Sanduku la Agano lilikuwa linawakilisha nini katika Agano jipya?

Sanduku la Agano lilikuwa linawakilisha nini katika Agano jipya?

JIBU: Shalom!, Kwa hali ya kawaida tunafahamu sanduku kazi yake huwa ni kuhifadhi vitu Fulani, inaweza ikawa ni fedha,vito,nguo, hazina, miili n.k. na ndio maana tukirudi kwenye biblia tunaona biblia inataja masanduku ya aina mbali mbali, kwa mfano pale Yusufu alipokufa biblia inatuambia mwili wake waliuweka kwenye sanduku (Mwanzo 50:26), hivyo kuna masanduku ya miili. Hali Kadhalika kulikuwa na masanduku ya kuhifadhia sadaka, ambayo yaliitwa masanduku ya sadaka au masanduku ya hazina, mahususi kwa kazi ya sadaka tu!. (Marko 12:41).

Vivyo hivyo na masanduku mengine yalikuwepo, ya fedha, ya vito n.k..   Sasa tukirudi kwenye sanduku la agano lililokuwepo Israeli katika agano la kale, mpaka limeitwa sanduku la agano ni wazi kuwa ndani yake lilikuwa limehifadhi maagano Fulani. Na kama ukisoma biblia utaona ndani ya sanduku lile ambalo Musa alipewa maagizo alichonge lilikuwa na vitu vitatu: kimoja ni zile mbao zenye zile amri 10 Mungu alizompa Musa akiwa mlimani, zilizoandikwa kwa kiganja cha Mungu mwenyewe, cha pili ni ile mana, na cha tatu ni ile fimbo ya haruni iliyochipuka.

  Na kila mojawapo hapo ilikuwa na maana yake. Musa aliagizwa avitunze vitu hivyo vitatu kwenye sanduku lile liwe kama kumbukumbuku la agano Mungu alilofanya na wana wa Israeli tangu walipotoka Misri mpaka walipoingia katika nchi ya ahadi. Vitu hivyo aliagizwa vikae kwenye sanduku kwa vizazi vyote kama ukumbusho.  

Waebrania 9:2 “Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate ya Wonyesho; ndipo palipoitwa, Patakatifu.

3 Na nyuma ya pazia la pili, ile hema iitwayo Patakatifu pa patakatifu,

4 yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano;

5 na juu yake makerubi ya utukufu, yakikitia kivuli kiti cha rehema; basi hatuna nafasi sasa ya kueleza habari za vitu hivi kimoja kimoja”.

  Fimbo ile ikimaanisha ukombozi wao waliopewa na Mungu kwa njia ya mti ule, Mungu alitumia kipande kile cha mti ule kumwadhibu Farao mpaka kuwaachilia watoke katika utumwa ule mgumu ambao kwa namna ya kawaida ilikuwa haiwezekani wao kutoka Kwahiyo fimbo ya Haruni ndio ile ile fimbo ya Musa).

 Kadhalika amri zile kumi zikufunua sheria zote na maagizo yote Mungu aliowapa wana wa Israeli walipokuwa jangwani kwamba waziendee hizo siku zote za maisha yao.

Na mana, inafunua chakula cha kiroho Mungu alichokuwa anawapa kule jangwani kilichoshuka kutoka mbinguni, ambacho kiliwapa nguvu ya kusonga mbele katika hali zozote walizokuwa wanapitia.   Sasa tukirudi katika agano jipya kama swali lilivyoulizwa Sanduku la agano linawakilisha nini katika agano jipya?.

Jibu ni kuwa mambo yote yaliyotendeka katika mwili kwenye agano la kale yalikuwa yanafunua mambo yanayoendelea katika roho kwenye agano jipya sasa. Hivyo sisi sote tunaoishi katika agano jipya, Na sisi pia Mungu aliingia agano na sisi na kutugawia FIMBO, AMRI, na MANA. Na hizo zote akazihifadhi katika sanduku lake moja litembee nasi. Na sanduku hili si lingine zaidi ya BIBLIA neno la Mungu.

Fimbo yetu ni msalaba ule ambao kwa huo Mungu aliutumia kumpiga shetani siku ile pale Golgotha, siku ile Bwana aliposema IMEKWISHA! Baada ya damu yake kumwagika Basi siku hiyo ulikuwa mwisho wa kila kitu kwa shetani, Bwana aliyotuweka huru mbali na utumwa na vifungo vya shetani (Farao).  

Kadhalika amri zile ni maagizo yote tuyasomayo katika Biblia Bwana aliyotupa,kila siku tuyafuate na Mana na ufunuo wa Roho ambao huo unashuka moja kwa moja kutoka mbinguni kwa Baba kutupa sisi nguvu ya kudumu katika IMANI.   Hivyo vitu hivyo vitatu vinakamilisha agano jipya na vyote hivyo vipo katika sanduku moja nalo ndio BIBLIA TAKATIFU.

 Na kama vile mahali popote wana wa Israeli walipoenda sanduku la agano lilifuatana nao kadhalika mtu yeyote aliye mkristo na anakaa mbali na biblia maneno ya Mungu ni wazi kabisa bado hajaingia kwenye hili agano jipya la damu ya Yesu Kristo.  

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO

MUNGU KUSEMA NA WEWE PEKEE, HAITOSHI KUKUPA USHINDI.

CHUKIZO LA UHARIBIFU.

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA TATU WA YOHANA.

KWANINI SAMWELI ALIRUHUSUIWA KUHUDUMU HEKALUNI KAMA VILE WALAWI WAKATI YEYE NI MU-EFRAIMU?

NINI MAANA YA HUU MSTARI “NIMEVIPIGA VITA VILIVYO VIZURI, MWENDO NIMEUMALIZA, IMANI NIMEILINDA;”?


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
6 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Joash Mbwelwa
Joash Mbwelwa
1 year ago

Mungu azidi kuwa bariki sana usiku na mchana ,kazi yenu ni njema nami nmebarikiwa mno kwayo, May Almighty God bless you forever and ever for this glorious spiritual service,I have blessed alot through this glorious work🙏🙏🙏🛑🛑

Zabron j mika
Zabron j mika
1 year ago

Asanten na mungu awabariki

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Asanten kwa mafundisho mazur!

KIZA RUHAMBIRIZA
KIZA RUHAMBIRIZA
2 years ago

Nafurai sana kuwapata kwa kunisaidia mafundisho mazuri

Amos Makoba
Amos Makoba
2 years ago

Amen.. 🙌🙏
Somo limenipa ufunuo wa jambo ambalo sikulijua hapo mwazo…

Anonymous
Anonymous
2 years ago
Reply to  Amos Makoba

MUNGU azidi kukuinua kwa somo zuri mtumishi