Yohana 2:13 ‘’Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu.
14 Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi.
15 Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;
16 akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.
17 Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila.
18 Basi Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara gani utuonyeshayo, kwamba unafanya haya? 19 Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha.
20 Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu?
21 Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake.
22 Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.’’
Tukisoma
kisa hichi ni rahisi kuwahukumu Makuhani na Mafarisayo na Wayahudi kuwa
walikuwa watu wasiofikiri…watu wanaoona miujiza lakini hawaamini…ni
kweli kuna mambo ya kulaumiwa lakini si yote…. hebu leo kwa sehemu
tuchunguze kama ni kweli walikuwa hawafikiri wakati wote..
Jaribu
kuchukua mfano wewe ni mtumishi wa Serikali, labda unatumika kwenye
shirika fulani la Umma..halafu siku moja anatokea mtu usiyemjua anaingia
mahali mnapofanyia kazi na kuanza kuvuruga vuruga nyaraka na hati
muhimu..huku anawapazia sauti na kuwaambia…msigeuze serikali ya Raisi
wangu kuwa pango la mafisadi….na mnapojaribu kumzuia na kumwuliza yeye
ni nani na nani kamtuma kufanya vile, anawajibu…jiuzuluni wote na
mwachie ngazi leo na baada ya siku tatu nitalinyanyua hili shirika upya.
Unafikiri
ni kitu gani..kitagonga kwenye akili…Moja kwa moja aidha utajua huyo
mtu karukwa na akili..Na pili jambo litakalofuata ni kutafuta njia ya
kwenda kumshitaki haraka…Kwasababu anakuja kuharibu kazi na kuzungumza
vitu visivyoeleweka…eti atalinyanyua shirika ndani ya siku
tatu!!…Shirika hili mpaka kulifikisha hapa tumetumia miaka Zaidi ya 20
wewe unataka kulinyanyua ndani ya siku tatu!..
Hebu
fikiria huyo mtu hata akienda mahakamani atashindaje kesi?..kwasababu
amesikiwa na watu wote kwa kinywa chake akisema atalinyanyua shirika kwa
siku tatu.
Na
ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana Yesu mahali Fulani, alipowakuta wayahudi
wanafanya biashara kule Hekaluni,aliwaambia wasigeuze nyumba ya Baba
yake kuwa pango la wanyang’anyi lakini walipomuhoji kwa ishara gani
unafanya haya? Akawaambia libomoeni hekalu hili na ndani ya siku tatu
nitalisimamisha.
Sasa
wayahudi walidhani wamemsikia vizuri na kumwelewa…kumbe hawajamwelewa
ingawa wamemsikia,..ndio maana Neno linasema ‘kusikia mtasikia lakini
hamtaelewa..Kutazama mtatazama lakini hamtaona (Mathayo 13:14)’…Walidhani
hekalu litakalobomolewa na kusimamishwa ndani ya siku tatu ni hilo la
mawe wanaloliona mbele yao..kumbe kulikuwa na hekalu lingine ambalo
lilikuwa ni mwili wa Bwana Yesu.
Na waliendelea na huo upofu mpaka siku ya mwisho, pale walipomsulibisha
Walisema maneno haya:
Mathayo
27:40 ‘’Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe
nafsi yako; ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, shuka msalabani’’.
Lakini
tunaona waliokuja kumwelewa ni wanafanzi wake tu! Tena dakika za
mwisho, Wale waliokuwa wanatembea naye kila siku. Ndio waliopewa neema
ya kumwelewa Bwana Yesu alikuwa anamaanisha nini katika maneno yake. Sio
kila mtu tu alikuwa anamwelewa Bwana Yesu.
Ndugu
huo upofu mpaka leo upo! Unaendelea kwa watu wengi wasio wanafunzi wa
Yesu Kristo..Bwana hana wanafunzi 12..alianza na wanafunzi 12, lakini
sasa anao wanafunzi wengi…Na hao ndio anaowafunua macho ya kuyaelewa
maneno yake…wengine walio nje maneno ya Yesu yatakuwa ni mafumbo
kwao…wataona wanamwelewa sana Bwana Yesu lakini kumbe hawamwelewi..
Watadhani
kwasababu Bwana aliyageuza maji kuwa divai basi alihalalisha unywaji wa
pombe, lakini hawaelewi kuwa Pia kitendo cha Bwana kula na makahaba na
wenye dhambi lengo lake halikuwa kuhalalalisha ukahaba wao wala dhambi
zao…Alifanya vile ili kutafuta njia ya kuwavuta watubu kwa upendo
wake….Na watu walipomwita kuwa mlevi haikumaanisha kuwa yeye kweli ni
mlevi..wewe unaweza kuitwa mlevi na maadui zako lakini isiwe ni mlevi
kweli…kadhalika walipomwita yeye ni mlafi haikumaanisha Bwana Yesu
alikuwa ni mlafi kweli…
Alipomwita
Herode Mbweha!..hakumaanisha kumtukana!!…ingekuwa ndio hivyo, basi yeye
mwenyewe amejitukana sana…alipokuwa anajiita mwanakondoo?..au
anapowafananisha watu wake na kondoo..kwa wale wafugaji wanaelewa ni
afadhali mtu akuite mbwa kuliko kondoo.
Kadhalika
aliposema mkawabatize watu wote kwa jina la Baba, na Mwana na Roho
Mtakatifu hakumaanisha hivyo vyeo bali alimaanisha ni jina moja ambalo
ndio la Baba, na ndio hilo hilo la Mwana na ndio hilo hilo la Roho
Mtakatifu na hilo sio lingine Zaidi ya Jina la YESU (Matendo 2:38).
Na
aliposema…’’aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa
milele’’..hakumaanisha tukamkamate na kumchinjwa na kunywa damu yake
kama simba…bali alimaanisha kuula katika roho na kuinywa damu yake
katika roho..Na chakula cha Roho zetu ni Maneno tunayosikia…Yakiwa ni
Maneno ya Mungu, basi ni chakula bora cha uzima wa milele, na yakiwa
maneno ya yule mwovu basi ni chakula kisichofaa cha mauti.
Kwahiyo
Biblia inatufundisha tuwe na masikio yanayosikia, na macho
yanayoona..ili kwamba tunaposoma Biblia tuielewe…Na hayo tutayapata kwa
kuwa wanafunzi wa Yesu tu!..kwasababu hao ndio Bwana alikuwa anawapa
kuelewa maneno yake…
Na vigezo vya kuwa mwanafunzi ni hivi..
Luka 14:25 ‘’Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,
26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
27 MTU YE YOTE ASIYEUCHUKUA MSALABA WAKE NA KUJA NYUMA YANGU, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
28 Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?
29 Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki,
30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.
31 Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?
32 Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali.
33 Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu’’.
Je!
Umeuchukua msalaba wako?..je! umewachukia ndugu zako, baba yako na mama
yako?…kuchukia kunakozungumziwa hapo sio kuchukia mtu kwa hasira au
chuki ya moyo…hapana! Bali ni kitendo cha kuyakataa na kuyachukia
maamuzi ya wazazi wako au ndugu zako yanayopingana na mapenzi ya Mungu
kwako, na kuamua kuyafuata yale mapenzi ya Mungu tu!..Huko ndio
kuwachukia kunakozungumziwa hapo juu!!…kama baba yako ni mlevi na
anakutaka na wewe uwe kama yeye…hapo unayachukia hayo maamuzi na kusema
hapana!..kama ni msengenyaji hivyo hivyo..kama ni mlarushwa na wewe
anataka uwe kama yeye unasema No! kama ni mchawi au Mwenda kwa
waganga..na anataka kukufundisha na wewe uwe kama yeye..hapo unasema
hapana! N.k.
Na
pia ili uwe mwanafunzi biblia inasema unapiga gharama!! Ukristo sio
jambo la kujaribu na kutoka! Biblia inasema utachekwa….Ukiamua kumfuata
Bwana Yesu, hesabu kuwa kuna kuonekana mpumbavu, kuonekana
mshamba…wakati mwingine kuonekana umerukwa na akili…Na pia ukristo sio
mteremko muda wote…piga hesabu kuwa kuna wakati Bwana anaweza kukuacha
kwa kipindi Fulani kirefu pasipo kuzungumza na wewe kwa njia unayotaka!
Je! Utaendelea kuwa naye!…utakapopitia shida, dhiki na wakati mwingine
misiba utamwacha?
Pia piga gharama! Je asipokupa vile vitu unavyohitaji! Utaendelea kuwa naye?.
Na
mwisho anasema ‘mtu yeyote asiyeacha vyote alivyo navyo hawezi kuwa
mwanafunzi wangu’..Kuacha vyote ulivyonavyo ni mfano wa wakina
Petro…waliacha vyote walivyo navyo na kumfuata Bwana…Kuacha vyote ulivyo
navyo sio lazima kwenda kuuza mali zako au hazina yako…bali ni kuishi
kana kwamba hivyo vitu sio vya kwako…kiasi kwamba hata ikitokea
kimepotea hakipo kwenye akili yako…umeshakiacha siku nyingi…akili yako
imetawaliwa na kutenda mapenzi ya Mungu na kuyaishi…hakina chochote
katika moyo wako…kiwepo au kisiwepo vyote kwako ni sawa sawa tu.
Ukishapiga
hizo gharama, na kujitwika msalaba wako, biblia inasema umekuwa
mwanafunzi wake…ambao wamepewa Neema ya kuzijua siri za ufalme wa
mbinguni…
Hivyo
kama hujampa Kristo Yesu Maisha yako, ni vizuri ukafanya hivyo leo… Na
ili uwe mwanafunzi wake piga gharama za kumfuata…na Bwana akusaidie
katika hilo.
Mungu akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Shalom
mwana wa Mungu, ikiwa Mungu amekupa neema ya kuiona siku hii ya leo,
basi usipuuze kujifunza ni kitu gani anataka kutoka kwako leo?, Kukutana
na ujumbe huu si kwa bahati mbaya bali Mungu anakusudi na wewe juu ya
wakati aliokupa hapa duniani.
Tukisoma Waefeso 5:15-18 biblia inatuambia hivi.. “15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
16 MKIUKOMBOA WAKATI kwa maana zamani hizi ni za uovu.
17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.
18 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;”.
Nataka leo tujifunze nini maana ya kuukomboa wakati kimaandiko. Tunajua tafsiri rahisi ya hili neno kuukomboa wakati ni “kuutumia muda vizuri”, tulipokuwa shuleni moja ya vitu ambavyo vilikuwa vinawachukiza sana walimu,ni pale walipokuwa wanaona wanafunzi wanautumia muda wao vibaya (hawaukomboi wakati), Hususani pale mwalimu anapotazama muda aliobakiwa nao mbeleni jinsi ulivyo mchache, topics bado ni nyingi za kusoma, halafu mwanafunzi, anaruka ruka hajisomei, anapiga kelele darasani, hazingatii masomo, haudhurii darasani, inawatia sana hasira waalimu pamoja na wazazi. Vivyo hivyo na katika mambo mengine.
Lakini
pia katika upande wa maandiko, tunafundishwa tuukomboe wakati,
kwasababu biblia imeweka wazi kabisa kuwa zamani hizi ni za UOVU,
na tunauokomboa wakati kwa namna gani? Biblia inasema ni kwa kutaka
kufahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Mungu kwetu.Huko ndiko kuukomboa
wakati kuliko na maana mbele za Mungu.
Ndugu
huu ulimwengu una mambo mengi na mahangaiko mengi, Ni kweli tunafahamu
kwa sehemu moja au nyingine hatuwezi kuepuka mihangaiko kama ipo lakini
tunaonywa tuishi kama watu wenye hekima, na sio wajinga, tukijua kuwa
sisi ni wapitaji tu hapa duniani, na siku zetu zinakimbia kwa kasi sana,
biblia inasema sisi ni kama MVUKE uonekanao kwa kitambo kisha kutoweka (Yakobo 4:14),
Mvuke sio kama moshi ambao unaweza walau ukauona ukipaa mawinguni,
mvuke wenyewe hata kwenye dari haufiki umeshapotea, ndivyo maisha yetu
yalivyo. Biblia inasema na mwanadamu ni kama maua ambayo hayo hayana
maisha marefu,(Zaburi 103:15 ”Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo).
Hata kama tutaishi miaka 60 tu au miaka 120 bado siku zetu zitabakia kuwa ni chache sana. Hivyo swali tunalopaswa kujiuliza tukifa leo huko tunapokwenda ni kitu gani cha maana kitaoneka tumekifanya hapa duniani?. Kwasababu kule hatutaulizwa tulikuwa na majumba mangapi, au magari mangapi, au biashara ngapi, au watoto wangapi,wala hatutaulizwa tulikuwa maskini kiasi gani LA! Tutaulizwa ni kitu gani tumeongeza katika ufalme wa mbinguni..Tukiliweka hilo akilini basi itatusaidia sana kuishi kwa uangalifu.
Tunamwona Bwana wetu Yesu alijua nini maana ya kuukomboa wakati, angalia alichowaambia wanafunzi wake..Yohana 9:4 ”Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi…”
Unaona
Japo alikuwa ni Mungu katika mwili alijua nini maana ya muda, kuwa kuna
kipindi kinachoitwa usiku (KIFO) ambacho mtu yoyote atatamani kufanya
kazi ya Mungu asiweze, Na tunamwona Bwana wetu japo aliishi miaka 33 tu
lakini kazi aliyoifanya ina matunda makubwa mpaka sasa tunayafaidi. Hiyo
ni kwasababu aliukomboa muda wake vizuri hapa duniani ipasavyo. Wakati
mwingine hakuwa na muda hata wa kula. Alipoletewa chakula.
NA SISI JE! TUNAWEZAJE KUUMBOA WAKATI WETU?
Tujijengee
utaratibu wa kila siku mpya inapoanza tumwombe Mungu atusaidie tufanya
kitu ambacho kitakuwa na manufaa katika ufalme wa mbinguni na katika
maisha yetu ya rohoni… tuzitazame siku zetu ikiwa inaweza kupita siku
nzima, wiki, mwezi bila kuona kitu chochote cha maana tulichokifanya kwa
ajili ya maisha yetu ya rohoni au kwa ajili ya ufalme wa Mungu, basi
tujue hatuukomboi muda haijalishi tunatengeneza mabilioni pa pesa kiasi
gani kwa siku. Ndugu huu ndio wakati wa kuanza kuitengeneza njia yako
upya mbele za Mungu, kabla ya siku ile kufika.
Muda
ambao unautumia kuchati kwenye magroup ya whatsapp, au kusoma habari
zisizokuwa na maana mitandaoni, komboa wakati kwa kutumia muda huo
kujifunza Neno la Mungu, au kusoma mahubiri au mafundisho ya Neno la
Mungu. hayo ndio mapenzi ya Mungu kwako, au tumia muda huo kukaa katika
utulivu kumsifu na kumwimbia Mungu wako..peke yako au pamoja na wakristo
wengine..
Tukiwa makazini kwetu, tumwombe Mungu atusaidie, sio wakati wote, tutakuwa buzy na shughuli, au kuongea na wafanyakazi wenzetu mambo ya kikazi, tutumie muda wetu wakati mwingine kuwashirikisha habari za Yesu, huku tukiwaelekeza katika vyanzo vizuri vya kupata habari za Mungu, kwa kufanya hivyo pia tutakuwa tumeukomboa wakati na siku yetu kuwa na maana mbele za Mungu.
Muda
ambao tumekaa hatuna shughuli yoyote, tunaweza tumia muda huo kwenda
kuomba, hata kama hatutakuwa na mahitaji wakati huo mbele za Mungu,
lakini pia tumeagizwa kuwaombea wengine, hivyo tumia muda huo kuwaombea
watu wengine, kuna ndugu zako, rafiki zako, jamaa zako, taifa lako,
kanisa n.k..Kwa kufanya hivyo utakuwa umeukomboa wakati. Na pia maombi
yanasaidia kuepukana na majaribu.
Kama biblia inavyosema Mungu utusaidie kuzihesabu siku zetu tupate mioyo ya hekima (Zab 90:12). Hivyo na sisi tupate leo hekima ya kujua kuwa muda unakwenda sana, na jukumu bado ni kubwa mbele yetu na mtihani ulio mbele yetu bado hatujauvuka. Basi tusiwe kama wajinga, tukaze mwendo, tuanze kutumia muda wetu sasa kwa vitendo kujifunza kwa bidii Neno la Mungu kuliko jana, tuombe, na tuifanye kazi yake pia kana kwamba hatuna tena mwaka mbele. Maana usiku waja asioweza mtu kuitenda kazi. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo
libarikiwe. karibu tujifunze Neno la Mungu ambalo ndio taa iongozayo
njia zetu. Biblia inasema “Mjue sana Mungu ili uwe na Amani(Ayubu 22:21)”..Siku zote ukijua sababu ya jambo Fulani basi unapata amani. Amani inakuja baada ya kujua sababu ya jambo Fulani.
Leo
tutajifunza juu ya vyanzo vya matatizo, na namna ya kuyatatua. Kama
tunavyojua wengi wetu vyanzo vya matatizo mengi ni shetani..huo ni
ukweli usiopingika. Lakini je! Shetani analetaje matatizo?.
Tukijifunza Mfano wa Ayubu, tunaweza
kupata majibu baadhi, tunaona shetani alimshambulia Ayubu baada ya
kupata kibali maalumu kutoka kwa Mungu, hiyo ikifunua kwamba shetani
hawezi kumgusa mtu yeyote wa Mungu pasipo ruhusa yeyote kwa Mungu..
Hivyo
Mungu anaporuhusu mtu ajaribiwe…anachokifanya ni kutoa ulinzi wake juu
ya Yule mtu, na akishatoa ulinzi wake maana yake shetani anapata nafasi
ya kumwingia. Hivyo anamshambulia.
Na shetani huwa ana njia kuu mbili za kuwashambulia watu.
1) Anatumia mapepo…Katika njia hii mtu atajikuta tu ameingia matatizoni pasipo kujua chanzo ni nini. Kumbe ni majeshi ya mapepo wabaya yamemvamia.
2) Na njia ya pili anatumia watu..(Na
watu atakaowatumia ni aidha watumishi wake wa uongo wanaovaa mavazi ya
kondoo lakini ndani ni mbwa-mwitu wakali…au atatumia wachawi na
waganga)….atatumia watumishi wa uongo kuwajaribu wale wanaomjua Mungu,
na atatumia wachawi na waganga kuwajaribu wale wasiomjua Mungu…au wakati
mwingine atatumia vyote viwili kuwajaribu wale watu wanaomjua Mungu.
Sasa
tukirudi kwenye mfano wa Ayubu..baada ya ulinzi wa kiMungu kuondoka juu
yake…shetani alimletea majaribu wengi… Kama haikuwa ni kazi ya mapepo
moja kwa moja basi kuna uwezekano mkubwa sana shetani alitumia watu
Fulani kumfanyia Ayubu yale mambo…Alichofanya shetani baada ya kuona
ukingo wa kiMungu umeondoka juu ya Ayubu ni pengine aliwatupia roho ya
wivu watu baadhi waliokuwa wanamzunguka…na ile roho ilipowaingia
pengine ikawasukuma kumwendea hata kwa waganga… labda walikwenda kwa
mganga fulani maarufu kwa kipindi hicho mwenye nguvu, wakaenda na picha
yake na za watoto wake..na nyayo zake labda..Na wakiwa kule wakaona
wanafanikiwa kumwona kwenye kioo chao cha kichawi, na pengine huyo
mganga akafanya mambo yake na kutuma kimbunga cha kichawi juu ya watoto
wake wakiwa karamuni, na kwasababu ulinzi wa kiMungu umeondoka juu ya
Ayubu jambo lile likafanikiwa na Kuwaua watoto wake wote. Na magonjwa ni
hivyo hivyo ni kikundi Fulani cha maadui zake Ayubu kilihusika kumletea
yale magonjwa.
Sasa
labda baada ya tukio hilo pengine Ayubu aliona tabia Fulani za watu
wanaomzunguka kufurahi..na pengine walisema vimaneno Fulani kuonyesha
kuwa wao ndio walifanya vile. Sasa kwa jicho la haraka haraka kama Ayubu
angekuwa sio mtu wa rohoni…angesema maadui zake wamemfanyia
visa..Lakini Bwana alimpa jicho la Mbali kujua mwanzo wa Matatizo yake
hayakuwa ni wale watu..bali alijua yalikuwa ni Mungu mwenyewe…kutoa
ulinzi juu yake. Ndio maana aliishia kusema “Bwana alitoa na Bwana
alitwaa, jina lake libarikiwe”…Alijua maisha yake ni makamilifu
isipokuwa ni Mungu tu katoa ulinzi juu yake kwa makusudi Fulani. Angalia
jinsi alivyouamini uhusiano wake na Mungu, kiasi cha kwamba hakuweza
kuyumbishwa ni kitu chochote, na sisi je! tunaweza tukawa hivyo?.
Na
mambo hayo hayo yanaendelea leo hii, watu wanatumiwa na shetani
kukuharibu, pengine ni wachawi au waganga…na kushindwa kuelewa chanzo
cha mambo yote ni nini?…chanzo cha mambo yote sio watu kukuonea wivu,
au wachawi kukuchukia hapana!..chanzo cha matatizo yote ni Ulinzi wa
kiMungu kuondoka juu yako..Usianze kupambana na watu wanaokuchukia, anza
kutafuta mzizi wa tatizo ni wapi..kama Ayubu.
Ayubu
alijua chanzo cha matatizo yake, kuwa ni Bwana ndiye kayaruhusu hayo
lakini njia zake ni kamilifu…alijua sio dhambi ndani yake iliyosababisha
ulinzi wa kiMungu uondoke juu yake.
Kadhalika
na sasa tunapaswa tujitathmini, kama kuna jambo Fulani limetokea ambalo
halipo sawa…chanzo chake ni nini?..Je! ni kama Ayubu? (Njia zetu ni
kamilifu isipokuwa ni Bwana anatujaribu tu) au ni kwasababu ya dhambi
zetu, kwasababu kitu pekee kinachotoa ulinzi wa kiMungu juu ya mtu ni
dhambi…
Ukiwa
mwasherati magonjwa yatakusumbua na wachawi watakusumbua sana, mapepo
yatakusumbua sana hakuna namna utaweza kuwashinda, hata uombewe kiasi
gani hakuna namna utaweza kuchomoka mikononi mwao…ukiwa mtazamaji wa
pornography na mfanyaji wa masturbation ni hivyo hivyo…ukiwa ni mzinzi,
ni shoga ni msagaji ni hivyo hivyo, watakusumbua na hakuna namna utaweza
kuwashinda…Usidanganywe kuwa kuna mchungaji yeyote duniani mwenye uwezo
wa kukuombea wachawi au mapepo yasikufikie wala kukudhuru, wala
usidanganyike kuwa kuna maji yoyote au mafuta yoyote ya upako
yanayowazuia wachawi wasiweze kufika nyumbani kwako…Usidanganyike
kabisa ndugu…
Kitu pekee kinachoweza kufukuza na kuzishinda nguvu za giza juu ya maisha yako ni MAISHA YA UTAKATIFU katika
Kristo Yesu, Uhusiano wako na Mungu ni wa kiwango gani, hicho tu! Wala
hakuna kingine….Maisha unayoishi ndio yanayoamua ulinzi wa kiMungu uwe
juu yako au uondoke.
Fanya
uamuzi sahihi leo, usitazame wachawi, wala waganga, kama ndio chanzo
cha matatizo yako…wala usiende kutafuta suluhisho kwa kuombewa, wala
kupakwa mafuta..Suluhisho lipo kwako ambalo ndio chanzo cha mambo
yote…suluhisho ni KUBADILIKA na kuishi maisha ya utakatifu, ambayo hayo
yanakuja kwa kutubu kwanza dhambi zako zote, na kudhamiria kuziacha
kabisa kuanzia sasa na kuendelea na kwenda kubatizwa na kisha kupokea
Kipawa cha Roho Mtakatifu ambaye atakusaidia kushinda dhambi.
Ukifanya
hivyo, ulinzi wa kiMungu utakuwa juu yako, haihitaji wewe kwenda
kuombewa wala kupakwa mafuta, wala kuwaogopa wachawi…Utaishi kwa Amani
sana, na wala hakuna chochote kitakachokugusa. Kwasababu nguvu iliyopo
ndani yako ni kubwa kuliko ya kwao..Bwana Yesu alisema..
Luka 6.17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio;…… watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa;…”
Bwana akubariki sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Jina
Bwana wetuYesu libarikiwe. Ni siku nyingine tena Bwana ametupa neema
kuiona hivyo nakukaribisha ndugu popote pale ulipo tushiriki pamoja
Baraka Bwana alizotuandalia leo.
Tukisoma Zekaria 12:9-14, inasema.
“ 9 Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba nitatafuta kuwaangamiza mataifa yote watakaokuja kupigana na Yerusalemu.
10 Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido.
12 Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao;
13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao.
14 Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao”.
Watu wanaozungumziwa hapo ni wayahudi (yaani Waisraeli) ,
Embu leo jiulize tu Israeli ni Taifa dogo sana kama mkoa wa njombe, ni
taifa ambalo huwezi hata ukaenda na kukutana na vitu vya kuvutia huko au
vya kushangaza kama mataifa mengine makubwa, lakini ni kwanini leo hii
imekuwa ni JICHO LA DUNIA?. Wapo
mbali na Mungu lakini ni watu wenye akili na wenye mafanikio makubwa
duniani, jiulize siku wakiwa karibu na Mungu itakuwaje?
Hayo
maandiko hapo juu ni lazima yatime, utafika wakati biblia inasema Roho
ya neema itaachiliwa juu yao na watamwamini huyu Yesu ambaye sasa
hawamwamini, Siku hiyo Watalia na kuomboleza baada ya kugundua makosa
yao kuwa Yule waliyemsulibisha na KUMCHOMA MKUKI miaka 2000 iliyopita
kumbe ndiye Masiya waliokuwa wanamsubiria kwa miaka mingi..Ile roho ya
ufarisayo na usadukayo itaondoka juu yao.
Kama vile biblia inavyotabiri kutakuwa na maombolezo makubwa sana huko Yerusalemu wakitubu makosa yao.
Sasa hicho ndio kile kipindi ambacho mtume Paulo alikiandika katika
Warumi 11:25 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili [anasema na sisi watu wa mataifa]; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.
27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao”.
Unaona
hapo unabii huo utatimia katika hiyo siku?, Huo wakati wa Israeli
kurudiwa na kutengwa na maovu yao upo karibuni sana, na utakapoanza tu
basi ujue utimilifu wetu sisi mataifa utakuwa umeshawasili yaani kwa
lugha nyingine neema kwetu itakuwa imeshaondoka na kurudi tena Israeli,
na hiyo itaambatana na tendo KUU la UNYAKUO.
Sasa
wayahudi ambao leo hii utawaona wanalia usiku na mchana pale kwenye ule
Ukuta wa maombolezo (wailing wall). wakimwomba Mungu wa Ibrahimu baba
yao aje kuwaokoa na maadui zao na kuleta utawala wa masihi duniani, ipo
siku hayo maombolezo yatakoma, na ndipo Mungu atawarudia kwa kuwafumbua
macho na kumwona YESU, Kumbuka Mungu aliwapofusha kwa makusudi kabisa
wasimwamini Kristo ili sisi mataifa tuipate neema vinginevyo huyu Yesu
wa thamani ambaye leo hii tunaifurahia neema yake, tungemsikilizia tu
kwa wayahudi, sisi tungeendelea kuwa waabudu miti,vinyago, na wachawi.
Na hata hivyo dunia ungekuta imeshakwisha siku nyingi, wakati ule ule tu
Yesu aliokuwa ndio ungepaswa uwe ni wakati wa wao kurejeshewa ufalme wa
dunia na Yesu.
Unakumbuka
mitume walimuuliza Yesu baada ya kufufuka je! Huu ndio wakati wa
kuwarudishia Israeli ufalme? Yesu akawaambia, sio kazi yenu kujua
nyakati wala majira.(Matendo 1:6), Hii ikiwa na maana kuna wakati utafika watarudishiwa na huyu huyu masihi Yesu Kristo.
Hivyo
huo wakati unafika, Pale Mungu atakaposimama tena upande wa Israeli na
kuwashindania kwa nguvu nyingi kama alivyokuwa anafanya zamani, pale
mataifa yote ulimwenguni yatakapoungana ili yaje kujaribu
kuisambaratisha Israeli katika ile vita ya Harmagedoni ndipo hapo Kristo
atakawapigania toka juu kwa nguvu na uweza mwingi…damu nyingi
itamwagika sana, maadui wote wa Israeli watakufa kama kuku waliochinjwa
wakaachwa, wakati huo Bwana atakapolipigania Taifa lake…. Tunalisoma
hilo katika..
Zekaria 14:1 “Tazama, siku moja ya Bwana inakuja, ambayo mateka yatagawanyika kati yako.
2 Kwa maana nitawakusanya mataifa yote walete vita juu ya Yerusalemu; na huo mji utapigwa, nazo nyumba zitatekwa, nao wanawake watatendwa jeuri; na nusu ya watu wa mji watatoka kwenda utumwani; ila mabaki ya watu wa mji hawatakatiliwa mbali.
3 Hapo ndipo ATAKAPOTOKEA BWANA, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita.
4 Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini.
5 Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la milima yangu; kwa maana bonde lile la milima litaenea hata Aseli; naam, mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku zaUzia, mfalme wa Yuda; na Bwana, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye.
Kwahiyo
tusifurahie tu kuona leo hii Israeli inazidi kufanikiwa lakini badala
yake tuogope na tujiulize maswali je! Wewe tumejiandaaje sasa?, neema
ndio hivyo inaondoka kwetu, tazama hata hali ya ukristo sasa hivi
duniani sio kama ile ya zamani, tazama mataifa ya ulaya ambayo ndio
yalikuwa ya kwanza kutuleta injili lakini sasa jinsi yanavyozidi
kujitenga na ukristo kwa kasi, hiyo ni dalili kuwa neema inaondoka kwa
mataifa, inakimbilia Israeli..Itafika wakati mataifa yote yataenda
kinyume na taifa teule la Mungu hata hili taifa letu vilevile litaungana
na yule mpinga-Kristo ili kuiangamiza Israeli.
Zekaria 12: 3 “Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake”.
Ndugu
wakati huo sio wa kuutamani kwanini tusubirie mpaka hayo yote yatukute
kwa ghafla wakati tunayo nafasi sasa? Neema inamalizikia AFRIKA, usiiche
ikupite, chukua hatua ya kumwamini Yesu ayasafishe maisha yako, ili uwe
tayari kwa unyakuo ulio karibuni kutokea.
Bwana akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Jina Bwana wetu Yesu libarikiwe. Ni siku nyingine tena Bwana ametupa neema kuiona hivyo nakukaribisha ndugu popote pale ulipo tushiriki pamoja Baraka Bwana alizotuandalia leo.
Tukisoma Zekaria 12:9-14, inasema.
“ 9 Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba nitatafuta kuwaangamiza mataifa yote watakaokuja kupigana na Yerusalemu.
10 Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido.
12 Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao;
13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao.
14 Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao”.
Watu wanaozungumziwa hapo ni wayahudi (yaani Waisraeli) , Embu leo jiulize tu Israeli ni Taifa dogo sana kama mkoa wa njombe, ni taifa ambalo huwezi hata ukaenda na kukutana na vitu vya kuvutia huko au vya kushangaza kama mataifa mengine makubwa, lakini ni kwanini leo hii imekuwa ni JICHO LA DUNIA?. Wapo mbali na Mungu lakini ni watu wenye akili na wenye mafanikio makubwa duniani, jiulize siku wakiwa karibu na Mungu itakuwaje?
Hayo maandiko hapo juu ni lazima yatime, utafika wakati biblia inasema Roho ya neema itaachiliwa juu yao na watamwamini huyu Yesu ambaye sasa hawamwamini, Siku hiyo Watalia na kuomboleza baada ya kugundua makosa yao kuwa Yule waliyemsulibisha na KUMCHOMA MKUKI miaka 2000 iliyopita kumbe ndiye Masiya waliokuwa wanamsubiria kwa miaka mingi..Ile roho ya ufarisayo na usadukayo itaondoka juu yao.
Kama vile biblia inavyotabiri kutakuwa na maombolezo makubwa sana huko Yerusalemu wakitubu makosa yao.
Sasa hicho ndio kile kipindi ambacho mtume Paulo alikiandika katika
Warumi 11:25 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili [anasema na sisi watu wa mataifa]; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.
27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao”.
Unaona hapo unabii huo utatimia katika hiyo siku?, Huo wakati wa Israeli kurudiwa na kutengwa na maovu yao upo karibuni sana, na utakapoanza tu basi ujue utimilifu wetu sisi mataifa utakuwa umeshawasili yaani kwa lugha nyingine neema kwetu itakuwa imeshaondoka na kurudi tena Israeli, na hiyo itaambatana na tendoKUU la UNYAKUO.
Sasa wayahudi ambao leo hii utawaona wanalia usiku na mchana pale kwenye ule Ukuta wa maombolezo (wailing wall). wakimwomba Mungu wa Ibrahimu baba yao aje kuwaokoa na maadui zao na kuleta utawala wa masihi duniani, ipo siku hayo maombolezo yatakoma, na ndipo Mungu atawarudia kwa kuwafumbua macho na kumwona YESU, Kumbuka Mungu aliwapofusha kwa makusudi kabisa wasimwamini Kristo ili sisi mataifa tuipate neema vinginevyo huyu Yesu wa thamani ambaye leo hii tunaifurahia neema yake, tungemsikilizia tu kwa wayahudi, sisi tungeendelea kuwa waabudu miti,vinyago, na wachawi. Na hata hivyo dunia ungekuta imeshakwisha siku nyingi, wakati ule ule tu Yesu aliokuwa ndio ungepaswa uwe ni wakati wa wao kurejeshewa ufalme wa dunia na Yesu.
Unakumbuka mitume walimuuliza Yesu baada ya kufufuka je! Huu ndio wakati wa kuwarudishia Israeli ufalme? Yesu akawaambia, sio kazi yenu kujua nyakati wala majira.(Matendo 1:6), Hii ikiwa na maana kuna wakati utafika watarudishiwa na huyu huyu masihi Yesu Kristo.
Hivyo huo wakati unafika, Pale Mungu atakaposimama tena upande wa Israeli na kuwashindania kwa nguvu nyingi kama alivyokuwa anafanya zamani, pale mataifa yote ulimwenguni yatakapoungana ili yaje kujaribu kuisambaratisha Israeli katika ile vita ya Harmagedoni ndipo hapo Kristo atakawapigania toka juu kwa nguvu na uweza mwingi…damu nyingi itamwagika sana, maadui wote wa Israeli watakufa kama kuku waliochinjwa wakaachwa, wakati huo Bwana atakapolipigania Taifa lake…. Tunalisoma hilo katika..
Zekaria 14:1 “Tazama, siku moja ya Bwana inakuja, ambayo mateka yatagawanyika kati yako.
2 Kwa maana nitawakusanya mataifa yote walete vita juu ya Yerusalemu; na huo mji utapigwa, nazo nyumba zitatekwa, nao wanawake watatendwa jeuri; na nusu ya watu wa mji watatoka kwenda utumwani; ila mabaki ya watu wa mji hawatakatiliwa mbali.
3 Hapo ndipo ATAKAPOTOKEA BWANA, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita.
4 Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini.
5 Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la milima yangu; kwa maana bonde lile la milima litaenea hata Aseli; naam, mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku zaUzia, mfalme wa Yuda; na Bwana, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye.
Kwahiyo tusifurahie tu kuona leo hii Israeli inazidi kufanikiwa lakini badala yake tuogope na tujiulize maswali je! Wewe tumejiandaaje sasa?, neema ndio hivyo inaondoka kwetu, tazama hata hali ya ukristo sasa hivi duniani sio kama ile ya zamani, tazama mataifa ya ulaya ambayo ndio yalikuwa ya kwanza kutuleta injili lakini sasa jinsi yanavyozidi kujitenga na ukristo kwa kasi, hiyo ni dalili kuwa neema inaondoka kwa mataifa, inakimbilia Israeli..Itafika wakati mataifa yote yataenda kinyume na taifa teule la Mungu hata hili taifa letu vilevile litaungana na yule mpinga-Kristo ili kuiangamiza Israeli.
Zekaria 12: 3 “Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake”.
Ndugu wakati huo sio wa kuutamani kwanini tusubirie mpaka hayo yote yatukute kwa ghafla wakati tunayo nafasi sasa? Neema inamalizikia AFRIKA, usiiche ikupite, chukua hatua ya kumwamini Yesu ayasafishe maisha yako, ili uwe tayari kwa unyakuo ulio karibuni kutokea.
Bwana akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Jicho la Mungu kidogo kidogo linaanza kuondoka kwa mataifa na kurejea Israeli. Wakati wowote Hekalu la tatu nitaanza kujengwa pale Yerusalemu kwani maandalizi yote yapo tayari.Kilichobaki ni amri tu kutolewa, Na kumbuka ujenzi wa sasa hivi sio kama ule wa zamani, haitachukua tena miaka 7 au 20 kukamilika, itakuwa ni kitendo cha wiki kadhaa tu, au miezi kadhaa tu, kila kitu kitakuwa kimeshakamilika. Na tunafahamu likishakamilika tu, Mungu ataliweka JINA LAKE HAPO kama alivyomwahidia mtumishi wake Daudi na Sulemani zamani (1Wafalme 9:3), na mahali popote jina la Mungu lilipo basi WIVU wake utakuwepo pia.
Na biblia inatuambia mpinga-kristo akishaliona hilo ataondoka moja kwa moja na kwenda kutaka kuketi pale kama Mungu kupatia unajisi ili Mungu atiwe wivu alete uharibifu duniani kote ndio maana kimaandiko huyu mpinga-kristo anajulikana kama (CHUKIZO LA UHARIBIFU), Yeye ndio atakayeleta dhiki kuu, wakati huo unyakuo wa kanisa utakuwa umeshapita.
2Wathesalonike 2:3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;
4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.
5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?
6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.
7 Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.
Unadhani muda tuliobakiwa nao sasa ni mwingi?.Uzuri ni kwamba hatuna haja ya kuelezeana kila kitu kwani mambo yote yapo wazi kwenye TV na Internet siku hizo zitakapofika.. Huu ni wakati wa kujifunga mkanda UNYAKUO upo mbioni.
Maran Atha.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Jina la mwokozi wetu YESU KRISTO litukuzwe mpendwa, karibu tujifunze habari za uzima.
Wapo wengi wanaojifariji kuwa baada ya unyakuo watakuwa na nafasi ya pili. Ndugu Kama hutataka kuitii nguvu ya Roho Mtakatifu itokayo kwa Mungu inayokushawishi leo hii umgeukie Mungu, basi fahamu kuwa hutakuwa na tumaini lolote huko mbele baada ya unyakuo biblia imeweka wazi kabisa kuna NGUVU nyingine itakayoachiwa kutoka kwa Mungu juu ya watu waliosalia kuwafanya wauamini uongo wa mpinga-kristo. Nguvu hiyo biblia inaiita nguvu ya upotevu.
Jiulize ni kitu gani kitakachomfanya mpinga-Kristo apate nguvu dunia nzima kwa muda mfupi sana kama huo, Unadhani ni jambo rahisi tu mtu mmoja atokee ateke dunia nzima, halafu ishikamane naye? Ni wazi kuwa kuna nguvu nyingine itaachiliwa hapo ndani ya mioyo ya watu wamwamini yeye, wazikubali sera zake na ustaarabu wake, na mfumo wake bandia, na ishara zake na ajabu zake za uongo.
Ndugu ukiwepo wakati huo hakuna namna utaweza kumchukia, utaungana naye tu, hatakuwa mtu mkatili kama wewe unavyomfikiria, kwamba atakuwa anaua watu ovyo ovyo tu barabarani, hilo halitawezekana ufalme wake utasimamaje sasa, sharti mataifa yamkubali , apendwe na watu wote na serikali zote na majeshi yote duniani..yafanye kazi pamoja na yeye, ili baadaye apate nafasi ya kuwaangamiza wayahudi na baadhi ya watu wachache watakoanekana huku kwenda kinyume na ustaarabu wake mpya.
Ikiwa leo hii bado hauuoni etendaji kazi wake, unatazamia vipi siku ile umtambue, kwasababu biblia inasema tangu kipindi cha mitume SIRI ya kuasi inatenda kazi, bado tu mwasisi wa hiyo ASI kufunuliwa tu, ambaye ndio mpinga-kristo mwenyewe.na hilo sio jambo kubwa kutokea, kama mipango yake yote imeshakita mizizi kinachongojewa ni nini kama sio kufunuliwa.
2Wathesalonike2:3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;
4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.
5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?
6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.
7 MAANA ILE SIRI YA KUASI HIVI SASA INATENDA KAZI; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.
8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutendakwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
10 na katika madanganyo yote yaudhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
11 Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo;
12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.
Unaona hapo? Sasa Mpinga-Kristo huyu atatokea katika utawala wa RUMI biblia imelithibitisha hilo, ndani ya dini yenye wafuasi wengi leo hii duniani, na kiongozi wake anapata sifa na kukubalika sasa na dini zote duniani na mataifa yote, Na katika kiti hicho anachokalia huko VATICAN ndicho hicho hicho mpinga-kristo atakaponyanyukia..
Ndugu, ulimwengu huu upo ukingoni sana, bado unayachezea maisha yako mpaka siku nguvu ya upotevu itokayo kwa Mungu ikuingie, ili uamini uongo uende kuzimu?. Ni jambo la kuogopesha sana. Geuza NIA yao mtazame YESU, UNYAKUO wa kanisa upo karibu.
Mungu akubariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo
libarikiwe…Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Ufunuo, ambapo leo
tutaitazama ile sura ya 16, ya kitabu hichi, Ni vizuri kama hujapita sura za
nyuma ungeanza kwanza kuzipita hizo ili uweke msingi mzuri wa kuzielewa sura zinazofuata.
Katika sura hii ya 16, habari kuu tunayoiona ni juu ya vitasa 7, “Vitasa ni VIBAKULI kwa lugha ya sasa”..Na hasira ya Mungu sehemu nyingine imefananishwa na mfano wa kimiminika fulani kinachojaa katika chombo, ambacho kwa jinsi hasira ya Mungu inavyozidi kuongezeka juu ya mtu au watu ndivyo kimiminika kile kinavyozidi kujaa ndani ya hicho kikombe au kibakuli…Na kikiisha kujaa kukaribia kumiminika, ndipo mtu au watu wanapewa wakinywe..na kunywa kunaashiria “kuipokea ghadhabu ya hasira ya Mungu (yaani kuadhibiwa)”.
Ndio maana ukisoma kwenye biblia
wakati wana wa Israeli walipomkosa Mungu hata Mungu akadhamiria kuwapeleka
Babeli, Nabii Yeremia alipewa maono ya kuwanywesha wana wa Yuda kikombe cha
ghadhabu ya Mungu…Na wakati ulipofika wa Neno hilo kutimia Mfalme wa Babeli
alishuka juu yao akawachinja chinja wanawake na watoto, na wale waliosalia akawachukua mpaka Babeli
utumwani..Na utaona kikombe hicho cha ghadhabu ya Mungu hawakunywesha tu wana
wa Yuda bali mataifa mengi duniani pia walinyweshwa.
Yeremia 25: 15 “Maana Bwana, Mungu wa Israeli, aniambia hivi, Pokea kikombe cha divai ya ghadhabu hii mkononi mwangu, ukawanyweshe mataifa yote, ambao nitakupeleka kwao;
16 nao watakunywa, na kulewalewa, na kufanya wazimu, kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka kati yao.
17 Ndipo nikakipokea kikombe kile mkononi mwa Bwana, nikawanywesha mataifa yote, ambao Bwana alinipeleka kwao;
18 yaani, Yerusalemu, na miji ya Yuda, na wafalme wake, na wakuu wake, ili kuwafanya kuwa ukiwa, na ajabu, na mazomeo, na laana; vile vile kama ilivyo leo;
19 Farao, mfalme wa Misri, na watumishi wake na wakuu wake na watu wake wote;
20 na watu wote waliochanganyika pamoja, na wafalme wote wa nchi ya Uzi, na wafalme wote wa nchi ya Wafilisti, na Ashkeloni, na Gaza, na Ekroni, na mabaki ya Ashdodi;
21 Edomu, na Moabu, na wana wa Amoni;
22 na wafalme wote wa Tiro, na wafalme wote wa Sidoni, na wafalme wote wa kisiwa kilicho ng’ambo ya pili ya bahari; 23 Dedani, na Tema, na Buzi, na watu wote wakatao denge;”
Na pia tutakuja kumwona jinsi Yule mwanamke(Babeli mkuu,Mama wa makahaba) akipewa kikombe hiki cha ghadhabu ya Mungu katika ufunuo.16:19.
Lakini katika sura hii, tunaona Malaika saba wakiwa na VIBAKULI saba. Hivi sasa ni vibakuli vya ghadhabu ya Mungu juu ya dunia nzima sio tena juu ya mataifa Fulani baadhi au watu Fulani wachache, ghadhabu ya Mungu juu ya watu wachache haihitaji kibakuli, kikombe tu kingeweza kutosha..lakini hapa ni maovu ya dunia nzima..Maovu ya wanadamu ndio yamevijaza vibakuli hivyo..Kimoja baada ya kingine kimejaa..Bwana hakukiweka kimoja kwa sababu yeye ni wa rehema bali aliviweka saba ingekuwa ni kimoja tayari siku nyingi sana tungeshaangamizwa kwasababu kingekuwa kimeshajaa..lakini wanadamu wamevijaza vyote saba…Na hivyo vitakwenda kumiminwa juu ya dunia nzima, kumbuka hawatanyweshwa watu bali watamiminiwa..hiyo ni hatari sana.
Lakini kabla ya kuviangalia hivi vitasa kuna vitu vichache vya utangulizi vya kufahamu..
Hii neema tulionayo leo itafika
mwisho, kuna baadhi ya misemo imekuwa ikisemwa kuwa Mungu wa agano la kale leo
hii hayupo, kama yupo zile ishara alizokuwa anatenda agano la kale ziko wapi
leo?. Lakini SIKU YA BWANA inakuja ndugu usitamani uwepo! USITAMANI UWEPO! ni
mambo ya kuogopesha ambayo usingetamani hata adui yako yampate, Mungu kuzuia
ghadhabu yake ni kwa ajili yetu sisi ili tutubu lakini tusipotubu hukumu
itatukuta wakati tusioutazamia.
Kuna vitu vitatu vya kutisha ambavyo
vipo mbele yetu sasa,
1) DHIKI KUU,
2) SIKU YA BWANA,
3) ZIWA LA MOTO.
Leo tutaitazama hii SIKU YA BWANA ni ipi, itakuja lini na itakuwa inamuhusu nani.
Kwa ufupi ndugu, DHIKI KUU itakuja
na tunafahamu itakuwa kwa wakristo watakaokataa kuipokea ile alama/chapa ya
mnyama. Hii itamuhusu mpinga-kristo akiwatesa wakristo wale waliokataa kuipokea
ile chapa ya mnyama, Ambapo mwishoni mpinga-kristo atafanikiwa kuwaua kikatili
wote wasioipokea chapa. Na hii dhiki itadumu kwa muda wa miaka mitatu na nusu,
ni wakati wa kutisha sana unakuja mbeleni. Kwahiyo wakati wakristo wachache
wanapitia dhiki kuu, wengine wote waliosalia watakuwa wanaendelea kujifurahisha
na mambo yao ya dunia wakimfurahia mpinga kristo na utawala wake.
Sasa SIKU YA BWANA itaanza mara tu baada
ya DHIKI KUU kuisha ambapo watakatifu wote wakati huo watakuwa
wameshaondoka,(wameuliwa na mpingakristo) na unyakuo utakuwa umeshapita wakati
huo, lakini hao waliobakia walioipokea chapa ya mnyama itawapasa waingie kwenye
adhabu kali sana ya Mungu mwenyewe, Kwasababu wameshirikiana na mpinga kristo
kuwaua watu wa Mungu na kwasababu wamekataa kumcha Mungu na kuzishika amri
zake, ndugu Hii SIKU YA BWANA usitamani uwepo. Kumbuka haitakuwa jehanamu ya
moto, bali itakuwa ni adhabu ya hapa hapa duniani.
maandiko yanasema:
Amosi 5:18 “Ole wenu! Ninyi mnaoitamani SIKU YA BWANA; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru.
19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga.
Pia tukisoma…
Isaya 13:6″ Pigeni kelele za hofu; maana SIKU YA BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu.
7 Kwa sababu hiyo mikono yote italegea, na moyo wa kila mtu utayeyuka.
8 Nao watafadhaika; watashikwa na utungu na maumivu; watakuwa na utungu kama mwanamke aliye karibu na kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.
9 Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
10 Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.
11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahariyao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;
12 nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri.”
Maandiko yanaposema SIKU YA BWANA
hayamanishi ni siku kama siku moja, bali inamaanisha ni kipindi fulani cha
WAKATI ambacho Bwana amekitenga kwa kusudi fulani. Kama maandiko yanavyotueleza
ni kipindi ambacho kimetengwa cha GHADHABU NA HASIRA ya Mungu kulipiza kisasi
kwa wanadamu wote wasiomcha Mungu. Kipindi Hichi cha SIKU YA BWANA kitadumu kwa
muda wa siku 75, Hizi zimepatikana kutoka katika kitabu cha Nabii Danieli
12:12, ambapo tunaona kipindi cha ile dhiki kuu kitadumu kwa muda wa siku 1260(sawa
na miaka 3 na nusu), na hapo zimeongezeka siku nyingine kutoka siku 1260 mpaka
kufikia siku 1335, kwahiyo ukichukua hizo siku 1335-1260=75. Kwahiyo hizi siku
75 zilizoongezwa ni mahususi kwa ajili ya BWANA kujilipizia kisasi kwa wanadamu
wote waliosalia juu ya uso wa nchi.
Kabla ya SIKU hiyo ya BWANA kuanza Kutakuwa na baragumu saba zitakazopigwa kuitangulia , Hizi Zitabeba hukumu kwa watu wote, kama onyo watu watubu kumgeukia Mungu, Dunia itapigwa kwa mapigo mengi ya ajabu ukisoma Ufunuo 8 ikiwemo, theluthi moja ya maji kuwa damu, theluthi ya maji duniani kutiwa uchungu, theluthi ya mwezi na jua na nyota kupigwa, hebu tafakari kutakuwaje duniani wakati huo mchana kutakuwa kama jioni, giza litakuwa nene usiku na baridi kali sana, nzige wa ajabu watapandishwa kutoka kuzimu, maumivu yao ni kama ya kung’wata na nge, na meno yao ni kama meno ya simba, n.k. Biblia inasema watu watakitamani kifo lakini hawatakiona, kumbuka hapo bado SIKU YA BWANA haijaanza huo ni mwanzo wa utungu tu, unatangaza hukumu KUU ya Bwana inayokuja mbeleni kwa urefu soma ufunuo sura ya 8 na ya 9. inaelezea haya mapigo ya baragumu saba za Mungu.
Lakini pamoja na mapigo yote hayo ya
baragumu biblia inasema watu watakaokuwa juu ya uso wa nchi hawatatubu maovu
yao kwasababu roho ya uovu imeshakaa juu yao kwa kuwa wote wamekwisha ipokea
ile chapa ya mnyama neema ya Mungu imeondoka juu yao hawawezi kutubu tena.
Kwahiyo mara baada ya dhiki kuu
kuisha wakristo kuuliwa na unyakuo kupita, Sasa Hawa wanadamu waliobaki ndio
watakaoingia katika SIKU YA BWANA inayotisha, ile inayowaka kama moto yenye
vile vitasa saba ambayo ndiyo yale mapigo saba ya mwisho ya Mungu, katika hayo
ghadhabu ya Mungu imetimia : Hebu tutazame vitasa hivi kimoja baada ya kingine.
KITASA CHA KWANZA:
Ufunuo 16:1 ” Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi.
2 Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na JIPU BAYA, BOVU, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake.”
Sasa adhabu hizi zitakuwa ni kwa Dunia nzima na sio theluthi tena ya dunia kama ilivyokuwa kwa zile baragumu saba. Majipu haya tunaona ni mfano wa yale yale waliopigwa wamisri, Kutakuwa na majipu ya ajabu usidhani ni haya ya kawaida uliyoyazoea, biblia imeyaita ni MAJIPU MABOVU bado hayajatokea kabisa duniani, huo ugonjwa bado haujazuka, Tuna magonjwa mengi ya hatari duniani lakini biblia haijayataja yote hayo, lakini ni huu ugonjwa wa MAJIPU tena jipu bovu ndio umetabiriwa utakuja, homa yake itakuwa sio kama hizi za kawaida tulizozizoea, na utakuwa na vidonda vikubwa sana, utampata kila mtu aliyekaa juu ya nchi, pamoja na wanyama Ndugu usitamani kuwepo huko wewe unayesema Mungu wa agano la kale haishi, siku hiyo utayaona haya wazi wazi.
KITASA CHA PILI:
Ufunuo 16:3 “Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.”
Duniani kutakuwa na harufu kama ya
damu ya mtu aliyekwisha kufa, damu ya mtu aliyekufa ni tofauti na ya aliye hai,
damu ya mtu aliyekufa inakuwa kama mgando Fulani mweusi hivi…ndivyo bahari
itakavyokuwa.. hakutakuwa na kiumbe chochote baharini chakula kitapungua
duniani, maji yataisha, shughuli za usafirishaji baharini vitakwama, mvua
zitaacha kunyesha duniani kutakuwa sio sehemu ya kuishi tena mwanadamu, taabu
itaongezeka duniani, hofu kuu itawaingia watu wakitazama ni mambo gani haya
yameipata dunia?..nini kinaendelea?.. lakini bado mapigo yatakuwa yanaendelea,
KITASA CHA TATU:
Ufunuo 16:4 ” Na huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji; zikawa damu.
5 Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi;
6 kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; nao wamestahili.
7 Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, ni za kweli, na za haki, hukumu zako”.
Baada ya bahari kugeuzwa kuwa damu
ya mizoga, watu wote tunajua wangekimbilia kutafuta maji katika mito na kwenye
chemchemi za maji, kutokana na kiu kali, lakini Bwana atayapiga pia maji ya
mitoni na kwenye chemchemi, wakati huo fedha itakuwa haifanyi kazi tena, Mtu
tajiri atakuwa ni mwenye kikombe cha maji safi mkononi mwake na sio fedha,
Kwahiyo Bwana atawalazimisha kuyanywa hayo maji ya DAMU kwasababu
walishirikiana na yule mnyama kumwaga damu ya watakatifu wa Mungu, hivyo nao
Bwana amewapa wainywe. Na kwasababu ya kiu kali watakunywa hiyo damu, na
wanadamu wengi wataangamia na kufa kwa pigo hilo.
KITASA CHA NNE:
Ufunuo 16:8 “Na huyo wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua, nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto.
9 Wanadamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu.”
Baada ya pigo la maji kuwa damu, jua
litashushwa chini, maunguzo yatakuwa ni makubwa sana, joto litaongezeka duniani
kwa nyuzi joto kubwa kuliko kiwango cha kawaida. Mimea yote itakauka ghafla,
dunia itafanana na jangwa ndani ya muda mfupi sana, jaribu kutafakari majipu ya
ajabu yanawapata watu wakati huo huo maji yote damu..na bado jua kali linapiga
na hakuna maji hata kidogo ya kujipooza,ni dhiki kiasi gani? ni mambo ambayo
huwezi dhania yatatokea lakini yapo mbioni kutokea. Lakini pamoja na hayo
mapigo yote biblia inasema watu watamtukana Mungu hawatatubu…watalia kwa
uchungu wa maumivu hayo watasema kama Mungu yupo kwanini anatufanyia hivi…na
kwasababu hawataona majibu yoyote wakati wanateseka watakasirika na kuishia
kumtukana Mungu.. Mfano tu wa kizazi chetu hichi watu wanapopatwa na majanga
badala wageuke na kumuuliza Mungu ni kwanini na kutubu, wao wanalaani na kutoa
maneno ya makufuru.
KITASA CHA TANO:
Ufunuo 16:10 “Na huyo wa tano akakimimina kitasa chake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama; ufalme wake ukatiwa giza; wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu,
11 wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao; wala hawakuyatubia matendo yao. “
Sasa pigo hili linamuhusu sana sana
yule mnyama aliyewakosesha wanadamu wote kuipokea ile chapa, mahali kiti chake
cha enzi kilipo ambapo ni VATICAN, Roma, Mungu ataachilia laana kwa mataifa ya
ulaya ambayo ndio zile pembe kumi, zitamchukia na kumwangamiza yule mwanamke
kahaba (Kanisa Katoliki) ambalo makao yake makuu ni VATICAN. Hii ni kutokana na
kwamba yale mataifa ambayo yalimtumaini mpinga kristo ayaletee amani duniani,
hayajaletewa zaidi ya yote mpingakristo (PAPA) ameiongezea dunia matatizo hivyo
basi watamchukia na kumwangamiza, tangu wakati huo utawala wa Roma, pamoja na
mpinga kristo (PAPA) na Vatican yake hawatakuwepo tena ufalme wao umekwishatiwa
giza. Wakati huo bado wataona bahari ipo vile vile damu, hakuna maji wala
umande, jua limegeuka kuwa moto, na majipu yanazidi kuwaharibu…wataona hakuna
sababu ya kuwepo na kiongozi mwongo kama asiyekuwa na msaada na mwongo.. hivyo
wakiwa katikati ya huo msiba mkubwa ulioikumba dunia watamgeuka Papa na kumwangamiza.
Soma ufunuo 17:16” Na zile
pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao
watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa
moto. ”
KITASA CHA SITA:
Ufunuo 16:12 “Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.
13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.”
Kitasa hichi kunazungumzia ile vita kuu ya HAR MAGEDONI ambayo itakuwa ni vita kati ya Mungu mwenyezi akilipigania taifa la Israeli dhidi ya wafalme wote wa dunia. karibu kila taifa litaunga mkono vita hii wakiongozwa na mataifa kutoka mawio ya jua. Haya mataifa ya mawio ya jua ni mataifa ya mashariki, nayo ni CHINA,JAPAN, KOREA na machache baadhi. Wakati huo Vatican itakuwa haipo, Marekani itakuwa haipo, Urusi itakuwa haipo yatatoweshwa katika vita vilivyoelezwa katikaEzekieli 38 & 39, Kwahiyo zile roho chafu ambazo zilikuwa zinaendesha Vatican na Marekani zitahamia kwenye haya mataifa ya mashariki yaliyosalia kwa ajili ya vita dhidi ya Israeli. Wakati huo ndio Bwana YESU atakapotokea kuwapigania watu wake Izraeli. Ndugu wakati huo dunia itakuwa mfano wa sayari ya Zebaki, hakutakuwa na maji, chakula, magonjwa, joto litakuwa juu sana, maji yote damu, machafuko pamoja na vita, itakuwa ni vilio na kusaga meno, siku hiyo watu watatamani siku hizi za neema tulizonazo leo hawataziona.
KITASA CHA SABA:
Ufunuo 16:17 ” Na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa.
18 Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.
19 Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.
20 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena.
21 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.”
Hili ni pigo la mwisho, na katika
hili ghadhabu ya Mungu imetimia tukisoma pale muhuri wa sita ulipofunguliwa
ulitoa picha halisi jinsi hii siku itakavyokuwa soma Mathayo 24:30-31 na pia
Ufunuo 6:12-17
Ufunuo 6:12-17 ” Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,
13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.
14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”
Pigo la saba la mwisho kama tunavyosoma ni baya kuliko yote yaliyotangulia maana jua linaondolewa, mwezi utakuwa damu, nyota zitatoweka, unaweza kuona kutakuwa na giza kiasi gani duniani, na baridi kiasi gani (wakati huu sasa jua litakuwa limeondolewa), kutakuwa ni giza zito sana, hakutakuwa na chanzo chochote cha umeme, wala nishati…shughuli zote za kimaendeleo zilishamalizwa katika mapigo yaliyotangulia, hadi kufikia hapa watu wachache sana watakuwa wamesalia duniani, kumbuka hapo bado ziwa la moto linasubiri watu, Hichi ni kisasi tu cha hapa hapa duniani.
Mvua ya mawe kubwa sana itanyesha, mawe kama talanta,(Talanta 1 ni kama kg 34), Huwezi kujificha kwenye nyumba yako ya bati au ya kigae, kg 34 ni uzani mkubwa sana ambayo yatashuka kwa kasi kubwa sana kutoka juu…itaambatana na tetemeko ambalo halijawahi kutokea, kiasi cha kwamba visiwa vitahama, kisiwa cha zanzibar kitapotea siku hizo, Milima itatapika volkano, kumbuka hayo yote yatafanyika katikati ya giza nene, hakuna mawasiliano, kutakuwa hakuna kuonana wala kupigiana simu.. hapo hakuna mfalme wala mtumwa, raisi wala mwananchi wote waliosalia watatamani wafe kuliko kuishi, watatamani milima iwaangukie waikwepe ghadhabu ya Mungu, Hapo ndipo itakapoonekana ishara ya mwana wa Adamu mawinguni.
Soma Mathayo 24:29 “Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;
30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. “
Rafiki haya mambo ni kweli
yatatokea, ndivyo yatakavyokuja kuupata ulimwengu na dalili zote zinaonyesha
kuwa yatatokea katika kizazi chetu tunachoishi mimi na wewe, Bwana amekwisha
kutuonya mbele, Nia yake ni sisi tuiepuke hiyo ghadhabu na ndio maana kuna
mahali alisema alipokuwa katikati ya kitasa cha sita (Tazama, naja kama mwivi.
Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu
yake). Kwahiyo ametuonya tukeshe na kuyatunza mavazi yetu, maana hii siku ya
ghadhabu itakuja ghafla.
Ndugu kimbia injili ambazo
zinakufanya usifikiri hatma ya maisha yako ya milele badala yake inakupeleka
kutazama mambo ya ulimwengu huu tu!. Hii ni roho ya shetani inayowapumbaza
wengi wafikiri mambo hayo yatakuja kutokea baada ya miaka 2,000 mbele,
usidanganyike ni uongo wa shetani, ndugu dalili zote zinaonyesha, unabii wote
umetimia kwamba tunaishi katika kizazi cha hatari sana. Chunguza maisha yako na
maandiko angali neema ipo, mambo hayatakuwa hivi siku zote, pale mlango wa
neema utakapofungwa kutakuwa hakuna kurudi nyuma itakuwa ni vilio na
maombolezo, kimbilia kalvari sasa tubu dhambi zako, uoshwe kwa damu ya Yesu, na
Upokee Roho Mtakatifu kabla ya huo wakati kufika. Kumbuka adhabu ya hii SIKU YA
BWANA, sio jehanamu ya moto, baada ya mapigo hayo ndipo ziwa la moto ziwa la
moto litafuata, wote waliokufa katika hii siku ya Bwana ambao ndio wale wote
walioipokea chapa ya mnyama…baada ya ule utawala wa miaka 1000 watafufuliwa
na kuhukumiwa katika kiti cheupe cha hukumu na kisha watatupwa katika lile ziwa
la moto.
Ikiwa unataka kumpa Bwana Yesu maisha yako na kugeuka leo tubu mwenyewe moyoni mwako au fuatiliza sala hii kwa imani:
⏩ SEMA: “Bwana Yesu, Leo hii nasogea mbele zako nikiwa mwenye dhambi, natubu makosa yangu yote niliyokukosea, naomba unisamehe, nimeamua kugeuka leo, nisaidie Bwana Yesu, neema yako iwe juu yangu, nikuishie wewe, siku zote za maisha yangu, asante Bwana Yesu kwa kunisikia na kunisamehe. AMEN! “.
Baada ya kutubu na kudhamiria
kutokufanya tena dhambi unahitaji kubatizwa, Hivyo basi tafuta kanisa
linalobatiza ubatizo sahihi nao ni kwa kuzamishwa kwenye maji mengi na ni kwa
jina la YESU KRISTO, Kwa kufanya hivyo Bwana atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu
na utakuwa umekamilisha wokovu wako.
Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara, kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP