Title June 2019

UFUNUO: Mlango wa 11

Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Ufunuo, biblia inasema Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu,. Heri maana yake ni amebarikiwa, hivyo umebarikiwa wewe ambaye unakiu ya kufahamu maarifa yaliyomo katika kitabu hichi cha Ufunuo, wengi hawakipendi, wengine wanakiogopa kwasababu kimebeba hukumu nyingi lakini pia wafahamu kitabu hiki kimebeba Baraka nyingi kwa yeye asomaye na kuyashika yaliyoandikwa humo.. leo tukiwa katika ile sura ya 11, Kama hujapitia sura zilizotangulia, ni vizuri ukazipitia kwanza taratibu kisha kwa Neema za Bwana tuendelee pamoja katika sura hizi za mbeleni. Kupata maelezo ya ufunuo sura ya 10 bofya hapa ⏩ ufunuo 10……Tusome:

Ufunuo 11:1 “Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo humo.

2 Na behewa iliyo nje ya hekalu uiache nje wala usiipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili”.

Hapa tunaona Yohana akipewa ono lingine likiwa baada ya Ono la yule Malaika Mkuu, maono haya yalifuatana lakini katika Ono hili aliona anapewa Mwanzi kama fimbo, na Mmoja akamwambia ainuke akalipime hekalu la Mungu na madhabahu, na hao wasujuduo humo..

Sasa katika Ono hili Yohana anapelekwa moja kwa moja katika mji mtakatifu, yaani YERUSALEMU, Na anafika anaonyeshwa Hekalu la Mungu, ambalo lipo Yerusalemu na anaambiwa alipime, Kumbuka hekalu la kwanza lililojengwa na Mfalme Sulemani, lilibomolewa na Mfalme Nebukadneza, Na baada ya wana wa Israeli kutoka utumwani Babeli, walijenga tena Hekalu lingine la pili mahali pale pale lilipokuwa limejengwa hekalu la kwanza…lakini nalo baada ya miaka kadhaa kama 585 hivi lilikuja kubomolewa tena na jeshi la Warumi (mwaka 70BK), Hivyo Israeli ikabaki bila hekalu tangu huo mwaka wa 70BK mpaka Leo…Takribani miaka 1949 mpaka sasa..

Sasa maandiko yanatabiri kuwa siku za mwisho, Hekalu hili litajengwa tena kwa mara ya tatu, na litakapojengwa, wayahudi watarejea katika desturi zao kama za kwanza za utoaji wa sadaka za kuteketezwa na kufanya ibada za upatanisho. Na hiyo yote inatokana na Wayahudi macho yao kufumbwa kutomjua kuwa YESU KRISTO waliyemkataa ndiye Masihi wao aliyetabiriwa na yeye ndiye Hekalu la Mungu, na yeye ndiye Sadaka iliyobora, kwamba wangemjua yeye kwa namna hiyo basi wasingekuwa na haja ya kurejea tena kufukiza uvumba na kuchinja sadaka za Wanyama na kushughulika na hekalu la kimwili…Lakini biblia inatabiri wataendelea na huo upofu hata mpaka watakapolijenga tena Hekalu la Tatu, na kipindi kifupi sana baada ya kumaliza kujilenga hekalu hili, baadhi yao watafumbuliwa macho na kuigundua sadaka ya kweli ni ipi na hekalu la kweli ni lipi kuwa ni YESU KRISTO, Hivyo hao watakaojua ndio watatiwa muhuri na Roho Mtakatifu mwenyewe..Ndio wale 144,000 tunawasoma katika Ufunuo 7..

Sasa kwasababu ni Mungu mwenyewe ndiye kawafumba macho wasimjue Kristo, hivyo bado yupo nao hajawaacha kabisa…Bado analipenda Taifa lake Israeli na kulilinda, aliahidi kutokuliacha kwa namna yoyote ile.

Isaya 44:21 “Kumbuka haya, Ee Yakobo; nawe Israeli, maana wewe u mtumishi wangu; nimekuumba; u mtumishi wangu; Ee Israeli, hutasahauliwa na mimi”. Soma pia 

Isaya 49:16-26.

Kwasababu hiyo basi hata katika Ujenzi wa Hekalu hilo la tatu watakalokuja kulijenga bado Bwana atakuwa pamoja nao..atawapigania na kuwatetea katika ujenzi huo, maadamu hawamjengei baali wala miungu migeni bali wanamjengea Mungu wa mbinguni hivyo Bwana atawaheshimu hata katika Imani hiyo. Kwahiyo biblia inatabiri watafanikiwa katika hilo, na watalisimamisha hekalu la tatu..

Sasa mahali ambapo Hekalu hili la tatu, linapaswa lijengwe leo pamesimamisha Msikiti wa Waislamu. Ingawa wapo watafiti wa kiyahudi ambao Wamejaliwa akili na Bwana wanasema…Hekalu la kwanza la Sulemani lilikuwa limejengwa futi 150, kutoka mahali Msikiti huo ulipojengwa..kwahiyo endapo wakitaka kulijenga tena Hekalu inaweza kufanyika hivyo pasipo kuugusa huo msikiti. Lakini kwa vyovyote vile mahali pale lazima pasafishwe kupisha ujenzi wa tatu wa Hekalu hilo, hivyo kama ni eneo la kwenye huo msikiti, itahitajika muujiza kuuondoa. Na maandalizi ya ujenzi huo yapo tayari sasa hivi tunavyozungumza…kila kitu kipo tayari ghafla tu! Siku sio nyingi kutasikika ujenzi umeanza huko. Na hiyo itakuwa ni ishara kubwa ya siku za mwisho, kwani ndio utakuwa mwanzo wa kufunguliwa kwa lile juma la 70 la mwisho la Danieli lililosalia. Ambayo ni miaka 7 tu.

Sasa wakati wa ujenzi wa Hekalu hili, shetani naye atajaribu kuingilia kwa namna zote, kuzuia au kujipendekeza kama alivyokuwa anataka kujiingiza na kujipendekeza wakati wa ujenzi wa Hekalu la pili, pale walipotaka kujiingiza katika kuchangia ujenzi wa hekalu lile…

Ezra 4:1 “Basi adui za Yuda na Benyamini, waliposikia ya kuwa wana wa uhamisho wanamjengea Bwana, Mungu wa Israeli, hekalu,

2 wakamkaribia Zerubabeli, na wakuu wa mbari za mababa, wakawaambia, Na tujenge sisi nasi pamoja nanyi; kwa maana tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi, nasi twamtolea dhabihu tangu zamani za Esarhadoni, mfalme wa Ashuru, aliyetupandisha mpaka hapa.

3 Lakini Zerubabeli, na Yoshua, na wakuu wengine wa mbari za mababa katika Israeli, wakawaambia, Ninyi haiwahusu kushirikiana nasi katika kumjengea Mungu wetu nyumba; bali sisi wenyewe peke yetu tutamjengea Bwana, Mungu wa Israeli, nyumba, kama mfalme Koreshi, mfalme wa Uajemi, alivyotuamuru.

4 Ndipo watu wa nchi wakaidhoofisha mikono ya watu wa Yuda, wakawasumbua, walipokuwa wakijenga”.

Na kadhalika katika ujenzi huu wa hekalu la Tatu, Mpinga-Kristo (Papa wa wakati huo) atataka kuingiza ushirika na Wayahudi kulijenga, na hivyo wayahudi watafanya kosa kubwa sana la kukubali kushirikiana naye (Na mwisho wa siku ataingia Agano na Taifa la Israeli), kama Danieli 9:27 inavyotabiri…atataka kuweka mchango wake mkubwa sana katika kazi hiyo, kwa njia ya mkataba..Kwani wakati huo pia atakuwa ameshapewa nguvu na mataifa yote ulimwenguni na kuaminiwa kuwa ni mtu wa Amani (Man of peace), mkataba huo au makubaliano hayo atakaoingia na Taifa la Israeli utakuwa ni wa miaka saba..kwamba ndani ya hiyo miaka saba tutafanya hichi na hichi kwa pamoja.Wayahudi pasipo kujua kuwa yule ndiye Mpinga-Kristo aliyetabiriwa katika Kitabu cha Danieli kuwa malengo yake ni kuabudiwa kama Mungu ndani ya hekalu la Mungu, watakubaliana naye…Sasa kumbuka Kanisa katoliki ndio kanisa lenye utajiri mkubwa kuliko taasisi zote za kidini na kisiasa ulimwenguni…

Huo utajiri lilianza kuupata wakati wa kipindi cha giza, watu walipoambiwa watoe michango ili wafanyiwe ibada Fulani za ukombozi, ilikuwa ili mtu wabarikiwe ni lazima utoe kiasi Fulani cha fedha, ili ndugu zao wapate kuokolewa kutoka toharani lazima utoe kiasi Fulani cha fedha n.k sasa kuanzi hicho kipindi mpaka leo, limekusanya utajiri mkubwa usioelezeka. Limejenga ngome kubwa duniani kote, Ukienda leo Israeli, kila mahali utakapoingia kuanzia Goligotha mpaka Galilaya na Yerusalemu ni Taasisi za kikatoliki tu zimefurika, kama hujui jambo hilo fuatilia utaona..Tunaishi ukingoni mwa muda sana.

Hivyo huyu Mpinga-Kristo atafanikiwa mpaka kujipenyeza katika Hekalu la Mungu, kwa nguvu zake za ushawishi na za kifedha..na hivyo kuwa CHUKIZO KUBWA SANA MBELE ZA MUNGU, Hilo ndilo chukizo la Uharibifu. Lililotabiriwa na Nabii Danieli na Bwana Yesu pia kulirudia tena kuwa litasimama patakatifu.. Na Mtume Paulo pia alikuja kulitilia msisitizo tena.

2Wathesalonike 2:3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;

4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe KUKETI KATIKA HEKALU LA MUNGU, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.

5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?”

Huyo mtu wa kuasi ni Mpinga-kristo, ukiendelea kusoma hiyo mistari utaona Paulo anamwelezea, hivyo huyu mpinga-kristo atajiingiza katika hekalu la Mungu, na ghafla ataanza kubadilika Tabia na kutaka kuabudiwa, na watu baadhi kutoka duniani kote wataanza kumwabudu na kumsujudia…

Sasa tukirudi kwenye lile ono ambalo Yohana anaambiwa alipime Hekalu la Mungu, utaona aliambiwa apime vitu vikuu vitatu..1) Alipime Hekalu lenyewe 2) Aipime madhabahu 3) Awapime watu wanaoabudu humo…Na behewa iliyokuwa nje aliiambiwa asiipime.

Sasa vipimo vinavyozungumziwa hapo sio vipimo vya kimwili..hapana bali ni vipimo vya kiroho, hata sasa sisi wakristo tunapimwa kuangaliwa tumesimamaje! Wale malaika wawili waliotumwa Sodoma walitumwa wakapime kiwango cha uovu na utakatifu kilichopo Sodoma na ghomora na kurudisha majibu, Ufalme wa Mfalme Belshaza ulipimwa kwenye mizani na kuonekana kuwa umepunguka n.k.

..Kadhalika hapa Yohana anaambiwa akalipime Hekalu la Mungu…maana yake akatazame mambo yanayoendelea kule katika Roho je yapo sawa kama yanavyopaswa yawe? Hiyo ndio maana ya kupima… Na pia anaambiwa apime madhabahu je! Vinavyofanyika vipo sawa? Na pia anaambiwa awapime hao wasujuduo humo? Je! Wanayemwabudu ni nani ndani ya hilo Hekalu? ni Mungu kweli wa Israeli? Na sasa tunajua ni lazima kasoro zionekane kwasababu anayeabudiwa ndani ya hilo hekalu ni Mpinga-Kristo Papa-wa-wakati huo na si Mungu..

Utaona pia alikatazwa asiipime behewa iliyo nje ya Hekalu, kumbuka behewa/ uwa wa nje ilikuwa ni sehemu ya hekalu la Mungu, ambalo watu wasio wayahudi waliompenda Yehova walimwabudia Mungu hapo, hawakuruhusiwa kufika uwa wa ndani..Lakini hapa anaambiwa hata asihangaike kuipima behewa iliyo nje ya madhabahu, kwasababu kwasasa haina kazi tena, jicho lake halipo kwao tena (yaani watu wa mataifa)..

Hii ni kuonyesha kuwa, mpaka hayo mambo yaanze, Mungu atakuwa kashamalizana na sisi watu wa Mataifa, neema itakuwa Imehamia Israeli, Hivyo kama hujatengeneza mambo yako sawa na Mungu sasa, usitazamie wakati huo kutakuwa na neema kwako..

Sasa tukirudi kwa Wayahudi ambao sasa, Mungu anawanyoa kwa vipimo vyake, na kuonekana kuwa wamepunguka, maneno haya ndio yaliyofuata…

MASHAHIDI WAWILI

Ufunuo 11: 3 “Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia.

4 Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi.

5 Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa”.

Bwana atawanyanyua hawa mashahidi wawili, watakaokuwa na Neema ya Mungu ya kipekee sana juu yao…Hawa mashahidi wawili watakuwa na kazi mbili tu! Ya kwanza ni kwenda kumfunua Yule Mpingamizi ajiinuaye nafsi yake na kutaka kuabudiwa ndani ya Hekalu la Mungu, kana kwamba yaye ndiye Mungu..Na pia mashahidi wawili watakuwa na kazi ya kuwafundisha wayahudi, Hekalu halisi ni lipi, na madhabahu ya kweli ni ipi, kuwa hekalu halisi na madhabahu halisi ni KRISTO YESU. watu hawa watakuwa ni Manabii…

Watawaambia wayahudi kuwa HUYU MTU NDANI YA HEKALU Ndiye Mpinga-Kristo mwenyewe. Ni shetani katika kiti cha enzi cha kibinadamu. Na pia hawa mashahidi wawili watawaambia kuwa Yesu Kristo waliyemkataa miaka 2000 iliyopita ndiye Masihi mwenyewe… sasa kutokana na Ishara kubwa watakazokuwa wanafanya hawa manabii wawili, wayahudi wengi wataamini…Kumbuka kigugumizi kikubwa walichonacho wayahudi sasa ni ISHARA, siku zote huwa wanataka ishara ili waamini,tangu kipindi cha Yesu ilikuwa hivyo, na ndio maana hata leo ukienda kuwauliza ni kwanini hawamwamini Yesu Kristo, watakwambia ikiwa huyu Yesu wenu ni Masihi basi tumwone leo akifanya ishara za manabii kama vile Musa na Eliya kushusha moto n.k.

Sasa Mungu atawapa wanachokitafuta, kwa kupitia injili za hawa mashahidi wawili ambao wanamtukuza Kristo,

Ndipo watakapojua na kutubu na kulia na kuomboleza na kusema hakika tulifanya makosa kumwua mwokozi wetu, Bwana wetu mwenyewe na kumwuza kwa watu wa mataifa…macho yao yatafumbuliwa watamwombolezea yeye waliomchoma kama Biblia inavyotabiri katika Zekaria 12:10.

Wale watakaoamini ushuhuda wa manabii hawa wawili(mashahidi wawili) watatiwa muhuri, ambaye ni Roho Mtakatifu…Kwa maelezo juu ya hili tafadhali rejea ufunuo, mlango wa saba katika mfululizo huu wa kitabu hichi.

Na Hawa mashahidi wawili ndio watakaotimiza sehemu ya zile baragumu nne za kwanza,kama tulizojifunza katika Ufunuo Mlango wa 8. Watafanya ishara kama zile za Musa, alizofanya ili kuwatoa wana wa Israeli kwenye Kamba za Farao, kadhalika na hawa watafanya ishara kama zile zile, bahari kuwa damu, jua kutiwa giza lengo ni kuwatoa wana wa Israeli katika kifungo cha Mpinga-Kristo..Na pia manabii hawa watafanya ishara kama zile za Eliya kufunga mbingu mvua isinyeshe, lengo ni kuigeuza mioyo ya watu imgeukie Mungu wa Israeli, kadhalika na hawa watafunga mbingu mvua isinyeshe na kuipiga dunia kila wanapotaka ili tu kuwageuza wana wa Israeli mioyo yao imgeukie Mungu, na kama ilivyokuwa kwa Eliya mtu yeyote aliyekuja kwa lengo la kumdhuru moto ulishuka ukawateketeza, vivyo hivyo na hawa manabii wawili itakuwa ni kitu kile kile, moto utashuka kuwateketeza maadui zao, Kumbuka shughuli yote hii ya itakapotokea Kanisa litakuwa limeshakwenda kwenye unyakuo.

Ufunuo 11:16 “Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo.

7 Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua.

8 Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulibiwa.

9 Na watu wa hao jamaa na kabila na lugha na taifa waitazama mizoga yao siku tatu u nusu, wala hawaiachi mizoga yao kuwekwa kaburini

10 Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi.

11 Na baada ya siku hizo tatu u nusu, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.

12 Wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama.

13 Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka; wanadamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu”.

Wakati huo Papa-mpingakristo atapata jeraha kubwa sana kwa mahubiri ya hawa mashahidi wawili…na mahubiri ya hawa manabii wawili yatamwuzunisha sana na kumwumiza kichwa kama vile zile taarifa za mamajuzi zilivyomhuzunisha Herode kipindi cha kuzaliwa Bwana Yesu…tutazidi kuielewa habari hii vizuri katika sura inayofuata…lakini kwa ufupi hawa Mashahidi wawili watatoa unabii kwa muda wa miaka mitatu na nusu, na watakapomaliza ushuhuda wao yule mnyama atokaye baharini (Yaani mpinga-Kristo,PAPA) Atafanya vita nao, atatangaza kwenye vyombo vyote vya habari kuwa kuna baadhi ya watu wanachafua amani ya dunia, na wanakwenda kinyume na makubaliano, atatuma vyombo vya usalama viwafuatilie lakini haitasaidia, mpaka mashahidi wawili hao, watakapomaliza ushuhuda wao, Bwana ataruhusu wauawe kama ilivyokuwa kwa Bwana alivyomaliza ushuhuda wake. Na watauawa mahali palepale Bwana wao alipouawa Yerusalemu, Golgotha..Ndio mji ambao kwa jinsi ya roho unaitwa Sodoma na Misri.

Ni Sodoma kwasababu ya mambo yatakayokuwa yanaendelea pale Yerusalemu wakati huo, na Misri kwa utumwa waliokuwa wanapitishwa katika roho na Mpinga-kristo. Na baada ya siku tatu na nusu watafufuka na kupaa juu adui zao wakiwatazama…wataingiwa na hofu kuu, na saa hiyo hiyo tetemeko kubwa la nchi litatokea na wanadamu 7,000 watakufa kwa tetemeko lile. Naam! Hata Kristo alipofufuka kulitokea tetemeko kubwa la nchi. Na wayahudi wachache watakaoiona hiyo ishara wataingiwa na hofu, na watazidi kumtukuza Mungu. Kumbuka baada ya hawa manabii wawili kuondoka ndipo Papa atavunja agano aliloingia na wayahudi na dhiki kuu kuanza kwa miaka mingine mitatu na nusu iliyosalia.

Tukiendelea na mistari unaofuata Biblia inasema…

Ufunuo 11:14 “Ole wa pili umekwisha pita, tazama ole wa tatu unakuja upesi.

15 Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.

16 Na wale wazee ishirini na wanne waketio mbele za Mungu katika viti vya enzi vyao wakaanguka kifulifuli, wakamsujudia Mungu.

17 wakisema, Tunakushukuru wewe, Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa sababu umeutwaa uweza wako ulio mkuu, na kumiliki.

18 Na mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, na hao walichao jina lako, wadogo kwa wakubwa, na wa kuwaharibu hao waiharibuo nchi.

19 Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana”.

Ole ya tatu ndio ole ya mwisho, na inahusu Baragumu la saba. Na baragumu hili lilipopigwa zikasikika sauti mbinguni zikisema…Ufalme wa duniani umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu Yesu Kristo, sauti hizi utaona zinatoka mbinguni na sio sauti ya mtu mmoja bali za wengi…na hao si wengine Zaidi ya watakatifu walionyakuliwa…maana hao Kristo ndio Bwana kwao. Hao ndio watakaorithi na Bwana katika Mbingu mpya na nchi mpya..ndio watakaokuwa wafalme katika nchi mpya.

Na katika Baragumu hili inaelezea SIKU YA BWANA..Siku ambayo Bwana atashuka kutoka mawinguni kuyahukumu mataifa, siku ambayo kila jicho litamwona..siku ambayo atakuja kuanza utawala mpya wa amani wa miaka 1000 hapa ulimwenguni.

Mstari wa mwisho unasema “Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake”..Tunajua kuwa mbinguni hakuna hekalu kama haya ya kiduniani…Hekalu la Mungu ni wale watakatifu walionyakuliwa…wale ndio hekalu la Mungu, Mungu anakaa katikati yao, na mbinguni pia hakuna sanduku la agano..Kwahiyo sanduku la agano hapo linafunua agano Mungu aliloingia na watu wake (Yeremia 31:33 “siku hiyo watakuwa watakuwa watu wangu na mimi nitakuwa Mungu wao”).Hivyo utakuwa ni wakati wa kufunuliwa wana wa Mungu, mbingu zitafunguka na watu wote waliosalia wa mataifa wasiokufa katika siku ya Bwana watamwona Bwana na watakatifu wake wakishuka mbinguni, waking’aa kama jua! Oo haleluya! Hao ndio hakalu la Bwana lililofunguliwa mbinguni.

Baada ya hayo kutakuwa hakuna tena muda, kama biblia inavyosema…Ufunuo 10:6 “akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya; 7 “..isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu;..”

Embu angalia mambo haya yalivyojibinja ndani ya kipindi kifupi, baragumu zote sana zitakuwa ndani ya miaka 7 tu ya mwisho, dhiki kuu, mapigo vya vitasa yote hayo ni ndani ya huo muda mfupi sana Je! Umempa Bwana Maisha yako? Je! Maisha yako yanastahili wokovu?..una uhakika Bwana akija leo utakwenda naye kwenye unyakuo?.Jibu unalo ndani ya moyo wako, ni maombi yangu, uchukue uamuzi sasa wa kumruhusu Bwana ayatawale maisha yako ndani ya hichi kipindi kifupi kilichobakia,

Neema ya Bwana iwe pamoja nawe.

 Bwana akubariki sana.

Maran atha!

Usikose mwendelezo huu wa sura inayofuata ya 12, bofya hapa.⏩ Ufunuo 12

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

MAANDALIZI YA UJENZI WA HEKALU LA TATU YAPO TAYARI.

CHUKIZO LA UHARIBIFU NI NINI?

MPINGA-KRISTO NI NANI?


Rudi Nyumbani

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 10.

Shalom…Karibu katika mwendelezo wa Kitabu cha Ufunuo..ambapo leo kwa Neema za Bwana tutaendelea na ile sura la 10..Kama hujapitia sura zilizotangulia, ni vizuri ungezipitia kwanza ili tuweze kwenda pamoja katika hizi sura zinazofuata.

Katika sura iliyopita tumeona malaika sita wakipita baragumu zao, na tuliona matukio yaliyoambatana na baragumu hizo, lakini katika sura hiyo hatukuona malaika wa saba akipiga baragumu lake, ikifunua kuwa kuna vitu Fulani vinapaswa viendelee kabla malaika wa mwisho kupiga baragumu…Na ndio tunaona katika sura hii ya 10, Yohana anakatishwa maono ya baragumu la mwisho la saba na kuonyweshwa ono lingine la Ajabu, ambalo ufunuo wake utatimia kabla ya baragumu la mwisho la saba kupigwa..Tusome.

Ufunuo 10: 1 “Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto”.

Sasa huyu malaika si mwingine Zaidi ya Bwana Yesu Kristo, kumbuka Bwana Yesu sio malaika viumbe wa rohoni wanaotumika mbinguni, hapana! Bali ni “MALAIKA WA AGANO” au kwa lugha nyingine “MJUMBE WA AGANO” (Malaki 3:1 Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule MJUMBE WA AGANO mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi.

…Kwa lugha ya kiingereza “ANGEL OF THE COVENANT or MESSENGER OF THE COVENANT”…Neno malaika ni neno la kigiriki lenye tafsiri ya MJUMBE…kwahiyo kuna aina mbili za wajumbe,1) Wajumbe wa kimbinguni ambao ndio malaika wa rohoni, 2) na pia wapo wajumbe wa kidunia, ambao hao ni wanadamu…Yohana Mbatizaji alikuwa ni Mjumbe wa Mungu wa kidunia, Gabrieli ni mjumbe wa Mungu wa kimbinguni…wote hawa ni Malaika, kwa kigiriki ‘Angelos’ kwa kiebrania ‘Malokh’ kwa Kiswahili ‘Malaika’. Kadhalika wale malaika saba wa makanisa saba ya Asia tuliowaona katika Ufunuo Mlango wa 2 na wa 3 wale ni wanadamu.

Hivyo katika Ono hili Yohana anaonyeshwa Malaika mwenye nguvu akitoka mbinguni, kirahisi Zaidi tunaweza kusema Yohana alimwona Mjumbe mwenye nguvu akitoka mbinguni…Sasa Mjumbe huyu si mwingine Zaidi ya BWANA YESU KRISTO, Akiwa katika mfumo wa ‘KIMALAIKA WA MBINGUNI’..Ni Yesu Kristo mwenyewe akijidhihirisha kama Malaika katika ono… lakini  utasema Bwana anaweza akajidhihirisha kama Malaika?…Jibu ni ndio! Anaweza…

Mwanzoni kabisa wa kitabu hichi tunamwona akijifunua kwa sifa kama za viumbe vya rohoni, malaika walizo nazo, utaona katika Ono Yohana alimwona ana macho kama miali ya moto…na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana. (Ufu.1:13-15), hakuna mwanadamu wa namna hiyo…Lakini alikuwa ni Bwana akijifunua kwa sifa za malaika..Na hapa hivyo hivyo ni Bwana Yesu yule yule akishuka kutoka Mbinguni kwa mfano wa Malaika…Uso wake uking’aa kama jua, na miguu yake kama nguzo ya moto…Uso wake kung’aa kama jua unadhihirisha utukufu wake… ukuu wake, kama vile jua linavyong’aa na kuangaza sana na kuwa Nuru ya Ulimwengu mzima..Kadhalika Kristo naye ni Nuru ya ulimwengu, maandiko yanasema hivyo katika Yohana 8:12..Na ni Kristo pekee ambaye uso wake unang’aa kama jua, hakuna mjumbe wowote wa duniani wala mbinguni ambaye uso wake unang’aa kama jua..Ndio maana utaona tena alijidhihirisha kwa namna hiyo mbele ya wanafunzi wake katika..

Mathayo 17: 1 “Na baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani; 2 akageuka sura yake mbele yao; USO WAKE UKANG’AA KAMA JUA, mavazi yake yakawa meupe kama nuru”.

Na pia katika Ono alilooneshwa Yohana alimwona, akiwa amevikwa wingu kama vazi, wingu linaashiria utukufu wa Mungu, ndio maana tunasoma mahali Fulani kwamba Kristo atakuja na Mawingu, kama alivyoondoka na mawingu, na sisi tutamlaki mawinguni (Utukufuni). Na pia tunaona juu ya kichwa chake kulikuwa na upinde wa Mvua, Upinde wa Mvua unaashiria Agano la Mungu analofanya na wanadamu, Kwamba Kristo ni Bwana wa maagano, kama vile alivyoweka Agano lake na nchi kuwa hataiangamiza dunia tena kwa gharika ya maji, na mpaka leo hilo Neno lake hajalitangua, vivyo hivyo, maneno yake mengine yote yaliyosalia hawezi kuyatangua, yeye ni Mungu wa kushika maagano, ndio maana unaona juu ya kichwa kuna moja ya ishara ya Maagano yake aliyoyafanya juu ya nchi kuashiria kuwa mwenye mamlaka ya kuangia maagano amesimama naye ni mmoja tu Yesu kristo.

Tukiendelea na mstari wa pili biblia inasema..

Ufunuo 10:2 “Na katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunguliwa. Akaweka mguu wake wa kuume juu ya bahari, nao wa kushoto juu ya nchi”

Katika mkono wake wa alikuwa na kitabu kilichofunguliwa..Kitabu hichi ni kitabu cha Ukombozi, ambacho ndio kile tulichokiona katika mlango wa 5 wa kitabu hichi cha Ufunuo..kitabu hichi ndio kimebeba siri zote za URITHI WA MWANADAMU, yaani mwongozo wote wa namna ya kuishi katika hii dunia milele kama Mungu alivyomkusudia mwanadamu aishi, na kilikuwa ndani na nje na kimefungwa na mihuri saba…Na kama tulivyosoma katika Ufunuo Mlango wa 5 hakuonekana mtu yoyote mbinguni au duniani aliyestahili kukifungua wala kukitazama kitabu hicho isipokuwa Mwana-Kondoo pekee tu peke yake, Na hivyo mwanakondoo ndiye akakipokea na akazivunja mihuri zake..Na hapa anaonekana akikishika kikiwa kimefunguliwa.

Ndugu, Siri zote za ukombozi zimuhusuzo mwanadamu, kuanzia kuumbwa kwake mpaka sasa, na urithi wote wa namna ya kuitawala hii dunia na siri zote, mpaka milele anazo sasa Bwana wetu Yesu Kristo, yeye ndiye aliyeketi sasa katika Kiti cha Enzi, alipokuwa hapa duniani alikuwa hajapokea bado mamlaka,hivyo hata siku ya kurudi kwake ilikuwa haijafunuliwa ndio maana akasema…siku hiyo hakuna aijuaye isipokuwa Baba tu!..Lakini sasa ameshakipokea hicho kitabu cha Ukombozi, hivyo siri zote zikiwemo tarehe na muda, na saa ya kuuhukumu ulimwengu anazijua, hakuna kilichojificha tena kwake. Mwanzo wa kuumbwa kwa ulimwengu, na vizazi vyote na kila kitu kimewekwa Dhahiri mbele zake.

Na hapa anaonekana amekishika hicho kitabu kikiwa kimefunguliwa, hakina tena mihuri kwasababu mihuri yote imeshavunjwa, na akashuka na kuweka mguu wake wa kuume juu ya bahari na wa kushoto juu ya nchi.

Kwanini ameweka hivyo miguu yake mmoja habarini mwingine nchi kavu…Tutakuja kuona hapo mbeleni kidogo sababu ya yeye kufanya hivyo.

Tukiendelea na mstari unaofuata Yohana anaendelea kuona na kusikia mambo mapya..

Ufunuo 10: 3 “Naye akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia, zile ngurumo saba zikatoa sauti zao.

4 Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie muhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike.”

Sasa tunaona pindi huyu Malaika aliposhuka tuu, alilia kwa sauti kuu…kama vile simba angurumaye…Naam Kristo ni Simba wa Yuda akinguruma, mbingu na nchi ni lazima zitetemeke…Yohana alimwona katika maono mengine mwanzoni kabisa wa kitabu hichi, akasema sauti yake ikiwa kama sauti ya maji mengi, lakini hapa anatoa sauti kama ya Simba. Na cha ajabu Zaidi, alipotoa hiyo sauti, ikaambatana na ngurumo..Ni kawaida mahali pakitokea sauti kubwa ni lazima hiyo sauti itikise vitu Fulani mahali Fulani ambavyo hivyo vitu kwa mtikisiko huo vitatoa sauti fulani…Hata ukiangalia spika kubwa zinazotumika kwenye mikutano..utaona zinapotoa yale mawimbi yake makubwa ya sauti, kuna kitu mfano wa kitambaa kigumu kimewekwa kwa mbele..na utaona na chenyewe sauti inapotoka kinakuwa kinatikisika na kama sio imara kinaweza hata kuchanika..kwaajili ya nguvu ya Sauti..Na pia utaweza kusikia mwangwi wake mahali Fulani kwa mbali…hata mara nne au tano…lakini ni sauti hiyo hiyo moja, imezaa nyingine nyingi…..Na ndivyo hapa, Sauti moja ya Kama mngurumo wa Simba imetengeneza ngurumo nyingine saba mahali Fulani.

Na Yohana aliposikia hizo sauti za Ngurumo saba…alikuwa tayari kuandika…kwasababu aliambiwa aandike kila alichokiona na kukisikia…Lakini alipokuwa katika kuandika sasa sauti ya hizi ngurumo saba, akasikia sauti ikimwambia “USIANDIKE! Hayo maneno uliyoyasikia yaliyonenwa na hizo ngurumo saba.”

Sasa hizi ngurumo saba ni sauti saba, ambazo zote zimeakisi kutoka kwenye ili sauti moja kuu ya KRISTO YESU..Ni kama mwangwi…Kwahiyo ni wazi kuwa zitakuwa zinazungumzia kitu kimoja…zitakuwa hazipingani…isipokuwa zitakuwa zinatofautiana kidogo sana katika kutoa ujumbe kwasababu hata mwangwi ulioakisiwa kwenye jiwe ni tofauti na uliokisiwa kwenye mwamba…ingawa maneno ni yale yale, isipokuwa yameakisiwa katika sehemu mbili tofauti..Na ngurumo saba zitakuwa ni sauti saba, zenye ujumbe unaokaribiana sana, usiopingana na mwingine…ambazo zitakuja kufunuliwa kipindi kifupi sana kabla ya unyakuo kufika. Katika hizo Bibi arusi atapata Imani ya kwenda kwenye unyakuo…Zitakuwa ni Siri Fulani baadhi ambazo zipo katika kile kitabu Bwana Yesu alichokishika katika mkono wake kilichofunguliwa…Na Siri hizo Bwana atazifunua kwenye Kanisa lake kupitia huduma 7/watu 7 ambao atawanyanyua kwa kipindi kimoja. Kumbuka mambo hayo hayajaandikwa kwenye biblia, yatakuwa ni mambo mapya kabisa, Kutakuwa na vitu vya kipekee kwa Bibi-arusi, na hiyo ndiyo itamletea Imani ya kwenda kwenye unyakuo…Kwa maelezo marefu kuhusu “ngurumo saba” bofya hapa⏩ NGURUMO SABA

Tukiendelea mbele Zaidi tunasoma..

Ufunuo 10:5 “Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni,

6 akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya; 

7 isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii”.

Sasa tukirudi pale, kwanini Mguu mmoja Bwana aliuweka juu ya nchi na mwingine juu ya Bahari…Ni kwasababu ya KIAPO kinachokwenda kufuata..

Katika hali za kawaida za desturi za kiulimwengu, watu wakienda mahakamani, wakitaka kutoa ushahidi au kuzungumza ukweli, sharti wasimame wima, hauwezi kuapa huku umekaa… na baada ya hapo, unanyoosha mkono wako mmoja wa kuume juu! Na kisha anaapa kusema ukweli…Kama ni kiongozi anaapishwa anakamata kile kitabu anachoapia na kukinyanyua juu na kuapa kupitia hicho.

Na hapa Bwana anakwenda kuapa! Na kuna vitu vitatu ambavyo wanadamu waliambiwa wasiape kabisa cha kwanza.1) MBINGU: kwasababu ndipo kiti cha Enzi cha Mungu kilipo 2) NCHI: kwasababu ndipo pa kuwekea miguu pa Mungu 3) KICHWA: kwasababu hatuwezi kuufanya unywele wetu kuwa mweupe au mweusi.

Mathayo 5:33 “Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;

34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;

35 wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.

36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi”

Lakini huyu Malaika Mkuu unaona anakiuka vyote hivyo…Kwanini? ni KWASABABU Kilichopo Mbinguni ndio kiti chake cha Enzi, hakuna aliye zaidi yake…Na pia anaapa kwa nchi kwasababu ndipo ilipo Miguu yake…Ndio maana unaona mguu mmoja upo juu ya Bahari na mwingine juu ya nchi. Na vilevile kuonyesha kuwa anamiliki vyote vilivyo chini ya nchi kuzimu(ambapo ni baharini) na juu ya nchi (ambapo ni duniani). Kwahiyo ni uthibitisho tosha kuwa huyo si mwingine Zaidi Ya MKUU WA UZIMA MWENYEWE YESU KRISTO, MUNGU MKUU.Haleluya!!…Na hapa anaapa kwa kusema kuwa…

“hapatakuwa na wakati baada ya haya; 7 isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii”

Hapatakuwa na wakati baada ya haya…anamaanisha kuwa, Dunia haitaendelea kuwepo tena baada ya hayo..isipokuwa katika siku za malaika wa saba atakapokuwa tayari kupita baragumu. Sasa kumbuka mpaka kufikia hapa Malaika wa saba alikuwa bado hajapiga baragumu lake..baragumu sita zimeshapita…Tutakuja kuona baragumu ya saba itapolia ni nini kitatokea…lakini kwa ufupi Baragumu la saba linahusiana na siku ya BWANA yenyewe. Ambapo hakuna tena muda.Mambo yote yatakuwa yamekwisha hakuna tena nyakati wala vipindi vya wanadamu…Utakuwa ni wakati wa kuanza majira mapya…

Kwahiyo huyu Malaika Mkuu anaapa ikimaanisha ni “hakika na ndivyo itakavyokuwa” kuwa hakutakuwa tena na muda wa nyongeza…Isipokuwa katika siku za malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu…Katika siku za Malaika wa saba kupiga baragumu hizo ndio siku za mwisho..hakutakuwa na baragumu la nane wala muhuri wa 8.

Lakini ukiendelea mbele kidogo inasema “7 isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii.”

Mwisho Malaika wa saba atakapopiga baragumu ndipo SIRI YA MUNGU itakapotimizwa. Ikiwa na maana kuwa hii siri ya Mungu bado haijatizizwa mpaka sasa…Maana yake bado yote haijafunuliwa…kuna sehemu haijatimizwa, na hiyo itatimizwa katika siku za Baragumu la malaika wa saba.. Sasa hapa biblia inasema ni SIRI itatimizwa…yaani ipo MOJA sio siri zitatimizwa kana kwamba zipo nyingi hapana.

Sasa hiyo SIRI ni IPI? Kwa ufupi SIRI HII ni YESU KRISTO..Yeye ndiye SIRI YA MUNGU

Wakolosai 1:26 “siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake;

 27 ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu”.

Sehemu ya kwanza ya siri hii ilifunuliwa ilifunuliwa kwetu sisi mataifa kwamba KRISTO YESU, yule Masihi aliyekuja hakuwa zawadi kwa wayahudi tu peke yao..bali hata kwetu sisi watu wa mataifa, kwasababu hiyo tukapata baraka kubwa sisi tuliokuwa hatustahili, hiyo ilikuwa ni SIRI iliyofichwa ndani ya YESU KRISTO, tunapokea uponyaji kwa Kupitia YESU Kristo, wafu wanafufuliwa, tunazungumza lugha mpya, tunawekea watu mikono wanapata afya nk. Tunahesabiwa kuwa uzao wa Ibrahimu. Mambo hayo ambayo zamani za agano la kale, yasingeingia akilini kwamba siku moja Masihi wanayemtarajia eti atawapa Uwezo wa kipekee namna hiyo watu wa mataifa, wasio hata wa uzao wa Ibrahimu kwahiyo hiyo ilikuwa ni siri na ilipokuja kufunuliwa iliwashangaza wengi sana.

Mtume Paulo aliiandika siri hiyo katika 

Waefeso 3:4 “Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo.

5 Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho;

6 ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili;

7 Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa.

Pia sehemu nyingine ya siri hiyo ambayo imefunuliwa kwetu ni kuwa YESU NDIO YEHOVA mwenyewe. Alipokuwepo duniani siri hiyo ilikuwa bado imefichwa miongoni wa wanadamu wote, wanamjua tu kama mwana wa Mungu mteule wa Mungu, lakini siku alipopaa na Roho Mtakatifu afumbuaye mafumbo aliposhuka juu ya mitume ndipo siri hiyo ikafichuka kumbe tulikuwa tunatembea na Mungu duniani pasipo sisi kujua. Mtume Paulo aliliweka wazi hilo na kusema..

1Timotheo 3:16 “Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.”

Unaona?…Kadhalika ipo sehemu nyingine ya Siri hii hii ya huyu mmoja ambayo bado haijatimia, mwishoni kabisa mwa wakati wa baragumu la saba ndio itakuwa imemalizika yote..Somo linalohusu SIRI YA MUNGU ni pana kidogo..unaweza ukalipata  kwa kubofya hapa ⏩ Siri ya Mungu.

Tukizidi kuendelea mbele tunasoma…

Ufunuo 10:8 “Na sauti ile niliyoisikia kutoka mbinguni ilinena nami tena, ikisema, Enenda, ukakitwae kile kitabu kilichofunguliwa katika mkono wa yule malaika, aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi.

9 Nikamwendea malaika yule nikamwambia kwamba anipe kile kitabu kidogo. Akaniambia, Kitwae, ukile, nacho kitakutia uchungu tumboni mwako, bali katika kinywa chako kitakuwa kitamu kama asali.

10 Nikakitwaa kile kitabu kidogo katika mkono wa malaika yule, nikakila; nacho kikawa kitamu kama asali kinywani mwangu, na nilipokwisha kukila tumbo langu likatiwa uchungu.

11 Wakaniambia, Imekupasa kutoa unabii tena juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi”.

Baada ya Malaika huyu Mkuu kuapa kwa sauti kuu, Yohana anaisikia tena ile sauti iliyomwambia asiandike zile ngurumo saba, ikimwambia akakitwae kile kitabu mkononi mwa yule malaika na akile, nacho kitakuwa kitabu kama asali kinywani bali tumboni kitakuwa kichungu.

Hapa Yohana anaambiwa akitwae akile, kwa namna ya kawaida huwezi kula kitabu, kwahiyo hilo ni ono, na kitabu hicho hakuambiwa akisome, hapana bali akile…kusoma ni tofauti na kula, mtu asomaye anaingiza taarifa katika Akili yake…lakini mtu alaye anaingiza taarifa au uzima ndani ya mwili wake…Kwasababu kile alichokila kinaingia katika tumbo lake kisha kinameng’enywa na kuingia katika damu na mfumo wa mwili mzima…baadaye kile alichokila kinageuka sehemu ya yeye kinageuka na kuwa nyama yake, misuli yake, Ngozi yake n.k…

Na sisi Neno la Mungu hatujapewa kulisoma tu au kulikariri  hapana! bali tumepewa tulile katika roho, ndio Maana Bwana anasema yeye ni “chakula cha uzima” ili kitakapoingia katika miili yetu ya roho kiwe ni sehemu yetu!..
Sasa hapa Yohana anaambiwa atwae akile, mfano ule ule wa  Nabii Ezekieli alioambiwa atwae GOMBO lile na kulila…

Ezekieli 2:8 Bali wewe, mwanadamu, sikia neno hili ninalokuambia; usiwe wewe mwenye kuasi kama nyumba ile yenye kuasi; funua kinywa chako, ule nikupacho. 9 Nami nilipotazama, mkono ulinyoshwa kunielekea; na tazama, gombo la chuo lilikuwa ndani yake.

10 Akalikunjua mbele yangu; nalo lilikuwa limeandikwa ndani na nje; ndani yake yalikuwa yameandikwa maombolezo, na vilio, na ole!Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha enenda ukaseme na wana wa Israeli.

Ezekieli 3: 1 “Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha enenda ukaseme na wana wa Israeli.

 2 Basi nikafunua kinywa changu, naye akanilisha lile gombo.

 3 Akaniambia, Mwanadamu, lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali.

 4 Akaniambia, Mwanadamu, haya! Waendee wana wa Israeli ukawaambie maneno yangu.”

Nabii Ezekieli alipewa alile lile gombo kabla ya kwenda kusema na Wana wa Israeli, gombo tafsiri yake ni KITABU. Kwahiyo Bwana alimpa Neema ya ufunuo wa kipekee juu ya maneno yake ili atakapokwenda kusema na wana wa Israeli na kuwaonya! Azungumze kitu anachokielewa na kinachotoka ndani yake..Na baada ya hapo tunamwona Ezekieli akipata nguvu ya ajabu katika kwenda kuwapa unabii wana wa Israeli waliohamishwa, utaona alikuwa ananguvu nyingi kiasi cha kuweza hata kustahimili ishara Mungu alizokuwa anampa, wakati mwingine alikuwa anaambia alale ubavu mmoja kwa siku 430 na ubavu wa pili kwa siku 40, sehemu nyingina anaambiwa ale kinyesi ili kuwa ishara kwa wana wa Israeli,sehemu nyingine Mungu anamuua mke wake aliyempenda, halafu anaambiwa asiomboleze bali avae nguo nzuri, awe kama mtu ambaye hana msiba wowote n.k .mambo hayo yote aliweza kuyafanya baada ya kulishwa hilo gombo..vinginevyo kwa hali ya kawaida asingeweza.

Kadhalika na Yohana hapa anapewa kile kitabu akile. Sasa Katika siku za Mwisho kutakuja uamsho wa mwisho, ambapo Roho Atamwagwa tena kama siku ile ya Pentekoste na kama ilivyotokea kule Mtaa wa Azusa, Marekani…Bibiarusi atapokea nguvu ya kwenda kutoa unabii kwa mataifa, lugha na jamaa wa dunia nzima..nguvu ya Roho Mtakatifu itamwezesha bibiarusi kufanyika ishara kwa dunia nzima kipindi kifupi kabla ya unyakuo, lakini ijapokuwa wengi wataona ishara za namna hizo lakini hawataamini. Kwahiyo Yohana katika hilo ono anamwakilisha bibiarusi wa Kristo atakavyokuja kupokea ufunuo katika siku za mwisho…Ingawa pia baada ya Yohana kutoka Patmo, alizunguka sehemu nyingi kutoa unabii kutimiza sehemu hii ya maandiko..lakini ufunuo halisi utakuja kutimia katika siku za mwisho ..

Je! Umempa Bwana Maisha yako?..Unaona ni kwa jinsi gani tunaishi katika muda wa kumalizia, Kristo yupo mlangoni, na hata kama huamini atakuja, basi fahamu kuwa hujui siku yako ya kufa, inaweza ikawa ni leo..Sasa huko utakapokwenda utakuwa mgeni wa nani ?..hukukaa kikao na yeyote cha kuamua wewe kuja duniani kadhalika hutakaa kikao na yeyote cha  kuamua ni lini utaondoka! Hukuja na kitu utaondoka bila kitu! Hivyo jitafakari Maisha yako yatakapoishia..Na kama umempa Bwana Maisha yako kumbuka maandiko yanasema “pasipo utakatifu hakuna mtu atakayemwona Mungu (Waebrania 12:14)je! Maisha yako yanastahili wokovu?.

Kama hujajiweka sana, na kujiandaa huu ndio muda wa kufanya hivyo haraka bila kuchelewa, tubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kutokuzifanya tena, na kisha katafute ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako kulingana na Matendo 2:38, na kisha Bwana atakuzawadia nguvu ya kushinda dhambi (Roho wake Mtakatifu). Na yeye ndiye atakayekutia MUHURI mpaka siku ya ukombozi wako Katika huyo utakuwa na uhakika wa kwenda mbinguni.

Usikose mwendelezo huu w asura zinazofuata.

Shalom! Maran atha! Kwa Mwendelezo >>>Ufunuo: Mlango wa 11

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312,jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana.

SIRI YA MUNGU

MJUE SANA YESU KRISTO.


Rudi Nyumbani

Print this post

RAHABU.

Shalom mtu wa Mungu, Karibu tujifunze Neno la Mungu ambalo hilo ndilo linalotufanya tuishi mpaka sasa hivi mimi na wewe.

Leo, tutajifunza Juu ya huyu mwanamke anayeitwa Rahabu wengi wetu tunaifahamu historia yake, ni mwanamke aliyekuwa kahaba katika nchi ile ya Yeriko, kipindi kile wana wa Israel wanatoka Misri kuelekea nchi ya ahadi, Ikumbukwe kuwa mji wa Yeriko ulikuwa mji uliosifika sana wakati ule katika ukanda wote wa Jordani, kwa utajiri, wa kifedha, kilimo, na hata wa kijeshi, embu fikiria enzi zile tayari mji wote ulikuwa umeshazungushiwa ukuta, jambo ambalo hata sasa hivi nchi nyingi hata kama ni ndogo kiasi gani hazijafikia hiyo hatua.

Leo hii tunaona ni sehemu ndogo tu ya Taifa la China imeweka ukuta na imewekwa katika maajabu ya dunia, Jeriko leo hii ingekuwapo, tungeiweka wapi?..Ukuta ule ulikuwa mkubwa kiasi cha kuruhusu magari ya farasi kupita juu yake na watu kujenga nyumba zao kando kando mwa kuta zile. Na zaidi ya yote watu waliokuwepo kule walikuwa ni majitu kweli kweli watu hodari wa vita..Kwahiyo kulikuwa hakuna namna yoyote mji huu usiogopwe na mataifa mengine.

Sasa huyu mwanamke naye alikuwa akiishi ndani ya mji huu, akifanya kazi zake za ukahaba,lakini ndani yake kulikuwa ni kitu kingine tofauti ambacho kilimfanya asiangamie pamoja na mji ule na zaidi ya yote alihesabiwa miongoni mwa wana wa Israeli, na kama hiyo haitoshi aliingizwa katika uzao ya kifalme, wa simba wa Yuda, wa Bwana wetu Yesu Kristo.Mfalme Mkuu Haleluya!!.

Ni siri kubwa sana imelala hapo, na hiyo inatuhusu kwa sehemu kubwa sisi kama kanisa la Kristo, watu wa mataifa katika nyakati hizi za mwisho tunazoishi.

Sasa tukimchunguza Rahabu, utaona ni mtu ambaye aliyaweka moyoni sana yale mambo ambayo Mungu alikuwa anawafanyia wana wa Israeli kule Misri Miaka 40 iliyopita na shuhuda zote alizokuwa anawafanyia kule jangwani..Na hiyo ilimfanya aamini kabisa kuwa ufalme wao ni lazima uje kuangushwa tu siku moja na ndio maana utaona makazi yake aliyaweka ukingoni kabisa mwa mji, na sio katikati ya mji.

Yoshua 2:9 “akawaambia wale wanaume, Mimi najua ya kuwa Bwana amewapa ninyi nchi hii, na ya kuwa hofu imetuangukia mbele yenu, na ya kuwa wenyeji wote wa nchi wanayeyuka mbele yenu.

10 Maana tumesikia jinsi Bwana alivyoyakausha maji ya bahari ya Shamu mbele yenu, hapo mlipotoka Misri, tena mambo hayo mliyowatendea wafalme wawili wa Waamori waliokuwa huko ng’ambo ya Yordani, yaani, Sihoni na Ogu, mliowaangamiza kabisa.

11 Na mara tuliposikia hayo mioyo yetu iliyeyuka, wala haukusalia ujasiri wo wote katika mtu awaye yote, kwa sababu yenu; kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu, katika mbingu juu na katika nchi chini.”

Hivyo utaona sasa wakati ule ulipofika wa wale wapepelezi kuingia katika nchi yeye ndiye aliyewakaribisha nyumbani kwake, na kuwaficha darini pale wenyeji wa nchi walipokuja kuwaulizia kwake, aliwaambia wameshaondoka kwake hivyo wawafuatie nje ya mji, ndipo baadaye baada ya wenyeji kuondoka akawashusha kwenye ukuta kwa kupitia dirisha la nyumba yake,

Lakini wale wapepelezi kabla hawajaondoka walimpa masharti matatu, ya kuzingati ndani ya siku chache zilizobakia kabla ya uharibifu kuanza, walimwambia:

1) Habari ile isijulikane na mtu mwingine yoyote isipokuwa yeye na familia yake tu.

2) Wafunge kamba ile nyekundu dirishani mwao ili siku ile watakapokuja kuuteketeza mji wawatambue.

3) Mtu yeyote asitoke nje ya malango:

Na kama tunavyosoma habari wana wa Israeli walipovuka tu Yordani, kuuzunguka ule mji, na baadaye kuanza vita, wale wapepelezi wawili wakamfuata Rahabu nyumbani kwake, na kumwondoa ndani yeye pamoja na ndugu zake wote, wakaweleta kambini walipokuwa wayahudi wengine wote kisha mji wote ukatetekezwa kwa moto hakukusalia kiumbe chochote kilicho hai.

Habari hii inatupa picha ya mambo yanayoendelea rohoni katika hizi siku za mwisho, Rahabu anawakilisha kanisa la Kristo (Bibi-arusi wa kweli) ambaye ameokolewa katika dhambi za uasherati wa kiroho unaondelea sasa hivi duniani.

Na cha kushangaza leo hii hakuna mtu yoyote asiyefahamu kuwa Kristo yupo mlangoni kurudi, na atakaporudi ulimwengu huu wote utateketezwa sawasawa na alivyoahidi hata ukimuuliza mtu asiye mkristo atakwambia nafahamu hilo. shuhuda zake tumezisikia tangu miaka 2000 iliyopita lakini bado watu wanaendelea kufanya maovu wakijifariji kwa kuta za dhambi walizojiwekea..Dalili zote zinaonyesha tunaishi katika kizazi ambacho kitashuhudia kurudi kwa pili kwa Kristo lakini watu bado wanafumba macho yao wasione hayo kama tu vile watu wa Yeriko walivyokuwa..

Lakini Rahabu japo alikuwa katika mji ule mwovu aliijenga nyumba yake ukingoni kabisa mwa mji, kuonyesha kuwa akili zake na mawazo yake yote yalikuwa nje! Kutazama mbali kinachokuja..Ndivyo walivyo wakristo wachache sana wa Bwana Yesu leo, japo wanaishi ulimwenguni lakini wapo ukingoni kabisa mwa ulimwengu, hawajichanganyi na uovu unaoendelea duniani mpaka kumsahau Mungu na ufalme wake ambao upo karibuni kutokea..Sikuzote mtu ukiwa katikati ya mji huwezi kuona au kujua yanayoendelea nje ya mji, ndivyo ilivyo kwa kundi kubwa la watu sasa, hawaoni kuwa Kristo yupo nje ya kuta zetu ni PARAPANDA TU! Inasubiriwa ilie wema waondoshwe waangamizi yaanze.

Tunaona pia Rahabu alipewa maagizo matatu, moja wapo, ni ile kamba nyekundu: Kuonyesha kuwa kitakachomwokoa mtu, ni agano lililokatika damu ya Yesu, na si kingine chochote, njia ni moja tu ya kumfikia Mungu, ikiwa humwamini Kristo leo huku unatumai uokoke kwa njia nyingine..utaangamia tu.Ni heri leo ukaitii injili uokolewe.

Pili aliambiwa mtu yoyote asitoke nje ya malango ya nyumba yako, atakayetoka hata kama ni ndugu yako damu yake itakuwa juu yake mwenyewe: Hii inafunua wale ambao wapo vuguvugu, katika siku hizi za mwisho ukiamua kumfuata Yesu mfuate kweli kweli, hakuna nafasi ya kuingia na kutoka, aidha aumue kuwa nje moja kwa moja, au ndani moja kwa moja…. vinginevyo utafananishwa na ule mfano Bwana Yesu aliousema wa mke wa Lutu. Na inasikitisha kuwa lipo kundi la wakristo (ambalo biblia inaliita pia wanawali wapumbavu (Mathayo 25)) watakao kosa unyakuo kwa tabia hizo za kutojali mambo ya muhimu ya wokovu. Na hao watabaki hapa kuingia katika ile dhiki kuu..Ndugu ni wakati wa kuchagua ni wapi unasimama leo?.

Tatu, waliambiwa habari zile asizifahamu mtu yoyote isipokuwa wana familia tu: Nataka nikuambie Jeriko ilipewa muda mrefu wa kutubu na kujisalimisha, miaka yote 40 Mungu aliyokuwa anawazungusha wana wa Israeli jangwani ulikuwa ni muda wa Taifa la Yeriko kutubu, na mataifa mengine yaliyokuwa Kaanani, walionyeshwa kwa vitendo jinsi Misri ilivyopigwa ndivyo watakavyokuja kupigwa na wao, lakini kama Taifa hawakutaka kusikia isipokuwa mtu mmoja tu aliyeitwa Rahabu, sasa siku wapepelezi walipokuja walimfunulia mipango yao na kumwambia asimwambie mtu yoyote isipokuwa wana familia tu!, Hii ni aina ya injili mpya ambayo alihubiriwa Rahabu yeye peke yake, na hiyo si injili ya kuambiwa atubu bali ni injili ya maagizo ya kujiokoa nafsi yako.

Halikadhalika, wakati huu ambao watu wengi wanaipuuzia injili itafika wakati Mungu ataanza kusema ni lile kundi tu ambalo limeshajiweka tayari..Hapa ndipo Mungu atakapoizidisha imani ya watu wake wawezi kunyakuliwa (watakuwa wanapewa maagizo fulani fulani)…Na ghafla tu ulimwengu utashangaa hao watu hawapo..kumbe siku nyingi tayari wapo mbinguni katika karamu ya mwanakondoo lakini wale waliosalia, ni dhiki na shida na ghadhabu ya Mungu inawahusu.

Na mwisho tunamwona Rahabu hakuwa mwanamke wa kiyahudi lakini aliingizwa kwa nguvu katika uzao wa kifalme wa Yesu Kristo Bwana wetu, mambo ambayo hata wayahudi wengi wa wazao ya Ibrahimu walikosa neema hiyo soma (Mathayo 1:5).

Vivyo hivyo na wewe leo hii ukiamua kutubu dhambi zako katika hizi siku chache zilizobakia kabla ya unyakuo, basi moja kwa moja utaingizwa katika mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, wa Yesu Kristo BWANA wetu. (1Petro 2:9). Usijiangalia kwasasa wewe ni mchafu kiasi gani, Rahabu alikuwa ni mchafu kuliko watu wengi wa Yeriko.

Ni rahisi tu kuingia katika huu ufalme! Tubu kwa kumaanisha kumwishia Bwana Yesu na kudhamiria kuacha dhambi, pili kabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa kwenye maji mengi katika jina la YESU KRISTO, na Mungu mwenyewe atakupa Roho wake atakayekusaidia kushinda dhambi na kukuongoza katika kuijua kweli yote mpaka siku ya UNYAKUO.

Ubarikiwe sana.

Tafadhali “Share” Ujumbe huu na kwa wengine.Na Mungu atakubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

UNYAKUO.

SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!

KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA…TUBU UMGEUKIE MUNGU

 EPUKA MUHURI WA SHETANI


Rudi Nyumbani

Print this post

IMANI NI KAMA MOTO.


Habari ya uzima wako mtu wa Mungu, Nakukaribisha tuzitafute kwa pamoja Tunu za rohoni (Neno la Mungu) Sabuni ya kweli ya roho zetu..

Leo tutaangazia siri mojawapo ya Imani ambayo tukiijua basi hatutaogopa jambo lolote liwe kubwa au dogo mbele yetu. Kama kichwa cha somo kinavyosema “Imani ni kama Moto”, Hii Ikiwa na maana tukiujua ufunuo ulio katika moto basi hatutaogopa ukubwa wa kichaka au msitu ulio mbele yetu, Embu jaribu kufikiria Leo unapokwenda katika mbuga za wanyama marufuku ya kwanza unayopewa kule ni “hakuna kuvuta sigara mbugani”, ni kwasababu gani, ni kwasababu wanajua ule moto kidogo, uliopo juu ya kile kipande cha sigara kinaweza kuleta madhara makubwa sana. Hata wewe leo hii hii ukapewa kiberiti na mbele yako zikapangwa kuni kama mlima, ni wazi kuwa huwezi kuugopa wingi ule wa Kuni kwasababu unajua ufunuo ulio katika moto.

Kwamba Moto kidogo tu unatosha kumaliza kila kitu, una tabia ya kukua na kuongezeka kulingana na ukubwa wa shuhuli yenyewe, kama ni kuunguza karatasi, utakuwa ukubwa wa kulingana na karatasi, kama ni kuunguza mbuyu utakuwa kulingana na saizi ya mbuyu kama ni kuunguza msitu vile vile utakuwa mkubwa sana kulingana na saizi ya msitu wenyewe..Lakini chanzo chake kilikuwa ni kitu kidogo sana yaani njiti moja tu ya kiberiti.

Na ndivyo ilivyo Imani,.. Imani inatabia ya kukua kulingana na ukubwa wa jambo, lakini inaanza kama chembe ya haradali, Usitazamie mpaka uwe na imani kubwa kama bomu la atomiki ndio utaweza kutatua tatizo Fulani kubwa, ukiwa na mtazamo huo basi uwe na uhakika kuwa utakwama tu, hicho kiwango hutakaa ukifikie, ni sawa na mtu ambaye anajaribu kupakia moto mwingi kwenye mashehena ili aende kuumwaga kwenye msitu ili uwake?, tengeneza picha mtu huyu kwanza atawezaje wezaje kuukusanya moto pamoja, kwasababu moto ni kitu kisichoweza kushikika, wala kukusanyika. Ndivyo ilivyo Imani usijaribu kuichanga imani iwe nyingi ili siku moja ujaribu kufanya jambo Fulani utakwama tu.

Sasa embu tutazame kisa kimoja katika Biblia ambacho na sisi tunaweza kujifunza Jambo ndani yake kuhusu somo hili. Zamani za waamuzi, wana wa Israeli wapomlilia Mungu awepe mfalme kama watu wa Mataifa mengine walivyo na wafalme..Mungu alisikia kilio chao na kuwapa mfalme mmoja aliyeitwa Sauli. Sasa huyu Sauli biblia inasema alikuwa ni mtu shujaa sana, mtu ambaye Mungu alimvika ujasiri mwingi katika vita..Na yeye alikuwa na mtoto wake kipenzi aliyeitwa Yonathani, wote hawa walikuwa mashujaa kweli walipigana vita vingi sana na Mungu kuwapa ushindi mkuu lakini ilifika wakati wafilisti waliwazingira, mambo yalikuwa magumu kweli kwa Israeli.

Wafilisti waliwapandia na jeshi lao lote, pamoja na magari mengi sana ya vita, na watu wasioweza kuhesabika kama mchanga wa baharini ili kupigana nao. Hivyo Israeli walipoona vile, walivunjika moyo sana, biblia inasema ndipo watu wakaanza kwenda kujificha katika mapango, na katika vichaka, na katika miamba, na katika mashimo, na katika mabirika. (1Samweli 13:6). Na wengine wakawa wakimbizi katika nchi jirani, Ndipo watu wengi wakamfuata Sauli kwa kutetemeka waone atachukua uamuzi gani, Sauli kuona vile akautafuta Uso wa Mungu kwa Samweli lakini Samweli hakuja kwa wakati alioutarajia, ndipo watu wengi wakamkimbia kwenda mbali kabisa na Israeli.. Maana jeshi lile lilivyokuwa kubwa walijua kabisa kulikuwa hakuna kupona mtu..si mfalme wala mtumwa.

Na kibaya zaidi hakukuwa na mtu hata mmoja aliyekuwa na Panga wala mkuki isipokuwa Sauli tu na Yonathani mtoto wake, kwani kipindi kile walikuwa wanawategemea sana wafilisti kama wahunzi wao wa kuwatengenezea silaha sasa, wahunzi wao ndio wamekuwa maadui zao, unaona hiyo ni shida mara dufu.. Jaribu kutengeneza picha labda Nigeria inakuja kupigana na Tanzania, na hakuna mwanajeshi hata mmoja mwenye silaha,isipokuwa raisi tu na mtoto wake, na unaambiwa wameshavuka Kagera wanashuka, hata kama ni wewe lazima hofu itakuingia na kikubwa utakachofanya ni kuondoka kukimbilia Kenya au nchi jirani unusuru roho yako na familia yako au kujificha. Ndivyo ilivyokuwa kwa Israeli kipindi hicho.

Lakini ilifikia sikumoja Yonathani akasema moyoni mwake ninachoogopea ni nini, akamwamini Mungu, akakusudia kuondoka kuwafuata mamilioni ya wafilisti akiwa yeye peke yake pamoja na mtumwa wake bila kumwambia mtu yoyote, hata baba yake hakumweleza..hapo ndipo Imani kama njiti ilipoanza kutenda kazi, kwenda kuchoma msitu…wakati mwingine ukikusudia kufanya kitendo cha Imani, usimshirikishe kila mtu, utakutana na vipingamizi visivyokuwa na sababu..

Tunasoma hayo katika:

1Samweli 14:6 “Basi, Yonathani akamwambia yule kijana aliyemchukulia silaha zake, Haya! Na twende tukawavukie ngomeni hao wasiotahiriwa; yamkini Bwana atatutendea kazi; kwa maana hakuna la kumzuia Bwana asiokoe, kwamba ni kwa wengi au kwamba ni kwa wachache.”

Yonathani hakusubiri Maono kutoka kwa Samweli ndio atende jambo, hakusubiri aote ndoto ndipo afanye jambo, hakungojea wapate msaada wa kijeshi kutoka nchi za jirani wapate jeshi la kutosha ndio Imani ya kupambana nao ije, hapana yeye aliifahamu siri ya Imani.

Na alipofika mbeleni alikutana kweli na jeshi la wafilisti, Yonathani na mwenzake wakasema tusimame hapa ikiwa watatuita tuwafuate kule walipo basi hiyo ni ishara tosha ya kuwa Mungu yupo upande wetu tuwamalize, na kweli walipowafikia pale wakawaambia pandeni huku, ndipo walipojua kuwa hawa ndio nyama yetu, walipanda kule juu sio kwa woga woga, bali walipanda kwa ujasiri na kwa kasi kama wanyama, kwa mikono yao na miguu yao..na walipofika pale ndani ya eneo dogo sana Yonathani aliwaua mashujaa 20 kwa mpigo,huku Yule kijakazi wake akiwamalizia, na pale pale kukatokea tetemeko kubwa lisilo la kawaida, wale wafilisti waliokuwa kwenye makambi, na wale waliokuwa wanaendelea kuteka nyara wakaogopa sana, mpaka nchi nayo ikatetemeka kwa Imani ile.. watu wakaanza kukimbia hovyo hovyo kama vichaa,..

Hadi huku nyuma Sauli alipokuwa amejificha na mashujaa wake, wakashangaa kelele zile zinatokea wapi, kuona vile wakanyanyuka na wao kushuka vitani, na kule vitani sasa cha ajabu ni kuwa upanga wa kila mmoja ukawa juu ya mwenzake, wakauana wafilisti wengi sana…na kulikuwa na baadhi ya wayahudi ambao Wafilisti waliwateka nyara na siku ile ya vita walishuka nao wawasaidie vitani, lakini walipoona wokovu unarudi kwao nao pia wakawageuka wakaanza kuwaua…Unaona jinsi imani kama moto inavyokuwa kulingana na ukubwa wa tatizo..

Hivyo nguvu ikazidi kuongezeka sana, hata na wale waisraeli wengine waliokuwa wamejificha mashimoni, na vichakani nao pia wakapata nguvu wakajitokezeka kuendeleza mapigo..Hiyo yote ni matunda ya imani ya mtu mmoja tu Yonathani. Siku hiyo wakapata ushindi mnono sana, kutoka kwa Mungu..(hapo nimeeleza kwa ufupi tu Kwa muda wako binafsi unaweza ukasoma habari yote 1Samweli 13&14,.)

Lakini nataka uone ni jinsi gani Imani inavyotenda kazi, Leo hii unapofikiria kumtumikia Mungu, usiangalie kanisa liko wapi,?, usiangalie ni watu wangapi wananisapoti, nina fedha kiasi gani za kuhubiri, ukifikiria hivyo ndugu hutafika popote, hapo ulipo anza, kitaonekana ni kidogo, lakini fahamu kuwa imani umbo lake sikuzote ni kama chembe ya haradali, lakini matokeo yake ni milima mikubwa..Na hiyo imani ipo ndani ya kila mmoja..

Vile vile na katika mambo yako mwenyewe binafsi, usifikirie labda ugonjwa huu hautibiki, au jeraha hili haliponyeki, mimi nimezaliwa katika ulemavu tangu utotoni siwezi kurudia katika hali yangu ya kawaida, nataka nikuambie Amini, tu kama unavyouamini moto..Tatizo lote litayeyuka kama utaendelea kudumu katika kumwamini YESU Mponyaji wetu.

Na pia katika kazi zako na shughuli zako binafsi, usiogope kidogo unachoanza nacho, ukiwa na imani huku ukiwa mwaminifu kwa hicho unachokifanya unatenda haki, hayo ni matendo ya imani, Mungu atakikuza na kuwa kikubwa..na kufunika vya wengine wote, ikiwa tu utafanya kwa uaminifu huku unamcha Mungu.

Bwana akubariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

NI NANI ALIYEIDHARAU SIKU YA MAMBO MADOGO?

MCHE MWORORO.

NGUVU YA MUNGU YA UUMBAJI

SAYUNI NI NINI?

TIMAZI NI NINI


Rudi Nyumbani

Print this post

NAMNA GANI NITAPOKEA NGUVU ZA BWANA YESU?.

Shalom. Jina la Bwana wa Utukufu Yesu Kristo, libarikiwe.Biblia inasema katika kitabu cha Marko..

Marko 5:21 ‘Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ng’ambo katika kile chombo, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari.

22 Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi, jina lake Yairo; hata alipomwona, akaanguka miguuni pake,

23 akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yu katika kufa; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishiAkaenda pamoja naye; mkutano mkuu wakamfuata, wakimsonga-songa.

24 Akaenda pamoja naye; mkutano mkuu wakamfuata, wakimsonga-songa.

25 Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili,

26 na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya

27 aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake;

28 maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona

29 Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule.

30 Mara Yesu, hali akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu?

31 Wanafunzi wake wakamwambia, Je! Wawaona makutano wanavyokusonga-songa, nawe wasema, Ni nani aliyenigusa?

32 Akatazama pande zote ili amwone yule aliyelitenda neno hilo.

33 Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote.

34 Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.

Katika mfano huu, tunaona Bwana Yesu akitokwa na Nguvu, lakini wengi wanafahamu kuwa nguvu hizo zilikuwa ni za mwili…na hata mimi nilikuwa nafahamu hivyo mwanzoni…kwamba yule mwanamke alipomgusa tu Bwana, Basi Bwana alihisi kuna udhaifu Fulani umeingia mwilini mwake..mfano wa mtu aliyekuwa amelima hekari 10 za shamba na nguvu kumpungukia na kukaa chini…Lakini tafsiri hiyo si kweli..Nguvu zilizomtoka Bwana ni nguvu za Rohoni ..Yaani nguvu za uponyaji. Na hazikutoka na kumwendea tu yule mwanamke aliyekuwa anatokwa na damu..bali zilikuwa zinatoka na kuwaendea watu wote waliokuwa wanamwendea waponywe.

Sasa hizo nguvu kwa ufupi kama tulivyosema ni nguvu za uponyaji…Na kama umegundua nguvu hizo, mtu anaweza kuzitwaa kutoka kwake Bwana pasipo hata idhini ya Bwana mwenyewe, kama huyu mwanamke alivyofanya…hakumwambia wala kumwomba Bwana amponye, wala hakuwa mfuasi wa Bwana Yesu…lakini aliutwaa uponyaji wake pasipo hata kumshirikisha Bwana…na pia Bwana mwenyewe anaweza kumpa mtu kwa idhini yake mwenyewe kama huyo mkuu wa Sinagogi alivyomtaka Bwana akamwekee mkono binti yake..Ni nguvu zile zile zilizomtoka Bwana na kumponya yule mwanamke ndio hizo hizo ambazo zilikwenda kumfufua yule binti wa Mkuu wa sinagogi…zote ni nguvu zilizotoka ndani ya Bwana.

Tukiendelea na mstari wa 35, tunaweza tukaona jambo hilo..

Marko 5:35 ‘’Hata alipokuwa katika kunena, wakaja watu kutoka kwa yule mkuu wa sinagogi, wakisema, Binti yako amekwisha kufa; kwani kuzidi kumsumbua mwalimu?

36 Lakini Yesu, alipolisikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sinagogi, Usiogope, amini tu.

37 Wala hakumruhusu mtu afuatane naye, ila Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye Yakobo.

38 Wakafika nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akaona ghasia, na watu wakilia, wakifanya maombolezo makuu.

39 Alipokwisha kuingia, akawaambia, Mbona mnafanya ghasia na kulia? Kijana hakufa, bali amelala tu.

40 Wakamcheka sana. Naye alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa babaye yule kijana na mamaye, na wale walio pamoja naye, akaingia ndani alimokuwamo yule kijana.

41 Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka.

42 Mara akasimama yule kijana, akaenda; maana alikuwa amepata umri wa miaka kumi na miwili. Mara wakashangaa mshangao mkuu.

43 Akawaonya sana, mtu asijue habari ile; akaamuru apewe chakula’’.

Hata sasa Bwana hajaishiwa nguvu…bado zinaendelea kutoka, na tunaweza kuzitwaa kwake pasipo hata idhini yake, na hapo kinachohitajika ni Imani tu!. Wengi wanajua mpaka upokee uponyaji Fulani inahitaji umjue sana Mungu, uwe kwenye maombi ya muda mrefu ya kufunga na kuomba..hapana Mungu hayupo hivyo kabisa….

Wakati mwingine ndio maana hata watu wasio waKristo, ambao hata hawaielewi Imani ya Kikristo, ni rahisi kupokea uponyaji kwa Yesu kuliko hata wakristo, Unajua ni kwanini?…Ni kwasababu hiyo hiyo, kupokea nguvu kutoka kwa Bwana haihitaji wewe umjue sana, formula yake ni ndogo sana! Kugusa pindo lake kwa Imani tu!..Na watu wengi wasio wa Kristo ndio wanapokeaga uponyaji wao kwa njia hiyo..wanamgusa upindo tu na wanavuta nguvu za Mungu ndani yao..Sasa sio kwamba ukiponywa na Mungu ndio upo sawa na Mungu, hapana! Hivyo ni vitu vingine, hapa tunazungumzia habari ya uponyaji.

Kadhalika na sasa, usingoje Umjue Bwana Zaidi ndio unufaike kutoka kwake,! Hapana bali hata katika hiyo hali yako ya kikristo, Mguse Bwana katika pindo lake upokee Neema za kumjua yeye Zaidi, mguse upindo wa vazi lake Upokee Roho Mtakatifu Zaidi, Mguse Upindo wa vazi lake upokee nguvu za kumwabudu yeye Zaidi na za kumwimbia, na za kuwahubiria wengine habari njema, mguse pindo lake akuongezee hekima…Hizo nguvu zipo, haihitaji umfahamu sana..ni Kuamini tu kwamba ukimwomba atakupa!!..na atakapokupa ndio itakuwa mwanzo wa wewe kumjua Zaidi…Na hivyo unamwendea kwa imani na kumwambia Bwana, leo hii nataka niwe chombo chako kiteule, nifinyange na kunitengeneza.

Baada ya kuomba hivyo hapo hapo anza kuishi Maisha yanayolingana na ulichomwomba, baada ya muda mfupi utaona mabadiliko makubwa kwenye Maisha yako, yote uliyomwomba utakuwa umeyapata.

Bwana akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

UPONYAJI WA YESU.

MADHAIFU

KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.

UMEFUNULIWA AKILI?

IPO NGUVU ITUVUTAYO KWA KRISTO, ITHAMINI!.


Rudi Nyumbani:

Print this post

SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?

Baada ya wana wa Israeli kutoka Misri na kuingia katika nchi yao ya ahadi Mungu aliwaagiza wazishike zile sikukuu 7 muhimu kama sikukuu za Bwana katika vizazi vyao vyote,.Kwa maelezo marefu juu ya Sikukuu hizi unaweza ukazisoma katika kitabu cha Mambo ya walawi mlango wa 23 wote, Na sikukuu zenyewe ndio hizi:

1) Sikukuu ya Pasaka:

2) Sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu:

3) Sikukuu ya Malimbuko(mzao wa kwanza):

4) Sikukuu ya majuma(Mavuno):

5) Sikukuu ya Baragumu/Tarumbeta:

6) Sikukuu ya upatanisho:

7) Sikukuu ya vibanda:

Sasa embu tuzichambue hizi kwa ufupi na tuone ni jinsi gani zinaweza kuwa na maana katika majira yetu tunayoishi sasa.

SIKUKUU YA PASAKA ni moja ya sikukuu zile tatu za kwanza zilizofuatana.Yaani ilikuwa ikitoka hii inafuata hii, ni sikukuu zilizotimia ndani ya juma moja tu(yaani wiki moja). Mungu aliwaambia wana wa Israeli kila ifikapo tarehe 14 ya mwezi wa kwanza kwa kalenda yao ya kiyahudi ambayo kwetu sisi inaangukia katikati ya mwezi tatu na wa wanne, Siku hiyo waliagizwa na Mungu waishike siku hiyo kama sikukuu ya pasaka, yaani katika siku hiyo wakati wa jioni watamchinja kondoo mume (ambaye ndio pasaka mwenyewe), kisha watamla wote usiku ule ule bila kusaza, wakiwa wamevaa viatu vyao miguuni na mikanda yao viunoni. Na ikitokea wamesaza basi mtu hataruhusiwa kumla siku inayofuata kama kiporo bali atachomwa moto wote ateketee. Mungu aliwaambia wafanye hivyo kila mwaka kama kumbukumbu lao la siku ile Bwana aliyowatoa Misri na kuwaagiza wamchinje yule Pasaka usiku ule kabla Farao kuwaachia waende zao, Siku ile ilikuwa ni ya tarehe 14 ya mwezi wao wa kwanza, ndio siku ambayo damu ya mwanakondoo Yule iliyochukuliwa na kupakwa kwenye vizingiti na miimo ya milango yao, ili malaika Yule wa mauti atakapopita asiwadhuru wazaliwa wa kwanza wa kiyahudi.

Hii inafunua usiku ule wa Bwana Yesu kabla kusulibiwa kwake alipoketi na wanafunzi wake ili kuila pasaka ile, Lakini yeye hakuila bali aliwapa wanafunzi wake divai ile na kuwaambia wanywe kama kumbukumbu la damu yake itakayokwenda kumwagika kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote.

Hivyo ashukuruwe Mungu sisi tuliompokea tumepita kutoka mautini kwenda uzimani, hatuna hati ya hukumu juu yetu, Siku ile Bwana atakapoanza kuangamiza na kuuhukumu ulimwengu wote sisi tutakuwa sehemu salama tumefichwa kwasababu pasaka wetu alishachinjwa kwa ajili yetu..Na kuonyesha jinsi matukio yalivyolandana siku hiyo ambayo Bwana anayasema hayo maneno kwa wanafunzi wake ilikuwa ni siku hiyo hiyo ya tarehe 14 ya mwezi wa Kwanza. Hakuna shaka yeye ndiye Pasaka, Haleluya?

Sikukuu inayofuata ilikuwa ni SIKUKUU YA MIKATE ISIYOTIWA CHACHU, hii ilianza moja kwa moja siku iliyofuata, Wana wa Israeli waliagizwa, wale mikate isiyotiwa chachu kwa muda wa siku 7 yaani kuanzia tarehe 15 ya mwezi ule ule wa kwanza, na mtu yeyote ambaye alionekana akila mikate iliyotiwa chachu (yaani hamira) mtu huyo aliuliwa bila huruma.

Walawi 23:6 “Na siku ya kumi na tano ya mwezi ule ule ni sikukuu kwa Bwana ya mkate usiotiwa chachu; mtaila mikate isiyochachwa muda wa siku saba.

7 Siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu msifanye kazi yo yote ya utumishi.

8 Lakini mtasongeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto siku saba; siku ya saba ni kusanyiko takatifu; msifanye kazi yo yote ya utumishi.”

Hii ikifunua Neno la Mungu lisiloweza kugoshiwa, kumbuka usiku ule ule Bwana Yesu alitwaa mkate na na kusema, huu ndio mwili wangu utolewao kwa ajili yenu uleni..Hata sasa sisi tuliookolewa tunaula mwili wa Kristo kila siku, ili tuwe na uzima ndani yetu. Yeye alisema asiyekula mwili wangu hana uzima ndani yake.(Yohana 6:53) Na mwili wa Kristo ni Neno lake lisiloweza kugoshiwa na mafundisho ya uongo(Chachu), ambao watoto wa Mungu wanakula.. Yesu ndiye mkate wa uzima kweli kweli, mikate mingine yote inayodai kutoa tumaini la baadaye ni mikate iliyotiwa chachu ambayo haiwezi kumpeleka mtu popote.. Mpaka hapo nadhani unaona ni jinsi gani hizi sikukuu zilivyokuwa na maana kwetu sisi wa agano jipya, zinafunua picha halisi ya mambo yatakayokuja kuendelea katika siku za neema.

Sikukuu iliyofuata waliyogizwa waishike ni sikukuu ya (MALIMBUKO)MZAO WA KWANZA: Ni sikukuu ambayo Mungu aliwaagiza waisraeli wote waishike kama kuonyesha shukrani na Heshima kwa Mungu, kwa Baraka Mungu alizowapa za mavuno ya kwanza na hiyo inaambata na kupeleka sehemu ya kwanza katika mavuno yao. Na hii inafanyika siku ya pili baada ya Sabato, yaani jumapili, kumbuka hizi zote zinafanyika ndani ya wiki hiyo hiyo moja.(Walawi 23:9-14). Waisraeli waligizwa hivyo lakini lakini hawakajua mambo hayo yanafunua nini rohoni katika wakati wetu.

Sisi tuliopo sasa ndio tunakuja kujua kuwa baada ya Kristo kukaa siku tatu kaburini, jumapili alfajiri, siku ya kwanza ya juma alifufuka,katika sikukuu hiyo hiyo ya malimbuko ya wayahudi kama mzaliwa wa kwanza katika ya wafu, na vilevile kama mzaliwa wa Kwanza katika ya ndugu wengi.. Kristo ndiye limbuko letu Haleluya..Yeye alikuwa wakwanza kufufuka hivyo na wote waliolala katika Bwana watafufuka na kuwa kama yeye baadaye.

Kisha baada ya sikukuu hiyo kupita Mungu aliwaagiza tena wana wa Israeli wahesabu majuma 7 saba, au sabato 7 kuanzia hiyo siku ya malimbuko ambazo zitakuwa ni siku 49, na itakapofika ile siku ya 50 itakuwa ni Sikukuu ya Mavuno(Au sikukuu ya majuma), Dhumuni kubwa la sikukuu hii ni kumshukuru Mungu kwa ajili ya mavuno ya mwisho. Na Kufunga wakati wa mavuno

Hii inatufunua moja kwa moja, mara baada ya Bwana wetu Yesu Kristo kufufuka siku ile ya jumapili alfajiri aliwaambia wanafunzi wake wasiondoke Yerusalemu mpaka watakapoipokea ile ahadi ya Baba, Na kama tunavyosoma biblia ilipofika siku ile ya Pentokoste, Mungu aliwamwagia kipawa cha Roho Mtakatifu, Sasa hii siku ya Pentekoste ndio kwa jina lingine inaitwa sikukuu ya majuma(Au sikukuu ya mavuno). Ilikuwa ni siku ya 50 baada ya Yesu kufufuka.. Unaona sikukuu hizi zilivyoambatana na matukio muhimu kwa agano letu jipya?. Nne ya hizo zimeshapita..bado tatu mbeleni zinakuja.

Na baada ya hapo tena Mungu aliwaagizwa wana wa Israeli waishike sikukuu ya Baragumu/Tarumbeta(Hesabu 29:1) Sasa hii inaangukia katika mwezi wao wa 7 tarehe ya kwanza, ambayo kwetu sisi ni katikati ya mwezi wa 9 na wa 10..Utaona hapo ni kipindi kirefu kidogo kinapita mpaka sikukuu nyingine kuanza, Ipo sababu Mungu kuruhusu iwe hivyo,..Sasa siku hii Tarumbeta/Mbiu inapigwa kwa Waisraeli wote kuwaamsha na kuwayafanya wajiweke tayari kwa sikukuu mbili kuu na takatifu zinazokuja mbeleni.

Sasa hii katika Roho inafunua nini? Kumbuka tangu siku ile ya Pentekoste(Yaani kipindi cha Roho Mtakatifu kuachiwa juu ya watu) mpaka sasa tunachosubiria ni Unyakuo ambao huo tunajua utaambatana na parapanda ya Mungu, Ukisoma 1Wakorintho 15:51 utaona inasema “ Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,

52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa PARAPANDA YA MWISHO; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.”

Unaona?. Sasa tangu huo wakati mpaka utaona kama ni muda mrefu wa takribani miaka 2000, kufunua kile pindi kirefu tangu ile sikukuu ya majuma, hadi ile sikukuu ya baragumu, baragumu kwa jina lingine ni tarumbeta, au mbiu au paraparanda.

Hivyo ndugu wakati umeshakaribia wa sikukuu hii ya 5 kujifunua kwetu, parapanda italia, na ikilia tu itatimiza makusudi mawili, la kwanza ni kuliondoa Kanisa la Mtaifa duniani kwa ule unyakuo, na la pili itakuwa ni kuwaamasha Wayahudi sasa wajiweke tayari kwa utakaso ambao Mungu anakwenda kuachia juu yao kwa sikukuu inayokwenda kufuata.

6) Sasa sikukuu inayofuata inajulikana kama sikukuuu ya upatanisho: Hii inakuja siku ya 10 ya mwezi huo huo wa saba. Ilikuwa ni siku ambayo Kuhani mkuu anafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi za waisraeli wote, ambayo ndio ile inayofanyika mara moja kwa mwaka, wakati huu kila mwisraeli anapaswa kujitaabisha nafsi yake, kwa kulia kutubia maovu yake, na mtu yeyote atakayeonekana anastarehe katika kipindi hicho mtu huyo atauawa, au yoyote atayeonekana anafanya kazi yoyote ile, vile vile mtu huyo atauawa.

Walawi 23:27 “Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa saba ni siku ya upatanisho; itakuwa kusanyiko takatifu kwenu, nanyi mtazitesa nafsi zenu; nanyi mtasongeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto”.

Sasa tukirudi katika agano jipya sikukuu hii inafunua nini, kumbuka kanisa wakati huo litakuwa limeshanyakuliwa, siku ile parapanda itakapolia, Na tunafahamu kuwa hadi wakati huu wayahudi wengi bado hawajampokea Kristo kama Masihi wao, sasa mara baada ya unyakuo kupita Mungu atawamwagia tena Roho ya Neema Wayahudi wote, kisha watafunguliwa macho na kugundua kuwa Yule Kristo waliyemchoma wakati ule pale Kalvari ndiye Masihi wao waliokuwa wanamtazamia, siku hiyo ndipo watakapolia na kuomboleza, watatubia maovu yao ndipo Mungu atakapofanya upatanisho wa dhambi zako, na kuwapokea na kuwapigania kama zamani, na wokovu kuanzia huo wakati utakuwa kwa wayahudi sasa wakati huo wale waliobakia katika mataifa ambao hawakwenda katika unyakuo neema itakuwa imeshaondoka kwao, kilichobakia kwao ni kujumuika na mpinga-Kristo kupambana na wayahudi na kikundi kidogo sana ambacho kilikuwa katika mstari lakini kilizembea neema, ndio wale wanawali wapumbavu wanaozungumziwa katika(Ufunuo 25).

Zekaria 12:10 “Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.

11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido.

12 Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao;

13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao.

14 Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao.”

Wakati huu ndipo Mungu ataanza kuyahukumu mataifa yote duniani kwa kupitia Taifa la Israeli watu wake. Unaweza kuona ni wakati gani huu tunaishi, Israeli sasa imeshakuwa taifa lililosimama, kinachongojewa ni unyakuo tu, Mungu aanze kutenda nao kazi..

Sikukuu ya 7 na ya Mwisho ni sikukuu ya VIBANDA: Sikukuu inaanza tarehe 15 ya mwezi huo huo wa 7, Ukiangalia utaona nazo hizi tatu za zinaongozana, kutoka tarehe 1, mpaka 10, na sasa 15, kama tu vile zile sikukuu tatu za kwanza zilivyoongozana..Ni kufunua kuwa tangu kipindi kile cha Unyakuo hadi mambo yote kuisha kitakuwa ni kipindi kifupi sana, yaani kulingana na biblia ndani ya miaka 7 mambo yote yatakuwa yameisha.

Sasa katika sikukuu hii Mungu aliwaagiza wana wa Israeli watengeze vibanda, nje ya nyumba zao kwa miti mbalimbali au majani ya mitende, na ni amri kwa kila mwisraeli ndani ya siku hizo yaani saba anapaswa alale nje kwenye vibanda hivyo walivyovitengeneza huku wakimfurahia Bwana wakikumbuka jinsi alivyowatoa katika nchi ya Misri na kukaa katika vibanda wakati ule walipokuwa jangwani. Wakati ambapo maskani ya Mungu ilikuwa na Watoto wake jangwani…Hizo ndizo sikukuu kuu 7 za Bwana ambazo aliwaagiza wana wa Israeli wazishike kila Mwaka milele na milele.

Sasa sikukuu hii ya saba katika Roho: Inafunua ule utawala wa miaka 1000 ambao Bwana Yesu atakuja kutawala hapa duniani kama mfalme wa wafalme na Bwana wa Mabwana, pamoja na watakatifu wake na wayahudi wake..Biblia inasema wakati huo. Mataifa yote yatapaswa yatii amri ya Mfalme Yesu, na kuishika sikukuu ya vibanda.

Zekaria 14: 9 “Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja.

10 Nchi yote itageuzwa kuwa kama Araba, toka Geba mpaka Rimoni upande wa kusini wa Yerusalemu; naye atainuliwa juu, atakaa mahali pake mwenyewe, toka lango la Benyamini mpaka mahali pa lango la kwanza, mpaka lango la pembeni; tena toka mnara wa Hananeli mpaka mashinikizo ya mfalme.

11 Na watu watakaa ndani yake, wala hakutakuwako laana tena; lakini Yerusalemu utakaa salama……………………….

16 Hata itakuwa, ya kwamba kila mtu aliyesalia wa mataifa yote, waliokuja kupigana na Yerusalemu, atakwea mwaka baada ya mwaka ili kumwabudu Mfalme, Bwana wa majeshi, na kuishika SIKUKUU YA VIBANDA.

17 Tena itakuwa, ya kwamba mtu awaye yote wa jamaa zote zilizomo duniani, asiyekwea kwenda Yerusalemu ili kumwabudu Mfalme, Bwana wa majeshi, mvua haitanyesha kwao.

18 Na kama jamaa ya Misri hawakwei, wala hawaji, pia haitanyesha kwao; itakuwako tauni, ambayo Bwana atawapiga mataifa, wasiokwea ili kushika sikukuu ya Vibanda.

Hii ni kuonyesha kuwa wakati huo, Bwana pamoja na watakatifu na wayahudi, watasterehe na Kutawala dunia nzima, ambapo Maskani ya Mungu itakuwa pamoja na wanadamu duniani.. na ndio biblia inasema Fimbo ya chuma itatumika kwa yale mataifa ambayo yataonekana hayatii Amri za Mfalme YESU na watakatifu wake.

Unaona jinsi siku zilivyoisha?, wakati wowote parapanda italia na bibi-arusi atakwenda kumlaki Bwana mawinguni, je! Na wewe utakuwa mmojawapo?. Kama huna uhakika basi muda unaosasa mchache wa wewe kutubu, geuka mfuate Kristo kwa nia moja, ulimwengu usikusonge ukasahau kuyaangalia na mambo yanayokuja. Dunia inapita ndugu, Je! Katika maisha unayoishi Kristo yupo ndani yako?. Uamuzi ni wako. Ombi langu ni utubu sasa.

Bwana akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

SIKUKUU YA PURIMU

SIKUKUU YA VIBANDA NI IPI?

SIKUKUU YA VIBANDA NI IPI?

Rudi Nyumbani

Print this post

MWE NA HASIRA, ILA MSITENDE DHAMBI.

Shalom Mtu wa Mungu, karibu tujifunza Maandiko..Leo kwa Neema za Bwana tutajifunza kwa ufupi juu ya HASIRA YA KIMUNGU…Tusome Mstari ufuatao kabla ya kuendelea ambao utatusaidia kuelewa kiini cha somo letu.

Waefeso 4:26 ‘Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;’’

Ukisoma mstari huu kwa haraka haraka ni rahisi Kuchanganyikiwa na kufikiri biblia imehalalisha mambo baadhi maovu..Lakini leo tutajifunza kwa ufupi tafsiri ya mfano huo, ambapo tukishaelewa itatusaidia na sisi kuenenda kama maandiko yanavyotaka tuenende.

Sasa ukiusoma kwa utaratibu mstari huo, unaona biblia inasema mwe na hasira ILA MSITENDE DHAMBI!…Haijasema tu mwe na hasira basi halafu ikaishia hapo, bali imesema mwe na hasira ila msitende dhambi…ikiwa na maana kuwa hasira inayozungumziwa hapo sio ile hasira inayozaa dhambi…

Mfano wa hasira inayozaa dhambi ni kama ile mtu anatukanwa na anakasirika na matokeo ya ile hasira ni kumwekea kinyongo yule aliyemtukana, au kumchukia, au kutafuta kisasi au kutokumsamehe…sasa hizo ni hasira zinazozaa dhambi ambazo sio zilizozungumziwa hapo kwenye Waefeso 4:26.…kwasababu kinyongo, kutokusamehe, kisasi, chuki, wivu nk hivyo vyote ni dhambi.

Sasa swali linakuja ni hasira gani inayozungumziwa hapo?…Ili kuielewa hiyo hasira inayozungumziwa hapo ambayo haizai dhambi tusome tena mstari ufuatao wa mwisho…tutapata majibu.

Marko 3: 1 ‘Akaingia tena katika sinagogi; na palikuwako huko mtu mwenye mkono uliopooza;

2 wakamvizia ili kuona kama atamponya siku ya sabato; wapate kumshitaki.

3 Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati.

4 Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza.

5 Akawakazia macho pande zote kwa HASIRA, AKIONA HUZUNI KWA AJILI YA UGUMU WA MIOYO YAO, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena’.

Umeona hapo Hata Bwana Yesu alikuwa na HASIRA, lakini hasira yake haikuwa hasira yenye hatima ya dhambi bali hatima ya HUZUNI kwa ajili upofu wao..Na hiyo ndio hasira Mtume Paulo aliyokuwa anaizungumzia katika Waefeso 4:26 kuwa ‘Mwe na hasira, ila msitende dhambi’…Hasira aliyokuwa anaizungumzia hapo ni hasira ya kutamani mtu Fulani apone na sio hasira ya kumwangamiza mtu. Kama Bwana Yesu alivyofanya hapo! Alikasirika kwa huzuni, aliona kwanini hawa watu wanaona miujiza yote hii lakini mioyo yao bado migumu? Ikamfanya akasirike huku akiwahuzunikia.

Ili tuweze kuelewa tena vizuri jaribu kuutafakari mfano huu , imetokea mwanao kafanya jambo Fulani baya sana, labda amekutukana wewe kama mzazi wake, na ulishamwonya mara nyingi awe na tabia njema…bila shaka utakasirika lakini hasira hiyo sio ya kumchukia au kumwekea kinyongo mwanao bali ya kumhuzunikia!…utakasirika huku unahuzunika, huzuni hiyo ni ya kutamani abadilike, sio afe.

Na sisi hasira zetu zinapaswa ziwe hivyo hivyo, unapotukanwa na mtu, au unapoaibishwa, au unapodhihakiwa na kuudhiwa kwa sababu ya jambo Fulani au kwasababu ya njia unayoiendea ya haki…hasira inaweza kuja wakati mwingine lakini hasira hiyo inapaswa isiwe kwa kutenda dhambi, bali kwa kuwahuzunikia kwa wanayoyafanya, kuudhiwa kama mkristo kupo kwa namna moja au nyingine, na kama haujakutana nako leo ipo siku utakutana nako

1 Timotheo 3:12 ‘Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu WATAUDHIWA.’

Sasa siku wanapokufanyia mambo yasiyostahili, sio wakati wa kuwaombea na wenyewe wapatwe na yaliyokukuta wewe, badala yake ni kuwahurumia ukijua si wao bali ni shetani anafanya kazi ndani yao..

Utaudhiwa kila mahali unapokwenda, utakutana na watu ambao hawatakuelewa kwa chochote utakachowaambia, kama ilivyokuwa kwa Bwana hakueleweka kwa baadhi ya watu mpaka jambo hilo likawa linamkasirisha. Walikuwa wanatoa maneno ya kumkera sana, na ndio siku ile kabla ya kuondoka kwake akawaambia mitume wake.

Yohana 15: 20 ‘Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi;…’’.

Bwana akubariki sana, naamini utakuwa umepata kitu…

Ukiwa bado hujampa BWANA YESU Maisha yako, basi jua Upo kwenye hatari kubwa kuliko hata hatari ya kupata ajali yoyote ile…Bwana Yesu ndio Njia, na kweli na Uzima..Mtu hafiki mbinguni bila njia yake yeye..Hivyo nakushauri ufanye maamuzi sahihi leo ya kumkaribisha moyoni mwako..atakusamehe bure pasipo gharama yoyote na atakufanya kuwa kiumbe kipya, kwasababu ndicho anachokitaka kwako..

Hivyo unachopaswa kufanya hapo ulipo, ni kujitenga kwa muda mchache na kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kutozifanya tena…unakusudia kuacha uasherati moja kwa moja, ulevi moja kwa moja, anasa na mambo yote mabaya ya ulimwengu huu…na ukishakusudia kufanya hivyo…Bwana ataona umemaanisha kumfuata kwa moyo..hivyo atakuandalia zawadi ya Roho wake Mtakatifu ambaye atauzika kabisa ule utu wako wa kale ambao ulikuwa unakufanya ushindwe kuishinda dhambi, na atakuvika utu upya ambao katika huo utaweza kuishinda dhambi kiurahisi kabisa..Lakini hilo ni mpaka umekusudia kweli kweli kumfuata yeye.

Hivyo mkaribishe leo, moyoni mwako kabla mlango wa Neema haujafungwa..

Maran atha! jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!

VITA DHIDI YA MAADUI

BWANA ALIKUWA NA MAANA GANI KUSEMA MATHAYO 5:39 “MTU AKUPIGAYE SHAVU LA KUUME, MGEUZIE NA LA PILI”?


Rudi Nyumbani

Print this post

TAFUTA KUMJUA MUNGU ZAIDI YA SHETANI

Jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.

Karibu tujifunze Neno la Mungu…Taa iongozayo miguu yetu na Mwanga wa njia zetu (Zab.119:105).

Karibia kila tukio linalotokea duniani baya au jema huwa linameruhusiwa na Mungu, hakuna kitu hata kimoja kinaweza kuendelea chini ya mbingu kama hakijaruhusiwa na Mamlaka iliyo kuu (yaani ya mbinguni). Utauliza hata zile ajali tunazoziona zimeruhusiwa zitokee?..jibu ni ndio…utauliza tena hata vifo vyote vya kikatili pamoja na shida na magonjwa ni Mungu kayaruhusu yatokee…jibu ni Ndio!…Mungu muumba wa Mbingu na nchi, aliyeumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana dunia haijamshinda kiasi kwamba jambo Fulani linaweza kutokea pasipo ridhaa yake…Tukilifahamu vizuri jambo hili litatufanya tumtazame Mungu kwa jicho lingine.

Sasa kwanini anaruhusu vimbunga juu ya watu wasiomjua yeye…ni kwasababu ya maasi na maovu ya watu… na kwanini anaruhusu vimbunga juu ya watu wake wanaomjua yeye?…ni kwasababu ile ile kama alivyovileta kwa mtumishi wake Ayubu.

Siku zote shetani hawezi kujiamulia kufanya jambo lolote kabla halijamfikia kwanza Mungu, lipitishwe, Tunaweza kuona jambo hilo katika kitabu cha Ayubu.

Ayubu 1:7 ‘Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.

8 Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.

9 Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure?

10 Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.

11 Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.

12 Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana’.

Unaona shetani hafanyi jambo lolote pasipo idhini ya Mungu..

Shetani anapompiga mtu kwa magonjwa na dhiki na tabu…cha kuangalia hapo sio kwenda kupambana na shetani..hapana! cha kufanya hapo ni kwenda kutafuta chanzo cha mambo hayo yote ni nini? Na ukishagundua kuwa ni Mungu karuhusu ndipo unapotakiwa kupoteza muda mwingi kumtafuta yeye kuliko kupambana na shetani…ili ujue sababu ya yeye kuyaruhusu hayo ni nini…kwasababu ukiacha kumwangalia Mungu na kupambana na shetani hutamweza hata kidogo…kwasababu yeye anafanya kazi kwa kibali maalumu kutoka juu na ana nguvu kuliko wewe..

Leo utaona mtu anaumwa na ugonjwa usiojulikana pengine kalogwa anatafuta kwenda kuombewa na kutafuta mchawi wake ni nani…anahangaika kwenda kukemea huo ugonjwa umtoke au huo uchawi umrudie mbaya wake na kupambana na shetani…lakini pasipo kujua kuwa mpaka ule ugonjwa umempata tayari Mungu mwenyewe alisharuhusu jambo hilo juu ya mwili wake…hivyo pa kwenda kutafuta suluhisho sio pengine zaidi ya kwa Mungu…

Ndio hapo itakubidi uende kwa Mungu kwa unnyenyekevu na magoti..Na kumwuliza Bwana sababu ya mambo haya yote ni nini? Ndipo Bwana atakufunulia…pengine Maisha yako si masafi mbele zake hivyo ameyaruhusu hayo shetani akupige ili wewe umrudie yeye na utakapotubu na kuyasafisha Maisha yako hilo tatizo linaondoka pasipo hata kuwekewa mkono na mtu yeyote…Au kama Maisha yako yapo sawa basi ameruhusu tu upitie hayo ili kukupeleka kwenye kiwango kingine cha kiroho kama alivyofanya kwa mtumishi wake Ayubu..nk zipo sababu nyingi.

Hebu fikiria endapo Ayubu angeacha kumfikiria Mungu na kuanza kukemea wachawi na mapepo yaliyowaua wanawe, au angeanza kutanga tanga huku na huko kusaka watumishi wamfanyie maombi ya kufunguliwa kwenye vifungo vya mikosi na laana na kupakwa mafuta angefikia wapi? Bila shaka angepoteza dira kabisa ya kujua sababu ya yeye kuyapitia hayo ni nini.

Kwahiyo kila kitu hata kama tunauhakika ni shetani katekeleza, tujue kuwa ni Mungu karuhusu shetani afanye hayo kwa namna ya kawaida hawezi kufanya kama kuna ulinzi wa kiMungu juu yako…Ukijifunza kufikiri hivyo hutakaa umwogope shetani kamwe! Wala hutakaa ujishughulishe kuijua elimu yake..utajikita katika kumjua Mungu Zaidi.

Tatizo la wakristo wengi wanaijua Zaidi elimu ya shetani Zaidi ya kumjua Mungu, mtu atakuelezea kwa mapana na marefu namna wachawi wanavyofanya kazi na namna wanavyologa na aina za majini na mapepo..na dawa za kienyeji, lakini mwambie akufafanulie hata mstari mmoja wa kwenye biblia kama anafahamu. Anamjua shetani Zaidi ya Mungu na hivyo linapotokea tatizo hawezi kujua chanzo chake.

Hivyo inatupasa tujizoeze kumtazama Mungu Zaidi badala ya shetani, biblia inasema Mjue sana Mungu ili upate kuwa na Amani, na sio tumjue sana shetani.

Bwana akubariki jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

MJUE SANA YESU KRISTO.

MAFUNDISHO YA MASHETANI

NITAZIJARIBUJE HIZI ROHO?

LULU YA THAMANI.


Rudi Nyumbani

Print this post

KWANINI YESU ALIMUITA BABA YAKE “ABA”?

Hili Neno Aba kwa mara ya kwanza katika biblia lilisikika likitamkwa na Bwana wetu Yesu, Hili ni Neno la Kiaremi(Aramiac), moja ya lugha ambayo Bwana Yesu alionekana akiizungumza mara kwa mara, maneno mengine yaliyorekodiwa ambayo Yesu alionekana akiyatamka yanayotokana na lugha hii hii ni pamoja na “Talitha kumi (Marko 5:41), Efatha (Marko 7:34), Eloi Eloi lama sabakthani (Mathayo 27:46) na hili Neno Aba lenyewe.”. Hivyo hii Lugha ya kiaremi ni lugha iliyokuwa imekaribiana sana na lugha ya kiyahudi isipokuwa hii ilikuwa imetohoa maneno mengi kutoka katika lugha za tamaduni nyingine kama vile Babeli n.k.. Hivyo kwa ujumla lugha hizi tatu yaani kiyahudi, kiaremi na kigiriki, Ni lugha ambazo Bwana Yesu alionekana akiziongea..

Sasa hili Neno Aba lina maana ya Baba katika lugha hiyo, Ni neno lenye uzito zaidi ya kusema Baba tu peke yake, Tukitumia mfano wa lugha ya kiingereza tunaweza kuelezea hali hiyo ikoje..kwamfano mtu anayemwita Baba yake, Father na yule anayemwita baba yake “Daddy”,kuna tofauti kubwa sana hapo. Utagundua huyu anayemwita Baba yake daddy anamahusiano ya karibu sana kuliko Yule anayemwita father,. Father anaweza akawa ni baba anayekupenda, anayekujali, anayehakikisha unapata mahitaji yako yote ya muhimu, chakula, nguo, shule, anakujengea nyumba, na n.k..lakini mtoto ambaye anamwona baba yake kama Daddy, licha tu ya kutimiziwa mahitaji yake muhimu, lakini juu ya hilo utamwona mtoto anamfurahia baba yake na anaoujasiri mwingi kwake, akimwona anaweza hata akaenda kumrukia, anaweza akamshirikisha mambo yake yote kama vile rafiki yake, hata wakitembea barabarani mtu anaweza asijue kama ni mtu na Baba yake wanatembea lakini kiuhalisi ni Baba yake tena anayemuheshimu sana. Hiyo ndio Daddy.

Sasa ndivyo hili Neno Aba lilivyomaanisha, Aba ni bonus+ ya BABA.. Kwa ule uhusiano ambao Bwana Yesu aliokuwa nao kwa Baba yake, hakukuwahi kutokea mtu yoyote duniani kuwa na uhusiano mkuu wa namna ile, utaona mpaka dakika ya mwisho anapitia majaribu mazito namna ile, akijua kabisa na Baba yake ndiye aliyempitisha katika hali ile mbaya ya dhiki, lakini bado utaona anamwita ABA..

Embu leo hii Mungu ayakorofishe mambo yetu yasiende vizuri, au tupungukiwe kidogo tu, utaona kila aina ya malalamiko na manung’uniko yatakayotoka katika vinywa vyetu kana kwamba Mungu anafurahia wewe uwe hivyo.

Marko 14:36 “Akasema, ABA, BABA, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.”

Hivyo unaweza pia ukaona lengo kuu la Yesu kuja duniani na kuishi maisha ya dizaini ile lilikuwa ni kututhibitishia sisi ni kwa jinsi gani Mungu anaweza akawa karibu na wanadamu kama mtoto na Daddy wake kwa viwango vya hali ya juu sana lakini ikiwa atukuwa tayari kutii.. Mambo ambayo hapo nyuma yalikuwa hayawezekani, na ndio maana hata wayahudi walimwona kama anakufuru kumuita Mungu Baba yake mpaka wakataka kumuua kwasababu hiyo (soma Yohana 5:18).

Mambo ambayo hata sasa bado yanawakera watu wengi hususani wale wa upande wa pili ( dini ya kiislamu), wanasema ni kufuru kumwita Mungu Baba kwani Mungu hajazaa, wala hana mshirika, sisi ni viumbe vyake basi, mengine zaidi ya hapo ni kufuru…Ni kweli kabisa wanachokisema ni sahihi, kwasababu mtu kufanywa kuwa mwana wa Mungu si jambo jepesi jepesi na la kujiamulia tu kwamba na mimi leo ni mwana wa Mungu, hiyo haipo hivyo huo ni UWEZO unatoka kwa Mungu mwenyewe..Na uwezo huo wanapewa wale tu wanampokea YESU kwa kumaanisha kabisa kumgeukia yeye. Sio kwa kukiri tu katika vinywa vyao, hapana bali ni kwa kukiri na kuamua kumfuata yeye.

1Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;

13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.”

Na ndio maana sisi tuliookolewa tuna ujasiri mwingi wa kumwendea Mungu, kwasababu yeye kwetu sio baba tu bali ni “ABA Baba”. Na Roho Yule Mtakatifu tuliyepewa anatushuhudia kuwa sisi tu watoto wa Mungu.Hivyo ujasiri wetu katika hilo ni mwingi.

Warumi 8:15 “Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.

16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;

17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.”

Unaona, ukiwa mtoto wa Mungu huna hofu yoyote, Ni wazi kuwa ujasiri utakuja wenyewe tu kwasababu Daddy yupo!!. Hii ni neema kubwa ambayo hatukustahili kuipata, ni neema ambayo mpaka kwa wengine inaonekana ni kufuru, kwanini tusiithamini.?

Wagalatia 4:6 “Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, ABA, YAANI, BABA.

7 Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.”

Pengine na wewe tangu zamani umekuwa mkristo-jina tu, Na ndio maana Huuoni u-baba wowote wa Mungu ndani yako, hiyo yote ni kwasababu umekuwa mtu wa nia mbili, huku unataka dunia huku na bado unamtaka Mungu..Na Bwana amesema huwezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja, ikiwa na maana huwezi kuwa na MA-BABA wawili kwa wakati mmoja. Ikiwa leo utachukua uamuzi wa kusimama upenda wa Kristo moja kwa moja nataka nikuambie ukweli Mungu hutamwona kama BABA tu, bali kama ABA…Kama Daddy ndani yako. Hilo ndio lengo Yesu lililomleta duniani ni ili akufanye wewe kuwa hivyo.

Tubu dhambi zako leo, kama hujaanya hivyo..na chukua uamuzi wa kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi, na katika jina la YESU KRISTO, kama hukubatizwa, kisha baada ya kutii maagizo hayo Mungu atakushushia mwenyewe Roho wake ndani yako atakaye lia Aba, Hiyo ni kukushuhudia kuwa wewe ni mwana wa Mungu, kweli kweli kuanzia huo wakati na kuendelea.

Bwana akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

  1. MWANA WA MUNGU.

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

JE! WEWE NI MWANA WA IBRAHIMU?

JE! WEWE NI MBEGU HALISI?


Rudi Nyumbani

Print this post

UMEITIKIA WITO INAVYOPASWA?

Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe.

Karibu tujifunze Biblia, Neno la Mungu, Taa ya miguu yetu na mwanga wa njia zetu.

Moja ya masomo mapana sana ni ‘Namna ya kusikia sauti ya Mungu na kuielewa’..Mungu huwa anazungumza na sisi kila siku, lakini ugumu unakuwa ni namna ya kuielewa sauti ya Mungu..Ni kweli sio kila kitu Mungu atakachozungumza na sisi tutakielewa..sio kila kitu kwasababu tuna mipaka Fulani ya kiufahamu kutokana na hii miili tuliyonayo ya kidunia…lakini tutakapoivaa ile miili mipya ya utukufu basi tutamsikia na kumwelewa Mungu kwa mapana Zaidi. Lakini ni muhimu kutafuta kuisikia na kuielewa sauti ya Mungu kwa kadri tuwezavyo sasa, kwasababu Mungu kila siku anazungumza na sisi.

Zipo sababu nyingi zinazofanya tusisikie sauti ya Mungu kabisa..mojawapo ni maovu yetu (Isaya 59:1-2) na kingine ni kusongwa na mambo mengi…masumbufu ya Maisha haya…hizo ni kama kelele masikioni mwetu zinazozuia tusisikie sauti ya Mungu…Unapokuwa unasongwa na sauti nyingi nyingi za mambo ya ulimwengu huu inakuwa ni ngumu sana kuisikia sauti ya Mungu, mtu anayejihusisha na utazamaji wa movies muda mrefu, anakuwa anajisikilizisha sauti nyingine ambazo zinazuia masikio yake kusikia sauti ya Mungu…ni sawa na Mtu aliyeweka earphones kwenye masikio yake…hawezi kusikia sauti ya mtu anayezungumza naye akiwa nje…au kama ataisikia ataisikia kwa mbali sana…au anaweza akasikia isivyopaswa.

Kadhalika mtu anayekuwa katika shughuli nyingi za utafutaji wa mali kuanzia asubuhi, mpaka jioni anafanya hivyo siku saba katika wiki na miezi 12 katika mwaka..ni ngumu sana kuisikia sauti ya Mungu ikizungumza naye..purukushani za huku na kule za Maisha, anakutana na watu hawa, wale..anakumbana na tatizo hili au lile, watu hawa wanamweleza hivi au vile n.k hiyo inazuia sana kuisikia sauti ya Mungu.

Lakini leo hatutaingia sana huko. Leo tutajifunza ni kwa namna gani tunaweza tukaitikia vyema wito wa Mungu..yaani wakati Mungu anapotuita.

Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa, Mungu anapozungumza sio kama wengi wetu tunavyotazamia..kwamba atazungumza nasi kwa radi mbinguni au mingurumo, au tutasikia sauti Fulani ya kipekee ya ajabu ikitunong’oneza masikioni. Inaweza ikatokea hivyo lakini hiyo sio njia ambayo Mungu anaitumia kusema na watu siku zote…wengi wanaitafuta hiyo njia lakini Mungu hatumii njia hiyo, sauti ya Mungu inapokuja ni kama ‘’mawazo Fulani yanaingia ndani yako ambayo yanakuwa yanakupa ufunuo fulani’’..Mawazo Fulani yanayokufumbua macho ya kuelewa jambo Fulani ambalo ulikuwa hulielewi au ulikuwa hulijui. Na hayo mawazo yanakuwa ni kama vile wewe umeyatengeneza…unaweza ukadhani ni wewe unajiambia mambo hayo, lakini sio wewe ni Bwana anazungumza na wewe…Sauti yake wakati mwingine inafanana na sauti yako kabisa, isipokuwa ya Mungu inakuja na ufunuo Fulani wa kimaandiko, ambao huo ukiupata unasikia kusisimka katika roho, unajisikia furaha kulijua hilo jambo, unajisikia amani, unajisikia kumgeukia Mungu Zaidi na kumpenda…unajisikia kutolewa sehemu moja hadi nyingine kiimani…Hiyo ni sauti ya Mungu imezungumza na wewe. Na mara nyingi hii inakuja ukiwa sehemu ya utulivu sana ukimtafakari Mungu, au ukiwa katika kulisoma Neno lake. Kwa jinsi unavyokuwa mtulivu zaidi na kulitafakari Neno la Mungu zaidi ndivyo wigo mpana wa kuisikia sauti ya Mungu unavyokuja.

Pia licha ya sauti ya Mungu kufanana sana na sauti yako, lakini pia inafanana na sauti ya Mtu mwingine ambaye yupo karibu na wewe kiimani..Mtu anaweza kuzungumza na wewe Neno Fulani la kiMungu ukaona limekupa msisimko fulani ndani yako ya kutaka kumjua Mungu Zaidi, au kumpenda Mungu, au kumtafuta..Huyo ni Mungu anazungumza na wewe, ingawa unaweza kudhani ni yule mtu kazungumza na wewe, lakini kiuhalisia si Yule mtu bali ni Mungu.

Unaweza pia kuwa katika utulivu..Bwana akaanza kuzungumza na wewe kupitia mahubiri ambayo ulishawahi kuyasikia huko nyuma, ukasikia kabisa kama vile yule mtu anakuhubiria masikioni mwako saa hiyo…ukapata kufunguliwa macho na kuona kitu kipya ambacho ulikuwa hukijui…Sasa huyo ni Mungu anazungumza ndani yako kupitia sauti ya yule Mtumishi uliyemsikia. Na kwasababu bado hujaijua sauti ya Mungu wewe utadhani ni yule mtumishi anazungumza na wewe na hivyo utatafuta njia yoyote ya kwenda kukutana naye au kujiunga katika dhehebu lake au kanisa lake..

Lakini nataka nikuambie hapo utakuwa hujaitikia vyema wito wa Mungu. Ingawa uliisikia kweli sauti ya Mungu. Lakini huko uendako unakwenda kupotea….Hebu tujifunze kidogo katika maandiko juu ya jambo hilo.

1 Samweli 3: 1 ‘Basi, mtoto Samweli akamtumikia Bwana mbele ya Eli. Na neno la Bwana lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri.

2 Ikawa wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona),

3 na taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la Bwana, palipokuwa na sanduku la Mungu;

4 basi, wakati huo Bwana akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa.

5 Akamwendea Eli kwa haraka, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akasema, Sikukuita; kalale tena. Naye akaenda, akalala tena.

6 Bwana akaita mara ya pili, Samweli! Samweli! Akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, Sikukuita, mwanangu; kalale tena.

7 Basi Samweli alikuwa hamjui Bwana bado, na neno la Bwana lilikuwa bado halijafunuliwa kwake.

8 Bwana akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli akatambua ya kuwa Bwana ndiye aliyemwita yule mtoto.

9 Kwa hivyo Eli akamwambia Samweli, Enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Basi Samweli akaenda akalala mahali pake.

10 Bwana akaja, akasimama, akaita vile vile kama kwanza, Samweli! Samweli! Ndipo Samweli akasema, Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia.

11 Bwana akamwambia Samweli, Angalia, nitatenda tendo katika Israeli, ambalo kila atakayelisikia masikio yake yatamwasha.

12 Siku hiyo nitayatimiza maneno yale yote niliyoyasema juu ya Eli katika habari za nyumba yake, tangu mwanzo hata mwisho.

13 Kwa maana nimemwambia ya kwamba nitaihukumu nyumba yake milele, kwa ajili ya ule uovu alioujua; kwa kuwa wanawe walijiletea laana, wala yeye hakuwazuia.

14 Na kwa hiyo nimeapa juu ya nyumba ya Eli, ya kwamba uovu wa nyumba ya Eli hautasafika kwa dhabihu wala kwa sadaka hata milele.’’

Katika habari hiyo tunamwona kijana Samweli…Na siku moja Mungu alipotaka kujifunua kwake, hakuzungumza naye na sauti mpya ya ajabu ya kipekee…bali alizungumza naye moyoni mwake na sauti inayofanana kabisa na ile ya Eli…’yaani kwa ufupi aliisikia sauti ya Eli ikimwita’..Na yeye kwasababu alijua Eli ni Mtumishi mteule wa Mungu, aliyechaguliwa na Mungu atumike katika nyumba ya Mungu…aliitikia wito isivyopaswa akamfuata Eli kwasababu tu ile sauti aliyoisikia ilikuwa kama ya Eli..akaenda kwa Eli lakini hakukipata kile alichokuwa anakitafuta kwa maana alitegemea aambiwe sababu ya kuitwa kwake lakini hakuambiwa..Akarudi kulala tena…akaisikia ile ile sauti kama ya Eli ikimwita mara tatu, bado akarudia kosa lile lile la kwenda kumfuata Eli mpaka Eli alipomsaidia kupata ufahamu kuwa Sauti aliyoisikia sio ya Eli ni ya Mungu, japokuwa inafanana na ya Eli mtumishi wa Mungu.

Na alipotulia kwa makini, na kuitikia vyema wito wa Mungu, ndipo Mungu akaanza kumwambia kusudi la wito wake…Samweli akaja kugundua kuwa kumbe huko kwa Eli alikokuwa anakwenda ndipo Mungu alipopachukia na ndiko Mungu anapotaka kumtuma akawaambie makosa yao.

Na sauti hiyo hiyo inawaita wengi leo hii…Lakini inapoita sio wakati wa kuitikia na kwenda kumfuata huyo mtumishi au dhehebu la huyo mtumishi unayesikia ujumbe kutoka kwake..Bwana ametumia tu sauti ya huyo mtumishi au sauti ya hilo dhehebu kukuita wewe…Lakini Bwana hayupo huko hata kidogo..Yupo hapo hapo ulipo?. Anapokuita ndugu usiende kujiunga na madhehebu utapofuka macho. Hutamsikia Mungu huko hata kidogo. Ndicho kilichomtokea Samweli mpaka alipoelewa somo.

Ndugu udhehebu ni mnyororo mbaya sana, ambao unawakosesha wengi na kuwapeleka kuzimu..Samweli hakujua uovu uliokuwa unaendelea kwenye nyumba ya Mungu ambao ulikuwa unaongozwa na Eli pamoja na wanawe..mpaka siku alipotoka na kuisikia sauti ya Mungu, akagundua kuwa kumbe Mungu ametukasirikia, kumbe japo watu kwa nje wanaona kila kitu kipo sawa lakini kumbe Mungu katukasirikia sisi tuliopo ndani…na hata huyu Eli ambaye Mungu alitumia sauti yake kuzungumza nami..kumbe hata yeye tayari kashaharibu mambo siku nyingi…hayo yote Samweli aliyajua baada ya kutoka kwenye udini na udhehebu wa Eli.

Hivi unajua chapa ya mnyama inauhusiano mkubwa sana na dini na madhehebu…Roho ya Mpinga-Kristo sasa inatenda kazi katikati ya madhehebu, kuhakikisha inawafunga matita matita watu na kuwapeleka watu jehanamu..sawasawa na Mathayo 13:30. Ndio maana unaona madhehebu yanaongezeka kila kukicha…Huo sio mpango wa Mungu kabisa…. Itafika siku moja baada ya unyakuo kupita, madhehebu yote yatasajiliwa katika umoja wa madhehebu duniani..na watu hawataweza kununua wala kuuza wala kuajiriwa wasipokuwa washirika wa mojawapo ya madhehebu yaliyosajiliwa katika umoja huo wa dini na madhehebu duniani…Siku hiyo mamilioni ya watu wataipokea chapa pasipo kujua kuwa wameipokea. Maelezo yake juu ya hayo ni marefu kidogo lakini..Kama hujafahamu kuhusu hayo basi yafuatilie na uyajue au unaweza ukanitext inbox nikutumie somo juu ya hayo.

Lakini huu sio wakati wa kujisifia dhehebu wala dini, ni wakati wa kutoka huko na kurudi kwenye Neno,(Ufunuo 18:4) huu sio wakati wa kusema mimi ni Muanglikana, Mlutheri, Mkatoliki, Mlokole, Msabato, Mbaptist, Mbranhamite, Mmennonites n.k Huu ni wakati wa Kuwa Mkristo wa kweli wa kimaandiko, Bibi arusi safi, aliyeisikia sauti ya Mungu kweli na kuitikia wito inavyopaswa kwa kuzaliwa mara ya pili na kuishi kulingana na Neno la kwenye biblia(Maisha ya utakatifu na yanayompendeza Mungu).

Mungu anapokuita itikia wito ipasavyo, Rudi kwenye Neno lake ndipo mahali salama, ujifunze ukue kiroho, Ona fahari juu ya Roho Mtakatifu anakushuhudia kila siku kuwa wewe ni mwana wa Mungu kuliko dini au dhehebu hivyo havitakufikisha popote.

Bwana akubariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Zinazoendana:

WITO WA MUNGU

JE! UMECHAGULIWA KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA ULIMWENGU?

IELEWE SAUTI YA MUNGU.

NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE

SADAKA ILIYOKUBALIKA.


Rudi Nyumbani

Print this post