MISTARI YA BIBLIA KUHUSU WATOTO.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU WATOTO.

  1. MISTARI YA WAZAZI/WALEZI KUHUSU WATOTO.

Haya Mafungu ya biblia ambayo wazazi/walezi wanapaswa wayajue kuhusu watoto wao.

Zaburi 8:2a “Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu;..”

Mungu anaonyesha kuwa kupitia watoto wachanga, ambao unaweza kuwadharau hawajui kitu, hapo ndipo Mungu ameweka nguvu zake. Hivyo anza kumlea mtoto katika misingi ya kumcha Mungu tangu akiwa mdogo, kwasababu hapo ndipo Mungu anapoketi.

 Na ndio maana biblia inasema..

Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

Tabia ya kudharau watoto, au kuona kama umri wao wa kumjua Mungu bado, Yesu aliukemea sana, tunalithibitisha hilo katika..

Marko 10:13 “Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea.

14 Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao.

15 Amin, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa.

16 Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabarikia”.

Biblia inasema pia..

Zaburi 127:3 “Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, Uzao wa tumbo ni thawabu”.

Biblia bado inasisitiza wazazi, wasiwaudhi watoto wao, kwasababu zisizo na msingi, kisa tu wao ni watoto,

Waefeso 6:4 “Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.

Kwasababu malaika wao mbinguni wanawatazama uwatendeapo mabaya..

Mathayo 18:10 “Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni”.

Zaidi pia Bwana Yesu anataka wazazi/walezi wajifunze kupitia watoto walionao, hivyo kwa kupitia wao tutapata kujua siri kubwa za ufalme wa mbinguni.

Mathayo 18 : 1-5

“1 Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakisema,

2 Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao,

3 akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

4 Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.

5 Na ye yote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi;”

Lakini bado Mungu anasisitiza juu ya kuwarekebisha watoto, kwamba ni jukumu la kila mzazi/mlezi kumwadhibu mtoto wake, pale anapokosea . Hilo ni agizo la Mungu. Usipomwajibisha mtoto wako, Mungu atakuwajibisha wewe siku ile, kwa kutomtengeneza mwanao.

Mithali 22:15 “Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali”.

Mithali 23: 13 “Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.

14 Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu”.

2) WAJIBU WA MTOTO.

Vilevile mzazi, unapaswa umfundishe mwanao wajibu wake kama mtoto, Sawasawa na Neno la Mungu linavyosema,

Na mojawapo ni kuwafundisha kukutii wewe.

Waefeso 6:1 “Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.

2 Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,

3 Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia”.

Mithali 1:8 “Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako,

9 Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako”.

Pia umfundishe kujua wajibu wake wa kumtafuta Mungu tangu akiwa mdogo..kwasababu kwa Mungu hakuna utoto.

Yeremia 1:6 “Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.

7 Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru”.

Na mwisho Mkumbushe pia hata watoto watahukumiwa, na  kuzimu wapo watoto ambao hawakuwajibika katika kuwatii wazazi wao, na kumcha Mungu.

Ufunuo 20:12 “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao”.

Bwana akubariki.

Maran atha.

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
10 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

Ameeeen barikiwa

Anonymous
Anonymous
1 year ago
Reply to  Admin

Please admin uniunge ndaniya groupe la Whatsapp

Ombi Mahenge
Ombi Mahenge
2 years ago

Thank for teachings

Friedrich the son of JESUS%
Friedrich the son of JESUS%
2 years ago

Amina mtumishi, BWANA azidi kukutumia kama chombo chake!

PASKALINA MARTIN
PASKALINA MARTIN
6 months ago
Reply to  Admin

Admin niunge Whatsapp mafundisho nimeyapenda

PASKALINA MARTIN
PASKALINA MARTIN
6 months ago

Namba ni +255784552974