JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.

JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.

Uchawi katika Biblia.

Mambo yote ambayo biblia imeyataja kama vile, kutazama bao(utambuzi), kubashiri, kuloga kwa kupiga mafundo. Kupandisha pepo/kupunga pepo, kuomba kwa wafu, kusihiri n.k. Yote haya kwa ufupi tunaweza kuyaweka katika kundi moja linalojulikana kama uchawi.

Na kazi hii imehasisiwa na shetani mwenyewe, baada ya kuona kuna upungufu wa taarifa Fulani za muhimu zimuhusuzo mwanadamu. na huku wanadamu wanao kiu ya kuzijua. ndipo hapo akabuni kitu kinachoitwa uchawi. Ni sawa na leo hii uone kisima kinachimbwa kijijini kwenu. Moja kwa moja utagundua kuwa ni kwasababu ya ukosefu au upungufu wa maji na ndio maana kisima kimekuja kuchimbwa.

Vivyo hivyo na Shetani naye, aliuleta uchawi baada ya kuona kuna taarifa Fulani zimuhusuzo mwanadamu zimekosekana au zimefichwa. Na aliyezificha ni Mungu mwenyewe kwa makusudi yake maalumu. ili wanadamu na viumbe vyake vyote viishi kwa kumtegemea yeye. Na si kwa kutegemea nguvu zao au akili zao.

Jambo hili lilimkasirisha shetani tangu mwanzo, na ndio maana aliasi ili ajitawale mwenyewe. Lakini alipoona ameshindwa kujua hata chanzo na mwisho wa maisha yake mwenyewe akaamua mawazo yake maovu ayalete kwa wanadamu kwa njia hiyo ya uchawi.

Uchawi ulianzi wapi?

Hivyo uchawi wa kwanza aliouleta, ulianzia pale Edeni, Mungu alipomweka Adamu na Hawa. Akawaagiza na kuwaambia wale matunda ya kila mti lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya wasile. kwasababu siku watakapokula, watakufa. Lakini tunamwona shetani akitokea ndani ya nyoka, Na kuanza kumwambia Hawa, Hakika hamtakufa…”Hilo Neno Hakika hamtakufa” Ndio Mwanzo wa siri za uongo, na vitu kama hivyo mwanadamu sikuzote anapenda kusikia,.akaendelea na kusema, kwasababu Mungu anajua siku mtakapokula mtafumbuliwa macho na kuwa kama Mungu: Mkijua mema na mabaya..

Unaona Yaani hapo shetani alikuwa anawafunulia siri kuu sana, kama tunavyojua mtu aliyefikia hatua ya kutambua mema na mabaya ni mtu aliyepevuka akili anaweza kujiongoza mwenyewe. na kujiamulia mambo yake mwenyewe,..Hivyo shetani hapo alikuwa anawaaminisha kuwa watakapoasi na kula tunda, basi watakuwa na uwezo wa kupanga na kuchagua juu ya maisha yao, bila msaada wowote wa Mungu. vile vile wanaweza kuamua lolote wajisikialo, huyu Mungu wa nini tena?..hawezi kuwaambia chochote kwani yeye ni nani?…Hivyo Hawa akavutiwa sana na taarifa hizo mpaka akadhubutu kufanya kile kitendo kiovu . Ambacho matokeo yake ndio tunayaona hadi sasa.

Na jambo hilo hilo shetani aliendelea kulileta ndani ya watu, kwa vizazi na vizazi watu wakiwa na tama ile ile kujua hatma za maisha yao zitakuwaje na huku hawataki kumwangalia Mungu. Shetani anapata nafasi ya kuwadanganya kwa elimu zake za uongo, za utazamaji nyota.

Anawadanganya watu kuwa nyota zinazoonekana mbinguni zimebeba hatma ya maisha yao.

Anawadanganya kuwa kuwa alama za mikono zimebeba siri za maisha yao, anawadanganya miti Fulani au majani, ukiyapaka, au ukiyachanganya na vitu Fulani wataona mafanikio ya maisha yao. Na mambo chungu nzima,..huku anafahamu kabisa anayejua hatma ya maisha ya mwanadamu na mambo yake yote si mwingine zaidi ya Mungu lakini kwasababu watu hawamtaki Mungu. hivyo yeye anafanya hivyo kwa lengo moja tu, kuzidi kuwafanya watu wazidi kupoteza uelekeo wao kwa Mungu, ili awavute kwake, na wakishakita mizizi kwake, basi awaangamize waishie jehanum.

Sasa unaweza ukauliza lakini mbona kweli mganga Fulani, aliniambia kila ikifika mwezi wa 6 niwe ninavaa gauni jekundu. Kwasababu nyota yangu ya mafanikio ipo hapo, inaniagiza hivyo? na kweli nimekuwa nikivaa na kuona mafanikio makubwa katika huo mwezi.

Nataka nikuambie shetani ni mjanja sana. Hakuna cha nyota yako hapo, wala hakuna chochote alichogundua juu ya maisha yako, kama tulivyosema lengo lake ni kukuvuta kwake.

sasa wewe unapokwenda pale kwa mara ya kwanza, au unapomsikiliza kwenye TV. Na kutii maagizo yake, kuvaa hilo gauni jekundu alilokuambia huo mwezi. Anachofanya ni anaagiza tu mapepo yake, kukufanyia wewe kazi unapofika huo mwezi wa 6. Na ndio hapo unaweza kuona kama ni wateja wako wanaongezeka, au kitu Fulani kinafanikiwa kirahisi katika huo mwezi..Lakini huo ni mtego wa awali anafanya hivyo kwako kwa mara ya kwanza ili umwamini yeye.

Na kwa namna ya kawaida mtu akishaona kafanikiwa atarudi tena kwa Yule mganga au msoma nyota aliyempa yale maagizo. Ashuhudie aombe msaada zaidi,.ndipo atapewa tena masharti mengi ya ziada. kwa kuahidiwa kuwa ili nyota yake ifanye kazi kiufasaha zaidi, anapaswa akapigiwe ramli nyumbani kwake, au alale chooni hicho kipindi. Na mambo ya ajabu ajabu mengi, na yeye atafanya. kwasababu alishaona mafanikio hapo mwanzo, baada ya muda tena aturudi kupewa maagizo mengine. Ataambiwa sasa atoe kafara ya mtoto wake ili kusafisha nyota, asipofanya hivyo wazee wa nyota yake watakasirika na hivyo atakufa, ataenda kufanya kwa woga.

Hivyo hivyo kesho kutwa tena ataambiwa tena, apae na ungo waende Jupita kuitembelea nyota yake, atapaa na ungo. siku moja atakasirishwa na jirani yake na ataenda kutafuta msaada na atapewa uwezo wa kumdhuru mtu (kuloga). mpaka mwisho wa siku anajikuta amekuwa mchawi mashuhuri. Na yeye anakuwa mganga wa kuwafundisha wengine mambo hayo. Na mtu huwa akishafikia hatua kama hizo kurudi tena ni Neema ya Kristo. Wengi wanafia huko, ninaweza kusema asilimia 99 wanafia kwenye uchawi… na kuishia motoni.

Hivyo ndivyo watu wanavyozama kidogo kidogo kwenye ushirikina na uchawi pasipo wao kujijua.

Leo hii utaona katika magazeti vipengele wanavyoviita NYOTA ZETU. kaa mbali na hayo mambo wala usisome, ni mtego wa ibilisi, anataka ukakijaribu kile kilichoandikwa pale, wala usidhubutu,kwasababu kweli anaweza kukuletea majibu chanya kutokana na kile ulichokisoma pale, lakini kumbe unaelekea shimoni.

UKWELI WA MAISHA YETU UPO WAPI?

Ndugu Ukweli wa maisha yetu upo mikononi mwa Mungu peke yake. Ikiwa utapenda kufahamu chochote kuhusu maisha yako ni heri ukapiga magoti na kumwomba akufunulie. Akikufunulia ni sawa asipokufunulia ni sawa vile vile ishi maisha ya amani ukijua kabisa wote waliomtumaini yeye watakuwa salama mikononi mwake…Pia hatima yetu imeandikwa kwenye Neno lake. Ukilisoma vizuri na kulielewa basi utakuwa umejua hatima ya Maisha yako. Njia za haraka haraka na za mkato kujua kesho yako itakuwaje, au za kutaka kujua ni nini kinaendelea kukuzunguka. Au za kutafuta mali za ghafla ziogope! Shetani kaweka mitego kila mahali.

Mungu aliwaonya sana wana wa Israeli juu ya jambo hili watakapofika nchi ya Kaanani.

Wasidhubutu mambo hayo, kwasababu hayo ndiyo yaliyomkasirisha Mungu mpaka wakaondolewa wale wenyeji wa Kaanani..

Kumbukumbu 18:10 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri.

11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.

12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.

13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako.

14 Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo.’’

Ndugu kama ulishawahi kujaribu mambo yoyote katika hayo. Tubu sasa, uombe rehema Mungu atakusamehe na uanze sasa kumfanya Mungu kuwa tumaini lako. Na yeye mwenyewe ndiye atakayekuongoza katika njia salama. Kwasababu hukumu ya Mungu ipo juu ya watu wote wanaojaribu kusikiliza mafundisho ya mashetani.

Malaki 3:5 “Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi,”

Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi. na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”

Ubarikiwe sana.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

HADITHI ZA KIZEE.

MAFUNDISHO YA MASHETANI

JE!MUNGU ANAWEZA KULETA MAJIBU KUPITIA NGUVU ZA GIZA KAMA TUNAVYOSOMA NABII SAMWELI KUPATA MAJIBU KWA MWANAMKE MCHAWI?


Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
6 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Muriithi Gitonga
Muriithi Gitonga
2 years ago

Ufafanuzi zaidi kuhusu mazingaombwe

Joel
Joel
2 years ago

Wazi kabiza nilipotea mimi

Juma Mwia
Juma Mwia
2 years ago

Vizuri sana mtumishi

Juma Mwia
Juma Mwia
2 years ago

Vizuri sana mtumishi