Unyenyekevu ni nini?

Unyenyekevu ni nini?

Biblia inasema nini kuhusu unyenyekevu?

Unyenyekevu ni ile hali ya “kujishusha” na kuwa tayari “kutumika kwa utumishi ule usiostahili kutumika” bila kiburi wala majivuno.

Biblia inasema Mungu huwapinga wote wenye kiburi na wajikuzao lakini “wanyenyekevu” anawapa Neema.

Yakobo 4:6 “Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, MUNGU HUWAPINGA WAJIKUZAO, bali huwapa neema wanyenyekevu”.

1Petro 5:5 “Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu MUNGU HUWAPINGA WENYE KIBURI, LAKINI HUWAPA WANYENYEKEVU NEEMA”.

Na tena kitabu cha Mithali kinasema…

Mithali 3:33 “Laana ya Bwana i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki.

34 Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema.”

Na zaidi ya yote, Injili ya Bwana Yesu ni kwa wote walio wanyenyekevu..

Isaya 61:1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta NIWAHUBIRI WANYENYEKEVU HABARI NJEMA; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao”.

Maana yake ni kwamba “watu wajikwezao” na “wenye kiburi”.. Hawawezi kuipokea Habari njema ya Yesu, Neema ya Wokovu inakuwa haipo juu yao.

Na pia Bwana Yesu alitufundisha ni kwa namna gani tutakuwa wa kwanza, katika ufalme wa Mbinguni.. alisema tukitaka kuwa wa kwanza, basi hatuna budi kujinyenyekeza na kuwa wadogo kuliko wote, maana yake tuwe watumwa na watumishi kwa wengine.. tofauti na hekima ya dunia inavyosema au kufundisha kuwa mtu mkubwa ni Yule anayetumikiwa na mwenye kiburi.

Marko 10.42 “Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.

43 Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu,

44 na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote.

45 Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi”.

Hivyo biblia inatufundisha kuwa wanyenyekevu siku zote, yaani kuwa “wadogo”, sehemu nyingine Bwana Yesu anasema tunapaswa tujinyenyekeze na kuwa kama vitoto.

Mathayo 18:3 “akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

4 Basi, YE YOTE AJINYENYEKESHAYE mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni”.

Unaweza kusoma pia, Mathayo 11:11, Waefeso 5:21, Zaburi 138:6, Mithali 11:2, na Mithali 18:12.

Hivyo na sisi hatuna budi kuwa wanyenyekevu siku zote, ili tukwezwe na tupate NEEMA zaidi, na sio tu kuwa wanyenyekevu kwa Mungu, bali pia kwa watu wengine wote, ikiwemo wazazi, wafanyakazi wenzetu na maboss zetu na kwa wenye mamlaka pia (Tito3:1).

Lakini tukiwa ni watu wa kiburi, au tukijiinua basi tutashushwa chini kama maandiko yanavyosema..

Luka 14:11 “Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa”.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

Neema ni nini?

SALA YA ASUBUHI

ILI NIWE KIELELEZO KWA WALE WATAKAOMWAMINI BAADAYE.

NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments