NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.

NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.

Shalom. Bwana Yesu alisema maneno haya;

Yohana 11:9 “…… Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.

10 Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake”.

Utajiuliza ni kwanini Bwana Yesu alijifananisha  na Nuru ya ulimwengu?  Ambayo ni JUA linalofanya kazi saa kumi na mbili tu, Ukilitafakari hilo kwa ukaribu ndipo utakapofahamu kuwa hii neema tuliyopewa sio ya kuichezea hata kidogo.

Zamani watu walikuwa hawajua tabia ya jua, walikuwa wanadhani kule linapochomoza, limetoka kuamka, na kule linapokwenda kuzama ndio linakwenda kulala. Lakini sisi tunaoishi sasa ndio tunafahamu vizuri  mambo yote, kwamba jua halilali wala haliamki, isipokuwa linalala linalala na kuamka kwetu sisi tunaolitegemea. Lakini lenyewe kama lenyewe linaangaza daima.

Wakati ambapo jua hulioni, wapo wengine wanaliona upande wa pili wa dunia, na wakati ambapo wale wa upande wa pili  hawaliona lipo upande wako wewe linaangaza.. Na kama ilivyo kawaida wakati ambao unaliona ndio unatumia fursa hiyo  kufanya mambo yako, kwa kujali muda, tangu asubuhi mpaka jioni, kwasababu unajua kabisa, kuwa  giza likishaingia, hakuna shughuli yoyote unayoweza kuendelea kuifanya.

Kama wewe ni msusi, kazi yako ya ususi siku hiyo inakuwa imeisha, kama wewe ni mkulima, unaweka jembe lako mgongoni unarudi nyumbani, kama wewe ni fundi wa nyumba unafunga marago yako, unakwenda nyumbani kupumzika na familia yako.. Kwasababu hakuna kazi yoyote inayofanyika kwa ufanisi usiku..

Muda wa kazi kwako unakuwa umeshakishwa kwasababu nuru haipo, ni wakati wa watu wengine walio  upande wa pili wa dunia kuamka na kufanya kazi. Na ndivyo ilivyo hata kwa Kristo Yesu Bwana wetu. Alisema

Yohana 9:4 “Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi.

5 MUDA NILIPO ULIMWENGUNI, MIMI NI NURU YA ULIMWENGU. Na tena alisema..

Yeye ni Nuru ambayo itaendelea kudumu kwa wakati wote humu duniani mpaka atakapurudi mara ya pili. Lakini wa bahati mbaya ni kuwa Nuru yake haidumu kwa watu wote ulimwenguni kwa wakati mmoja..

Ikiwa na maana  kuwa neema yake ya wokovu, haipo kwa watu wote duniani sasa hivi, kwa wakati mmoja. Hili jambo linaweza likawa ni gumu kwako kulielewa, lakini ndio ufahamu leo kuwa neema ya wokovu haipo kwa watu wote unaowaona leo hii duniani..

Biblia inatufundisha kuwa wayahudi walipata neema ya kuhubiriwa na Yesu lakini walimkataa, hawakujua kuwa hilo jambo sio la kudumu milele. Na ulipofika wakati wa masaa yao 12 kuisha neema hiyo ilihamia kwetu sisi watu wa mataifa, tukaanza kuhubiriwa na sisi  injili, wao wakabakia kama vile wapagani, na jambo hilo liliendelea kwa muda mrefu hadi sasa ni miaka takribani 2000 bado neema hiyo hajawarudia ya kuiamini injili. Hili jambo linatisha sana.

Sio kwamba mioyo yao ni mizito kupita sisi, hapana, ni kwasababu Nuru ya wokovu haipo tena kwao, ipo upande wa pili wa ulimwengu ambao ni ndio sisi watu wa mataifa..

Lakini hilo nalo sio la kujisifia, kwasababu na kwa upande wetu sisi, bado kila eneo na taifa, lina masaa yake 12, na ndio maana ukiangalia katika historia ya kanisa utaona, kanisa la kwanza lilianzia kule Bara la Asia, na wakati wao ulipopita, ikahamia, bara la Ulaya, na wao pia wakati wao ulipopita ilihamia bara la Amerika, na wakati wao pia ulipopita ndio ikarudi bara letu la Afrika.

Na ndio maana kwanini leo hii unaona kuna mwitikio mkubwa wa Mungu huku Afrika kuliko sehemu nyingine yoyote ulimwenguni, nikwasababu Nuru ya ulimwengu ipo kwetu sasa, Lakini na sisi tupo ukiongoni kabisa wa saa zetu 12,kwasababu sisi ndio tunaomalizia kabla ya neema hii kurudishwa Israeli tena. Kama ulikuwa hujui mpaka sasa wayahudi Mungu ameshawaandaa moyo ya kumwamini Kristo na neema hiyo ikishapita kwetu ndugu yangu, dunia nzima, yaani sisi tuliobakia mataifani, hakutakuwa na neema tena ya wokovu..tutabakia tu kuwa wapagani kuliko hata wapagani wenyewe walivyo.

Lakini hilo la neema kuwepo Afrika sio la kujivunia kwasababu bado neema hii, inazunguka kati ya mtu na mtu. Yaani mimi na wewe kila mmoja wetu, ametengewa muda wa kuiona Nuru hiyo ya ulimwengu (yaani Yesu Kristo), Na kama usipojua wakati wako wa kujiliwa ni upi na ni nini unapaswa ufanye kwa wakati huo, kama ilivyokuwa kwa Israeli wakati ule Yesu alipowalilia, hakapuuzia, na wewe ukadhani Roho Mtakatifu atakuwa na nafasi kila siku ya kukuvuta kwake umwamini Kristo, nataka nikuambie ndugu yangu umekwisha.

Ikiwa leo hii, unasikia msukumo fulani wa kumgeukia Kristo, ujue huyo ni Roho Mtakatifu ndani yako, ujue hiyo ni Nuru ya Kristo ndani yako inakumulikia, uone njia.  Ni jukumu lako kuifuata, na kuitii bila kupoteza poteza muda, na kutenda yanayokupasa kufanya..

Kumbuka tena alisema..

Yohana 11:9 “Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.

10 Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake”.

Akiwa na maana kuwa kuna wakati utafika,  hutampata  Kristo hajialishi kuwa utajifanya unamtafuta kiasi gani, utaishia tu kujikwaa, na unajua kujikwaa kunavyoumiza, Maana yake ni kuwa utakuwa unatilia shaka kila kitu kwenye maandiko, utafikia wakati utasema hata Mungu hayupo, utaishia kuamini, historia za wanasayansi, na sio Mungu tena, utaishia kudhihaki tu injili, au kusema hakuna Mungu, hiyo yote ni kwasababu Nuru hiyo haipo ndani yako tena. Hata uhubiriweje vipi, kamwe huwezi kushawishika tena tena kama unavyoshawishika leo.

 Lakini wakati huo huo utaona jirani yako, anaamini injili na anasimama, na Kristo anatembea naye, wewe utabakia kusema Yule ni mwandawazimu tu.

Umeona, hii neema sio ya kuchezea kabisa, ni kweli bado ipo duniani haijaondoka, lakini huwa haina tabia ya kuganda sehemu moja, inazunguka, , kama wakati wako umefika halafu unaipuuzia, ikiondoka hutaipata tena. Tujifunze kwa waisraeli ili tumwogope Mungu.

Lakini kama leo utaahirisha  maisha yako ya dhambi, na unataka kumpa Yesu maisha yako, akuokoe, basi tutafute inbox, au piga namba hizi tuombe kwa pamoja +255789001312

Bwana akubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Alan Nyundo
Alan Nyundo
2 years ago

Amen