Category Archive waongofu wapya

FAHAMU VIASHIRIA VYA MTU ALIYESAMEHEWA DHAMBI ZAKE.

Si kila mtu anayesema “amemwamini” Yesu ni kweli, ameokoka, au amepokea msamaha wa dhambi zake. Ukweli ni kwamba kuupokea msamaha wa dhambi kwa kuiamini kazi aliyoimaliza Yesu Kristo pale msalabani ya ukombozi wa wanadamu si kugumu, Lakini haiji kwa kusema “naamini tu” halafu basi ndio uwe tayari umetiwa muhuri na Mungu kwamba ni wake milele.

Imani ya namna hiyo inatiwa imani ya” bure” (1Wakorintho 15:2).

Na sehemu nyingine inajulikana kama  “imani ya wote” ambayo hata mashetani wanayo. Wanamwamini Yesu kuwa ni mwokozi, lakini pia wanaiamini vizuri sana kazi ya msalaba (Yakobo 2:19). Lakini je! Wamesamehewa dhambi zao?

Zipo injili zinazowafundisha watu, “kuamini tu” au “kukubali tu msamaha” inatosha. Hakuna la ziada baada ya hapo. Ndugu hizo sio sifa za mwaminio yoyote.

Neno “kuamini” kwa kigiriki ni PISTIS, lenye maana ya sio tu kuwa na ujasiri na Mungu wako kwa kile anachokupa au kukuelekeza,lakini pia kuwa ‘mwaminifu”.

Maana yake ni kuwa ili tuseme tumeamini ni lazima pia tuwe waaminifu kwa Yule tuliyemwamini.

Sasa mtu yeyote aliyemwamini Kristo. viashiria hivi vitatu(3) utaviona ndani yake

  1. Atakuwa ni kondoo

Yohana 10:2  Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. 3  Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje. 4  Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. 5  Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni…

27  Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. 28  Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. 29  Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.

Umeona, ni kondoo tu, ndio hawawezi kupokonywa katika mikono ya mchungaji wake. Lakini mbuzi wanaweza, kwasababu hawategemei sana sauti ya mchungaji, wanaweza kujichunga wenyewe. Ukiona mtu anasema ameokoka, halafu, maisha yake ni kama ya mbuzi, ujue huyo si wa Kristo. Haisikii sauti ya Kristo ikimwelekeza aache maisha ya kiulimwengu, ajitofautishe na watu wa kidunia, . Ujue huyo bado hajapokea kweli msamaha wa dhambi, kwasababu hajaamini. Anapaswa ashuhudiwe mpaka aamini. Na aseme kuanzia leo, Kristo ndio kiongozi wa maisha yangu na sio dunia tena. Akubali TOBA ya kweli.

2. Atakuwa Ni kiumbe kipya.

Yesu alisema..

Yohana 1:12  Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.

13  waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu

Wenye sifa ya kwamba wamemwamini Yesu ni lazima pia wawe wamegeuzwa kuwa watoto wa Mungu, yaani wamezaliwa mara ya pili kwa mbegu isiyo ya kibinadamu, bali ya Mungu mwenyewe.

Na kama tunavyofahamu mtoto hubeba tabia za Baba. Vivyo hivyo mwaminio ni lazima moyoni mwake kuwake, tamaa za Baba yake. Maandiko yanasema Baba ni Mtakatifu, vivyo hivyo tamaa ya mwaminio huyo mpya itakuwa ni kupenda utakatifu, na kuutafuta huo kwa bidii.

Haiwezekani mtu aliyemwamini Yesu, awe na raha tena katika maisha ya kidunia ya dhambi. Au asipige hatua yoyote ya kuutafuta ukamilifu. Halafu tuseme ni mwaminio si kweli.

1Yohana 3:9  Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu

3) Atakuwa ni mwanafunzi

Mwaminio mpya amefananishwa na mwanafunzi, na mwanafunzi sikuzote huwa yupo tayari kujifunza, na kukua kiufahamu.

Matendo 2:41  Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 42  Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.

Hivyo mtu yoyote anayesema amemwamini Yesu, na hapendi fundisho, hapendi kuchungwa, hapendi kufuatiliwa maendeleo yake ya kiroho, anapinga ubatizo, na wakati mwingine kufanya ushirika, huyo mtu bado hajaamini.

Lakini akiwa na sifa zote hizo tatu, ni uthibitisho kuwa amemwamini Yesu, na hivyo kaupokea pia msamaha wa dhambi. Mtu wa namna hiyo wokovu kwake ni uhakika. Kwasababu Yesu ameumbika ndani yake. Kazi ya Mungu kamilifu imetimilika ndani ya mwanadamu.

Je! Na wewe Umepokea ondoleo la dhambi zako? Je! Ni mwanafunzi, ni kondoo, ni mwana wa Mungu?. Kama bado basi fahamu unamwihitaji Kristo, fungua moyo wako mkaribishe ndani yako akuokoe. Sasa, Maanisha tu tangu sasa kuwa na badiliko na yeye mwenyewe atakuokoa.

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

JE! UNAMPENDA BWANA?

NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE

LISHA KONDOO WANGU, LISHA WANA-KONDOO WANGU.

Rudi nyumbani

Print this post

UJAZO WA BIBLIA KATIKA MGAWANYO WAKE.

> Kuna vitabu vingapi katika Agano Jipya na Agano la Kale?,

> Kuna sura/milango mingapi katika kila mgawanyo?

> Na watu gani waliotajwa sana katika biblia zaidi ya wengine wote?

KUJUA HAYO YOTE, TAZAMA MAJEDWALI YAFUATAYO 

(Slide kushoto kusoma zaidi taarifa katika jedwali).

N/AMGAWANYOIDADI YA VITABUIDADI YA SURA (MILANGO)IDADI YA MISTARI
1.AGANO LA KALE3926023,145
2.AGANO JIPYA279297,957
JUMLA661,18931,102

JINANAFASI (KATIKA BIBLIA)IDADI ALIZOTAJWA (Mara ngapi)NAFASI
YOABUJemedari wa Mfalme Daudi12916
ISAKAMwana wa Ibrahimu12915
SAMWELINabii (Mwana wa Elkana)14214
YEREMIANabii (Mwana wa Hilkia)14513
PETROMtume (Mwana wa Yona)19312
YOSHUAJemedari wa Israeli21911
PAULOMtume (Mwenyeji wa Tarso)22810
YUSUFUMwana wa Yakobo2469
SULEMANIMfalme (Mwana wa Daudi)2728
ABRAHAMUBaba wa Imani2947
HARUNIKuhani Mkuu3426
SAULIMfalme (Mwana wa Kishi)3625
YAKOBOIsraeli (Mwana wa Isaka)3634
MUSANabii (Mwana wa Amramu)8033
DAUDIMfalme (Mwana wa Yese)9712
YESU KRISTOMFALME wa Wafalme, Bwana wa mabwana, Mwana wa Mungu, Mwokozi, Simba wa kabila Yuda, Mesia, Mwokozi na Mchungaji Mkuu.1,2811

Kwanini YESU KRISTO ndiye anayeonekana kutajwa sana katika Biblia??.. Ni kwasababu yeye ndiye kitovu cha UZIMA, na Biblia yote inamhusu yeye, na kutuelekeza kwake.

YESU KRISTO, ndiye Njia, KWELI na UZIMA.. Mtu hawezi kumwona MUNGU nje ya YESU KRISTO (Yohana 1:18 na 14:6)

Tafadhali shea na wengine;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MAJINA YA MITUME WA BWANA YESU

Mgawanyo wa Vitabu vya Biblia

TAKWIMU ZA KIBIBLIA

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 2

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1

Rudi nyumbani

Print this post

Mistari ya biblia kuhusu shukrani.

Ifutayo ni mistari kadhaa ya biblia ihusuyo shukrani/ kushukuru.


Zaburi 9:1 “Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu”.

Zaburi 18:49 “Basi, Bwana, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako”

2Samweli 22:50 “Basi, Bwana, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako”.

Zaburi 30:12 “Ili utukufu wangu ukusifu, Wala usinyamaze. Ee Bwana, Mungu wangu, Nitakushukuru milele”

Zaburi 35:18 “Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa; Nitakusifu kati ya watu wengi”

Zaburi 52: 9 “Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako”

Zaburi 118: 21 “Nitakushukuru kwa maana umenijibu, Nawe umekuwa wokovu wangu”.

Zaburi 71:22 “Nami nitakushukuru kwa kinanda, Na kweli yako, Ee Mungu wangu. Nitakuimbia Wewe kwa kinubi, Ee Mtakatifu wa Israeli”.

Zaburi 119: 7 “Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo, Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako”

Zaburi 106:1 “Haleluya. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele”.

Zaburi 28:7 “Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru”.

2Wakorintho 2:14  “Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu”.

Wakolosai 4:2 “Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani”.

Zaburi 100:4 “Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake”

Zaburi 107:7 “Akawaongoza kwa njia ya kunyoka, Wapate kwenda mpaka mji wa kukaa

8 Na wamshukuru Bwana, kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu”.

1Wakorintho 15:57  “Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo”.

Zaburi 95: 2 “Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi”.

Wakolosai 3:15  “Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani”.

Ufunuo 11:17 “wakisema, Tunakushukuru wewe, Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa sababu umeutwaa uweza wako ulio mkuu, na kumiliki”

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU WATOTO.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU UPENDO.

NENO LA FARAJA KWA WAFIWA.

MISTARI YA BIBLIA YA FARAJA.

Rudi nyumbani

Print this post

Mistari ya biblia kuhusu maombi.

Ifuatayo ni mistari michache ya biblia inayohusu maombi.


Zekaria 10:1 “Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika, naam, Bwana afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni.”

Mathayo 7:7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;

8  kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.”

Marko 13:33 “Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo”

Luka 22:40 “ Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni.”

Yohana 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”

Yohana 16:24 “Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu”

Wafilipi 4:6 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu”.

Marko 11:24  “Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu”.

Wakolosai 4:2 “Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani”

Waefeso 6:18  “kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote”

1Wathesalonike 5:17 “ombeni bila kukoma;”

1Yohana 5:14  “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia”.

1Timotheo 2:1 “Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote”

Yakobo 5:16  “Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii”

Kwa mwongozo wa maombi ya kujikuza kiroho  fungua hapa >> MWONGOZO WA MAOMBI YA KUJIKUZA KIROHO.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho,

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU BARAKA

MISTARI YA BIBLIA YA FARAJA.

IFAHAMU FAIDA YA KUMKIRI KRISTO UKIWA HAPA DUNIANI.

Rudi nyumbani

Print this post

NJIA/BARABARA YA WOKOVU NDANI YA KITABU CHA WARUMI.

“Romans road to salvation”

Njia ya wokovu ndani ya kitabu Cha Warumi ni Nini? 

Ni mpango wa wokovu wa mwanadamu, ambao umeainishwa vyema kutoka katika kitabu Cha Warumi.

Kitabu hichi kinaeleza jinsi mtu anavyoweza kuupokea wokovu kutoka Kwa Mungu.

Hivyo ikiwa wewe bado hujaufahamu mpango wa Mungu kwako, wa namna ya kuupokea wokovu basi kitabu hichi kimeanisha vifungu ambavyo vinakuonesha ni jinsi gani utaweza kuupokea.

Lakini pia ikiwa wewe hujui ni wapi pa kuanzia unapokwenda kuwashuhudia watu habari za wokovu, basi kitabu hichi kinakupa mwongozo wa namna ya kuwahubiria wengine habari njema. Na vifungu muhimu vya kusimamia..

Hivi ni vifungu “mama”

Cha kwanza: Warumi 3:23

Warumi 3:23

[23]kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;

Tuendapo Kwa Mungu, lazima tujue hakuna mwenye haki hata mmoja sote Tumepungukiwa na utukufu wa Mungu. Tumetenda dhambi, Vilevile ikiwa wewe ni mhubiri/mshuhudiaji, huna budi kumuhubiria mtu jambo hilo, kwamba hakujawahi kutokea mwema hapa duniani. Hivyo wote tunauhitaji mpango wa Mungu wa wokovu katika maisha yetu.

Kifungu Cha pili: Warumi 6:23

[23]Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Hapa, Mungu anatuonesha, matokeo ya kudumu katika dhambi zetu, ambazo wote tulikuwa nazo, kuwa ikiwa tutaendelea kubaki katika Hali hiyo hiyo basi tutakutana na mauti ya milele, lakini tukipokea zawadi ya Mungu basi tutapata uzima wa milele.

Kifungu Cha Tatu:  Warumi 5:8

[8]Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.

Kwamba sasa hiyo zawadi ya Mungu ambayo itapelekea uzima wa milele ni Yesu Kristo, yeye ndiye aliyetolewa na Mungu kuzichukua dhambi zetu zote, kwa kifo cha pale msalabani. Pale tuliposhindwa sisi wenyewe basi Yesu alikuja kutusaidia kuchukua makosa yetu.

Kifungu Cha nne: Warumi 10:9-10.

Hiki sasa kinaeleza Namna ya kuupokea wokovu;

Warumi 10:9-10

[9]Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.

[10]Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

Kwa kuamini kwetu kuwa Yesu Yu hai, na kwamba anakomboa wanadamu, na vilevile kumkiri Kwa kinywa kuwa ndiye Bwana na mwokozi wetu. Basi tunaupokea msamaha huo wa dhambi Bure, bila gharama yoyote. Na deni letu la dhambi linakuwa limefutwa tangu huo wakati

Hivyo ni sharti ujue kuwa msamaha wa dhambi hauji Kwa matendo Yako mema, Bali unakuja Kwa kuikubali kazi ya Yesu msalabani iliyofanyika Kwa ajili ya ukombozi wako.

Halikadhalika Wewe kama mshuhudiaji vifungu hivi viwepo kichwani mwako.

Kifungu Cha tano cha mwisho: Warumi 5:1

[1]Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,

Maana yake ni kuwa baada ya mtu kumkiri Kristo, na kumkubali kama Bwana na mwokozi wake. Basi anapaswa awe na AMANI na Mungu kwasababu hakuna mashtaka yoyote ya adhabu juu yako. Hakuna hukumu yoyote ya mauti ipo juu yake.

Huo ndipo mpango wa awali wa wokovu wa Mungu Kwa mwanadamu. Ambapo tunapaswa kufahamu kama ulivyoanishwa katika  kitabu hichi Cha Warumi.

Kisha baada ya hapo tunawafundisha watu kuitimiza haki yote au kusudi lote la Mungu juu yetu, Ikiwemo ubatizo wa maji, na ule wa Roho Mtakatifu.

Ikiwa bado hujaokoka, na utapenda kuupokea msamaha wa Yesu Bure maishani mwako, basi Unaweza kuwasiliana na sisi Kwa namba uzionazo chini ya chapisho hili kwa ajili ya mwongozo huo Bure. Vilevile na Ule wa ubatizo.

Bwana akubariki.

Shalom

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

Je! sheria ilikuwaje dhaifu kwasababu ya mwili? (Warumi 8:3)

TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!

Je Kauli ya Mungu katika Warumi 11:4 na 1Wafalme 19:18 inajichanganya?.

Nini tofauti ya haya maneno. 1) KUOKOKA, 2) WOKOVU, 3) KUONGOKA.?

Je mwanamke Fibi, alikuwa ni askofu wa makanisa, kama mitume?

USIISHIE TU KUPATA HAKI, BALI PATA NA WOKOVU.

Rudi nyumbani

Print this post

MWONGOZO WA MAOMBI YA ASUBUHI.

Watu wengi wanapofikia hatua ya kuomba, wanashindwa kuomba vizuri au  kudumu kwa muda mrefu, sio kwamba hawana nguvu za rohoni, hapana bali wakati mwingine ni kwasababu wanakosa mwongozo wa vitu vya kuombea. Hivyo tumeona tuutoe mwongozo huu mfupi ambao utakusaidia, unapoingia katika maombi yako ya asubuhi. Zingatia: Hii sio kanuni ya daima, Zipo nyakati Roho atakuongoza cha kuombea. Lakini hapa tunakupa mambo muhimu ambayo unapaswa uyajumuishe katika maombi yako ya asubuhi kila siku .

Kiwango cha chini kiwe ni Saa moja (1).

1. SHUKRANI:  Ombi la kwanza liwe ni shukrani, Kumbuka umeianza siku mpya, huna budi kutanguliza shukrani kwa Mungu wako, kwa ajili ya uzima, afya,familia,wokovu, chakula,amani n.k.

Wakolosai 3:15 “…..tena iweni watu wa shukrani”

2. MWONGOZO WA SIKU MPYA: Omba Bwana akutangulie katika siku yako mpya. Ukayatende yale yote aliyokusudia uyatende katika siku hiyo. Usitoke nje ya mpango wake. Ili siku Yako isiwe Bure Rohoni.

Mithali 16:3 “Mkabidhi Bwana kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika”.

3. NENO LA MUNGU : Omba uwezo wa kulikumbuka na kuliishi Neno la Mungu katika siku yote mpya. Neno lake Lisidondoke moyoni mwako, Usisahau agizo lake hata moja.Uishi Kwa hilo

Zaburi 119:16 “Nitajifurahisha sana kwa amri zako, Sitalisahau neno lako”.

4. ULIMI WAKO: Katika siku yenye masumbufu na pilikapilika ya mambo mengi, Ni busara umwambie Bwana aweke mlinzi katika kinywa chako usijikwae kwa maneno mahali popote.

Zaburi 141:3 “Ee Bwana, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu”

5. UTUKUFU WA MUNGU: Mwambie Mungu mambo yote uyafanyao ndani ya siku mpya yawe ni kwa utukufu wake. Na sio wa adui au mwanadamu.

1Wakorintho 10:31  “Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu”

6.WAKATI: Omba Mungu akusaidie kuukomboa wakati wako, siku yako isiwe na mapengo, usipite hivi hivi hujafanya jambo la msingi katika wokovu au maisha yako kwa ujumla.

Waefeso 5:15  “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16  mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu”

7. INJILI YA KRISTO: Mwambie Bwana akupe ujasiri wa kuwashuhudia wengine injili, popote uwapo. Vilevile ombea injili ya Kristo ienee kwa nguvu siku hiyo ulimwenguni kote. Ombea pia watumishi wa Mungu wanaotenda kazi yake, wapewe nguvu ili waitimize huduma hiyo ya Bwana.

Matendo 4:31  “Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri”

8. NDUGU NA FAMILIA: Ipeleke familia yako/ ndugu zako kwa Kristo akutane nao katika siku hiyo/ waokoke/ wadumu katika wokovu. Umepewa ndugu ili usimame Kwa ajili Yao.

Warumi 10:1  “Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe”.

9. JAMII: Utakutana na watu mbalimbali, mazingira mbalimbali, Hivyo huna budi  uyaombee Amani, utulivu n.k. Ili uweze kuishi pia kwa amani, katika utumishi wako Kwa Bwana.

Yeremia 29:7 “Kautakieni amani mji ule, ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, mkauombee kwa Bwana; kwa maana katika amani yake mji huo ninyi mtapata amani”.

10. ADUI: Mwambie Bwana akuepushe na Yule mwovu. Katika siku yako, mwovu asikujaribu katika imani, afya, kazi n.k

Mathayo 6:13  Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]

Ukitumia walau dakika sita (6), kuombea kila kipengele. Utakuwa umekamilisha SAA MOJA (1), La maombi. Na ukijijengea utaratibu wa kufanya hivi kila siku asubuhi, utaona mabadiliko makubwa sana ya maisha yako ya kiroho na kimwili.

WoKovu bila maombi ni sawa na gari zuri lisilo na mafuta. HUFIKI POPOTE.

Bwana akubariki. Nikutakie maombi mema.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

LITURJIA NI NINI? NA JE IPO KIMAANDIKO?

Je ile nyota ya asubuhi inamwakilisha shetani au Bwana Yesu?

Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?(

Sadaka ya Amani ilikuwaje?

KUNA AINA NGAPI  ZA MAOMBI?

IJUE FAIDA YA KUFUNGA PAMOJA NA WANYAMA WAKO.

Rudi nyumbani

Print this post

NIFANYE NINI ILI NISILALE NINAPOSOMA BIBLIA.

Mara nyingi tunapojikuta tumelala tunaposoma biblia, huwa moja kwa moja tunamsingizia shetani. Lakini ukweli ni kwamba shetani anahusika kwa sehemu ndogo, sehemu kubwa ni hali zetu za kimwili ndio zinakuwa adui katika jambo hili. Mazingira ambayo ni mashambulizi kutoka kwa adui mfano wake yanakuwa ni  kama haya; pengine mtu akianza tu kusoma biblia anasikia maumivu makali kwenye kichwa, au mwili, lakini akiacha tu kusoma hali yake inarudia kama kawaida, au anaona giza au vitu kama mianga mianga kwenye macho na hivyo inamfanya asiweze kuisoma biblia, au kila anapotaka kusoma anapoteza hapo hapo kumbukumbu zote kwamba alikuwa anasoma biblia, na hatimaye anajikuta yupo usingizini, au anafanya mambo mengine kabisa, hiyo ndio mfano ya mashambulizi.. Na inahitaji kuombewa, au kushindana na hiyo roho hadi ikutoke.

Lakini ukijiona unaposoma biblia usingizi mzito umekukamata, unasinzia sinzia, unapiga piga miayo, huyo sio adui huo ni mwili wako, usiopenda mambo ya rohoni. Hivyo ni lazima uushinde huo.

Wagalatia 5:17  “Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka”

Hivyo hizi ni njia ambazo zitakusaidia usilale pale unaposoma biblia.

1) Omba kabla ya kusoma biblia

Usipende kufungua biblia kama kitabu cha riwaya, unasoma tu utakavyo. Kumbuka yale ni maneno ya ROHO, na hivyo inahitaji umkaribishe Roho akusaidie. Hivyo  usiwe mvivu wa kuomba, pata dakika, kadhaa za kufanya hivyo. Ni jambo ambalo nimejifunza sana, wakati nasoma biblia bila kuomba, na pale ninapoomba kisha nikaisoma, kuna tofauti kubwa sana ya kiuelewa na kiutulivu. Maombi pia yanasaidia kama kuna mashambulizi yoyote, basi yanatowekea hapo.

2) Pata muda wa kupumzika.

Ikiwa umechoka sana, si lazima usome biblia muda huo huo. Pendelea kuruhusu mwili wako upumzike vizuri, kwamfano umetoka kazini, umeshughulika kutwa nzima, ni rahisi sana kukabwa na usingizi muda huo huo usomapo biblia peke yako. Hivyo tumia busara, wahi kulala, kisha amka usiku. Ukilala hata masaa 3, mwili unapokea taarifa kuwa huyu mtu tayari alishapumzika. Hivyo ukiamka ukajimwagia maji, ukaketi utajiona unafuu mkubwa, na utapata kitu kikubwa kuliko kulizimisha mwili wakati umechoka.

3) Usipende kusomea biblia kitandani:

Tafuta meza ukae, mwili wako uwe kama mtu aliye darasani, sio kama aliye hospitalini mgonjwa unasubiriwa kuhudumiwa. Kaa kwenye meza, kisha ndio usome biblia yako

Luka 12:35  Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka

4) Kuwa na daftari na kalamu.

Kusoma kwa kuandika na kwa sauti, huwa kuna matokeo makubwa kuliko, kutumia tu macho yako. Hivyo andiko vifungu unavyovisoma, na ufunuo unaopata, itakuongezea umakini katika usomaji wako, na hivyo Roho Mtakatifu atapata nafasi ya kukufindisha kwa urahisi zaidi.

5) Soma na wengine.

Ukiona huwezi kujiwekea ustaarabu wa kuzingatia ratiba yako ya usomaji, pendelea kujifunza na wengine. Kaa na familia yako, au ndugu zako, au rafiki yako katika Bwana jiwekeeni ratiba ya usomaji wa biblia pamoja, kisha mnachambua kile mlichojifunza, kwa namna hiyo itakusaidia sana kuielewa ..

Mathayo 18:20  “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao”

 6) Soma kwa vituo.

Kusoma biblia sio mashindano kwamba ni lazima uimalize yote kwa siku moja, soma vifungu kadhaa, kisha tumia muda mwingi, kuvitafakari hivyo vilimaanisha nini. Roho Mtakatifu anapenda kutufundisha taratibu sana, hataki tuvuke madarasa ya juu wakati ya chini bado hatujayamaliza. Hivyo zingatia kusoma kwa muktadha wa kuelemishwa na Roho Mtakatifu, sio kumaliza silabasi. Kusoma vifungu vitano kwa dakika mbili, kisha ukavifakari kwa masaa 2, ni bora kuliko kusoma vifungu elfu kwa saa2, halafu hakuna tafakari yoyote.

7) Mifungo

Mfungo ni jambo zuri ambalo huupa mwili wepesi, kwasababu mwili unapotaabika kwa kunyimwa haja zake kwa kawaida roho yako huwa inakuja juu. Hivyo ukiwa katika kipindi cha mfungo, utaona wepesi Fulani wa kuisoma biblia kwa masafa marefu kidogo, kuliko kipindi kingine. Fungu mara kwa mara, au ukiwa unatamani wiki hiyo kuitumia vizuri usiku katika kusoma Biblia, basi hakikisha wiki hiyo yote unafunga, utajiona mwepesi sana hususani wakati wa usiku unapotulia.

8) Mshirikishe mkufunzi wako

Si kila jambo utaweza kulitatua tu peke yako mengine, utahitaji msaada, hivyo hakikisha maendeleo yako ya kiusomaji, kiongozi wako anayafahamu, hatua zako unamshirikisha mchungaji wako, itakusaidia sana, kupata ushauri au maombi , au ushuhuda kwa yale ambayo pengine usingeyafahamu uwapo peke yako. Na hiyo itakupa hamasa zaidi na shauku ya kusoma.

Bwana akubariki.

Hakikisha unasoma BIBLIA kila siku.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Jinsi ya kuandaa Somo la kufundisha

JINSI YA KUSOMA BIBLIA.

Tirshatha ni nini? (Ezra 2:63)

HEKIMA YA KIMUNGU, INAINGIAJE MIOYONI MWETU?

UFUNUO NI NINI, NA NITAPOKEAJE UFUNUO KUTOKA KWA MUNGU?

Biblia inamaana gani inaposema tutoapo unabii tutoe kwa kadiri ya imani?

Rudi nyumbani

Print this post