofu wanadamu wote wasifikie katika viwango vya MAARIFA/ELIMU ambayo Bwana anataka watu wake wavifikie.

Na ndio maana biblia inasema katika Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;”..Shetani ataendelea kutuangamiza kama tutakosa maarifa ya kimbinguni.

Sasa Elimu hizo mbili yaani (Elimu ya dunia na Elimu ya ufalme wa giza), japo kila moja inajitahidi kwa upande wake, kutatua kila jambo, lakini hata moja haijaweza kuleta suluhisho la mambo ya msingi yamuhusuyo mwanadamu. Kwamfano hakuna elimu yoyote inayoweza kuleta dawa ya kifo na kutoa uzima wa milele, au kufufua mfu, au kuumba, au kusimamisha jua, au kuupiga mwezi, au kuamisha visiwa na milima, hakuna hata moja inayoweza kutabiri mambo yanayokuja,..hakuna hata moja ya hizo inazoweza kufanya jambo kama hilo. Wanasayansi wote pamoja na shetani mwenyewe hawana maarifa hayo.

Ni ELIMU moja tu YA KWELI ambayo Mungu aliiweka tangu mwanzo ndiyo inayoweza kufanya mambo yote, nayo ni ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI BASI!!.

Hivyo pale Biblia inaposema katika Mithali 4:13 “Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.”

Haimaanishi ELIMU yoyote tu ile, iliyopo kila mahali, hapana sio elimu ya ulimwengu huu, kama vile isivyokuwa elimu ya wachawi, bali Elimu inayozungumziwa pale ni Elimu inayohusiana na hicho kitabu chenyewe (yaani BIBLIA).

Na kama vile Elimu yoyote ile ilivyo na gharama kuipata kadhalika na kuisoma, vivyo hivyo na hii ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI izidiyo elimu zote inayo gharama nyingi za kuipata. Kila mkristo anapoamini na kumpa Bwana maisha yake ni sawa na mtoto kwa mara ya kwanza aliyeenda kuanzishwa elimu ya awali, anaitwa mwanafunzi, tunafahamu kuwa siku hiyo hiyo hawezi kujua kila kitu kinachohusu shule, siku hiyo hiyo hawezi kupaisha ndege, au kufanya operesheni, hapana bali atakavyozidi kuonyesha bidii ya kujifunza kila siku, kidogo kidogo atajikuta anaongeza kitu katika kichwa chake, atavuka darasa moja, anakwenda lingine hivyo hivyo mpaka baadaye akifika chuo kikuu, ambapo kiwango cha yale maarifa kitakuwa kimeshakolea ndani yake sasa hapo ndio anakuwa na uwezo wa kurusha ndege.

Na ndivyo tunavyojifunza kwa Bwana wetu YESU KRISTO, tunamwona kama vile alivyo, hakuzaliwa na kipawa tu basi cha kuwa na hekima nyingi kiasi kile na kujawa uwezo mkuu kama ule. Biblia haitufundishi hivyo bali tunamwona Bwana tangu akiwa mdogo alikuwa ni mtu mwenye bidii sana KUSOMA ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI, alikuwa akijifunza kupita kiasi hata akiwa na umri wa miaka 12 tu, biblia inarekodi siku tatu usiku na mchana alikuwa akijifunza habari za YEHOVA kwa marabi(Waalimu wa Torati), akiuliza maswali, pale ambapo hakuwa anapaelewa, alisahau hata kula kwa ajili ya KUSOMA TU! Aliwasahau wazazi wake, aliona ule muda walioenda Yerusalemu na wazazi wake ni mchache sana wa yeye kujifunza,

Tunasoma;

Luka 2:45 “na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta.

46 Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, AKIWASIKILIZA NA KUWAULIZA MASWALI.

47 Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake”.

Biblia inasema pia aliendelea kuwa mtu wa namna hiyo hiyo, akitoka katika hatua moja ya hekima hadi nyingi.. Tunasoma

Luka 2:52 Naye Yesu akazidi kuendelea katika HEKIMA NA KIMO, akimpendeza Mungu na wanadamu.

Unaona hapo aliendelea katika Hekima, siku baada ya siku na KIMO kinachozungumziwa hapo sio urefu wa mwili, bali ni KIMO cha KUMJUA MUNGU. Aliweza kuona mahali waandishi walikwama, yeye hakuridhika akavuka pale na kuzidi kujifunza zaidi mpaka siku moja akawa ZAIDI ya wale MARABI waliokuwa juu yake wakimfundisha.

 Tunasoma;

Mathayo 13:51 “Yesu aliwauliza, Mmeyafahamu hayo yote? Wakamwambia, Naam.

52 Akawaambia, Kwa sababu hiyo, kila mwandishi mwenye ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI amefanana na mtu mwenye nyumba atoaye katika hazina yake VITU VIPYA NA VYA KALE”.

Bwana yeye kama mwandishi mkuu pia aliweza kutoa katika hekima yake vitu vipya na vitu vya kale (Agano jipya na Agano la Kale), kwasababu Elimu ya Ufalme wa mbinguni ilikuwa imemkaa sana ndani yake.

Hiyo ni sababu leo hii tunamwona Bwana kuwa mtu ambaye hakushindwa na jambo lolote, hakukuwa na tatizo lolote lililoweza kusimama mbele yake, alipewa maarifa yote na Mungu, alipewa maarifu ya namna ya kuutoa uhai wake na kuurudisha, ni nani leo hii anaouwezo huo?, aliweza kuamrisha mbingu, bahari, na upepo vyote vikamtii,hakukuwa na mgonjwa yoyote aliyeletwa mbele zake asiweze kumponya, Mungu alimpa kila kitu angali akiwa bado hapa duniani.. Na ndipo hapo shetani akajua kuwa hakuna tena tumaini kwake kwasababu vyote alivyovitarijia siku moja avipate vyote vimeshafunuliwa kwa BWANA wetu YESU KRISTO. Haleluya!. Kazi aliyobakiwa nayo sasa ni kutuangamiza kwa kukosa kwetu maarifa ya kumjua YESU KRISTO BWANA WETU.

Bwana YESU alitupa ushauri sisi wote, kwamba “TUJIFUNZE KWAKE” (Mathayo 11:29). Na pia alisema yeye ndiye njia ya kweli na uzima, mtu hafiki kwa Baba isipokuwa kwa njia yake yeye (Yoh 14:6). Hivyo ni lazima tujifunze katika NJIA ZAKE ili na sisi tupate akili tupone.

Kama wachawi na wanasayansi hawalali kila siku wapo wanachunguza na kutafiti juu ya mambo yao na ufalme wao, inatupasaje sisi wakristo ambayo ELIMU YETU inaweza kufanya makubwa zaidi ya hayo?

Ukristo mwanzo wake ni kuamini na kubatizwa, lakini pia ni zaidi ya hapo. Bwana anataka kutupa maarifa ya ziada katika maisha yetu ya kumjua yeye, ili na sisi pia tukue katika kimo na hekima, kama Bwana, lakini tunakuwa wavivu wa KUSOMA na KUJIFUNZA NENO LA MUNGU kila siku.

Japokuwa Paulo alikuwa ni mtume wa Kristo aliyejaa mafunuo mengi, na ambaye mpaka sasa tunatumia nyaraka zake kama urejesho wetu wa kimaandiko, lakini hakuacha KUSOMA na KUJIFUNZA kila siku Elimu ya Ufalme wa mbinguni. Tunasoma akimwambia Timotheo..

2Timotheo 4: 13 Lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa, ujapo ulilete, NA VILE VITABU, HASA VILE VYA NGOZI.

Unaona hapo?, alihitaji Kusoma, kwasababu Elimu ya ufalme wa mbinguni ni kuu sana haina mwisho wake. Hakujiona kuwa amefika au anafahamu kila kitu bali alitaka zaidi na zaidi kujifunza kumjua Mungu katika upana wake na marefu yake. Na hakuishia hapo bali alimwagiza pia Timotheo afanye vivyo hivyo, kama tunavyosoma katika

1Timotheo 4:12 “Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

13 Hata nitakapokuja, UFANYE BIDII KATIKA KUSOMA na kuonya na kufundisha.”

Hivyo na sisi pia kama watoto wachanga, tuitafute sana Elimu ya ufalme wa mbinguni, kwa kutafiti na kuchunguza mambo yote yamuhusuyo MUNGU wa ISRAELI na YESU KRISTO BWANA WETU katika maandiko angali tunaishi sasa, ili tukifikie kile cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo. Amen.

Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani NA KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, NA KUCHUKULIWA NA KILA UPEPO WA ELIMU, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.”

Ubarikiwe sana.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

MAFUNDISHO YA MASHETANI

JE! UMEFUNDISHWA?

UPEPO WA ROHO.

NINI MAANA YA “NITAWAVUTA WOTE KWANGU” (YOHANA12:32)?

JE KUNA ANDIKO LINALOMRUHUSU MWANAMKE KUWA SISTER?

YOHANA MBATIZAJI ALIBATIZWA NA NANI?


Rudi Nyumbani

Print this post

TUZIJARIBU HIZI ROHO.

Biblia inatuambia katika 2Timotheo 3:1 kwamba siku za mwisho kutakuwa na NYAKATI ZA HATARI SANA, na kama ni nyakati za Hatari tunapaswa tuchukue tahadhari kubwa zaidi kuliko hata za watakatifu waliokuwa wanaishi nyakati za kale kabla yetu, kwasababu biblia pia inasema shetani angali akijua kuwa muda wake ni mchache anafanya juu chini awaangushe wengi kwa njia yoyote ile. Mkristo ni kuwa makini huu sio wakati wa kuamini kila “roho” inayodai kuwa ni ya Mungu, biblia imetuonya na kutuambia,

1Timotheo 4:1 “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani”

Sasa mambo ya duniani yanatufundisha nini?, kwamba tunajua hakuna mtu yeyote asiyependa kununua kitu kilicho katika uhalisia wake (original), na kama kitu hicho kitasifika kweli kuwa ni original basi hakitakosa kuwa na feki yake baada ya muda fulani,

Lakini utakuta kwa mwanzo kilipoanza kutolewa masokoni labda tuseme ni simu utaona kuwa karibia simu hizo zote zilikuwa ni original, lakini kwa jinsi siku zilivyokuwa zinazidi kwenda, kidogo kidogo utashangaa kuona feki chache zipo humo humo zikifanana kabisa na zile original, na kwa jinsi siku zitakavyozidi kuendelea kwenda, hata zile original huwa zinazidiwa na feki sokoni, Feki zinakuwa ni nyingi, na matokeo yake huuzwa kwa bei rahisi, na hizo ndio watu hupenda kuzikimbilia kwasababu ni bei nafuu..Lakini baadaye wanajikuta wanaangukia katika majuto pale wanapogundua kuwa hazidumu, halafu bado hazikidhi mahitaji yale ambayo aliyoyatarajia kuyaona kutoka katika hizo simu..

Na ndio hapo inampelekea mtu kuhangaika kutoka kwa fundi huyu hadi fundi yule,na kutumia gharama kubwa zaidi hata ya ile aliyoinunulia, akiona tatizo bado lipo anachukia kabisa kuwa na simu na kujuta ni kwanini alinunua simu na mwisho wa siku kuitupa..tatizo sio AINA YA ILE SIMU bali tatizo ni U-FEKI wa simu.

Kadhalika katika ukristo hakuna kitu ambacho shetani hajafanikiwa kukiundia feki chake, biblia inasema, anao wachungaji wa uongo (Yer 23:1), anao mitume wa uongo (2Kor 11:3), anao waalimu wa uongo, watumishi wa uongo na manabii wa uongo (2Petro 2:1). Kama vile tu Bwana alivyokuwa na watumishi wake wanaomtumikia, Sasa shetani kuwa na watumishi wa uongo tu haitoshi ni vema pia kujua hao watumishi wanamtumikia nani, au wanamtangaza nani, au wanamuhubiri nani?.

Kama vile tu mitume, wainjilisti, waalimu, na manabii wa Bwana walikuwa wanafanya kazi moja ya kumtangaza YESU KRISTO ili watu wote wamwamini yeye, kadhalika hawa nao wanafanya kazi moja ya kumtangaza “yesu” wao ambaye siye yule YESU tunayemwambudu wa kwenye maandiko, na wanafanya hivyo ili watu tu wamwamini huyo waangamie siku za mwisho.

Biblia ilishaweka wazi kabisa, kuwa yupo “yesu” mwingine, yupo “roho” nyingine, kadhalika ipo nayo “injili nyingine” ambayo sio ile Bwana aliyoitoa kupitia mitume wake watakatifu tangu mwanzo, soma

2Wakorintho 11:4 “Maana yeye ajaye akihubiri YESU MWINGINE ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea ROHO NYINGINE msiyoipokea, au INJILI NYINGINE msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!”

Unaona hapo? Kazi ya hawa watumishi wa uongo ni kumtangaza yesu mwingine anayoonekana kama ni YESU halisi, na roho mwingine anayeonekana kama ni ROHO wa Mungu halisi ya Mungu na Injili nyingine ineyoonekana kama ni injili halisi ya Mungu lakini kumbe ni yesu-FEKI, roho-FEKI, na injili-FEKI. Lakini tunajua kitu feki kwa mwonekano wa nje! ni ngumu kugundua kwasababu vyote vitaonekana kuwa ni sawa lakini utendaji kazi wake, na udumuji wake ndio vitakavyowatenganisha..wote watalijata jina la YESU katika shughuli zao za ibada, watatolea mapepo na kutabiri n.k..

Na ndio maana Bwana alisema mtawatambua kwa MATUNDA YAO, hicho tu!.

Mathayo 7.15-23 “ Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.

16 Mtawatambua kwa MATUNDA YAO. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?

17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.

18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.

19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.

20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.

21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”

Ndugu kumbuka ili uwe na uhakika YESU uliyempokea katika maisha yako, ni HALISI, ni lazima ujiulize, JE! UNAUHAKIKA UMEOKOLEWA NA KUSAFISHWA DHAMBI ZAKO KWA DAMU YAKE?, Kiasi kwamba hata ukifa sasa bila shaka yoyote utakwenda mbinguni moja kwa moja?. Kwasababu kumbuka kiini cha Kristo kuja duniani mpaka kufikia hatua ya kuitoa nafsi yake sio wewe kuwa bilionea hapana bali ni suala la UKOMBOZI, je! wewe tangu umfahamu YESU, alishawahi kuyabalisha maisha yako, na kupata uhakika wa wokovu ndani ya nafsi yako?. Jana yako inatofauti na leo yako? Kama sivyo basi! Ujue ulimpokea YESU mwingine ambaye siye aliyehubiriwa na mitume.

Kadhalika unasema unaye ROHO MTAKATIFU, je! huyo Roho aliyeko ndani yako anakufanya kuwa MTAKATIFU kama jina lake lilivyo?, na Je! anakuongoza katika kuijua kweli yote kama maandiko yanavyosema (Yohana 16:13)?, na Je! anakushuhudia kila siku katika maisha yako kuwa wewe ni mwana wa Mungu?(Warumi 8:16). Kama sio basi ufahamu kuwa ulipokea roho nyingine ambayo sio ROHO MTAKATIFU. Kadhalika ulihubiriwa injili nyingine ambayo sio injili iliyohubiriwa na watumishi wa Mungu hao mitume (yaani biblia).

Na ndio maana hauwezi kudumu katika IMANI, ni kwasababu gani? Ni kwasababu hukumpokea Kristo HALISI katika maisha yako, leo unasimama kesho unaanguka, Huyo ni yesu mwingine ulimpokea asiyeweza kukupa wokovu wa uhakika katika maisha yako. Dhambi inakutawala, unashindwa kuitawala dhambi na bado unasema umeokoka, unashidwa KUJILINDA hapo ndugu hujaokoka, biblia inasema wote waliozaliwa na Mungu hawatendi dhambi, ikiwa na maana kuwa dhambi haiwatawali 1Yohana 5.18 “Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu HUJILINDA, wala yule mwovu hamgusi.”

Na ndio sababu huwezi kudumu katika imani kwasababu ni yesu-feki ulimpokea ukidhani ni BWANA YESU KRISTO. Kumbuka kazi ya Mungu haiwezi kuwa na kasoro, Kristo akimwokoa mtu kamwokoa kweli kweli wala habahatishi kwasababu msalaba una nguvu kuliko kitu chochote kilichowahi kusikika chini ya jua hili.

Ulikuwa hivyo ni kwasababu ulikuwa radhi kusikiliza injili isiyo ya gharama,(unayoweza kuipata sokoni muda wowote), ile ambayo manabii wa uongo wanayoifundisha kwamba unaweza ukawa ni mkristo bado pia ukawa ni wa kidunia, unaweza ukawa mkristo bado usijikane nafsi yako usiishe kama mitume walivyoishi kujikana nafsi zao, bado uwe unaishi maisha kama mfano wa watu wa ulimwengu huu na huku umeokoka, ukristo usioweza kuachana anasa, ukristo ambao unaruhusu mwanamke kuvaa suruali na vimini, pamoja na mawigi, na Kupaka lipsticks na wanja, ukristo unaosema Mungu siku zote ni wa rehema, hawezi kuwaangamiza watu wake aliwaumba hivyo ishi tu atakurehemu kwa neema zake maadamu umemkiri kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako inatosha.

Injili ambayo haina muda kusisitiza mtu kuishi maisha ya kujilinda roho yako kila siku, bali unasisitiza kila siku kuulinda mfuko wako. Ukristo unatoa tu mafundisho ya mafanikio ya kidunia na kupuuzia mafanikio ya kimbinguni..

Hizo zote ni INJILI nyingine zisizoweza kumwokoa mwanadamu, na zinatumia jina la “yesu” mwingine linalofanana na BWANA YESU KRISTO kuwatumainisha watu wajione kuwa wapo salama kumbe Kristo hawatambui!, Kinachowatambulisha kwamba wao sio WA-KRISTO ni matunda yanaonekana ndani ya maisha ya watu wanaowahubiria.

Ndugu shetani ni wa HILA tangu mwanzo, alimdanganya ADAMU na kufanikiwa. hashindwi kutundanganya sisi na kufanikiwa kama hatutathamini roho zetu. Tusijipe matumaini ya bure kwamba tumeokoka na huku maisha yetu hayauhakisi wokovu. Ukristo halisi sio rahisi kuupata kama vile kitu original kisivyo rahisi kukipata, Ukristo wa YESU KRISTO MWOKOZI wa ulimwengu una gharama zake.

Ikiwa umekubali kweli ayaokoe maisha yako dhamiria kweli kweli kutoka moyoni, kwamba upo tayari kumwishia yeye, kwa gharama zozote zile atakazokuambia, na yeye akishaona hiyo nia yako na utayari wako basi moja kwa moja ATAKUPA UWEZO WA KUFANYIKA MTOTO WA MUNGU (Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;).

Sasa UWEZO huo wa kufanyika mtoto wa Mungu hauji kwa kila mtu tu ambaye anasema kampokea YESU bure bure, hapana bali unakuja kwa wale tu! waliodhamiria kwa dhati ndani ya mioyo yao kuanzia huo wakati na kwendelea kumwishia BWANA kwa gharama zozote zile, hapo ndipo yule Roho Mtakatifu sasa anaushusha huo uwezo, na hapo ndipo utakapoweza kuishinda dhambi na kudumu katika Imani ya YESU KRISTO BWANA wetu.

Ni maombi yangu kuwa ikiwa tunatamani kweli tuponywe roho zetu, basi tumtafute YESU HALISI, bila kukwepa vigezo vyote vitakavyoambatana na kumfuata yeye. Vinginevyo tutajikuta tumeangukia katika matumaini ya uongo ya manabii na watumishi wengi wa uongo ambao hawana huruma na hatma ya maisha ya mtu bali mambo ya ulimwengu huu tu, na katika siku ile tukajikuta tunaanza kumwambia Bwana mbona nilinena kwa lugha?, mbona niliongozwa sala ya toba?, mbona nilibatizwa? mbona nilikuona wewe kwenye maono? Na yeye atakwambia “Sikukujua kamwe; ondoka kwangu, wewe utendaye maovu”!!.

Ni hali gani utajisikia siku hiyo ukingundua kuwa ulimpokea yesu mwingine ambaye siye yeye HALISI?. Hizi ni nyakati za mwisho za HATARI mtafute YESU KRISTO wa kwenye Biblia, ambaye hasa lengo lake la kwanza ni kuigeuza roho yako kukupa uzima wa milele, na si kitu kingine.SIMAMA IMARA! BWANA ATAKUIMARISHA.

Ubarikiwe sana.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

JIHADHARI NA ROHO ZIDANGANYAZO.

UTHABITI WA AGANO LA MUNGU KWA MKRISTO.

ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO

BWANA ALIPOSEMA “SIKUJA KUTANGUA TORATI BALI KUITIMILIZA” ALIKUWA ANAMAANISHA NINI?

KATIKA 1YOHANA 5:6-9, (A) NI KWA NAMNA GANI YESU ALIKUJA KWA MAJI NA DAMU?


Rudi Nyumbani

Print this post

MAISHA YETU NI MILKI YA YESU KRISTO.

Kanisa linafananishwa na mwanamke, Bwana ndio kapenda kulifananisha kanisa lake na mwanamke, akifunua kwamba kama vile mwanaume ampendavyo mkewe ndivyo Kristo anavyolipenda kanisa lake. Na kama ijulikanavyo huwa kuna hatua zinafuatwa kabla ya mwanamume kumtwaa mwanamke awe mkewe, na moja ya hatua muhimu sana inakuwa ni MAHARI. Mahari kazi yake ni kumwongezea ujasiri mwanamume kwamba hakumpata mke wake kirahisi, amemgharimia. Na baada ya kulipa mahari ,ni ndoa kufungwa,hapo Yule mwanamke anahama kwao na kuhamia kwa mume wake, na zaidi ya yote jina lake la ukoo linabadilika, Jina la ukoo linabadilika kuonyesha kwamba kuanzia huo wakati na kuendelea yeye sio milki ya ukoo wa wazazi wake tena, bali anakuwa milki ya ukoo mwingine wa mume wake.

Sasa Bwana aliruhusu huo utamaduni uendelee kuwepo mpaka leo katikati ya wanadamu, ili kuufanya wokovu ueleweke kirahisi kwetu, kwa kulinganisha namna mwanamke anavyotwaliwa kutoka kwa wazazi wake, mpaka anapotolewa mahari, mpaka anapokuwa mke halali wa mwanaume tutapata picha namna kanisa la Kristo navyo lilivyotawaliwa kutoka katika dunia.

Hatua ya kwanza Kristo anawahubiria watu wake watoke katika ulimwengu kwa ishara na miujiza mingi, kama vile mwanamume amshawishivyo mwanamke katika hatua za awali, kisha baada ya hapo Bwana Yesu ni kulipia mahari, na Mahari anayolipa ni damu yake aliyoimwaga pale Golgotha ambapo alitoa nafsi yake kama fidia kwa mkewe (YAANI KANISA), Gharama hii aliyoingia ilimfanya yeye awe na uhalali wa kulimiliki kanisa asilimia 100%.

Na hatua ya mwisho ni mtu kubadilishwa jina na kupewa jina jipya la mumewe, kama vile jina la mwanamke la ukoo linavyobadilika na kuhamia moja kwa moja kwa mumewe. Sasa mwanamke au mwanamume asipopitia hatua zote hizo ndoa yake inakuwa sio halali.

Sasa mimi na wewe, ili kwamba tuweze kuwa wake halali wa Bwana wetu Yesu Kristo, sharti ni lazima tukubali kumwamini na kumgeukia yeye na kuacha wazazi wetu waliotuzaa, yaani kuuacha ulimwengu na mambo yake yote, sharti lazima tumtii kwa kutubu na kumaanisha kabisa kuacha dhambi na maisha ya nyuma ya anasa na kufanyika viumbe vipya.

Kisha hatua inayofuata baada ya kumkubali Yesu moyoni mwetu, Ni Bwana Yesu mwenyewe kutusafisha kwa maji na kwa damu kwa gharama aliyoingia pale Golgotha, Na ndio maana pale Golgotha wale askari wa kirumi walipomchoma mkuki ubavuni, kulitoka maji na damu, ambayo ile ni kama ishara ya mahari kwetu, kwamba tunasafishwa kwa maji na damu.

1 Yohana 5: 6 Huyu ndiye aliyekuja KWA MAJI NA DAMU, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli”.

Hatua hii inamfanya mtu kuwa mke halali aliyetwaliwa kwa gharama, Bwana anakusafisha dhambi zako zote, na kukuweka kuwa huru na dhambi. Na Neno lake ndio maji yanayotusafisha na Neno lake linasema…

Matendo 2: 37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.

Unaona hapo? namna mke halali wa Yesu Kristo anavyoandaliwa?…sio kwa kujiunga na dhehebu au kanisa bali ni kwa KUTUBU, Na KUBATIZWA KATIKA JINA LA YESU KRISTO, na kupokea kipawa cha Roho. Na kuanzia huo wakati jina lako linabadilika, na kuitwa Mkristo au wa-Yesu Kristo. Kwasababu umebatizwa kwa hilo jina, na Huwezi kuwa mkristo kama hujapitia hizo hatua.

Huwezi kuitwa wa Yesu Kristo kama haujabatizwa kwa hilo jina, sehemu zote kwenye maandiko watakatifu walibatizwa kwa hilo jina, yaani jina la Yesu, ukisoma mistari ifuatayo utaona jambo hilo {Matendo 2:38. Matendo 8:12, Matendo 8:16, Matendo 10:48 na Matendo 19:5}

Kwahiyo kama tu mwanamke aliyeolewa,anakuwa hawezi kujiamulia tu mambo, kwamba anaweza akalala popote atakapo, au akafanya chochote atakacho juu ya mwili wake, bali anakuwa ameingia kama kwenye kifungo Fulani, ambacho hakimpi uhuru wa kuwa na mahusiano ya karibu na kila mtu. Vivyo hivyo na kwa mkristo aliyempa Bwana maisha yake kwa kutubu na, na kubatizwa kwa jina lake Yesu Kristo, anakuwa ni milki halali ya Yesu Kristo, hana ruhusa ya kujiamulia mambo tu, au kufanya chochote anachojisikia akiwa katikati ya mahusiano yake yeye na Bwana.. Na ndio maana Biblia inasema katika

1 Wakoritho 6: 19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? WALA NINYI SI MALI YENU WENYEWE;

20 maana MLINUNULIWA KWA THAMANI. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.

Unaona hapo, biblia inasema “SISI SI MALI YETU WENYEWE” ikiwa na maana kwamba ni “sisi tuliozaliwa mara ya pili ni milki ya mtu mwingine” na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO, hivyo hatuwezi kujiamulia chochote katika miili yetu, au katika aina ya maisha tunayotaka tuishi, Kwasababu yeye (Yesu Kristo) alitununua kwa thamani, nyingi maandiko yanasema hivyo.

Kwahiyo Bwana anao uhalali wa kutufanya chochote endapo tukijihusisha na mambo yoyote katika maisha yetu au katika miili yetu yatakayomtia wivu, au kumuudhi au kumhuzunisha. Kama biblia inavyosema katika..

1 Wakoritho 3: 16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

17 KAMA MTU AKILIHARIBU HEKALU LA MUNGU, MUNGU ATAMHARIBU MTU HUYO. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.

Sasa tukiliharibu hekalu la Mungu yaani miili yetu, Bwana naye atatuharibu, kwahiyo tunapokuwa wakristo sio suala la kujichagulia maisha hapana ni suala la kuchaguliwa maisha na yeye aliyetutolea mahari sisi, Wivu wa Bwana unakuwa kwa wale aliwatolea mahari yaani wale aliowasafisha dhambi zao kwa damu yake, Maovu makubwa yanayomchukiza sio ya watu waliomkataa, hapana bali ni yale ya watu walio wake na bado wanafanya dhambi,(wanakuwa vuguvugu) katika maisha ya kawaida hakuna mwanamume yeyote aonaye wivu akiona mwanamke mwingine asiye wake anafanya uasherati, lakini ataona wivu zaidi endapo akimwona mke wake aliyemtolea mahari na kumwoa anamsaliti na kufanya uasherati. Na ndio maana Bwana baada ya kuwatoa wana wa Israeli Misri aliwapatia amri 10 wao tu! Hakuwapa zile amri kumi watu wote wa ulimwengu mzima, au watu wa Misri. Kwanini? Ni kwasababu Misri hakuwa mke wake halali bali Israeli.

Dada/kaka unayesoma ujumbe huu, kama kweli umeamua kumfuata Bwana na umepita hizo hatua tatu, yaani KUTUBU, na KUBATIZWA KATIKA JINA LA YESU na kupokea ROHO MTAKATIFU. Na bado unajiamulia maisha, nakushauri usifanye hivyo tena, badilisha mtazamo wako, usiwe kama mwanamke mpumbavu aliyeingia kwenye ndoa na asijue mikataba na makubaliano ya hiyo ndoa, kama umeamua kuwa mkristo mwili wako ni hekalu ya Roho Mtakatifu, usilichore tattoo, usifanye uasherati, usiunyweshe pombe, wala usiuvutishe sigara, usiuvalishe nusu uchi, wala usiuvalishe mavazi yasilolipasa ya jinsia nyingine, wala usiufanye mwili usiwe katika hali yake ya asili. Kwasababu mwili huo sio milki yako mwenyewe ni Milki ya mtu mwingine ambaye anaweza kukufanya lolote endapo ukiuharibu na hautapata mtetezi.

Zipo faida leo ukidumu katika uaminifu wako kama bibi-arusi wa Kristo, asiye na hila wala mawaa, kwasababu biblia kama inavyosema katika mbingu mpya na nchi mpya Uje mji mtakatifu wa Mungu yaani YERUSALEMU mpya ushukao kutoka mbinguni ndio bibi-arusi wa Kristo(Ufunuo 21), Mungu atakaa ndani yake, Na katika huo (ambao ndio sisi) Mungu ndio atafanya maskani kumbuka hatafanya maskani kwa kila mtu tu atakayekuwepo huko hapana, bali kwa bibi-arusi tu.. Hivyo tukaze mwendo kama bibi-arusi wa kweli wa Kristo.

Ubarikiwe.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine, na Bwana akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.

JE! NYWELE ZAKO ZINAOTA AU ZIMESIMAMA?

UNAFANYA NINI HAPO?

BWANA ALIMAANISHA NINI KWENYE MSTARI HUU MARKO 2:21″ HAKUNA MTU ASHONAYE KIRAKA CHA NGUO MPYA KATIKA VAZI KUKUU;?

ULE MFANO WA WANAWALI 10 (MATHAYO 25), WALE WATANO HAWAKUWA NA MAFUTA YA ZIADA KATIKA CHUPA ZAO JE YALE MAFUTA YA ZIADA YANAWAKILISHA NINI?


Rudi Nyumbani

Print this post

ITAMBUE KARAMA YA MUNGU.

Bwana Mungu wetu kaumba vitu vyote vya mwilini, kufunua vitu vya rohoni, aliumba milima, kufundisha kuwa kuna milima ya rohoni, aliumba maji kuonyesha kwamba kuna maji ya rohoni, aliruhusu mauti iwepo kufunua kwamba kuna mauti ya kiroho,aliruhusu vyakula viwepo ili kufunua kwamba kuna vyakula vya rohoni, kwasababu mwanadamu ameumbwa katika pande mbili, rohoni na mwilini. Na ndio maana alisema kwenye Neno lake Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu (Mathayo 4:4)”.

Hivyo kama kuna mauti ya mwilini, ni wazi kuwa ipo pia mauti ya rohoni. Na kama vile, mauti ya mwilini ilivyo na nguvu leo, kiasi kwamba kila nafsi lazime ipitie, vivyo hivyo mauti ya rohoni ina nguvu ile ile ambayo inalazimisha kila kiumbe kife kwa namna ya roho. Na hii mauti ya rohoni iliingia pale Edeni, Adamu na Hawa walipoasi. Na kama tunavyojua leo hii hakuna dawa ya kifo cha mwilini, Kifo ni kifo tu! Vivyo hivyo na dawa ya Kifo cha rohoni haikuwepo mpaka njia ya mti wa uzima YESU KRISTO ALIPOFUNULIWA. Ndio tiba ya kifo ikapatikana vinginevyo hakungekuwa na uzima wa milele kwa kiumbe chochote kile.

Kwahiyo mara nyingi Bwana anapenda kutufundisha kwa kutumia mifano ya mwilini, kufunua vitu vya rohoni, kwamfano tunamwona yule mwanamke msamaria siku moja alipokwenda kisimani kuteka maji akakutana na Bwana, na Bwana akamwomba maji, na yule mwanamke alipotaka kuanza maandalizi ya kumpatia maji kutoka katika kisima kile, kwa kumuuliza baadhi ya maswali,Bwana alimkatisha palepale na kumwambia… “ kama ungaliijua KARAMA YA MUNGU, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, UNGALIMWOMBA YEYE, NAYE ANGALIKUPA MAJI YALIYO HAI (Yohana 4:10)”

Na palepale yule mwanamke alidhani Bwana anazungumzia habari za maji yale ya mwilini ya kwenye kwenye visima, akafurahi akatamani apewe yale maji. Tunaweza kuona mistari hiyo tuone jambo..

“11 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai.

12 Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake?

13 YESU AKAJIBU, AKAMWAMBIA, KILA ANYWAYE MAJI HAYA ATAONA KIU TENA;

14 walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi HATAONA KIU MILELE; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, YAKIBUBUJIKIA UZIMA WA MILELE.

15 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka”

Unaona hapo, Bwana anazidi kumtoa yule mwanamke Msamaria kwenye mawazo ya maji ya mwilini na kumpeleka kwenye mawazo ya maji ya rohoni, lakini bado alikuwa hajamwelewa. Alijaribu kutumia mfano wa maji ya mwilini ili kumwonyesha umuhimu wa maji ya rohoni lakini bado hakumwelewa vizuri mpaka baadaye kidogo. Alijaribu kumfunulia KARAMA YA MUNGU lakini bado ilimuwia ngumu kumuelewa kwa wakati ule kwasababu ya mapokeo ya kibinadamu aliyokuwa nayo. Bwana alichotaka kwa yule mwanamke ni KUTUBU, NA KUACHA DHAMBI ALIZOKUWA ANAZIFANYA, NA KUMGEUKIA MUNGU kwa moyo wake wote! Na kuishi maisha mapya yanayompendeza Mungu Hicho tu! ndio Bwana alichokuwa anatafuta kwa yule mwanamke. Hiyo ndiyo KARAMA YA MUNGU aliyokuwa anataka kumpa yule mwanamke…ili asife kwa kukosa maji ya uzima akaukosa uzima wa milele..Na ndio maana biblia inasema katika..

Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; BALI KARAMA YA MUNGU ni UZIMA WA MILELE katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Na baada ya Bwana kumfunulia siri ya moyo wake kwamba anao waume watano na yule aliyenaye sasa si wake, ndipo alipotambua kwamba yeye ni mwenye dhambi, na kwamba Bwana alikuwa hazungumzii maji ya mwilini bali ya roho yake, yatakayompa uzima wa milele.

Tunaweza tukajifunza tena mfano mwingine katika maandiko wa Mtu aliyeielewa haraka KARAMA YA MUNGU pasipo Bwana kutumia nguvu nyingi kumfafanulia, na huyu si mwingine zaidi ya Petro. Wakati Fulani Bwana alimwendea Petro kwa mara ya kwanza kama alivyomwendea yule mwanamke Msamaria, akamkuta anaosha nyavu, kwasababu wamefanya kazi ya kuchosha usiku mzima bila kupata kitu, Na Petro alipomwona Bwana alidhani ni muhubiri tu wa kawaida, mwalimu wa torati kama walimu wengine, hivyo kwa heshima yake akaona bora amtii tu, Tunasoma hayo katika..

Luka 5: 4 “Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.

5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.

6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;

7 wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama.

8 Simoni Petro alipoona hayo, alianguka magotini pa Yesu, akisema, ONDOKA KWANGU, KWA KUWA MIMI NI MTU MWENYE DHAMBI, BWANA.

9 Maana alishikwa na ushangao, yeye na wote waliokuwa pamoja naye, kwa sababu ya wingi wa samaki walioupata”;

Unaweza ukaona hapo, Petro baada ya kuiona ile ishara ya kupata samaki wengi namna ile, akatambua KARAMA YA MUNGU nyuma ya ile ishara, akatambua kuwa mtu aliyesimama mbele yake ni MKUU WA UZIMA, na yeye ni mtakatifu na hachangamani na uchafu, akaogopa akamwangukia chini akamwambia “ONDOKA KWANGU, KWA KUWA MIMI NI MTU MWENYE DHAMBI, BWANA” alitambua Bwana Yesu hakuja kumpa yeye VIKAPU VYA SAMAKI, hakumfanyia ile ishara ili kumfanya yeye kuwa milionea, bali aliifanya ile ishara ili kumwonyesha Petro kwamba yeye ni mwenye dhambi kiasi gani na kwamba anahitaji UZIMA WA MILELE. Bwana hakumfanyia ile ishara Petro kwasababu anavutiwa sana na ile kazi aliyokuwa anaifanya ya kuvua samaki, hapana alimfanyia Petro ile ishara kwasababu aliona dhambi ndani ya Petro na hakutaka Petro apotee, Na Petro alilitambua hilo akatubu mbele zake.

Na jambo hili hili linaendelea leo, Bwana Yesu anakutembelea kwenye mambo yako unayoyafanya, labda shughuli Fulani ya kujipatia kipato, au labda elimu, au mali, au afya…Inatokea umepitia au ulipitia hali Fulani ulikuwa unaugua sana na Bwana akakuponya kimiujiza, na ndani ya moyo wako ukashuhudiwa kuwa ungestahili kufa lakini umepona… Sasa huu si wakati wa kuanza kutazama mambo ya mwilini, kwamba sasa umepata afya ndio wakati wa kusaka fedha kwa nguvu uwe tajiri kwasababu Mungu kakunyanyua tena, au ukadhani kwamba Bwana alikuponya kwasababu alikuhurumia sana ulipokuwa unateseka na maumivu ya magonjwa yako,

Nataka nikwambie ndugu Bwana hakukuhurumia kwasababu ulikuwa unateseka na maumivu ya ugonjwa bali alikuhurumia akakuponya kwasababu alikuhurumia usije ukafa na dhambi ulizo nazo ndani yako na ukaingia kwenye lile ziwa la moto hivyo ni muhimu sana kuielewa KARAMA YA MUNGU juu maisha yako? Bwana alikuponya kimiujiza ili UKATUBU, ukaache uasherati, ukaache anasa, ukaache usengenyaji, ukaaache rushwa,ukaache kuishi na mume au mke ambaye hamjafunga ndoa, ukaache kuiba, ukaache pombe, alikuponya magonjwa ya zinaa ili ukaache uasherati na uzinzi n.k

Bwana hakukufanikisha kwenye kazi yako ya kujipatia kipato, kwasababu anataka sadaka au fungu la kumi kutoka kwako, au kwasababu alikuhurumia sana ulikuwa maskini kwa muda mrefu na ulikuwa unateseka hapana!! Bwana alikufanikisha kwenye shughuli zako kwasababu anaona maisha yako kuna sehemu pengine hayajakamilika mbele zake, anakufanyia ishara kubwa namna hiyo kama alivyomfanyia Petro, anataka UANGUKE CHINI utambue kwamba, Jicho la Mungu linakutazama kuliko unavyodhani, mambo yako na dhambi zako za siri anayoana kuliko unavyofikiri, ziko wazi mbele zake, anataka uone kwamba MTAKATIFU WA WATAKATIFU AMEKUSOGELEA, Anataka uone kwamba hatua moja mbele yako kasimama mtu asiyechangamana na dhambi. Na anataka akupatie uzima wa milele!

Biblia inasema mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme wa mbinguni, (Yohana 3:3). HIYO NDIYO KARAMA YA MUNGU KWAKO.

Bwana Azidi kukubariki sana, Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

KARAMA ILIYO KUU.

MOYO ULIOELEKEA KWA MUNGU.

MTUME PAULO ALIKUWA NA MAANA GANI KUSEMA NIKAKUFA KILA SIKU??

MBONA MUNGU ANARUHUSU WATU WAPATE SHIDA, ILHALI ANA UWEZO WA KUTUEPUSHA?


Rudi Nyumbani

Print this post

UMEPATA UHAKIKA WA KUTOKUINGIA HUKUMUNI KATIKA SIKU ILE?

Jaribu kufikiria dikteta Adolf Hitler wa ujerumani Yule aliyesababisha vita ya pili ya dunia, na kuhusika kwa mauaji ya mamilioni ya raia wasiokuwa na hatia ulimwenguni kote, mfano leo hii angekuwa hai, unadhani hatma ya maisha yake ingekuwa ni nini?, watu wa ulimwengu mzima wangetaka Yule mtu apewe adhabu gani?, Ni wazi kuwa kila mtu angetoa maoni ya adhabu yake ya kipekee ya mateso yasiyokuwa ya kawaida ambayo walau yangeweza kulipiza kisasi cha yale mabaya yote aliyowafanyia watu wasiokuwa na hatia, wale watu aliowachoma katika matanuru ya gesi na kuwaua kwa vifo vya kikatili na mateso na kusababisha vita ya pili ya dunia. Yeye naye angepewa adhabu mojawapo ya hizo watu wangeridhika kumuona analipa deni la alichokipanda.

Lakini pia jaribu kufikiria mfano amekamatwa na kwenda kuhifadhiwa mahali Fulani pa siri, kisha ukasikia baada ya siku chache kaachiwa huru, sasa ni raia wa kawaida kama raia mwingine ambaye hajafanya kosa lolote, na cha kushangaza zaidi sio tu kutokupewa adhabu yoyote bali hata MAHAKAMANI penyewe mahali ambapo ni pa haki hajapandishwa kushitakiwa. Badala yake kaachiwa yupo huru na anaendelea na maisha yake ya kawaida…

Kwa namna ya kawaida hilo ni jambo lisilokaa liwezekane, lakini kwa Mungu limewezekana..

Bwana Yesu anasema.. Yohana 5:24 “Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; WALA HAINGII HUKUMUNI, BALI AMEPITA KUTOKA MAUTINI KUINGIA UZIMANI”.

Ndugu yangu mimi na wewe nafsi zetu zinatushuhudia kabisa sio wakamilifu kwa asilimia zote, na kama sio wakamilifu mbele za Mungu amri ni moja tu, ni lazima tukahukumiwe adhabu kwa kutokukamilika mbele zake, Na biblia ipo wazi juu ya hilo, Lakini ashukuruwe Kristo alisema amwaminiye yeye, yuna uzima wa milele, WALA HAINGII HUKUMUNI, BALI AMEPITA KUTOKA MAUTINI KUINGIA UZIMANI.

Ikiwa na maana kuwa siku ile Kristo atakaposimama kuyahukumu mataifa yote ulimwenguni katika kile kiti chake cheupe cha enzi wale wote waliomwamini yeye hawatakuwepo hapo, badala yake wao ndio watakaosimama na Kristo kuyahukumu mataifa yote.Tunasoma..

Ufunuo 20.11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.

12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.

13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.

15 Na iwapon mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.

Unaona hapo? Leo hii wewe ni mlevi,mtazamaji wa pornography, mfanyaji wa mustarbation, msengenyaji, mwizi, mzinzi, maisha yako hayana matumaini, unaishi kwa hofu, kila siku unahisi kuhukumiwa ndani ya nafsi yako, kuwa njia unayoiendea ni ya mauti, na unafahamu kabisa kuwa hata ukifa leo utahukumiwa tu na kwenda katika ziwa la moto, kwanini unaendelea kuyahatarisha maisha yako, kwa kuishi maisha ya namna hiyo ya kutokujali?, kwanini unaipuuzia neema hii ya kipekee ya kuvukishwa toka mautini mpaka uzimani? Neema ya kutokuingizwa hukumuni? Bwana anasema NJOO! KWANGU unywe maji ukate hiyo kiu..Lakini bado upo vuguvugu, unadhani kwa matendo yako utaweza kusimama mbele zake siku ile? hii neema haitadumu milele..Ni neema ambayo mwanadamu yoyote asingestahili kupewa.

Ni maombi yangu, tusitamani KUSIMAMA MBELE YA KITI CHEUPE CHA HUKUMU CHA MUNGU siku ile kwasababu tukishajikuta tu tumesimama pale, habari yetu imekwisha hatutakuwa na cha kujitetea, kwa njia yoyote makosa ni lazima tu yaonekana ndani yetu. Na baada ya hapo ni safari ya moja kwa moja kwenda katika lile ziwa la moto.

Tuipishe hukumu ya Mungu hakuna anayependa kupandishwa mahakamani hata  katika mahakama za kibinadamu tu hakuna anayenda kufikishwa kule, itakuwaje siku ile kukutana uso kwa uso wa Mungu mwenyewe katika mahakama? Ni jambo la kutisha sana, tusitamani tuwepo.

Tubu sasa maadamu muda upo, salimisha maisha yako kwa Kristo leo, kesho haipo, kabatizwe katika ubatizo sahihi baada ya kuamini kwako kama haujafanya hivyo haraka iwezekanavyo ili upate ondoleo la dhambi zako, na ubatizo sahihi ni ule wa kuzamishwa kwenye maji mengi na uwe ni kwa jina la YESU KRISTO ubatizo mwingine nje ya huo ni batili, Kisha Bwana atakupa Roho wake mtakatifu na hapo utakuwa UMESHAZALIWA MARA YA PILI..Na kama hizo hatua hazijakamilika ndani yako, hapo bado hujazaliwa mara ya pili. Bado hujavuka toka mautini kwenda uzimani, bado hujaikwepa hukumu…

Fanya bidii kumtafuta YESU siku hizi ni za hatari.

Ubarikiwe sana.

Tafadhali “share” kwa wengine ujumbe huu, 

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU.

NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!

UPUMBAVU WA MUNGU.

JE! NI HALALI KWA MTU WA MUNGU KUTUMIA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO?

JE! NI DHAMBI KWA MKRISTO KWENDA HOSPITALI AU KUTUMIA MITI SHAMBA ANAPOUGUA?


Rudi Nyumbani

Print this post

MTETEZI WAKO NI NANI?

Mwinjilisti mmoja maarufu wa Marekani aliyeitwa Danny Martin, katika jitihada zake nyingi za kumtumikia Mungu siku moja usiku alijiona kwenye ndoto kwamba amekufa,na huko upande wa pili alijikuta yupo safarini kuelekea mbinguni, kwa mbali aliyaona malango makubwa sana, lakini alipokaribia mahali pale alisikia mtu mmoja akimwambia “Ni nani huyu anakaribia hapa?” Kwa ujasiri akajibu ni “mimi Martin Muhubiri wa Injili” lakini wale watu wakamwambia kabla hujaingia ndani subiri kwanza hapo mlangoni tuliangalie jina lako kama lipo kwenye KITABU au la!

Hivyo walipoangalia na kulikosa wakasema “Jina lako halimo huku”…Lakini Danny akasema “Haiwezekani jina langu kukosekana humo mimi ni mtumishi wa Mungu” wale watu wakamwambia hiyo haijalishi ulikuwa nani duniani ukishafika hapa kama jina lako halipo huku, hatuna cha kukusaidia huwezi kuingia ndani ya malango haya ya mbinguni.

Ndipo Danny akawaomba wale watu wamsaidie afanye nini? Lakini wale watu wakamwambia sisi hatuwezi kukusaidia labda kama unataka kukata rufaa kwa Mungu mwenyewe katika kile KITI CHAKE CHEUPE CHA ENZI . 

Ndipo Danny akasema sina namna inanipasa nifanye hivyo. Basi wakamruhusu kuelekea mahali kilipo kiti cheupe cha Enzi cha Mungu, juu sana. (Anaeleza Danny) kwa jinsi nilivyokuwa ninazidi kuelekea juu ndivyo mwanga mkali ulivyokuwa unazidi sana, nilikuwa ninakwenda kwa haraka lakini ilinibidi nipunguze mwendo na baada ya muda kidogo nikasimama kabisa. Ndipo nikasikia sauti ikisema ni nani huyu anayekikaribia kiti changu cha hukumu cha haki?..Ndipo nikasema ni mimi Danny, mwinjilisti wa Kimarekani niliyevuna roho nyingi sana za watu kwako, lakini nilipofika getini wale walinzi walinizuia nisiingie.

Ndipo ile sauti ikamwambia “Vema mimi ninapenda haki”..”Mimi ninazo AMRI”..Je! Danny katika maisha yako yote hujawahi kusema uongo? . Danny anaelezea akisema “nilidhani mimi nimekuwa mtu mwaminifu siku zote lakini nilipofika mbele ya ule uwepo wa ajabu wa Mungu nilijiona kuwa kumbe sikuwa hivyo”..Ndipo nikasema …”Hapana Bwana nimekuwa nikisema uongo”…Akaniuliza tena…Danny ulishawahi kuiba?…Danny anasema: hapo nyuma nilidhani kuwa mimi ni mwaminifu sana lakini mbele zake siku hiyo niliona mapungufu mengi sana ndani yangu..Ndipo nikamwambia “Ndio Bwana nilishawahi kuiba”…

Akaniuliza tena, Danny ulishawahi kutenda dhambi?..Nikamjibu Ndio Bwana..

Akaniuliza..ulishawahi kufanya hivi, ulishawahi kufanya vile?…..Nikasema Ndio Bwana nilishafanya..

Danny anazidi kuelezea ( wakati huo nilisikia kama mifupa yangu inachomoka kwenye maungio yangu, nikitazamia tu kusikia lile neno Bwana alilolisema katika Mathayo 25: Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;))..

Lakini muda huo wakati nayatazamia hayo yafuate nyuma yangu nilisikia sauti nzuri ya unyenyekevu na ya kupendeza,ikizungumza na nilipogeuka nikaona sura nzuri ya tabasamu ambayo sikuwahi kuiona hapo kabla katika maisha yangu..Akasema:

Baba ni kweli Danny kwa bidii zake alijitahidi kufanya kilicho kizuri japo alishindwa, lakini kipo alichokifanya alipokuwa duniani, yeye alitia juhudi zote kusimama kwa ajili yangu Hivyo mimi nami nipo hapa kusimama kwa ajili yake.

Ndugu yangu Je! Bwana hakusema? Katika Luka 9: 9.23 Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.

24 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.

25 Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?

26 KWA SABABU KILA ATAKAYENIONEA “HAYA” MIMI NA MANENO YANGU, MWANA WA ADAMU ATAMWONEA HAYA MTU HUYO, ATAKAPOKUJA KATIKA UTUKUFU WAKE NA WA BABA NA WA MALAIKA WATAKATIFU.

Ipo siku ambayo Bwana atatukiri mbele za Baba yake, pia ipo siku ambayo Bwana atatukana mbele za Mungu.

Leo hii tunamwoneaje Kristo HAYA?. Ni pale tunapokataa kujikana nafsi zetu kwa Kristo kila siku, pale tunapoambiwa tutubu tukaoshwe dhambi zetu sasa wakati muda angali bado upo lakini sisi tunaona kama siku tukiwa hivyo watu watatuona kama washamba, pale unapoona siku ukiwa mkristo, pombe hutakunywa tena, pale unapoona siku ukiwa mkristo disco hutakwenda tena, unapoona siku ukiwa mkristo uasherati hutafanya tena, pale unapoona siku ukiwa mkristo kampani zako mbovu hutaongozana nazo tena, unakataa kufanya hivyo sasa kwasababu unaupenda ulimwengu kuliko Mungu…Hapo ni sawa na kumwonea HAYA Kristo na maneno yake. Biblia inasema katika

1 Yohana 2 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.”

Ndugu kama ukifa leo hii utaenda kuwa mgeni wa nani huko? Ni nani atakayesimama huko kukutetea mbele ya kile kiti cheupe cha hukumu cha Mungu?. Bwana anasema KWA SABABU KILA ATAKAYENIONEA “HAYA” MIMI NA MANENO YANGU, MWANA WA ADAMU ATAMWONEA HAYA MTU HUYO, ATAKAPOKUJA KATIKA UTUKUFU WAKE NA WA BABA NA WA MALAIKA WATAKATIFU.

Unakataa kuchukua msalaba wako sasa umfuate Kristo, kwasababu unajua ukristo hauhitaji mwanamke anayevaa nguo zinazochora maungo, na suruali, unajua mwanamke wa kikristo havai mapambo ya kikahaba na kiasherati, unaogopa utaonekana wa kale, hivyo unaona ni bora uwe vuguvugu, huko ni kumwonea HAYA KRISTO. Ni kweli leo utafanikiwa kukwepa hayo kwa kitambo sasa lakini siku ile ambayo utasimama kwa nafsi yako, mahali ambapo utahitaji mtetezi utakosa, utagundua kuwa ulivyoipenda nafsi yako wakati ulipokuwa duniani ndivyo ulivyokuwa unaipoteza, na siku hiyo ndiyo utagundua kuwa Bwana hakudanganya alivyosema “”Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.

Ndugu yangu maisha haya yanapita, unatafuta mali kupita kiasi unamsahau Mungu muumba wako, unapendezwa na mambo ya ulimwenguni hata muda na Mungu wako huna, kuna siku itafika utamuhitaji sana Kristo awe mtetezi wako lakini yeye atasimama kando asikujibu lolote kwasababu hataona la kukujibu, Badala yake atakukana na kusema sikujui wewe. Utajisikiaje siku hiyo?, mbele ya mahakama ya haki ya Mungu?

Hizi ni nyakati za hatari biblia ilizozisema, ni heri ujisalimishe kwake, kwa hii miaka sabini themanini uliyopewa hapa duniani kuliko ukawe na majuto ya milele baada ya kufa. Isikie sauti ya YESU KRISTO leo na usiyaonee haya maneno yake. Anza maisha yako upya uchukue msalaba wako sasa umfuate, uwe radhi kuipoteza nafsi yako kwa ajili yake ili uwe na uhakika siku zinazokuja kwamba utaipata kuliko kuipata sasa kwa anasa na raha za kitambo za dunia kisha siku ile uipoteze milele.

Tubu dhambi zako muda huu, na ikiwa bado hujabatizwa katika ubatizo sahihi wa maji tele katika JINA LA YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako,(kulingana na matendo 2:38,8:16, 10:48 na 19:5 na Mathayo 28:19) fanya bidii ufanye hivyo, naye Mungu aliyemwaminifu atakugawia kipawa cha Roho Mtakatifu. Ili uwe na uhakika wa kuzaliwa mara ya pili.

Ubarikiwe sana.

Tafadhali wape ujumbe huu na wengine.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

JINSI ITAKAVYOKUWA KATIKA SIKU ILE

LENGO LA SHETANI KWA WATOTO WA KIZAZI HIKI

BWANA YESU ALIMAANISHA NINI PALE ALIPOSEMA “MKONO WAKO UKIKUKOSESHA UKATE?

TOFAUTI KATIKA YA ZAKA NA SADAKA NI IPI?


Rudi Nyumbani

Print this post

BADO KITAMBO KIDOGO HAMNIONI

Bwana Yesu alisema, ilimpasa yeye aondoke ili Roho Mtakatifu aje, hata hivyo Roho Mtakatifu sio kitu kingine tofauti na Yesu, bali ni yeye yeye Bwana Yesu katika mfumo wa Roho,

Kwamfano Mchawi anapotaka kukiloga kikundi cha watu Fulani au kijiji, hawezi kufanya uchawi wake kwa namna ya kimwili bali atakiendea kijiji kile au watu wale kwa namna ya Roho isiyoweza kuonekana kwa macho na kuleta madhara makubwa sana katika kile kijiji. Atakuwa ana uwezo wa kudhuru watu hata 100 kwa mda mfupi kuliko kuwa katika mwili. Sasa ni Yule Yule mchawi ila anatenda kazi katika namna ya roho.

Ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ili kwamba ajipatie matokeo makubwa zaidi ilimpasa aondoke katika namna ya kimwili, ili aje tena katika namna ya roho ili alete matokeo makubwa zaidi katika ulimwengu.

Na ndio maana Bwana Yesu kabla ya kuondoka aliwaambia wanafunzi wake, kwamba bado kitambo hawamwoni na tena bado kidogo watamwona tena, akimaanisha kuwa muda mfupi baadaye atakwenda kusulibiwa na atachukuliwa juu mbinguni nao hawatamwona tena, lakini baada ya kusulibiwa na kupaa muda mfupi baadaye watamwona tena (atakuja kwao) kwa namna ya Roho katika siku ile ya Pentekoste..

Tunasoma ;

Yohana 16:12 “Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa.

13 Lakini yeye atakapokuja, HUYO ROHO WA KWELI, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.

15 Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.

16 BADO KITAMBO KIDOGO NANYI HAMNIONI; NA TENA BADO KITAMBO KIDOGO NANYI MTANIONA.

17 Basi baadhi ya wanafunzi wake wakasemezana, Neno gani hilo asemalo, BADO KITAMBO KIDOGO NANYI HAMNIONI, NA TENA BADO KITAMBO KIDOGO NANYI MTANIONA? NA HILO, KWA SABABU NAENDA ZANGU KWA BABA?

18 Basi walisema, Neno gani hilo asemalo; hilo, Bado kitambo kidogo? Hatujui asemalo.

19 Yesu alifahamu ya kwamba wanataka kumwuliza, akawaambia, Ndilo hilo mnaloulizana, ya kuwa nalisema, BADO KITAMBO KIDOGO NANYI HAMNIONI, NA TENA BADO KITAMBO KIDOGO NANYI MTANIONA?”

Kwahiyo ili Bwana Yesu aweze kuhudumia mamilioni ya watu waliopo duniani asingeweza kubaki katika ile hali ya mwili, ilimpasa aje kwa namna ya Roho, ili aweze kuwaganga moyo wengi waliovunjika moyo, ili aweze kuwafundisha watu wengi wa ulimwengu mzima, ili aweze kuwatembelea majumbani mwao, mtu mmoja mmoja, lakini katika ile hali ya mwili aliyokuwepo ingekuwa ni ngumu, ingechukua mamilioni ya miaka kutimiza kusudi lake, hivyo ilimpasa abadili njia ya kuwafikia wanadamu, kwa sababu hiyo basi akawaambia wanafunzi wake bado kitambo kidogo nanyi hamnioni na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona, na kweli siku ile Bwana Yesu alipoondoka wanafunzi wake walihuzunika sana, wakajihisi kuwa mayatima, wakajifungia ndani kwa hofu ya wayahudi, mioyo yao ilikuwa mizito kwasababu Bwana ameondoka, lakini tunasoma katika siku ile ya Pentekoste Roho Mtakatifu alipowashukia mioyo yao ilihuishwa tena, wakapata ujasiri wa hali ya juu, wakamwona Kristo tena, wakamuhisi wapo karibu naye kuliko hata hapo kabla walipokuwa naye. Walipokea nguvu ya ajabu, Huyo alikuwa ni Yule Yule Kristo katika Roho. Na baada ya hapo ndio tunaona injili ikaenda duniani kote.

Injili ilianza kuenea kwa kasi duniani kote nguvu sana, kwasababu Kristo hatendi kazi tena katika mwili mmoja bali katika Roho, hivyo matokeo yake yanakuwa ni makubwa zaidi, ni Kristo Yule Yule hajabadilika lakini sasa hatumii tena njia ile aliyokuwa anaitumia, bali anatumia njia iliyobora zaidi kuufikishia ulimwengu wokovu.

Ni sawa na mtu aliyekuwa anatangaza biashara yake kwa mabango barabarani kwenye hari za jua kali, lakini baadaye akabadilisha mbinu na kuanza kutumia mitandao kutangaza matangazo yake ili kupata matokeo makubwa zaidi, sasa huyo mtu hajabadilika ni yeye Yule Yule isipokuwa tu amebadilisha njia ya kuwafikia watu. Badala ya yeye kwenda kugonga nyumba moja moja kutangaza biashara yake, ambapo pengine kwa siku angewafikia watu 100 tu! sasa anatumia mitandao ya kijamii ambapo kwa siku anaweza kuwafikia hata watu laki moja na zaidi, pasipo hata yeye kuwepo maeneo yao. Kwa kupitia mitandao anakuwa anatimiza kusudi lile lile kama tu angetumia miguu yake..tena zaidi ya yote anapata matokeo bora zaidi.

Kadhalika Bwana Yesu alisema.. “Walipo wawili au watatu wamekusanyika kwa jina langu, MIMI NIPO PAPO HAPO KATIKATI YAO”

Unaona hapo? Hayupo kwa namna ya kimwili lakini yupo kwa namna ya Roho, kwahiyo kama wakikusanyika wawili au watatu kwa jina lake, hasemi uongo ni kweli yupo katakati yao, sawa tu na kama angekuwepo kwa namna ya kimwili.

Kaka/ Dada unayesoma ujumbe huu, ni muhimu kujua kwamba Kristo yupo leo anatembea ulimwenguni, anafanya kazi zile zile, isipokuwa tu haonekani kwa macho, ni Kristo Yule Yule aliyekuwa anatembea na wakina Petro, ni Yule Yule aliyekuwa anagonga kwenye jumba za watu, na kwenye miji ili aingie aihubiri injili. Na wale waliomkubali aliwapa uzima wa Milele na wale waliomkataa aliwaacha na kwenda kwa wengine, Na leo ndio Yule Yule anagonga katika mioyo ya watu kwa namna ya Roho akitaka aingie ayabadilishe maisha ya watu na kuwaletea wokovu. Aliwaambia wanafunzi wake maneno haya wakati anawatuma kwenda kuhubiri injili…

Luka 10:10 “Na mji wo wote mtakaouingia, NAO HAWAWAKARIBISHI, TOKENI HUMO, nanyi mkipita katika njia zake semeni,

11 HATA MAVUMBI YA MJI WENU YALIYOGANDAMANA NA MIGUU YETU TUNAYAKUNG’UTA JUU YENU. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia.

12 Nawaambia ya kwamba SIKU ILE ITAKUWA RAHISI ZAIDI SODOMA KUISTAHIMILI ADHABU YAKE KULIKO MJI HUO”.

Umeona ndugu?, hakuna nafasi ya pili kama ukimkataa Kristo kwa makusudi sasa, unapohubiriwa injili yake kwa Roho wake, anaondoka na kwenda kwa mwingine? Na kwako inabakia kuwa hukumu. Biblia inasema waasherati wote, wasengenyaji, walafi, walawiti, walevi,wachafu,watukanaji, wala rushwa, waabudu, sanamu sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti, HAIDANGANYI!! Ni kweli itakuwa hivyo, mtu yeyote anayekuambia kwamba walevi wataokolewa anakudanganya, yeyote anayekuambia kwamba wanaopaka wanja na lipstiki na kuvaa wigi na suruali na herein wataokolewa kwamba Mungu haangalii Roho anaangalia mwili, nataka nikuambia jambo hili moja Roho Mtakatifu anasema sehemu yao itakuwa ni KATIKA LILE ZIWA LA MOTO!!. Anayekuambia kwamba kuwa kuishi na mwanamume au mwanamke ambaye hamjafunga ndoa au ambaye ameachana na mke/mume wake sio dhambi, anakudanganya Yesu Kristo anazungumza na wewe leo kwa namna ya Roho, kwamba “AMWACHAYE MKE WAKE NA KUOA MWINGINE AZINI, NAYE ALIYEMUOA YULE ALIYEACHWA AZINI” Mtii Yesu Kristo leo na maneno yake, Usiusikilize uongo wa shetani ambao baadaye utakufanya ujute milele.

Bwana alisema..UFUNUO 3: 20 “TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI, NABISHA; MTU AKIISIKIA SAUTI YANGU, NA KUUFUNGUA MLANGO, NITAINGIA KWAKE, NAMI NITAKULA PAMOJA NAYE, NA YEYE PAMOJA NAME”.

Tubu leo kama hujafanya hivyo, mpe Bwana maisha yako ayabadilishe, kabla hajaacha kugonga ndani ya moyo wako na kuhamia kwa mwingine, ukishatubu fanya hima ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa kwenye maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo, kwa ajili ya ondoleo la dhambi, uwe na uhakika wa wokovu wako na BWANA mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake, ndipo utakapokuwa na uhakika wa kuzaliwa mara ya pili.

Bwana akubariki.

Print this post

VIUNO VYENU VIWE VIMEFUNGWA NA TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA

Luka 12:35 “VIUNO VYENU na viwe vimefungwa, na TAA ZENU ziwe zinawaka;

36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.

37 Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.

38 Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao.”

Tunaweza kujiuliza ni Kwanini ni VIUNO na ni kwanini ni TAA..Katika mfano huu tunaona kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na watumwa wake wanaomtumikia sikuzote nyumbani kwake, lakini ilitokea siku moja alipokea kadi ya mwaliko wa harusi mahali Fulani. Na kama tunavyofahamu sikuzote harusi nyingi huwa zinafanyika usiku. Na kama ni usiku basi itamgharimu kuchelewa kidogo kurudi nyumbani Kwasababu Harusi itatarajiwa iishe usiku sana. Na yeye akiangalia anao watumwa nyumbani kwake ambao pengine mkataba alioingia nao wa kufanya kazi mwisho unapaswa uwe ni saa moja jioni. Na baada ya hapo watumwa hao wanakuwa huru kwenda kumpumzia au kufanya shughuli zao binafsi.

Lakini hapa limetokea jambo ambalo linamgharimu Bwana wao kuchelewa, hivyo inamlazimu kuwasihi wamsubirie wasilale mpaka atakaporudi kutoka Harusini ili waje kumfungulia pindi tu atakapogonga malango ya nyumba … Unajua Kwa hali ya kawaida, wapo watumwa wengine watasema, huyu bwana amevunja mkataba tulioingia naye hivyo sisi hatutaweza kumngojea mpaka muda huo, kwanza katufanyisha kazi mchana kutwa tena na bado hapa anataka tukeshe mpaka usiku wa manane, atatupa fedha ya ziada? Wengine watasema sisi tutamngojea lisaa limoja au mawili na asipoonekana tutalala.

Lakini wengine wakarimu watasema hapana tusifanye hivyo bwana wetu huwa hana desturi ya kutufanyia hivi sikuzote, imekuwa ni dharura tu,na ni leo tu kesho haitakuwa hivi, hivyo tuvumilie kwa siku hii moja tumngojee bwana wetu asije akalala nje! Kwenye hatari nyingi.

Hivyo ni wazi kuwa wapo watakaokataa na watakaokubali. Lakini habari hiyo inaendelea kutuambia nini?

“37 Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo ATAWAKUTA WANAKESHA. Amin, nawaambieni, ATAJIFUNGA NA KUWAKARIBISHA CHAKULANI, ATAKUJA na KUWAHUDUMIA.”

Unaona hapo mfano huo unaturudisha pia kuitafakari habari ya wana wa Israeli siku ile ambayo Mungu aliona vema kuwatoa utumwani baada ya kukaa miaka 430 katika hali ya mateso, Kwa kuwa hatuna muda wa kuelezea matukio yote lakini tunafahamu siku ile ya mwisho ya wao kukaa katika nchi ya Misri Mungu aliwapa maagizo, na ikumbukwe kuwa hawakutoka nchi ya Misri MCHANA, hapana bali ilikuwa ni USIKU wa manane kwasababu ndio uliokuwa mpango wa Mungu watoke usiku.

Lakini kabla ya kutoka kwao Mungu aliwapa maagizo na maagizo na mojawapo ya maagizo hayo ilikuwa ni KUFUNGWA MKANDA VIUNONI na KUVALIWA kwa VIATU. Tunafahamu mtu akienda kulala ni lazima azilege nguo zake, atoe mikanda kisha azime taa na alale. Lakini kama nguo zako bado zimebanwa na mkanda pamoja na viatu ni wazi kuwa mtu huyo yupo katika mazingira ya kutoka muda wowote.

Lakini wana wa Israeli hawakujua uzito wa wao kuambiwa hivyo, mpaka tunavyosoma pale Farao na wamisri wote wakiwafukuza wenyewe kutoka Misri pamoja na zawadi nyingi usiku ule ule, hapo ndipo walipotambua kuwa kumbe! KUVAA KULE NDIO ILIKUWA NI KUONDOKA! Wengine waliwaza mbona! imekuwa Ghafla ghafla tu, hili jambo si lingesubiria walau asubuhi tu, tuanze kuweka vitu vyetu vizuri, tuwaage majirani zetu, tuwafuate wadeni wetu watulipe kwanza?, tukavune ngano zetu tupate chakula cha kusafiria? Nk. Lakini mbona jambo hili Mungu kaliharakisha mapema hivi?….Tunasoma usiku ule ule safari ilianza (Kutoka 12), lakini jaribu kifikiria kama mwisraeli mmoja asingetiii yale maagizo na kwenda kuamua kujifungia ndani kwake na kuvua nguo zake na kulala, unadhani atakapoamka ni jambo gani atakutana nalo?, WENZAKE HAWAPO!!. Na ndivyo itakavyokuwa katika siku hizi za mwisho Bwana alisema.

“VIUNO VYENU na viwe vimefungwa, na TAA ZENU ziwe zinawaka;

36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka ARUSINI, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.

37 Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.

38 Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao.”

Unaona hapo, laiti kama hawa watumwa wote wangekuwa tayari kumngojea bwana wao mpaka atakaporudi kutoka arusini ili wamfungulie, kwa fadhila Bwana wao asingewaambia laleni mpumzike, hapana badala yake kwa kuwa VIUNO VYAO VIMESHAFUNGWA ikiashiria utayari wao wa kuondoka.

Moja kwa moja yeye mwenyewe atawakaribisha katika karamu yake aliyokwenda kuiandaa baada ya kutoka arusini, na kuwahudumia kwa kila kitu ambacho wangekihitaji, usiku ule ule wangeondoka pale nyumbani na kwenda mahali pengine kabisa kula raha ya daima. Kadhalika wao nao wangestaajabia kwanini Bwana wetu asingesubiri walau asubuhi ifike tuoge, tuvae vizuri tuwaambie na wenzetu kisha ndio tuende kwa pamoja huko kwenye hiyo karamu aliyotuandalia…kwanini kachukua maamuzi ya haraka haraka usiku huu?.. Lakini hivyo ndivyo ilivyompendeza Bwana wao.

Ndugu siku ya kuondoka kwa wana wa Mungu hapa duniani hakutakuwa kwa kukutazamia kama wengi wanavyodhani. Utakuwa ni wakati usiofaa kwa wengi hata katikati ya watumishi wake waaminifu.

Bwana alipotupa maagizo kwamba TUKESHE, TAA ZETU ZIWE ZINAWAKA na VIUNO VYETU VIWE VIMEFUNGWA. Alijua kabisa itakuwa ni wakati wa usiku wa manane ndio muda utakuwa wa kurudi kwake . Na sasa ndio tupo hicho kipindi ambapo dunia ipo katika kilele cha giza kuu kuliko hata vizazi vyote vya nyuma vilivyotutangulia. Maovu yameongezeka kuliko hata kipindi cha Sodoma, ushoga unahalalishwa hata mahali patakatifu. Hizo ndio dalili madhubuti kuonyesha kwamba tupo katika giza nene la usiku wa manane.

Lakini kumbuka pia Bwana wetu yupo karibu kurudi kutoka katika arusi ya faragha aliyoalikwa na BABA yake mbinguni. Na watakaokwenda naye ni wale tu ambao TAA zao zinawaka na VIUNO vyao vimefungwa, yaani wale ambao kila siku macho yao yapo mbinguni. Biblia inasema “jifungeni KWELI kiunoni” na kweli ni NENO LA MUNGU (Waefeso 6:14). Hivyo wale wote wataokadumu katika msingi ya Neno la Mungu wakielekeza macho yao mbinguni bila kujali mambo yanayopita ya ulimwengu, kadhalika pia wale ambao TAA zao zinawaka, kumbuka ili taa iwake inahitaji mafuta, na mafuta ni ROHO MTAKATIFU, Hivyo wale ambao waliotajazwa Roho na kila wakati wanaufanya uteule wao na wito wao imara bila kumzimisha Roho wa Mungu ndani yao, hao ndio siku ile BWANA atakapogonga watamsikia na kuingia kwenye Karamu aliyoiandaa yeye mwenyewe. Na pia ili taa iwake lazima kuwe na giza, taa haiwezi kuwashwa wakati wa mchana, hivyo wakati huu ambapo dunia imejaa matendo ya giza, ndio wakati wa kuzifanya taa zetu ziwake.

Lakini wengine wote waliosalia, wapendao matendo ya giza hawatajua lolote, itakapopambazuka tu ndipo watakapogundua kuwa wenzao hawapo, na ndiko kutakako kuwa na kilio na kusaga meno. Katika dhiki kuu, na katika siku ile ya BWANA.

Ni kwanini leo maisha yako yasiuhakisi wokovu?, Ni kwanini bado upo usingizini?. Na uzingizi hauna nguvu mchana,JE! Unao huhakika hata Bwana akija leo, utakuwa mwepesi kumsikia akigonga mlango wa moyo wako?, Mambo ya ulimwengu huu yanakusonga?, Unawatazama wanadamu? Hao watakusaidia nini endapo umesikia unyakuo umekupita, ? na wewe umebaki? ujana wako, mali zako na nguvu zako zitakuwa msaada gani kwako katika siku hiyo?

BWANA ANASEMA..

Waefeso 5:14 “……AMKA, WEWE USINZIAYE, UFUFUKE KATIKA WAFU, Na Kristo atakuangaza.

15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;

16 MKIUKOMBOA WAKATI KWA MAANA ZAMANI HIZI NI ZA UOVU.”

Kama haujatubu ndugu fanya hivyo sasa, huu si wakati wa kuishi maisha ya kubahatisha, UKOMBOE WAKATI! nenda ukabatizwe katika ubatizo ulio sahihi wa maji mengi katika jina la YESU KRISTO haraka baada ya kutubu dhambi zako ili upate ondoleo la dhambi (Matendo 2:38) …Kumbuka kuzaliwa mara ya pili ni kutubu, kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho, na kuishi maisha matakatifu katika Kristo, na si vinginevyo. Ikiwa bado hujapitia hatua hizo zote hapo bado hujazaliwa mara ya pili. Na Bwana alisema mtu wa namna hiyo hawezi kuuona ufalme wa mbinguni (Yohana 3:5).

Fanya bidii utubu na Bwana atakuangazia neema yake.

Ubarikiwe sana.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine, Na Bwana atakubariki

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

KAMA MWIZI USIKU WA MANANE:

BEI YA UFALME WA MBINGUNI:

JE! UMECHAGULIWA TANGU ASILI?

ZILE TUNU (DHAHABU, UVUMBA NA MANEMANE) MAMAJUSI WALIZOZITOA KWA BWANA (MATHAYO 2) . ZILIWAKILISHA NINI?

SAYUNI NI NINI?


Rudi Nyumbani

Print this post